KAGAME ANAMTANDAO WAKE NCHINI

JEURI ya wazi inayoonekana kuwemo ndani ya taarifa ambazo zimekuwa zikichapishwa mara kwa mara na vyombo vya habari vya serikali ya Rais Paul Kagame wa Rwanda dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na serikali yake, inaelezwa kujengwa na ushirika wake wa kiintelijensia alioupandikiza ndani ya mfumo wa serikali na taasisi mbalimbali hapa nchini, MTANZANIA limedokezwa.

Taarifa zilizolifikia gazeti la MTANZANIA kutoka kwa watu waliokaribu na viongozi wa Rwanda na wale walioko kwenye taasisi mbalimbali za kiserikali hapa nchini, zinaeleza kuwa taarifa ambazo zimekuwa zikiripotiwa na vyombo vya habari vya serikali ya nchi hiyo, msingi wake unaweza kuwa mtandao ambao serikali ya Kagame imeujenga hapa nchini.

Kwamba Rwanda, mbali na kufanikiwa kupenyeza watu wake kwenye mifumo ya kitaasisi hapa nchini, pia imefanikiwa kujenga ushirika na watu wa kada mbalimbali wenye umaarufu, ushawishi na wanaoheshimika nchini, wakiwemo baadhi ya wasomi na wanasiasa.

Kuvuja kwa taarifa hizi, kumekuja wakati ambao gazeti la serikali ya Rwanda, Rwanda Times na mtandao wa News of Rwanda, yakiripoti taarifa zinazoigusa serikali ya Rais Kikwete, ikinukuu vyanzo vya kutoka hapa nchini, japo ukweli wa taarifa hizo ukiwa haujulikani, kutokana na Ikulu ya Dar-es-salaam kuzikanusha mara kwa mara.

Dhana hii inapewa nguvu na taarifa mpya kabisa zilizotufikia, ambazo zinadai kuwa katika kuendelea kuimarisha mtandao wake, Serikali ya Rwanda imechangisha fedha kwaajili ya baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini ili kulinda maslahi yake.

Taarifa hizo zinamtaja Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo, Profesa Silas Lwakabamba, ambae aliwahi kusoma na kuishi nchini kuwa ndiye aliye endesha harambee hiyo ambayo inadaiwa ilimshirikisha Rais Kagame.

Habari zaidi ambazo MTANZANIA imezipata zinadai kuwa katika harambee hiyo, iliyohudhuriwa na baadhi ya Mawaziri wa serikali ya Rwanda pamoja na wafanyabiashara wakubwa nchini humo, Rais Kagame kwa upande wake alichangia Dola 500,000.

Gazeti hili limedokezwa kuwa, lengo la harambee hiyo, ni kuhakikisha ushawishi wake unafanikiwa, hasa kwa watu ambao wamekuwa wakiiunga mkono Rwanda, hususani wakati huu mgumu ambao inakabiliwa na tuhuma za kuchochea mapigano katika eneo la Mashariki ya Congo, ambako Tanzania imepeleka wanajeshi wake.

Katika mkakati huo, walengwa ni vyama vya upinzani, kutokana na kuwa na uhusiano wa shaka na serikali iliyoko madarakani.

Tayari mara kadhaa vyombo vya habari Rwanda, hususani vile vya serikali, vimekuwa vikitumia kauli zinazotolewa na wapinzani hapa nchini, kama hoja ya utetezi wake dhidi ya uhusiano mbaya na Ikulu ya Dar-es-salaam.

Profesa Lwakabamba, ambaye anatajwa kuongoza zoezi la sasa, inaelezwa kuwa serikali ya Rwanda imeamua kumtumia kutokana na uelewa wake kuhusu Tanzania.


Kabla ya taarifa hizi, Lwakabamba aliwahi kuripotiwa na gazeti moja (si MTANZANIA) kwamba ni waziri mwenye asili ya Tanzania aliyechaguliwa katika serikali ya Rwanda.
Inaelezwa kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, lakini pia alisoma Chuo Kikuu Dar-es-salaam (UDSM) Kitivo cha Uhandisi, na mwaka 1981 alikuwa Mkuu wa kitivo cha Uhandisi, kazi aliyoifanya mpaka anaondoka nchini.
Profesa Lwakabamba, ambaye anaelezwa kuijua vyema Tanzania kutokana na kuishi muda mrefu, alipata elimu ya msingi Muleba, mkoani Kagera na baadaye kujiunga na shule ya sekondari ya Ihungo.
Mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika Kitivo cha Uhandisi, baada ya kujiunga na Chuo cha Leeds, Uingereza kwaajili ya shahada ya fani hiyohiyo.


Msomi huyo anaelezwa kwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame, ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake, baada ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.


Gazeti hili lilimtafuta Profesa Lwakabamba kwa njia ya mtandao ili kupata ufafanuzi kuhusiana na harambee hiyo, lakini hakuweza kujibu maswali aliyoulizwa.

Juhudi za kumtafuta Profesa Lwakabamba bado zinaendelea. Wakati hayo yakitokea,taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa katika mkakati huo,mbunge mmoja (jina tunalo), hivi karibuni alisafiri kwenda Rwanda akipitia Afrika Kusini.

Inaelezwa kuwa mbunge huyo alionana na baadhi ya viongozi wa serikali ya nchi hiyo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Rais Kagame kuhakikisha anaimarisha mtandao wake hapa nchini.

Mbali na mbunge huyo, taarifa hizo zimewataja baadhi ya wanasiasa wengine ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakifaidika na fedha za serikali ya Rais Kagame, kwa kujua ama pasipo kujua kama lengo lake ni kuwaweka katika mtandao wake huo.


Chanzo: Mtanzania

MAPIGANO YAZUKA SUDAN KUSINI

Mapigano yanaripotiwa kuzuka Sudan Kusini kwa mara ya kwanza tangu serikali na waasi kutia saini makubaliano ya kusitisha vita mwezi Januari.

Waasi wanaomtii makamu wa Rais wa zamani Riek Machar, wameshambulia mji wa Malakal, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Upper Nile linalozalisha mafuta kwa wingi.

Majeshi ya serikali, yamepambana vikali na waasi hao katika maeneo tofauti ya mji huo.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa mjini Juba, (Toby Lanzer), amezitaka pande zote kwenye mzozo huo, kulinda raia.

Makabiliano hayo bila shaka yanazua wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika visima vya mafuta Kaskazini mwa nchi.

Mafuta ya Sudan Kusini ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hiyo

ANUSULIKA KIFO MBELE YA CHUI

Mwanamume mmoja nchini China amenusurika kifo katika hifadhi ya wanyama pori nchini humo, baada ya kujirusha ndani ya hifadhi hiyo akisema alitaka 'kuwalisha' wanyama hao hatari.

Mwanamume huyo alitaka kujitoa uhai kwa kujirusha ndani ya chumbacha kuhifadhia Chui wakubwa wenyeMilia au Tiger katika hifadhi ya wanyamapori nchini China.

Wageni waliopigwa na mshangao, walitizama mwanamume huyo aliyejulikana tu kama Yang Jinhai, mwenye umri wa miaka 27 akiumwa, kugwaruswa na kubururwa na wanyama hao kabla ya walinzi kumuokoa.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la China, Chengdu, watalii waliokuwa katika hifadhi hiyo walidhani kuwa bwana Yang alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa hifadhi hiyo kwani walioshuhudia wanasema walimuona akibeba begi mabegani na kupanda mti kama aliyetaka kuwalisha wanyama hao wakubwa.

Lakini baada ya watalii kuanza kumpigia mayowe wakimtaka arejee, bwana Yang alijirusha kutoka mtini na kuanguka ndani ya sehemu walimokuwa wamefungiwa Chui hao.

Watalii hao walisema kuwa Yang alijirusha akitaraji kuwa Chui hao wange mshambulia na kumuua , lakini wanyama hoa waliokuwa Chui Milia Dume na Jike walionekana kushtuka zaidi kwa kumuona Yang huku Chui jike akitoroka kuliko kutaka kumla Yang."

Bwana Yang alionekana akijaribu kuwafanyia vitendo vya kuwakasirisha ili wanyama hao waweze kumshambulia lakini hakufanikiwa. Hatimaye Chui Dume alimshambulia Yang baada ya kushikwa na hasira na kuanza kumuuma na kumgwara lakini aliokolewa na walinzi wa hifadhi hiyo.

Yang alipata matibabu lakini baada ya kutibiwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa nia yake ilikuwa 'kuwalisha wanyama hao.'

Familia ya Yang ilisema kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili na kuwa walikuwa wamepanga kumpeleka hospitalini kwa ushauri nasaha,.

Walinzi wa hifadhi hiyo walisema kuwa Yang alikuwa na bahati mno kuweza kunusurika kifo.

POSHO BUNGE LA KATIBA 300000 KWA SIKU

BUNGE Maalumu la Katiba litafunguliwa rasmi Jumatano ijayo ya Februari 26, mwaka huu likiwa na wajumbe 629 na imethibitishwa kuwa kila mjumbe atalipwa Sh 300,000 kwa siku. Katibu wa Bungela Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Thomas Kashillilah, aliwaambia waandishi wa habari hayo jana ndani ya ukumbi mpya wa Bunge, walipoingia kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi huo kuangalia mfumo wa kisasa wa sauti na mambo mengine.

Dk Kashillilah akiwa amefuatana na Katibu Msaidizi wa Baraza la Wawakilishi na maofisa wengine wa Bunge la Jamhuri, alisema ratiba ya mkutano wa Bunge Maalumu la Katiba inaonesha kuwa litazinduliwa rasmi Februari 26, ingawa kesho litaanza kwa mkutano wa maelekezo ya ukaaji na jiografia ya ukumbi.

Alisema ratiba imeanza jana kwa kusajili wajumbe hao, kazi ambayo inaendelea leo na kesho asubuhi kutafanyika mkutano huo wa maelekezo na saa 8 mchana, kutasomwa tangazo la kuitisha Bunge Maalumu, uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda na kuandaa na kupitisha Kanuni za Bunge hilo.

"Mwenyekiti wa muda atachaguliwa kwa utaratibu maalumu uliowekwa na Katibu wa Bunge la Muungano na wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambao utaratibu tutatoa kesho (leo). Mwenyekiti wa Muda atasimamia kuchaguliwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba," alisema Dk Kashillilah.

Alisema Mwenyekiti wa Muda pia atasimamia kuandaliwa kwa Kanuni, na baada ya kupatikana kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, ndipo atateuliwa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo kwa mujibu wa sheria kwani yeye na mwenzake wa Zanzibar, kwa sasa wanasimamia tu mchakato huo.

Alisema kabla ya Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kuanza kazi zao, kwanza watasubiri Rais kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu, na ndipo Katibu wa Bunge hilo, atakuja kumwapisha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti; na Mwenyekiti kuwaapisha wajumbe wake.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Jumatano na Alhamisi zitatumika kwa kikao cha kazi cha kuandaa Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalumu, wakati Ijumaa itakuwa siku ya kupitisha Azimio la kuridhia Kanuni za Bunge Maalumu, uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na kiapo cha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalumu (ingawa hiyo siyo shughuli ya Bunge Maalumu).


Dk Kashillilah alisema Jumamosi, itakuwa ni kiapo cha Mwenyekiti naMakamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu na kufuatiwa na kiapo cha wajumbe wa Bunge Maalumu ambacho kitaendelea hadi Jumapili.

Aidha, Jumatatu pia kutakuwa na kiapo cha wajumbe saa 4 asubuhi na kuunda Kamati za Bunge Maalumu, kabla ya ufunguzi rasmi wa Bunge utakaofanywa na Rais Jakaya Kikwete, saa 10 jioni.

Katibu huyo wa Bunge la Muungano alisema uwasilishwaji wa Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu itakuwa ni Jumanne na Jumatano ya Februari 26, mjadala wa kupitisha Rasimu ya Katiba utaanza hadi Aprili 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge Maalumu litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha masharti ya Katiba inayopendekezwa na kutunga masharti ya Mpito na masharti yatokanayo kama Bunge Maalumu litakavyoona inafaa.

Kupitisha Katiba Ili Katiba inayopendekezwa ipitishwe katika Bunge Maalumu la Katiba, itahitajika kuungwa mkono kwa wingi wa theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge Maalumu kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, muda ambao Bunge Maalumu litajadili Rasimu ya Katiba hautazidi siku 70 kuanzia tarehe ambayo Bunge Maalumu lilipoitishwa, hivyo uhai wa Bunge hili unatarajiwa kukoma Aprili 30, mwaka huu, lakini unaweza kuongezwa kwa mashauriano kati ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu na Makamu wake kwa ridhaa ya Rais kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar.

Akizungumzia gharama za ukarabati wa jengo na miundombinu mingine, Dk Kashillilah alisema ni Sh bilioni 8.2, ambazo zote zimetoka katika Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/14 ambayo ilishapitishwa na Bunge ikiwamo posho za wajumbe ambazo ni Sh 300,000 kwa siku kwa mjumbe.

"Fedha zote hizo zilikuwapo katika Bajeti ya Serikali iliyopitishwa Juni mwaka jana, kwa hiyo siyo suala geni. Na zimetumika katika ukarabati wa jengo la ukumbi, vifaa vikiwamo viti 678 ambavyo gharama yake ni dola za Marekani milioni moja," alifafanua Katibu wa Bunge.

Alisema katika posho, wajumbe watalipwa posho ya kawaida ya Serikali ya siku (haikutaja), lakini alisema kutawakuwa na kodi maalumu ambayo itahusisha poshoya kikao, usafiri, malipo kwa madereva na mengineyo, ambayo itakuwa ni Sh 220,000.

Hivyo posho ya kawaida itakuwa Sh80,000 ukijumuisha na Sh 220,000 unapata Sh 300,000 watakazolipwa kwa siku.

Alisema Bunge Maalumu litajumuisha wajumbe 629 ambao ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 357, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW) 82 na wajumbe wa kuteuliwa kwa uwakilishi 201.

Aliongeza katika idadi hiyo, unapunguza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambao pia ni wajumbewa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sita, Mjumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa uteuzi wa Rais wa Zanzibar, wabunge wawili waliofariki na nafasi mbili za uteuzi wa Rais zilizowazi, unapata wajumbe 629, ambao zaidi ya 120 walikwisha jisajili hadi kufikia jana mchana.

PEMBE ZA NDOVU KILO 130 ZANASWA

Ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kukiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu linaloielemea Tanzania, Jeshi la Polisi mkoani Mtwara na Singida linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha nyara za Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga alisema kuwa jeshi hilo limewakamata watu watatu wakiwa na meno ya tembo 58 yenye uzito wa kilogramu 130.6 yenye thamani ya Sh700.3 milioni.

Kamanda alieleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa saa 11:00 alfajiri katika Kijiji cha Chungu Kata ya Nanyumbu, Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara wakiwa katika kizuizi cha barabara ya Mtambaswala – Mangaka wakielekea jijini Dar es Salaama.


"Tunawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali ambazo ni meno ya tembo 58 yenye uzito wa kilogramu 130.6 na thamani ya 700.3 milioni, ambapo ni sawa na tembo 29 waliouawa yakiwa ndani ya gari ainaya Toyota Land Cruiser," alisema Kamanda Manganga.

Alisema mbinu waliyotumia watuhumiwa hao ni kukata sakafu ya gari ya chini ya kiti cha nyuma yadereva na kutengeneza tanki la bandia na kuweka meno hayo kishakuweka kapeti juu yake.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamidu Ngunde (40) dereva, Geraldat Lukas (36) dereva na Boniphace Kosan (29) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam na kusema kuwa gari iliyotumika kusafirisha meno hayo ni mali ya Hilali Rashid.


Wakati huo huo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alisema wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, Februari 13 mwaka huu saa 2.30 asubuhi katika kizuizi cha Mazaoa ya Misitu na Chakula kilichopo katika Kijiji cha Ukimbu Kata ya Mgandu, tarafa ya Itigi, Wilaya ya Manyoni.

Alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia gari aina ya Toyota lenye namba T.797 CQL kusafirisha nyara za Serikali kutoka Kijiji cha Mwamangembe kwenda Itigi Mjini.

"Nyara alizokamatwa nazo mtuhumiwa zilikuwa zimewekwa kwenye mabegi mbalimbali ya nguo," alifafanua.

Kamwela alisema uchunguzi wa awali, umeonyesha kuwa vipande hivyo 21 vinakadiriwa kuwa vya tembo wanne, vina uzito wa kilogramu 49 na thamani ya Sh43.1 milioni.

MVUA YAUWA NA KUEZUWA NYUMBA

Nyumba 62 zilizopo katika Vijiji vya Wilaya ya Kilindi, zimeezuliwa na nyingine kubomoka kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga.

Maafa hayo yamesababisha mtoto mmoja kufa kwa kuangukiwa na nyumba, huku zaidi ya wanavijiji 110 kukosa mahala pa kuishi.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa ni kuwa nyumba hizo zimeezuliwa usiku wa kuamkia Ijumaa wiki iliyopita baada ya kunyesha mvua iliyoambatana na upepo.

Mvua kubwa ilinyesha katika vijiji mbalimbali vya wilayani hapa na kusababisha madhara hayo.

Akithibitisha tukio hilo, Liwowa alivitaja vijiji vilivyokumbwa na maafa hayo kuwa ni Songe, ambako mtoto mmoja amekufa kwa kuangukiwa na ukuta.

Vijiji vingine ni Kwasetemba, ambako nyumba 16 zimeanguka naGitu zilikobomoka na kuezuliwa ni nyumba 42.

Alisema ya maafa hayo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Kilindi iliweza kutembelea kwa lengo la kujionea athari, ambapo hatua inayofuata ni kutuma wataalamu kutathimini athari na mahitaji kwa waathirika.

MOQTADA AJIUZULU WADHIFA WAKE

Kiongozi wa Dhehebu la Shia nchini Iraq Moqtada al-Sadr ametoa taarifa akitangaza kujiuzulu kwake katika ulingo wa kisiasa.

Katika tangazo ambalo halikutarajiwa na wengi na ambalo liliwekwa katika mtandaowake,Bwana Sadr amesema kuwahatashikilia wadhfa wowote wa serikali wala kuwa na wawakilishi bungeni.

Taarifa hiyo pia imesema kuwa atazifunga afisi zake zote isipokuwa zile za kutoa misaada pekee.

Bwana Sadr na wanamgambo wake wa Mahdi walipata ushawishi nchini Iraq baada ya uvamizi wa marekani nchini humo mnamo mwaka 2003.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni amepoteza umaarufu wake kufuatia mzozo kati yake nawaziri mkuu nchini humo Nouri al-Maliki.

Wakati huohuo Aliyekuwa makamu wa rais nchini Iraq amemlaumu waziri mkuu Nouri Al Maliki kwa kusababisha ghasia kati ya wanamgambo wa dhehebu la sunni na vikosi vya serikali ambavyo vinaushikilia mkoa wa Anbar tangu mwezi Disemba.

katika mahojiano na BBC,Tariq al-Hashemi ameishtumu serikali hiyo inayoongozwa na watu wa dhehebu la shia kwa kuzua mgongano huo, kupitia kuwabagua watu wa dhehebu la sunni mbali na kupuuzilia mbali maandamano ya amani.

Bwana Hashemi kwa sasa anaishi kama mkimbizi nchini Uturuki baada ya mahakama moja nchini humo kumpatia hukumu ya kunyongwa kwa madai ya kuendesha magenge ya uhalifu,mashtaka anayoyapinga.

Bwana Hashemi anasema kuwa madai ya serikali ya Iraq kwambauasi huo unaongozwa na vikosi vinavyoshirikiana na kundi la Alqaeda ni njama ya kutotaka kuwajibika mbali na kuvutia hisani kutoka kwa jamii ya kimataifa.

JOSEPH MINALA ANA MIAKA 17

Klabu ya Lazio imesisitiza kuwa mmoja ya wachezaji wao-Joseph Minala wa Cameroon ana umri wa miaka kumi na saba kama alivyosema baada ya ripoti kusambazwa kuwa ana miaka arobaini na moja.

Klabu hiyo imesema kuwa cheti cha kuzaliwa cha mchezaji huyo kilikuwa halali.

Minala, ambaye ameshiriki katika mashindano ya vijana chipukizi katika klabu hiyo, pia alitoa taarifa akikana madai kuwa aliliambia mtandao moja wa Kiafrika kuwa alikuwa amedanganya umri wake.

Sakata hiyo sasa huenda ikahujumu mchezo wa Minala ambao katika miezi ya hivi karibuni imekuwa ikiimarika na huenda akakosa fursa ya kujiungana vilabu vingine endapo mzozo huo utaendelea.

Shirikisho la mchezo wa soka nchini Italia, halijasema lolote kuhusu suala hilo sawai na shirikisho la mchezo wa soka nchini Cameroon.

Katika miaka ya hivi karibuni wachezaji wengi wa Kiafrika wameshutumiwa kwa kudanganya umri wao ili kushiriki ligi ya vijana chipukizi ili kuimarisha nafasi yao ya kujiunga na vilabu vya ulaya.

AL-SHABAAB WAPATA SILAHA ZA SERIKALI

Ripoti ya umoja wa mataifa imeonya kuwa silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa vikosi vya serikali ya Somali zimeingia katika mikono ya kundi la Al-shabaab kutokana na ukiukwajiwa utaratibu katika serikali.

Uchunguzi huo uliofanywa na wataalam walio huru umesema kuwa silaha za kudungua ndege,mabomu na risasi zilizotoka nchini Uganda na Djibout haziwezi kuwajibikiwa.

Ripoti hiyo sasa inataka taifa la Somali kuwekewa vikwazo vya silaha ambavyo viliondolewa mwaka uliopita.

Wataalam hao wamesema kuwa wana ushahidi kwamba mshauri mkuu wa rais nchini Somali amekuwa akihusika na mpango wa kuwapelekea silaha wapiganajiwa Alshabaab.

NDOA ZA JINSIA MOJA ZAPINGWA UINGEREZA

Maskofu wakuu katika kanisa moja nchini Uingereza wamewaambia viongozi wa dini kwamba hawataruhusiwa kuingia katika ndoa za jinsia moja,na kusema kuwa hawatakubali viongozi wa dini masenge kwenda kinyume na maagizo hayo.

Viongozi wa dini wa kanisa la Ki-Anglikana wanakubaliwa na kanisa hilo kuingia katika uhusiano wa kimapenzi lakini kwamaelewano kwamba hawatashiriki ngono.

Katika mwelekeo wao, maaskofu hao pia wamepiga marufuku maombi yoyote maalum kwa wanadoa wa jinsia moja licha ya ripoti rasmi ya kanisa hilo kupendekeza kwamba viongozi wa dini wanaweza kufanya hivyo iwapo wanajihisi.

Hata hivyo amesema kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutoa maombi yasio rasmi kwa wanandoa walio katika uhusiano wa jinsia moja.

MPANDA NAKO WAGOMEA EFD

Wafanyabiashara wa Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi wameungana na wafanyabiashara wenzao hapa Nchini kufunga maduka yao kwa siku mbili kuanzia leo ilikuishinikiza Serikali kusikiliza malalamiko yao ya kiwango kikubwa cha bei za mashine za Kielekroniki za kutoza kodi EFD Wafanyabiashara hao walifikia uamuzi hou baada ya baadhi ya wafanyabiashara wenzao kupita kwenye maduka yao na kuwahimiza kufunga biashara zao za maduka.

Baadhi ya wafanyabiashara hao walisema kwamba wanapinga vikali matumizi ya mashine za EFD kutokana na kwamba ni mzigo kwa wafanyabiashara na zinapatikana kwa gharama kubwa ukilinganisha na mahitaji ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Katavi Walisema licha ya machine hizo kuuzwa kwa bei kubwa utengenezwaji wake pia gharama zake ni kubwa kwani pindi zinapoharibika mfanyabiashara analazimika kuwatafuta mafundi kutoka Dares salaam auMbeya ndio waje kutengeneza kwani Mkoa wa Katavi hauna fundi hata mmoja wa kutengeneza mashine hizo.

Mgomo huo ambao ulianza jana umewafanya wananchi wa Mji wa Mpanda wakose huduma mbalimbali walizokuwa wakizihitaji na hasa vifaa vya ujenzi kutokana na maduka yote yanayouza vifaa hivyo yalioko maeneo ya karibu na Soko kuu kufungwa Badhi ya wamiliki wa maduka ambayo hayapo katika orodha ya kutakiwa kutumia mashine hizo kwa kuwa mauzo yao hayafikii shilingi milioni 14 kwa mwaka wamejikuta wakifunga maduka yao kwa kufofia kufanyiwa fujo na wafanyabiashara wenzao.

Kwa upande wake mwenyekitiwa chama cha Wafanyabashara viwanda na kilimo wa Mkoa wa Katavi Hassanali Dalla alisema jana aliombwa na baadhi ya wafanyabiashara wa mji wa Mpanda aitishe mkutano bbaina ya wafanyabiashara na Mkuu wa Mkoa wa Katavi iliwaweze kumweleza msimamo wao wa kupinga mashine hizo.

Alisema hata hivyo aliwapa maelekezo ya kufuata iliaweze kuandaa mkutano huo lakini hadi jana wafanyabiashara hao walikuwa hawajatekeleza utaratibu ambao alikuwa amewalekeza zaidi ya wao kuamua funga maduka yao pasipo kumtalifu mwenyekiti wao.

Pia alisema mpaka sasa mamlaka ya mapato katika Mkoa wa Katavi haijawaandikia barua yoyote wafanyabiashara ambao wanatakiwa watumie mashine hizo hivyo hakuona kama kuna sababu ya msingi ya wafanyabiashara kufunga maduka yao wakati hawana barua yoyote ya kuwaelekeza.

DADA AMSAIDIA KAKA KUMNAJISI MSICHANA WA MIAKA 12

MKAZI wa mtaa wa Tambukareli wilayani Mpanda, Helen Simon (20)anashikiliwa Polisi na kaka yake, Afred Mnyonge (24) kwa tuhuma za kumsaidia kaka huyo kumnajisi msichana jirani yao, mwenye umri wa miaka 12.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Kamishina wa Polisi, Dhahiri Kidavashari, alidai msichana huyo alinajisiwa juzi saa tatu usiku.

Akisimulia mkasa huo, Kamanda Kidavashari alisema usiku huo wa tukio, mtuhumiwa Helen alifika nyumbani kwa msichana huyo aliyekuwa akiishi na shangazi yake, Kibena Hussen na kumtaka msichana huyo amsindikize sehemu ambayo hakuitaja.

Inadaiwa kuwa msichana huyo huyo pasipokuwa na shaka wala wasiwasi wowote, alimsindikiza Helen hadi nyumbani kwa kaka yake huyo na wote wakaingia ndani ya nyumba hiyo."Muda mfupi baadaye Helen alimtaka msichana huyo asiondoke bali amsubiri kidogo kwa kuwa alikuwa anaenda wuani kujisaidia ndipo alipotoka na kufunga mlango wa nyumba hiyo kwa nje".

Msichana huyo baada ya kugundua kuwa mlango wa nyumba hiyo umefungwa kwa nje alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada lakini hakuna jirani aliyejitokeza kumsaidia, alibainisha Kidavashari.

Kwa mujibu wa kamanda Kidavashari mtuhumiwa Alfred alimkamata kwa nguvu na kumbaka huku akiwa ameuziba mdomo wa msichana huyo kwa kipande cha nguo.

Inadaiwa baada ya kumfanyia msichana huyo unyama huo alimwamuru aondoke nyumbani kwake ndipo alitoka na kurejea nyumbani kwa shangazi yake ambapo alimkuta akiwa bado macho, hajalala ambapo alimsimulia mkasa mzima uliomkumba.

Inadaiwa shangazi ya msichana huyo aliongozana na binti huyo hadi Kituo cha Polisi mjini Mpanda ambapo alipewa fomu PF 3 ambapo msichana huyo alipata matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na baadae akaruhusiwa kurejea nyumbani.

Kwa mujibu wa Kamanda wanandugu hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara tu uchunguzi wa awali wa shauri lao litakapo kamilika.

KENYA KUTOTEKELEZA MATAKWA YA ICC

Mwanasheria mkuu wa Kenya Profesa Githu Muigai ameiambia mahakama ya kimataifa ya ICC kwamba serikali ya Kenya haiwezi kutekeleza matakwa ya kiongozi wa mashitaka katika mahakama hiyo ya kuwashurutisha mashahidi waliojiondoa kutoka kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta kwenda kutoa ushahidi.

Pia amesema kuwa hawawezi kuagiza kutolewa kwa nyaraka za Benki za Rais Kenyatta za wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi miaka sita iliyopita.

Profesa Githu Muigai amekuwa mbele ya mahakama ya ICC kujibu madai ya upande wa mashtaka kwamba serikali ya Kenya imekuwa ikiweka vizingiti kwenye kesi dhidi ya Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda alitaka serikali ya Kenya iwasilishe stakabadhi za Benki za Rais Kenyatta za wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi.

Pia alitaka serikali iwalazimishe mashahidi saba waliojiondoa kutoka kesi hiyo kwenda ICC kutoa ushahidi, akidai walijiondoakutokana na shinikizo za serikali.

Lakini Bwana Muigai ameiambia mahakama kwamba mkataba wa Roma uliobuni mahakama ya ICC hauruhusu mashahidi kushurutishwa kutoa ushahidi.

Kuhusu kutolewa nyaraka za Benki za rais Uhuru Kenyatta, Bwana Muigai amesema ombi hilo lilitakiwa kutoka kwa majaji wanaosikiza kesi na wala sio kiongozi wa mashitaka.

Lakini pia amesema sio jukumu lake kuagiza kutolewa kwa stakabadhi hizo, bali ni mchakato wa mahakama, ambayo inaweza kuridhia ombi hilo, au kulikataa kama idara huria.

Mawakili wa Bwana Kenyatta wanataka kesi hiyo itupiliwe mbali, huku kiongozi wa mashitaka Bi Bensouda akitaka iahirishwe kumpa muda kusubiri nyaraka hizo ambazo anasema zitampa ushahidi zaidi wa kujenga hoja. Kikao kitaendelea hapo kesho.

PUTIN AUNGA MKONO FIELD MARSHAL AL-SIS KUGOMAEA URAIS

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema anaunga mkono amiri mkuu wa majeshi ya Misri Abdul Fattah al-Sisi Kuwania urais wa taifa hilo.Putin alimweleza Al-Sisi kuwa alifahamu kuhusiana na niya yake ya kuwania urais.

Hata hivyo hakujakuwa na dhibitisho lolote kutoka kwa ujumbe wa serikali ya Misri.

Kiongozi huyo wa jeshi la Misri ndiye aliyeongoza mapinduzi yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi mwezi julai mwaka uliopita.

Katiba mpya ya taifa hilo inashurutisha kufanyika kwa uchaguzi ifikiapo katikati ya mwezi Aprili mwaka huu.


KHERI NJEMA

Mwandishi wa BBC anasema iwapo uchaguzi wa urais utafanyika sasa kiongozi huyo wa jeshi anapigiwa upatu kushinda kwa sababu ya umaarufu wake.

Aidha hakujajitokeza mpinzani mwenye ushawishi mkubwa

Putin "Nakutakia kheri na ufanisi katika juhudi zako kwa niaba yangu binafsi na wananchi wa Urusi ''

Field Marshal Sisi yuko mjini Moscow kujadili mkataba wa silaha wenye thamani ya dola bilioni 2.

Mkataba huo unawadia baada ya serikali ya Marekani kusitisha makubaliano ya Mauzo ya silaha na Misri baada ya kungolewa madarakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi julai mwaka uliopita.

MAKAO MAKUU YA CHADEMA YANUSURIKA KUUNGUA

Makao makuu ya chama cha demokrasia na maendelea Chadema yaliyopo jijini Dar es salaam yamenusurika kuteketea kwa moto baada ya watu wasiojulikana kufanya jaribio la kulipua makao hayo usiku wa kuamkia tarehe 11 Febuari mwaka huu.

ITV imefika katika makao makuu ya chama hicho na kushuhudua askari wa upelelezi wakiendelea na hatua za awali za upelelzi huku katibu mkuu wa chama hicho Dkt Wilbrodi Slaa akilaani kitendo hicho na kutaja tukio Hilo ni mwendelezo wa matukio ambayo yamekuwa yakikikumba chama hicho na kuitaka serikiali kuwa makini na vitendo hivyo kwani vinaweza kuchangia upotevu wa amani hapa nchini.

Aidha Dr Slaa amefafanua kauli yake aliyowahi kuitoa kwa rais Kikwete kuwa kama hata ingilia kati vitendo hivyo nchi haita tawalika kwani itafika kipindi vitendo kama hivyo havitavumilika miongoni mwa Watanzania na kuitaka serikali aingilie kati ili wale wote wanaoendelea kufanya vitendo hivyo wawezea kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.


Chanzo:ITV

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA KIMBARI WAPATA AFUENI

Mahakama maalum ya Kimataifa ya Rwanda- ICTR imefutilia mbali kesi dhidi ya maafisa waandamizi wawili watuhumiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda.

Uamuzi huu umetolewa katika kesi yao ya rufaa.

Walishitakiwa kuhusika na mauajiya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, ambayo inakadiriwa watu laki nane walipoteza maisha.

Aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi Augustin Ndindiliyimana, ameelezewa kama mmoja wa watu wa ngazi ya juu waliohukumiwa na mahakama hiyo inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Afisa wa pili, Francois-Xavier Nzuwonemeye alikuwa kamanda msomi wa kikosi cha jeshi.

Mahakama ya ICTR pia imepunguza muda wa kifungo cha afisa wa tatu.

Hata hivyo uamuzi kuhusu rufaa ya mkuu wa zamani wa Jeshi Augustin Bizimungu haujatangazwa bado.

WATU 100 WAFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE

Ndege ya usafiri ya jeshi imeanguka ikiwa imebeba zaidi ya watu 100.

Redio ya taifa inasema ndege hiyo imeanguka katika eneo la milima katika jimbo la Oum El Bouaghi kusini mashariki mwa mji mkuu , Algiers na ilikuwa imewabeba abiria 103 wakiwemo wafnyakazi wa ndege hiyo.

Kuna taarifa kwamba ndege hiyo ilikuwa imebeba familia za maafisa wa jeshi.

Ndege hiyo ya wanajeshi inaripotiwa kuanguka katika eneo lililo na milima mingi mashariki ya nchi hiyo. Kituo cha Redio ya nchi ya Algeria inasema kuwa kulikuwa na waabiri 103, wakiwemo watumishi wa ndege hiyo.

Hakuna ripoti rasmi za majeruhi, ila vituo vya habari vya nchi hiyo vinapeana matumaini kwa uchache mno juu ya manusura.

Ndege hiyo inasemekana ilikuwa ikibeba wanajeshi na watu wa familia zao waliokuwa wakisafiri kuelekea jiji la Constatine. Jeshi halijatoa taarifa yoyote mpaka sasa.

MAJAMBAZI WAVAMIA SHULE YA SEKONDARI, WAUWA MWANAFUNZI MMOJA

Majambazi nchini Kenya wamemuua mwanafunzi mmoja wa shule ya upili na kuwajeruhi wengine wengi katika uvamizi waliofanya dhidi ya shule ya mabweni ya St Charles usiku wa kumakia leo.

Wanafunzi wa shule hiyo iliyo viungani mwa Nairobi,walisimulia ambavyo majambazi waliwashambulia usiku wa manane wakiwa wamelala katika mabweni yao na kusababisha kifo cha mmoja wao.

Wanafunzi walionusurika walisema majambazi hao ambao idadi yao inakadiriwa kuwa hamsini , walivunja madirisha na milango na kisha kuingia katika mabweni yao.Waliwachapa wanafunzi kwa mijeledi na kuwapiga mawe na kisha kuwashuturisha kutoroka.

Baada ya uvamizi huo walitoka nje na kuharibu magari ya walimu yaliyokuwa yameegeshwa nje pamoja na mabasi ya shule. Ni nadra kusikia uvamizi kama huu dhidi ya shule.

Mkurugenzi mkuu wa shule hiyo bwana Charles Niyamote aliambia BBC kuwa nia ya wavamizi haijulikani ingawa alidokeza kwamba huenda ni wivu uliowachochea majambazi hao kutenda uhalifu huo.

Hata hivyo tetesi zinasema kuwa huenda ni mzozo wa ardhi uliosababisha uhalifu huo.

Kwa sasa shule hiyo imefungwa kwa muda wa wiki moja wakati polisi wakiendelea na uchunguzi wa kina.

Visa vya ukosefu wa usalama vimeongezeka katika mji wa Nairobina viunga vyake katika siku za hivi karibuni na pia sio jambo la kawaidakwa wanafunzi kuvamiwa shuleni nchini Kenya.

SHABIKI WA ARSENAL AMDUNGA KISU MWENZIE WA LIVERPOOL BAADA YA KICHAPO CHA 5 KWA 1

Mwanamume raia wa Kenya anayeshabikia klabu ya soka ya Uingereza ya Liverpool amedungwa kisu na mwenzake wa klabu ya Arsenal na kufariki dunia katika eneo la Meru Mashariki mwa Kenya.

Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo wawili hao walianza malumbano baada ya mechi kati ya vilabu hivyo kumalizika hapo Jumamosi.

Wawili hao walikua katika baa moja iliyojaa mashabiki wa timu hizo mbili.

Shabiki wa Arsenal anayefanya kazi ya Boda Boda alijawa na hasira baada ya timu yake kukemewa na shabiki wa Liverpool kiasi cha kumdunga mwenzake kisu mara kadhaa, kabla ya kutoweka.

Watu waliokua karibu na eneo la tukio hilo walimsaidia mwathiriwa aliyetambuliwa kama Anthony Muteithia na kumpeleka katika hospitali kuu ya Meru ambapo alifariki dunia wakati akipokea matibabu.

Mkuu wa polisi eneo la Meru Tom Odero amesema wanamsaka shabiki huyo wa Arsenal ambaye amekwenda mafichoni.

Hapo Disemba mwaka jana shabiki wa klabu ya Manchester United nchini Kenya kwa jina Jimmy Macharia alijiua baada ya klabu hiyo kuendelea kuorodhesha matokeo mabaya.

Na mnamo mwaka 2012 Suleiman Alfonso Omondi shabiki wa Arsenal alijitia kitanzi baada ya timu hiyo kushindwa kwenye mechi.

Ligi ya Premia nchini Uingereza huvutia ushabiki mkubwa nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla.

RWANDA YAPITISHA SHERIA YA KUJIMILIKISHA MALI ZA RAIA WASIOISHI NDANI YA NCHI

Bunge la Rwanda limepitisha sheria tata inayoruhusu serikali kudhibiti mali ya raia wa nchi hiyo ambao hawaishi nchi humo.

Wakosoaji wa serikali hata hivyo wanasema kuwa hii ni njama ya serikali kuchukua mali ya watu wanaoonekana kuwa wapinzani wakuu wa serikali ya Rais Paul Kagame.

Wizara ya sheria ambayo ilipendekeza mswada huo, bungeni ilisema kuwa sheria yenyewe inanuia kuzuia migogoro yoyote inayotokana na mali ya watu.

Ushindani wa kumiliki ardhi nchini Rwanda , umesababisha mvutano na hata umetajwa kuwa moja ya mambo yaliyosababisha mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Serikali inasema kuwa sheria hiyo italenga tu mali ambayo wamiliki wao hawajulikani au wamefariki bila ya watu kurithi mali hiyo.

Hata hivyo mgogoro umezuka kuhusu serikali kutaka kudhibiti mali ya mmoja wa matajiri wakubwa wa nchi hiyo Tribert Rujugiro, ambaye sasa anaishi uhamishoni.

Wakosoaji wanasema kuwa mpango huo unalenga mali ya tajiri huyo ikiwemo jengo kubwa la kibiashara ambalo limekuwa likidhibitiwa na serikali tangu mwaka jana.

Mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa wakati mmoja mshirika mkubwa wa chama tawala RPF alikosana na Rais Kagame baada ya kumwambia kuwa haheshimu sheria pamoja na kumkosoa kwa kuingilia hukumu zinazotolewa na mahakama Serikali imekanusha madai hayo ikisema kuwa haina nia ya kuchukua mali ya watu bila kuelezea ni kwa muda gani.

Wizara ya sheria inasema kuwa zaidi ya watu 700 wataathirika.

Kwa sasa mswada huo umepitishwa na bunge na kilichosalia ni kupigiwa kura na baraza la Senate kabla ya kutiwa saini na Rais Kagame.

MGOMO WA WAFANYAKAZI WA TRENI HUENDA UKA ATHIRI MECHI ZA EPL

Mechi ya ligi kuu ya Premier kati ya Fulham na Liverpool siku ya Jumatano, huenda ikahairishwa ikiwa mgomo wa wafanyakazi wa treni mjini London utaendelea kama ulivyopangwa.

Wafanyakazi hao wa treni wanatarajiwa kuanza mgomo wa saa 48 kuanzia leo, hali ambayo inaweza kutatiza shughuli za usafiri kama ilivyokuwa wiki iliyopita mjini humo.

Wasimamizi wa Fulham wana wasi wasi kuwa wafanyakazi wao huenda washindwe kufika kazini kwa muda unaofaa au hata kukosa kufika ili kuhakikisha kuwa mechi hiyo imeendelea.

Klabu hiyo inatarajiwa kutangaza baadaye hii leo ikiwa mechi hiyo itahairishwa au la.

Wamiliki wa klabu hiyo wamekuwa na mazungumzo na maafisa wa baraza la mji wa London pamoja na maafisa wa polisi na wamesema kuwa wana matumaini kuwa mechi hiyo itachezwa kama ilivyopangwa.

Huku hayo yakijiri, leo hii kutakuwa na mechi kadhaa za ligi kuu ya premier.

Cardif City itakuwa mwenyeji wa Aston Villa, Southampton kusafiri ugenini kucheza na Hull City.

West Ham itakuwa nyumbani kutoana jasho na Norwich, ili hali West Brom kualika vinara wa ligi hiyo kwa sasa Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani.

MHUBIRI AOMBA MSAMAHA BAADA YA KUKUTWA AKILA URODA NA MKE WA MTU

Mhubiri mmoja mkristo nchini Kenya ameomba msamaha kanisani baada ya kupatikana akila uroda na mke wa mwanamume mwingine mjini Nyeri eneo la Kati mwa Kenya.

Mhubiri huyo alipangisha chumba katika mkahawa mmoja mjini humo, ingawa hakujua kuwa alikuwa amefuatwa na waandishi wa habari waliompata katika kitendo hicho na mke wa watu.

Alisema kuwa mbali na kutaka msahama wa waumini wa kanisa lake pia ameomba msamaha kwa Mungu.

Lakini huku wakazi wa Embu anakotoka kasisi huyo, wakitafakari msamaha kwa mhubiri huyo, viongozi wa kanisa anakotumikia wamemwachisha kazi kwa muda wakifanya uchunguzi kuhusu kashfa hiyo.

Kasisi Anthony Maina alijitokeza hadharani na familia yake baada ya maombi siku ya Jumapili na kutaka viongozi wa kanisa hilo la Assemblies of God kumsamehe kwa kuzini na mke wa wenyewe.

Mkewe mhubiri huyo na wanao walisema kuwa wamemsamehe kwa kile alichofanya.

Akiongea na waandishi wa habari,muhubiri huyo alisema kuwa hakwenda kanisani mjini Embu kujitetea.

Alikiri kuwa amemkosea Mungu na kusema kuwa tayari ameomba msamaha kutoka kwake.

Mmoja wa viongozi wa kanisa hiloalisema wakati kunatokea kitendo kama hiki, kasisi huondolewa katika majukumu yake kwa muda kabla ya kurejeshwa kazini.

Askofu mkuu wa kanisa hilo aliwasihi wananchi kutofurahia wakati, mtu anapopatikana na mkosi kama huo

MUSLIM BROTHERHOOD WASHUTUMIWA KUUNDA JESHI

Utawala nchini Misri, umeishutumu, vugu vugu la Muslim Brotherhood, lililopigwa marufuku kwa kuunda kitengo maalum cha kijeshi Kusini mwa nchi hiyo, ili kufanya mashambulio dhidi ya wanajeshi wa serikali.

Wizara ya usalama wa ndani nchini Misri, imetoa orodha ya majini ya watu kumi na wawili wakitengo hicho, na kuwashutumu kwa kuwauawa maafisa watano wa polisi katika mkoa wa Beni Suef.

Maafisa wa Ulinzi nchini Misri wamewauawa takriban wafuasi elfu moja wa vugu vugu hilo la Muslim Brotherhood, tangua jeshi la nchi hiyo lilipomuondoa madarakani, rais Mohamed MorsiJulai mwaka uliopita.

Kundi hilo limesema kuwa linapinga vikali ghasia na machafuko, lakini kumekuwa na mashambulio kadhaa dhidi ya maafisa wa ulinzi yanayotekelezwa na watu wanaoaminika kuwa wapiganaji wa Kiislamu.

Awali siku ya Jumapili, kiongozi mmoja mwandamizi wa Kiislamu, Abdel Moneim Aboul Fotouh alisema kuwa, taifa la Misri limegeuka na kuwa Jumuhuri la uoga.

KESI DHIDI YA BOSCO NTAGANDA KUANZA ICC LEO

Kesi dhidi ya aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda, inatarajiwa kuanza hii leo katika mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.

Mahakama hiyo inatarajiwa kuamua ikiwa Bosco Ntaganda atafunguliwa mashtaka ya mauaji, ubakaji, utumwa wa ngono na kuwasajili watoto jeshi.

Mshukiwa huyo ambaye pia anafahamika kama ''The Terminator'' ni mwanzilishi kwa kundi la waasi la M23, ambalo lilishindwa na utawala wa Kinshasa mwaka uliopita, baada ya miezi kumi na nane na mapigano makali, katika eneo la Kivu ya Kaskazini, Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Lakini atakapofika mbele ya mahakama hiyo, Ntaganda atafunguliwa mashtaka kumi na tatu ya uhalifu wa kivita na mengine matano ya ukatili wa kibinadam, uhalifu uliotekelezwa zaidi ya miaka kumi iliyopita wakati alipokuwa mbabe wa kivita katika eneo la Ituri, Kaskazini mwa Congo.


*ZAIDI YA WATU 800 WALIUWAWA

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Fatouh Bensouda, amesema kuwa takriban watu mia nane waliuawa na wapiganaji wa Patriotic Foces for Liberation of Congo, FPLC, walioongozwa na Bwana Ntaganda.

Wengi wa wapiganaji wake walitoka kabila la Hema ambao walikuwa wakipambana na wapiganaji wa wa Lendu, kuthibiti maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa na Bensouda katika mahakama hiyo, Ntaganda aliongoza na kuidhinisha mashambulio kadhaa dhidi ya watu wa kabila la Lendu.

''Wanjaeshi wa Ntaganda walishambulia vijiji kadhaa kwa kutumia silaha nzito nzito na kuwafukuza watu, huku wakifanyamsako wa nyumba hadi nyumbana pia katika misitu iliyokuwa katika eneo hilo'' Alisema Bensouda.

Kiongozi huyo wa zamani wa waasi anatuhumiwa kuharibu mali ya raia kwa kuteketeza makaazi yao baada ya kupora mali.


*ATUHUMIWA KUSAJILI WATOTO JESHINI

Ripoti zinasema Ntaganda alizuru kambi kadhaa ambako watoto walio na chini ya umri wa miaka kumi na mitano walipewa mafunzo ya kijeshi na kuwa alifanya mashambulio pamoja nao.


Katika kikao chake cha kwanza katika mahakama hiyo mwezi Machi mwaka uliopita, Ntaganda aliwaambia majaji hao wa ICC kuwa ''Nimefahamishwa kuhusu mashtaka ya uhalifu yanayonikabili na kuwa anakiri kuwa hana hatia'' Majaji wa mahakama hiyo ya ICC wana muda wa wiki mbili kuamua ikiwa kesi dhidi ya Bwana Ntaganda itaendelea au la.

Mshukiwa mwingine ambaye alifunguliwa mashtaka kwa pamoja na Ntaganda alihukumiwa kifungo cha miaka kumi na minne gerezani.

Ntaganda ni mshukiwa wa kwanza ambaye alijisalimisha kwa mahakama ya ICC, baada ya kujisalimisha kwa ubalozi wa Marekani mjini Kigali miezi kumi na moja iliyopita na kuomba awasilishwe kwa mahakama ya ICC.


*NTAGANDA ALIJISALIMISHA KWA NIA GANI?

Wachanganuzi wanasema kuwa Ntaganda alihofia maisha yake kama mtoro kutoka kwa viongozi wengine hasimu wa M23 lakini hadi sasa dhamira ya kujisalimisha kwake haijajulikana.

Mahakama ya ICC ilitoa vibali vyakukamatwa kwa Ntaganda mwakawa 2006 na nyingine iliyokuwa na mashtaka zaidi mwaka wa 2012.

Ntaganda ambaye alizaliwa mwaka wa 1973, ni Muafrika wa tano ambaye anazuiliwa na mahakama hiyo ya Kimataifa ya Jinai.

Kiongozi huyo wa waasi alikwea kukamatwa wakati vibali hivyo vilitolewa kwa kuwa alikuwa afisa mwandamizi jeshini.

Mwaka wa 2006, aliteuliwa kiongozi wa CNDP, kundi lingine la waasi la watu wa kabila la Watutsi lililoongozwa na Laurent Nkunda.


Mapigano nchini Congo yalimalizika kufuatia mkataba wa amani ulioidhinisha waasi hao kuteuliwa kujiunga na jeshi la serikali. Ntaganda naye akateuliwa kuwa generali katika jeshi la serikali na mara tu akaanza kuunda kikosi chake ndani ya serikali.

Kwa mara nyingine tena alifufua mitandao yake na mwaka wa 2012 aliunda kundi la M23, wakati rais Joseph Kabila alipoonyesha ishara kuwa yuko tayari kutekeleza agizo la mahakama ya ICC ya kumkamata na kumuwasisha mbele ya mahakama hiyo.

Umoja wa Mataifa umeishutumu Rwanda kwa kumfadhili Ntagandana kundi lake la M23, madai ambayo yamepingwa vikali na utawala wa rais Paul Kagame.

MBUNGE AUWAWA CAR

Mbunge mmoja wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele kupinga mauaji ya Waislamu nchini humo, ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

Jean-Emmanuel Ndjaroua aliuawa na watu waliokuwa wamejihami kwabunduki waliokuwa wakitumia pikipiki, siku moja tu baada ya kutoa hotuba kulaani mauaji yanayoendelea nchini humo.

Msemaji wa shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch, Peter Bouckaert ameonya kuwa hali nchini humo inaendelea kuwa mbaya kila uchao na raia wotewa nchi hiyo ambao ni Waislamu huenda wakalazimika kutoroka katika kipindi cha wiki chache zijazo.


Maafisa wa kutoa misaada ya kibinadam wamesema kuwa watu tisa wamefariki dunia kufuatia mapigano makali na uporaji uliotokea katika mji mkuu jamuhuriya afrika ya kati wikendi iliyopita.

Ripoti zinasema kuwa watu wawili wanaoaminika kuwa waislamu waliuawa kinyama wakati wa machafuko hayo.

Vita vikali vilitokea siku ya Jumamosi kati ya wanamgambo wa Kikristo na Waislamu Magharibi mwa mji mkuu wa Bangui ambapo majengo kadhaa yaliharibiwa kwa kuteketezwa.

*MAPIGANO YAENDELEA SEHEMU KADHAA

Mkaazi mmoja wa Bangui alisema kuwa mtu mmoja ambaye anatuhumiwa kumuua mama mmoja Mkristu aliuawa na mwili wake kuchomwa na umati nje ya ukumbu wa baraza la mji huo.


Wanamgambo wengine wa Kikristu walimuua mtu Muumini mwengine wa Kiislamu na wakati umati ulipokuwa ukijiandaa kuuteketeza mwili wake, wanajeshi wa Rwanda, ambao ni sehemu ya kikosi cha jeshi la kutunza ambani ya Muungano wa Afrika, MISA walifika mahala hapo na kumpiga risasi.

Watu wengine watano waliuawawa kati hali isiyojulikana.

Peter Bouckaert wa shirika la kutetea haki za kibinaadamu alithibitisha mauaji hayo na kuongeza kuwa mtu mwingine aliuawa kinyama siku ya Jumapili karibu na soko kuu mjini Bangui.

Bwana Bouckaert alisema kuwa majeshi ya Rwanda wamemueleza kuwa hali katika CAR inawakumbusha mauaji ya halaiki iliyotokea nchini mwao miongo miwili iliyopita.


Jamuhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na mapigano kwa karibu mwaka moja sasa tangu kundi la waasi la Seleka lilipomteua Michel Djotodia kuwa rais wa kwanza Muislamu kufuatia mapinduzi ya kijeshi mnamo machi mwaka wa elfu mbili kumi na tatu.

Mapigano hayo yameendelea hata baada ya Djotodia kujiondoa na bunge kumuidhinisha Catherine Samba Panza kuwa kaimu rais wa nchi hiyo mwezi uliopita na waislamu wamekuwa wakitoroka mapigano hayo kwa maelfu.

Afisa huyo mwandamizi wa shirika la kutetea haki za kibinaadamu ameiambia BBC kwamba baada ya siku au majuma machache Waislamu wote wataihama Jamhuri ya Afrika ya Kati.

WALIOCHAGULIWA MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014(SEASON 4)

Baada ya zoezi la kupitia fomu za vijana na wakulima wanawake kutoka nchi nzima, wafuatao wamechaguliwa kwa ajili ya usaili wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula 2014.

Vijana 40 waliochaguliwa watagawanywa katika makundi mawili ya vijana 20. Kundi moja litapelekwa katika kijiji cha awali Iringa na kundi jingine katika kijiji cha awali Zanzibar.

Huko watatakiwa kuishi na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika vijiji hivyo. Mwisho wanakijiji watatakiwa kuwapigia kura ili kupata washiriki 9 kutoka kila kijiji hivyo kuwa na jumla ya vijana 18. Hawa wataungana na wenzao 12 kutoka nchi za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.

Mama shujaa wa chakula 30 watafanyiwa uhakiki 'verification' wataarifa zilizojazwa kwenye fomu, zoezi hilo litaambatana na upigaji picha za mnato pamoja na video na kisha kupigiwa kura kupitia mtandao pamoja na SMS (meseji) ilikupata washiriki 20 ambao wataenda katika kijiji cha Maisha Plus kuungana na vijana.


MAISHA PLUS 2014

1. Adolph Anacleth - Mwanza
2. Agatha Kalesu – Rukwa
3. Ally Thabit - Mwanza
4. Anastazia John – Mara
5. Asumta Mwingira – Dar es salaam
6. Ausi Abdul Moyo – Ruvuma
7. Bakari Khalid – Shinyanga
8. Boniphace Meng'anyi Nyankena – Dar es salaam
9. Charles Daniel – Simiyu
10. Douglas Said Msalu - Arusha
11. Ellymathew Kika – Njombe
12. Elizabeth Joachim - Tabora
13. Fahamni Kaite Mwadini – Zanzibar
14. Farida Ally – Pwani
15. Fadhili Isanga - Kilimanjaro
16. Flora John - Singida
17. Frederick Joseph Ndahani – Singida
18. Hyasinta T. Hokororo - Mtwara
19. Jane Julio Kalinga – Iringa
20. John Sylvester Malima - Geita

21. Joyce Jacob Mushy - Arusha
22. Marriam Mosses - Shinyanga
23. Mary Nicholaus Kavishe – Manyara
24. Mbonimpaye N. Nkoronko – Rukwa
25. Mohammed Selemani Lipemba - Lindi
26. Moureene K. Daud - Kagera
27. Nelson Daniel – Dar es salaam
28. Ngoma Abdallah – Kigoma
29. Osama Norman – Mbeya
30. Otilia Selestin Simime - Mbeya
31. Said Salum – Katavi
32. Salumu Saidi Johari – Mtwara
33. Scholastica Deusidedith – Geita
34. Seif Mohamed Salum - Tabora
35. Shaaban Masoud Shaaban – Zanzibar
36. Shida Keneth Mganga – Dodoma
37. Shishira G. Mnzava - Morogoro
38. Thomas P. Mgazwa – Dodoma
39. Yassini Hamisi Suddi – Dar essalaam
40. Zaharani Yusuph Hossen – Tanga


MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014

1. Amina Kupela Chikaponya – Mtwara
2. Anna James Yuda – Morogoro
3. Anna Mwanilyela Chrisant – Katavi
4. Bahati Muriga –Mwanza
5. Clara Ancilla Ibihya – Pwani
6. Cristina Kurwa Malale – Zanzibar
7. Dina Rusoti – Mara
8. Dionisia Rashidi Karata – Tanga
9. Doricus Msafiri Shumbi – Singida
10. Edina Jamas – Mbeya
11. Elinuru Moses Pallangyo – Arusha
12. Elizabeth Matayo – Geita
13. Elizabeth Simon – Morogoro
14. Ezeleda Chedego – Dodoma
15. Fredina M. Said – Shinyanga
16. Gladness Ebenezery Mmary –Kilimanjaro
17. Grace G.D. Mahumbuka – Kagera
18. Janeth Niima – Manyara
19. Kuruthumu Ramadhani Mwengele – Tanga
20. Leah Dominick Mnyambugwe– Dodoma
21. Mary Athanaz Ndasi – Rukwa
22. Mary John Mwanga – Singida
23. Mary Kessy – Dar es salaam
24. Neema Robert – Simiyu
25. Nyachum Haji Ame – Zanzibar
26. Pendo Musa – Morogoro
27. Santina Mapile – Njombe
28. Thereza Kitinga – Mwanza
29. Zaituni Shedrack Kalenbi – Kigoma
30. Zamda Daniely Mgonganga – Iringa


Tunatoa pongezi kwa wote waliochaguliwa kwa ajili ya usaili. Asanteni na pole kwa wengine wote walioshiriki lakini hawakubahatika.

Tunasikitika hatukuweza kuwachagua wote. Tafadhali jaribuni msimu ujao.

MCHUNGAJI MTIKILA ASISITIZA KWENDA MAHAKAMANI KUDAI TANGANYIKA HURU

*Asisitiza kwenda Mahakamani wiki ijayo, kudai Tanganyika huru LICHA ya kuteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wanaounda Bunge la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameibuka na kubeza uteuzi huo, akidai kuwa kibarua hicho ni sawa na kufanya kazi kama roboti kwa manufaa ya utawala na si ya wananchi.

Kauli ya Mchungaji Mtikila imekuja ikiwa ni siku mbili tu tangu Ikulu itangaze majina ya wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba, linalotarajiwa kuanza vikao vyake Februari 18, mwaka huu, mjini Dodoma.


Akizungumza kwa nyakati tofauti, Mchungaji Mtikila alisema kuteuliwa kwake hakumzuii kudai madai yake ya siku nyingi kuhusu serikali ya Tanganyika na kwamba suluhu anayoiona sasa ni kuundwa kwa serikali ya mpito.

"Hii ni roboti inayokwenda kufanyakazi ya wenye utawala, si kwa manufaa ya wananchi, azima yanguya kwenda mahakamani iko pale pale, kuchaguliwa kwangu hakuizimi, lazima iundwe serikali ya mpito ili tumpate mama yetu Tanganyika," alisisitiza Mchungaji Mtikila.

"Kuteuliwa kuingia katika Bunge la Katiba hakubadilishi mtazamo wangu kwa Watanganyika, huwezi kutafuta hatma ya Watanzania wakati kuna Watanganyika haki zao zinakandamizwa, hili litakuwa Bunge la wendawazimu, kwanza mchakato mzima wa kudai Katiba mpya haukuwa halali, hivyo unatakiwa ushughulikiwe," alisema Mchungaji Mtikila.

Mchungaji Mtikila, ambaye amekuwa na msimamo wa kudai Serikali ya Tanganyika kwa miongo na miongo, alisema mara atakapofika kwenye Bunge hilo katika kikao cha kwanza, atatoa hoja ya kutaka iundwe kwanza Katiba ya Watanganyika na endapo hatosikilizwa, itampa urahisi wa kufungua kesi ya kudai Tanganyika huru.

"Wakikataa hoja hiyo, ina maana dhamira yangu ya kufungua kesi iko pale pale na kesi yenyewe nitaifungua mapema wiki ijayo. Nikishaifungua kesi ina maana mchakato mzima wa Bunge la Katiba utasimama."

Ikumbukwe kuwa tunapozungumzia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenzetu Wazanzibari wao walishajitoa siku nyingi, kwasababu wamefuta kile kipengele cha wao kuwa nchi ndani ya Muungano.

Kwamba wao ni nchi inayojitegemea, nafasi hii niliyoipata nitakwenda kuitumia kutibu wagonjwa, kwasababu ninayo ya kuzungumza. Uteuzi huu umeongeza mafuta katika moto nitakaouwasha juu ya Watanganyika kupata Katiba yao," alisema Mchungaji Mtikila.

Alisema kitendo cha uhuru wa Tanganyika kubatilishwa na kuungana na Wazanzibari hakikubaliki na kinakwenda kinyume na matakwa ya wananchi.

Akisisitiza kuhusu hilo, alisema uhuru ni haki kuu ya watu wote duniani, ambayo ilisababisha kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka 1945 (The right to self determination).


Kutokana na hilo, Mtikila alisisitiza kuwa uhuru wa Watanganyika ni haki ya Watanganyika wenyewe, hivyo wana wajibu wa kuutunza uhai wao katika mipaka ya ardhi kwa utaratibu waliojiwekea kwa kutumia maziwa na asali yao.

Mtikila alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa katika kesi ya madai ya Tanganyika huru, mmoja wa washitakiwa atakuwa ni hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere, kutokana na kuhusika katika kuwapunguzia Watanganyika ubinadamu kwa kulazimishwa kuwa 'watumwa wa Wazanzibari'.


"Tunataka Mahakama ya Kimataifa itupatie haki ya uhuru wetu (The right to self determination of the people of the Republic of Tanganyika) kama binadamu wengine wote katika mipaka ya nchi zao, tunaiambia mahakama yaulimwengu kwamba muungano ni kongwa la utumwa katika Tanganyika," alisema Mchungaji Mtikila.

Mchungaji Mtikila, ambaye ni miongoni mwa wanasiasa waanzilishi wa siasa za mageuzi, mara kadhaa amekuwa akiushambulia utawala wa CCM tangu enzi za hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mpaka sasa chini ya Rais Jakaya Kikwete, anatazamwa kuleta changamoto kubwa ndani ya Bunge hilo, kutokana na hoja yake ya kudai Tanganyika huru.

Mwanasiasa huyo alianza kudai serikali huru ya Tanganyika tangu enzi za utawala wa Hayati MwalimuNyerere, hiyo ikiwa kabla ya kuundwa kwa kundi la wabunge 55, maarufu kama (G55), ambalo lilikuwa na mtazamo kama huo.

Hoja ya kurudisha serikali ya Tanganyika ambayo ilianza kutikisa tangu miaka ya nyuma, inatarajia kujirudia safari hii katika Bunge la Katiba, kutokana na baadhi ya wajumbe kupishana katika maoni yao, hususani kwenye vyama.

Hatua hiyo inatokana na sehemu kubwa ya wabunge na wafuasi wa CCM kutaka muundo wa serikali mbili, huku upande mwingine ukiungana na mapendekezo ya Mwenyekiti wa Tume ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba.

Wengi wanamtazama Mtikila katika kundi linalotaka mfumo wa serikalitatu, lakini mwenye hoja tofauti yakudai kwanza Tanganyika huru, kabla ya mchakato wa kuunda Katiba ya Muungano, jambo ambalo linaweza kuliweka Bunge njia panda, endapo ataamua kung'ang'ania msimamo wake huo.

ANAEDAIWA KUWA JAMBAZI LINALOUWA WATU LAKAMATWA

MTU anayedaiwa kuwa ni jambazi anayeua raia wasiokuwa na hatia katika vijiji mbalimbali Wilaya ya Tarime mkoani Mara, amekamatwa. Muuaji huyo anayetembea na bunduki ya SMG,alikamatwa juzi katika Mkoa wa Tanga, wakati akitoroka baada ya kuua watu 10 wasiokuwa na hatia mwishoni mwa mwezi Januari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime /Rorya, Justus Kamugisha alisema mtu huyo alikuwa akitumia majina mengi kwa ajili ya kumfanya asitambulike haraka na kwa urahisi.Kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha, mtu huyo amekuwa akijitambulisha kwa jina la Charles Range Kichune, Josephat Chacha, Charles Joseph Msong'o (38) mkazi wa Kijiji cha Kenyamanyori Kata ya Turwa wilayani Tarime."

Mtu huyu amekamatwa mkoani Tanga Februari 6 majira ya saa 1:30 jioni. Hata hivyo hakuwa na silaha yoyote ndani ya begi lake la nguo. Takribani raia 10 wameaga dunia kwa kuuawa na mtu huyu, ambaye amekiri kuhusika na matukio hayo yote.

"Baada ya kumweka chini ya ulinzina kuanza kumhoji, ndipo tukagundua kuwa si yeye peke yake anayefanya matukio haya bali wako wengi japokuwa aliyekuwa akifahamika ni yeye tu," alisema.


Kamanda Kamugisha alisema, alipohojiwa zaidi mtu huyo alieleza ilipo silaha anayoitumia na kuwaomba askari kuwapeleka alikokuwa ameificha."Polisi mkoani Tanga waliondoka hadi mkoani Mara, ambapo aliwafikisha kwa jambazi mwenzake aliyemwachia baada yakuona kuwa Jeshi la Polisi limeanza kumtafuta.

"Aliwapeleka maofisa wa Jeshi la Polisi hadi Kijiji cha Bweri Musoma mjini, kwa mwenzake aliyemtaja kwa jina la Marwa Keryoba au Alex anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na38, ambaye ni mkazi wa Sirari akiishi Musoma."

Wakati polisi wanaingia kwa Keryoba, aliwasikia na kutoka nje akiwa amevaa koti refu jeusi kisha kulitupa chini kwa lengo la kupoteza mwonekano wake.

"Hata hivyo polisi walipiga risasi juu kumtaka ajisalimishe, japo alianza mashambulizi kuwashambulia maaskari hao.

"Askari walimuua Keryoba kwa kumpiga risasi baada ya kukaidi amri ya Jeshi la Polisi, lililomtaka ajisalimishe, kwa vile alikuwa amebeba silaha ya SMG iliyokatwa kitako na mtutu huku imefutika namba," alisema Kamugisha na kuongeza:

"Baada ya kumpekua walimkuta akiwa na vitu vifuatavyo, SMG iliyofungwa tochi kwenye mtutu, magazine moja yenye risasi kumi na kwenye nyumba aliyokuwa anaishi marehemu zilipatikana simu mbili za mkononi.

"Vitu vingine ni CD 21 za picha mbalimbali, deki moja, viatu pea mbili aina ya buti, tochi mbili na mpira wa baiskeli pamoja na bidhaa mbalimbali za dukani," alisema.

Kamugisha aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kurahisisha utendaji wa kazi wa chombo hiki chenye dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

WAKANUSHA WABEBA UNGA KUNYONGWA CHINA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imekanusha madai kuwa Watanzania 160 wamenyongwa nchini China baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.

"...habari za uhakika kutoka China zinasema Watanzania wenzetu 160 wamenyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya," ilisema taarifa katika mtandao.

Hata hivyo, Mkubwa alisema hadi kufikia Julai mosi mwaka jana, idadi ya Watanzania waliokuwa wanatuhumiwa kwa makosa hayo huko China ilikuwa 176.

Alisema hata kama ingekuwa wamethibitika kutenda makosa na kuhukumiwa kifo, ingekuwa rahisi watu 160 kunyongwa kwa wakati mmoja.

"Inawezekana huyo anayedaiwa kwamba amefariki na ndugu zake wamepata kibali cha kufanya matanga, amekufa kifo cha kawaida akiwa hajahukumiwa, kwa sababu mtu anapohukumiwa kifo na adhabu kutekelezwa, hakuna utaratibu wa ndugu kupatiwa kibali cha matanga," alisema.

Alisema hata hivyo, Serikali kupitia ubalozi wake nchini China, itafuatilia ili kufahamu kinachoendelea dhidi ya watuhumiwa wa kusafirisha dawa za kulevya nchini humo.

Pia alifafanua kuwa Tanzania haina mkataba na China kuhusu kubadilishana wafungwa, na kwamba watakaotiwa hatiani kwa vyovyote watanyongwa hadi kufa kulingana sheria za nchi hiyo.

ZAIDI YA SIMU 600 ZADAKWA GEREZANI

Zaidi ya simu 600 za mkononi pamoja na takriban laini 5,000 za simu zimenaswa katika gereza la Kamiti Maximum baada ya msako wa kushtukiza uliofanywa chini ya usimamizi mkuu wa gereza hilo.

Naibu ofisa mkuu katika gereza hilo, Patrick Isaboke alisema msakohuo uliodumu kwa siku nne ulifanywa baada ya uchunguzi kubaini kuwepo na ujumbe mwingi wa kutishia raia hutoka magerezani. Isaboke alisema kuwahawakuweza kuwajua wafungwa wanaomiliki simu hizo kwani walitolewa wote ndani ya sehemu wanazoishi ndani ya gereza hilo, kabla ya msako kufanywa.

Msako huo umethibitisha hofu kwamba Gereza la Kamiti linahusika kwa kiasi kikubwa katika visa vya utekaji nyara jijini Nairobi na viungani mwake, kutokana na mawasiliano ambayo yamekuwa yakiendelea baina ya wafungwa waliopo gerezani humo na jamaa au makundii yao yaliyopo uraiani.

Juzi, wafungwa walizua vurugu baada ya msako. Katika vurugu hizo, wale walioitwa kuripoti katikaviwanda vya gereza hilo waligoma na badala yake kuandamana. Walinzi walilazimika kufyatua risasi hewani ili kutuliza vurugu hizo.

Angalau wafungwa wanne walijeruhiwa lakini wasimamizi wa gereza hilo walikataa kutoa taarifa yoyote kuhusu kisa hicho, kwa kuwa taarifa za mambo mengi yanayoendelea ndani ya magereza hufanywa siri.

Taarifa zilieleza kwamba baadhi ya walinzi walizidiwa wakati wa vuruguhizo na ikamlazimu mkuu wa gereza hilo kuwaita walinzi kutoka magereza mengine na wale walio katika Chuo cha Magereza cha Ruiru.

Vyanzo muhimu katika tukio hilo vilikaririwa vikieleza kwamba ofisa mkuu wa Serikali alimwamuru Waziri wa Usalama, Joseph ole Lenku kufanya msako wa kunasa vitu visivyoruhusiwa magerezani baada ya uchunguzi kuhusu kisa chautekaji nyara kuonyesha kuwa kilikuwa kinapangwa gerezani humo.


KUADHIBIWA

Ingawa maofisa hao wanapaswa kuwafanyia msako wafungwa wote, ripoti zinaeleza kuwa baadhi ya walinzi wa gereza wanashirikiana nawafungwa ili kupeleka vitu hivyo haramu gerezani. Duru zinasema kuwa maofisa hao huwauzia wafungwa simu hizo."

Baadhi ya wafungwa hawa adhibiwi wanapokutwa wakiwa wanamiliki vitu haramu kama hivyo, ambavyo kimsingi huwa havitakiwi kabisa kuwepo gerezani.

Kuna viranja ambao ni macho ya walinzi katika kila seli," alisema mlinzi mmoja wacheo cha chini ambaye aliomba asitajwe jina.

Ilielezwa kwamba mara nyingi simuhubebwa na maofisa wakuu ambao huwa hawafanyiwi msako wanapoingia katika taasisi hiyo. Maofisa hao hukabidhi simu hizo kwa walinzi wanaosimamia vitengo tofauti.

WAZIRI WA UHAMIAJI UINGEREZA AJIUZULU

Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.

Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.

Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.

Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadhatu.

DK. MTIKILA, PROF. LIPUMBA NDANI YA BUNGE LA KATIBA MPYA

RAIS Jakaya Kikwete ametangaza wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba kwa mujibu wa sheria, huku akiwajumuisha watu mbalimbali wenye umaarufu katika jamii.

Miongoni mwao wamo wanasiasa maarufu wa sasa na wa zamani, wakiwamo wenyeviti wa vyama vyasiasa nchini pamoja na viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wanahabari.

Katika wanasiasa wamo, aliyewahi kuwa Waziri tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Tadea, Lifa Chipaka, Peter Mziray (APPT-Maendeleo), Dk Emmanuel Makaidi (NLD), James Mapalala, mwanzilishi wa CUF, Christopher Mtikila (DP), Profesa Abdalla Safari kutoka Chadema, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro.

Pia wamo wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Tabora, Hassan Wakasuvi na wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Paul Makonda (Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM), Mwenyekiti wa Wazazi Taifa CCM, Abdallah Bulembo, Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini, Elizabeth Minde, Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, aliyekuwa mbunge na Naibu Waziri, Shamim Khan, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Shaban Muyombo.

Wengine ni ambaye ni Rais wa Chama cha Wakulima Tanzania (AFT), Rashid Yussuf Mchenga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Viajana wa CCM(UVCCM), Sixtus Mapunda, wabunge na mawaziri wa zamani Paul Kimiti(Sumbawanga Mjini) na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga.

Katika uteuzi huo, Rais Kikwete pia amewateua wanahabari wanne, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Zanzibar, Yussuf Omar Chunda, Mhariri wa Mlimani Media, Hamis Dammbaya na Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valerie Msoka.

Aidha, katika uteuzi huo, kundi la viongozi wa dini, Rais amewateua Mussa Kundecha ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Imamu wa Msikiti wa Manyema Dar es Salaam, Hamid Masoud Jongo, Askofu mstaafu wa Kanisa laAnglikana, Donald Mtetemela, Profesa Ricky Costa Mahalu aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

Katika uteuzi huo, yumo mtoto wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk Sengondo Mvungi, Dk Natujwa Mvungi ambaye amepitia kundi la wasomi akitokea Chuo Kikuu cha Bagamoyo sawa na Profesa Mahalu.

Akitangaza uteuzi huo Ikulu Dar es Salaam jana kwa niaba ya Rais Kikwete aliyefanya uteuzi huo kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Florens Turuka, alisema Rais amezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, na katika hilo, kwa kundi la vijana wa miaka 22 hadi 35, ameteua wajumbe 35; miaka 36 hadi 64 wajumbe 145 na wazee, ameteua 21.

Kwa upande wa uwiano wa kijinsia, Dk Turuka alisema Rais ameteua wanawake 100 na wanaume 101. Aidha, alisema watu 118 walijipendekeza wenyewe majina yao, jambo ambalo ni kinyume chasheria huku majina yaliyopendekezwa na makundi na taasisi mbalimbali yalikuwa 3,636.

Bunge Maalumu la Katiba linatarajiwa kukutana kuanzia Februari 18, mwaka huu mjini Dodoma, likiwa na aina tatu wa wajumbe wa Bunge la Katiba ambao ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na wajumbe hao 201 alioteua Rais.

Majina yote kamili haya hapa:


TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)

Magdalena Rwebangira ,Kingunge Ngombale Mwiru, Asha D. Mtwangi, Maria Sarungi Tsehai, Paul Kimiti, Valerie N. Msoka, Fortunate Moses Kabeja, Sixtus Raphael Mapunda, Elizabeth Maro Minde, Happiness Samson Sengi, Evod Herman Mmanda, Godfrey Simbeye, Mary Paul Daffa

TANZANIA ZANZIBAR (7)

Idrissa Kitwana Mustafa, Siti Abbas Ali, Abdalla Abass Omar, Salama Aboud Talib, Juma Bakari Alawi, Salma Hamoud Said, Adila Hilali Vuai


TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)

Tamrina Manzi, Olive Damian Luwena, Shamim Khan, Mchg. Ernest Kadiva, Sheikh Hamid Masoud Jongo, Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela, Magdalena Songora, Hamisi Ally Togwa, Askofu Amos J. Muhagachi, Easter Msambazi, Mussa Yusuf Kundecha, Respa Adam Miguma, Prof. Costa Ricky Mahalu.

TANZANIA ZANZIBAR (7)

Sheikh Thabit Nouman Jongo, Suzana Peter Kunambi, Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu, Fatma Mohammed Hassan, Louis Majaliwa, Yasmin Yusufali E. H alloo, Thuwein Issa Thuwein.


VYAMA VYOTE VYA SIASA VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)

TANZANIA BARA (28)

Hashim Rungwe Spunda, Thomas Magnus Mgoli, Rashid Hashim Mtuta, Shamsa Mwangunga, Yusuf S. Manyanga, Christopher Mtikila, Bertha Ng'angompata, Suzan Marwa, Dominick Abraham Lyamchai, Mbwana Salum Kibanda,Peter Kuga Mziray, Isaac Manjoba Cheyo, Dr. Emmanuel John Makaidi, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Modesta Kizito Ponera, Prof. Abdallah Safari, Salumu Seleman Ally, James Kabalo Mapalala, Mary Oswald Mpangala, Mwaka Lameck Mgimwa, Nancy S. Mrikaria, Nakazael Lukio Tenga, Fahmi Nasoro Dovutwa, CostantineBenjamini Akitanda, Mary Moses Daudi, Magdalena Likwina, John Dustan Lifa Chipaka, Rashid Mohamed Ligania Rai.


TANZANIA ZANZIBAR (14)

Ally Omar Juma, Vuai Ali Vuai, Mwanaidi Othman Twahir, Jamila Abeid Saleh, Mwanamrisho Juma Ahmed, Juma Hamis Faki, Tatu Mabrouk Haji, Fat –Hiya Zahran Salum, Hussein Juma, Zeudi MvanoAbdullahi, Juma Ally Khatibu, Haji Ambar Khamis, Khadija Abdallah Ahmed, Rashid Yussuf Mchenga.


TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA

Dr. Suzan Kolimba, Prof. Esther Daniel Mwaikambo, Dr. Natujwa Mvungi, Prof. Romuald Haule, Dr. Domitila A.R. Bashemera, Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa, Prof. Bernadeta Kilian, Teddy Ladislaus Patrick, Dr. Francis Michael, Prof. Remmy J. Assey, Dr.Tulia Ackson, Dr. Ave Maria Emilius Semakafu, Hamza Mustafa Njozi.

TANZANIA ZANZIBAR (7)

Makame Omar Makame, Fatma Hamid Saleh, Dr. Aley Soud Nassor, Layla Ali Salum, Dkt. Mwinyi Talib Haji, Zeyana Mohamed Haji, Ali Ahmed Uki.


WATU WENYE ULEMAVU- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)Zuhura Musa Lusonge, Frederick Msigala, Amon Anastaz Mpanju, Bure Zahran, Edith Aron Dosha, Vincent Venance Mzena, Shida Salum Mohamed, Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi, Elias Msiba Masamaki, Faustina Jonathan Urassa, Doroth Stephano Malelela,John Josephat Ndumbaro, Ernest Njama Kimaya.

TANZANIA ZANZIBAR (7)

Haidar Hashim Madeweyya, Alli Omar Makame, Adil Mohammed Ali, Mwandawa Khamis Mohammed, Salim Abdalla Salim, Salma Haji Saadat, Mwantatu Mbarak Khamis.


VYAMA VYA WAFANYAKAZI- (WAJUMBE 19)

TANZANIA BARA (13)
Honorata Chitanda, Dr. Angelika Semike, Ezekiah Tom Oluoch, Adelgunda Michael Mgaya, Dotto M. Biteko, Mary Gaspar Makondo, Halfani Shabani Muhogo, Yusufu Omari Singo, Joyce Mwasha, AminaMweta, Mbaraka Hussein Igangula, Aina Shadrack Massawe, Lucas Charles Malunde.

TANZANIA ZANZIBAR (6)

Khamis Mwinyi Mohamed, Jina Hassan Silima, Makame Launi Makame, Asmahany Juma Ali, Mwatoum Khamis Othman, Rihi Haji Ali .


VYAMA VINAVYOWAKILISHA WAFUGAJI-( WAJUMBE 10)

TANZANIA BARA (7)

William Tate Olenasha, Makeresia Pawa, Mabagda Gesura Mwataghu, Doreen Maro, Magret Nyaga, Hamis Mnondwa, Ester Milimba Juma.

TANZANIA ZANZIBAR (3)

Said Abdalla Bakari ,Mashavu Yahya, Zubeir Sufiani Mkanga.


VYAMA VINAVYOWAKILISHA WAVUVI –(WAJUMBE 10)


TANZANIA BARA (7)

Hawa A. Mchafu. Rebecca Masato, Thomas Juma Minyaro, Timtoza Bagambise, Tedy Malulu, Rebecca Bugingo, Omary S. Husseni.

TANZANIA ZANZIBAR (3)

Waziri Rajab, Issa Ameir Suleiman,Mohamed Abdallah Ahmed.


VYAMA VYAWAKULIMA- (WAJUMBE20)


TANZANIA BARA (13)

Agatha Harun Senyagwa, Veronica Sophu, Shaban Suleman Muyombo,Catherine Gabriel Sisuti, Hamisi Hassani Dambaya, Suzy Samson Laizer, Dr. Maselle Zingura Maziku,Abdallah Mashausi, Hadijah MilawoKondo, Rehema Madusa, Reuben R. Matango, Happy Suma, Zainab Bakari Dihenga.


TANZANIA ZANZIBAR (7)

Saleh Moh'd Saleh, Biubwa Yahya Othman, Khamis Mohammed Salum, Khadija Nassor Abdi, FatmaHaji Khamis, Asha Makungu Othman, Asya Filfil Thani.


WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)


TANZANIA BARA (14)

Dr. Christina Mnzava, Paulo Christian Makonda, Jesca Msambatavangu, Julius Mtatiro, Katherin Saruni, Abdallah Majura Bulembo, Hemedi Abdallah Panzi, Dr. Zainab Amir Gama, Hassan Mohamed Wakasuvi, Paulynus Raymond Mtendah, Almasi Athuman Maige, Pamela Simon Massay, Kajubi Diocres Mukajangwa, Kadari Singo.


TANZANIA ZANZIBAR (6)

Yussuf Omar Chunda, Fatma MussaJuma, Prof. Abdul Sheriff ,Amina Abdulkadir Ali, Shaka Hamdu Shaka na Rehema Said Shamte.

MCHUNGAJI AHUKUMIWA KWA UBAKAJI

Kiongozi wa kanisa moja nchini Zimbabwe amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu na kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana.

Kiongozi huyo, Martin Gumbura (57) wa Kanisa la RMG Independent End Time Message alitiwa hatiana katika makosa manne ya ubakaji kwenye mahakama ya mjini Harare. Gumbura ana wake 11 na watoto 30 na aliiambia mahakama kwamba alikuwa akitarajia kupata watoto 100 katika maisha yake.

Wake zake wote walikuwa wakihudhuria mahakamani hapo wakati wa kesi hiyo na walikuwa wakijumuika na watu wengine waliokuwa wakihudhuria makahamani hapo hadi siku hukumu ilipotolewa.

Alihukimiwa kifungo cha mika 50 jela lakini miaka 10 imepungizwa katika adhabu hiyo baada ya kuonyesha tabia njema wakati wa kesi hiyo.

Hukumu nyingine ya kifungo cha miaka minne jela kwa kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana itatumikiwa sambamba na hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 40. Waendesha mashtaka waliiomba mahakama kwamba Gumburu anatakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka 25 jela kwa kila kosa, lakini hakimu alieleza kwamba hana mamlaka ya kutoa hukumu ya kifungo cha muda mrefu namna hiyo.

Hakimu huyo alimwelezea Gumbura kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo ambaye amekuwa akiwaghilibu waumini wa Kanisa hilo.

"Mahakama imejaribu kutoa adhabu ambayo itawatendea haki wote, malalmikiwa na walalamikaji.

Mtuhumiwa hutu ni kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo," alisema.

"Msingi wa huduma ya Kanisa ni kumwabudu Mungu na si kuzini na mabinti na wanawake na kuwatishia kwamba kwa kutofanya hivyo watapatwa na balaa," aliongeza hakimu huyo.

Alisema ni wajibu wa wachungaji nawasimamizi wa kanisa kujua kuhusumadhila yanayowakumba waumini wao, pia kujua udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia unaowakumba wanawake na kutafuta namna ya kuukemea.

Awali Gumbura alikuwa akikabilwia na mashtaka tisa ya kuwalaghai na kuwabaka wanawake sita lakini alifutiwa mashtaka manne yaliyowahusisha wanawake watatu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Hivi karibuni, mtu mwingine mjini Harare alihukumiwa kifungo cha miaka 290 jela kwa kosa la kuwadhalilisha na kuwabaka wanawake 13. Mtu huyo, Thomas Chirembwe (30) alitiwa hatiani kwa makosa 21 ya ubakaji na ujambazi wa kutumia silaha baada ya mfululizo wa matukio yaliyoutikisa mji wa Harare.

Kwa mujibu wa takwimu za polisi, zaidi ta watoto 400 walibakwa na wanawake 392 walinyanyaswa kijinsia mwaka 2013, ambapo wanawake walibakwa wakiwa njiani na watoto wengi walibakwa na majirani au watu wao wa karibu.

MTUHUMIWA AMUUWA ASKARI KWA JIWE

Askari polisi F. 5264 PC Sabato (37) wa Kituo cha Polisi cha Longido, wilayani Monduli, ameuawa kwa kupigwa jiwe na mtuhumiwa aliyekuwa akimpeleka mahabusu katika Gereza la Kisongo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema mauaji hayo yamefanywa na mtuhumiwa aliyekuwa akipelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya kuvunja na kuiba.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, kesihiyo iko katika Mahakama ya Wilayaya Longido.


"Baada ya kufika njia panda ya Gereza la Kisongo, mtuhumiwa alimwomba PC Sabato amfungue mkono ili ajisaidie haja ndogo, lakini alipofunguliwa, ghafla aliokota jiwe na kumpiga askari huyo kwenye paji la uso, akaangukana kuzimia," alisema Kamanda Sabas Kamanda Sabas alisema kwa mujibu wa waendesha bodaboda walioshuhudia tukio hilo, baada ya askari kuanguka chini, mtuhumiwa alitumia pingu aliyokuwa amefungwa mkononi, kuendelea kumshambulia kabla ya kutimua mbio.

Alisema hata hivyo waendesha bodaboda waliamua kumkimbiza nakufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Kamanda huyo alisema kitendo hicho kilifuatiwa na kutoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege na baada ya muda, askari walifika na kumchukua pamoja na majeruhi ambaye hata hivyo, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana, katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

Kwa mujibu wa Sabas, polisi wanaendelea kumhoji mtuhumiwa kabla ya kupandishwa kizimbani kwa shtaka la mauaji.

MTANZANIA MWENYE KESI NA MKE WA RAIS ZUMA HUENDA AKARUDISHWA NCHINI

Mtanzania Stephen Ongolo anayekabiliwa na madai ya kutishia kutoa siri za mke wa Rais Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli (MaNtuli), huenda akarudishwa nchini na kuzuiwa kuitembelea Afrika Kusini milele.Hayo yalisemwa na Mkuu wa Tawi la Uchunguzi wa Kesi, katika Jimbo la Kwa Zulu-Natal, Brigedia CliffordMarion, wakati kesi ya Ongolo ilipokuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya Camperdown, jijini Durban.

Ilielezwa kuwa, Ongolo si raia wa Afrika Kusini na kwamba alirudi nchini humo Januari 19 mwaka huubaada ya kurejea kutoka katika mizunguko yake katika nchi kadhaa za Afrika zikiwamo, Tanzania, Malawi, Msumbiji na Ethiopia.Ilielezwa kuwa visa yake inamalizika Februari 18 mwaka huu.

"Atarudi nchini mwake Tanzania na hatarudi tena Afrika Kusini," alisema Marion.

Chanzo chetu cha habari kilichohudhuria kesi hiyo, kilisema Brigedia Marion alihojiwa kuhusu taarifa za mashtaka dhidi ya Mtanzania huyo ambapo alitoa ushahidi kuwa Ongolo amekuwa akituma ujumbe mfupi kwenye simu ya MaNtuli, akimtishia kuwa atatoa siri kuhusu uhalali wa mtoto wake (MaNtuli).

Inadaiwa kuwa Ongolo katika ujumbe wake alidai kuwa mtoto mmoja wa MaNtuli si wa Rais Zuma.

Kabla ya kukamatwa, Ongolo alikwenda katika vyombo vya habari kadhaa vya nchini humo na kudai kuwa, anafahamu siri nzito kati ya MaNtuli na Phinda Thomo, aliyekuwa mlinzi wa MaNtuli.

Thomo, alikutwa amejiua mwaka 2009 bafuni kwake, lakini Ongolo anadai kuwa Thomo hakuuawa na badala yake, kifo chake kilipangwa kutokana na uhusiano wa siri kati yake na MaNtuli.

Mashtaka ya kutishiwa kuvujisha siri zake, yalitolewa na MaNtuli ambaye alidai kuwa Ongolo amekuwa akimlazimisha kumkutanisha kibiashara na Rais Zuma.

Brigedia Marion alitoa ushuhuda mahakamani na kuiomba mahakama kukataa kutoa dhamana kwa Ongolo ambaye alikamatwa mwishoni mwa Januari mwaka huu.

"Tofauti na inavyoandikwa kwenye magazeti, Ongolo alikamatwa baadaya kufika ofisini kwangu akija kulalamika kuwa kuna kesi ya wizi na uvamizi kwenye nyumba ya dada yake ambayo inasimamiwa vibaya," alisema Brigedia huyo.

Alisema, Ongolo alipofika ofisini hapo alijitambulisha kama Stephen Ongolo lakini baadaye alibainika kama Stephen John Masunga ndipo Marion akalikumbuka jina kwani MaNtuli alikuwa ameshawasilisha mashtaka hayo polisi.

"Kukamatwa kwake ilikuwa ni bahati. Nilipoona jina ni lilelile, nikaangalia namba ya simu niliyopewa na MaNtuli na kuanza kuipiga na simu ya Ongolo ikaita nahapohapo nikamweka chini ya ulinzi," alisema Marion.

Ilidaiwa kuwa baada ya Ongolo kukamatwa, simu yake na hati ya kusafiria vilichukuliwa na alipotakiwa kumpigia simu wakili wake, hakufanya hivyo na badala yake alimpigia simu mwandishi wa habari wa gazeti la Sunday Independent, Nathi Olifant.

Marion alisema, alikusanya ujumbe mfupi kutoka kwenye simu za Ongolo na MaNtuli na kubaini kuwa wawili hao waliwahi kukutana mwaka 2010.

KANISA KATOLIKI LAFIKISHWA KORTINI POLAND

Mwanaume mmoja kutoka Poland aliyedhulumiwa kimapenzi na padri mmoja akiwa mdogo ndiye mtu wa kwanza katika taifa hilo kujitokeza na kudai fidia kutoka kwa kanisa katoliki.

Mwaka uliopita ,Kanisa Katoliki liliwaomba radhi watu wote waliodhulumiwa kimapenzi na mapadri kote ulimwenguni.

Hata hivyo kanisa hilo lilitupilia mbali hoja ya kuwafidia maelfu ya watoto waliodhulumiwa na makasisi na mapadri wa kanisa hilo.

Padri aliyemdhulumu mtu huyo anayefahamika kama, Marcin K ,tayari anatumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Marcin K anaiomba mahakama kitita cha dola elfu sitini na tano za marekani.

Kesi yake ya kutaka fidia imedhaminiwa na mashirika yanayopigania haki za kibinadamu.

Jumatano iliyopita tarehe 5 februari , Umoja wa Mataifa uliishtumu Kanisa katoliki kwa kuendeleza sera ya kuwaficha mapadri na makasisi waliowadhulumu maelfu ya watoto ndani ya kanisa katoliki kote duniani.

MAREKANI NA EU KATIKA MZOZO JUU YA UKRAINE

Tofauti za sera kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya kuhusiana na mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine zimebainika wazi baada ya kuibuka mazungumzo ya siri baina ya maafisa wawili wakuu wakidiplomasia Kiev.

Mazungumzo yanayotajwa kuwa yalinaswa kisiri kati ya wanadiplomasia wawili wakuu wa Marekani wakizungumzia mstakabali wa Ukraine baada ya tandabelua la kisiasa yameiacha marekani ikionekana Mshari.

Katika mazungumzo hayo yaliyonaswa kisiri naibu waziri wawa mambo ya nje wa Marekani, Sauti ya Victoria Nuland, anasikika akimwambia balozi wa Marekani nchini Ukraine, Geoffrey Pyatt, kuwa hamtaki aliyekuwa mwanamasumbwi, Vitali Klitschko katika serikali ijayo badala yake anasikika akisema 'Yats', akiashiria Arseniy Yatsenyuk ndiye anayepaswa kuwa na usemi mkubwa kutokanana tajriba yake kuu ya kiuchumi na Utawala.

''Yats ndiye anayepaswa Kuingia serikalini na afanye mazungumzona Klitschko mara nne kila juma''

Nuland anasikika akiitusi Umoja wa Ulaya na kusema kuwa Umojawa Mataifa ndiyo unaopaswa kuwa na usemi kuhusiana na hali ilivyo Ukraine kwani Kulinga naye' Umoja wa mataifa ndio unapaswa kusaidia makundi ya upinzani kushikamana

Msemaji katika wizara ya mashauri ya kigeni ya marekani Jen Psaki, hakupinga uhalali wa taarifa hizo.

Msemaji wa ikulu ya White House Jay Carney, amesema kuwa taarifa hizo ziliwekwa kwenye mtandao wa Twitter na afisa wa Urusi.

Kashfa hii ya kidiplomasia inatukia baada mshauri mkuu wa Rais Putin kulaumiwa na Marekani kwa kujiingiza katika siasa Ukraine.

Sergei Glazyev ameilaumu Marekani kwa kutoa mamilioni yadola kwa vyama vya upinzani mbali na kuwakabidhi silaha.

Mshauri huyo wa Putin anasemahatua ya Marekani kuingilia maswala ya ndani ya Ukraine kimsingi inaipa Urusi uhuru na haki ya kuingilia kati.

Rais Putin anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake wa Ukraine Viktor Yanukovych wakatiwa michezo ya olympiki ya msimu wa baridi huko in Sochi.

WANANCHI WAFUNGA BARABARA

Wananchi zaidi ya 300 kwa mara nyingine wamefunga barabara eneo la Melela wilayani Mvomero wakiishinikiza Serikali kuwaondoa wafugaji ambao wamekuwa wakiingia kwa wingi na kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kuwapiga.

Kufungwa kwa barabara hiyo kwa takribani saa nne kumesababisha magari zaidi ya 400 kukwama eneo hilo la barabara ya Iringa na Morogoro pamoja na kuleta usumbufu mkubwa kwa abiria waliokuwa wakielekea maeneo mbalimbali nchini.

Sasa imekuwa ni mazoea kwa wakazi wa mkoa wa morogoro kutumia njia hii ya kujichukulia hatua ya kufunga barabara pale wanapohitaji kutatuliwa kero zao.

Katika tukio la leo wananchi hao wameamua kufunga barabara mapema asubuhi wakishinikiza serikali ya wilaya hiyo kuwaondoa wafugaji kwa sababu wanalisha mifugo kwenye mashamba yao nakuwapiga wakulima hali iliyopelekea wakulima hao kufunga barabara kwa kuitaka serikali kuingia kati suala hilo.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo ameelezea kuhusu tukio hilo na kuwaomba wanananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani hinaleta madhara kwa wetu wengine ambao hawausiki na mgogoro huo.

Hii ni mara ya 10 kwa kumbukumbu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita wananchi wamekuwa wakifunga barabara kwa mawe na magogo pale wanaposhinikiza kutatuliwa kwa kero zao hali ambayo husababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hizo.

AAMKA NA KUKUTA AMEKATIKA MIGUU

Mmkazi wa Ludewa, Mkoani NjombeMmkazi wa Ludewa, Mkoani Njombe, Yohana Nkwera (54) anadai kukatika miguu katika hali ya kushangaza.

Yohana anasema katika maisha yake amekuwa ni mwenye hofu kubwa baada ya kukumbwa na tukio hilo la ainayake la kukatika miguu akiwa usingizini. Anasema hadi sasa haelewi namna hasa tukio hilo lilivyomtokea, kwani hakuhisi maumivu yoyote.

Anasema tukio hilo la aina yake lilimtokea mwaka 1992, lakini halikuwahi kuandikwa wala kutangazwa, badala yake ni watu wachache waliokuwa wakilifahamu.

Anasema siku hiyo usiku alikwenda kulala kama ilivyo kawaida, alipoamka asubuhi alikuta miguu yake imekatika.

Kilicho mshangaza zaidi ni kwamba hapakuwa na damu wala jeraha lilionekana. Palionekana pana kovu, kana kwamba alikatika mguu muda mrefu uliopita.

Anasema mara ya kwanza ulianza kupotea mguu wa kulia, hiyo ilikuwa ni mwezi Machi, 1992. Kutokana na tukiohilo, ndugu zangu walifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufanya maombi katika nyumba mbalimbali za ibada, huku wengine wakienda kwa kuwaona waganga wa jadi.

"Kama binadamu wa kawaida ilichukua muda sana kuamini kilichotokea ndani ya maisha yangu na mguu wangu," anasema.

Mwezi mmoja baadaye yaani mwezi Aprili mguu wa kushoto nao ulikatika katika mazingira yaliyo sawa na yale ya awali.

Inaweza kuwa vigumu kuamini lakini ulimwengu ndivyo ulivyo.

Anakumbuka mazingira ya kukatika kwake yanahusishwa na imani za kishirikina kwa sababu siku chache zilizopita kabla ya kukumbana na dhahama hiyo aliwahi kukorofisha na mtu katika vilabu vya pombe za kienyeji anayesadikiwa kufanya tendo hilo.

Baada ya miaka saba kupita Yohana alipelekwa Hospitali Teule ya Ikonda wilayani Makete kupata huduma za tatizo lake. Alifanikiwa kupata msaada wa baiskeli ya magurudumu, ambayo aliitumia kwa miaka mitano.

Kwa sasa baiskeli hiyo haifanyi kazi kutokana na watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi kuiba matairi na vyombo muhimu vinavyoiwezesha baiskeli hiyo kufanya kazi.

Pamoja na kupewa baiskeli hiyo na wasamaria wema, Yohana anakiri pia kuchongewa viatu na hospitali hiyo ambavyo vinamuwezesha angalau kutembea umbali mfupi.

Kutokana na ulemavu huu wa kimiujiza, Yohana anakiri ndoto zake za maisha hazijatimia mpaka leo na inawezekana zikawa zimepotea kabisa.


MIPANGO YAKE

Alipinga mambo mengi yakiwemo kusoma na hata kufungua miradi ya maendeleo. Sasa ni kama anaona haiwezekani tena kwa sababu hana uwezo thabiti wa kufanya kazi; ukizingatia ni kijijini ambako kazi kubwa inayotegemewa kiuchumi ni kilimo cha jembe la mkono.

Ulemavu huo umesababisha ashindwe kuoa, kwani anasema katika ulimwengu wasasa ni ngumu kuoana na mtu kama huna uwezo wa kumhudumia.

Anasema ilikuwa ni ngumu kwa ndugu kuamini kinachotokea lakini anawashukuru wasamaria wema walioendelea kumhudumia mpaka pale alipoikubali hali yake na kuanza kuishi katika huo mfumo mpya wa maisha.

Kwa sasa Yohana anaishi na dada yake mkubwa aitwaye Lucy Nkwera akimsaidia kwa mahitaji ya kila siku ikiwemo chakula na huduma za usafi na usalama kwa jumla.

Akisimulia kwa hisia, Yohana anakumbuka jinsi alivyokuwa katika hali ya uzima wa miguu na kujitegemea, kwamba anashangaa sana kuona leo amekuwa ni mtu wa kuomba msaada; kwa sasa msaada wake mkubwa ni dada yake huyo.

Lucy anasema, "Maisha ni magumu sana kwa kuwa anatakiwa kuwa karibu naye, kwani hakuna mwingine wa kumsaidia."

Mbali na kupata huo ulemavu wa miguu, Yohana anaumwa ugonjwa wa kifafa, ambao nao aliupata baada ya kukatika miguu.

Ugonjwa huu unamfanya kupoteza fahamu mara kwa mara kitendo ambacho ni hatari kwa afya na maisha yake.

Anamshukuru Lucy kwa kuendelea kumhudumia kwa sababu kwa mazingira ya kawaida ni wachache wenye moyo wa huruma kiasi hicho, hasa kumhudumia mgonjwa ambaye hatarajii kupona leo hata kesho.

Anashukuru pia ndugu zake kutoka maeneo mengine akisema kuwa nao wamekuwa wakija kumtaka hali na kumletea vyakula.

Anaishukuru Serikali ya Kijiji cha Ludewa anachoishi, kwa kumkumbuka na kumhudumia kwa kadiri wanavyoweza.

Anasema kama Serikali na ndugu wasingekuwa wanamsaidia, huenda hali yake ingekuwa ngumu zaidi na ilivyo sasa kwani kwa jumla afya yake ni dhaifu.


USHAURI WAKE

Yohana anawaomba watu kuachana na tabia za kunyanyapaa walemavu.

Anasema baada ya kuwa na ulemavu, kuna marafiki zake walimtenga.

"Inauma sana kuona kumbe wengine ni marafiki wa wakati wa raha...Ukiwa na matatizo wanakukimbia, hii tabia si nzuri, ni lazima tuwe na moyo wa kusaidiana wakati wote," anasema Yohana.

Anaongeza kuwa hata yeye hakupenda kuwa katika hali ambayo anayo sasa. Ndiyo kusema kwamba yeyote anaweza kupatwa na lolote kabla ya hajafa, tusinyanyasane.

Chanzo;Mwananchi

ICC KUENDESHA KESI YA KENYATTA?

Pande zinazohusika katika kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC Mjini The Hague zimekuwa na kikao cha kujadili mstakabali wa kesi hiyo.

Kiongozi wa mashtaka wa ICC Fatou Bensouda amekiri kuwa bado hana ushahidi wa kutosha kuwezesha kesi hiyo kuendelea.

Mawakili wanao mwakilisha Rais Kenyatta wanataka kesi hiyo kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007 itupiliwe mbali.

Bensouda amesema kuwa bado kuna maswala yanayozua utata naambayo yanahitaji uchunguzi wa kina.

Mawakili wa Kenyatta wanatuhumu upande wa mashitaka kwa kusisitiza kutaka taarifa kuhusu akaunti ya benki ya Rais Kenyatta kuona ikiwa kuna pesa zozote zilizotolewa kwa lengo la kutumika wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuuwa mwaka 2007/08 Wakili wa waathiriwa mesisitizia mahakama kuwa kutupiliwa mbali kwa kesi kuwakosesha waathiriwa haki. Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi katika siku chache zijazo.


ICC NA AFRIKA

Mataifa ya Afrika yamekuwa yakikosoa ICC kwa kulenga tu viongozi wa Afrika.

Kesi dhidi ya Kenyatta ni muhimukwa ICC ambayo imefanikiwa tu kumhukumu mtu mmoja huku nyingi ya kesi zinazofikishwa katika mahakama hiyo zikitupiliwa mbali kutokana na sababu nyingi tu tangu kubuniwa miaka 11 iliyopita.

Wadadisi wanasema kuwa huendakesi hiyo ikaleta msukosuko katika kanda ya Afrika Mashariki ikiwa viongozi wa mashitaka watasisitiza iendelee.

Rais Kenyatta alifikishwa ICC kutokana na tuhuma kuwa alikuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007/2008. Anakabiliwa na makosa ya mauaji na uhalifu mwingine dhidi ya binadamu.

Kadhalika Kenyatta alishitakiwa pamoja na makamu wake wa RaisWilliam Ruto kwa tuhuma sawa. Kesi dhidi ya Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.

Mataifa ya Magharibi ambayo yanajitolea katika kuunga mkono ICC, pia yana wasiwasi kuhusu uhusiano wao na Kenya ambayo inaonekana kama mshirika mkubwa katika vita dhidi ya kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia.Watu 1,200 walipoteza maisha yao katika ghasia za uchaguzi mkuu mwaka 2007/08 huku maelfu wakilazimika kutoroka makwao. Wote wamekanusha mashitaka.

Viongozi wa mashitaka ICC wanasema kuwa Kenyatta aliongoza ghasia hizo lakini kesi dhidi yake imefanywa dhaifu kutokana na baadhi ya mashahidi kujiondoa katika kesi hiyo tangu kesi hiyo kuwasilishwa katika mahakama hiyo miaka minne iliyopita.

Kesi yenyewe ilitarajiwa kuanza Jumatano, lakini ikaahirishwa kwamara ya nne mwezi jana wakati ambapo wendesha mashitaka waliposema kuwa shahidi mwingine alijiondoa kwenye kesi huku wakiomba mahakama kuwapa muda zaidi kutafuta ushahidi.

Viongozi wa mashitaka wanasemakuwa mashahidi wengi wamehongwa au kutishwa kiasi cha kujiondoa katika kesi hiyo.

UN YABEZA SERA ZA KATOLIKI

Umoja wa mataifa umetuhumu makao makuu ya kanisa katoliki la Vatican kwa kuidhinisha na kutumia sera zilizowezesha mapadre kubaka na kuwalawiti maelfu ya watoto.

Kamati ya umoja wa mataifa ya haki za watoto imesema kanisa hilo linapaswa kuondoa wote wanaokiuka haki za watoto kutokanafasi za uongozi na kuanzisha uchunguzi dhidi yao.

Kamati hiyo imekiri kuwa japo Vatican imeshiriki mazungumzo na kuahidi mageuzi, bado inahitaji kupiga hatua kubwa zaidi.

Mengi yaliyoandikwa katika ripotihii yamekuwa yakiangaziwa na vyombo vya habari. Shutma hizo ni pamoja na kuharibu watoto, kuwapa adhabu kali na kuwatenganisha na wazazi wao.

Umoja wa mataifa unasema uongozi wa kanisa katoliki unapaswa kufanya juhudi zaidi ili kuzuia makosa yaliyowahi kutokea.

Umoja wa mataifa pia umesifia marekebisho yalioyafanywa katika sheria za Vatican lakini umesema kwamba utekelezaji unahitajika kwa kasi.

Kwa upande wake kanisa katoliki limekiri kwamba linahitaji kuhakikisha kwamba sheria zake zinaambatana na sheria za umojawa mataifa kuhusu haki za watoto.

Ripoti hiyo pia imekosoa msimamo wa Kanisa katoliki mapenzi ya jinsia moja,upangaji uzazi na uavyaji mimba.

WACHIMBAJI 17 WAKWAMA MGODINI

Vikosi vya uokozi vimeingia katika mgodi wa dhahabu nchini Afrika Kusini kujaribu kuwaokoa wafanyakazi 17 wa kuchimba mgodi waliokwama mgodini baada ya moto kuzuka.

Kampuni hiyo ya madini Harmony Gold,inasema kuwa moshi uliofuka pomoja na mawe yaliyokuwa yanaanguka yanasemekana kutatiza shughuli ya uokozi.

Kampuni hiyo inasema kuwa imeweza kuwasiliana na wachimba migodi walionaswa.

Kadhalika imesema kuwa imeweza kuwasiliana na wafanyakazi wengine 8 walioweza kujiokoa kutokana na moto uliozuka Jumanne usiku na kutafuta hifadhi katika kituo kimoja kilicho umbali wa mita 1700 chini ya ardhi.

Wachimba migodi tisa bado hawajulikani waliko.

WATOTO SITA WAUWAWA BENGHAZI

Watoto sita wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa nchini Libya baada ya shule yao mjini Benghazi kushambuliwa kwa guruneti.

Maafisa wanasema kuwa gureti hilo lilitupwa mahala watoto hao walipokuwa wakicheza katika shule binafsi eneo la Tabilinu wakati wa mapumziko.

Mji wa Benghazi, umeshuhudia, misururu ya mashambulizi katika mwaka mmoja uliopita, lakini mashambulizi dhidi ya shule sio rahisi kutokea.

Haijulikani nani aliyehusika na shambulizi hilo.

Mkazi mmoja wa Mji wa Benghazi, ameambia BBC kuwa aliona mtu mmoja akitengeza guruneti kwa mdomo wake tayarikwa mashambulizi.

Kisha akaitupa guruneti hiyo shuleni humo kabla ya kutoroka kwa gari moja dogo.

Watu walionekana wakikimbilia usalama wao baada ya shambulizi hilo.

Shambulizi lenyewe lilifanyika kabla ya saa tano asubuhi watoto walipokuwa nje wakicheza.

Afisaa mmoja wa usalama amesema kuwa shambulizi halikuwa na nguvu kubwa, na kuwa polisi wameanza kuwasaka washukiwa.

Mji wa Benghazi ulikuwa kitovu cha harakati za mapinduzi ya kiraia mwaka 2011 ambayo yalimuondoa mamlakani hayati Muammar Gaddafi.

Tangu hapo, mji huo umekuwa ukikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya taasisi za serikali.

MKENYA AENDELEA KUSHIKILIWA DAR

Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, kinaendelea kumshikilia raia wa Kenya, Abdulrahman Salim.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na kete 141 za dawa za kulevya aina ya cocaine, hadi jana zilikuwa zimefikia 142.

Salim alikamatwa Januari 31 mwakahuu saa 7:00 usiku akitokeaa nchiniBrazil, kupitia nchini Ethiopia akiwa amepanda ndege ya Shirika la Ethiopia kuja nchini ili aelekee Mombasa nchini Kenya.

Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Kamanda Alfred Nzowa alisema mtuhumiwa huyo hadi sasa ametoa kete 142 nakwamba, anaendelea kutoa zingine.

Nzowa alisema walipomhoji mtuhumiwa aliwaeleza kuwa, zilizobaki tumboni zinakadiriwa kuwa tatu hadi tano na inadaiwa idadi hiyo inaweza kuzidi.

"Mpaka sasa tunamshikilia huku tukiendelea kumhoji, inavyoonekana zitazidi idadi aliyotaja mtuhumiwa," alisema Nzowa.

Nzowa alisema kuna baadhi ya watuwa mataifa ya nje wanatumia uwanje wa JNIA kupitisha dawa hizo, wanapokamatwa wanaonekana ni Watanzania wakati siyo kweli.

"Hali hii inachafua taswira ya nchiniyetu, kwa sababu watu wengi wanaokamatwa na dawa za kulevya ni wapita njia kutoka mataifa mengine ikiwamo Kenya, Nigeria na Pakistani," alisema Nzowa.

Tayari, baadhi ya watuhumiwa kutoka mataifa hayo wamekamatwa kwenye uwanja huo.

IKULU: RAIS JAKAYA HATO IDHINISHA ONGEZEKO LA POSHO

Ikulu imesema Rais Jakaya Kikwete hatakubali kuidhinisha kama akipelekewa ombi la kuongeza kiinua mgongo cha wabunge kutoka Sh43 milioni hadi Sh160 milioni.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana kuwa Rais Kikwete hajapokea maombi hayo huku akipinga maelezo kuwa Serikali ilishayakubali.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alisema Serikali ilikuwa imepitisha kupandishwa kwa kiwango cha kiinua mgongo kutoka Sh43 milionihadi Sh160 milioni baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitano.

Waziri huyo alikaririwa akisema kuwa kiwango hicho kilipitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na tayari wabunge walishaanza kuchukua fedha hiyo licha ya ukweli kuwa Bunge hili halijamaliza muda wake.

Hata hivyo, Rweyemamu alisema nao wamelisoma suala hilo kwenye magazeti na kwamba halijafika Ofisiya Rais... "Suala hili halijafika Ofisi ya Rais hata kama litaletwa, `I really doubt if the President will endorse such matter' (Nina shaka kama Rais ataidhinisha suala hili)."

Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi tayari imekanusha vikali taarifa za kupandishwa kiwango hicho cha malipo kwa wabunge.

NYOKA WAVULUGA SHUGHULI ZA MAHAKAMA

CHANGAMOTO nyingi za muda mrefu zinazoikabili idara ya mahakama katika wilaya ya Ukerewe, Mwanza sasa zimechukua sura mpya kwa baadhi ya shughuri za mahakama kuvulugwa na Nyoka.

Maelezo ya tukio hilo la aina yake lililoshutua wengi yameelezwa katika siku ya sheria ambayo kiwilaya ilifanyika katika uwanja wa mahakama ya wilaya hiyo mjini Nansio.

Akizungumzia changamoto zinazoikabili idara ya mahakama hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo Bukonyo Malisel Ndimila alisema hali ya uchakavu wa majengo ya mahakama zote katika wilaya hiyo inatisha.

Akifafanua alisema mbali ya changamoto nyingine ikiwemo watumishi wa idara hiyo kutokuwa na nyumba na nyezo za usafiri lakini majengo ya mahakama hasa jengo la mahakama ya mwanzo Bukonyo sasa limegeuka pango la Popo na makazi ya Nyoka.

Katika maelezo yake zaidi Ndimila alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa tangu apelekwe katika mahakama hiyo hapo mwaka jana hadi sasa amenusulika kuumwa na nyoka katika matukio matano tofauti.

Alisema katika matukio hayo Nyoka hao utokea juu ya daliya jengo la mahakama hiyo na uanguka chini wakati mwingine shughuri za mahakama zikiendelea na kusababisha mtafaluku mkubwa.

Akithibitisha tatizo hilo hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyo Faustin Kishenyi alisema mbali ya hali mbaya ya uchakavu wa majengo ya mahakama pia watumishi wote wakiwemo mahakimu wote wanne pamoja na yeye awana nyumba.

Nae Luhasha Rouben aliyekuwa hakimu wa wilaya hiyo kabla ya kustahafu hapo mwaka jana alisema changamoto hizo zinatokana na idara hiyo kutengewa bajeti kidogo isiyokidhi maitaji.

Alisema taarifa zilizopo zinaonyesha kuanzia bajeti ya miaka miwili iliyopita kuludi nyuma idara ya mahakama kwa nchi nzima utengewa fedha isiyozidi bil. 17 kwa mwaka lakini fedha inayopelekwa uwa chini ya kiasi kilichotengwa.

Katika maelezo yake zaidi Luhasha alisema katika mwaka wa fedha wa 2013/014 idara hiyo kwa nchi nzima ilitengewa sh. Bil 42 lakini hadi sasa fedha iliyotolewa ni sh. Bil. 5.5 na kuzitaka mamlaka za juu kuwana mtizamo mpya dhidi ya idara hiyo vinginevyo matatizo yataendelea kubaki kama yalivyo.

Mkuu wa wilaya hiyo Mery Tesha akizungumza baada ya kupokea maelezo hayo amekili kuwa matataizo hayo yanatokana na ufinyu wa bajeti na kutaka wadau mbali mbali kushiliki kutatua.

Hata hivyo alisema serikali anatambua umuimu wa idara hiyo na kuongeza kuwa wakati inakamilisha ujenzi wa mahakama ya mwanzo na kituo cha polisi kwa gharama ya sh. Mil. 250 katika kisiwa cha Ilugwa pia imetenga sh. Mil. 120 kwaajili ya ujenzi wa mahakama ya mwanzo katika kisiwa cha Ukara.

NGONO YA MDOMO YATAJWA KUWA HATARI ZAIDI

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama 'Oral Sex".

Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili, pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.

Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.

Katika utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.

Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono.

Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi,huku wengi wakiwa hawajui athari zake.

Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.

Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.


Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya koo ni ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume nchini, ikiongozwa na ile ya ngozi (Karposi's Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.

Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.

"Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa," anasema Dk Kahesa na kuongeza.

WHO YAONYA WIMBI LA SARATANI

Shirika la Afya duniani WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa saratani kote duniani.

Shirika hilo limesema nusu ya ugonnjwa wa Saratani yanaweza kuzuiwa na kwamba juhudi mpya zinastahili kufanyika ili kukabiliana na tatizo la kunenepakupita kiasi, ulevi na uvutaji sigara.

Watu milioni kumi na nne wanajulishwa kuwa wanaugua saratani kila mwaka, lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia milioni ishirini na nne katika kipindi cha miongo miwili ijayo.

Taasisi ya utafiti wa kimataifa kuhusu ugonjwa wa Saratani katika shirika la WHO lilionya kuwa gharama ya matimabu inaongezeka kwa kiwango ambacho ni vigumu kumudu.

Taasisi hiyo imesema serikali zinahitajika kutekeleza sheria kalizaidi kuhusu matumizi ya pombe na sukari kama vile kuongeza bei na marufuku ya matangazo ya kibiashara ya bidhaa hizo.