LOWASSA AKERWA NA MITANDAO

(Noti ya Sh.500 Iliyowekwa picha ya Lowassa)

Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amekerwa na tabia ya baadhi ya watu wanaosambaza uzushi katika mitandao ya kijamii kwa kutumia jina lake.

Lowassa alisema kuna watu wanaoendeleza kusambasa picha yanoti ya Sh500 yenye picha yake huku wakiongeza maneno mabaya juu yake.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake, Lowassa alisema, "Kitendo hicho siyo utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Taifa na mamlaka ya nchi."

"Hizi ni alama za Taifa ambazo zinatakiwa kulindwa na kuheshimiwa na watu wote, si busara kwa hao wanaozichezea kuendelea kufanya hivyo, kwani ni dharau kubwa kwa Taifa' alisema.

Katika noti hiyo ya Sh500 inaonekana upande wa kulia wa noti hiyo picha ya Edward Lowassa, huku ikikaribiana na ngao ya Taifa huku ikionyesha kuwa ilitolewa na Benki Kuu ya Tanzania..

Alisema anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi hao kutumia nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi badala ya kuzusha mambo yasiyo na tija. Kwa nyakati tofauti, picha hiyo imekuwa ikisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo ya Facebook, Instagram, Whatsapp, na Twitter huku kukiwa na maneno kama "timu Lowassa" na mengineyo.

Ikumbukwe kuwa Lowassa yupo katika adhabu ya kutoshiriki katika masuala yoyote yahusianayo na kampeni za chinichini za urais, baada ya kamati ya maadili ya CCM)kutoa hukumu yake mwezi uliopita.

Adhabu hiyo pia iliwakumba wengine watano wakiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Moja ya sababu ya adhabu hiyo ya miezi 12 ilikuwa ni kuanzisha kampeni za chinichini za kugombea urais mwaka ujao nje ya muda uliopangwa, ambapo baadhi ya wanachama akiwamo Lowassa walituhumiwa kuhusika kuandaa makundi na fulana za kujinadi.

JE ARSENAL KUWAONDOSHA THE BAVARIANS KWAO?

Michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya kuendelea leo usiku huku kukiwa na mechi mbili.

Arsenal, inaelekea, Bonn, kutoana jasho na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich ambayo ilishinda mechi ya raundi ya kwanza kwa mabao mawili kwa nunge katika uga wa Emirates.

Hata hivyo Arsenal itakosa huduma za mcheza kiungo wake Kieran Gibbs ambaye kwa sasa anauguza jeraha la mkuu na mshambulizi Yaya Sanogo, lakini mlinda lango Laurent Koscielny, ambaye alikuwa akiuguza jeraha la paja anatarajiwa kurejea.

Kipa Lukasz Fabianski naye atachukuwa mahala pa Wojciech Szczesny, ambaye amesimamishwa kucheza kwa muda baada ya kupewa kadi nyekundu wakati wa mechi ya raundi ya kwanza.

Mwaka uliopita Arsenal iliishinda Bayern kwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya marudiano lakini ilibanduliwa nje ya mashindano hayo baada ya kupoteza raundi ya kwanza 3-1.


Katika mechi nyingine ya marudiano leo usiku itakuwa kati ya Atletico Madrid na AC Milan.

Madrid ilishinda awamu ya kwanza kwa bao moja kwa bila.

Mario Balotelli huenda akajumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji kumi na mmoja wa AC Millan, baada ya kuuguza jeraha la mgongo alilopata siku ya Jumamosi dhidi ya klabu ya Udinese.

Atletico nayo inamkaribisha mchezaji wake aliyefunga idadi kubwa yua magoli Diego Costa huku ikijaribu kufunzu kwa robo fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na saba iliyopita.

Na ili kufuzu, mabingwa hao mara saba wa Ulaya ni sharti waandikishe historia ya kuwa timu ya tatu katika historia ya kombe hilo kuwahi kushindwa nyubani katika mechi ya raundi ya kwanza na ishinde mechi ya marudiano ugenini.


*BARCELONA KUIMALISHA MPIRA SOMALIA

Klabu ya soka ya Hispania Barcelona, imezindua mpango wakutoa mafunzo kwa makocha wa Somalia.

Mpango huo ujulikanao kama Futbal Net unalenga kuimarisha soka miongoni mwa vijana nchini Somalia, huku nchi hiyo ikijaribu kujiondoa kutoka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kamati ya michezo ya Olimpiki pia inaunga mkono mpango huo.Wanatumai kufungua vituo kadhaa vya mafunzo kote nchini humo.

Soka na michezo mingine ilikandamizwa na kundi la wanamgambo la Al Shabab kabla ya kuondolewa mjini Mogadishu miaka mitatu iliyopita.


*MASHABIKI KUTIZAMA MPIRA BURE

Mashabiki wa soka nchini Afrika Kusini watapata fursa ya kutizama mechi za ligi kuu ya England, katika bustani mpya itakayo funguliwa mjini Johannesburg mwisho wa mwezi huu.

Mechi tano, ikiwemo ile kati ya Arsenal na Manchester City itaonyesha moja kwa moja kwenye runinga kubwa katika bustani hiyo tarehe 29 na 30 mwezi huu.

Hafla hiyo ambayo haitatoza ada yoyote, inaandaliwa kwa mara ya kwanza na mashabiki elfu kumi na mbili wataruhusiwa kuingia ndani ya bustani hiyo ya Zoo LakeSports Club kila siku.

Mashabiki hao pia watapata fursa ya kukutana na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya AfrikaKusini, Bafana Bafana akiwemo Mark Fish na Lucas Radebe.

Vile vile wachezaji wa zamani wa Liverpool, Robbie Fowler na mchezaji wa zamani wa Chelsea na nahodha wa Ufaransa Marcel Desailly watakuwepo.

Wakati wa hafla hiyo mashabiki watakuwa na fursa ya kuona na kupiga picha kombe la ligi kuu ya Premier ya England.

WAANDAMANA DHIDI YA UN

Zaidi wa raia elfu moja wa Sudan Kusini, wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba, dhidi ya Umoja wa Mataifa, wakiishutumu kwa kuwapa waasi wanaopambana na serikali silaha.

Waandamanaji hai wamemtaka mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo Hilda Johnson kujiuzulu.

Siku ya Ijumaa, serikali ya Sudan Kusini, ilisema kuwa ilinasa msafara wa magari yaliyokuwa yakisafirisha silaha ambazo huku zikidai kuwa zilikuwa zikisafirisha misaada ya chakula.

Umoja wa Mataifa umekanusha shutuma hizo, lakini imekiri kuwa imekiuka mkataba waliosaini na serikali ya nchi hiyo, kwa kusafirisha silaha wakitumia magari badala ya ndege.

Taifa la Sudan Kusini, limekumbwa na mzozo wa kisiasa tangu Desemba mwaka uliopita, wakati wanajeshi watiifu kwa makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo Riek Machar, kuanzisha mapigano katika kambi kuu ya jeshi mjini Juba.

Mazungumzo ya amani kati ya wawakilishi wa serikali ya Sudan Kusini inayoongozwa na Salva Kirrna makamu wake wa zamani RiekMachar, yanaendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia.

MELI YA KOREA KASKAZINI YAKAMATWA LIBYA

Wakuu nchini Libya, wamesema kuwa wameikamata meli moja iliyokuwa na bendera ya Korea Kaskazini, ikiwa na shehena haramu ya mafuta katika bandari inayodhibitiwa na waasi.

Msemaji wa shirika la kitaifa la mafuta, amesema kuwa meli hiyo ilisimamishwa ilipokuwa ikijaribu kungoa nanga na kwa sasa inasindikizwa katika bandari inayodhibitiwa na serikali ya Libya.

Maafisa wa serikali ya Libya waliisimamisha Meli hiyo ya Korea Kaskazini ilipokuwa ikiondoka kutoka bandari inayodhibitiwa na waasi siku ya Jumatatu ikiwa imesheheni mzigo usio rasmi wa mafuta ghafi.

Jeshi la nchi hiyo limethibitisha tukio hilo.

Waasi wa zamani wanaotaka kuitenga eneo la Libya Mashariki, wamekuwa wakimiliki bandari ya Al-Sidra na vituo vingine muhimu vya kuuzia bidhaa nje katika eneo hilo tangu Julai mwaka uliopita.

Mnamo siku ya Jumamosi, walianza kupakia shehena ya mafuta yasiyosafishwa ndani ya meli hiyo ya Korea Kaskazini iitwayo Morning Glory, iliyokuwa imetia nanga katika bandari ya Al-Sidra.

MAREKANI WASUSIA MAZUNGUMZO NA URUSI

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa Waziri wa mambo ya nje John Kerry, amekataa kukutana na Rais wa Urusi, Vladmir Putin, mpaka pale Moscow itakaporidhia mapendekezo ya Marekani kuhusu kumaliza mzozo nchini Ukraine.

Kerry amemwambia waziri wa mambo ya nje wa Urusi kuwa uvamizi wa kijeshi wa Urusi mjini Crimea umefanya mazungumzo ya kufikia muafaka kuwa magumu mno.

Maafisa wa Marekani wamesema ikiwa kura ya maoni iliyopendekezwa itapigwa mwishoni mwa juma kuhusu kuridhia kwa Crimea kuwa sehemu ya Urusi, hakuta kuwa nasuala jingine la kuzungumza.

Maafisa hao wamesema kuwa ikiwa hali itafikia hivyo, Marekani itaiwekea Urusi vikwazo vikali.

MISHAHARA YA RAIS, MAKAMU NA MAWAZIRI KUPUNGUZWA KWA 20%

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameamuru maafisa wakuu watendaji wa mashirika ya serikali kukubali mishahara yao kukatwa kwa asilimia 20, la sivyo waachishwe kazi.

Akiongea kwenye kongamano la kitaifa kuhusu gharama kubwa ya matumizi ya serikali, Rais Kenyatta alisema kuwa hatua yake na naibu wake pamoja na baraza la mawaziri kupunguza mishahara yao kwa asilimia 20 haikuwa kwa sababu ya kufurahisha watu.Kadhalika Kenyatta ameongeza kusema kuwa uchumi wa nchi hauwezi kuwa mzuri ikiwa kila mtu anataka nyongeza ya mishahara badala ya kuzingatia kupunguza gharama ya maisha nauzalishaji wa bidhaa.

''Wakuu wa mashirika ya serikali watatakiwa kukubali mishahara yao kupunguzwa kwa asilimia 20. Kuna wakenya ambao wanaweza kushikilia nyadhifa hizo kwa pesa ndogo ikilinganishwa na zile wanazopata wakuu hao,'' aliongeza kusema Kenyatta.

Kenyatta amesema matumizi ya pesa za serikali ni ya juu mno na kwamba hayawezi kudhibitiwa ikiwa baadhi ya wafanyakazi wa sekta ya umma wataendelea kupata mishahara mikubwa.Rais alisema lazima safari za kwenda nje ambazo zinafanywa na baadhi ya wafanyakazi wa serikali, kupunguzwa. Wakati huohuo, Rais aliwataka wabunge kukubali mishahara yao kukatwa kwani ni baadhi ya wabunge anaopokea mishahara mikubwa duniani.

Swala la mishahara ya wabunge ni swala tete sana nchini Kenya.

Rais Kenyatta, alisema kuwa serikali inatumia kati ya dola dilioni 4.6 kwa mishahara ya wafanyakazi wa umma na kutumia dola bilioni 2.3 kwa maendeleo.

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KULAWITI

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu Wiliamu George 32 Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa Wilaya ya Mpanda kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti kijana mwenzie 22 Mkazi wa Mtaa wa Mpanda hoteli baada ya kumnywesha pombe ya kienyeji kupita kiasi.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na hukumu hiyo kuvuita hisia za watu mbalimbali wa maeneo ya mjiwa Mpanda na Mkoa wa Katavi.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu wa mahakama hiyo baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wa upande wa mashitaka na upande wa utetezi Katika kesi hiyo hapo awali mwendesha mashita mkaguzi wa jeshi la polisi Ally Mbwijo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Novemba 21 mwaka jana majira ya kumi na mbili jioni katika mtaa wa Mpanda Hotel.

Mshitakiwa siku hiyo ya tukiokabla ya kutenda kosa hilo la kumlawiti kijana huyo alidaiwa kunywesha pombe ya kienyeji aina ya komoni walikuwa wakichanganya na bia nyumbani kwa mwamke aliyekuwa akiwauzia pombe aliyetambulika kwa jina moja la Lita katika mtaa huo wa Mpanda hotel.

Ilielezwa na mwendesha mashita Ally Mbwijo kuwa mshitakiwa baada ya kuona mwenzake ametoka nje kwenda kujisaidia alimwagiza dukani Lita aende akamnulie sigara.

Aliileza mahakama baada ya kijana huyo ambae jina lake limehifadhiwa kurudi ndani aliendelea na kunywa pombe ambayo alikuwa imeisha kwenye chupa yake na ndipo alipoteza fahamu na mshitakiwa alitumia nafasi huyo kumwingilia kinyume cha maumbile yake huku akiwa amemlaza kwenye kochi.

Mwendesha mashitaka alieleza Lita alipotoka dukani alimkuta mshitakiwa akiwa amekaa karibu na kijana huyo ambae alikuwa amevuliwa nguo yake ya saruali na akiwa ajitambui na sehemu zake za matakoni zikiwa na mbegu za kiume.

Mshitakiwa baada ya kufanya kitendo hicho siku iliyofuata alimtuma mama yake mzazi aende kwa kijina huyo akamwombee samahani kwa kile alichoeleza kuwa anahofia kufungwa jela.

Baada ya mama mshitakiwa Wiliamu George kumwombea msamaha kwa kijana alilawitiwa alikubali kumsamehe mshitakiwa kwa kuhofia kupata aibu.

Mshitakiwa baada ya kusamehewa alianza kumtangaza kijana huyo kwa rafiki zake na kuwafahamisha kuwa kijana huyo ni shemeji yao kitendo ambacho kilimkasilisha kijana huyo na kuamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ya kulawitiwa kwake na Mshitakiwa Wiliamu George.

Hakimu mkazi mfawidhi Chiganga Ntengwa kabla ya kutowa hukumu hiyo aliiambia mahakama kuwa mahakama imemtia hatiani mshitakiwa Wiliamu George kwa kosa la kumwingilia kijana huyo kinyumbe na maumbile yake hivyo mahakama inatowa nafasi kwa mshitakiwa kama anasababu ya msingi ya kuishawisha mahakama impunguzie adhabu aieleza mahakama hiyo.

Katika uetezi wake mshitakiwa aliiomba mahakama imwachie huru kwani yeye hakutenda kosa hilo na pia umri wake bado ni kijana mdogo na wazazi wake bado wanamtegemea maombi ambayo yalipingwa vikari na mwendesha mashitaka.

Hakimu Chiganga baada ya kusikiliza utetezi huo aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa amehukumiwa na mahakama baada ya kupatikana na hatiaya kumwingilia kinyume na maumbile kijana huyo na anahukumiwa na adhabu ya kifungu cha sheria namba 235 sura ya 20 ya mwaka 2009 hivyo Wiliamu George mahakama imehukumu kutumikia jela kuanzia jana kifungo cha miaka 30 jela.

Chanzo: Katavi yetu

JUHUDI ZA KUTAFUTA NDEGE YA MALAYSIA ZAENDELEA

Wakati juhudi za kuisaka ndege iliyopotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Malasyia kuelekea Uchina zikiendelea, ndege moja ya Vietnam imeripoti kuwa imeona kitu kinachofanana na mlango wa ndege kwenye ufuo wa bahari ya Kusini mwa Uchina kwenye mwambao wa taifa hilo.

Hata hivyo hakuna thibitisho kuwa mlango huo ni wa ndege iliyopotea ya Malaysia, iliyokuwa na abiria mia mbili na thelathini na tisa.

Uchunguzi kuhusiana na kilichosababisha kupotea kwa ndege hiyo mapema siku ya Jumamosi, inawalenga abiria wawili wanaodaiwa kuwemo ndani ya ndege hiyo, waliotumia paspoti iliyoibiwa.

Stakabadhi hizo mbili za kusafiria kutoka Italia na nyingine Australia inaaminika kuibwa nchini Thailand.

Idara ya polisi ya Kimataifa, Interpol, inasema kuwa ni mapema mno kuhusisha pasi zilizoibwa na kutoweka kwa ndege hiyo.

Na huku kushughuli za kuisaka ndege hiyo zikiendelea, Msemaji wa shirika la ndege la Malysia amewaambia jamaa ya watu waliokuwemo katika ndege hiyo, kujiandaa kwa taarifa mbaya.

Amesema kufikia sasa hakuna mawasiliano yoyote na ndege hiyo masaa 30 sasa tangu itoweke.

Wakuu wa Malysia wanasema jumla ya meli 30 na ndege 44 kutoka mataifa tisa tofauti duniani, yamejiunga katika shughuli za kuitafuta ndege hiyo.

Kamanda William Marks wa kikosicha saba cha jeshi la wanamaji la Marekani, ametuma ndege aina ya USS Pinckney kusaidia katika usakaji huo.''

Jambo la kwanza kufanywa ni kukadiria mahala na kwa sasa tunalenga mawasiliano ya mwisho kutoka kwa ndege hiyo kabla ya kutoweka na mawasiliano ya rada.

Kutoka hapo tunahesabu mwendo kasi yaupepo na mawimbi. Kutoka hapo tunagawanya na eneo na tunatafuta kutumia kila kifaa tuliyonayo na hiyo siyo tu kutumia vifaa kutoka Marekani lakini pia kutumia meli na anga kutoka mataifa mengine ya dunia." Alisema kamanda huyo.

Ameonya kuwa shughuli hiyo ya kutafuta ndege hiyo inakumbwa na changamoto nyingi.

MWANAMKE AHUKUMIWA KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA POLISI

MWANAMKE mmoja amehukumiwa na mahakama ya wilaya ya Musoma, mkoani Mara, kutumikia kifungo cha miaka mitano na miezi sita jela, baada ya kupatikana na makosa ya kutoa matusi na kushambulia askari polisi wawili waliokuwa wanataka kumkamata.

Aliyekumbwa na adhabu hiyo ni Mary Jumanne, mkazi wa mjini Musoma, ambapo pia ameamriwa kuwalipa fidia ya shilingi laki moja kila mmoja askari polisi hao.

Hukumu hiyo imetolewa juzi na hakimu mwandamizi Richard Maganga, wa mahakama ya wilaya ya Musoma, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka.

Awali, imedaiwa mahakamani hapona mwendesha mashitaka wa serikali, Jonas Kaijage, kuwa mshitakwa huyo alitenda kosa hilo machi 3, mwaka huu, mjini Musoma.

Kaijage alisema kuwa mshitaikiwa huyo aliwashambulia na kutoa lugha ya matusi askari polisi wawili, PC. Hamis na WP.Kuruthumu kutoka ofisi ya afisa upelelezi wa mkoa wa Mara, waliokuwa wamekwenda kumkamata akikabiliwa na kosa jingine la kutoa lugha ya matusi.

Alisema kuwa baada ya polisi hao kutaka kumkamata ndipo mwanamke huyo alipowatukana nakisha akamshambulia askari wa kike WP.

Kuruthumu na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake. Mshitakiwa huyo baada ya kusomewa mashitaka yake alikiri kutenda makosa hayo huku akiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu, ombi lililotupiliwa mbali na mahakama hiyo.

Kufuatia ushahidi huo hakimu Maganga alihukumu kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kushambulia askari na kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kutoa lugha ya matusi.


Source:Habari leo

ITV, STARTV NA RFA VYAPEWA ONYO

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imevipa onyo kali vyombo vya habari vya Independent Television (ITV), Star Tv na Radio Free Africa (RFA) kwa kutangaza maudhui yanayoelezwa kuchochea uvunjifu wa amani na kuzuia wananchi kulipa kodi.

Aidha, sambamba na onyo hilo, piaimevitaka vyombo hivyo kuwasilisha kwa mamlaka hiyo miongozo yao ya kuchuja vipindi wanavyorusha hewani baada ya kubaini baadhi yao hawakuwa na miongozo hiyo na kuwataka wazuiewatangazaji kuingia na miziki yao binafsi studio.

Onyo hilo lilitolewa jana, Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Magreth Munyagi, ikiwa ni sehemu ya hukumu kwa vyombo hivyo kwa kukiuka Kanuni za Utangazaji za mwaka 2005 na kuhatarisha mshikamano wa Taifa, usalama wa Taifa na maadili bora.

Akisoma hukumu hiyo mbele ya waandishi wa habari katika Makao Makuu ya TCRA kabla ya kuwakabidhi wahusika, Munyagi alisema Kamati ya Maudhui ya TCRA inayosimamia maadili na maudhui ya utangazaji nchini ilibaini ukiukwaji wa kanuni hizo mwaka jana na mwaka huu na kabla ya uamuzi huo, ilikutana na wahusika kwa majadiliano na kufikia muafaka.

"Hivyo kwanza, kamati inatoa onyo kali kwa wahusika, pili, inawataka kuwasilisha mwongozo wa uchujaji wa vipindi vyao kwa mamlaka na tatu, ikiwa watarudia kosa hili, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Wahusika wana uhuru wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu katika kipindi cha siku 30 baada ya tamkohili," alisema Munyagi akisoma hukumu hiyo.

Akifafanua kuhusu uvunjifu huo wakanuni, Munyagi alisema kituo cha televisheni cha ITV na Star Tv kwa nyakati tofauti vilirusha hewani tangazo la taasisi ya Policy Forum linalohamasisha wananchi kutolipa kodi katikati ya taarifa za habari za usiku (saa 2:00 hadi 3:00) kinyume cha kanuni namba 5(a) na 6(b) za kanuni hizo.

Kuhusu RFA, alisema Juni 27 mwaka jana katika kipindi cha "Sindano tano za moto" kilichorushwa kati ya saa mbili hadisaa tatu asubuhi na radio hiyo, mtangazaji alipiga wimbo wa msanii Nashi (MC) inayoamsha hisia za uchochezi wa kisiasa, maandamano na uvunjifu wa amani kutokana na maudhui ya wimbo wenyewe.

Kufuatia majadiliano na pande zotembili, Munyagi alisema wahusika walikiri kutoa maudhui hayo kupitia vyombo vyao ambapo katika majadiliano Mkurugenzi wa ITV na Radio One, Joyce Mhavile alieleza kuwa, wao hawakuona uvunjifu wa amani katika tangazo hilo, bali elimu kwa umma kuhusu misamaha ya kodi na uwajibikaji wa serikali na jamii.

Aidha, Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki Star TV na RFA, kupitia Mkurugenzi wake Anthony Dialo na Meneja Mipango na Utafiti, Nathan Lwehabura, walikiripia kutumia muziki na tangazo hilona kuiomba TCRA isiwape adhabu kali kwa kuwa hawakuwa na mwongozo wa kuchuja muziki na maudhui kabla ya kuyarusha kwa jamii.

Akizungumza jana na waandishi mara baada ya hukumu hiyo, Lwehabura alisema hatua hiyo ni changamoto kwa vyombo vyote vya habari kwa kuwa wao binafsi hawakuona kosa kutokana na ukweli kwamba hata baadhi ya viongozi wa serikali huzungumza wazi wazi kuhusu misamaha ya kodi lakini wanaheshimu uamuzi wa TCRA na tayari wamesitisha matangazo hayo.

"Tumekiri kwamba tulitangaza maudhui yaliyosomwa, lakini hili linazungumzika na pia ni suala la mjadala kwa wanahabari wote, StarTV na ITV ni kama kondoo wa kafara tu, tunapaswa kujadili nini ni uchochezi maana hili la kodi hata Bungeni linazungumzwa, tumejifunza unapopata tangazo kutoka taasisi hizi binafsi, lazima utafsiri kama ni uchochezi ama la,"alisema Lwehabura.

ICC YAMPATA NA HATIA GERMAIN KATANGA

Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imempata na hatia ya uhalifuwa kivita mbabe wa kivita kutoka Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Germain Katanga.

Hata hivyo Katanga hakukutwa nahatia katika shtaka la udhalilishajiwa kijinsia.

Alituhumiwa kuhusika na mauaji ya wanavijiji zaidi ya 200 mwaka 2003 katika jimbo la Ituri lenye utajiri wa dhahabu, kaskazini mashariki mwa Congo.

Katanga ni mtu wa pili kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC tangu ianzishwe mjini The Hague, Uholanzi mwaka 2002.

Katika shambulio hilo lililotokea mnamo Februari 24, 2003 watu 200 waliuawa katika kijiji cha Bogoro karibu na mpaka wa Uganda,Katanga wakati huo akiwaKamanda wa kundi la waasi la Patriotic Resistance Force of Ituri(FRPI) lililotekeleza mauahi hayo.

Mwendesha mashtaka amesema nia yao kuu ilikuwa kuangamiza kijiji kizima.

Germain Katanga kwa jina la utani Simba alikanusha mashtaka hayo yote dhidi yake .

MWANAJESHI FEKI ATUPWA JELA MIAKA MITATU

MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela mwanamume aliyejifanya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kufanya utapeli.

Bakari Saibo (32) mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam, alihukumiwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Bunda, Said Kasonso, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa mashitaka.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Masoud Mohamed, alidai kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 28 mwaka huu, saa 12:15 jioni.Alidai mshitakiwa huyo akiwa katika eneo la nyumba moja ya kulala wageni iitwayo Mori iliyoko mtaa wa Posta mjini Bunda, alijitambulisha kwamba ni askari wa JWTZ.

Aidha alidai mshitakiwa alijitambulisha kwa Kamira Nkengemkazi wa mtaa huo aliyemtilia shaka na kutoa taarifa Polisi. Alidaimbali na kujitambulisha hivyo, pia alimtapeli Nkenge nguo zake zenye thamani ya Sh 100,000 na kwamba baada ya polisi kupata taarifa hiyo, walimkamata na kumpeleka mahakamani hapo.

Hakimu Kasonso alisema kosa la kwanza la kujifanya mwanajeshi wa JWTZ, anamhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kosa la pili la utapeli anamhukumu kifungo cha miaka miwili jela.

Adhabu hizo zatazitumika kwa pamoja. Kabla ya hukumu kutolewa mwendesha mashitaka wa Polisi, aliiomba Mahakama hiyokutoa adhabu kali kwa mshitakiwa, kwani tabia hiyo inachafua sifa za majeshi.

MTU MMOJA AFARIKI NA WENGINE 38 KUJERUHIWA

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 38 kujeruhiwa, kati yao 14 vibaya, baada ya magari matatu waliyokuwa wakisafiria, kugongana, mawili uso kwa uso, huku jingine likijaribu kukwepa ajali, katika eneo la Bwawani, barabara kuu ya Morogoro-Dar es saalam, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

ITV imefika eneo la tukio na kushuhudia magari mawili kati ya yaliyohusika na ajali, yakiwa yameharibika vibaya, hasa sehemu ya dereva, ambapo mkuu wa usalama barabarani Chalinze mkoani Pwani, Inocent Sule, amesema chanzo cha ajali ni basi la abiria, mali ya kampuni ya Linowele class, lililokuwa likitokea dar es salaam kuelekea malinyi wilayani ulanga, , likiendeshwa na mtu aliyefahamika kwa jina moja la musa kujaribi kulipita gari jingine lililokuwa mbele na kukutana uso kwa uso na tenka la mafuta aina ya Iveco, ambapo dereva wa tenka, ali hassan ngoma, mkazi wa korogwe mkoani tanga, amefariki dunia papo hapo, huku yule wa basi hali yake ikiwa ni mbaya sana na la tatu mali ya kampuni ya adventure aina ya nisan diesel, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Kigoma liliyagonga magari hayo yaliyokuwa yamepata ajali.

Mashuhuda wa ajali hiyo, wakiwemo majeruhi walionusurika kifo katika ajali hiyo, ambao baadhi yao wamekimbizwa kupatiwa huduma ya kwanza katika zahanati ya magereza bwawani, wamezungumzia kuhusiana na namna walivyobaini ajali hiyo, huku mganga wa zahanati ya sekondari ya magereza Bwawani, Lazaro Mdeka, akikiri kupokea majeruhi 38, na 14 hali zao ni mbaya na wamekimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro kwa matibabu.

Katika hospitaliya mkoa wa Morogoro, huduma za kuwapokea na kuwahuduma majeruhi hao zimekutwa zikiendelea, huku wengi wakishindwa kuzungumza kutokana na hali mbaya.

Chanzo:ITV

NDUGU WAWILI WATUHUMIWA KUMUUA MPENZI WA MAMA YAO

NDUGU wawili wa kiume wa familia moja wilayani Mlele mkoa wa Katavi, wanatuhumiwa kumuua mpenzi wa mama yao kwa kumchinja, kisha kutelekeza mwili wake porini. Wakazi hao ambao mmoja ni mtoto mwenye umri wa miaka 16 ni wakazi wa Kitongoji cha Milumba Kata ya Kibaoni na aliyeuawa ni Kitungulu Luhende (65).

Inadaiwa mama yao, Sai Mponje (65) ambaye ni mjane anayeshikiliwa na polisi kwa sasa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Luhende, jambo ambalo watoto hao hawakufurahishwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alitaja watuhumiwa hao ni Nyengu Kashele (19) na nduguye mwenye umri wa miaka 16.

Mtoto huyo anashikiliwa wakati Nyengu amejificha kusikojulikana. Mwili wa marehemu uligundulika Machi 3, mwaka huu saa 3:30 asubuhi katika milima ya kitongoji hicho cha Milumba ukiwa umeharibika.

Mwili huo uligundulika kutokana na msako uliofanywa na askari wa jadi(sungusungu) kwa kushirikiana na polisi na wananchi. Kidavashari alisema Februari 22, mwaka huu saa 2 asubuhi, Luhende ambaye pia ni mkazi wa kitongoji hicho cha Milumba, alimuaga mkewe kwamba anakwenda kijiji cha Kirida ambako ana mke mwingine.

Hata hivyo, Kamanda alidai kuwa badala ya kwenda kijijini Kirida, aliko mke wake mwingine, kwanza alipitia nyumbani kwa rafiki yake katika kitongoji hicho cha Milumba, aitwae Milembe Katembeni ambako aliacha pikipiki yake yenyenambari za usajili T449 BAF. Inadaiwa kisha alikwenda moja kwamoja kwa Sai (mama wa watuhumiwa).

Kamanda alisema tangu hapo hakuonekana hadharani hadi mwili ulipokutwa umetelekezwa eneo la milimani huku pembeni kukiwa na leseni yake ya udereva.

Akielezea sababu za kuanza kumtafuta, Kamanda alisema baada ya kutorejea kwa rafiki yake kuchukua pikipiki, Katembeni aliingiwa wasiwasi ndipo Machi 2 , mwaka huu aliamua kutoa taarifa kwa kiongozi wa sungusungu na kisha polisi, na msako ukaanza.

MCHUNGAJI ASHIKILIWA KWA MAUWAJI

MCHUNGAJI mstaafu wa Kanisa la Anglikana, Usharika wa Mfarasi kata ya Madilu wilayani Ludewa, mkoani Njombe, Petro Chambachamba (87) anashikiliwa Polisi akihusishwa kwenye kesi ya mauaji.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani, amesema jana kuwa Chambachamba pamoja na watu wengine wanane, wamekamatwa wakihusishwa na mauaji yaliyotokea Februari 25, mwaka huu saa 8 mchana katika kijiji cha Mfarasi.

Alisema watu hao wanatuhumiwa kuchukua sheria mkononi kwa kumpiga hadi kumsababishia kifo Boniface Mtweve (35), mkazi wa kijiji cha Ilininda kilichoko kata ya Madilu wakimtuhumu kuiba simu tatu mali ya Nuru Ngairo.

Kamanda alisema kwa kupitia taarifa za siri kutoka kwa wakazi wakijiji hicho, Februari 28, watu hao walikamatwa na kufikishwa mikononi mwa dola. Wengine waliokamatwa ni Linus Chaula, Stanley Katembo, Ery Mwapinga, Kedimoni Mwapinga, Phillimon Mgimba, Richard Mvalla, Meshack Mgaya na Nuru Ngairo.

"Ushahidi wa awali unawahusisha watu hao tisa akiwemo mchungaji huyo, hata hivyo wanaweza kuachiwa huru endapo baadaye wataonekana kutohusika na tuhuma hiyo na uchunguzi unaendelea," alisema Kamanda.

Hata hivyo, waumini wa usharika huo wamedai vyanzo vya taarifa za Polisi zinazomuhusisha mzee huyo katika kesi hiyo, ni vya uongo na wameomba aachiwe huru.

Zaidi ya wananchi 600 wa kijiji hicho, juzi walishiriki mkutano maalumu wakishutumu kuchukuliwa kwa mchungaji pamoja na watuhumiwa wengine.

Katika mkutano wa kijiji uliofanyika katika kijijini Mfarasi, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Petro Mwapinga alisema, " inasikitisha Polisi walivamia kijijini hapa usiku wa manane na kuwakamata ndugu zetu bila kushirikisha uongozi wa kijiji."

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Samwel Mtewele alisema wote wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji hayo, ni wale waliotoa taarifa katika kituo cha Polisi cha Lugarawa wilayani Ludewa, kwamba nyumba zao zilivunjwa na mali zao mbalimbali ziliibwa.

Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisala Anglikana Dayosisi ya Kusini Magharibi, Michael Lugome, alieleza kushangazwa na hatua ya Polisi kumkamata mchungaji huyo na wenzake.

"Taarifa tuliyopewa na Kijiji inaonesha kwamba kabla ya mauajihayo, Mchungaji wetu mstaafu na watuhumiwa wengine, walivunjiwa nyumba zao na mali zao kuibwa; taarifa hizo zilipelekwa Polisi, na askari walipaswa kuzifanyia kazi taarifa za wizi huo," alisema Lugome.

"Hili ni tukio la aina yake na yawezekana likawa la kwanza; lakini tuna maswali ya kujiuliza ni wapi na katika mazingira gani tukiohilo lilitokea na watu hawa akiwemo mzee huyo wa miaka 87 alishirikije katika tukio hilo," alisema Mwenyekiti wa Idara ya Uinjilisti ya Dayosisi hiyo, Nicholaus Mgaya.

Mke wa Mchungaji huyo, Lea Chambachamba, alisema mumewealikuwa nyumbani wakati watu wenye hasira kali kijijini hapo wakimpiga mtuhumiwa.

Alisema kabla ya tukio hilo, nyumba yake ilivunjwa na vitu kuibwa ambavyo inadaiwa mtuhumiwa huyo aliyeuawa, alikutwa navyo.

"Polisi hawajatenda haki, mume wangu ana miaka 87, mimi nina miaka 70; mzee wa umri huo anawezaje kwenda kwenye kundi lenye watu wengi na kushiriki kumshambulia mtu?" alisema.


Source: Habari Leo

JUHUDI ZA KERRY ZAGONGA MWAMBA

Juhudi za marekani kuwakutanisha kwa mara ya kwanza ana kwa na mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi na Ukraine kuhusu mzozo unaoendelea katika jimbo la Crimea zimegonga mwamba.

Ingawa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Marekani John Kerry amekanusha kwamba palikuwa na nia ya kumkutanisha mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov na waziri mpya wa mashauri ya nchi za wa Ukraine Andrii Deschchytsia iwapo wawili hao wangekutana mjini Paris ingekuwa ni mafanikio makubwa ya kidiplomasia.

Sergei Lavrov alikataa kukutana na waziri huyo mpya wa Ukraine kwa sababu Urusi haitambui utawala mpya wa mjini Kiev.

Akizungumza mjini Paris Bwana Deschchytsia amesema licha ya vuta nikuvute hiyo anaamini kwamba kuna dalili ya mafanikio katika mashauri." Kwa hiyo baada ya kuwa hapa siku nzima mjini Paris, inaonekana kwamba tunaendeleana mashauri yetu na tunaamini kwamba tutapata mwafaka.

Ninaelekea mjini Brussels kukutana na waziri mkuu kujadili hatua zaidi za kuchukua. Shukran.

"Na alipoulizwa na mmoja waandishi wa habari ni kwa nini hakuweza kukutana na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi Sergey Lavrov hivi leo, bwana Deschchytsia alijibu- ''kamuulize Lavrov mwenyewe.''

Hata hivyo bwana Lavrov alifanya mazungumzo ya kina na waziri wamashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry na mawaziri wengine wa umoja wa ulaya. Bwana Kerry alitaja mkutano huokuwa mgumu lakini akasema ana ujumbe atakaoupeleka kwa rais Obama na mazungumzo yataendelea.

Waziri wa mashauri ya nchini za kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius kadhalika alielezea matumaini ya mazungumzo hayo kufanikiwa."

Tumekubaliana kuendelea na mashauri kwa sababu mambo bado na hali sio rahisi anasema bwana Fabius. Lakini tunayo furaha kwamba siku ya leo mjini Paris imeturuhusu kuanzisha mikakati.''

Kwa upande mwingine rais wa Urusi Vladmir Putin alifanya mazungumzo kuhusu mzozo huo na chanzela wa Ujerumani Angela Merkel kwa njia ya simu.

Wakati huo huo Mwakilishi mkuu wa Umoja wa mataifa huko Crimea, Robert Serry, amelazimika kukatiza ujumbe wake baada ya kutishiwa na watu waliojihami alipokuwa akitoka katika makao makuu ya jeshi la wanamaji la Ukraine katika bandari ya Simferopol.

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA DAR ZAZUA MAAFA

Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam, zimesababisha maafa kutokana na baadhi ya magari kupinduka barabarani mengine kukwama kwenye mashimo na msongamano wa muda mrefu kutokana na magari kuteleza na miundombinu ya barabara kuharibika.

Akizungumza katika eneo la tukio Kongowe Mzinga jijini Dar es Salaam kondakta wa lori lililopinduka katika barabara hiyo Casmir Michael amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya mwenye daladala kusimama ghafla mbele ya lori lao ndipo breki za gari lao kukataa na tairi kupoteza mwelekeo kisha gari kupinduka.

Baadhi ya mashuhuda wa ajali ya haisi wamesema chanzo ni baada ya haisi kuigonga gari nyeupe iliyokuwa imeharibika barabarani lenye namba za usjaili T591 CGP na kushindwa kushika breki saa chache kabla halijatumbukia mtaroni kwa kuwa mbele kulikuwa na shimo kubwa lililochimbika baada ya kunyesha kwa mvua.

Nao madereva waliokumbwa na adha ya mrundikano wa foleni barabani wameiomba serikali kutengeneza makarabati imara na barabara za pembeni ili magari yaweze kupita kwa urahisi zinapotokea ajali kwenye barabara hiyo.

Imeshuhudiwa gari la magereza nalo likiwa limenasa kwenye barabara ya pembeni hali iliyowalazimu askari magereza kushuka kwenye gari lao kisha kulisukuma walipokwama wakiwa njiani kuelekea wilayani Mkuranga mkoani Pwani kusindikiza mahabusu wao.

KIJANA AJICHINJA MPAKA KUFA(SAHAMANI KWA MUONEKANO WA PICHA)

AMA kweli duniani kuna mambo kwani dereva na abiria wa basi la Manchester ambalo namba yake haikujulikana mara moja, lililokua likitoka Lindi kwenda jijini Dar es Salaam walijikuta wakiangua vilio baada ya kumuona mwenzao akijichinja hadi kufa kwa kisu ndani ya gari hilo.

Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa alasiri, Jumatano wiki iliyopita mara basi hilo lilipofika katika hoteli moja ya Nangulukulu kwa ajili ya kupatia chakula.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya abiria walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa mara walipofika katika hoteli hiyo, kila mmoja alitawanyika kwa lengo la kujipatia chakula na baadhi yao walienda maliwatoni akiwemo marehemu huyo.

Walisema kwamba marehemu huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, wakati wa kushuka hakuonekana na kisu aina ya sime lakini baadaye abiria wachache waliotangulia kwenye gari, walimshuhudia akiwa ameshika sime hiyo mkono pasipokujua aliipata wapi.

"Hata sisi tulishangaa kumuona akiwa karibu na usukani wa dereva huku akizamisha sime tumboni kisha kuichomoa na kujichinja shingoni hadi pale alipokuwa akivuta koromeo na kuning'inia.

"Tulichanaganyikiwa kwani ni kitu ambacho hatukukitarajia na wala hatujawahi kushuhudia tukio kama hilo la mtu kujichinja hadharani, tulibakia kutokwa machozi huku akina mama wakipiga yowe, hakuna mtu aliyethubutu kumsogelea kumuokoa kwani kila mmoja alimuogopa.

"Tulishindwa kupanda basi hilo kwani ni tukio la ajabu pia ndani kwa mbele kulikuwa kumetapakaa damu, ghafla alidondoka chini ndani ya gari, aliomba kalamu na karatasi ili kuandika ujumbe.

"Dereva alichukua kalamu na kipande cha karatasi na kumpa, alianza kuandika huku damu ikimbubujika tumboni na shingoni, hatukujua alichokiandika, aliishiwa nguvu taratibu akadondoka.

"Abiria walimsogelea na kumuinua na walimueleza kuwa atubu kwa Mungu kosa alilolifanya kabla hajafa, alipiga magoti na kuomba, ghafla alidondoka tena.

"Kaka yake ambaye alikuwa akisafiri naye kuelekea Dar es Salaam alichanganyikiwa kwani hakutegemea kuwa mdogo wake angejiua, kwani alisema hana historia ya kuugua ugonjwa wa akili.

Polisi walipigiwa simu na walifika kumchukua lakini baada ya muda mfupi akawa amefariki dunia.

"Sisi abiria wengine tuliendelea na safari kuelekea Dar es Salaam ambapo marehemu na kaka yake walibakia huko mkoani Lindi.

"Mara tulipofika Dar es Salaam dereva alitusihi tukae kimya kwa dakika moja na kuomba kutokana na tukio lililotupata, tulifanya hivyo baadaye kila mmoja alitawanyika na kuelekea kwake,"kilisema chanzo kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alipoulizwa mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusiana na tukio hilo alikiri kutokea.

"Ni kweli tukio hilo lilitokea lakini kwa sasa sina data kwani nipo njiani nikitokea Nairobi, Kenya kikazi kuelekea Lindi, mara nitakapofika huko ofisini ndipo nitapata tukio zima lilivyokuwa,"alisema Kamanda Mzinga.


Chanzo: Jf

WAWILI WANUSURIKA KUFA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI KWA SIKU TANO

Watu wawili wamenusurika kufa baada ya kufukiwa na kifusi kwa siku tano katika machimbo ya dhahabu mkoani Geita na kuokolewa wakiwa katika hali mbaya.

Eneo hilo lipo chini ya leseni ya mgodi wa dhahabu wa Geita na shimo hilo lilikuwa likitumika zamani ambapo kwa sasa halitumiki, mara kwa mara vijana waishio katika mji wa Geita na vijiji vya jirani hufika eneo hilo kuchimba ili kuweza kuambulia angalau masalia ya mchanga wenye dhahabu hata hivyo uongozi wa mgodi huo kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamekuwa wakijitahidi kuwazuia vijana hao kutofika eneo hilo kwa kuwa si salama.

Daktari mfawidhi katika hospitali ya wilaya ya Geita Adam Sijaona amethibitisha kupokelewa kwa vijana hao amesema hali zao zinaendelea vizuri, ambapo kwa upande wa mgodi wa dhahabu wa Geita wamewataka viongozi na wananchi waishio kandokando ya mgodi huo kuwaelimisha vijana wao kutovamia maeneo hatarishi kama hayo.

Imedaiwa kwamba kuna baadhi ya wanasiasa ndio wanaowashawishi vijana hao kuvamia maeneo ya uchimbaji yasiyo rasmi ili kuweza kujiongezea mvuto kwa wapiga kura ambapo jeshi la polisi limewataka wananchi kutovunja sheria kwa shinikizo la wanasiasa.

WAISLAM WALAANI KUCHANWA KWA KORAN

Mamia ya waislam wamefanya maandamano katika mji mkuu wawa Mauritania Nouakchott, baadaya kuenea kwa taarifa kuwa Koran imechanwa msikitini.

Imam ameripoti kuwa watu wanne waliokuwa wamefunika nyuso zao waliingia msikitini , wakachana nakala za Koran na kuzitupa chooni.

Polisi walifyatua mabomu ya kutolea machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa na jazba, na mtu mmoja aliuawa, duru za polisi zilieleza.Mauritania ni taifa la kiislam , likiwa na idadi ndogo ya wakristo.

Imekuwa mshirika muhimu wa nchi za magharibi katika kampenidhidi ya al-Qaeda na makundi mengine ya wanamgambo yanayoendesha harakati katika kanda hiyo.

Mwandishi wa habari Hamdi Mohamed El Hacen aliyeko mjini Nouakchott anasema waandamanaji walichoma vizuizi na maduka mengi na masoko yalifungwa jana siku nzima.

Mamia ya waandamanaji walikusanyika kati kati mwa mji mkuu na nje ya msikiti wakipaza sauti "Mungu ni mkuu" wakidai wahusika wakamatwe na kuhukumiwa kifo kwa madai ya kukufuru uislam, alisema.

PUTIN: URUSI HAIJAPELEKA MAJESHI UKRAIN

Rais Vladimir Putin wa Urusi, amesema bado hakuna haja kwa nchi yake kupeleka majeshi nchini Ukraine.

Bwana Putin amesema Urusi ina haki ya kutumia njia zote kulinda raia wake walioko mashariki mwa Ukraine.

Amekanusha taarifa kwamba majeshi ya Urusi yamewazingira raia wa Ukraine walioko katika jimbo la Crimea, bali ni watu wanaoiunga mkono Urusi na ambao wanajilinda wenyewe.

Bwana Putin amesema kuondolewa madarakani kwa RaisViktor Yanukovych katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev ni "ukiukaji wa katiba na uporaji wa madaraka kijeshi.".

Amesema wapiganaji hao wameitumbukiza Ukraine katika"vurugu". Pia amesema wapiganiautaifa na wapinga usemiti wanarandaranda katika mitaa ya Kiev na miji mingine.

Amesema iwapo watu wanaozungumza Kirusi mashariki mwa Ukraine watahitaji msaada wa Urusi, basi Urusi itakubaliana na ombi lao.

"kama tutaona hali hii ikianza kutokea maeneo ya mashariki, tuna haki ya kutumia kila njia" amesema.

Bwana Putini amesema katika jimbo la Crimea watu wenye silaha wanaoiunga mkono Urusi na raia wamezingira kambi za kijeshi za Ukraine, sio askari wa Urusi.

"Majeshi ya eneo hilo kwa ajili yakujilinda" ndiyo yanayohusika na kuchukuliwa kwa majengo ya serikali katika Crimea, amesema.

Ukraine imesema Urusi imepeleka maelfu ya askari katika eneo la Crimea hivi karibuni.

Uhasama umeongezeka katika kituo cha kijeshi cha Belbek karibu na Sevastopol, mji wa bandari ambao ni kambi ya majeshi ya majini ya Urusi.

Akizungumzia kupinduliwa kwa Bwana Yanukovych, Bwana Putin amesema kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani nchini Ukraine alikubali matakwa yote ya wapinzani.

Bwana Putin amesisitiza kuwa Bwana Yanukovych bado ni rais halali wa Ukraine.

Amesema kuna mambo matatu ya kumwondoa madarakani rais, ameyataja kuwa ni kifo, kujiuzuluau kushtakiwa.

Bwana Yanukovych alikimbilia Urusi, na Bwana Putin aliwaambia waandishi wa habari:

"Sifikiri kama ana mustakabhali mwema kisiasa".

Urusi ilimsaidia kwa sababu za"kibinadamu", amesema,

"vinginevyo angekuwa ameuawa".

WABUNGE WA BUNGE LA KATIBA WATOFAUTIANA

Wajumbe wa bunge la katiba wamekuwa na mtazamo tofauti wa kuwasilisha mapendekezo ya vifungu vya rasimu ya kanuni za bunge vilivyo na matatizo baada ya baadhi ya wabunge kuonyesha kutokubaliana na pendekezo la mwenyekiti wa muda lililotaka wawasilishe kwa maandishi kwa kamati ya kanuni.

Hatua hiyo ya wajumbe ilizua kutokusikilizana kwa baadhi ya wajumbe na mwenyekiti huku wajumbe wengine wakisimama na wengine kuwasha vipaza sauti bila ya utaratibu hali iliyomlazimu wa mwenyekiti wa semina ya wajumbe kuzungumza.

Katika semina hiyo baadhi ya wajumbe wameshauri rasimu hiyo ipitiwe kurasa kwa kurasa huku wengine wakipongeza utaratibu wa mwenyekiti wa muda unaotaka mapendekezo yawasilishwe kwa kamati ya kanuni kwa maandishi.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wajumbe wamelalamikia wajumbe wa kamati ya kanuni kuzingatia zaidi hoja za makundi makubwa na kuziacha hoja za watu wachache katika kutengeneza rasimu ya kanuni za bunge maalum.

DARAJA LA KIGAMBONI LAKAMILIKA KWA 45%

Daraja la Kigamboni limekamilika kwa zaidi ya asilimia arobaini na tano na matumaini makubwa ya kumalizika kwa ujenzi huo kwa muda uliopangwa Julai mwakani yakionekana huku nyumba zilizokuwa zinazuia ujenzi huko zikibomolewa kwa nguvu na serikali.

Akizungumza na ITV jijini Dar es Salaam meneja mradi huo injinia Karim Mattaka amesema ujenzi huo umeshaanza kuleta matumaini makubwa kutokana na nguzo mbili zilizokuwa zinakwamisha kuwa tayari na zoezi linaloendelea ni kuhamisha maji katika maeneo yalinayochimbiwa nguzo hizo sambamba na kuchimbia nguzo kubwa za kupokea baraja hilo upande wa barabara ya Mandela.

Aidha injinia Karimu amejaribu kufafanua mfumo wa barabara na daraja hilo namna utakavyotumika baada ya kukamilika na kuwahakikishia watanzania ujenzi huo utakamilika kwa wakata kama mambo yataenda kama yalivyopangwa.

Mwenyekiti serikali ya mtaa wa Vijibweni Bw. Athman Ally akielezea kuhusiana na hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuvunja nyumba za baadhi ya wakazi waliogomea fidia amesema wao walipewa taarifa na mwanasheria mkuu na baadaye akatakiwa kwenda kusimamia zoezi la uvunjaji wa nyumba hizo.


Chanzo:ITV

CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY(ACT) CHATAMBULISHWA

KILE kinachotafsiliwa kuwa Demokrasia nchini imeanza kukuwa kutokana na wingi wa vyama vya kisiasa nchini vinaanzishwa, hivi leo chama kipya cha kisiasa nchini kimeanzishwa chama hicho kinajulika kama ACT,(Alliance for change And Transparency)maana yake ni Umoja wa Mabadiliko na Uwazi.

Hayo, yamethibitishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho kipya, Limbu Lucas Kadawi Wakati akitambulisha Chama hicho kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari, ambapo alisema wamefikia maamuzi ya kuanzishwa chama hicho kutokana na Malengo mahususi ya kuwaleta watu pamoja.

"Tumeanzisha chama hichi cha kisiasa kwa malengoma hususi ya kuwaleta watu pamoja watanzania wanaoamini kwamba nguvu ya Pamoja inaitajika katika kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa katika nchi hii, na kwamba uwazi na uadilifu ni tunu ambazo taifa hili linaitajika kwa sasa na Baadaye"alisema Limbu

Limbu alisema chama hicho cha ACT kinatakuwa kinaongozwa na misingi mikuu mitano ambayo ndio itakuwa nembo ya chama hicho.

"ACT tutakuwa na inaongozwa na misingi mikuu mitano ambayo ni Uzalendo,Usawa,Uadilifu Uwazi na uwajibikaji pamoja na Demokrasia ya Kweli" Alizidi kuongezea Limbu.

Limbu ikumbukwe Mwaka 2010 alikuwa Mwanachama wa cha Wananchi CUF na aligombania Ubunge kupitia Chama hicho kwenye Jimbo la Temeke na Alibwagwa kwenye uchaguzi huo na Mbunge wa CCM kupitia Temeke, Mr Mtevu na Baada ya Hapo na kwenda kuanzishwa chama cha ADC kabla ya kuanzishwa chama hichi.

Aliwataka wananchi wakiamini chama hicho kuwa ni Chama kitakachowaletea maendeleo.

Kwa upande wake Katibu mkuu Taifa wa Chama hicho Samsoni Mwigamba alisema Chama hicho kwa sasa kimeanda mipango mikubwa ya kuhakikishwa kinashinda kwenye Chaguzi Mbalimbali Zinazokuja.

"Kwa sasa ACT Tanzania imekwisha Kukamilisha Rasimu ya awali ya Katiba ambaye iliwezesha kupata usajili wa Muda na Zoezi la kuandikishwa wananchama katika mikoa kwa ajali ya kuomba usajili wa kudumu kwa mujibu wa sheria limekwisha kamilika"

"Tumewapata Wanachama katika mikoa yote ya Tanzania Bara,hata ivyo tumechagua mikoa kumi ambayo tungependa Msajili akahakiki kama sheria inavyotaka"alisema Mwigamaba.

Ikumbukwe Samsoni Mwigamba kabla ya kujiunga na chama hichi cha ACT alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoani Arusha na pia alikuwa mhasibu Mkuu wa Chama hicho na Baada ya hapo Chama chake cha Chadema kilimvua uwanachama kwa kile chama hicho kinadai kuwa Mwigamba alikuwa anafanya Uasi katika chama hicho, ambapo Kamati kuu ilimvua uwanachama pamoja na Wananchama wengine akiwemo Ziito Kabwe pamoja na Dk Kitara Mkumbo.

Wachambuzi wa Masuala ya Kisiasa waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu walisema chama hicho kipya cha kisiasa nchini uwenda kikawa kimeanzishwa kwa mahususi ya kuwachukua wanachama waliokuwa wamevuliwa uwanachama kwenye vyama tofauti vya kisiasa nchini, huku wachambuzi hao wakihoji kwanini chama hicho cha kisiasa kimeanzishwa sasa, wakati vyama vya kisiasa nchini vikiwa katika hali ya sitofamu.

Ambapo Kauli hiyo ilipingwa vikali na Mwenyekiti wa Chama hicho cha ACT alisema chama hicho wala hakina uhusiano wowote na Mtu wala mikoa bali chama hicho kinawahusishwa watanzania wote.

WABUNGE WASHAMBULIWA LIBYA

Wabunge wawili nchini Libya walipigwa risasi na kuumizwa baada ya kundi la waandamanaji kuwashambulia bungeni katika mji mkuu wa Tripoli.

Walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa wawili hao walipigwa risasi walipojaribu kutoroka kutoka katika eneo hilo.

Waandamanaji hao waliokuwa na ghadhabu walilishambulia bunge hilo, huku wakitaka bunge lifungwe na tarehe mpya ya uchaguzi wa mapema itangazwe.

Kumekuwa na wimbi la maandamano nchini humo kutokana na uamuzi wa bunge la nchi hiyo kuahirisha tarehe ya uchaguzi hadi baadaye mwakani.

Waliolishambulia bunge siku ya Jumapili walisema kuwa walighadhabishwa pia na "kutekwa nyara" kwa waandamanaji waliokuwa na kikao nje ya bunge.

Walisema kuwa waliohusika na utekaji nyara huo walikuwa chini ya uongozi wa waasi wanaotumikia amri ya bunge.

Waandamanaji hao ambao wengi wao ni vijana walijihami kwa visu na vijiti, wakalishambulia bunge huku wakiwa na ujumbe kwa wabunge kwa kuimba "jiuzulu, jiuzulu", kwa mujibu wa taarifa ya ashirika la habari la AFP.

Bunge la nchi ya Libya limeshambuliwa mara kadhaa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Nuri Abu Sahmein ambaye ni spika wa bunge hilo aliambia kituo cha televisheni cha Al-Nabaa kuwa maandamano yaliyokuwa ya amani, yalivurugwa na watu waliojihami.

"Wabunge wawili walipigwa risasi pale walipojaribu kutoweka mahali hapo kwa kutumia magariyao," alisema.

Haikuwezakana kubaini papo hapo idadi ya wabunge walioumia.

Picha zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha waandamanaji wakivuta kile kilichokusudiwa kuwa kiti cha Spika wa bunge hilo nje ya bungena kukichoma.

Mwandishi wa BBC Rana Jawad ambaye yuko Tripoli anasema kuwa bunge la Libya limeshambuliwa mara kadhaa na makundi tofauti, yakiwemo makundi ya waasi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Uchaguzi uliokuwa wa amani ulifanywa na nchi ya Libya katika mwezi wa Julai mwaka jana, ila bado nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ingali inang'ang'ana kupata utulivu, miaka mitatu baadaye tangu kufurushwa kutoka maamlakani kwa aliyekuwa rais, hayati Muammar Gaddafi.

OSCAR PISTORIUS AKANA MASHITAKA

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amekanusha mashitaka ya kumuua mpenzi wake wakati kesi yake ikianza kusikilizwa mjini Pretoria.

Pistorius ambaye ana ulemavu wa miguu na ambaye hutumia miguu bandia ameshitakiwa kwa kumuua mpenzi wake na mwanamitindo Reeva Steenkamp.

Oscar amesema alimpiga risasi marehemu kimakosa kwani alidhani alikua mwizi.

Katika siku ya kwanza ya kesi hiyo jirani wa Oscar Michelle Burger , ameambia mahakama kuwa alisikia mwanamke akipiga mayowe mapema asubuhi tarehe14 mwezi Februari mwaka 2013.

Bwana Pistorius amekanusha madai dhidi yake kuwa alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Alimpiga risasi na kumuua Steenkampe aliyekuwa na umri wa miaka 29 mwanamitindo na muigizaji akisema kuwa hakumuua kwa maksudi.

Jirani ya Oscar alisema kuwa kiliocha mwanamke huyo kilifuatiwa na milio ya risasi ''alipiga nduru akitaka msaada. Pia alisikia mwanamume akipiga mayowe naye akiomba msaada, ''alisema mwanamke huyo.

Alisema punde alipopiga simu kutaka msaada kutoka kwa polisi hapo ndipo alisikia milio ya risasi.

Kukamatwa kwa Pistorius kulishangaza wengi nchini Afrika Kusini.

Pistorius mwenye umri wa miaka 27 alishinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya walemavu mjini London mwaka 2012 na pia alishindana katoka michezo rasmi ya olimpiki.

Kesi hiyo ilicheleweshwa wa dakika 90 kwani mkalimani wa lugha ya Afrikaans hakuwepo mahakamani.

Pistorius inasemekana alionekana mtulivu alipowasili mahakamani.

Pistorius anasema kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake. Mauaji yake yalitokea siku ya Valentines mwaka jana.

Wiki jana mashirika ya habari za michezo, yalipata idhini ya kupeperusha kesi ya Pistorius moja kwa moja kutoka mahakamani.

CHATU AMSHINDA MAMBA NA KUMMEZA

Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa Queens Land, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.

Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.

Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.

Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.

Nyoka alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji Chatu huyo alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake

Tiffany Corlis, mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi."lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC

"Tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumbana mamba hasa katika sehemu ya miguu ili kumdhibiti.''
"Pambano lilianzia ndani ya maji.

Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''

"Baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kuanza kumla,'' alisema Tifanny.

Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua nyoka muda wa robo saa kumla mamba huyo.

''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.

Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu saa 5. Hatimaye wote walionekana wachovu.

''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.

WACHAPANA MAKONDE MSIKITINI KUMPINGA IMAMU

katika hali ambayo haikutarajiwa waumini wa Dini ya Kislamu wanaosari katika Msikiti wa Mji wa Zamani uliopo katika mtaa wa Mji Mwema Wilayani Mpanda wamepigana makonde ndani ya Msikiti kutokana na na pande mbili kupingana baini yao juu ya nani awe Imamu wa Msikiti huo.

Tukio hilo la aina yake liltokea hapo Februari 21 mwaka huu majira ya saa nane mchana mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti huo iliyokuwa ikiongozwa na Shehe Hussein Mkumba.

Hali ya hewa ndani ya msikiti huo ilibadirika mara baada ya swala hiyo ilipomalizika ambapo Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Ally Hussein ambae pia ndiye shehe mkuu wa wilaya ya Mpanda aliposimama na kuwaeleza waumini hao kuwa hatua inayofuata ni ya kumkabidhi hati ya Uimamu mpya wa msikiti huo Yassin Kasote.

Baada ya kuuli hiyo Shehe Ally Hussen alianza kusoma hati hiyo kitendo ambacho kiliwaudhi baadhi ya waumini hao ambao hawakubaliana kuongozwa na Imamu Yassin Kasote ambaye alichaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi uliofanyika Januari 29 baada ya kumshinda mgombea mwenzake wa nafasi hiyo Muajiri Mzee.

Wakati akiendelea kusoma hati hiyo kundi hilo linalompinga Kasote liliokuwa likiongozwa na Ally Kibauka Mawisa walikwenda kufunga milango ya misikiti huo na kutangaza kuwa hatoki mtu humo ndani Baada ya kufunga milango walimfuate Kasote wakimtaka awapatie hati ambayo alikuwa amekabidhiwa na viongozi wa Bakwata waliokuwa wameongozwa na Kaimu shehe wa Mkoa wa Katavi kitendo ambacho Kasote kakukubaliana nacho.

Shehe Kasote alipoona anataka kupolwa hati hiyo alianza kuwashambulia kwa makonde hali ambayo iliwafanya waumini wanao muunga mkono nao kuungana nae hali ambayo ilisababisha mapingano kuanza baina ya pande hizo mbili.

Hata hivyo wakati mapingano yakiwa yanaendelea baadhi ya waumini waliokuwa ndani ya msikiti huo wakiwemo askari polisi wa Dini hiyo waliweza kufanikiwa kufungua milango ya msikiti huo na kufanikiwa kumaliza vurugu hizo na kisha makundi hayo yote mawili walikwenda kituo cha polisi cha mpanda mjini kutoa taarifa kuhusiana na vurugu hizo.

Kwa upande Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Shehe Ally Hussen amewaomba waumini wa Dini hiyo ya Kislamu wawe na utulivu wakati wa kipindi hiki cha mgogoro huo.

Amesema kikubwa anachotaka waumini wa Dini hiyo ni kuhakikisha wanaendeleza amani katika msikiti huo sio kuleta machako ndani ya msikiti na nje ya msikiti.

Nae mmoja wa kundi linalompinga Imamu mpya alisema wao hawako tayari kuongozwa na Imanu Yassin Kassote kutokana na uchaguzi uliofanyika wa kumchagua ulikiuka taratibu za katiba yao.

Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limekiri kuwepo kwa vurugu kwenye ibada hiyo siku hiyo ya tukio katika msikiti huo wa Mji wa Zamani.

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUFUKUA KABURI

Mkazi wa kijiji cha Ikola Wilayaya Mpanda Mkoa wa Katavi Richard Clavery 34 amefikishwa Mahakamani katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda kujibu tuhuma za kufanya vitendo vya ushirikina wa kufukua kaburi la mwanamke aliyekufa Mtuhumiwa alifikishwa kizimbani hapo Februari 25 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakamaya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka Godfrey Luzabila.

Mwendesha mashitaka alidai Mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo hapo Februali 18 mwaka huu majira ya saa nne usiku nyumbani kwa Lenada Sakafu Mwendesha mashitaka Luzabila aliiambia mahakama kuwa siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alifika nyumbani kwa Lenada Sakafu na kufukua maiti ya mdogo wake na Lenada aitwaye Tabu Omera ambae alikuwa amefarii siku tatu kabla ya tukio hili.

Aliendelea kuieleza Mahakama siku hiyo Lenanda alikuwa nyumbani kwake pamoja na majirani na ndugu zake wakiendelea kuomboleza msiba ghafla alitokea mtoto wake aitwaye Brandina na kuwaeleza kuwa ameona mtu nje akifukua kaburi la marehemu ambae alikuwa amezikiwa kwenye eneo la nyumba yao.

Alieleza ndipo watu hao walipoamua kutoka nje na kumkuta mtuhumiwa Richard Clavery akifukua kaburi hilo huku akiwa amevua nguo zake zote ambazo alikuwa amezitundika kwenye msalaba wa kaburi hilo na walipomsemesha mtuhumiwa alijifanya kupandisha majini.

Mtuhumiwa baada ya kusomewa mashitaka alikana na Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga Ntengwa aliharisha kesi hiyo hadi hapo machi 6 na mtehumiwa alipelekwa lumande baada ya kushindwa kutimiza mashariti ya mdhamana ambapo alitakiwa adhaminiwe na mtu mmoja kwa dhamana ya shilingi milioni moja.

Chanzo: KATAVI YETU

WANAFUNZI WA KIKE WAPATWA NA UGONJWA WAKUANGUKA

WAZAZI na walezi ambao watoto wao wanasoma katika Shule ya Msingi Inyonga wilayani Mlele, mkoani Katavi wameitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutumatimu ya wataalamu wa afya kuchuguza ugonjwa wa ajabu unaowakumba wasichana wanaosoma katika shule hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, wazazi hao wameelezea kupata hofu ya afya ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, baada ya kukumbwa na ugonjwa huo wa ajabu ambao unasababisha waanguke wakiwa shuleni huku wakiweweseka na kupiga kelele.

"Tunaiomba Serikali iingilie kati ili kunusuru maisha ya watoto wetu hawa ambao sasa hawasomi tena, tunaomba watume wataalamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuja huku kufanya uchunguzi wa kitabibu ili kubaini ugonjwa huu," anasema mmoja wa wazazi hao, Isabela John.

Isabela alisema wasichana hao wanaosoma darasa la tatu hadi la saba wakiwa na umri wa miaka katiya 12 na 16, wamekuwa wakishambuliwa na ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi minne sasa.

"Ajabu ni kwamba watoto wetu hawa wanakumbwa na ugonjwa huu wa ajabu ambao hata wataalamu wa afya wilayani hapa wamekiri kuwa kila wanapowachunguza kitabibu watoto hawa hawaoni ugonjwa wowote. Isitoshe watoto hawa wakifika nyumbani, hawashambuliwi na ugonjwa huo isipokuwa pale wanapokuwa katika eneo hilo la shule," alisema mzazi mwingine, Patrick Ndolezi.

Wazazi wengine waliohojiwa na gazeti hili wamekiri kuwahamisha watoto wao wanaosoma katika shule hiyo wakihofia afya zao na wakiri kuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikiana kwamba shulehiyo imekumbwa na pepo wabaya.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, Mganga Mkuu wa Wilayaya Mlele, Dk Admihabesi Koni, alisema ugonjwa umewastaajabisha hata wataalamu wa afya wilayani humo kwani unawakumba wasichana tu wanaosoma katika shule hiyo wakati wanasoma pamoja na wenzao wa kiume."

Watoto hao wakikumbwa na ugonjwa huo hakika wanakuwa na nguvu ya ajabu, ni vigumu watu kuwathibiti kirahisi …Ugonjwa huu ulianza kwa wasichana wanaosoma darasa la tano, sita na saba lakini sasa umewakumba pia wanafunzi wa kike wanaosoma darasa la nne na la tatu.

"Lakini wanafunzi wa kike wanaosoma darasa la kwanza na la pili hawajakumbwa na ugonjwa huuna wamekuwa wakiendelea na masomo yao shuleni hapo kama kawaida," alisema.

Kwa mujibu wa Dk Koni, wanafunzi hao wanapokumbwa na ugonjwa huo wamekuwa wakifikishwa hospitalini kwa matibabu na kutibiwa kwa kudungwa sindano za 'valium' ambapo baadae wakizinduka hushikwa na butwaa na kuhoji walipo na kwa nini wamefikishwa hapo.

"Sisi wataalamu wa afya hatuamini kama ugonjwa huu unahusu imani za kishirikina, isipokuwa wanapofika hospitali kwa matibabu tunawakagua kitabibu na kuthibitisha kuwa hakuna dalili za ugonjwa wowote uliowakumba," alisema.

Aliongeza kuwa jitihada kadhaa zimeshafanyika ili kunusuru hali hiyo kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kuitwa kufanya ibada maalumu, lakini hali haijabadilika.

"Kulikuwa na uvumi uliozagaa kuwashule hiyo imekumbwa na mapepo wachafu na majini, hivyo waganga wa jadi walifika shuleni hapa na kufanya vitu vyao lakini wapi bila ya mafanikio yoyote yale," alisema Dk Koni.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mlele, Ephras Tenganamba alipozungumza na gazeti hili, amesema jitihada kadhaa zimefanyika bila mafanikio na hata baada ya kuwahamishia wanafunzi hao katika Shule ya Sekondari Inyonga jirani na shule hiyo, bado watoto hao waliendelea kuanguka huku wakipiga kelele.


Chanzo: Habari leo

OFISI ZA CHADEMA MPANDA ZAFUNGWA

MGOGORO wa uongozi ndani ya Chadema, umeingia katika hatua nyingine baada ya makada wa chama hicho wanaopingana kimisimamo, kufunga ofisi za chama hicho mjini Mpanda kwa zaidi ya wiki sasa.

Makada hao wamegawanyika na kuwa na kambi mbili tofauti, ambapo kila upande umeweka kufuli lake na walinzi wake, kuhakikisha hakuna atakayevunja na kuingia ofisini humo.

Ofisi za chama hicho ambazo ziko katika Mtaa wa Mji wa Zamani mjini hapa, kabla ya kufungwa zilikuwa zikitumiwa na viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya na mkoa pamoja na viongozi Jimbo la Mpanda Mjini ambalo kwa sasa Mbunge wake ni Said Arfi (Chadema).

Mvutano huu wa uongozi uliibuka mwanzoni mwa wiki iliyopita, ambapo viongozi wa chama hicho waliosimamishwa hivi karibuni, walifika ofisini hapo ili waendelee na shughuli zao za kiofisi na kukutaofisi zimefungwa kwa kufuli linginetofauti na waliloliweka wao.

Baada ya kubaini hivyo, viongozi hao wa Jimbo la Mpanda Mjini, walilazimika kuwahoji wenzao wa wilaya kulikoni ofisi za chama hicho kufungwa kwa kufuli lingine, tofauti na hilo, ndipo walipojibiwa kuwa wao si viongozi tena, kwa kuwa tayari wamesimamishwa uongozi.

Pia, uongozi wa wilaya wa chama hicho, wanadaiwa kuwajibu wenzao hao kuwa kwa kuwa wamesimamishwa uongozi, hawana mamlaka tena ya kufanya shughuli zozote za chama ndani ya ofisi hizo.

Hivi karibuni kikao cha maridhianoya chama hicho kilichofanyika kwenye ofisi cha chama hicho zilizopo katika mtaa wa Mji wa Zamani mjini hapa, kiliwasimamisha uongozi baadhi yaviongozi waandamizi wa chama hicho mkoani hapa na wengine wawili kusimamishwa uanachama.

Kikao hicho kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda Magharibi, Masanja Katabi, kiliwasimamisha uongozi Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Katavi, John Malack, Katibu Mwenezi wa chama hicho mkoani hapa, John Matongo na Mwenyekitiwa Jimbo la Mpanda Mjini, Seif Sipia.

Wengine ni Katibu Mwenezi wa Jimbo la Mpanda Mjini Joseph Mona, ambaye pia ndiye Katibu wa Mbunge, Arfi na Katibu Mwenezi wa Jimbo la Mpanda Mjini, Godfrey Kapufi.

Mbali ya kusimamishwa uongozi, kikao hicho kimependekeza Kapufi na Diwani wa Kata ya Makanyagio, Idd Nziguye wavuliwe uanachama, kama ilivyokuwa kwa akina Dk Mkumbo na Mwigamba.

Pia, kikao hicho pia kiliazimia Arfi achunguzwe, wakimtuhumu kudhamini mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Maridadi mjini hapa, unaodaiwa kutumika kuwakashifu Lema na Mnyika.

ACT YASHUSHA BENDERA ZA CHADEMA

Chama cha Alliance For Change and Transparency Mkoa wa Kigoma, kimeshusha Bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tawi la Ujiji stendi ya zamani na kupandisha bendera ya (ACT) wakati wa uzinduzi rasmi wa matawi sita katika manispaa ya kigoma ujiji.

Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Katibu wa ACT Mkoa Athuman Kabogo alidai lengo la kushusha bendera hiyo ni hatua ya kukataa kugeuzwa kuwa vibaraka wa watu wengine kwa kukosa haki ya kuhoji na kuwania nyadhifa za chama hicho nahivyo kuanzisha ACT kama chama cha wanyonge kinachoweza kuwasikiliza na kutoa haki kwa kila mmoja Kabogo aliwataka wanachama wahitaji, wachukue kadi za ACTili chama kipate usajili kamili kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu husika pamoja na kutoa michango endelevu,ikiwa ni jitihada za makusudi kuhakikisha chama kinasonga mbelekwa maslahi ya Taifa.

"Wananchi nyie ni chachu ya chama kuwepo kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kukiamini na kukipatia ridhaa kiweze kuletamabadiliko ya kimaendeleo" alisema Juma Ramadhan aliyekuwa katibu kampeni wa CUF kigoma.

Kwa upande wa Katibu ACT Kanda Magharibi Wiston Moga alisema, lengo la chama ni kuleta mabadiliko kwenye ulingo wa siasa, ambapo wao wamedhamiria kutetea maslahi ya umma kwa lengo la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambayo ni chachu ya vyama vya siasa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.

Katika ziara hiyo ya uzinduzi wa matawi ya chama husika, ACT kimefanikiwa kufungua matawi kwenye kata sita kati ya kata 19 zilizopo katika manispaa ya kigoma ujiji, huku baadhi ya viongozi kutoka UPD, CHADEMA na CUF wakijiunga na chama hichokwa kudai wanahitaji chama chenye uchungu na kukabilianana changamoto za wanyonge.

Hata hivyo wanachama 3500 wa chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema katika tawi la Ujiji mkoani Kigoma wamehamia chama kipya cha Alliance For Change and Transparency (ACT).

Chanzo:Kigoma Yetu

SAMUEL ETO'O ANA UMRI WA MIAKA 39

KOCHA, Claude Le Roy, amesema alizungumza na Samuel Eto'o kwenye simu na kwamba alikasirikasana kwa kitendo cha umri wake kuhojiwa.

Kocha wa sasa anayemnoa straika huyo wa Cameroon kwenye klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, kwenye mazungumzo yake ya kawaida tu natajiri mtengeneza saa wa Uswisi ambayo yalinaswa kwa siri na kurekodiwa, alisema hafahamu umri halisi wa Eto'o kama ni miaka 32 kama ilivyo kwenye pasipoti yake ya kusafiria au ni miaka 35.

Kabla ya kufikia kwenye kuhoji umri wa Eto'o, Mreno Mourinho alikuwa akijadili uwezo wa mastraika wake kwenye klabu ya Chelsea na mustakabali wa kunyakua ubingwa msimu huu.

Mourinho alilalamika kwamba washambuliaji wake wote wanamwangusha kutokana na kushindwa kufunga mabao. Washambuliaji waliopo kweye kikosi cha Chelsea wote ni makini; Demba Ba, Fernando Torres na Eto'o, lakini wote hao wamekuwa butu na kushindwa kufunga mabao.

"Tatizo la Chelsea hakuna wafungaji," alisema Mourinho. "Ninaye Eto'o, lakini umri wake ni miaka 32, pengine inaweza kuwa 35, huwezi kujua," alisema Mourinho.

Kocha, Le Roy, aliyewahi kumnoa Eto'o kwenye kikosi cha Cameroon, anasema straika huyo hakupendezwa na kauli ya Mourinho kumsema kwamba umri wake ni mkubwa kuliko unaotambulika rasmi.Eto'o amesisitiza kwamba umri wake ni miaka 32. Jumatano iliyopita, Chelsea ilikuwa na mechi muhimu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray na kwamba iliaminika kwamba baada ya mchezo huo, Mourinho na Eto'o watahitaji kuwekana sawa.

Lakini, wakati Eto'o akisisitiza kwamba umri wake ni miaka 32, kama ulivyoandikwa kwenye pasipoti yake, mke wa zamani wa staa huyo ameibuka na kuchafua zaidi hali ya hewa baada ya kueleza kwamba umri wa supastaa huyo wa zamani wa Barcelona ni mkubwa kuliko hata uliotajwa na Mourinho.


*MKEWE AFICHUA

Mrembo, Anna Barranca, ambaye alizaa na Eto'o mtoto mmoja, amefichua wazi na kusema umri wastaa huyo ni miaka 39.

Mourinho alihisi Eto'o anaweza kuwa na umri wa miaka 35, lakini mwanamke huyo wa Kitaliano ametoa kali baada ya kudai kwamba Eto'o amepunguza miaka saba ya umri wake wa kweli.

Anna anasema: "Nadhani Samuel umri wake si miaka 35 ni zaidi ya 39. Samuel alizaliwa 1974 na sasa ana umri wa miaka 39."

Anna umri wake wa sasa ni miaka 43, mtoto aliyezaa na Eto'o anaitwa Annie.

Baada ya mjadala wa umri wa Eto'o kushika kasi, gazeti la The Sun lilimtafuta aliyekuwa mke wa staa huyo na kufanya mahojiano naye ilikufahamu ukweli halisi, ndipo mwanamke huyo alipasua kwamba Mcamerooni huyo ana umri wa miaka 39.

Anna na Eto'o walimzaa Annie wakati mchezaji huyo alipokuwa akiichezea Mallorca. Kuna wakati fulani, mwanamke huyo aliwahi kumlalamikia mchezaji huyo kutokana na kushindwa kutoa huduma kwa ajili ya malezi ya mtoto.


*TABIA YA ANNA

Mwanamke huyo anayefanya kazi saluni, anadaiwa kuwahi kuuza habari zake kwenye gazeti akimtuhumu Eto'o kwamba hana anachokifanya kwa mtoto wake na kwamba haishi kwa kutegemea pesa za mwanasoka huyo.

Mrembo huyo alisema Eto'o amekuwa akishindwa kutimiza wajibu wake wa kumlea mtoto wao,kabla ya sasa kuibuka na kusisitiza kwamba umri wa mchezaji huyo si miaka 32 na kwamba umri wake ni zaidi ya miaka 39.


*ETO'O ANG'AKA

Kwenye hali ya kuonekana kuwa na hasira, Eto'o alijifanya kupuuza kauli ya Mourinho kudai kwamba staa huyo ana umri mkubwa baada ya kusisitiza kwamba ataendelea kufunga mabao hata kama atafikisha umri wa miaka 50.Staa huyo kwa kejeli alisema aliweza kuifunga 'hat-trick' Manchester United licha ya kuwa na umri huo mkubwa, hivyo suala la kufunga mabao kwake ni jambo la kawaida.

"Mimi ni Samuel Eto'o, nitasemaje sasa?" Alisema alipozungumza na Sky Sports News baada ya mechi dhidi ya Galatasaray.

"Kama kwenye umri wa miaka 36 na 37 naweza kuifunga mabao matatu Manchester United kwenye mechi moja, hiyo ina maana kwamba naweza kuendelea kutikisanyavu hadi nitakapokuwa na umri wa miaka 50. Mimi sijali kitu, kitu muhimu kwangu ni kujitolea kwa nguvu zote katika kuisaidia timu yangu ili kutwaa mataji."

Kwenye mchezo dhidi ya Galatasaray, Eto'o aliingizwa katika dakika 68, kuchukua nafasi ya Torres ambaye alifunga bao kwenye sare ya bao 1-1 katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika Istanbul, Uturuki, Jumatano iliyopita.


Chanzo:Mwanaspoti

DK. MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI

Kampuni ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijiniDar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu.

Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki.

Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Saddik ambaye aliambatana na Waziri Magufuli katika ziara hiyo, amewataka wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya sehemu ambayo mkandarasi anaendelea na kazi waondoke kwani hiyo mbali ya kuwa kinyime na taratibu za uendeshaji biashara zilizowekwa lakini pia imekuwa ni moja ya kisingizio kinachotolewa kwamba uendeshaji wa shughuli hizo unachangia kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.

Waziri Magufuli akizungumza wakati wa kuhutimisha ziara hiyo, amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha mradi huo kwa muda na viwango vilivyokusudiwa.

"Na kwa wale walio ndani ya eneo la ujenzi ni lazima sheria ichukue mkondo wake" alisisitiza Waziri Magufuli huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni Mhandisi Mussa Natty kuhakikisha anasimamia zoezi hilo la kuondoa haraka wale wote wote walioingia katika eneo hilo la barabara kinyume na sheria.

Aidha, Waziri Magufuli alielezea kushangazwa kwake kwa kuchelewa kuondolewa kwa nyaya za Tanesco katika maeneo ya City Squire na Morocco kwani fedha za kutekeleza kazi hiyo tayari zimelipwa muda kirefu.

"Ucheleweshaji wa ainaa hii ndiyo unaotoa mwanya kwa mkandarasi kuanza kutoa visingizio vya kutokamilika kazihii kwa wakati" ametahadharisha Mhe. Magufuli.

Hata hivyo katika hatua nyingine Mhe. Magufuli amemtaka mkandarasi kuharakisha taratibu za kuifungua barabara hiyo upande wa kuingia Dar es Salaam ambako kwa sasa hivi hakuna shughuli kubwa zinazofanyika ili kupungiuza adha ya msongamano wa magari yanayopishana katika njia moja ya upande wa kutokea mjini katika barabara hiyo ya Morogoro hasa kwa eneo kati ya Ubungo na Kiamara.

Naye Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari ameelezea kuwa, utekelezaji wa mradi huu wa usafiri wa haraka utajengwa katika awamu sita.

Awamu ya kwanza ambayo ujenzi wake ndio huu unaoendelea inahusisha barabara zenye jumla ya kilometa 20.9 ambazo ni Kimara – Kivukoni, Magomeni –Morocco na Faya – Karikaoo. Hadi sasa mkandarasi amekwisha kamilisha asilimia 55 ya mradi wote.

MTU MMOJA AFARIKI, 38 WAJERUHIWA

Mtu moja amefariki duni na wengine 38 wamejeruhiwa baada ya basi la Bunda kugonga kichwa cha treni katika makutano ya reli na barabara wilayani Manyoni.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Bunda lenye usajili wa namba T 782 BKZ lililokuwa likitokea mkoani Dodoma na kuelekea mkoani Mwanza, mkuu wa wilaya ya Manyoni bi Fatuma Toufiq amesama ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi saa mbili tarehe 28 katika makutano ya barabara na reli mjini Manyoni.

Akiongea na ITV na Radio one muuguzi mkuu wa haspitali ya wilaya ya Manyoni Bi. Heliechi Malisa amesema wamepokea maiti moja ambayo imetambulika kwa jina la Perina Bikombo mkazi wa Manyoni na majeruhi thelasini na nane wamelazwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.


Chanzo:ITV

SERIKALI YANUNUA AK-47 500

Siku moja baada ya Tanzania kutajwa na Shirika la Polisila Kimataifa (Interpol) kuwa kinara wa biashara ya meno ya tembo Afrika Mashariki, Serikali imelipia kodi na kukabidhiwa bunduki 500 aina ya AK47 ili kukabiliana na ujangili katika hifadhi na mapori ya akiba nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa silaha hizo zilizokuwa chini ya Mamlaka yaMapato Tanzania (TRA), tangu Novemba 2012 kutokana na kutokulipiwa kodi, zitasambazwa Ngorongoro, Selous, pamoja na Hifadhi za Taifa za Tanapa.

Kati ya silaha hizo, 250 zitapelekwa Idara ya Wanyamapori, 200 Tanapa na 50 Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.

"Silaha hizi jumla ya Sh427 milioni kuzinunua lakini zilikwama TRA kwasababu ya kutolipiwa kodi na ushuru mbalimbali, hivyo wizara yangu leo inatoa Sh212 milioni kwaajili ya malipo hayo," alisema Waziri Nyalandu.

Alisema silaha hizo zimekombolewa ikiwa sehemu ya kutekeleza maazimio ya Bunge na ahadi ya Serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira.

Akizungumzia sababu za kuchelewa TRA, Nyalandu alisema kulikuwa na ubishi wa ama zilipaswa kulipiwa kodi au la, lakini mamlaka hiyo ilifafanua kuwa hayo ndiyo matakwa ya sheria, hivyo akaamua kutoa fedha hizo.

Alipoulizwa ni jinsi gani Serikali itadhibiti silaha hizo, Nyalandu alisema wizara yake inaandaa miikoya matumizi yake ikiwamo kufuatilia makabidhiano yake na askari wanaokabidhiwa.

"Kumbuka hizi si silaha za kwanza kuwa nazo, tunazo nyingine za AK47 na hizo zimetuwezesha kukamata silaha haramu zaidi ya 2,000 zinazotumiwa na majangili," alisema.

Silaha hizo zimepatikana ikiwa ni takriban wiki mbili tangu Rais Jakaya Kikwete abanwe na vyombo vya habari vya kimataifa akitakiwa kueleza mikakati iliyopo kupambana na ujangili ambao umeharibu sura ya Tanzania nje ya nchi.

Itakumbukwa kuwa miezi miwili iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kupangua Baraza la Mawaziri na kuwatimua mawaziri wanne kutokana na vitendo vya kinyama vilivyobainishwa na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili.


*MAJANGILI PAPA 40

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Waziri Nyalandu alisema majina ya majangili papa 40 ambayo Rais Kikwete alisema anayo, 'yatabandikwa' hivi karibuni.

"Serikali ina mkono mrefu sana, hatupendi mtu aache mke na watoto wake afungwe miaka 50. Kama ni majina tutayabandika, nimeshakubali, tutayabandika, ni kwamba tu sina hiyo orodha hapa," alisema.

Alisema, Serikali inawafahamu majangili hao kwa undani, wanapokunywa chai, wanapotembelea na shughuli zao za kila siku.

Alisema majina yao si siri kwani tayari wameshafunguliwa mashtakana wapo chini ya mfumo wa Mahakama na wamekamatwa na vidhibiti.

Hivi karibuni, Rais Kikwete alihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), alisema Serikali ina majina 40 ya majangili papa na mkuu wao yuko Arusha.


*SELOUS YAIMARISHWA

Katika hatua nyingine, Nyalandu alitangaza kuzipandisha hadhi kanda nane zilizopo katika Pori la Akiba la Selous ili ziweze kujitegemea kiutendaji kwa kuwekamkuu wa kila kanda.

Alisema pori hilo lina ukubwa unaokaribia hifadhi zote za Taifa chini ya Tanapa, jambo linalolifanyakuwa kubwa kimenejimenti na kiuendeshaji.

Pori la Selous lina kilomita za mraba 55,000 wakati mapori yote nchini kwa ukubwa wake ni kilomitaza mraba 57,000.

Katika kuweka mazingira ya uangalizi wa kina ya kupambana na ujangili aliiagiza Idara ya Wanyamapori kukamilisha mchakato wa kufungua akaunti maalumu za benki kwa kila kanda ili kuwawezesha wakuu wa kanda kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Chanzo:Mwananchi

WAJUMBE ODM WAZUA VURUGU

Vurugu zimezuka katika uchaguzi wa kuwachagua maafisa wapya wachama kikuu cha upinzani cha ODM nchini Kenya, chake aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo Raila Odinga.

Polisi waliwasili katika ukumbi wauwanja wa michezo wa kimataifa wa Kasarani viungani mwa jiji la Nairobi kurejesha utulivu baada ya baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliodaiwa kuwa walinda usalama kurusha viti pamoja na masanduku ya kupigia kura wakijaribu kuvuruga uchaguzi huo.

Ugomvi ulizuka baada ya kuzuka madai kuwa kulikuwa na orodha ya wajumbe bandia iliyokuwa ikisambazwa pamoja na makaratasi bandia ya kupigia kura. Mbunge maalum Isaac Mwaura ambaye anaishi na ulemavu wa ngozi-Albino-alionekana akisukwasukwa na wajumbe baada ya kuzua zahama kuhusu madai hayo ya udanganyifu katika zoezi hilo la upigaji kura.

Chama cha ODM ndicho chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Kenya kikiwa na idadi kubwa ya wabunge katika bunge la kitaifa pamoja na Senate. Chama hicho kimemudu mgao mkubwa zaidi wa pesa za kufadhili shughuli za vyama vya kisiasa kutoka kwa serikali ya Kenya.

Kutokana na raslimali za chama hicho uchaguzi wa leo umeonekana kuzua msisimko mkali pamoja na patashika baina ya wanasiasa mashuhuru ambao wanagombania vyeo mbali mbali.

Bwana Odinga ambaye alishindwana rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliokumbwa na madai ya udanganyifu mwezi Machi mwaka uliopita anatetea kiti chake kama kiongozi wa chama, dalili kwamba huenda akagombea tena kiti cha urais mwaka 2017.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura Bwana Odinga alizungumzia maswala mbali mbali yanayohusiana na usalama nchini Kenya pamoja na kuiponda serikali ya mpinzani wake Rais Uhuru Kenyatta kwa kushindwa kuleta suluhu ya matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wakenya.

BENKI YA DUNIA YABANA MSAADA KWA UGANDA

Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuizinisha sheria mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayata athirika.

Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda.

Wahisani kama Denmarkna Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.

Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.

Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.

Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.

Hadi kufikia sasa Waziri wa FedhaWa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yoyote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.

Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda.

Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.

TFF YAVUNJA MKATABA NA KIM POULSEN

Hatimaye Shirikisho la Kabumbu nchini Tanzania TFF limetangaza kuvunja mkataba wake na Kocha mkuu wa Timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen kwa kile kilichoelezwa maafikiano ya pamoja baina ya kocha huyo, TFF, na Serikali.

Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa Shirikisho la soka Tanzania amesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida hasa baada ya wadau mbali mbali kuona kuwa huu ni wakati wa kufanya mabadiliko ya lazima katika benchi la ufundi la Taifa Stars ambayo inajiandaa kwa mechi za kufuzu kwa Fainali za kombe la mataifa Afrika hapo mwakani zitakazofanyika nchini Morocco.

Kuhusu gharama za kuvunja mkataba na Kocha huyo Bwana Malinzi amesema serikali haitagharamia uvunjaji huo wa mkataba na kocha huyo na badala yake wapo wadau waliojitokeza kugharamia kutokana na kuona umuhimu wa kufanya mabadiliko katika kipindi hiki kwa faida ya soka la Tanzania.

Kwa Upande wake Kocha Kim Poulsen amesema na rekodi yake inaonyesha kuimarika kwa soka la Tanzania katika kipindi cha takriban miaka miwili aliyokuwa akikinoa kikosi cha Taifa Stars lakini kusitishwa mkataba ni jambo la kawaida kwa kocha yeyote baada ya kipindi fulani kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na ndiyo sehemu ya maisha.

"Kama kocha unapoona ndiyo umefanya kazi yako, unapaswa kuangalia mbele zaidi baada ya kufanya kazi yako si lazima uendelee kuwa hapo, mnakaa na kujadiliana na kuachana kwa amani kisha unapaswa kusonga mbele, ninaondoka nikiwa najivunia kipindi nilichofundisha soka hapa, na ninawatakia kila la kheri Tanzania na Taifa Stars kwa ujumla."alisema Poulsen.

Kuhusu Kocha mpya wa Taifa Stars Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa TFF amesema hadi sasa wapo makocha watatu raia wa Uholanzi ni wawili na Mjerumani mmoja wanaosailiwa kwa ajili ya kumrithi Kim Poulsen,lakini mojaya vigezo Malinzi amesema kuwa ni lazima kocha huyo awe amewahi kuipeleka kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika moja ya nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara.

Katika hatua nyingine kocha Salum Madadi ameteuliwa kukaimu nafasi iliyoachwa wazi na Kim Poulsen ambapo kocha huyo akisaidiwa na Hafidh Badru kutoka Zanzibar watasimamia Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyoko kwenye kalenda ya FIFA baadaye mwezi ujao.

MADRID YAIFUMUA SCHALKE 04, CHELSEA YABANWA MBAVU

Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo Gareth Bale na Karim Benzima walifungamabao mawili kila mmoja na kuisaidia Real Madrid ya uhispania kufuzu kwenye robo fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea Schalke 04 ya Ujerumani mabao 6-1 katika mkondo wa kwanza uliosakatwa huko Ujerumani.

Benzima ndiye aliyefungua kivuno hicho cha mabao baada yanipe nikupe kunako dakika ya 13.

Mchezaji aliyeigharimu Madrid kitita kikubwa zaidi msimu huu Gareth Bale akafanya mambo kuwa mawili kwa nunge dakika saba baadaye.

Kuanzia hapo kampeini ya vigogo hao wa ligi ya uhispania kunyanyua taji lao la kumi barani Uropa ilikuwa mbioni kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

Ronaldo alimpangua Joel Matip kwa miondoko ya aina yake na kufunga la tatu akimwacha kipa wa Schalke Fahrmann asijue azibe wapi azue wapi.

Masaibu ya wenyeji hao yaliongezeka Karim Benzema alipofuma bao la nne.

Bale akaongezea bao la tano kisha nyota wa Ureno Ronaldo akafunga kiziba mkonga na kudidimiza kabisa mtumaini ya timu ya tatu ya Ujerumani baada ya mabingwa Bayern Munich na washindi wa pili Borussia Dortmund kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya mchuano huo msimu huu.

Uchungu uliwazidi mashabiki wa nyumbani na wachache waliosalia uwanjani walishuhudia bao la kukata na shoka la nyota wao Klaas-Jan Huntelaar.

Huntelaar aliyeichezea Madrid (2009) kwa mkopo alifuma mkwaju wa kipekee uliomwacha Iker Casillas ameduwaa.

Hata hivyo bao hilo la kufutia machozi la dakika ya mwisho ya mechi haitakuwa na faida mbali na kunusuru hadhi ya kocha Jens Keller Schalke itakapozuru bernabou baada ya majuma mawili kwa mkondo wa pili.

Katika mechi nyengine iliyosakatwa usiku wa jana huko Instabul, Uturuki ,matumaini ya pekee ya timu ya Uingereza kusonga mbele katika hatua ya robo fainali yalitegemea matokeo baina ya wenyeji Galatasaray na Chelsea

Matokeo ya mkondo wa Kwanza

*.Barcelona 2-0 Man City

*.Paris St-Germain 4-0 Bayer Leverkusen

*.Atletico Madrid 1-0 AC Milan

*.Bayern Munich 2-0 Arsenal

*.Manchester United 0-2 Olympiakos

*.Borussia Dortmund 4-2 Zenit St Petersburg

*.Chelsea 1-1 Galatasaray

*.Real Madrid 6-1 Schalke


Kwa kila hali na mizani mechi hii ilitarajiwa kuwa ngumu kwa Galatasaray chini ya kocha wa zamani wa Manchester city Roberto Mancini ikiongozwa na aliyekuwa mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba na Emmanuel Ebuoe zamani akiichezea Arsenal ilikuwa inakabiliana na The Blues chini ya Kocha Jose Mourinho.

Uwanjani mashabiki wa nyumbani walinyamazishwa na bao la dakika ya 9 ya kipindi cha kwanza iliyofungwa na Fernando Torres.

Roberto Mancini alilazimika kufanya badiliko la mapema ilikuzia kuabishwa na wimbi la mashabulizi ya vijana wa Mourinho.

Katika kipindi cha pili juhudi za Galatasaray kujinasua zilizaa matunda Aurelien Chedjou alifunga bao la kusawazisha baadaya kutumia vyema mpira wa kona uliomchanganya Peter Cech.

Bao hilo ndilo litakaloamua mshindi baina ya timu hizo mbili zitakapokutana katika mechi ya mkondo wa pili tarehe 18 mwezi Machi huko Stamford Bridge.

MAREKANI YAIPIGA MKWARA URUSI

Marekani imeionya serikali ya Moscow isithubutu kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Ukraine.

Hatua hii inawadia siku moja tu baada ya Urusi kuamuru kufanyika kwa mazoezi ya kijeshi yanayoshirikisha askari wapiganaji laki moja na nusu kwenye mpaka wake na Ukraine.

Kujitokeza kwa wanajeshi wa Urusi kwenye mpaka na Ukraine kumeimarisha uhasama ulioko kati ya Urusi na mataifa ya Magharibi.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema kuwa Urusi inapaswa kukubali ushauri ya kwamba mataifa ya kigeni yasiingile mambo ya ndaniya Ukraine.

Alisema kuwa kujiingiza kijeshi katika hali ilivyo nchini Ukraine kwa hivi sasa ni kosa kubwa.

Mawaziri wa ulinzi kutoka mataifaya muungano wa NATO wametoa taarifa ambapo wamesema kuwa wanachama wake wataendelea kuunga mkono uhuru na hadhi yataifa la Ukraine.

Serikali ya Marekani imesema kuwa imetenga mbinu mbalimbali inazotazamia kutumia kuimarisha Ukraine kiuchumi, huku kukiendelea kuwa na hofu kuwa huenda taifa hilo likashindwa kuendelea kulipamadeni yake.Kwa wakati huu msaada wa kijeshi pekee kwa Ukraine hautoshi kwani taifa linalotaka kusaidia lazima kwanza liimarishehali ya kukubaliwa kwake katika taifa hili ambalo limegawanyika kwa imani yake kati ya Urusi na mataifa ya Magharibi.

Wabunge kadhaa wa Marekani wameonya kuwa Jumuiya ya Ulaya na Marekani wasipotoa msaada wa pesa taslimu Urusi huenda ikafanya hivyo.

KENYA KUPELEKA MAJESHI SUDAN KUSINI

Kamati Kuu ya Usalama Nchini Kenya imependekeza kwa bunge liidhinishe nyongeza ya idadi ya wanajeshi wake wa kudumisha amani walioko nchini Sudan Kusini, chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa, kwa majeshi 310.

Kamati hiyo chini ya uenyekiti waRais Uhuru Kenyatta imesema imechukua hatua hiyo kufuatia ombi la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililofanywa Desemba 24, mwaka jana.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa ikulu ya Nairobi usiku wa kuamkia leo, kamati hiyo ambayo imekutana kwa mara ya kwanza tangu Rais UhuruKenyatta kuanza utawala wake mwaka mmoja uliopita ilisema kuwa Kenya itawatoa wanajeshi wengine ili kufanya idadi ya wanajeshi wake walioko Sudan Kusini kufikia 1,000.

Taarifa hiyo ilieleza wazi kuwa wanajeshi wa Kenya wanaingia huko chini ya Umoja wa Kimataifa na wala sio kama taifa huru.

Itakumbukwa kuwa mara tu baada ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kuanza kati ya jeshila Sudan Kusini linalomuunga mkono Rais Salva Kiir na wanajeshi waasi wanaomuunga mkono makamu wa rais wa zamani Daktari Riek Machar, Uganda iliwatuma wanajeshi nchini humo kuunga mkono Rais Salva Kiir.

Katika taarifa hiyo kamati ya usalama nchini Kenya ilisema kuwa hali ya usalama nchini Sudan Kusini imeathiri Kenya.

Wakimbizi wengi wametorokea Kenya, taifa ambalo kwa hivi sasalinakabiliwa na matatizo yake mengi ya kiuslama kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wa Somalia.

Miongoni mwa matatizo ya kiusalama yaliyotajwa katika taarifa hiyo ni mapigano kati ya makabila mbalimbali nchini Kenya na pia hatari ya mashambulizi ya kigaidi katika uwanja wake wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Mkutano huo wa usalama ulioongozwa na Rais Uhuru Kenyatta ulisema usalama katika uwanja huo utaimarishwa kwa kuimarisha mitambo ya kuwapekua wasafiri wa kimataifa.

Nairobi ni kitovu kikubwa cha usafiri kwa watalii na wafanyabiashara katika eneo zima la ukanda wa mashariki na upembe wa Afrika.

Rais Uhuru Kenyatta hii leo atasafiri hadi mji Mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kama hatua mojawapo ya viongozi wa eneo la Afrika Mashariki la kutafuta suluhu la mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.


*OBAMA KUONDOA MAJESHI AFGHANISTAN

Rais Obama ameagiza makao makuu ya ulinzi nchini Marekani Pentagon kuandaa mipango ya kuwaondoa wanajeshi wake wote kutoka Afghanistan ifikapo mwisho wa mwaka huu iwapo hakutakuwepo maafikiano rasmi na Serikali ya Afghanistan.

Rais Obama alimpigia simu Rais Karzai wa Afghansitan juu ya mipango hiyo yake.

Rais Karzai amewaudhi Marekani kwa kukataa kata kata kutia sahihi muafaka ambao ungeruhusu baadhi ya wanajeshi kuendelea kukaa Afghanistan baada ya mud auliokubaliwa awali wa mwisho wamwaka huu wa 2014.

Mpango huo ambao tayari ulikuwa umekubaliwa na baadhi ya viongozi wa kikabila wa Afghanistan - unaandaa wajibu wawanajeshi wa NATO unaoshirikisha kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afghanistan na kusaidia Serikali ya taifa hilo kukabiliana na wapiganaji wa Kitaliban.

Mkataba huo pia unawapa kinga ya kisheria wanajeshi wa Marekani walioko nchini Afghanistan.

Ikulu ya White House inasema kuwa hakuna uwezekano wa Karzai kutia sahihi mapatano hayo kabla ya kuondoka mamlakani Aprili mwaka huu.

DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI

Hospitali ya taifa Muhimbili imemkamata daktari feki hospitalini hapo asubuhi ya tarehe ishirini na tano akiwa na baadhi ya kadi za wagonjwa na vipimo huku historia yake ikionesha aliwahi kuajiriwa na serikali kama utabibu katika hispitali ya amana na Mwananyamala kabla ya kuacha kazi mwaka 1997.

Akitoa taarifa za kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo afisa uhusiano mwandamizi wa hospitali hiyo Bw. Aminieli Aligaesha amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Kitano Kitani mwenye umri wa miaka 52 ambaye alijifanya daktari upande wa wazazi alikamatwa bada ya kujaribu kuwatapeli watu mbalimbali hospitalini hapo na amekuwa akionekana mara kwa mara na wagonjwa wengi walidhani kuwa yeye ni daktari halali.

Mtuhumiwa huyo licha ya kukiri kufanya kazi ya utabibu kwa miaka mingi amekana kuhusika na tukio lolote la utapeli hospitalini hapo na kubaini amekuwa akifika hospitalini hapo kwa mambo yake binafsi na kukiri kuendelea kutoa huduma mtaani mara baada ya kuacha kazi ya utabibu.

Raisi wa chama cha madaktari Tanzania daktari Primas Saidia amekiri ongezeko la madaktari feki kwenye hospitali mbalimbali nchini na kushindwa kuthibitisha moja kwa moja kama wanashirikiana na madaktari halali kwenye hospitali husika na kuwa tayri wamejipanga kupambana na matukio hayo kwa kuwapa madaktari mihuri na makoti maalimu yenye nembo ili kuwafanya wagonjwa kutambua nani daktari halali ama la.

BOKO HARAM WAUWA WANAFUNZI

Wanamgambo wa Kiislam wa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria wametuhumiwa kushambulia shule moja na kuwaua wanafunzi kadhaa.

Polisi nchini Nigeria wameliambia Shirika la Habari la Uingereza, Reuters kwamba wotewaliouawa ni wavulana na kwamba baadhi ya miili ya wanafunzi hao imeungua na kubaki majivu.

Taarifa ya jeshi la Nigeria imesema shambulio hilo limefanyika katika jimbo la Yobe.

Wakaazi wa mji wa Buni Yadi katika jimbo hilo, wamesema washambuliaji hao walivamia usiku na kuwachinja baadhi ya wanafunzi.Wamesema baadhi waliuawa kwa kupigwa risasi.

Walimu katika chuo cha serikali ya shirikisho katika mji wa Buni Yadi wameliambia shirika la habari la AP kwamba wanafunzi wapatao 40 waliuawa katika shambulio hilo ambalo lilianza mapema Jumanne asubuhi.

Jeshi limethibitisha kwamba shambulio hilo limetokea katika hosteli za wanafunzi lakini limesema haliwezi kutoa taarifa zaidi kwa sasa.

Kundi la Boko Haram limekuwa likishutumiwa kuendesha vitendovya mauaji kaskazini mwa Nigeria, yakiwemo mauaji ya mapema mwezi huu katika jimbola Yobe.

Boko Haram, lina maana ya"Elimu ya Magharibi ni dhambi" katika lugha ya Kihausa, mara kwa mara limekuwa likishambulia shule katika siku za nyuma.

Watu kadhaa wameuawa katika mashambulio mawili yaliyotokea wiki iliyopita.

Katika tukio moja, wanamgambo hao wa Boko Haram, waliteketeza kijiji kizima na kuwapiga risasi wakaazi wa eneo hilo waliokuwa wakijaribu kutoroka.

MOURINHO ALALAMA KUREKODIWA KWA SIRI

Kocha wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameshutumu tabia ya kurekodi kwa siri mazungumzo yake kuhusu wachezaji wa timu hiyo.

Mourinho amesema lilikuwa jambo la aibu kuona kwamba mazungumzo binafsi kuhusu wachezaji wa timu yake, yanawekwa hadharani na kampuni moja ya televisheni nchini Ufaransa.

Mourinho amesema alikuwa anatania alipokuwa akilalamika kuwa Chelsea inakosa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji na alimtania Eto'o kuhusu umri wake.

"The problem with Chelsea is we lack a scorer," the Portuguese said in footage captured by Canal Plus."I have one (Eto'o) but he's 32. Maybe 35, who knows?."

"Yalikuwa mazungumzo ya utani na mtu ambaye hahusiki na masuala ya ulimwengu wa soka," amesema Mourinho.

"Ni fedheha kwa mtu kurekodi mazungumzo binafsi."

MAREKANI KUANGALIA UHUSIANO WAKE NA UGANDA

Marekani haikufurahishwa na hatua ya Uganda kuidhinisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema tangu Uganda iidhinishe mswada huo miaka minne iliyopita, Marekani ilieleza wazi kwamba sheria hiyo inakiuka jukumu la kuhakikisha kuwepo haki za binaadamu ambalo tume ya haki za binaadamu Uganda inatambua linaambatana na sheria ya Uganda.

Kerry amesema,' Baada ya kuidhinishwa sheria hii, tunaanza ukaguzi wa ndani wa uhusiano wetu na serikali ya Uganda, kuhakikisha kwamba pande zote za uhusiano wetu, ukiwemo miradi ya msaada, zinapinga sera na sheria zinazowaonea watu na tuwe na uhusiano unaodhihirisha maadili yetu'.

Sheria mpya imezusha hisia kaliTamko hilo limetolewa siku moja baada ya rais Yoweri Museveni kukaidi shinikizo la kimataifa na kutia saini sheria hiyo iliyo zusha mzozo, inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja Uganda, hatua iliyozushahisia kali.

Baadhi ya mataifa ya magharibi tayari yanatishia kukatiza msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Uganda.

Marekani inasema kuidhinishwa kwa sheria hiyo kunatishia hatari ya kurudi nyuma katika uwajibikaji wa Uganda kulinda haki za raia wake nakutishia jamii ya wapenzi wa jinsia moja Uganda.

Hivi kwani ni lazima mtu kufanya kile ambacho wew hufanya, nazani ni muda muafaka kwa viongozi wa afrika kuangalia mara mbili mahusiano yao na nchi za magharibi, pongezi kwa Museveni unastaili kuigwa