WAFANYA BIASHARA WAVAMIA GHALA LA HALMASHAURI YA JIJI

Vurugu kubwa za wafanyabiashara wadogo jijini Arusha maarufu kama wamachinga wamevamia ghala la manispaa ya jiji kwa lengo la kutaka warudidshiwe mali zao hatua iliyozua tafrani kubwa iliyosababisha naibu meya kupigana na baaadhi ya mgambo wa jiji waliokuwa wanajaribu kuwadhibiti wananchi hao.

Katika tafrani hiyo mgambo wa jiji aliyetajwa kwa jina la Marry Msuya amejeruhiwa na kulazwa hosipitali akidai kuwa amepigwa na naibu meya Mh Prosper Msofe huku naibu meya aliyekuwa anawatetea wananchi hao naye akidai kuwa amepigwa na mgambo huyo .

Baadhi ya wananchi wamelaalamika kuwa wamekuwa wakipigwa na kuporwa mali zao hata wakiwa wanatembea barabarani bila kuvunja sheria zilizowekwa.

Mkurugenzi wa jiji Bw Juma Iddy amesema suala la wananchi kupigwa halikubaliki lakini suala la zoezi la kusafisha jiji ni endelevu na amesisitiza kila mmoja kuheshimu sheria.

ZITTO: SERIKALI 3 HAZITA VUNJA MUUNGANO

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Zitto Kabwe amesema kuandikwa kwa Katiba isiyokubaliwa na pande zote kutasababisha gharama kubwa kuliko zile zinazotajwa za serikali tatu.

Akichangia hoja kwenye Bunge hilo jana, Zitto alisema kuna kila sababu ya kukaa na kukubaliana ili kupata Katiba itakayokubalika pande zote.

"Muundo wa Muungano una hatari ya kuvunjika iwapo hakuna matakwa ya dhati ya watu kuungana... Maneno ya kusema Serikali tatu zitavunja Muungano ni ya siasa na hayana msingi wa kisayansi. Urusi ilivunjika sababu haikuwa na demokrasia na siyo sababu ya idadi ya Serikali,"alisema.

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC), alisema hofu ya gharama inayotajwa katika uendeshaji wa muundo wa serikali tatu haina msingi wowote kwa kuwa hakuna ushahidi wa kitaalamu unaothibitisha gharama hizo.

"Nimesikia watu wanasema eti tutalazimika kujenga ikulu mpya, nani kasema lazima tuwe na marais watatu? Tunaweza kuwa na rais mmoja kwenye nchi na wakuu wa nchi washirika wawili… Ni jambo la makubaliano tu," alisema.

Alisema bajeti ya mwaka huu ni Sh18 trilioni, kati ya hizo Sh5.3 trilioni ndizo zinazohudumia wizara za Muungano, lakini serikali ina uwezo wa kukusanya kodi zaidi ya Sh10 trilioni pamoja na mapato mengine."
Kuna jumla ya Sh2.3 trilioni hatuzikusanyi kila mwaka kutoka kwenye kampuni kubwa, kwa uwezo wetu wapato la ndani asilimia 17 tunao uwezo wa kuendesha serikali ya muundo wa idadi yoyote.

"Hofu ya Serikali ya Muungano kutokuwa na fedha ni sababu halisi, ni kweli kwamba ushuru wa bidhaa pekee yake hauwezi kutuendeshea serikali. Sasa nini kazi yetu, tunaingia hapa ili kuboresha hayo maeneo, kama hatuwezi tumekuja kufanya nini hapa?" alihoji.





MSICHANA AFUNGIWA NA KUTESWA KWA MIAKA 9

Polisi nchini Argentina wamemwokoa msichana mwenye umri wa miaka kumina mitano ambaye alifungi wakatika chumba cha kuegesha magari na kunyimwa chakula pamoja na kupigwa na wazazi waliokuwa wamemuasili, kwakipindi cha miaka tisa.

Msichana huyo alikuwa na uzani wa kilo ishirini pekee.

Viumbe wa pekee walioishi naye ni mbwa pamoja na Tumbili.

Msichana huyo amesema alipigwa kila mara iwapo angejaribu kula mabaki ya chakula kilichotupwa kwa wanyama hao.

Amesema alifanikiwa kuondoka katika eneo hilo la kuegesha magari mara mbili tu katika kipindi cha miaka tisa.

Walezi wake wamekamatwa na kufunguliwa mashItaka ya kumdhulumu na kumweka kama mtumwa msichana huyo.

Msichana huyo ambaye amelazwa hospitlaini, alipatikana na dadake wa kuzaliwa naye mjini Buenos Aires.

Kwa mujibu wa maafisa wakuu, wazazi hao walimuasili mwaka 2001 baada ya mahakama kuamuakuwa wazazi wake wa kumzaa hawakuwa na uwezo wa kifedha kuweza kumlea.

Walikuwa wanasubiri stakabadhi za kukamilisha mpango wa kumuasili mtoto huyo.

WAISILAMU KUTOPELELEZWA TENA NEW YORK

Idara ya polisi mjini New York Marekani, imefunga kitengo chake maalum cha ujasusi ambacho huwapepeleza waisilamu ili kuchunguza kama kuna tisho lolote la ugaidi.

Kitengo hicho kilikuwa kinatumia polisi waliokuwa wanavalia nguo za kiraia kusikiliza kisiri mawasiliano ya simu kati ya waisilamu na hata kuzuru maeneo yanayotembelewa sana na waisilamu.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinasema kuwa kitengo hicho kiliwahi kushitakiwa mara mbili kwa mbinu zao za ujasusi na pia kulaaniwa na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu.

Pia kiliwaghadhabisha waisilamu hasa kwa kuwachunguza.

"mageuzi haya ni hatua muhimu sana katika kuondoahali ya wasiwasi na kutoaminiana kati ya polisi najamii ili jamii iweze kusaidia polisi kuwashika wahalifu,'' ilisema taarifa kutoka katika ofisi ya meya wa New York Bill de Blasio.


'Vita vya kisaikolojia'

Hatua ya kusitisha mpango huo, ilifikiwa na kamishna mpya wa polisi wa kituo hicho, na inaonekana kama njia moja ya kubadili mbinu za kukusanya ujasusi ambazo wengi wanasema zilichangia mashambulizi ya Septemba 9/11

Kitengo hicho, kilichoanzishwa mwaka 2003,na baadaye kuitwa, ' Zone Assessment Unit ' kilipeleleza waisilamu hasa maeneo walikofanya kazi, kuswali, kununua madukani na hata mikahwa walikokuwa wanakulia.

Wakuu wa kitengo hicho wanasema kuwa kazi yao iliathiri sana uhusiano kati ya jamii na polisi

JUHUDI ZA UOKOAJI ZAENDELEA KOREA KUSINI

Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara zadharura zilizoripotiwa kutoka meli moja iliyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini.
Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo wanatumia, meli za wanamajiwa Korea pamoja na ndege za uokoaji kuwaokoa watu waliokuwa katika meli hiyo.
Shughuli zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry hiyo.
Jeshi la wanamaji likishirikiana na maafisa wanaolinda usalama katika bahari ya rasi ya Korea wanasema watu wengi wamefanikiwa kuolewa.
Maafisa wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo imepata matatizo ikiwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju.
Waokoaji wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke baharini iliwaokolewe.
Walioshuhudia wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kuzama zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.
Shughuli ya uokoaji bado inaendelea.





UKAWA WASUSIA BUNGE

Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameondoka kwa hasira katika kikao cha bunge hilo kinachoendelea mjini Dodoma.

Hasira yao inatokana na madai kwamba maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya yamekuwa yakipuuzwa.

Wajumbe wa bunge hilo ambao ni kutoka upande wa upinzani chini ya umoja unaojulikana kama UKAWA, yaani Umoja wa Katiba ya Wananchi, wameamua kutoka nje kupinga kile wanachosema ni kupuuzwa kwa makusudi maoni ya wananchi wanaotaka muungano wa muundo wa serikali tatu kama yalivyopendekezwa katika rasimu ya katiba hiyo.


Kilio cha mwananchi

Akichangia katika kikao cha bunge hilo Jumatano jioni, mmoja wa wajumbe Profesa Ibrahim Lipumba amelalamikia kauli za ubaguzi zinazotolewa na baadhi ya wajumbe, hususan wanaotaka muundo wa muungano wa serikali mbili, alieleza sababu za kutaka serikali tatu kuwa zitasaidia kutatua matatizo yaliyopo katika muundo wa sasa.

Hata hivyo hakusita kupinga kile anachokiita kauli za ubaguzi kutoka kwa wajumbe wanaopinga mawazo ya wachache bungeni humoi.

"Hatuwezi kuwa kama kundi la wapiganaji linalohamamisha ubaguzi ndani ya Tanzania, hili hatulikubali, hatulikubali, hatulikubali, watu wote tunaotaka katiba ya wananchi tunawaachia muendelee na kikao chao. Ahsanteni sana".

Mara baada ya kusema hivyo, wajumbe waliounga mkono kauli yake waliinuka na kutoka nje.

Hata hivyo, kikao cha bunge hilo kiliendelea baada ya makamu mwenyekiti wa bunge hilo kusema idadi ya wajumbe waliobaki walitosha kuendelea na kikao hicho.


Muundo wa serikali

Wanaounga mkono muundo wa serikali tatu, wanasema muundo wa sasa wa serikali mbili umeshindwa kutatua masuala yenye mgogoro katika muungano, maarufu kama kero za muungano, hivyo kudhoofisha muungano huo.

Hata hivyo wajumbe wanaounga mkono serikali mbili, yaani serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanasema muundo wa serikali tatu ni kuvunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar na pia itakuwa gharama kuiendesha serikali ya tatu.Bunge hilo lenye zaidi ya wajumbe mia sita linaundwa na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la wawakilishi Zanzibar na wajumbe 201 walioteuliwa narais wa Tanzania kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.

Wajumbe 191 kutoka upinzani walitoka nje ya bunge kupinga mwenendo wabunge hilo katika kujadili rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

PICHA YA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI KIM JONG-UN YAZUA GUMZO

Viongozi wa Korea Kaskazini walitembelea saluni moja iliyoko mjini London, kutaka kujua ni kwa nini walitumia picha ya kiongozi wao Kim Jong-un katika bango la kibiashara.
Bango hilo lenya picha ya rais huyo, lilitumiwa kutangaza kupunguzwa kwa bei ya kunyolewa katika saluni moja.
Bango hilo katika M&M Hair Academy lilikuwa na picha ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini pamoja na maneno "Bad Hair Day?" yaani je unahitaji kutengezwa nywele?....
Kinyozi kwa jina Karim Nabbach alisema kuwa maaafisa wa ubalozi wa Korea walifukuzwa na mkurugenzi wa saluni hiyo walipojaribu kuingia katika saluni hiyo huku wakiwa wakali wa maneno.
Polisi nao kwa upande wao wamesema kuwa walizungumza na pande zote mbili husika na hakuna kosa lolote lilibainika.
Saluni hiyo ilibandika bango hilo tarehe 9 Aprili na keshoye wakapokea wageni wawili waliodai kuwa walikuwa maafisaa wa ubalozi wa korea kaskazini walio taka kumwona mkurugenzi wa saluni hiyo.
Karim Nabbach amenukuliwaakisema kuwa waliweka mabango ya kutangaza kupunguzwa kwa bei ya kunyolewa kwa wanaume katika mwezi Aprili.Bango hilo lilitokana na habari za hivi karibuni kuwa wanaume wa Korea wametakiwa kunyoa nywele kwa mtindo mmoja tu kama alivyonyolewa Rais Kim Jong Un.
Mkurugenzi wa saluni hiyo anasemekana kuwa aliwaeleza wageni wake kuwa walikuwa nchini uingereza nchi ya kidemokrasia na kuwataka waondoke kwenye saluni yake na kisha aliwafahamisha polisi kuhusu yaliyotokea pamoja na ubalozi wa Korea Kaskazini kuwa alikuwa amewasiliana na polisi.
Akizungumza na kipindi cha BBC radio 4 Karim Nabbach alisema kuwa kutoka wakati ule hawakupata shida yeyote ile na kuwa licha ya hayo bango hilo liliwavutia wateja wengi waliodhania kuwa lilikuwa la kuchekesha.
Wakati huo huo aliongeza kuwa bango hilo halikuwa linatumika kisiasa mbali lilitumika tu katika matangazoyao ya kibiashara ili kuwavutia wateja.
Mwezi uliopita Radio Free Asia iliripoti kwamba wanafunzi wa kiume katika vyuo vikuu vya korea kaskazini walitakiwa kunyoa nywele yao kwa mtindo sawa na ule wa kiongozi wao.








MTANDAO WA GOAL.COM WAIONGEZA TANZANIA KATIKA MTANDAO HUO

Mtandao wa goal.com umeiongeza Tanzania katika listi ya nchi itakapokuwa ikifanya huduma zake za kutoa taarifa za michezo kuanzia Taifa Stars, Ligi kuu ya vodacom, Uibuaji wa vipaji kufuatilia wachezaji wa Tanzania waliotapakaa kokote duniani.

The launch of the Goal Tanzania edition comes at a time when we are spreading our wings worldwide

The launch of the Goal Tanzania edition comes at a time when we are spreading our wings worldwide. After years of success covering world football, we are ready to devote a well-deserved edition to Tanzania.

We are driven by the vision and desire to bring you up to speed with the latest in Tanzanian football and this launch comes after the successful experience of launching other African editions, Goal Nigeria, Ghana, Kenya and South Africa.

The launch of Goal Tanzania will bring the number one sport a step closer to the people of the football-loving nation and we promise not todisappoint in delivering the goods.

We will dedicate a great deal of effort, time and energy in offering unrivalled coverage of the Taifa Stars, the Vodacom Premier League, grassroots football, and Tanzanians plying their trade around the world.

We promise to not only inform, but also to entertain with well researched articles and editorials. Our match reports will not only be timely but also accurate and well balanced. Our promise isto represent the Tanzanian people with a Goal voice.

We believe that the media has an important role in the improvement and continued growth of local football, and we are pleased to play our part in making the league better and seeing it flourish.

Our dedicated team of sportsjournalists have a wealth of experience in the industry, and we will go beyond the call of duty to give you exclusive interviews with the Tanzania football news-makers, be they on or off the pitch.

We will uncover Tanzania's young talent and give them a platform from which they will strive to reach the heights of their footballing careers, wherever that may take them.

So whether you access your football news and views via the web, mobile or through our various apps, you know that you can count on Goal Tanzania to provide you with the latest news, insightful commentary and worldwide match coverage.

April 15th is a new dawn in Tanzanian football, and we are here to serve the Tanzanian people. Join us in pursuing this dream at http://www.goal.com/en-tz. Welcome and enjoy!
Karibuni sana.

MZEE MTEI ASIKITISHWA NA TUNDU LISSU KUMKASHIFU MWL. Jk

Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.

Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha.

Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.

Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu.

Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke:
Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao.

Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

JAMAA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJITOSA MAJINI KUTAFUTA BAISKELI

Mtu mmoja amenusurika kifo kwa kujinusuru katika kichaka katikati ya maji yanayo kwenda kasi akisubiri kuokolewa katika eneo la ruvu mkoani Pwani baada ya kuzidiwa nguvu na maji alipojitosa kwenye maji kwa nia ya kutafuta baiskeli yake huku hali ya usafiri ikitarajiwa kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya maji kupungua huku wakandarasi kutoka Tanroad wakihangaika kutengeneza maeneo yaliyoharibiwa na mvua.

Wakisimulia tukio hilo mashuhuda wamesema kuwa mtu huyo alijitosa mwenyewe kwenye maji kwa nia ya kutafuta baiskeli yake aliyodai imesombwa na maji na kisha kuzidiwa nguvu na kasi ya maji katika eneo hilo na kisha kunasa katika kichaka akisubiri kuokolewa huku baadhi ya mashuhuda wakiwa kando wasijue la kufanya kumnusuru.

Katika tukio jingine limeshuhudiwa msururu mkubwa wa magari ukisubiri kupita katika eneo la mto ruvu ambapo baadhi ya wasafiri waliokwama katika eneo hilo wakielezea tabu wanayoipata pamoja na kuwa na hofu ya kuibuka maradhi kutokana na wingi wa watu wanaojisaidia hovyo katika vichaka.

Aidha maji yaliyokuwa yamefunika barabara katika eneo la daraja la mto Ruvu yamepungua huku magari nayo yakiruhusiwa kupita moja moja wakati makandarasi kutoka tanroads wakiendelea kukarabati eneo ambalo lilimong`onyolewa na maji huku eneo zima linalozunguka mto ruvu likiwa limezungukwa na maji na baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakioneka kutega nyavu bila kujali hatari inayoweza kuwapata.

Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoani Pwani Ulrich Matei amesema licha ya msongamano mkubwa wa magari hali ya usala katika eneo hilo ni kubwa kutokana na kupata msaada kutoka kwa vijana wa JKT Ruvu na kwamba katika kipindi kifupi kijacho hali ya usafiri itarejea katika hali yake ya kawaida.

WASICHANA 200 WATEKWA NIGERIA

Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa shule ya mabweni ya wasichana imeshambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo huku wasichana wakitekwa nyara.

Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao.

Washambuliaji wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram. Utekaji nyara huo ulifanyika usiku wa manane katika shule ya Chibok ksuini mwa mji wa Borno , karibu na mpaka na Cameroon.

Inaarifiwa wasichana 300 walikuwa wanajiandaa kwa mitihani yao. Mmoja wa wasichana alifanikiwa kutoroka na aliambia BBC kuwa walikuwa wanalala wakati walipovamiwa na wanaume waliokuwa wamejihami.

Walio washambulia wanaaminika kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Wanaume hao waliingiza magunia ya chakula katika malori yaona kuwaamuru wasichana kuyapanda malori hayo.

Wasichana 15 walifanikiwa kutoroka baada ya lori walimokuwa kukumbwa na hitilafu.

Wakazi wa kijiji cha Chibok wanasema kuwa walisikia milipuko kadhaa huku nyumba 170 zikiteketezwa.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili waliuawa huku mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo mjini Chibok.

Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi yawatu 70, waliuawa katika milipuko miwili ya mabomu katika kituo cha mabasi mjini Abuja.

Kundi la Boko Haram pia limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.

MARUFUKU KUTEMBEA KIFUA WAZI KATIKA BUSTANI UINGEREZA

Wanaume wanaovua mashati wamepigwa marufuku kuitembelea bustani ya mapumziko na kujivinjari ya Adventure Island.

Ni eneo ambalo watu wanakwenda kujivinjari na familia zao, kwa kutazama wanyama, watoto hupata kubembea na pia watu huota jua.

Bustani hiyo iliyopo mjini Southend nchini Uingereza, imeweka ilani zinazowaomba wanaume wasivue mashati yao, na kwamba watakao patikana watafukuzwa.

Mkurugenzi mkuu, Marc Miller, amesema anataka wanaume waonyeshe "ustaarabu".

Bustani hiyo inasifika duniani kwakuwa na idadi kubwa ya watu walio uchi walioipanda bembea ya 'Rollercoaster' - licha ya kwamba ni jambo linalofanyika faraghani.

'Kuilenga Familia'

Zaidi ya watu 100 walivua nguo ilikuipanda bembea hiyo ijulikanayo kama Green Scream mnamo 2010.

Miller anasema: "Katika miaka yahivi karibuni, tumekuwa tukiongeza idadi ya vijana na wanaume ambao huvua mashati yao ili kupata joto la jua kwa wingi. Hilo ni sawa kabisa lakini katika mazingira yanayofaa".

"Tunajaribu sana kufanya biashara inayoivutia familia na sio kila mtu anavutiwa kuona vifua wazi".

Pamoja na kuwa na idadi kubwa duniani ya watu wasio vaa nguo, Adventure Island pia ilijaribu kuweka rekodi mpya ya kuwa na watu wengi wanaocheza mpira wagofu wakiwa uchi, mnamo mwaka 2012.

Msemaji mmoja anasema michezo yote hufanyika faraghani.

"Wanaohudhuria michezo hiyo ni waliojisajili kushiriki, ili kuchanga fedha nyingi za misaada ya kukabiliana na magonjwa kama saratani ya matiti na ya uume," alisema.

"Marufuku hiyo imetolewa wakatibustani imefunguliwa kwa umma."

DK. BILALI MKUMZIKA GURUMO LEO

Makamu wa Rais Dk.Gharib Bilal anatarajiwa kuongoza msafara wa mazishi ya mwanamuziki nguli Muhidin Maalim Gurumo yatakayofanyika leo katika Kijiji cha Masaki Wilaya ya Kisarawe Pwani.

Dk. Bilal ataambatana na viongozi wengine wa Serikali na wasanii mbalimbali katika mazishi ya nguli huyo aliyefariki Aprili 14 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo uliomsumbua kwa muda mrefu.

Akizungumza jana nyumbani kwa marehemu Mabibo External, msemaji wa familia Yahya Mikole alisema marehemu anatarajiwa kuzikwa leo mchana, nyumbani kwao Masaki kabla ya kusomewa dua asubuhi ya saa tatu nyumbani kwake jijini.

Mke wa mwanamuziki huyo Pili Kitwana akizungumza kwa uchungu, alisema kuwa haamini kama mtu aliyeishi naye kwa miaka zaidi ya 40, amemtoka.

"Ninachoweza kusema ni kumshukuru Mungu kwa kuwa kazi yake haina makosa, namuombea apumzike kwa amani."

Wakati huohuo;Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemtuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwanamuziki huyo.

"Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Muhidini Maalim Gurumo ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wa muziki wa dansi nchini, waliolitumikia Taifa hili kwa bidii tangu miaka ya sitini kupitia sanaa ya muziki katika bendi mbalimbali za muziki wa dansi, kuanzia Bendi ya NUTA Jazz, Mlimani Park Orchestra, Orchestra Safari Sound (OSS) na Msondo Ngoma ambayo ameitumikia hadi alipostaafu mwaka 2013", alisema Rais Kikwete katika salamu zake.

OSCAR PISTORIURG AMALIZA KUJITETEA

Upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji dhidi ya Oscar Pistorius umemaliza kumhoji mwanariadha huyo.

Oscar aliyekatwa miguu yote miwili anakana kutekeleza mauaji hayo akisisitiza kwamba alidhani marehemu Steenkamp alikuwa jambazi aliyevamia nyumba mwake.

Anakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka 25 au maisha gerezani, iwapo atapatikana na makosa ya mauaji ya kupangwa.

Kabla ya kuanza kusikizwa kesi hiyo, mwendesha mashitaka Gerrie Nel alisema kuwa alitumai kumaliza kumhoji mwanariadha huyo siku ya Jumanne.

Alimuomba Jaji Masipa aahirishe kesi wakati wa mapumziko ya pasaka hadi tarehe 5 Mei.

Ameeeleza kwamba mawakili wenzake wanakabiliwa na kesi nyengine 'nzito zaidi' wanazostahili kuzishughulikia pamoja na 'masuala ya kibinafsi'.

Ombi hilo liliungwa mkono na upande wa utetezi, uliosema kwamba kesi hiyo inapaswa kumalizika tarehe 16 Mei kama ilivyopangwa. Jaji alisema atatoa hukumu yake ya ombi hilo siku ya Jumatano.

Siku ya Jumatatu, Bwana Nel alipendekeza kwamba Pistorius anajifanya kuzidiwa na hisia kuficha matatizo anayopata kujibu masuali mazito anayoulizwa.

Jaji Thokozile Masipa alisitisha kwa muda kesi hiyo mara mbili siku ya Jumatatu baada ya Pistorius kuanza kulia.

Muda mfupi kabla kesi kumalizika kwa siku, Nel alisema:" unazidiwa na hisia sasa kwa sababu unaudhika, kutokana na kuwa ushahidi wako huenda si wakweli.

"Mwendesha mashtaka huyo anayejulikana kwa mtindo wake wa kutishia watu anapowahoji, baadaye alimuuliza Pistorius: " Hautumii hisia zako kukwepa kujibu maswali?"

Pistorius alisema akili yake haikumanika kama inavyostahili wakati wa ufyetuaji risasi huo.

Awali, kwa mara nyengine Nel alimdadisi kwa uzito Pistorius kuhusu wakati alipompiga Bi Steenkamp risasi.

Mwanariadha huyo alisisitiza kwamba hakuna na nia ya kumuua mtu yoyote, alisema: "Nilifyetua risasi kutokana na uoga."

Nel baadaye alisema kwamba Pistorius alibadili ushahidi wake kutoka kusema alikuwa akijikinga na hadi kusema kwamba alifyetua risasi kwa makosa.

Mwendesha mashtaka akasema hii ni kutokana na kuwa ukweli ni: "Ulimfyetulia Reeva risasi."

"Sio kweli," Pistorius akajibu, huku akibubujikwa kwa machozi na kuilazimu mahakama kusitisha vikao kwa muda.

Pistorius alisema yeye na marehemu Steenkamp walibarizi jioni pamoja kabla ashutuke usingizini kutokana na kusikia sauti iliyotoka bafuni.

Mashahidi wa upande wa mashitaka walieleza kusikia mwanamke aliyepiga mayowe, lakini upande wa utetezi unakana ushahidi huo.

BALOZI WA JORDAN ATEKWA TRIPOLI

Balozi wa Jordan nchini Libya ametekwa nyara mjini Tripoli, katika shambulizi ambalo limemwacha dereva wake na majeraha mabaya.

Maafisa wakuu kutoka wizara ya mambo ya ndani wamethibitisha tukio hilo, wakisema kuwa dereva wake anapokea matibabu.

Ubalozi wa Jordan mjini Tripoli pia umethibitisha taarifa hiyo bila ya kutoa maelezo zaidi.

Libya imekuwa ikizongwa na misukosuko tangu makundi ya wapiganaji kumuondoa mamlakani hayati Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Haijulikani nani ametekeleza shambulizi hilo.

Mnamo mwezi Januari, wafanyakazi watano wa ubalozi wa Misri walitekwa nyara mjini Tripoli kwa siku chache kabla ya kuachiliwa huru.

Makundi ya wapiganaji yamekuwa yakilaumiwa kwa kutekeleza visa kadhaa vya utekaji nyara wa maafisa wakuu nchini Libya

Mara kwa mara hulipwa na serikali ili kuwaachilia watu waliotekwa nyara ingawa haijulikani yanaongozwa na nani.

BERLUSCONI ADHIBIWA NA MAHAKAMA

Waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi, amepewa kifungo cha nje na kushuritishwa kufanya kazi ya kuhudumia jamii kwa mwaka mmoja.

Mahakama moja mjini Milan imetoa adhabu hiyo kwa Barlusconi kutokana na kesi yake ya kukwepa kulipa kodi.

Mahakama ya juu zaidi ilikuwa imemhukumu jela Berlusconi lakini kwa sababu ya umri wake alitakiwa kuchagua kati ya huduma kwa jamii na kifungo chanyumbani.

Mawakili wa Berlusconi walimuombea adhabu ya kufanyakazi na kuhudumia jamii na mahakama ikakubali.

Berlusconi mwenye umri wa miaka 77 tayari amepigwa marufuku kugombea katika uchaguzi mkuu kwa miaka sita.

Alipatikana na hatia ya kosa hilo katika kashfa iliyohusu ununuzi wa haki miliki ya televisheini katika kampuni yake ya utangazaji, Mediaset.

Haijulikani kazi atakayoifanya Berulsconi kama adhabu yake ya huduma kwa jamii lakini duuru nchini humo zinasema kuwa huenda akafanya kazi katika makao ya kuwahudumuia watu wenye ulemavu.

Bilionea huyu amekuwa akikumbwa na kesi nyingi mahakanai kutokana na kashfa mbali mbali.

BARCLAYS KINONDONI YAVAMIWA

Watu wasiojulikana wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia benki ya Barclays tawi la Kinondoni nakupora kiasi kikubwa cha fedha ambazo idadi yake haijajulikana mara moja.

Tukio hilo limetokea muda huu saa nne , katika tawi la benki hiyo iliyopo Kinondoni eneo la Bakwata likihusisha watu watatu waliokuwa na pikipiki mmoja wao akiwa na bastola. Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova amefika katika eneo la tukio na kuahidi kuanzaupelelzi mara moja.

PUTIN NA OBAMA WAFANYA MAZUNGUMZO

Rais wa Urusi Vladimir Putin na rais wa Marekani Barack Obama wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu.

Masuala mbali mbali kuhusu mzozo wa Ukraine, hususan upinzani wa wanaharakati wa kusini mashariki mwa taifahilo dhidi ya sera za serikali ya sasa ya Kiev yamejadiliwa baina ya viongozi hao.

Afisa wa ngazi ya juu wa ikulu ya White house amesema mazungumzo hayo yamefanyika kwa ombi la Urusi na yalikuwa ya kirafiki na ya moja kwa moja.

Ikulu ya White House inasema Rais Obama amesema wazi kuwa Marekani ingetaka mzozo kati ya Urusi na Ukraine usuluhishwe kwa njia ya kidiplomasia.

Hata hivyo amesikitika kuwa vitendo vya Urusi katika siku za hivi karibuni havionekani kuzingatia hilo.

Katika mazungumzo hayo Rais waUrusi Vladmir Putin amesisitiza kuwa maandamano yanayofanyika kusini mashariki mwa Ukraine ni kutokana na nchihiyo kutojali maslahi ya Urusi na raia wanaozungumza Kirusi.

Amemuomba Rais Obama kutumia raslimali za Marekani kuzuia umwagikaji damu.

Marekani na Urusi zimelaumiana kwa kuingilia kati maswala ya Ukraine huku Urusi ikilalamika kuhusu ziara ya mkuu wa idara ya ujasusi ya Marekani mjini Kiev.

Mazungumzo hayo yameonyesha wazi jinsi misimamo ya Marekanina Urusi kuhusu hali ya baadaye ya Ukraine ilivyotofautiana Wakati huohuo, Umoja wa Ulaya na Marekani zinapangia kuiongzezea vikwazo Urusi.

Mawaziri wa maswala ya kigeni wa Ulaya jana waliafikiana kuongeza idadi ya watu watakao wekewa vikwazo vya kiuchumi na usafiri.

Mawaziri hao waliokutana huko Luxembourg walikubaliana kuipa Ukraine msaada ya dola bilioni moja nukta nne mbali na kuiondolea taifa hilo vikwazo vya kodi kwa muda katika muungano huo.

Kauli hiyo inawadia huku taharuki ikitanda katika miji ya mashariki mwa Ukraine ambapo makundi ya waandamanaji wanaunga mkono Urusi wakivamia makao makuu ya serikali ya Kiev na kuziteketeza moto.

Marekani ilisema kuwa ndege ya kivita ya Urusi ilipaa karibu sana na manuari ya kivita ya Marekani katika bahari ya Black sea.

Huko Washington, mkutano bainaya waziri wa maswala ya kiuchumi wa Marekani Jacob Lew na mwenzake kutoka Ukraine , Oleksandr Shlapak uliafiki na kutia sahihi mkopo wa dola bilioni moja.

Awali Kaimu rais wa Ukraine Olexander Turchynov aliwaonya waasi kuwa watakabiliwa na vikosi vya jeshi kutoka Kiev huku akiiomba Umoja wa mataifa kuingilia kati katika operesheni hiyo.

KINANA AGEUKA MBOGO

KATIBU Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, amejikuta akigeuka mbogo na kuwaomba radhi wakazi wa kata ya Kirema, wilayani Mpanda mkoani Katavi, baada ya kubaini kuwa, watendaji wa Serikali wamempatia zabuni ya ujenzi wa bandari nne mkandarasi asiye na uwezo kifedha na kitaalamu.

Kutokana na hali hiyo, Kiongozi huyo, amesema chama chake kamwe hakitowavumilia watendaji wanaoendekeza vitendo vya urasimu na umangimeza wa kutumia makaratasi ofisini badala ya kuwatumikia wananchi kwa kuwajibika ipasavyo.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa gati ya bandari ya Kirema na baadaye katika mkutano wa hadhara walayani hapo, alisema ni jambo laaibu kwa watendaji wa Serikali kumuachia mkandarasi asiye na sifa miradi muhimu kwa muda wa miaka mitatu bilo kufuatilia utendaji wake.

Mkandarasi huyo wa Modispan Enterprises Limited, pamoja na mradi huo wa ujenzi wa gati katika bandari hiyo ya Karema ambayo thamani yake ya ujenzi ni Sh bilioni 1.5, pia anajenga gati katika bandari za Mwangosa, Sibwete na Lupili.

Alisema atahakikisha analifikisha suala hilo katika vikao vya juu na kulivalia njuga ili kubaini mkandarasi huyo ni nani, alipataje zabuni hiyo na akina nani walihusika kumpatia na kwanini hadi leo hajachukuliwa hatua za kunyang'anywa miradi hiyo isiyoendelea.

Pamoja na suala hilo la bandari pia Kinana alitembelea mradi wa ujenzi wa Mwani ambao utatumika kama soko na eneo la kuhifadhia samaki ambako nako, alikuta mradi huo, umechelewa kukamilika na kupitisha miaka miwili ya zaidi ya muda uliopangwa kwenye mkataba.

"Hili ni tatizo kubwa katika maeneoyote niliyopita kwenye ziara yangu, nimekumbana na adha hii ya miradi kusimama, kuchelewa na mingine kutelekezwa kwa sababu ya kuchelewa kwa fedha, na hata zikija ni kidogo hazitoshi," alisema.

Aliitaka Serikali kuanza kuchukua hatua za haraka za kurekebisha kasoro hiyo, kwa kuhakikisha fedhaza miradi zinafika maeneo husika kwa wakati muafaka lakini pia kuhakikisha watendaji wasiowajibika wanachukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa.

Awali wakati Kinana akitembelea mradi huo, Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso, alimtaarifu kiongozi huyo, kuwa mkandarasi aliyepewa mradi huo wa bandari ambaye ni Modispan Enterprises, hana uwezo wala utaalamu wa kuukamilisha na jinsi ulivyo ni kama umetelekezwa.

Alisema akiwa kama mbunge aliwasiliana na Serikali kupitia Naibu Waziri wa zamani wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba na kumueleza hali halisi na baadae aliwasiliana na Naibu waziri wa sasa wa wizara hiyo, Dk Charles Tizeba na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ambao walimuahidi kushughulikia suala hilo.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya Karema, Michael Kapata, alimuomba Kinana, aingilie kati suala hilo la ujenzi wa bandari kwa kuwa muda mrefu limekuwa likisababisha CCM ichukiwe na wananchi, kwa kuwa mradi huo haueleweki.

TUNDU LISSU ATIKISA BUNGE

Mjumbe wa Bunge laKatiba, Tundu Lissu amesema Tanganyika ilikufa kwa amri iliyotolewa na Mwalimu Julius Nyerere na siyo kwa makubaliano katika hati ya Muungano.

Lissu alitoa kauli hiyo jana alipopata fursa ya kukamilisha dakika 16 za hotuba yake ya ufafanuzi wa maoni ya walio wachache iliyokuwa imekatishwa baada ya matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni ya Taifa (TBC1) kukatika Jumamosi iliyopita.

Huku akinukuu maneno yaliyopo katika vitabu vilivyoandikwa na Profesa Issa Shivji na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, Lissu alisema Jamhuri ya Muungano ilizaliwa bila uhalali wa kisheria kwa kuwa hayakuwapo makubaliano ya kila upande wa Muungano.

Alisema Aprili 26, 1964 (Siku ya Muungano), Mwalimu Nyerere alitoa amri ya masharti ya mpito yamwaka 1964 ambayo pamoja na mambo mengine iliifuta Tanganyika. Akichambua kitabu cha '50 Years of Independence: A Concise Political History of Tanzania' (Miaka 50 ya Uhuru: Historia fupi ya Tanzania), kilichoandikwa na Msekwa na kuchapishwa Januari mwaka huu, Lissu alisema: "Msekwa anasema katika kitabu hicho kuwa amri hiyo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali la siku hiyo. Kwanza, iliwabadilisha waliokuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano."

Alisema hata Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Tanganyika iligeuzwa kuwa nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.

Alisema tarehe hiyohiyo, Mwalimu Nyerere alitoa amri ya Katiba ya muda ya mwaka 1964 na ilitangaza kuwa Katiba ya Tanganyika ndiyo iwe Katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano.

"Kifungu cha nne cha amri hii ndicho kilichoipatia Serikali ya Muungano majukumu kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano yote na vilevile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika," alisema Lissu huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo.

Alisema Juni 15, 1964, Mwalimu Nyerere alitoa amri nyingine iliyoitwa 'Amri ya Masharti ya Mpito' ambayo ilieleza kwamba mahali popote ambako sheria zilizokuwapo zimetaja jina la 'Tanganyika' basi jina hilo lifutwe nabadala yake jina la 'Jamhuri ya Muungano' liwekwe.

Huku akimnukuu Msekwa, Lissu alisema kigogo huyo wa CCM katikakitabu chake amesema, "Uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za jumla za amri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndiyo ilikuwa Tanganyika lilitolewa uhai wake moja kwa mojakwa amri. Hii ndiyo sababu hata jina la eneo la kijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi libadilishwe na kuwa Tanzania Bara."

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lissu aliyoitoa jana, Msekwa alisema: "Kitabu kipo na ukikisoma kwa umakini utagundua kuwa alichokisema Lissu siyo ambacho kimeandikwa. Sasa umhoji kuhusu hayo aliyoyasema, muulize ameyapata wapi?"


Kuhusu Shivji

Akimnukuu Profesa Shivji katika kitabu chake 'Pan Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika– Zanzibar Union', Lissu alisema Profesa huyo ameeleza kuwa Muungano huo ulilazimishwa.

"Profesa Shivji amethibitisha kwamba kile kinachoitwa Sheria ya Kuthibitisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964 iliandaliwa na kuandikwa na maofisa wa sheria wa Tanganyika wakiwa Tanganyika," alisema.

Alisema kuwa Profesa huyo ameeleza sababu ya ukweli wa kisiasa uliokuwapo wakati huo ambao Baraza la Mapinduzi kwa jumla wake halikukaa kuukubali Muungano.

"Profesa Shivji alisema hakuna shaka kwamba Muungano 'ulilazimishwa.' Hivyo, maofisa wa kisheria wa kigeni wa Serikali ya Tanganyika (waliokuwa pia marafiki wa Nyerere) walitumia mbinu ya kisheria ya kuchapisha Sheria ya kuthibitisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka 1964," alisema huku akikatishwa mara kwa mara na wajumbe waliokuwa wakiomba miongozo ya mwenyekiti.

"Profesa ameeleza kuwa, kwa sababu utaratibu huo ulikiukwa, kitendo cha kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika hakikupata baraka za Baraza la Mapinduzi na kuthibitishwa na kikao halali cha Baraza la Mawaziri la Zanzibar," alisema Lissu na kuongeza: "Jamhuri ya Muungano ilizaliwa bilauhalali wowote wa kisheria kwa maneno ya Profesa Shivji."

Alisema hata aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, SalimSaid Rashid kati ya Januari 18 na Juni 1964, alitamka kuwa:

"Hakuwahi kupokea maagizo kutokakwa Rais wa Zanzibar kwa ajili ya kuitisha kikao cha kujadili na kupitisha mkataba wa kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika," alisema Lissu.

Alisema katika kitabu hicho, Profesa Shivji alieleza jinsi Rashid alivyoeleza utaratibu wa kisheria uliotakiwa kufuatwa: "... Kwa mujibu wa amri ya mwaka 1964; kila jambo lilitakiwa kujadiliwa na kikao cha Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu kuarifiwa atayarishe 'presidential decree' kwamujibu wa utaratibu."

Alisema baadaye yeye (Rashid), akiwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri Zanzibar alitakiwa asaini na kisha Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na baadaye kutolewa katika gazeti la Serikali.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo ya Lissu kuhusu kitabu chake, Profesa Shivji alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno akisema: "Itakuwa vizuri ukisoma wewe mwenyewe."


Mbowe: Takwimu za Tume zimetengenezwa na vigogo wa Serikali

Akichangia maoni ya walio wachache kutoka Kamati Namba Nane, Freeman Mbowe alisema kitendo cha wajumbe wanaotokana na CCM kubeza takwimu za Tume ya Jaji Joseph Warioba ni kuwakana Watumishi wa Serikali akisema ilikuwa na watumishi wa Serikali 190 wakiwamo wanasheria waandamizi.

"Tunapohukumu Tume imefanya kazi chafu ya kuchakachua takwimu hizi, mjue zimetengenezwa na watumishi waandamizi kutoka Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar. Kwa hiyo wanaobeza taarifa ya Tume, wajue wanaikana Serikali, wanawakana watu ambao wana dhamana ya kusimamia nchi hii," alisema na kuongeza:

"Tunapata wapi ujasiri wa kuwadhalilisha wajumbe wa Tume ya Rais iliyoongozwa na Warioba?... Tume iliyojaa viongozi walioitumikia nchi hii kwa uaminifumkubwa, tunafanyaje jambo hili?"

Mbowe alisema Jaji Warioba aliwahikushika nyadhifa mbalimbali za juu ikiwamo Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais na kuhoji wajumbe wanapataje ujasiri wa kuwadhalilisha. Aliwataja wajumbe wengine wa tume hiyo wanaoheshimika kuwa ni pamoja na Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhan na Waziri Mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim.

Mbowe pia alishangaa kiwango cha fedha kilichotumiwa na tume hiyo Sh68.88 bilioni kufanya utafiti ambao leo wajumbe walio wengi kutoka CCM wanaukana.

Alisema endapo wajumbe wanapuuza msingi wa Rasimu iliyotokana na Tume ya Jaji Warioba, ni vyema Bunge hilo lisiwepo ili CCM wakae upya na kutengeneza rasimu wanayoitaka ya serikali mbili. Alisema Tanzania haiwezi kupata Katiba Mpya kwa uongo na rushwa na kuzuia watu kujadili kasoro za muungano kwa uhalisia wake.


Jussa awabana mawaziri SMZ

Akitoa ufafanuzi kuhusu maoni ya wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Sita, Ismail Jussa aliwabana mawaziri watatu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kwa kushindwa kueleza udhaifu wa muundo wa serikali mbili bungeni wakati kwenye semina ya Baraza la Wawakilishi kuhusu mchakato wa katiba walisema hivyo wazi.

Alisema mawaziri hao walilalamikia jinsi wanavyodhalilishwa na muundo wa serikali mbili wanapokwenda nje ya nchi.

"Kuna rekodi hata ya CD, siyo ya Hansard tu (kumbukumbu rasmi za Bunge), hata ukiitaka mheshimiwa mwenyekiti nitakupatia. Haya yalikuwa katika semina ya Baraza la Wawakilishi iliyoitishwa na Spika wetu, Mzee Pandu Ameir Kificho," alisema.

Aliwataja mawaziri hao kuwa ni Dk Mwinyi Haji Makame, Haroun Ally Seleman na Omary Yusuf Mzee. "Walichofanywa Dodoma sijui mheshimiwa mwenyekiti, lakini wote pamoja na wengine walionyesha jinsi mfumo huu (serikali mbili) hautusaidii Zanzibar na umetukwamisha," alisema.

Alitoa mfano mwingine kuwa kuna siku Zanzibar walikuwa wakijadili muswada wa utalii ambapo yeye alipendekeza waweke kipaumbele cha ajira kwa Wazanzibari kwa kuwawizara hiyo si ya Muungano na kilikataliwa.

"Mimi na Asha Bakari tu wa CCM tulitoka nje na akalalamika kuwa wenzake wamemgeuka. Kwa tabia hii mheshimiwa mwenyekiti tunapokuwa Zanzibar, tunasema wengine tunapokuja Dodoma tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu," alisema.

Awali akisoma maoni ya walio wengi, Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita, Stephen Wassira alisema walio wengi walipendekeza muundo wa serikali mbili kwa sababu unatoa fursa kubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa pande zote mbili na kuondoa tabaka la ukabila na udini ndani ya Jamhuri.

"Mfumo wa serikali mbili ukifanyiwa marekebisho ya kikatiba utaondoa kero na manung'uniko ambayo yameelezwa kuwa msingi wa mapendekezo ya Tume ya kutaka mfumo wa serikali tatu," alisema.

Chanzo: Mwananchi

MAELFU WA ABIRIA WAKWAMA UBUNGO

Uharibifu wa barabara uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha, umeendelea kuwatesa wakazi wa Dar es Salaam na mikoa mbalimbali nchini hasa baada ya mabasi ya mikoani kuzuiwa kufanyasafari zake jana.

Amri ya kuzuia mabasi hayo ilitolewa jana ikiagiza mabasi yote yasiondoke katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo hadi itakapotangazwa vinginevyo, kutokana na uharibifu wa Barabara za Kilwa, Morogoro na Bagamoyo ambako madaraja yamevunjika.

Dereva wa Basi la Adventure liendalo Kigoma, Joseph Luciano alisema walitangaziwa na Sumatra na trafiki kuwa wasubiri mpaka hapo watakapojulishwa kuondoka.

"Hatuwezi kuondoka mpaka Serikali itakapotangaza ili kuepuka faini ambayo wenzetu, wale wanaopakia nje, wametozwa," aliongeza huku ikielezwa kuwa baadhi ya mabasi yalitozwa faini kwa kukiuka amri hiyo.

Abiria anayesafiri kwenda Kibondo,Kigoma, Lydia Lutakinikwa alisema: "Nilikuja kuchukua mzigo wa duka langu tangu Ijumaa na nimekuwa nikilala gesti. Nimeishiwa hela hivyo nalazimika kuendelea kuwapo kwenye hili basi kwa kuwa sina tena pesa ya kwenda kulipia malazi."

Kondakta wa Basi la Taqwa liendalo Nairobi, Yahaya Maulid alisema wameruhusu kubadilishwa tiketi za abiria wao, kama walivyoelekezwa na mamlaka husika ili kutoa nafasi kwao kujipanga upya.

Mkuu wa Usalama Barabarani Ubungo, Inspekta wa Polisi, Yusuf Kamutta alisema zaidi ya mabasi 400 yameathiriwa na uamuzi huo..."Tumezuia mawakala wasitoe tiketi mpya kwa sababu abiria wa leo (jana) ndiyo wanaotarajiwa kusafiri kesho, hivyo wanaweza kuuza tiketiza kuanzia kesho kutwa."

Msururu wa magari Pwani Kutokana na kuharibika kwa baadhi ya madaraja katika Mkoa wa Pwani, magari yaliyokuwa yakisafiri kutoka maeneo mbalimbali yalikwama katika maeneo tofauti.
Baadhi yalikwama Visiga na mengine Mlandizi jirani na Kituo cha Polisi katika misururu mirefu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei aliwataka wamiliki wa magari makubwa ya mizigo wanaotumia barabara hiyo kusitisha safari zao kwa kipindi hiki hadi hapo hali itakapotengamaa.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani na uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ililazimika kuweka kambi kwa siku nzima eneo la Mlandizi jirani na daraja la Ruvu kusimamia shughuli ya ukarabati wa daraja dogo lililokuwa na hitilafu.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani, Tumaini Sarakikya alisema hadi jana mchana magari yalikuwa yameanza kupita upande mmoja, lakini baadaye jioni yangeanza kupita bila wasiwasi.

IDADA YA WALIOKUFA KATIKA MAFURIKO YAFIKIA WATU 13

Idadi ya waliokufa kutokana na mafuriko jijini Dar es Salaam imefikia watu 13 kufikia Jumatatu.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sadiq Meck Sadiq amesema idadi hiyo huenda ikaongezeka baada ya kupata taarifa za matukio ya mafuriko kutoka maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa siku tatu mfululizo tangu Ijumaa iliyopita, mvua kubwa ziliendelea kunyesha na kusababisha madhara makubwa vikiwemo vifo, uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja, hivyo kukata mawasiliano na mikoa ya jirani ya Pwani na Morogoro na hata ndani ya mkoa wenyewe.

Karibu maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam yameathirika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko, huku wakaazi wa maeneo ya mabondeni wakiathirika zaidi baada ya nyumba zao kujaa maji.

Miundombinu ya barabara na madaraja mbalimbali yanayounganisha jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake pia imeharibiwa.

Mradi mwingine muhimu wa mabasi yaendayo kasi, DART unaolenga kutatua tatizo la usafiri jijini Dar es Salaam, nao umeathiriwa na mafuriko hayo ambapo magari, mashine na mifuko ya saruji imechukuliwa namaji hivyo kusitisha shughuli zake za ujenzi zilizo katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi huo.

Shughuli za urejeshaji wa miundombinu zimekuwa zikiendelea ikiwa ni pamoja na matengenezo katika daraja la Mpiji linaloiunganisha mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Hata hivyo Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania, TMA, yametahadharisha kuhusu kuendelea kunyesha kwa mvua na kuwataka watu wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhama ili kusalimisha maisha na mali yao.

WAKAMATWA KWA KULA MAITI YA BINADAMU

Ni visa mbavyo wengi tulivisikia katika hadithi za kale, watu kuliwa na majitu, lakini katika siku za karibuni tumeshuhudia watu wakila viungo vya wenzao Jamhuri ya Afrika ya Kati katika jazba yakulipiza kisasi dhidi ya watu waliowadhulumu katika uongozi uliongolewa mamlakani wa Seleka.

Nchini Pakistan Polisi wamewakamata wanaume wawili kwa makosa ya kuiba maiti ya mtoto kutoka kaburini na kisha kumla.

Wawili hao Arif Ali na kakake Mohammed Farman Ali waliachiwa huru baada ya kuwa jela kwa miaka miwili kwa kula nyama ya binadamu.

Hata hivyo wawili hao wameonekana kuwa na tamaa kubwa ya mchuzi wa nyama ya binadamu.

Wakaazi hao wa kijiji cha Daryabn Khan jimbo la Punjab walikamatwa mwaka 2011.

Polisi walisema kwamba walipata kiwiliwili cha maiti ya msichana mdogo kikiwa bila miguu na mikono.

Wawili hai walikiri kwamba walikua kapika mchuzi wa nyama ya viungo hivyo na kuvila.

Walishtakiwa kwa makosa ya kuharibu kaburi kwani nchini Pakistan hakuna sheria inayozungumzia hatia ya mtu kumla mwenzie.

Punde baada ya kuachiwa nguvu Arif Ali aliambia BBC kwamba anajutia makosa hayo na kwamba hatarudia tena.

Hata hivyo punde si punde polisi wamesema waliitwa na majirani ya jamaa huyo wakilalamikia uvundo mkali kutoka kwa nyumba yake.

Walipoingia chumbani humo Lo ! wakapata kichwa cha mtoto.

Kiwiliwili hakijulikani kililiwa au kapotelea wapi.

Arif Ali tena amekamatwa kwa mara ya pili na msako unaendelea kumsaka kakake.

Polisi wanaamini ndugu hawa walifukua maiti ya mtoto ambaye kichwa kilipatikana ndani ya makaazi yao.

Arif anamlaumu kakake Farman.

Wawili hao waliwahi kuoa na hata wakajaliwa na watoto, hata hivyo wake zao waliwatoroka kabla yao kwenda jela kwa kisa cha awali.

SERIKALI YAONESHA HATI YA MUUNGANO

Hatimaye serikali imeonyesha hati halisi ya muungano na kusema kuwa ipo tayari kuiwasilisha katika bunge maalum la katiba kama mwenyekiti wa bunge hilo ataona inafaa kufanya hivyo.

Akizungumza na wandishi wa habari katibu mkuu kiongozi Mh Ombeni Sefue amesema serikali imesikitishwa sana kuona wapo baadhi ya watu wanaodhiriki kusema kuwa hati hiyo haipo.

Akasema pia kwamba ni kwa busara za mwenyekiti wa bunge maalum l katiba akiona kuna haja ya hati hiyo kupelekwa katika bunge maalum serikali ipo tayari.

Aidha akasema kuwa zipo hati ambazo serikali inazihifadhi kwa umakini mkubwa ili kuhakisha kuwa zinaendelea kubaki salama kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Kiongozi huyo akaongezea kuwa ni matumaini ya serikali kuwa baada ya kuitoa hati hiyo hadharani watu wataendelea na mambo ya msingi yaliyopo mbele yao na siyo kuendeleza malumbano ambayo hayana tija kwa taifa.

Chanzo: ITV

KITUO CHA MABASI CHALIPULIWA NIGERIA

Milipuko miwili imetokea katika kituo cha mabasi katika vitongoji vya mji mkuu wa Nigeria, Abuja, na kuna taarifa ya watu wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo.

Mwandishi wa BBC, nchini Nigeria, Haruna Tangaza anasema milipuko hiyo ilitokea wakati abiria wakiwa katika harakati za kupanda mabasi na teksi wakienda maofisini katikati ya mji wa Abuja.

Shirika la habari la Uingereza, Reuters, limewakariri watu walioshuhudia tukio hilo wakisema mabasi mawili yaliyokuwa yamejaa abiria yalilipuliwa.

Mmoja wa mashuhuda wa shambulio hilo, Badamsi Nyanya ameiambia BBC kuwa ameona miili 40 ikiondolewa.

"Asubuhi hii kulikuwa na mlipukokatika eneo la maegesho ya magari ya Nyanya Motor Park," anasema Manzo Ezekiel wa Wakala wa Usimamizi wa Taifa wa Majanga.

Vikosi vya uokoaji tayari vipo katika eneo la tukio.

Shuhuda mwingine Bi Mimi Daniels, ambaye anafanya kazi mjini Abuja, anasema: "nilikuwa nasubiri basi niliposikia mlipuko mkubwa halafu nikaona moshi," ameiambia Reuters.

"Watu walikuwa wakikimbia ovyo kutokana na taharuki."

MZEE MUHUDIN GURUMO AFARIKI

Mkongwe wa Muziki wa Dansi, Muhidin Gurumo (aliyekuwa Msondo Ngoma kabla ya kustaafu mziki) amefariki dunia akiwa Muhimbili alipokuwa amelazwa!

Mungu ailaze roho yake mahara pema peponi

TAARIFA YA POLISI KWA MAAFA YALIYOLETWA NA MVUA

Kutokana na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la Dar es salaam pamoja na kusababisha mambo mengi kusimama, miundombinu kuharibika hasa madaraja yanayounganisha njia kuu, pia zimesababisha vifo vya watu 10.

Nyumba nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia kuhama kutoka kwenye makazi yao ambapo mpaka sasa Polisi Dar es salaam inasema watu kumi waliofariki, wamo watoto watano na watu wazima watano.

Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam amesisitiza hali sio nzuri hivyo wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi zina mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyolazima barabarani.

VIONGOZI WANUSURIKA KIFO BAADA YA HELKOPTA KUPATA AJALI

Katika kukagua uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua kubwa katika Jiji la Dsm, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Meck Sadiki na Afande Kova wamenusurika ajali ya helikopita iliyotokea leo Jijini Dsm.

DUNI AWAZIMA WANAOTAKA SERIKALI MBILI

Shamrashamra za wajumbe wanaounga mkono serikali tatu na mbili, nje ya Bunge jana, ziliendelea baada ya Mjumbe,Juma Duni Haji kutoa ufafanuzi wa kutetea serikali tatu na kuwavutia wajumbe, ambao walitoka ukumbi wa bunge wakimshangilia babu, babu, hawatuwezi hawatuwezi.

Tukio hilo ambalo ni mfululizo wa vijembe, baina ya wajumbe wa CCM na upinzani, kuhusu hoja ya serikali tatu au mbili, lilisababisha viwanja vyote vya bunge jana mchana, kutawaliwa na kelele za kushangilia na kuzomeana.

Akitoa ufafanuzi wa kamati namba 11, Duni alisema siyo serikali tatu ni ufumbuzi wa malalamiko ya Muungano, ambayo yanaifanya Zanzibar kuendelea kubanwa na kushindwa kuwapatia maendeleo wananchi wake.

Alisema serikali iliyopo madarani kwa miaka 50 sasa, imeshindwa kutumia rasilimali zilizopo Zanzibar na kuifanya iwe kutovu cha utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati badala yake inazuia kila jambo jema la maendeleo.

"Kama mngekuwa na dhamira ya dhati na Zanzibar, leo Zanzibar ingekuwa kama Hong Kong ya Afrika lakini hakuna, Zanzibar imefungwa mikono na miguu hata kutembea haiwezi," alisema.

Alisema hoja kuwa katika muundo wa serikali tatu, ukianza Zanzibar haiwezi kuchangia Muungano siyo ukweli kwani, uchumi wa wananchi wa Zanzibar hauna tofauti na uchumi wa Watanganyika kwa mtu mmoja moja. Akizungumzia takwimu za tume ya mabadiliko alisema zipo sahihi kuwa waliotaka Muungano wa Serikali tatu ni wengilakini kinachofanywa na wanaotaka serikali mbili ni kupotosha ukweli.

Haji alitolea mfano katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kuwa walioandikishwa kupiga kura walikuwa ni watu 20 milioni, waliopiga kura ni watu milioni nanena ambao walimchagua Rais Jakaya Kikwete ni watu milioni sita hivyo kwa hoja ya wanaCCM kuhusu Rasimu ina maana watu 14 milioni hawamtaki Rais Kikwete.

Akizungumzia gharama za Muungano, alisema fedha nyingi zaidi ya asilimia 70 za Muungano, zinatumika katika kuendesha Serikali ya Tanganyika jambo ambalo siyo sahihi.

Huku akitoa takwimu mbalimbali, alisema kwa maana hiyo uchangiaji wa Muungano kamwe hauwezi kuwa sawa kwa pande zote. "Katika jambo moja tu la askari polisi, tafitiza kimataifa zinaonesha kuwa askari mmoja anafaa kulinda watu 400, kwa Zanzibar yenye watu 1.3 milioni inahitaji askari 3,000 tu, lakini Tanganyika yenye watu zaidi ya 40 milioni inahitaji zaidi ya askari 120,000 hivyo uchangiaji wa Muungano hauwezi kuwa sawa," alisema.

Haji pia alieleza kuwa, hati za Muungano ambazo waliowengi wanasema zinamsingi wa serikali mbili, siyo kweli bali hati hizo zinatambua serikali tatu, ikiwapo ya Tanganyika.

Hata hivyo, alisema msingi wa serikali mbili ni mkakati wa CCM ambao ulianza tangu enzi za TANU mwaka 1977, kutaka kuwa na serikali moja na hivyo, kuifanya Zanzibar kuwa siyo nchi.

MIRUNGI YA VIDONGE YATEKA WATANZANIA

Unapolitaja neno 'mirungi' macho na hisia zako zitakupeleka katika dawa zakulevya zilizo katika mfumo wa majani au mimea ambazo ni maarufu Afrika Mashariki. Hapa nchini mirungi imeharamishwa kulingana na sheria ya dawa za kulevya.

Hata hivyo kwa sasa, mirungi hii haitumiwi ikiwa katika hali ya mimea tu kama ilivyozoeleka bali katika mfumo wa kidonge (kitaalamu synthetic cathinone) ambacho ni vigumu kufahamu kama ni mrungi.

Dawa hii ya kulevya ni maarufu na ina majina mengi hapa duniani, baadhi ya majina hayo ni miraa, khat kwa Kiingereza, ghat, qat, hagat, bushman tree (Afrika Kusini) na baadhi wanauita mmea huu Arabian.

Imebainika kuwa mirungi ya vidonge huingizwa nchinikatika vifurushi vilivyobandikwa lebo kama vile dawa za kuua wadudu, bath salt, sumu kali, dawa za kusafishia vioo au simu na mimea.

Mwaka 1980, Shirika la Afya Duniani liliipanga mirungi kuwa katika kundi la dawa za kulevya na mihadarati inayosababisha utegemezi, wakati hapa nchini mirungi ilipigwa marufuku Aprili 1991.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mshauri wa watumiaji wa dawa za kulevya, Innocent Godman, alifanya utafiti mwaka 2004 kuhusu utumiaji wa mirungi hapa nchini, ambao ulibaini kuwa kuna ongezeko kubwa la watumiaji wa mirungi ya kidonge.

"Ingawa mirungi ya vidonge imeanza kutumika katika siku za karibuni, lakini mirungi ya mimea, ilianza kutumiwa miaka 800 iliyopita," anasema Dk. Godman.

Mirungi ya kidonge inatajwa kuwa na madhara makubwa kuliko ile ya mimea, kwani husababisha mtumiaji kupata raha ya ngono au kilele cha mapenzi kwa sekunde 17 tofauti na hali ya kawaida ambapo binadamu hupata kilele hicho kwa sekunde tatu tu.

"Kidonge cha mirungi kimekuwa maarufu zaidi kwa sababu mtumiaji hupata raha ya mapenzi kwa muda mrefu na hivyo kumfanya asiwe na sababu ya kuwa na mwenza," anasema na kuongeza:

"Mirungi hii ina kileo kinachoitwa 'cathinone' mbacho ni kichocheo kinachobadilisha kasi ya ufanisi wa ubongo. Kinasogeza mbele uchovu, njaa na kuongeza umakini. Kikubwa zaidi kileo hicho husababisha raha ya ngono (euphoria) kudumu kwa muda mrefu."

Dk. Godman anasema, matumizi ya kidonge cha mirungi hapo zamani yalizoeleka zaidi kwa watu wazima wenye umri wa miaka 50 na kuendelea wenye matatizo ya nguvu za kiume, lakini hivi sasa, vijana wadogo wanatumia vidonge hivyo.

Katika utafiti huo ilibainika kuwa watumiaji wa mirungi hupenda kutembelea maeneo maalumu kwa mfano Dodoma, ni karibu na soko kuu na Arusha, ni maeneo ya Ngaramtoni, Makao Mapya na Kaloleni.

Lakini yapo maeneo maarufu katika Jiji la Arushana Dar es Salaam yanayoitwa Manjili Sairat ambayo yanasifika kwa kuuza mirungi ya majani na kidonge.

Mirungi ya kidonge kwa kawaida humezwa au mtumiaji kujidunga kama watumiaji wa dawa za kulevyawanavyojidunga, kukichanganya kwenye chai, lakini baadhi hukiingiza katika njia ya haja kubwaau (booty bombing).Matumizi ya mirungi licha ya kutopewa uzito mkubwa hapa nchini, lakini imebainika kuwa inatumiwa na watu zaidi ya milioni 10.Kamishna wa Kitengo cha Kupambana na dawa za Kulevya, nchini, Alfred Nzowa, anasema hana taarifa za kuwepo kwa mirungi ya vidonge zaidi ya mirungi ya majani.Hata hivyo Nzowa anasema, watatafuta mirungi na watapeleka sampuli kwa mkemia mkuu ili kujua madhara zaidi na iwapo wanachanganya na vitu vingine."Kikosi kazi changu kitaisaka mirungi hiyo kwa namna yeyote ilewanayoifungasha na tutaipima, ingawa kisheria tangu zamani mirungi haikubaliki hapa nchini," anasema Afande Nzowa.

*Waganga wa jadi nao wamo

Pia matumizi hayo yameenda mbali zaidi ambao hata waganga wajadi wanatumia mirungi ya majani kama dawa ya kifafa, kuongeza nguvu za kiume, kutibu maradhi ya pumu na dawa za kuongeza bahati.

"Kwa baadhi ya tamaduni, iliaminika mtu kuweka jani la mrungi katika mfuko au wanawake kulifutika katika maziwa, wakati anapokwenda kufanya biashara, kunaleta bahati,"anasema.

Si hivyo tu, kwani zipo baadhi ya nchi zimeruhusu wakazi wake kutumia mirungi kama mmea unaosaidia kuondoa usingizi na uchovu, hivyo wanafunzi, madereva na madaktari wamekuwa wakiutumia ili kupoteza usingizi.

Kamishna Msaidizi Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Aida Tesha pia hafahamu uwepo wamirungi ya vidonge.

"Tutaliwasilisha hilo jambo mbele ya wenzetu na kuanza kulifanyia utafiti, kwangu hii ni habari mpya kabisa," anasema.

Utafiti wa Dk. Godman unaonyesha kuwa watumiaji wa mirungi hasa ule wa kidonge wametofautiana kimadaraja kwa mfano, watumiaji wa mirungi walioajiriwa ni asilimia 59, wakati ambao hawaja ajiriwa ni asilimia 11 na wanafunzi ni asilimia tisa.

Makundi mengine ya watumiaji wa mirungi yalichambuliwa na kuonekana kuwa ambao hawana wenza ni asilimia 30, waliooa ni asilimia 60 na waliochana ni asilimia 10 wakati wajane ni asilimia 10.

*Madhara ya kiafya ya mirungi

Mirungi (ya mimea na ya kidonge) ina madhara ya kifikizia na kitegemezi kama ilivyo mihadarati mingine.

Kwa mfano mtumiaji huweza kutanuka mboni ya jicho lake, ndoto mbaya usiku, msonono, ongezeko la kasi la damu, kukosa hamu ya kula, na kuongezeka kwa kiwango cha raha ya tendo la ndoa.

Yapo matokeo ya papo kwa papo yakutumia mirungi ambayo ni pamoja shinikizo la damu, kukosa uhalisia wa dunia(kujihis tajiri, mwenye pesa au upo nchi za Ulaya) kitaalamu ni Cycosis.

Madhara yanayoweza kumpata mtumiaji baada ya kipindi kirefu ni pamoja na wazimu, maradhi ya saratani hasa ya mdomo, kiharusi, kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo na kuharibika kwa ini.

WAVUVI KUUA WANAWAKE ILI KUVUTIA SAMAKI

WAKATI Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu ametuma timu maalumu ya wataalamu wilaya ya Butiama mkoani Mara, kuchunguza matukioya mauaji yanayowalenga wanawake, taarifa zinasema mauaji hayo hufanywa na wavuvi.

Timu hiyo ya wataalamu itakayoongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),Issaya Mngulu, itaongeza nguvu ili kuhakikisha kwamba wote wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka.

Jeshi la Polisi nchini limewaomba wananchi, wenye taarifa za wahalifu hao, kutoa taarifa hizo kupitia namba za simu 0715 009930 na 0754 785557 au katika kituo chochote cha Polisi.

Habari kutoka mtandao wa kijamii wa http://www.jambotanzania.com, unaohusisha mabloga wanaodhaminiwa na Mfuko wa Kusaidia Vyombo vya Habari (TMF), zimesema kwamba mauaji hayo, yanafanywa kwa sababu za kishirikina.

"Mauaji ya wanawake mkoani Marahususani wilayani Butiama, hufanywa kwa sababu za kijinga na zisizo na ukweli za haja ya kupata samaki wengi kwa kutumia viungo vya mwanamke, ambavyo hudaiwa kuvuta samaki," umeandika mtandao huo kupitia mwandishi wake, homari Binda.

Mtandao huo ambao umedai kufanya utafiti wa kina, umesema wauaji ni wale wanaojishughulisha na uvuvi, wakiwa na imani kuwa wanapomuua mwanamke na kuchukua baadhi ya vitu kwenye mwili wake kama sehemu ya siri na nywele za ukeni, hupata samaki wengi wanapoenda kuvua.

Serikali na viongozi wa dini wamefanya jitihada kubwa, kukomesha mauaji hayo. Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, zilizonukuliwa na mtandao huo ni kuwa katika kipindi cha miezi mitatu, wanawake zaidi ya 15 wameuawa.

Miongoni mwa waliouawa ni Catherine Mandela (21) kutoka kijiji cha Kigera Etuma Tarafa ya Kusenyi wilayani Butiama. Taarifa za awali zilizoonesha kwamba mwanamke huyo, kauawa kwa imani za kishirikina.

"Huyu ni mwanamke wa pili katika kipindi cha mwezi mmoja kuuawa katika eneo letu katika mazingira ambayo naweza kusema ni imani za kishirikina na mahitaji ya utajiri wa haraka kwa wanadamu wasiomuogopa Mungu," alisema Maiga Maingu wa Kijiji cha Kigera Etuma.

Alisema imani za kishirikina ndio chanzo kikubwa cha mauaji hayo.

Alidai kuwa wanaotekeleza mauaji hayo ni wale wanaojishughulisha na uvuvi kwenye kambi za uvuvi, wakiamini wanawake wana mvuto wa kuvuta samaki kwenye mitego.

Maingu ambaye ni mvuvi mstaafu, alisema kwa sasa imani hiyo imeshika kasi na wanawake wengi wamekuwa wakiuawa, kutokana na imani hiyo potofu.

Masatu Mfungo wa Kijiji cha Esiri Kata ya Kigera Etuma, alisema kuibuka kwa mauaji hayo ya wanawake, kumewafanya wanawake kwenye Kijiji hicho, kuogopa kwenda kulima shambani.

Mwanamke mwingine aliyeuawa niwa Kijiji cha Nyegina Kata ya Nyegina wilayani Butiama, Mkaguru Magee, ambaye aliuawa shambani kwake na kisha kufukiwa shambani.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa alipambana vikali kuhakikisha mauaji dhidi ya wanawake Butiama yanakomeshwa. Kabla hajafariki, aliagiza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa kujitahidi kukomesha mauaji ya wanawake yanayoendelea Butiama.

MVUA YAZIDI KULETA MAAFA DAR

Watu wanane wamepoteza maisha jijini Dar es Salaam, huku mawasiliano kati ya jiji la Dar-Es-Salaam na wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani yakisimama kwa zaidi ya siku tatu, mara baada ya tuta la barabara pembezoni mwa daraja la mto Mpiji kusombwa na maji umbali wa mita arobani na kuleta adha kwa wananchi wanao tumia barabara hiyo.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa mapema asubuhi hii ya leo, wakati kuta za barabara ya inayounganisha kati ya jiji la Dar-es-salaam na Bagamoyo mkoa wa Pwani, lilivyokuwa likimomonyoka kadri mvua zilivyokuwa zikiendelea kunyesha katika eneo hilo la Bunju Mpiji mpakani mwa Bagamoyo na jiji la Dar-es-salaam.

Akiongea na wananchi waliokuwa wamefurika katika eneo hilo, waliokuwa wanahitaji kusafiri kati ya Bagamoyo mkoani Pwani na Dar-es-salaam, waziri wa ujenzi Mheshimiwa John Pombe Magufuri, aliyefika katika eneo hilo ili kushuhudia kadhia hiyo ya mvua na kutoa kauli ya serikali amesema kuwa, tayari amewasiliana na jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) ili kupata madaraja ya muda huku zaidi maroli elfu moja ya mawe yakihitajika kujazwa eneo hilo ili kuruhusu magari na watu kuweza kupita katika eneo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam bwana Saidi Mecki Sadik aliyeambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar-es-Salaam, amesema kuwa mpaka sasa jiji la Dar-es-Salaam limepoteza watu wa nane kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini, huku akisisitiza kuwa, uhamaji wa mito na kuharibu kingo za madaraja jijini Dar-es-Salaam, zinatokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo uchimbaji holela wa mchanga na kulima karibu na mito.

Baadhi ya wanafunzi mbalimbali waliokuwa wakitoka jijini Dar-es-Salaam na wale waliokuwa wakitoka mashuleni, mara baada ya shule kufungwa kwa wiki moja, ili kupisha mapumziko ya sikukuu za pasaka, wamejikuta wakilazimika kuzungukia njia mbadala za bunju, Goba kutokea na kuingilia Boababu ili kupata mawasiliano kati ya Bagamoyo na Dar-es-salaam.

katika eneo hilo la tukio, tingatinga na askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) tayari walikuwa katika eneo hilo la tuko ili kuweza kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo huku jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar-es-salaam na wale wa Bagamoyo mkoa wa Pwani wakiimalisha ulinzi katika eneo hilo.

MVUA, UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA KUENDELEA KUBULUZA

MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo vipindi vya mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi makubwa baharini kwa siku nne mfululizo.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa TMA, Dk Agness Kijazi ilisema kiwango cha uhakika wa kuwapo kwa matukio hayo ni kwa asilimia 70.

Alisema matukio hayo yameanza Aprili 11, mwaka huu na yataendelea hadi 14 mwaka huu.

Alisema kutakuwepo na vipindi vyamvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24, upepo mkali unaozidi kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa, yanayofikia mita mbili katika ukanda wa pwani.

Alitaja maeneo yanayotarajia kuathirika kuwa ni Visiwa vya Unguja na Pemba, mikoa ya Dar esSalaam, Pwani, Tanga.
Kuna uwezekano mikoa ya Lindi, Mtwara na Morogoro nayo itaathirika na hali hiyo.

Dk Kijazi alisema hali hiyo, inatokana na kuimarika zaidi kwa ukanda wa mvua wa 'Inter-tropical Convergence Zone (ITCZ)', ambao umeambata na na ongezeko la unyevunyevu katika eneo la Bahariya Hindi.

Alionya wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa bahari na mamlaka zinazohusika na maafa, kuchukua tahadhari zinazotakiwa, kutokana na hali hiyo.

Alisema kwamba mamlaka hiyo inaendelea kufuatilia hali hiyo na itatoa taarifa kila itakapobidi.

BODABODA WAZUA TAFRANI MBEYA, MABOMU YA MACHOZI YAPIGWA

Vurugu kubwa zimetokea mkoani Mbeya baina ya Jeshi la Polisi na waendesha bodaboda(pikipiki) baada ya jeshi la polisi kutaka kuzima jaribio la kutaka kuvunja nyumba.

Boda boda hao walifunga barabara na kuzua taflani baina yao na jeshi la Polisi baada ya Jeshi hilo kuingilia kati kumuokoa Mke wa derevawa pikipiki baada ya maderevahao kuvamia nyumba yake maeneo ya Forest wakitaka kubomoa wakimtuhumu kuhusika na kifo cha mumewe.

Tukio hilo limetokea leo majiraya saa nne asubuhi baada ya waendesha bodaboda kutaka kumdhuru mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua dereva mwenzao ndipo jeshi la polisi lilipoingilia kati hivyo kusababisha vurugu kubwa baina ya madereva hao na jeshi la polisi.

Hata hivyo madereva wa pikipiki zaidi ya 20 walilivamia gari la Polisi na kuvunja kioo cha mbele hali iliyopelekea dereva wa gari hilo kulikimbiza hadi kituo cha Polisi cha Kati ili kuomba msaada kwa askari wenzie waliojitokeza wakiwa na silaha za moto na kuwatawanya kabla ya kufunga barabara na kuanzisha vurugu.

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha bodaboda Jiji la Mbeya, Vicent Mwashoma, amelaani kitendo hicho na kuongeza kuwa jeshi la polisi limetumia nguvu kubwa kupambana na madereva wa bodaboda ili hali kuna uongozi unaotambuliwa na kusimamiwa na baadhi ya Askari.

Akizungumzia chanzo cha vurugu hizo, mwenyekiti huyo amesema juzi aliuawa dereva mwenzao aliyemtaja kwa jina la Siza Mwambenja ambapo baada ya kuzika madereva hao walianza kufanya upelelezi na kupewa taarifa kuwa aliyehusika ni mkewe aliyeachana naye kwa kusuka njama na wauaji.

Amesema baada ya kupata taarifa hiyo walienda nyumbani kwake kwa lengo la kumkamata hali iliyosababisha jeshi la polisi kufika na kuwatawanya lakini jazba ziliwapanda madereva hao baada ya baadhi ya maaskari kuanza kuvunja pikipiki na kuwapiga.

Kwa mujibu wa mashuhuda watukio hilo wamesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi baada ya marehemu kuachana na mke wake huyo anayetuhumiwa kusuka njama za mauaji na kuoa mke mwingine hali iliyosababisha mwanamke huyo kupata wivu na kulazimika kufanya mipango ya mauaji hayo.

Wakati vurugu hizo zikiendelea Shule ya sekondari ya Forest ya Jiji la Mbeya ililazimika kuahirisha mitihani ya kufungiamhula kutokana na wanafunzi kuathirika na mabomu yaliyokuwa yakirushwa na jeshi la polisi.

Hata hivyo kufuatia vurugu hizo waendesha boda boda kadhaa wanashikiliwa na jeshi la polisi akiwemo Katibu wa chama hicho kwa kuhusika na uvunjaji wa Sheria na uharibifuwa miundombinu ya barabara na gari la Polisi.


Chanzo: Mbeya Yetu

MVUA YASOMBA TUTA LA RELI YA TAZARA

Shughuli za uchukuzi wa mizigo toka bandarini kwenda mikoani na nchi za jirani kwa njia ya reli ya Tazara zitasimama kwa siku saba, kufuatia maji ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar-es-Salaam, kusomba tuta la reli ya tazara umbali wa mita arobaini na kuacha mataruma ya reli hiyo yakining'inia.

Meneja mkuu wa mkoa wa mamalaka ya reli ya Tanzania na Zambia Tazara, mhandisi Abdalah Kimweri amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar-es-Salaam, zimeathiri miundombinu ya mamlaka hiyo umbali wa kilometa nane kati ya maeneo ya kurasini na yombo jijini Dar-es-Salaam.

Mhandisi huyo amedai kuwa, katika maeneo mengi inapopita reli hiyo hasa jijini Dar-es-Salaam, makambako mkoani njome na tunduma jijini mbeya baadhi ya wananchi wamejenga karibu kabisa na reli hiyo jambo ambalo ni hatari kwao na kwa reli ya Tazara na kudai kuwa tayari wameisha wajulisha wananchi kuondoa maendeleo yao kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Mhandisi ujenzi wa mamlaka hiyo ya Tazara kwa upande wa Tanzania mhandisi Richard Festo, amesema kuwa katika maeneo ya temeke jijini Dar-es-salaam, ujenzi holela wa mfumo wa mitaro kuelekezewa kupita kwenye njia ya reli kumechangi kwa kiasi kikubwa kuchangia kuharibu miundombinu ya mamlaka hiyo, huku baadhi ya wananchi wakitaka kulipwa fidia kwa makaburi yao yaliyosombwa na maji.

Reli ya tazara yenye historia ya urafiki baina ya nchi tatu za Tanzania ,Zambia na uchina ikiwa na urefu wa kilometa 1860 kutoka jijini Dar-es-salaam nchini Tanzania hadi new kaplimposhi nchini Zambia, iliyoanza kutumika kusafirisha abiria na mizigo kwenye mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa na Mbeya iliyo anza kutoa huduma hiyo mwanzaoni mwa miaka ya 1976 ikiwa imejengwa na kampuni kutoka China.

MADAKTARI WAKUZA UKE KATIKA MAABARA

Madaktari nchini Marekani wamefanikiwa kuwatengezea wanawake wanne sehemu ya uke kwa njia ya kisayansi.Walitumia mfano wa seli ya uke na mifupa ya mwili kuweza kukuza uke huo katika maabara kwa kuzingatia wastani na umbo la kila mwanamke.

Baada ya matibabu hayo, wanawake hao wote inaarifiwa walielezea kupata hisia sawa na kamilifu,matamanio, kuridhishwawakati wa tendo la ndoa pamoja na kutopata maumivu yoyote wakati wa tendo la ndoa.

Wataalamu walisema kuwa utafitiwao, ambao matokeo yake yalichapishwa katika jarida la kisayansi la Lancet, ni mfano wa hivi karibuni wa nguvu za mbinu tofauti na za kisasa za matibabu.

Wanawake hao walizaliwa na uke ambao haukuwa umeumbika vyema yaani ulikuwa na kasoro ya maumbile , tatizo linalojulikana kama 'vaginal aplasia.'

Matibabu ya kisasa kwa tatizo kama hilo la kiafya yanaweza kuhusisha upasuaji ambapo ngoziau sehemu ya utumbo inatumika.

Celi zilichukuliwa kutoka kwa kizazi cha kila wanawake hao ambacho kilikuwa na kasoro ya maumbile na kukuzwa katika maabara ili kuweza kuzaana.

Picha za kizazi cha wanawake hao zilitumia kuwarekebishia uke wao.

Hili bila shaka ni jambo geni katika sayansi ya matibabu na piainatoa taswira ya mambo yatakavyokuwa katika siku za usoni.

Jambo la Kutumia celi za mwili kubadilisha maisha ya wagonjwa tayari limefanyika na kuwasiaidia wagonjwa kupata kibofu cha mkojo, mishipa ya damu na koo.

Sasa unaweza kuongeza kwenye orodha hiyo, uke na pua.

POLISI WAKAMATA SILAHA ZA KIVITA ZANZIBAR

POLISI Zanzibar, wamefanikiwa kukamata silaha mbili za vita na risasi 40 zinazosadikiwa kutumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu, likiwemo la mauaji ya askari polisi mmoja lililotokea Machi 2, mwaka huu huko kwenye Hoteli ya Kitalii ya Pongwe Bay mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar.

Katika tukio hilo askari polisi Koplo Mohammed Mjombo(44) aliuawa huku mwenzake mwenye namba Konstebo Ibrahim Juma Mohammed(35) akijeruhiwa vibaya kwa risasi kabla ya kuporwa silaha aliyokuwa nayo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, SACP Yusufu Ilembo amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa silaha hizo pia watuhumiwa watatu kati ya wanne waliohusika katika mauaji ya Polisi wamedakwa.

Alisema silaha hizo zilikamatwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa anayeishi eneo la Mkokotoni katika mkoa wa Kaskazini Unguja zikiwa zimefungwa na vipande vya plastikina vitambaa na kuviringishwa katika waya mpya wa kupigilia madirisha.

Bila ya kuwataja majina yao kwa sababu za kiupelelezi, DCI Ilembo ameainisha wazi kuwa baadhi ya watuhumiwa hao ni wenyeji wa Pangani mkoani Tanga na wengine ni wenyeji wa Kisiwa cha Pemba Zanzibar.

Amesema katika mahojiano na makachero wa Polisi, Majambazi hayo pia yalikiri kuhusika na matukio mbalimbali katika mikoa ya Visiwani na Mikoa ya Tanzania Bara matukio ambayo yangali yakichunguzwa katika Vituo mbalimbali vya Polisi.

Watuhumiwa hao pia walipatikana na vitu mbalimbali zikiwemo fedha taslimu shilingi 490,000 za Kitanzania, dola 75 za Kimarekani, Euro na fedha kadhaa za Kichina pamoja na vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi.

MSEKWA ATOBOA SIRI YA MUUNGANO

Wiki mbili kabla ya Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa ametoboa siri ya Muungano huo akisema "mchakato wa kuundwa kwake ulifanywa kwa siri na haraka sana," kutokana na upepo wa kisiasa na usalama wa kipindi hicho.

Akizungumza katika moja ya mfululizo wa vipindi vya miaka 50 ya Muungano vinavyorushwa na Redio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa), Msekwa alisema woga wa hayati Abeid Amani Karume kupinduliwa na maadui, ulikuwa ni miongoni mwa sababu za kuharakisha Muungano huo.

Msekwa aliyekuwa Katibu wa Bungela Tanganyika wakati Muungano unaasisiwa, alisema pia yeye na wenzake walichelewa kujua kwamba Mwalimu Julius Nyerere (Rais wa Kwanza wa Tanganyika) na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Karume walikuwa na majadiliano yakuunganisha nchi hizo.

"Kikubwa cha kusema ni kwamba mazungumzo ya Muungano huo yalifanywa kwa siri.... kwa siri sana baina ya waasisi wa nchi hizo. Kwa nini yalifanywa kwa siri? Siyo kwa sababu walikuwa wababe, la hasha, bali kwa mazingira ya wakati ule, kulikuwa na maadui ambao wasingependa nchi hizi kuungana," alisema Msekwa na kuongeza:

"Kwa woga huohuo, ndipo Mwalimu alipokubaliana na mwenzake wafanye mazungumzo ya siri mpaka waliposaini yale makubaliano na kunijulisha."

Msekwa ambaye pia amewahi kuwa Spika wa Bunge la Muungano, alisema baada ya makubaliano ya Muungano, Nyerere alimwita na kumjulisha kuwa walishakubaliana (na Karume) kuungana, hivyo walihitaji baraka za Bunge kuridhia Muungano huo.

"Mwalimu akaniambia, 'wewe Katibu wa Bunge unaweza ukawaita wabunge wakaja kwa harakaharaka kuridhia makubaliano?'

"Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Jumanne na Mwalimu alipendekezawabunge wafike Ijumaa ya juma hilohilo, nao wabunge wakaja wakaridhia."

Simulizi hii ya Msekwa kuhusu Muungano imekuja wakati kukiwa na vuguvugu la muundo wa Muungano katika Bunge Maalumu la Katiba, kutokana na mapendekezo yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba kupendekeza serikali tatu badala ya Serikali mbiliza sasa.


*Bunge kuridhia

Aliongeza kuwa, baada ya Bunge la Tanganyika kuridhia Mwalimu Nyerere aliutaka muswada huo "kwa haraka sana" ili aufanye kuwa sheria na alitaka kupelekewa kwa mkono."

Baada ya wabunge kuridhia pale Karimjee, nikauchukua muswada na kuupeleka Ikulu, sio mbali pale.

"Mwalimu alifurahi sana, alishajua kuwa ulikuwa umesharidhiwa kwa sababu alikuwa anafuatilia mkutano wa Bunge kupitia redio, ukumbuke zamani hakukuwa na televisheni," Msekwa anasimulia.


*Sababu za kuharakisha

Msekwa alisema kulikuwa na sababu kuu mbili za kuharakisha Muungano; moja ni Mwalimu Nyerere kutaka nguvu ya Afrika itokane na miungano ya nchi, wakati Karume alitaka kuimarisha usalama wa Zanzibar miezi miwili baada ya kuuondoa utawala wa Sultani Januari 12, 1964.

Aliongeza kuwa Nyerere alikuwa amejifunza kutokana na makosa ya awali ambapo maadui waliharibu mpango wa kuziunganisha nchi za Afrika ya Mashariki na kuwa shirikisho.Hata hivyo, Msekwa aliongeza kuwa, Mwalimu alimwambia Karume wangoje kwa muda, lakini kiongozi huyo wa Zanzibar hakuafikiana na wazo hilo kutokana na masuala yake ya kiusalama.

Alisema hata wakati Bunge la Tanganyika likiridhia muswada wa kuanzisha Muungano, tayari wenzaowa Zanzibar walikuwa wamekwishauridhia.


*Muundo wa Muungano

Msekwa alisema suala la kubuni muundo wa Muungano ambalo linasumbua vichwa wajumbe wa Bunge la Katiba sasa, halikuwa tatizo kubwa wakati huo, japo Karume alimwomba Nyerere watengeneze Serikali moja.

"Karume alimtaka Mwalimu waunde serikali moja; yeye awe Makamu wa Rais na Nyerere awe Rais. Lakini Mwalimu hakutaka wazo hilo akihofia maadui wangesema ameimeza Zanzibar na pia alizingatia udogo wa nchi hiyo pamoja na hofu ya kuwa mkoloni mamboleo," alisimulia Msekwa.Msekwa alisema mara tu baada ya Nyerere kusaini muswada wa Muungano kuwa sheria, alianza kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano na aliwachukua wajumbe 20 kutoka Zanzibar kuingia katika Bunge la Muungano.

Alisema baada ya Muungano huo hakukuwa na chokochoko zozote na hata maadui waliotaka kuipindua Serikali ya Zanzibar walikata tamaa.

"Hakukuwa na kitu kinachoitwa kero za Muungano mpaka pale Aboud Jumbe alipoingia madarakani baada ya kifo cha Karume 1972. Jumbe na wenzake walikuwa wanahoji Tanganyika tuliyoungana nayo ipo wapi?" alisema.

Aliongeza kuwa baada ya miaka kadhaa ya uongozi wake, Jumbe alianza harakati za kuandaa Katiba ya Serikali tatu kimyakimya.

"Jumbe alimwomba Mwalimu apatiwe mwanasheria mzoefu ili awe Mwanasheria Mkuu Zanzibar licha ya kuwa tayari alikuwapo mwanasheria mkuu.

Nyerere alimpatia Jaji Damian Lubuva, ambaye alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa upande wa Muungano, huku Joseph Warioba akiwa Mwanasheria Mkuu.

Alisema baada ya miaka takriban sita, Jumbe alimrudisha Jaji Lubuva Tanzania bara akidai ameshampata mwanasheria mwingine na hapo siri za kuunda Katiba mpya zilianza kugundulika mwanzoni mwa mwaka1984.

"Jumbe alikuwa na mpango wa kumtafuta mwanasheria mkuu kutoka Ghana.
Mwanasheria huyo walimuozesha binti wa Kizanzibari kabisa na baadaye walianza mchakato wao wa kutengeneza Katiba ya Serikali tatu kwa siri," alisema Msekwa.Hata hivyo, usiri wa Jumbe ulivuja na kumfikia Mwalimu, ndipo katika Mkutano Mkuu wa CCM, chama kilimwadhibu kwa kumtaka ajiuzuluna rais huyo alifanya hivyo bila hiyana.

Hata baada ya Jumbe kujiuzulu, Msekwa alisema bado madai ya Serikali tatu yaliendelea kuibuka katika tume mbalimbali ikiwamo ile ya Jaji Francis Nyalali, Kundi la Wabunge (G55) na hata sasa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba.


*Utashi wa kisiasa

Mwanasiasa huyo mkongwe anasema hatima ya Muungano ipo mikononi mwa wajumbe wa Bunge la Katiba ambao jana walianza kujadili mapendekezo ya kamati kuhusu Ibara za Kwanza na Sita za Rasimu ya Katiba, zinazozungumzia Muungano."

Muungano wowote unahitaji utashiwa kisiasa. Kuna watu wanasema kero za Muungano zitaondolewa na Serikali tatu na huku wengine, kikiwamo CCM, wanasema watahakikisha wanatatua kero hizo kwa kutumia Serikali mbili.

Hivyo, mimi naona iwapo uamuzi wa Bunge la Katiba utaondoa kero za Muungano, sawa na wananchi wakiridhia uamuzi huo sawa, hakuna tatizo kwa sababu hapo awali, uamuzi ulitoka kwa Serikali pekee," alisema Msekwa.

KAFULILA ASISIMUA BUNGE

Mjumbe wa Bunge la Katiba, David Kafulila jana aligeuka shujaa bungeni na kubebwa juujuu na wajumbe wenzake kutoka kundi la walio wachache baada ya 'kusambaratisha' hoja za wajumbe wanaopinga Serikali tatu.

Kafulila ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), alifanya hivyo alipokuwa akifafanuahoja kutoka kundi la walio wachache katika Kamati Namba Tano.

Miongoni mwa hoja ambazo alizijibu na kushangiliwa na wajumbe, ni juu ya gharama za Serikali tatu, kuwa zitavunja Muungano, kwamba Serikali ya Muungano itakosa mapato, hoja ya kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere na uhalali wa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Alisema hoja kuwa Serikali tatu ni kuvunja Muungano si za kweli, akisema ni propaganda zilezile ambazo CCM ilizitumia mwaka 1992 kutembea nchi nzima kupingamfumo wa vyama vingi.

"Wakati ule CCM ilitembea nchi nzima huku wakionyesha video kuwa vyama vya upinzani vitaleta vita, lakini leo miaka 20 baada ya kukubali mfumo wa vyama vingi hakuna vita vilivyoletwa na upinzani," alisema Kafulila. Alisema haiwezekani tume zote ambazo zinaundwa na Serikali zipendekeze serikali tatu na kila wakati serikali iliyopo madarakani ikatae.

"Hoja ya serikali tatu siyo hoja ya Warioba, tume zote zilizowahi kuchunguza muundo ya Muungano zote zilipendekeza serikali tatu," alisema na kuongeza: "Ofisi ya Rais ilipendekeza serikali tatu, ofisi ya Waziri Mkuu ilipendekeza serikali tatu, inatuwia vigumu ndani ya muda mfupi, vyombo hivi vibadilike na kutaka serikali mbili." Alisema wanaotaka serikali tatu wanataka kwa namna ambayo inaimarisha Muungano, tofauti na maoni ya walio wengi kuwa serikali ya Muungano itakuwa legelege kwa kuwa itakosa nguvu za kiuchumi.

"Ni kweli inawezekana vyanzo vya mapato vilivyopendekezwa havitoshi kuendesha Bunge, lakini ndiyo sababu tupo hapa, haiwezekani ripoti ya Tume iwe imekamilika pande zote," alisema na kuongeza:

"Wamependekeza badala ya kutegemea vyanzo vya washirika, tumependekeza kodi ya bandari ambayo ni karibu Sh 3.6 trilioni inaweza kuwa ni kodi ya Serikali ya Muungano. Kodi hiyo pekee inatosha kuendesha wizara zote ambazo gharama yake si zaidi ya Sh 3 trilioni."

"Kuna hoja hapa, haiwezekani kuwa fedha za bandari zote ziwe zinachangia Muungano kwani ni fedha za Tanganyika, lakini Muungano wowote ni lazima kukubali nchi kubwa kuchangia zaidi."

Kafulila ambaye hata baada ya kumaliza muda wake wajumbe walipiga kelele wakitaka aendelee, alisema kwa Serikali ya Muungano kupata mapato hayo tu, itakuwa haina haja ya kusubiri fedha za nchiwashirika na pia itakuwa na uwezo wa kuchangia fedha kwa nchi washirika.

"Haiwezekani Watanganyika wakubali kubeba gharama kubwa yaserikali mbili badala ya gharama ndogo za serikali tatu na hii ndiyo inawapa hofu Wazanzibari kudhani kuna kitu kinachofichwa," alisema. Kuhusu hoja ya kutumia maneno ya Nyerere kupinga Muungano wa serikali tatu, alisema Mwalimu hakuwa nabii, alitazama mambo kwa wakati ule na alikuwa akibadilika kutokana na wakati.

Alisema mwaka 1965, Mwalimu Nyerere alifuta vyama vingi... "Angekufa mwaka huo, tungebaki kuwa alikataa vyama vingi, lakini Nyerere huyu mwaka 1992 alikubali vyama vingi na hiyo inaonyesha kuwa kila jambo lina wakati wake na kwa sasa hakuna namna na kupinga serikali tatu. Hivi sasa tunapata ugumu wa lazima kutokana na misimamo ya vyama, lakini katika jambo hili la serikali mbili na tatu na wengi wameamua."

Alisema suala hilo likiachwa kama lilivyo waliopo madarakani sasa wataendelea kulifunika lakini itakuja kuwa hasara kwa nchi: "Leo mna nafasi ya kutengeneza serikali tatu kiuhalisia zaidi kuliko baadaye, mtakosa nafasi hii, huko baadaye haiwezekani kuwa na wingi huu, leo mnaweza kuamua serikali bora zaidi, huu ni wasia tu," alisema huku akishangiliwa.

Akizungumzia uwiano, alisema mataifa yote duniani yanapoungana huwa hayana uwiano ulio sawa.

Alisema Jimbo la California peke yake nchini Marekani linachangia zaidi ya asilimia 20 ya mapato yote.

Baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge, Kafulila ambaye alichambua kwa kina takwimu za Tume ya Warioba alipokewa kwa shangwe na wajumbe wa kundi la Ukawa, wakimsifia kwa kuzungumza kishujaa.

SHERIA YA KUWEZESHA WAZAWA KWENYE GESI YAJA

RAIS Jakaya Kikwete amesema serikali ipokwenye hatua za mwisho za kuandaaa sheria, kanuni na taratibu kwa ajili ya uwekezaji wenye tija kwa wazawa katika sekta ya gesi na mafuta.

Alisema kazi hiyo itafanywa na Bunge laAgosti mwaka huu ambapo miswada ya sheria hiyo itajadiliwa.

Rais Kikwete alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 19 la mwaka lililozindua pia ripoti ya utafiti wa Shirika la Utafiti na Kupunguza Umaskini (REPOA).

"Baada ya kugundulika kwa zile kyubiki futi za ujazo milioni 46 wa gesi… kazi iliyopo ni kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya rasilimali ile kwa manufaa ya Watanzania wote inapatikana ili Oktoba mwakani nistaafu kwaamani," alisema Rais Kikwete.

Alisisitiza kwamba lazima serikali na wadau muhimu wa sekta hiyo wajiridhishe kwamba hakuna wizi ili kumletea mwananchi wa kawaida maendeleo na kuzuia hujuma, wizi na rushwa kwa lengo la kuleta matokeo chanya.

Akizungumzia tafiti zinazofanywa na REPOA alisema: "Tafiti hizi za kila mwaka zimekuwa na msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima na wananchi wa kawaida katika kufanya uamuzi sahihi kwenye maeneo."

Alisema kwamba Tanzania zipo ajira ndogo ndogo milioni tatu zinazohusisha wananchi milioni 5.2 huku kati yao asilimia 64 ni wanawake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Profesa Samwel Wangwe, alisema kwamba tafitihizi zinalenga kuwasaidia wananchi wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kupunguza umaskini.

Alisema malengo ya tafiti pia ni kuongeza tija kwa kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni jinsi ya kujenga viwanda, usindikaji wa chakula na kupambana na tatizo la ajira hasa kwa vijana na wanawake.

AFISA MASOKO COCA-COLA AUWAWA

OFISA Masoko wa Kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola, Steven Mbilo (40), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi maeneo ya kifuani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, ACP Wankyo Nyigesa, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 asubuhi katika Kijiji cha Mtiri, Tarafa ya Ifwagi, wilayani Mufindi.

Nyigesa alisema marehemu baada ya kupekuliwa alikutwa na sh milioni 4.7 pamoja na simu yake ya mkononi.

Alisema hadi sasa watu wawili wanashikiliwa na Jeshila Polisi kutokana na kuhusishwa na mauaji hayo ambao ni Paschal Benedict(44) mkazi wa Tunduma na Seleman Juma (42) mkazi wa Soweto.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ilikubaini chanzo cha kifo hicho.

Wakati huo huo, Aloyce Mlimakifye (60) mkazi wa Mtitu, amekufa maji baada ya kutumbukia kwenye Mto Kikonde.

Kamanda huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea janasaa 12:30 asubuhi katika kijiji hicho Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa huku akieleza kuwa chanzo cha kifo hicho kimetokana na ulevi.

KAMATI 6 ZA BUNGE LA KATIBA HAZIJAWASILISHA TAARIFA

KAMATI sita kati ya kamati 12 za Bunge Maalumu la Katiba, zimeshindwa kuwasilisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu tayari kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni leo.Jana, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samia Suluhu Hassan, alipokea taarifa za kamati sita zilizomaliza kazi kwa wakati, huku kamati zingine zikiandika barua kuomba kuongezwa muda.Akizungumzia hali hiyo, Samia alisema kamati ambazo hazijakabidhi taarifa zao, zitaendelea kukabidhi taarifa hizo leo wakati zilizowahi kuwasilisha taarifa zao mbele ya Bunge Maalumu.

Alisema taarifa za kamati zilizokwisha wasilishwa, zitatolewa nakala ili kazi ya kuwasilishwa ndani ya Bunge leo iendelee wakati kamati zilizochelewa, zikiendelea kuwasilisha taarifa zao.

Samia pia alibainisha kuwa Kamati ya Uongozi iliyoanza kikao chao jana saa mbili usiku, ilitarajiwa kutoa ratiba kamili leo kuhusu kitakachofuata katika Bunge Maalumu.

Waliokabidhi Kamati ya Kwanza kuwasilisha taarifa yake ni Kamati Namba Tisa inayoongozwa na Mwenyekiti Kidawa Hamidi Saleh na Makamu Mwenyekiti, Wiliam Ngeleja na kufuatiwa na Kamati Namba Tano, inayoongozwa na Mwenyekiti Hamad Rashid Mohamed na Makamu Mwenyekiti, Assumpter Mshama.

Kamati zilizofuata ambazo ziliwasilisha jana saa 10 jioni ni pamoja na Kamati Namba Mbili, inayoongozwa na Mwenyekiti Shamsi Vuai Nahodha na Makamu wake, Shamsa Mwangunga na Kamati Namba 11, inayoongozwa Mwenyekiti Anne Kilango Malecelana Makamu Mwenyekiti, Hamad Masauni.

Kamati ya tano kuwasilisha taarifa yake kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu ni Kamati Namba 12, inayoongozwa na Mwenyekiti Paul Kimiti na Makamu Mwenyekiti, Thuwaybah Kisasi na Kamati Namba 10, inayoongozwa na Mwenyekiti Anna Abdallah na Makamu Mwenyekiti, Salmin Awadh Salmin, ilikuwa ya mwisho kuwasilisha taarifa zake.

Theluthi mbili Ukiacha Kamati Namba Tisa inayoongozwa na Mwenyekiti Kidawa, ambayo imepata theluthi mbili katika kila ibara ya sura ya kwanza na sura ya sita za Rasimu ya Katiba mpya, kamati zingine tano hakuna hata moja iliyopata theluthi mbili katika ibara zote.

Nahodha katika taarifa yake, alisema katika kamati yake katika Sura ya Kwanza, hawakupata theluthi mbili ya kura zote katika ibara ya kwanza na ibara ya nane kifungu kidogo cha nne.

Anne Kilango katika taarifa yake, alisema walifanya kazi mpaka usikuna katika Sura ya Kwanza, walipata theluthi mbili ya kura za Tanzania Bara, lakini Zanzibar hawakupata.

Anna Abdallah alisema muda haukutosha na katika majadiliano, misimamo ya vyama vya siasa ilionekana wazi na hivyo hata katika kuamua kwa kura ni mambomachache, ndiyo walipata theluthi mbili ya kura kutoka Tanzania Barana Zanzibar.