DPP APINGA DHAMANA KWA WACHINA

MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amewasilisha hati ya kupinga ombila dhamana ya raia watatu wa China, wanaokabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni 5.4.

Hata hivyo, washitakiwa hao kupitia kwa mawakili Richard Rweyongeza na Edward Chuwa, wamedai hati hiyo haijawasilishwa kwa usahihi kwa kuwa DPP amekosea kutumia sheria.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Hakimu MkaziKisutu, waliwasilisha ombi la dhamana katika Mahakama Kuu wakidai ni haki yao ya msingi. DPP alipinga ombi hilo kwa maslahi ya nchi.

Wakili Rweyongeza alidai kuwa katika hati ya kuzuia dhamana, DPP ametumia Sheria ya Mwenendo wa Mkakosa ya Jinai (CPA) badala ya Uhujumu Uchumi, ambayo ndiyo wanashitakiwa nayo washitakiwa hao pia alipaswa kuliwasilisha baada ya upelelezi kukamilika.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Faraja Nchimbi anayemuwakilisha DPP, alidai Sheria zote zinaweza kutumika na DPP anaruhusiwa kuwasilisha hati hiyo wakati wowote.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili wakati wa usikilizwaji waombi la dhamana hiyo, Jaji Rose Teemba alisema atatoa uamuzi keshokutwa.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Huang Gin (50), Xu Fujie (22) na Chen Jinzhan (31), kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Novemba 9 mwaka huu.

Wakati hayo yakiendelea katika Mahakama Kuu, jana kesi hiyo ilitajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuahirishwa hadi Desemba 30 mwaka huu itakapotajwa tena.

Washitakiwa wanadaiwa Novemba 2 mwaka huu katika eneo la Mikocheni B, walikamatwa na nyara za Serikali ambazo ni vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 vyote vikiwa na thamani ya Sh bilioni 5.4 mali ya Serikali bila kuwa na kibali.

VULUMAI KATIKA FAMILIA YA MANDELA LAFUMUKA UPYA

SIKU mbili baada ya maziko ya Raiswa Kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, ugomvi kati ya watoto na wajukuu wa shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi duniani, umeibuka upya.

Inadaiwa siku chache kabla ya maziko ya Mandela, mjukuu wake mkubwa, Mandla alifukuzwa katika nyumba ya babu yake katika kijiji cha Qunu.

Mbali na kufukuzwa, inadaiwa vitasa vya nyumba hiyo vilibadilishwa na huduma za maji na umeme zilizokuwa zikitumika katika nyumba ya Mandla kijijini hapo, zilisitishwa.

Hata usafiri kwa ajili ya kwenda mazikoni haukutolewa kwa ndugu waliozaliwa pamoja na Mandla na wanasiasa na viongozi wa dini waliokuwa wakishirikiana na mjukuu huyo, walitengwa na wengine kukosa mwaliko wa kuhudhuria maziko ya Jumapili.

Inadaiwa kwamba mtoto mkubwa wa kike wa Mandela, Makaziwe, alimtaka Mandla, ambaye ni Chifu wa Mvezo, kijiji alichozaliwa Mandela, kutoa mifugo yake iliyokuwa katika eneo la nyumba hiyo.

Gazeti la The Times, limebainisha kwamba mjane wa Mandela, Graca Machel na mwanasheria wa siku nyingi wa kiongozi huyo, George Bizos, walijaribu kuwataka wanafamilia hao kudhibiti hali hiyo isijioneshe lakini bila mafanikio.

Kiini Ugomvi huo ulitokana na mgogoro ulioibuka wakati Mandela akiwa mahututi katika Hospitali ya Med Clinic, kuhusu wapi alipaswa kuzikwa kati ya kijiji alichozaliwa cha Mvezo au alichokulia cha Qunu.

Wosia wa Mandela uliofunguliwa akiwa katika hospitali hiyo ya Pretoria, ulieleza wazi kuwa alipenda azikwe karibu na wanawe walikozikwa na kwa wakati huo, makaburi yao yalikuwa Mvezo.

Wanawe hao, Makgato aliyefariki dunia mwaka 2005; Makaziwe, ambaye ni mwanawe wa kike wa kwanza aliyefariki dunia akiwa mchanga mwaka 1948; na Madiba Thembekilea, aliyekufa kwa ajali yagari mwaka 1969; walizikwa Qunu.

Hata hivyo, Mandla, ambaye ni mtoto wa Makgato na kiongozi mkuu wa ukoo wa Madiba, anaotoka Mandela na Mbunge wa ANC, alifukua miili hiyo mwaka 2011 na kuizika upya Mvezo, alikozaliwa babu yake.

Mahakamani Uamuzi huo wa Mandla ambao haukushirikisha familia, ulisababisha watoto wa Mandela, wakiwakilishwa na Mwanasheria, Sandla Zigadla, kwenda mahakamani kutaka mabaki ya ndugu zao, yarudishwe Qunu.Jaji Lusindiso Pakade, alitoa amri kumtaka Mandla aache kuingilia mchakato wa kuhamisha mabaki yamiili hiyo kutoka Mvezo kwenda Qunu.

Mandla alifanya jaribio la kuzuia mchakato huo, lakini Jaji Pakade, alizuia jaribio hilo na badala yake akakazia hukumu kutaka miili hiyo ifukuliwe haraka.

Nguvu yatumika Baada ya hukumu hiyo, huku vyombo vya habari vya Afrika Kusini na kimataifa vikishuhudia, maofisa wa Serikali walivunja lango la makazi ya Mandla kwa vifaa maalumu, ili kutoa nafasi kwa gari la kubeba maiti kuingia ndani yalikokuwa makaburi hayo.

Miili ilifukuliwa na uchunguzi wa kisayansi kufanyika kwa takribani saa mbili na kuthibitisha kwamba ni mabaki ya watoto hao, kabla ya kuzikwa upya Qunu.Juzi, Mandla alisema:

"Kama ilivyo kwa karibu kila mmoja wetu katika familia, kabla ya kifo cha babu, nilidhamiria kutoomboleza, nilijiandaa kusherehekea mazuri yote aliyoniachia na aliyoacha kwa ajili ya ulimwengu.

"Hata hivyo, nilikosea, kwa kuwa maumivu ya kumpoteza tata bila kutarajia, yaliniingia kama vile niliyekatwa nakitu chenye ncha kali."

Mjukuu huyo, alisema alijikuta akiugua upweke siku chache baada ya kifo cha Madiba, pamoja na kuwa karibu na familia.

"Hata hivyo ujumbe wa kututakia faraja ulivyokuwa ukitufikia, nilianza kupona," alisema Mandla. Pia alishukuru Serikali kwa kuandaa masuala yaliyokuwa yakifanyika katika siku hizo 10 za maombolezo na kuongeza kuwa kila kitu kilifanyika vizuri.

WATAKAO SIMAMA KWENYE MAGARI KUPIGWA FAINI

POLISI Kikosi cha Usalama Barabarani, inaandaa sheria itakayosaidia kudhibiti ujazaji wa watu kwenye magari ya abiria, ambayo abiria atakayekutwa amesimama, atatozwa faini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alisema kabla ya sheria hiyo kutungwa na kutekelezwa, watatafuta njia ya kutatua tatizo la usafiri kwanza."

Ni kweli kuna maeneo ambayo kuna tatizo la usafiri, kwa maana hiyo kabla ya sheria hii kuanza kutekelezwa, ni lazima itafutwe dawa ya tatizo la usafiri na baada yahapo ndiyo sheria ianze kutumika," alisema Mpinga.

Akizungumzia usalama katika msimu wa siku kuu za mwishoni mwa mwaka, Kamanda Mpinga alisema matukio ya ajali ya kutisha yametokea ndani ya mwezi huu.

Alitaja ajali ya mkoani Tanga katika eneo la Kwalaguru katika barabara ya Chalinze – Segera, ambako basi la Kampuni ya Burudani lilipinduka na kusababisha vifo vya watu 12 na majeruhi 76.

Pia mkoani Arusha gari aina ya Noah ilisababisha vifo vya watu sita na majeruhi 12, Tanga katika eneo la Segera magari yaligongana na kusababisha vifo vya watu nane na majeruhi 17.

Alitaja pia ajali ya mkoani Dodoma, ambako basi la Kampuni ya Simiyu Express lilipata ajali na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 14."

Haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea kwa mwezi huu wa Desemba, mwaka huu katika mikoa mbalimbali nchini, ambayo yamesababisha majonzi miongoni mwetu na vyanzo vya ajali hizi ni mwendo kasi," alisema.

Chanzo: Habari leo

MTU MMOJA AFARIKI NA WENGINE 19 WAJERUHIWA BAADA YA BUS KUPATA AJARI

Mtu mmoja Beritine Batazal 42 Mkazi wa Kijiji cha Mwese Wilaya ya Mpanda amekufa baada ya basi dogo alilokuwa akisafiria kupinduka baada ya kuacha njia na kusababisha watu wengine 19 kupata majeruhi na kulazwa Hospital.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina Dhahiri Kidavashari ajari hiyo ilihusisha basi dogo aina ya Hino lenye namba za usajiri T 894 APW lililokuwa likiendeshwa na mmiiliki wa gari hilo Dickson Kinyonto ambae alitoroka baada ya kutokea tukio Kidavashari alieleza ajali hiyo ilitokea hapo Desemba 16 majira ya saa sita na nusu mchana katika eneo la Ilembo umbali wa kilimeta tatu kutoka Mpanda mjini barabara ya Mpanda ya kwenda Sumbawanga Mkoa wa Rukwa.

Alisema gari hilo ambalo lilikuwa litikokea Tarafa ya Mpimbwe Wilaya yaMlele likielekea Mpanda mjini lilipata ajali hiyo baada ya taili lambele la upande wa kushoto kupasuka na ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha Beritine na majeruhi 19 ambao wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda na watatu kati yao hari zao sio nzuri.

Kamanda Kidavashari aliwataja majeruhi hao kuwa ni Charles Sokoni 25 mkazi wa mtaa wa Nsemlwa mjini Mpanda ,George Sengeka 48 mkazi wa Mpimbwe, January Damiano 38 mkazi wa mtaa wa Kasimba Ezekiel Benjamin 44 mkazi wa Kashaulili Mpuluku Magobo mkazi wa Ikingwa Saimoni Bala 25 Mkazi wa kata ya KibaoniMajeruhi wengine ni Paul Clement 28 mkazi wa kijiji cha Tinde Lyoba Mengo 36mkazi wa Majimoto E 3170 CPL Albano polisi wa kituo cha Kibaoni Selemani Njala 62 mkazi wa kijiji cha Sosayati Magret Cosmas 29Usinge Justine Michael 17 Bariadi Shinyanga , Cristina Gabriel 60 Stalike Mlele , na Kabura Sahani Majimoto Mpimbwe.

Kidavashari alisema majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na mwili wa marehemu Beritine wamekabidhiwa ndugu zake kwa ajali ya mazishi yatakayofanyika kesho kijijini kwao mwese.

Jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtumiwa dereva wa gari hilo Dickson Kinyonto ambae alitoroka baada ya Tukio ili aweze kufukishwa mahakamani kujibu tuhuma za kusababisha ajali.

CHELSEA WANG'OLEWA CAPITAL ONE

Sunderland imesonga mbele hatua ya nusu fainali ya michuano ya ya Kombe la Capital One baada ya kuichapa Chelsea mabao 2-1.

Chelsea ilimiliki mchezo huo kwamuda mrefu katika dakika zote 90, huku Chelsea ikipata goli kutokana na mchezaji wa Sunderland, Lee Cattermole kujifunga mwenyewe.

Chelsea walionekana kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali hadi dakika za mwisho za mchezo, lakini ndoto hiyo ilizimwa na Fabio Borini aliyesawazisha goli dakika ya 88 na kulazimisha mchezo huo kuingia muda wa ziada.

Sunderland ilipigana na kufanikiwa kupata bao la ushindi katika dakika ya 118 likifungwa na Ki Sung-Yueng.

Muda wa ziada ulizidi kumkoroga kocha wa Chelsea Jose Mourinho, ambaye tayari amekuwa akilalamikia ratiba ya michezo kuibana timu yake, akionyesha kuwa Arsenal ina siku zaidi za kupumzika kulinganisha na wao katika kujiandaa kwa mchezo watakaopambana na Arsenal katika mechi za Ligi Kuu ya England, Jumatatu.

Matokeo mengine ni Manchester City kuichapa Leicester mabao 3-1. Magoli ya ManCity yamefungwa na Kolarov dakika ya8 na Dzeko akifunga katika dakikaza 41 na 53. Bao la kufutia machozi kwa Leicester limetumbukizwa kimiani na Dyerkatika dakika ya 77.

LIVERPOOL WAMUANDALIA SUAREZ MKATABA MNONO

Klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo na wakala wa Luis Suarez kuhusu mkataba mpya ambao utamfanya mshambuliaji huyu wa Uruguay kua mchezajji mwenye mshahara mkubwa kupita wote katika historia ya klabu hiyo.

Mkurugenzi mkuu Ian Ayre alirejea Liverpool kutoka Uhispania siju ya Jumaanne baada ya kufnya mazungumzo na wakala wa Suarez, Pere Guardiola.

Wamiliki wa Liverpool wameidhinisha mkataba huo lakini haijulikani kama Suarez, mwenye umri wa miaka 26, atakubali kuendelea zaidi ya mwaka 2016, wakati mkataba wake utakapomalizika.

Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers alisema hivi karibuni : " Suarez ni mwenye furaha hapa anacheza kwa tabasamu na shauku kubwa.

Mashabiki wanamuenzi na unaweza kuona uhusiano wao nae.."

Huenda ikahitajika mkataba wa karibu pauni £200,000 kwa wiki ikiwa maradufu ya pato lake la sasa kumshawishi kusaini kandarasi mpya. Hata hivyo uhusiano wake na maafisa wakuu wa Anfield umeimarika kwa kiwango kikubwa tangu alipojaribu kulazimisha auzwe Arsenal mwanzoni mwa msimu huu.

Arsenal ilijaribu mara mbili kumnunua Suarez bila mafanikio yoyote.

Lakini pia kumekua na fununu kwamba Real Madrid ya Uhispania nao pia wana hamu ya kumsajili.

MADAKTARI WA SYRIA WAUWAWA SOMALIA

Madktari raia wa Syria na wa jamii ya kisomali wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kufanyika shambulizi karibu na mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia BBC kuwa watu wenye silaha walishambulia gari lililokua likielekea katika hospitali moja.

Walinzi wao wawili pia waliuawa katika shambulio hilo, huku daktari mmoja wa Syria na mwingine wa Somalia walijeruhiwa.

Wanamgambo wa kiislamu, Al Shabaab wamekuwa wakisabisha hali ya usalama kuzorota nchini Somalia, hata hivyo haijathibitika ni nani anayehusika na shambulio hilo.

Madaktari wa Syria wanaelezwa kuwa walikua nchini Somalia kwa ajili ya shughuli za kutoa misaada.

Mwandishi wa BBC ameripoti kuwa shambulio hilo lilitokea katika wilaya ya Siinka Dheer inayodhibitiwa na Serikali, eneo lililo kusini mwa Mogadishu.

Madaktari waliojeruhiwa wako hospitalini wakipatiwa matibabu mjini Mogadishu, halikadhalika miili ya Watu sita waliouawa katika shambulio hilo wamefikishwa hospitalini.

ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS SUDAN KUSINI AKANA JARIBIO LA MAPINDUZI

Aliyekuwa makamu wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar aliyekimbilia mafichoni amekataamadai kuwa amehusika katika jaribio la mapinduzi.

Ameiambia BBC kuwa wa kulaumiwa kwa machafuko yaliyotokea katika mji mkuu wa Juba ni rais Salva Kiir ambaye anadai kuhusika kwake.

Machar ambae alifarakana na Rais Salva Kiir mnamo mwezi wa Julai alimshtumu kwa "kuchochea mapigano ya kikabilai" ili kuficha udhaifu wake.. Rais Kiir amesema kikundi cha wanajeshi wanaomuunga mkono Bwana Machar kilijaribu kutwaa madaraka kwa nguvu usiku wa Jumaapili lakini walishindwa.

Alisema mapigano hayo yalianza pale watu waliovalia mavazi ya kijeshi walipofyatua risasi katika mkuano wa chama kinachotawala cha (SPLM). Lakini Bw Machar aliiambia BBC: "Hakukuwepo jaribio lolote la mapinduzi."

Rais wa baraza la usalama la umoja wa mataifa Gerard Arud amesema kuwa mzozo unaoendelea nchini Sudan Kusini ambao umechukua mrengo wa kikabila unaweza kugeuka na kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bwana Arud ameiambia BBC kwamba umoja wa mataifa umepata habari kwamba mamia ya watu tayari wamepoteza maisha yao tangia jaribio la mapinduzi lifanyike siku ya jumapili, ijapokuwa amesisitiza kuwa sio raia wanaolengwa.

Ameiambia BBC kwamba takriban raia elfu 20 wamepewa hifadhi katika makao ya umoja wa mataifa katika mji wa Juba na kwamba wanakumbwa na uhaba wa chakula na madawa.

AU YAIONYA SUDAN KUSINI NA KUTAKA KUKOMESHA MAPIGANO

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AU, Nkosazana Dlamini-Zuma, ameelezea kusikitishwa na hali ilivyo Sudan Kusini, kufuatia kuzuka kwa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba, siku ya Jumapili.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu na kuchapishwa katika gazeti la Sudan Tribune, mwenyekiti huyo amesema ana wasiwasi hasa na hali ya usalama wa wananchi.

Mapigano yalizuka katika mji wa Juba, Jumapili jioni kati ya vikundi vyenye silaha katika kambi ya jeshi na mapigano hayo yaliripotiwa kuendelea Jumanne, huku milioni ya bunduki ikisikika katika maeneo yote ya mji wa Juba mbali na kuhakikishiwa na serikali ya Sudan Kusini kuwa imedhibiti hali hiyo.

Dlamini-Zuma ameitaka serikali ya Sudan Kusini na makundi mengine yanayohusika katika mapigano hayo kujizua na aina yoyote ya kuendelea kwa mgogoro huo.

Pia amezitaka pande zinazohusika na mgogoro huo kutafuta suluhisho la amani kutokana na tofauti zao, "kwa kuheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu na uhalali wa kikatiba", akisema AU iko tayari kusaidia kutafuta suluhisho la hali ya sasa.

Wito wa AU umekuja wakati Marekani ikizitaka pande zinazohusika katika mgogoro wa Sudan Kusini kujizuia na ghasia nakutafuta suluhisho la amani.

Mjumbe maalum wa Marekani Donald Booth alitumia mawasiliano ya Twitter siku ya Jumatatu akitaka kuwepo kwa haliya utulivu, akisema migogoro ya kisiasa lazima imalizike kwa njia ya mazungumzo na sio vurugu.

Rais Salva Kiir amemshutumu naibu wake wa zamani, Riek Machar, kwa kuchochea jaribio la kutaka kuiangusha serikali yake.

Mawaziri kadha wa zamani wamekamatwa, wakihusishwa na jaribio hilo, ambapo mawaziri wengine hawajulikani walipo.

Bwana Kiir ametangaza amri ya kutotembea ovyo usiku katika mji wa Juba, ambapo maeneo mengi yenye pilikapilika za kibiashara, yamekimbiwa kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, mazingira ya jaribio hilo hayako bayana, huku kukiwa na taarifa zinazokinzana na kauli rasmi ya serikali kuhusu tukio hilo, zikidai kuwa msuguano wa uongozi katika chama tawala, SPLM katika wiki za karibuni ulisambaa hadi katika jeshi, SPLA, na kuchochea mapigano kati ya wafuasi wa Bwana Kiir na Machar.

Jumatatu, walinzi wa rais waliizingira nyumba ya Bwana Machar katika eneo la Amarat, nakuharibu sehemu kubwa ya nyumba hiyo. Hakuwa nyumbani wakati huo na mpaka sasa hajulikani alipo.

Maafisa wa afya wanasema watu wapatao 26 wamethibitika kufariki dunia katika hospitali ya Juba, wakati zaidi ya watu 113 wametibiwa kutokana na majeraha ya risasi.

PICHA ZA MATUKIO KATIKA KIVUKO CHA MV MAGOGONI

Ilikuwa ni mida ya saa nane mchana ambapo Pantoni kubwa ya Mv. Magogoni ikiwa imesheheni abiria ikiwavusha kutokea Posta kuelekea Kigamboni , ilipatwa na wakati mgumu baada ya kushindwa kutia nanga ili iweze kusimama na abiria waweze kushuka.

Tukio hilo ambalo chanzo chake kimetokana na Injini za Pantoni hilo kushindwa kufanya kazi haikuweza kutia nanga kwa muda wote huo.. na ambapo kulikuwa na upepo mkali sana ambao ulisababisha Pantoni hiyo kukosa muelekeo na kuanzakuambaa ambaa mpaka maeneoya Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere kisha kusukumwa zaidi hadi eneo la bandari ya Zanzibar.

Hata hivyo baada ya hali kuzidikuwa si nzuri walilazimika kuita meli ndogo za uokoaji ambapo meli ya kwanza haikuweza kuvuta pantoni hiyo na kulazimika kuongeza meli nyingine ili iweze kuongeza nguvu pamoja na boti za Jeshi lapolisi ambazo zote zilifika na kwa ushirikiano mkubwa ziliweza kufanikiwa zoezi hilo la kuirudisha pantoni hiyo katika eneo lake husika.Na abiria ambao walinusurika kuweza kushuka na kuendelea na shughuli zao za kawaida.


Picha Chanzo: Dar es salaam yetu

MAMA NA WATOTO WAKE WABAKWA NA MAJAMBAZI

Watu wanaokadiriwa kufikia saba wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na mapangana marungu, wamevamia nyumbani kwa mkazi wa kijiji cha Kaduda kata ya Katoro wilayani Geita na kuwabaka kwazamu mama na wanawe watatu kwa zaidi ya saa mbili.Hali kadhalika, watu hao walimjeruhi mmoja wa watoto wake wa kiume aliyekuwa akishuhudia unyama huo ukifanyika.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 15, mwaka huu baada ya kuvamia na kuvunja mlango wa nyumba walimokuwa wamelala wakati baba mwenye mji huo akiwa safarini.

Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Jumanne Faida, alisema baada ya kutekeleza ukatili huo, mama na watoto hao walipiga yowe kuomba msaada.

Faida alisema kuwa watu hao walikuwa wakimbaka mama huyo na wanawe hao wenye umri wa kati ya miaka 14, 10 na 17 kwa kupokezana mbele ya mtoto wa kiume ambaye walimjeruhi kwenye paji la uso kumcharanga kwa panga.

Mganga wa zamu wa Kituo cha Afya cha Katoro, Dk. Daneil Izengo, alithibitisha kuwapokea mama na watoto wake hao kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi na wa kiume kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, hakupatikana kuzungumzia tukio hilo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Omary Mangochie, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema polisi walikuwa hawajamfahamisha rasmi.

Hata hivyo, Mangochie aliahidi kufuatilia ili waliohusika wasakwe na kukamatwa kisha kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.


CHANZO: NIPASHE

MV MAGOGONI YAPOTEZA MUELEKEO

Kivuko kikubwa cha MV Magogoni kinachofanya safari zake kati yaKivukoni na
Kigamboni jijini Dar es Salaam kimekosa muelekeo majini katika bahari ya
Hindi kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya
kazi.
Mpaka sasa abiria wote wameokolewa, na magari kubaki kwanza. Tutaendelea
kuwapa taarifa zaidi

--
Posted By Blogger to Michael M. Mazalla at 12/18/2013 04:35:00 PM

MV MAGOGONI YAPOTEZA MUELEKEO

Kivuko kikubwa cha MV Magogoni kinachofanya safari zake kati yaKivukoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam kimekosa muelekeo majini katika bahari ya Hindi kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya kazi.

Mpaka sasa abiria wote wameokolewa, na magari kubaki kwanza. Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi

MCHAKATO WA KUTAFUTA MWANAMUZIKI BORA WA MKOA WA KATAVI

Hello Ndugu Mwananchi Mpigie kura msanii chipukizi Francis Christopher a.k.a Fc rapper kuwa sanii Bora wa mkoa wa Katavi.

Kumpigia Kura Andika Neno
HBR Acha Nafasi andika FC Rapper tuma kwenda15678 hakuna ukomo wa kupiga kura, Piga mara nyingi uwezavyo. Vigezo na masharti kuzingatiwa

Shindano hili linaendesha na kituo cha radio cha mkoani Katavi Mpanda fm. Ni katika mchango wao kuinua sanaa ya mkoa na Tanzania kiujumla.

MAKAHABA NCHINI KENYA WATAKA USAWA

Makahaba mjini Nairobi Kenya waliungana na wenzao duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga unyanyasaji dhidi yao.

Waliandamana Jumanne kulalamikia kile wanachosema ni unyanyasaji wanaofanyiwa na polisi pamoja na askari wa barazala jiji wakati wakiendesha biashara zao.

Walikusanyika katikati ya mji na kuelekea katika ofisi za baraza la jiji kuwasilisha malalamiko yao wakisema kuwa wamechoka kuhangaishwa na polisi na wanataka ulinzi.

Mwanaharakati wa maswala ya biashara ya ngono, John Mathenge aliyekuwa miongoni mwa waandamanaji, alisema kuwa wengi wao wameuawa na kunyanyaswa hata na wateja wao pamoja na maafisa wa usalama.

Siku hii ya kimataifa, huadhimishwa kila mwaka tarehe17.

Biashara ya ngono imeharamishwa nchini Kenya lakini baadhi ya watetezi wa makahaba wanasema kuwa katiba haijaeleza bayana ikiwa mtu atakayekamatwa akijihusisha na biashara hiyo achukuliwe hatua gani za kisheria.Mathenge alielezea kuwa lazima watu wakome kuwabagua wanaofanya biashara ya ngono, kwani ni kazi kama kazi nyingine tu.

Wengi walilalamika kuwa jamii imepuuza watu wanaofanya biashara ya ngono wala haiwatetei wakati wanaponyanyaswa au kuuawa.

Ripoyi iliyotolewa mwaka jana kuhusu makahaba mjini Nairobi ilisema kuwa wanahangaiswa sana na askari wa baraza la jiji na kuwa wengi wao huachiliwa tu pindi wanapotoa rushwa.

WANAJESHI 66 WAUAWA JUBA

Afisaa mkuu msimamizi wa hospitali ya kijeshi ya Juba, Brigedia Gen Dr Ajak Bullen, ameambia shirika la redio la Miraya mjini Juba kuwa wanajeshi 66 wameuawa katika mapigano ya siku mbili.

Watafanyiwa mazishi ya pamoja.

Wakati huohuo afisaa mmoja wa serikali amesema kuwa raia 26 wameuawa katika mapigano ya siku mbili mjini Juba.

Zaidi ya watu miamoja wamejeruhiwa huku maafisa wakuu wakijaribu kudhibiti mji huo kufuatia kile ambacho serikali ilisema ni jaribio la mapinduzi mbalo liliweza kutibuliwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin amesema kuwa vikosi vya usalama vinawasaka wanajeshi watiifu kwa Riek Machar aliyekuwa makamu wa Rais wa Salva Kiir anayedaiwa kupanga njama hiyo ya mapinduzi.

Taarifa zinasema kuwa milio ya risasi ingali inasikika mjini Juba huku wanasiasa kumi wakikamatwa kuhusiana na njamahiyo ya mapinduzi.

MANGARIBA 38 WAKAMATWA

Afisaa mmoja wa serikali kaskazini mwa Tanzania ameambia BBC kuwa kikundi kikubwa cha watu waliokamatwa kwa kuhusika na ukeketaji wa wasichana mjini Moshi watafikishwa mahakamani Jumatano.

Kamishna wa wilaya katika eneo la Kilimanjaro (Herman Kapufi,) amesema kuwa watu 38 waliokamatwa Jumatatu miongoni mwao ni wazazi wa wasichana waliokuwa wanakeketwa.

Alisema kuwa wasichana waliokeketwa wanapokea matibabu.

Maafisa wakuu mjini Moshi Tanzania, waliwakamata wanawake 38 mnamo siku ya Jumatatu waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.

Haijulikani idadi ya wasichana walioathirika. Lakini ripoti zinasemakuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.

Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini Tanzania , hilo sio jambo la kawaida kutokea mjini Moshi.

Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.Baadhi ya wasichana inaarifiwa badowalikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.

Ukeketaji umeharamishwa nchini Tanzania tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.

Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwanchini humo.

DR. SLAA KURUHUSU GONGO ENDAPO ATAKUWA RAIS

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.

Chanzo:Nipashe

SHAMBULI NDANI YA MATATUU WATANO WADAIWA KUFA

Watu kadhaa wamehofiwa kufariki kufuatia mlipuko uliotokea ndani ya gari moja dogo la abiria katika mtaa wa Pangani mjini Nairobi.

Duru zinaarifu kuwa karibu watu 5 huenda wamefriki katika shambulizi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu 15 waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.

Hata hivyo polisi hawajatangaza idadi rasmi ya watu waliojeruhiwa wala wale waliofariki.

Mlipuko huo umesemekana kutokea ndani ya matatu iliyokuwa inakwenda katika mtaa wa Eastleighambao una idadi kubwa ya wasomali wanaoishi huko.

Athari za mlipuko huo hazikuyasaza magari mengine manne yaliyokuwa karibu na matatu hiyo.

Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliokusanyika katika eneo la shambulizi kujionea yaliyokuwa yanajiri.

SHUGHULI ZA MAZISHI ZAENDELEA QUNU

Mazishi ya Nelson Mandela yanaendelea katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa wa Afrika mwendazake Nelson Mandela.

Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.

Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa

WATU SITA WAMEKUFA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI

WATU sita wakiwemo wanafunzi wawili wamekufa papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa, baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga katika eneo la Pumwani wilayani Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro. Tayari serikali imeyafunga machimbo yote mkoani humo yakiwamo yaliyosababisha vifo hivyo, ili kuepusha athari zaidi kwa wachimbaji wengine, ikizingatiwa kuna mvua za vuli zinazoendelea maeneo mbalimbali nchini.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo la juzi majira ya saa 10.30 jioni wakati wachimbaji hao wakichimba mchanga kwa ajili ya biashara.

Waliofariki wametajwa kuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Ebenezer –Sango, David Macha (18)na Marwa Mwita (14) aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Uparo.

Wanafunzi hao walikuwa wakifanya vibarua vya kuchimba mchanga kwa ajili ya kutafuta fedha za kujikimu pamoja na kusaidia maendeleo ya kitaaluma katika shule walizokuwa wakisoma.

Wengie waliofariki ni Ephraim Assei (27), mkazi wa Kawawa, Ludovick Venance (16), Omari Masoud (33) na Augustine Lyimo (26), wote wakazi wa Pumwani ambao miili yao imehifadhiwa hospitali ya mkoa ya Mawenzi.

Kamanda aliwataja waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi ni dereva wa lori aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 167 AQG, Antipus Babu (56), ambaye alipata majeraha kichwani.

Wengine ni utingo wa lori hilo, Simon Mosha (21), aliyepata majeraha madogo na kutibiwa eneo la tukio huku mtu mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Charles (30), mkazi wa Sango akiwa amejeruhiwa vibaya.

Alisema Charles amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya KCMC.

Kamanda alitoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo yote yanayochimbwa mchanga na moramu kuepuka kufanya kazi hiyo kienyeji, hususani kipindi hiki cha mvua za vuli.Hata hivyo baada ya kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dk Ibrahim Msengi ni miongoni mwa watu waliosaidia zoezi la uopoaji wa miili ya waliokufa.

Gama alitangaza kufungwa kwa machimbo hayo na kutaka wataalamu wa ofisi ya madini Kanda ya Kaskazini waliopo mkoaniArusha kupima eneo hilo iwapo linastahili kuendelea na uchimbaji wa mchanga au la.

Mkuu wa mkoa ambaye aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, alisema pamoja na eneo hilo, lakini pia machimbo mengine yote mkoani humo ikiwamo ya moramu nayo yanasimamishwa hadi yapimwe.

ABILIA WANUSURIKA KUFA BAADA YA NDEGE KUPASUKA MATAIRI, BAADHI MAJERUHI WA AJARI YA BASI WARUHUSIWA

ABIRIA kadhaa akiwemo Waziri Mkuu wa zamani ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, wamenusurika kufa baadaya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Arushauliopo eneo la Kisongo, jana mchana.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR yenye namba PW 0422 ilipata ajali hiyo wakati ikitua. Kutokea kwa ajali hiyo kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas aliyesema ndege hiyo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Arusha.

Kamanda Sabas alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 7 mchana baada ya matairi yake manne ya nyuma kupasuka wakati ikitua katika uwanja mdogo wa ndege wa Kilimo Anga Arusha. "Ajali imetokea majira ya saa saba mchana lakini hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo kwa kuwa ilitua salama," alisema.

Alisema mpaka hivi sasa ndege hiyo ipo katika uwanja huo huku wataalamu mbalimbali wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini sababu ya ndege hiyo kupasuka magurudumu yake yote manne ya nyuma.

Hata hivyo, Kamanda Sabas alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa huenda sababu kubwa ya kupasuka kwa magurudumu hayo ni kutokana na matope yaliyokuwepo katika njia ya kukimbilia ndege kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.

Alisema kwa taarifa hizo za awali alizonazo, hakuweza kupata nambaya ndege hiyo iliyopata ajali wala idadi ya abiria wake kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi yake na kuahidikuitolea ufafanuzi zaidi atakaporejea ofisini.

Majeruhi ajali ya Tanga Wakati hayo yakitokea Arusha, kutoka Tanga Mwandishi Wetu Anna Makange anaripoti kuwa, majeruhi 35 kati ya 93 walionusurika kifo katika ajali ya basi la Kampuni ya Burudani linalosafiri kati ya Korogwe na Dar es Salaam, wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na hali ya afya zao kuonekana inaendelea vizuri.

Majeruhi hao ni wale waliopokelewa juzi kwenye Hospitali ya Magunga iliyoko wilayani Korogwe kutoka kijiji cha Kwalaguru kilichopo wilayani Handeni eneo ilikotokea ajali hiyo iliyosababisha abiria wengine 12 kupoteza maisha papo hapo akiwemo dereva wa basi hilo, Luta Mpenda.

Miili ya marehemu hao iliyokuwa imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Magunga hadi jana mchana tayari ilikuwa imetambuliwa na kuchukuliwa na familia zao kwa ajili ya shughuli za maziko zilizofanyika katika maeneotofauti ya wilaya hiyo ya Korogwe.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Magunga, Dk Aedes John amethibitisha kuruhusiwa kwamajeruhi hao alipozungumza katika mahojiano na wanahabari hospitalini hapo jana mchana.

Alisema majeruhi wengine 15 wamelazimika kuwahamishia katika Hospitali za Rufaa za Bombo(Tanga), KCMC (Moshi) na Taasisi yaMifupa na Mishipa ya Fahamu ya Muhimbili (MOI) kutokana na kupata majeraha makubwa yaliyosababishwa na kuvunjika kwa viungo ikiwemo miguu, mikono na kifua pamoja na kuvuja damu kwa wingi. "Kati ya majeruhi hao tuliowapa rufaa yumo mtoto mdogo mmoja, wanawake wanne pamoja na wanaume 10 na kwamba kati yao waliopelekwa MOI ni watano, hospitali ya Bombo mmoja, majeruhi kumi walihamishiwa KCMC," alisema.Aidha, alibainisha kwamba kuhusu majeruhi wengine waliosalia akiwemo mtoto mmoja wanawake 15 pamoja na wanaume tisa ambao bado wamelazwa katika hospitali hiyo ya Magunga hali ya afya zao imeendelea kuimarika.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa Mkoani Tanga waliozungumzia kwa nyakati tofautitukio la ajali hiyo walimtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Costantine Massawe kuwawajibisha askari wa usalama barabarani waliokuwa zamu jana katika vituo vya ukaguzi vya askari barabarani vilivyopo kati ya Korogwe na eneo la ajali, kwani waliruhusu basi hilo kuendelea na safari licha ya kujaza abiria kupitia kiasi.

Simiyu Express nalo laua Mwandishi wetu Sifa Lubasi kutoka Dodoma anaripoti kuwa, siku moja baada ya ajali ya basi la Burudani mkoani Tanga, basi jingine la Simiyu Express limeua abiria wawili na kujeruhi wengine 14 baada ya basi hilo kupinduka katikaeneo la Ihumwa nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma.

Basi hilo lenye namba za usajili T 717 ANL aina ya Scania lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la MrambaIssa (31).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Susan Kaganda, alisema kuwa basi hilo lilikuwa linatokea Bariadi kwenda Dar es Salaam likiwa na abiria 60 liliacha njia na kupinduka kutokana na mwendo kasi.

Kamanda alisema kwamba ajali hiyo ilitokea jana alfajiri majira ya saa tisa katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam eneo la Elshadai. Kamanda Kaganda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na dereva wa basi hilo Mramba Issa mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam na FloraErnest (21) Mwalimu wa shule ya msingi Mwamoto Kolokolo, Bariadi.

Aidha kamanda akizungumzia zaidi ajali hiyo alisema kwamba basi hilolilikuwa likiwakwepa askari wa barabarani kwa kupita njia za panya.

Alifafanua kuwa kwa basi hilo kusafiri usiku huo ni kukwepa askari.

Aliwataka pia wamiliki wa magari kuweka madereva wawili kwa magari ya masafa marefu na pia wazingatie sheria za barabarani.


Chanzo: Habari leo

MJOMBA WA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI ANYONGWA

Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, limetangaza kuwa Jang Song-thaek, mtu mwenye nguvu kisiasa nchini humo na ambaye ni mjomba wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, amenyongwa.

Shirika hilo limesema Jang alituhumiwa kutumia vibaya madaraka, kupinga vitendo vya kiwana mapinduzi na kukengeuka kitabia.

Bwana Jang alihukumiwa na mahakama maalum ya kijeshi na kunyongwa papo hapo kama msaliti.

Mapema wiki hii, picha za televisheni zilimwoonyesha Jang Song Thaek akiondolewa na walinzi wenye kuvalia sare kutoka katika mkutano wa Chama tawala cha Kikomunisti.

Wachambuzi wa mambo wanaona kunyongwa kwake kama jaribio la kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un kujiimarisha kiutawala.

Ni tukio kubwa kutokea tangu Bwana Kim amrithi baba yake, Kim Jong-Il miaka miwili iliyopita.

Shirika la habari la Korea Kaskazini, limesema Jang alikiri makosa katika mahakama ya kijeshi Alhamisi, kutaka kuiangusha serikali, na alinyongwa mara moja.

Bwana Jang, ambaye anafikirika kumjenga mpwa wake, wakati wa kipindi cha mpito wa uongozi kutoka kwa Bwana Kim Jong-il kwenda kwa mtoto wake Kim Jong-un mwaka 2011, "alikuwa mbaya kuliko mbwa" limesema shirika hilo.

Alikiri kutumia vibaya nafasi zake zauwajibikaji ili kuunda kikundi cha upinzani dhidi ya serikali na kulinda maslahi yake ya kisiasa, imesema taarifa ya shirika hilo la KCNA.

Kim Jong-un kiongozi wa Korea Kaskazini Nchini Marekani.

Ikulu ya nchi hiyo, imesema haiwezi kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo, "lakini halinasababu za kutilia mashaka taarifa hizo" "Kama itathibitika kuwa kweli, huu ni mfano mwingine wa ukatili uliopita kiasi, unaoendeshwa na utawala wa Korea Kaskazini.

Tunafuatilia kwa karibu zaidi taarifa hizo na kushauriana na nchi washirika na marafiki katika eneo hilo.," imesema taarifa ya Ikulu ya Marekani.

Picha ya Bwana Jang akiwa mahakamani, mikono yake ikiwa imefungwa, imetolewa Ijumaa.

Kabla ya kutoweka kwa neema yake, mara kwa mara alipigwa picha akiwa pembeni mwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye amesema Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha "utawala wa hofu" Bwana Jang Song-thaek aliyemuoa dada wa kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini Kim Jong-il ambaye ni baba wa kiongozi wa sasa Kim Jong-un alijiunga na chama cha Kikomunisti mwaka 1972 na kupanda ngazi za uongozi katika chama hicho na pia akipanda ngazi ya juu kijeshi chini ya kiongozi Kim Jong-un.

SERIKALI YA DRC NA M23 WASAINI MKATABA WA AMANI

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hatimaye imesaini mkataba wa amani na waasi wa kundi la M23 waliokuwa wakifanya mashambulio ya mara kwa mara mashariki mwa nchi hiyo.

Waasi wa M23 walijilsalimisha mwezi uliopita baada ya kushindwa katika oparesheni iliyoendeshwa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo ikisaidiwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa.

Alhamisi, maraisYuweri Museveni, ambaye ndiye mwenyekiti wa kongamano la kimataifa juu ya usalama katika maziwa makuu, na Joyce Banda, raiswa Malawi, ambaye ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC, walisaini kama wadhamini wamkataba huo.

Marais hao walisaini mkataba huo wakiwa jijini Nairobi walikohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Kenya.

Makubaliano

>Kundi la M23 limeweka rasmi katika mkataba huo kuwa watasitisha maasi yote na kulivunja kundi lao kama vugu vugu la waasi na badala yake kusukuma ajenda zake kupitia njia za kisiasa.

>Serikali ya Congo nayo imeweka masharti ya kutolewa msamaha kwa waasi hao na mpango wa kupokonywa silaha wote wanaojisalimisha kutoka kwa kundi hilo.

>Serikali hiyo pia imekataa kuwa jumuisha kijumla waasi wote waliojiondoa kutoka M23, katika jeshi lake.

Safari ndefu

Juhudi za awali kutafuta amani kati ya serikali ya DRC na waasi hao wa M23 zilishindikana.
Mwaka mzima baadaye, licha ya kuandikwa mkataba huo, pande mbili zilikataa kusaini kutokana na kushindwa kukubaliana jina litakalopewa. Upande wa serikali ya DRC ulisisitiza kuwa hakuna mkataba wa amani na waasi, hasa baada ya kuwa wamewashinda vitani.

Tangu kupigwa na kufukuzwa kwa waasi hao kutoka mkoa wa Kivu ya kaskazini, waasi hao wa M23 wamekuwa wakijisalimisha kwa serikali ya Uganda na kuomba hifadhi. Serikali ya DRC imetaka warudishwe nchini humo ili wakabiliwe na mashtaka ya mauaji, ubakaji na uhalifu mwinigne wa kivita. Hata hivyo Uganda imekataa kuwakabidhi ikisema kuwa ni wakimbizi wanaosubiri uamuzi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi, UNHCR.

Hadi sasa amani imeanza kurejea katika maeneo yaliyokombolewa kutoka mikono ya waasi wa M23.

Hata hivyo mwandishi wa BBC katika eneo hilo Lubunga Bya Ombe, anasema kuwa bado serikali hiyo ya DRC ina kibarua kigumu kukabili makundi mengine madogo ya waasi yaliyo kita kambi katika eneo hilo.

Wiki hii serikali ya DRC ikishirikiana na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa imetangaza oparesheni mpya dhidi ya Kundi la waasi la FDLR.

Masuala tete

Lakini masuala mengine yamesalia bila kutatuliwa. Mfano, bado haijulikani serikali ya DRC itachukua hatua gani kwa baadhi ya viongozi wa Kundi hilo la M23, ambao hawapati msamaha kutokana na kuwa wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji, ubakaji na uhalifu wa kivita.Viongozi hao wameorodheshwa katika orodha ya jamii ya kimataifa ya wahalifu wa kivita.

Miongoni mwa viongozi wa kundi hilo ambao hawajapewa msamaha ni aliyekuwa kiongozi wao Askofu Runiga, Brg. Jenerali Bouduain Ngaruye na Kanali Sultan Makenga na wengineo Pia haijabainaka wazi hatma ya zaidiya waasi wa zamani 1500 wa M23 waliojisalimisha nchini Uganda iwapo watarudi Congo au la.

KIONGOZI WA UPINZANI RWANDA AHUKUMIWA MIAKA 15 JELA

Mahakama ya juu zaidi nchini Rwanda imeendeleza hukumu ya kwanza aliyopewa kiongozi wa upinzani nchini humo Victoire Ingabire na kuiongeza kutoka miaka 8 hadi 15.

Awali mwezi Oktoba, bi Ingabire ambaye ni wa asili ya ki Hutu alipatikana na hatia ya ugaidi, na kukana kutokea mauaji ya kimbari dhidi ya kabila la wa Tutsi.

Mauaji hayo yalifanyika mwaka wa 94 ambapo zaidi ya watu 800 wa kabila la wa Tutsi waliuawa.

Bi Ingabire alikata rufaa dhidi ya hukumu ya awali aliyopewa japo upande wa mashtaka nao ulitaka aongezewe hukumu hiyo na hata kupendekeza apewe hukumu ya maisha gerezani.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeshutumu namna kesi ya Bi Ingabire imeendeshwa.

Bi Ingabire amekumbwa na matatizo na sheria ya Rwanda baadaya kurejea nchini humo mwaka wa 2009, kutoka Uholanzi alikoishi kwa miaka kadhaa.

Alieleza wazi nia yake kuwania urais nchini humo lakini hakupata fursa kwani punde tu alipowasili alifunguliwa mashtakahayo.

Kutokana na kujivuta kwa kesi yake, hakushiriki uchaguzi uliofuata wa mwaka wa 2010. Tangu wakati huo, amekuwa kizuizini.

Amekuwa akiwakilishwa na wakili kutoka Uingereza.

WEZI WAVUNJA NYUMBANI KWA DESMOND TUTU

Wezi wamevunja na kuingia nyumbani kwa Askofu mstaafu Desmond Tutu.

Polisi wamesema wizi huo ulifanyika wakati bwana Tutu akiwa katika ibada ya Nelson Mandela Mjini Johannesberg.

Inaarifiwa Tutu aliibiwa vitu vyake wakati akiwa anahudhuria ibada maalum ya kumuaga Hayati Nelson Mandela siku ya Jumanne.

Aidha wameelezea kuwa uvamizi ulifanyika nyumbani kwake mjini Cape Town Ahamisi jioni baada ya kutoa hotuba katika ibada ya Mandela siku hiyo.

Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa FNB mtaani Soweto.

Wizi na uvamizi wa nyumba za watu ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini ambako visa vya uhalifu viko juu sana.

WAASI 19 WA LRA WAKAMATWA

Jeshi la Uganda linadai kuwa limewakamata waasi 19 na kumuua kamanda mmoja kwa jina Kanali Samuel Kangul.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, msemaji wa jeshi la Uganda Luteni Kanali Paddy Ankunda, amesema kuwa waasi hao kumi na tisa waliokuwa wanaongozwa na kamanda Obur Nyeko walijisalimisha pamoja na bunduki 9aina ya SMG.

Ankunda amesema kuwa wote waliojisalimisha ni raia wa Uganda wakiwemo watoto 6 waliokuwa wanatumika kama wapiganaji wa kundi la LRA.

Jeshi la Uganda likishirikiana na kikosi cha Muungano wa Afrika, wamekuwa wakiendesha harakati zakuwasaka waasi wa LRA baadhi yao wakiwa wanatakiwa na mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC kama kiongozi wao Joseph Kony.

Bwana Ankunda amenukuliwa akisema kuwa jeshi la Uganda litaendelea kuwapokea waasi wanaoasi vita.

''Tukiendelea kufanya kazi kuambatana na sheria za kimataifa tuko tayari kuwapokea waasi wote wanaorejea nyumbani,'' alisema Ankunda.

BIBI KIZEE AULIWA KIKATILI HUKO KIGOGO

Bibi kizee ameuliwa kikatili kwa kukatwa vibaya na mapanga Kigogo
Bibi kizee mmoja mwenye umri wa mika 65 ameuawa kikatili kwa kukatwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kusababisha kifo chake katika eneo la Kigogo Mburahati national housing jijini Dar es Salaam.

Kutokana na tukio hilo la kikatili aliofanyiwa bibi huyo kizee aliyefahamika kwa jina na Bi Asia Mohamed maarufu kwa jina la bibi Chadego, ITV ilifika nyumbani kwa bibi huyo mwenye umri wa miaka 65 na kuzungumza na mjumbe wa eneo hilo bi Hidaya Salum na kusema bibi huyo ameuawa kikatili akiwa nyumbani kwake huku mtoto wa marehemu naye akieleza kusikitishwa na kifo cha mama yake.

Baadhi ya wasamaria wema ambao hawakutaka kutaja majina yao kwa usalama wao.

Wamesema bibi huyo alikuwa akihusishwa na mambo ya ushirikina na baadhi ya familia yake baada ya vifo vya wajukuu wake watatu ambao walifariki kwa nyakati tofauti kipindi cha nyuma ambao licha ya kudaiwa wajukuu hao kufariki kwa mambo ya kishirikina lakini ukweli ni kwamba bibi huyo hakuwa mchawi wala hakuhusika na vifo hivyo huku ikidaiwa kwamba bibi huyo hakuuawa na mjukuu wake kama inavyodaiwa ila kuna mchezo uliochezwa na watu fulani ili kumuua na kisha kugeuza kuwa ni mjukuu wake mwenye tatizo la akili.

Kamishna msaidizi wa polisi kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni ACP Camilius Wambura, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba licha ya mjukuu wa bibi huyo kushikiliwa na jeshi la polisi kwa madai ya upotevu wa godoro lakini upepelezi wa uhakika bado unaendelea kuhusu tukio hilo hivyo wananchi wameombwa kutoa ushirikiano ambapo pia mganga mkuu wa hospitali ya mwananyamala dakta Sophinias ngonyani amekiri mwili wa marehemu kuhifadhiwa katika hospitali hiyo.

Chanzo:ITV

WATU WAWILI WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUKANYAGWA NA TEMBO

Watu wawili wamekanyagwa na tembo na kupoteza maisha katika kitongoji cha Nyampindi wilayani Uyui mkoani Tabora, huku familia tisa zikikabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na akiba yao kuliwa na wanyama hao, kutokana na kile kilichodaiwa kuwa wananchi wanalima na kuishi katika njia za tembo hao.

Hayo yamebainishwa na mtendaji wa kijiji cha Songambele kata ya miyenze wilayani Uyui mkoani Tabora Bi Malieta Makenga wakati akitoa taarifa kwa mwenyekiti wa umoja wa wabunge wanaojihusisha na uhifadhi wa mazingira na wanyamapoli, tembo na faru pamoja na vyanzovya maji waliokwekuwa katika kukagua hali ya uhalibifu wa mazingira, katika mikoa ya Lindi, Rukwa Katavi na Tabora.

Akizungumza na wananchi waliokumbwa na adha hiyo katika kijiji cha Songambele, mwenyekiti wa umoja huo Mhe. Riziki Saidi Ruliga, mbunge viti maalum CCM mkoa wa Lindi, amesema kuwa pamoja na kuwepo uharibifu mkubwa wa mazingira, ameitaka serikali kuanzisha rasmi tume ya haki za wanyama, kwa lengo la kuhifadhiwanyama hao.

Aidha akizungumzia fursa za wananchi katika kupambana na mauaji ya wanyama ambao ni rasilimali za taifa, makamu mwenyekiti wa umoja huo mbunge wa jimbo la Igarula Mhe. Mhandisi Dk Athumani Mfutakamba amewataka wananchi kwa pamoja kuwa na mshikamano wa kuchukia vitendo vya ujangili, vinavyofanywa na baadhi ya watuna kutoa taarifa za siri ili watiwe mbaloni.

Source:ITV

MAELFU WAJITOKEZA KUMUAGA MANDELA

Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia watakaohutubia muhadhara huo.

Viongozi hao pia watahutubia wananchi sawa na wajukuu wanne wa Mandela.

Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB.

Afrika Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili.

Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.

Viongozi wanaohudhuria misa ya wafu ya Mandela
Rais wa Marekani Barack Obama
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
Rais wa Cuba Raul Castro
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
Rais wa Brazil Dilma Rousseff
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Watu wengi wamekaidi hali mbaya ya hewa ambapo mvua kubwa imenyesha huku wakikusanyika uwanjani humo wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya misa hiyo kuanza muda mfupi uliopita.

Waliohudhuria misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.

Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani.

Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu.

Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.

LIBYA KUKAGULIWA KIWANGO CHA URANIUMU

Hali ya wasiwasi imetokana na utovu wa usalama Libya, Umoja wa Mataifa umesema wakaguzi wa silaha za nyuklia watatembelea Libya kukagua kiasi cha madini ya Uranium,kilichohifadhiwa nchini humo, wakati huu kukiwa na wasiwasi wa hali ya usalama nchini Libya.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Tarek Mitri, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa timu ya shirika la kimataifa la nguvu za nyuklia,IAEA, litawasili nchini humo baadaye mwezi huu.

Amesema mapipa 6,400 ya malighafi ya Uranium, maarufu kama keki ya manjano, yalihifadhiwa katika kambi ya zamani ya kijeshi kusini mwa Libya, yakilindwa na kikosi cha jeshi.

Mali ghafi hiyo inatumika katika uzalishaji wa nishati na silaha za nyuklia.

Bwana Mitri, mwakilishi maalum waKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, amesema timu ya wakaguzi kutoka IAEA watatembelea Libya mwezi huu kuthibitisha kiasi cha nyuklia kilichohifadhiwa na hali ya sehemu ilipohifadhiwa katika kambi ya zamani ya kijeshi karibu na mji wa Sabha, kusini mwa Libya. "Malighafi hiyo ya nyuklia inadhibitiwa na kikosi cha jeshi" amesema.

Wataalam kutoka IAEA walitembelea eneo la Sabha mwaka2011, muda mfupi baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya.

Bwana Mitri alikuwa akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati huu ambapo wasiwasi umekuwa ukiongezeka juu ya serikali ya Libya kushindwa kudhibiti vikundi vya wapiganaji ambavyo vimepata ushswishi na udhibiti katika miji muhimu tangu kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.

ABU QATADA AKANA MASHTAKA YA UGAIDI

Mhubiri matata wa kidini, Abu Qatada amekana mashtaka ya ugaidi yanayomkabili aliposomewa katika mahakama moja nchini Jordan.

Mtuhumiwa huyo Mpalestina, Mjordan alihukumiwa bila kuwepo mahakamani kwa kuhusika na shambulio la kigaidi la mwaka 1998 na kula njama ya kufanya shambuliola kigaidi mwaka 2000, lakini sasa amesomewa upya makosa hayo.

Jitihada zake za miaka minane kutaka kubakia Uingereza, zilimalizika mwezi Julai mwaka huu aliporejeshwa nchini Jordan ili akakabiliane na mashitaka hayo.

Ameiambia mahakama kuwa Jordanimevunja makubaliano na Uingereza kwamba angepewa nafuukatika mashitaka yake kwa sababu mmoja wa majaji walioteuliwa kusikiliza kesi hiyo ni kutoka jeshini. "mahakama imekiuka masharti yaliyonifikisha hapa," amesema.

"nataka haki yangu- Siitambui mahakama hii.

"'msingi wa kukiuka mkataba'Wakati Abu Qatada akipinga kuondolewa nchini Uingereza, serikali ya Jordan aliwahahakikishia mawaziri kuwa kesi yake ingesikilizwa na majaji wa kiraia pekee.

Japokuwa Abu Qatada alihukumiwa kifungo cha maisha siku za nyuma bila kuwepo mahakamani, lakini kwa mujibu wa sheria za Jordan anaweza kushitakiwa upya kwa makosa hayo akiwepo mahakamani.

Abu Qatada alipewa hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza mwaka 1994 lakini alipogundulika kuwa msimamo wake unazidi kuwa mkali, vyombo vya usalama vilimwona kuwa mtu hatari na kutakiwa kuondolewa nchini humo.

WANAJESHI WAWILI WA UFARANSA WAUWAWA AFRIKA YA KATI

Wanajeshi wawili wa Ufaransa wameuawa katika mapigano katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande"amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa" kwamba askari hao waliuawa usiku mjini Bangui.

Hivyo ni vifo vya kwanza kwa askari wa Ufaransa kuuawa tangu Ufaransa itume askari wake 1,600 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wiki iliyopita wakiwa katika operesheni ya kijeshi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa katika ghasia tangu kiongozi wa waasi Michel Djotodia amtimue madarakani Rais Francois Bozize mwezi Machi mwaka huu.Akajitangazia madaraka kama kiongozi wa kwanza wa Kiislam nchini humo ambao idadi kubwa ya wananchi ni Wakristo na hivyo kuchochea umwagaji damu kwa miezi kadhaa kati ya wapiganaji wa Kiislam na Wakristo.

Spika wa bunge la Ufaransa Claude Bartolone, amewaambia waandishi wa habari kwamba askari hao wa kikosi cha anga walipata ajali ya ndege karibu na uwanja wa Bangui.

"Walijeruhiwa na haraka kupelekwa kituo cha upasuaji, lakini kwa bahati mbaya walipoteza maisha," amesema.

Taarifa kutoka ofisi ya Rais Hollande imesema askari hao walipoteza maisha yaoili kulinda maisha ya watu wengine".

"Rais ameelezea shukrani zake kwa askari hao wawili waliojitolea maisha yao na ameelezea imani yake kamili kwa vikosi vya Ufaransa vilivyoko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ya kulinda amani nchini humo, katika kuwalinda watu na kuhakikisha misaada ya kibinadamu," taarifa hiyo imesema.

Mapigano kati ya Wakristo na waasi wa Kiislam wa Seleka yamesababisha vifo vya watu wengi.

Kundi la Wakristo walishambulia msikiti mjini Bangui Jumanne.

Rais Hollande amehudhuria ibada ya kumwombea marehemu Nelson Mandela, nchini Afrika Kusini na anatarajiwa baadaye Jumanne kuelekea mjini Bangui, Jamhuri yaAfrika ya Kati.

Mwandishi wa BBC,Thomas Fessy katika mjiwa kaskazini wa Bossangoa amesema vikosivya Ufaransa, pamoja na vile vya kulinda amani vya Afrika - Jumatatu, walifanya operesheni ya kuwapokonya silaha wanamgambo na wapiganaji wa Kiislam ambao wanadai wawe sehemu ya jeshi jipya la taifa la nchi hiyo.

Hali ya wasiwasi imebakia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, amesema mwandishi wetu.

Vikosi zaidi vya jeshi kutoka Ufaransa viliongezwa Ijumaa baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono azimio la kurejesha utulivu kwa"njia zozote zinazowezekana".

Chama cha Msalaba Mwekundu, kimesema watu 394 walkiuawa katika siku tatu za mapigano mjini Bangui. Wengi wao wakiwani watoto.

Jeshi la Ufaransa limesema limefanikiwa kurejesha hali ya utulivu katika baadhi ya maeneo mjini Bangui kufikia Jumatatu usiku.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema askari wa kulinda amaniwapatao 9,000 watahitajika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na ana matumaini kuwa hatimaye watakuwa sehemu ya operesheniya Umoja wa Mataifa.

Inakadiriwa kuwa asilimia 10% ya watu milioni 4.6 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameyakimbia makaazi yao, wakati ambapo zaidi ya milioni moja wanahitaji msaada wa dharura wa chakula, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

JK AWASAMEHE WAFUNGWA ZAIDI YA 1000

KATIKA kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru, Rais Jakaya Kikwete ametoamsamaha kwa wafungwa 1,475.

Amewasamehe kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana.

Alisema ni mategemeo ya Serikali, kwamba watakaoachiwa huru, watarejea katika jamii kushirikiana na wananchi wengine katika ujenzi wa Taifa na watajiepusha na makosa ili wasirejee tena gerezani.

Alisema katika msamaha huo, wafungwa wote wapunguziwe mojaya sita ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida, lililotolewa chini ya Kifungu 49(1) cha Sheria yaMagereza Sura ya 58, isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 3(1-xiii).

Aidha, alisema msamaha huo, unawahusu wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kifua kikuu, kansa na Ukimwi ambao wako kwenye hatua za mwisho na wamethibitishwa na jopo la waganga, chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Mganga Mkuu wa Wilaya.

Wengine ni wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ; na umri huo umethibitishwa na jopo la waganga, chini ya Uenyekitiwa Mganga Mkuu wa Mkoa au Mganga Mkuu wa Wilaya.

Pia, msamaha huo unawahusu wafungwa wa kike, walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonyesha na wasionyonyesha.

Wengine waliopata msamaha huo ni wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili ;na ulemavu huo uwe umethibitishwa na jopo la waganga, chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Mganga Mkuu wa Wilaya.

Dk Nchimbi alisema msamaha huowa Rais, hauwahusu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha gerezani.

Pia, msamaha huo hauwahusu wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha, wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, ikiwemo cocaine, heroin na bangi.

Wengine ni wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupokea au kutoa rushwa, wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang'anyi na unyang'anyi wa kutumia silaha, wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na risasiau silaha.

Msamaha huo pia hauwahusu wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kunajisi, kubaka na kulawiti, wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari wa kutumia silaha na wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao.

Aidha hauwahusu wafungwa waliohukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa shule za msingi na shule za sekondari ;na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka18 na kuendelea.

MECHI YA STARS NA KENYA YAHAMISHWA

TANZANIA VS KENYA SASA SAA MOJA:

Mechi ya Kili Starsvs Kenya ya Kombe la Chalenji iliyopaswa kuchezwa saa 7 na nusu mchana huu Uwanja wa Kenyatta, Machakos imehamishiwa Nyayo, Nairobi kutokana na uwanja kufurika.Kocha Kim Poulsen wa Kili Star s, ambao walikuwa wa kwanza kufika Kenyatta, alilalamikia ubovu wa uwanja huo toka mapema, akiwaambia viongozi wa Shirikisho la Soka Kenya kuwa haustahili kutumika kwa mechi za kimataifa kwa viwango vya Fifa.

Mwandishi wetu toka Machakos anatuambia kuwa pamoja na jitihada za vigogo wa Soka wa Kenya kutaka kulazimisha mechi hiyo ichezwe Kenyatta mchana huu, viongozi wa timu pande zote mbili walikubaliana kwamba hali yauwanja hairuhusu kandanda hilo kuendelea kwani nyasi zimejaa maji kiasi kwamba mpira hata kudunda hauwezi.

Hadi saa nane hii, tunaambiwa wachezaji wa Tanzania wameshaondoka Machakos wakielekea Nairobi kujiandaa na mechi jioni, huku wenzano wa Kenya wakibaki wanashangaa-shangaa hapo Kenyatta Stadium


Chanzo: Mwanaspoti-fb

DROGBA AND EBOUE ARE FACING PUNISHMENT FOR MANDELA'S TRIBUTE

Seriously, what is wrong with the world?
Galatasaray's Didier Drogba and teammate Emmanuel Eboue both face punishment from the Turkish FA for paying homage to Nelson Mandela after Friday's 2-0 win over Elazigspor.

One night after Mandela's death, Drogba revealed a shirt with the  message"Thank You Madiba,"(Madiba is Mandela's clan name) while Eboue's undershirt read"Rest In Peace Nelson Mandela."

Both players of course are African, and this was a show of their appreciation for one of the most important civil rights leaders in world history.

However, the Turkish FA deemed the messages to be the kind of"political expressions"they are currently trying to discourage players and fans from making at games. And despite the fact Drogba and Eboue's messages were a tribute rather than a manifesto, the pair has been summoned to appear before the Turkish Professional Football Discipline Committee because they had not asked for permission first.

In response, Drogba took to Instagram with this message:
I'd be very interested to see your comments on this…but I'm sorry if I had to I would do it again and again.

Nor because of political beliefs but because this man inspired me,a country, a continent, the world!!!!! Thanks again Madiba

MTOTO WA MANDELA AELEZEA SIKU ZA MWISHO ZA BABA YAKE

Huku bunge la afrika kusini likifanyakikao maalum cha kumheshimu mandela ,mwanawe mkubwa wa kike Makaziwe ameiambia BBC kuhusu siku za mwisho za maisha yababaake.

Amesema kuwa ijapokuwa hakuwa akifungua macho mara kwa mara, alikuwa na uhakika kuwa aliweza kusikia vile familia yake ilivyompenda.

Makaziwe amekiri kuwa hakuweza kuwasiliana vyema sana na babake na kwamba babaake hakuweza kuonyesha hisia zake,lakini yote hayo alitaka familia yake kupatana.

Amesema kitu kikubwa alichoelimishwa na babaake ni kuwana ujasiri wa kusamehe.

MAHAKAMA YAMHUKUMU KIFUNGO CHA NDANI ALIYEDAIWA KUBAKWA

Mahakama nchini Somalia, imemhukumu kifungo cha nyumbani mwanamke aliyedai kubakwa pamoja na waandishi wawili wa habari waliomhoji kuhusiana na madai hayo.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 19, alipewa kifungo cha nje cha miezi sita kwa kile mahakama ilisema ni kutoa taarifa zisizokweli.

Atalazimika kukaa nyumbani kwake bila kutoka nje kwa miezi sita.

Mmoja wa waandishi wa habari, aliyemhoji mwanamke huyo naye alipewa kifungo cha nje cha mwaka mmoja huku mwenzake akipokea kifungo cha miezi sita.

Waandishi hao wanafanya kazi na kituo cha redio Shabelle ambacho serikali ilifunga matangazo yake mwezi Oktoba baada ya polisi kuvamia ofisi zake.

TABU LEY AZIKWA KINSHASA

Shughuli ya mazishi ya marehemu Tabu Ley Rochereau gwiji wa Rumba Afrika, inaendelea mjini Kinshasa, DRC.

Viongozi wa serikali ya DRC wamehudhuria mazishi hayo huku waakilishi kutoka nchi jirani ya Congo Brazaville pia wamehudhuria mazishi hayo.

Tabu Ley alifariki mwezi Novemba akiwa na umri wa miaka 76 akipokea matibabu nchini Ubelgiji.

Tabu Ley alikiri rasmi kwamba ana watoto 49.

Lakini mwandishi wa BBC katika mazishi hayo anasema kuwa zaidi ya watu 80 wamejitokeza na kusema kuwa baba yao nimwanamuziki huyo na kwamba wengi waowanataka kuzungumza katika sherehe hiyo.

Tabu ley aliyejulikana kama mfalme wa muziki wa rumba aliaga dunia mwezi uliopita mjini Brussels ,ubelgiji akiwa na miaka sabini.

Wengi walimkumbuka Tabu Ley kwa mziki wake na kwa talanta yake kwa utunzi wa nyimbo zake zilizowagusa watu wengi Afrika. Tabu Ley amefanyiwa mazishi ya kitaifa Mwanamziki huyo ambaye pia alikuwa mwanasiasa, hakuwahi kupona tangu alipougua kiharusi mwaka 2008 na hali yake iliendelea kuwa mbaya hadi alipofariki Novemba 30.

Alizaliwa mwaka 1937 katika kijiji kimoja kidogo Magharibi mwa mkoa wa Bandundu, na hapo ndipo nyota yake ilianza kung'aa a katika fani ya muziki wa Rumba mapema miaka ya sitini.

Baadhi ya nyimbo alizoimba zilikuwa Adios Thethe na Mokolo nakokufa, na zilisaidia katika kufanya mziki wa Rumba kupendwa sana.

Tabu Lei alitaka sana kuwa waziri wa utamaduni katika serikali ya Laurent-DesireKabila --babake rais Joseph Kabila, lakini badala yake akawa naibu gavana wa mji waKinshasa.

Alikimbilia usalama wake wakati wa utawala wa aliyekuwa rais Mobutu Sese Seko kati ya mwaka 1965 to 1997, na mnamo mwaka 1990, serikali ya Mobutu ikapiga marufu album yake Trop, c'est trop.

KIONGOZI WA MUSLIM BROTHERHOOD AFIKISHWA MAHAKAMANI

Kiongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake.

Hata hivyo mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Februari 11 mwaka 2014,Wadadisi wanasema ni sehemu ya kampeini ya serikali dhidi ya vuguvugu hilobaada ya jeshi kumuondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohamed Morsi.Mohamed Badie -- aliyefikishwa mahakamani na viongozi wengine wa kundi hilo, alikanusha madai kua alitumia kundi hilo kuchochea ghasia.

Miongoni mwa washitakiwa wenza wa Badie ni pamoja na Isam al-Iryan, Muhammad al-Biltaji, Basim Udah na Safwat Hijazi. Makosa mengine wanayokabiliwa nayo ni pamoja na kuundagenge la kuwahangaisha watu, uharibifu wamali ya watu binafsi na kumiliki silaha kinyune na sheria.

Makosa wanayokabiliwa nayo yanatokana na ghasia za mwezi Julai ambapo makabiliano yalizuka kati ya wafuasi elfu tano wa Mohammed Morsi pamoja na majeshi katika eneo la Giza na katika msikitiwa Al-Istiqamah baada ya kungo'olewa mamlakani kwa Mohammed Morsi.

Hata hivyo Badie Alihoji kwa nini uchunguzi haukufanyika kuhusu kifo cha mwanawe pamoja na kuteketezwa kwa makao makuuya Brotherhood.

Wanafunzi katika chuo kikuu cha Al Azhar wameendelea kuandamana na kulazimisha polisi kuingia chuoni humo ili kusitisha vurugu zao.

WAASI AFRIKA YA KATI KUPOKONYWA SILAHA

Wanajeshi wa Ufaransa, wanatarajiwa kuanza kuwapokonya silaha wapiganaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, kuanzia Jumatatu kwa kutumia nguvu ikiwa watalazimika kufanya hivyo.

Kikosi cha wanajeshi 1,600, kimepelekwa nchini CAR baada ya siku kadhaa za mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 400.

Kiongozi wa waasi, Michel Djotodia, aliingiamamlakani mwezi Machi kwa usaidizi wa wapigajani wake ambao wengi wao ni waasi wa zamani. Djotodia amechukua mamlaka baada ya kumpindua aliyekuwa Rais Francois Bozize.

Wanajeshi wa Ufaransa, sasa wanashika doria katika barabara na mitaa ya mji mkuu Bangui.

Walikwenda Bangui siku ya Ijumaa baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono azimio la kurejesha utulivu nchini humo kwa kutumia njia yoyote itakayofaa, hata kama ni kwa nguvu.

Nyumba zimeharibiwa kwa maguruneti kufuatia makabiliano makali kati ya waasi hao na wanajeshi na pia kutokana na vita vya kidini ambavyo vimetokana na vurugu hizo.

Wakati wa mapigano, mamia ya watu waumini wa kiisilamu walikimbilia katika nyumba ya Imamu mmoja ambako walikwenda kutafuta hifadhi.

JK ASHAURIWA KUMNG'OA PINDA

Rais Jakaya Kikwete, ameshauriwa kumng'oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikielezwa sababu kuwa ndiye kikwazo katika utendaji wa Serikali na kwamba akiachwa ataipeleka pabaya Serikalina CCM.

Kikwete pia ameshauriwa kumfukuza kazi Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, kwa kushindwa kukabiliana na matatizo ya ubadhirifu katika halmashauri nchini."

Kama (Rais) unaitakia mema nchi na CCM kuchukua hatua za kuwafukuza kazi Pinda na Waziri Ghasia," alisema Mbunge wa Mwibara, Khangi Lugola (CCM), juzi alipochangia taarifa za Kamati za Bunge kuhusu hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka jana."

Kwa nini Watanzania wafe kwa kunyimwa misaada na wafadhili kwa sababu ya mtu mmoja tu Pinda, kwa ajili ya Ghasia ameiendesha Tamisemi kama Saccos ama Vikoba?" alihoji."

Mchawi wetu ... ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekuwa mpole mno hawajibiki," alisema Mh. Lugola na kuongeza, "Kuanzia jana (juzi) Waziri Mkuu anahudhuria mahafali."

Wakati Lugola akizungumza mawaziri waliokuwepo bungeni ni wanne, manaibu mawaziri wawiliwawili, wakati mawaziri wote

KILLI STARS WAUWA WAGANDA HUKU IVO MAPUNDA AKIIBUKA SHUJAA

Ivo Mapunda ameibuka shujaa wakati Kilimanjaro Stars ikitinga nusu fainali ya michuano ya CECAFA katika mchezo uliofanyika jijini Mombasa.

Uganda walikuwa wa kwanza kuliona lango la Stars katika dakika ya 16 kupitia kwa Dani Sserunkuma huku Stars ikichachamaa na kusawazisha kupitia kwa Mrisho Ngassa katika dakika ya 18. Ilikuwa ni Ngassa alieziona nyavu za Uganda kwa mpira ya adhabu ndogo baada ya Mbwana Samatta kufanyiwa madhambi na kufanya hadi mapumziko Stars wawe mbele kwa2-1.

Kipindi cha pili Stars ilipata pigo baada ya Salum Abubakar kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 53 na kufanya Stars icheze kipindi kikubwa cha pili ikiwa pungufu.

Katika dakika ya 73 Uganda walisawazisha kupitia kwa Martin Mpuga na kufanya dakika 90 za mchezo zimalizike matokeo yakiwa 2-2 na kulazimika kwenda kwenye mikwaju ya penati.

Kevin Yondan, Athumani Iddi na Amri Kiemba walifunga kwa upande huku Mbwana Samatta na Erasto Nyoni wakikosa na Ivo Mapunda kupangua mikwaju miwili ya penatina kuipeleka Stars nusu fainali.

HONGERA SANA Kilimanjaro Stars.

Picha ya Siku

Hakuna kisicho wezekana ukiweka nia

WALIMU WATATU NA MFANYABIASHARA WAHUKUMIWA MIAKA 579 JELA

Mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imewahukumu waalimu watatu wa Shule ya Msingi Tukoma iliyoko Tarafa ya Nsimbo Wilayaya Mlele Mkoa wa Katavi na Mfanyabiashara wa Mjini Mpanda kifungo cha miaka 579 jela kwa wote baada ya kupatikana na hatia ya kuiba fedha za shule kiasi cha shilingi milioni ishirini na moja.

Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kuwatia hatiani kwa jumla ya makosa sitini na nane.

Washitakiwa waliohumumiwa hapo jana ni Joel Mwakyusa (37) Mwalimuwa shule ya Msingi Tukoma Mkazi wa Kawajense ambae amehukumiwa kifungo cha miaka 255 baada ya kupatikana na makosa arobaini ya wiziwa fedha, Lenatus Ngalo (50) mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Tukoma Mkazi wa Nsemlwa amehukumiwa kifungo cha miaka 148 baada yakupatikana na hatia ya makosa 38 Wengine walio hukumiwa ni Joachimu Katabi (39) Mwalimu wa shule ya Msingi Tukoma Mkazi wa Majengo ambae amehukumiwa kifungo cha miaka 143 na Fredilik Mlenje (50) mkazi wa Nsemulwa Mfanya biashara ambae akaunti yake ilitumika kuibia fedha hizo shilingi milioni 21 mali ya shule hiyo Washitakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo la wizi wa fedha za shule ya Msingi Tukoma hapo mwaka 2009 kwa kugushi nyaraka ambazo ziliwawezesha kuiba fedha hizo kwa kupitia akaunti ya mshitakiwa wanne Fredilik Mlenje.

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua masaa mawili kuisoma Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga Ntengwa alisema baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi mahakama yake imewaona wshitakiwa wanapatikana namakosa kwa mujibu wa vifungu vya sheria Namba 384,335, 337,270 na 242 Washitakiwa kabla ya kusomewa hukumu walipewa nafasi ya kujitetea ambapo waliomba mahahama iwasamehe kwani kuna familia zao zinawategemea pamoja na wazazi wao.

Baada ya maombi hayo mwendesha mashitaka Mkaguzi wa Polisi Ally Mbwijo alipinga maombi hayo na kuiomba mahakama itowe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za kuiba mali ya umma Ndipo hakimu alipowasomea washitakiwa adhabu hiyo ya kifungo jela kwa washitakiwa hao na kuwataka watakapo maliza kifungo hicho wote kwa pamoja walejeshe fedha hizo mali ya shule ya Msingi Tukoma.

Chanzo: Katavi Yetu Blog

TANZANIA, VENEZUELA KUOMBOLEZA SIKU TATU KIFO CHA NELSON MANDELA

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.

"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.

Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi, mvumilivu na mstahimilivu".Ameongeza Rais Kikwete.

Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake".

Rais ameongeza kusema,"Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".

Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.

Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.
Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,

DAR AS SALAAM.

06 Desemba, 2013

Sambamba na Tanzania, Rais wa Venezuela nae ametangaza siku tatu za maombolezo

WATANZANIA WAISHIO NJE WAZUA KIZAAZAA BUNGENI

SUALA la kuruhusiwa kwa Watanzania waishio nje ya nchi kupiga kura ya maoni ya kupitisha Katiba mpya, limezua mjadala bungeni, ambapo wabunge wengi wameonesha wasiwasi na kutaka utaratibu huo usitishwe, kwa kuwa unaweza kuzalisha mamluki na kuweka nchi hatarini.

Pia, Spika Anne Makinda na baadhi ya wabunge wazoefu akiwemo Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Muhammed (CUF), wamewaasa wabunge kuhakikisha kuwa wanaweka itikadi zao pembeni ndani ya Bunge hilo na kuungana kwa pamoja katika mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba mpya.

Aidha, bungeni hapo kuligeuka uwanja wa kusutana baada ya wabunge watokao Zanzibar kurushiana vijembe hasa baada ya kuibuka kwa mjadala wa kupinga kutumika kwa Sheria ya Uchaguzi Zanzibar na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika uchaguzi wa kura ya maoni.Akichangia mjadala huo bungeni hapo, Mbunge wa Same Magharibi,Anne Kilango alitahadharisha juu ya uwezo wa Serikali kuweza kuwafikia Watanzania wote wanaoishi nje ya nchi na iwapo takwimu na idadi yao halisi ipo."Ikumbukwe kuwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni wengi na wanaoishi duniani kote si hapo London pekee, humu kwenye Sheria tumesema tutaunda kamati za kura za maoni, wasimamizi je huko nako tutaweza kuunda kamatihizi duniani kote? Uwezo huo tunao kweli? Alihoji.

Kwa upande wake, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF) alitahadharisha juu ya kipengele hicho kinachotoa fursa kwa Watanzania waishio nje ya nchikupiga kuwa huenda fursa hiyo inaweza kutumiwa vibaya.

Aidha, aliwataka wabunge kutumia busara na kuweka itikadi zao pembeni wanapojadili masuala yanayohusu mchakato wa Katiba ili kutokutoa fursa kwa watu wenye nia mbaya kuliangamiza taifa.Alisema kumekuwepo na watu ambao hawaitakii mema Tanzania na kwamba huangalia fursa yoyote ya kutokuelewana na kujipenyeza kwa ajili ya kuliangamiza taifa kwa maslahi yao.

"Haiwezekani kwa mazingira yoyote kutunga Sheria ikawa kamilifu anayeliweza hilo ni Mungupekee, ila kama kuna makosa ni vyema kuweka uzalendo mbele bila kuingiza siasa na kuyabainisha ili yaweze kufanyiwa kazi," alisisitiza.

Alisema haipendezi kutengeneza matabaka na makundi ndani ya chombo hicho kwa mambo ambayo yanaweza kurekebishwa na matokeo yake kuonekana kwa Watanzania wote.

"Kwa sasa kuna familia za Wazanzibari takribani 118,000 waliopo Tanzania bara na kila familia ina watoto zaidi ya wanane,Zanzibar pia kuna familia za Watanzania Bara 15,000 wanaishi huko na watoto watano kila familia, sasa kwa haya tunayoyafanya hapa jamii itaenda wapi? Alihoji.

Aliwaomba wabunge hao kuhakikisha mchakato huo hauwagawi Watanzania na kuangamiza taifa kama ilivyokuwa kwa mataifa ya Libya na Iraq ambayo kwa sasa baada ya kusambaratika maliasili zake ikiwemo mafuta zinatafunwa na wajanja.

Spika Makinda naye alionesha kushangazwa na hali ya sasa ya Bunge hilo, ambapo kumekuwa na mabishano na majibizano huku hoja muhimu zinazohitaji kuboreshwa zikiachwa."Kuna wasomi humu ndani jamani wakiwemo wanasheria, tumieni taaluma zenu kurekebisha, tatizo la Bunge hili kila kitu kinafanyika kivyama. Kosoeni na kusema tufanye nini, sasa nyie mkilalamikamlipo humu ndani waliopo nje naowafanye nini? Alihoji.Mbunge wa Viti Maalum, Tauhida Gallas (CCM), alionesha kushangazwa na kauli za wabunge wengine za kupinga kutumika kwa daftari hilo la kudumu katika uchaguzi huo wakati daftari na sheria hizo ndio zilizotumika katikakupiga kura ya maoni ya kupitisha mfumo wa Serikali ya Umoja (SUK)visiwani humo.

"Masuala ya Wazanzibari tuachieni wenyewe sie tunajuana, ni Waarabu wa Pemba, hili daftari na sheria inayokataliwa vilitumika kupigia kura ya maoni ya SUK, sasaleo kwenye Katiba iweje ikataliwe, wenzetu hebu tuambieni kuna ninihapa? Alihoji.

Alisema hata suala la kulaumiwa kwa masheha halina mashiko, kwa kuwa masheha hao wamekuwa wakifanyakazi bila kuzingatia uchama hali iliyosababisha kulalamikiwa vyama vyote.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, alisisitiza juu ya umuhimu wa suala hilo la Katiba kujadiliwa bila kuingiza vyama kwa kuwa kwa hali inayoendelea bungeni humo imeonesha kutokuwepo kwa dhamira ya kupatikana kwa Katiba ya Watanzania.

Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mohammed Mnyaa, alipinga vikali suala la kuachwa kwa Sheria hiyo ya Zanzibar katika mchakato wa Katiba kwa kuwa imekuwa ikipindisha haki ya watu wegi kushiriki kwenye uchaguzi akiwemo Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.

"Sheria hii sijui kwanini bado inafumbiwa macho, kwani kupitia Sheria hii Rais Shein ndio Rais wa kwanza duniani kutojipigia kura kwa kuwa tu haimtambui," alisemaMnyaa.

BREAKING NEWS: MZEE MANDELA AFARIKI DUNIA

‎Breaking‬: Rais wa Afrika Kusini na mpigania uhuru wa nchi hiyo, Nelson Mandela amefariki usiku huu, Rais JacobZuma atangaza muda huu, Usiku huu.

MMAREKANI AUWAWA LIBYA

Mwalimu anayeaminika kuwa raia wa Marekani ameuawa kwa kupigwarisasi mjini Benghazi Mashariki mwa Libya.

Maafisa wanasema kua mwalimu huyo kutoka mjini Texas Marekani, alifundisha somo la Kemia katika shule moja ya kimataifa.

Mwanamume huyo anayesemekana kuitwa Ronnie Smith, anasemekana kupigwa risasi alipokuwa anafanya mazoezi katika mtaa wa Fweihat.

Hata hivyo ubalozi wa Marekani haujatoa taarifa yoyote kuhusiana na mauaji hayo.

Pia hakuna kundi lililojitokeza kuhusika na mauaji hayo.

Shule ya kimataifa alikokuwa anafunza mwalimu huyo, sio ya kimarekani, bali inafuata mfumo washule za Marekani.

BANGUI KWACHAFUKA

Kumekua na mapigano makali ya kurushiana risasi na silaha nzito nzito katika mji wa Bangui nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati saa moja kabla Baraza kuu la Umoja wa Mataifa halijapitisha azimio la kupeleka majeshi ya kutoka Afrika na Ufaransa.

Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo katika mji wa Bangui anasema ameona magari ya kivita yakiendeshwa yakipita katika mitaa na kwamba watu wengi bado wamejifungia majumbani mwao.Balozi wa Ufaransa katika Umoja waMataifa Gerald Araud ameiambia BBC kuwa kuongezwa majeshi ya kimataifa utasaidia hali ya usalama ndani ya wiki chache.

Bwana Araud amesema Majeshi ya Umoja wa Afrika na yale ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kusimamia sheria na utulivu katika mji wa Bangui kabla ya kuangalia usalama katika miji mingine nchini Jamuhuriya Afrika ya Kati.

PAPA AIDHINISHA KAMATI YA KUPAMBANA NA WATAKAO NAJISI WATOTO

Baba mtakatifu Papa Francis ameidhinisha kamati ya Vatican itakayopambana na visa vya unajisi wa watoto katika kanisa katoliki pamoja na kuwasaidia waathiriwa kwa kuwapa ushauri nasaha.

Tangazo hili limelotolewa na naibu askofu mkuu Sean O'Malley mjini Boston Marekani, na linakuja baada ya kufanyika mkutano kati ya Papa na makadinali wake wanane ambao humshauri.

Kadhalika tangazo lenyewe linakuja baada ya Vatican kukataa ombi la Umoja wa Mataifa la kutaka ukabidhiwe taarifa za kanisa hilo kuhusu madai ya makasisi na watawa wanaodaiwa kuwanajisi watoto.

Papa Francis, amesema kuwa swala la kukabiliana na visa vya makasisi kuwanajisi watoto ni muhimu sana ili kuweza kulirejeshea hadhi kanisa Katoliki.

Kadinali, Sean O'Malley, naibu askofu mkuu wa kanisa hilo mjini Boston, alisema kuwa kamati hiyo inaweza kutoa mwongozo wa kikazi kwa makadinali na maafisa wa kanisa ili kulainisha utenda kazi wa viongozi wa kanisa.

Mji wa Boston ndio ulikuwa kitovu cha madai ya makasisi kuwanajisi watoto nchini Marekani mwaka 2002.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, naibu Askofu alisema kuwa kamati hiyo mpya ilipendekezwa nabaraza la makadinali, ambalo lilibuniwa ili kufanyia mageuzi kanisa katoliki. Papa aliliidhinisha Alhamisi.

DR. MTIKILA ADAI KUNA CHADEMA MBILI, CHADEMA CHUMBANI NA CHADEMA SEBURENI

Mchungaji Christopher MTIKILA azidi kupiga msumali wa MOTO katika JENEZA la Chadema mashumbulizi yake yamuelekea Edwin MTEI "Amemtuhumu mmoja wa wanzilishi na m/kiti wa kwanza wa chadema Edwin MTEI, akidai kuwa ni muasisi wa dhana ya UKABILA na UKANDA katika chama hicho huku m/kiti wa sasa Freeman MBOWE na Katibu wake SLAA wakidaiwa kuboresha mfumo huo KISASA zaidi kwa kuweka NAKSH NAKSH" Hata kinacho wafukuza Zitto na wenzake ktk Chadema ni matokeoya kuota mizizi kwa mfumo wa UKABILA na UKANDA ambao hauruhusu mwanachama yoyote kuhoji mapato na matumizi ndai ya chama "WATANZANIA waelewe Chadema si chama cha siasa na VIONGOZI wake si wanasiasa wa kweli, kwani hawana MAONO wala MALENGO ya kuwakomboa watanzaniaKWA UJUMLA NI GENGE LA WALAJI TU!!!

Ndani ya chadema kuna kundi linaitwa "BIG EIGHT " ambalo linaudwa na wazee wa KICHAGA na kiongozi wao mkuu ni Edwin MTEI akisaidiwa na akina Mariale na Ndessamburo,

Hawa ndio wenye chadema yao ambapo moja ya MAJUKUMU yao ni kulinda maslahi ya kichaga ndani ya chama, Kuna Chadema mbili kuna chadema ya CHUMBANI na Chadema ya SEBULENI"

PAPA FRANCIS ADAIWA KUTOROKA VATICAN

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amedaiwa kutoroka usiku Makao Vatican ili apate fursa ya kwenda kutoa misaada kwa walemavu na watu wasiojiweza.

Tetesi za Papa Francis kuwatembelea maskini hao usiku kwa kujificha zimekuja baada ya mahojiano yaliyofanywa na Askofu Mkuu, Konrad Krajewski ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya fedhatoka kwa wasamaria wema na kuwapelekea maskini.

Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwendakuwapa misaada maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.

Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francisamekuwa akipenda kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.

"Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda kufanya kazi hiyo," alisema Padri Krajewski.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo Papa aliwahi kwenda naye nje ya mji kwaajili hiyo, Askofu Krajewski, alisita kujibu swali hilo.

Wakati huohuo, gazeti la HuffingtonP ost limeripoti kuwa walinzi wa Uswisi, wamethibitisha kuwa Papa amekuwa akizunguka maeneo mbalimbali usiku akiwa amevalia mavazi ya kawaida ya wachungaji nakuwapa misaada, wanaume na wanawake wenye shida mbalimbali.

Tangu kuteuliwa kwake, papa Francis amevipamba vichwa vya habari duniani baada ya kuonekana akijaribu kuvaa kofia za polisi wa zimamoto, kuwaruhusu vijana wadogo wa kiume kuibusu miguu yake na kuwapigia simu waumini wake na kuzungumza nao.

Hivi karibuni, aliripotiwa katika vyombo vya habari akiwabusu na kuwafariji waumini walemavu katika Kanisa la Mtakatifu Peter, huku taarifa nyingine zikionyesha kuwa ametuma fedha zake binafsi kwa wahamiaji na wanaohangaikia mafao yao.

Alipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis alifahamika kwa kutoroka usiku na kuwatafuta watu, kuzungumza nao na wakati mwingine kuwanunulia chakula.

Mapapa wengine waliopita pia wametajwa kutoroka usiku, kwa mfano papa John wa X111 alikuwa na tabia ya kutoroka usiku na kwenda mitaa ya Rome kufurahia uzuri wa jiji hilo, wakati Papa Pius wa X11 alivalia kama Mfaransa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kwenda mipakani kuwasaidia Wayahudi wa Kirumi kisha kuwaweka katika sehemu salama.

LUKAS PODOLSKI TO RETURN ON FULL TRAINING THIS WEEK

Arsenal forward Lukas Podolski will return to training this week after more than three months out with a left hamstring injury, handing the Premier League leaders an alternative up front for the busy festive period.

Olivier Giroud has been shouldering the attacking burden for Arsenal since Podolski was hurtduring the Champions League playoff win over Fenerbahce at theend of August.

Arsenal manager Arsene Wenger says Podolski will be back in training after Wednesday's match against Hull, adding that "it will take at least a week with normal training to consider him fit for the squad.

"The game against Hull is the first of eight matches in a 28-day span through to January 1 for Arsenal, which leads the league by four points after 13 games.

PICHA YA SIKU

Kutoka kwa Masoud Kipanya

YAYA TOURE MCHEZAJI BORA TUZO ZA BBC

Yaya Toure ametangazwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwaka 2013 ya mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika.

Mchezaji huyo wa Ivory Coast, na ambaye pia ni kiungo wa klabu ya Manchester City ya Uingereza, na ambaye jina lake limekuwepo kwa miaka minne iliyopita katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, aliwashinda Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa, katika kuibuka mshindi.
Mchezaji huyo ana umri wa miaka 30.

Orodha fupi ya waliowania tuzo hiyo ilitayarishwa na wataalamu 44 wa soka kutoka kote barani Afrika, na wakizingatia hasa maarifa ya mchezaji, kiufundi, ushirikiano na wenzake katika timu, na kwakucheza mchezo safi na kwa haki.

Kisha, kupitia idadi kubwa kabisa kuandikishwa kwa wapiga kura, mashabiki waliweza kushiriki katika shughuli hiyo katika mtandao, au kupitia ujumbe wa simu ya mkononi.

Mashabiki hao wameamua kwamba Toure ndiye bora zaidi, kwani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, raia huyo wa IvoryCoast alicheza kwa bidii, kuonyesha mchezo wa kasi, ubunifu, na vile vile kwa kufunga magoli.

Ingawa mwaka 2013 ulikuwa ni wa ufanisi kwa Toure hasa kwa kupata vikombe, hakuweza kuisaidia nchi yake, wala klabu, kupata kombe lolote lile, lakini bado alionyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo.

Baada ya kuvunjika moyo kwa kushindwa kuutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Premier wa mwaka 2012 akiichezea Manchester City, Toure alirudi uwanjani akijizatiti, na kuimarisha mikwaju yake ya free-kick.

Alitumbukiza wavuni bao, kwa mpira wa kupinda, katika siku ya kwanza ya msimu mpya wa ligi kuu ya Premier, wakati timu yake ilipocheza na Newcastle, na akarudia hayo hayo katika mechi iliyofuata wakati Hull walipo watembelea katika uwanja wao wa nyumbani.

Toure amefunga magoli manne ya kupangakwa makini shambulio, na hayo yakiwa ni kati ya magoli saba kwa jumla aliyoweza kuifungia klabu ya Man City msimu huu.

Kufikia sasa, mwaka huu wa 2013, Toure ametumbukiza wavuni jumla ya magoli 12; ya klabu na vile vile ya nchi yake, na hiyo nirekodi nzuri sana kwa mchezaji wa kiungo cha kati.

Mbali na ustadi huo katika kumalizia, Toureni kiongozi bora katika timu, na maarifa yake yameiwezesha City kufikia sasa kuwa katika nafasi ya nne katika ligi kuu ya England.

Aliisaidia kikamilifu nchi yake ya Ivory Coast kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka ujao itakayofanyika nchiniBrazil.

Timu yake ya Tembo,The Elephants ilihitaji kuusahau mwanzo mbovu hapo awali katika kampeni yao ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na walipo ondolewa katika robo fainali na Nigeria, ambao hatimaye waliibuka mabingwa, na Toure akiwapa matumaini ya kufanya vyema baadaye.

Nje ya uwanja, Toure ameongoza vita dhidiya ubaguzi wa rangi katika soka, hasa baada ya matusi kuelekezwa kwake katika mechi ya ligi ya klabu bingwa dhidi ya CSKA Moscow, mwezi Oktoba, na akionyesha moyo wa uvumilivu na wa kimichezo unaostahili uwanjani.

Tukio kama hilo linaweza kumvunja moyo mchezaji asiyejiamini, lakini Toure ameendelea kuwa mchezaji wa kipekee tangu wakati huo.

Na katika mwaka wa tano baada ya jina lake kupangwa katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, hatimaye Toure ametajwa kama mshindi wa tuzo ya mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika.

BOKO HARAM WASHAMBULIA KITUO CHA ANGA

Wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia ngome ya kikosi cha anga cha Jeshi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuharibu helkopta mbili maafisa wa serikali wamesema.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mamia ya wapiganaji wameshambulia maeneo kadhaa katika mji wa Maiduguri kuanzia mapema asubuhi siku ya jumatatu.

Amri ya kutotembea ovyo ya saa 24 imetangazwa katika jimbo la Maiduguri. Nauwanja wa ndege unaotumiwa na wananchi umefungwa kwa muda.

Mwandishi wa habari wa BBC anasema shambulio hilo lililopangwa ni shambulio kubwa ambalo limerudisha nyumba juhudiza Jeshi la Nigeria.

Maelfu ya watu wameuwawa nchini Nigeriana wapiganaji hao tangu mwaka 2009 wakati Boko Haram walipoanza mashambulizi ya kutaka kusimika utawala unaoegemea sharia ya kiislamu.

UN YAANZA KUTUMIA NDEGE ZISIZO NA RUBANI DRC

Majeshi ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yameanza kutumia ndege zisizo rubani kuchunguza harakati za waasi katika mipaka na Rwanda na Uganda.

Hii ni mara ya kwanza kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa kutumia ndege za aina hiyo.

Ndege mbili za kwanza zilirushwa kutoka mji wa mashariki wa Goma ambao mwaka jana ulikaliwa kwa muda mfupi na waaasi wa kundi la M23.

Ndege mbili za kwanza zinaundwa na shirika la Italia la Selex ES.

Jeshi la Umoja wa mataifa katika Jamhuri yaKidemokrasi ya Congo ndio kubwa kupita yote duniani na lilichangia kwa kiasi kikubwa mwezi uliopita ushindi dhidi ya waasi wa kundi la M23;lakini bado kuna makundi mengine kadhaa ya wanamgambo nchini humo.Kikosi kipya kilichoimarishwa nguvu cha Umoja wa Mataifa kilitumia ndege za helikopta kulisaidia jeshi la Congo dhidi ya waasi hao wa M23.

Eneo tajiri la madini la mashariki mwa Congo limekumbwa na vita kwa kipindi chamiongo miwili iliyopita lakini kushindwa kwa M23 kumeleta matumaini fulani ya kupatikana utulivu zaidi kwa eneo hilo.

Mwandishi wa BBC, mashariki mwa Congo Maud Jullien amesema kwa muda mrefu kumekuwa na tuhuma kwamba vikundi mbalimbali vyenye silaha katika jimbo la Kivu Kaskazini wakipata msaada kutoka nchi jirani.

Rwanda na Uganda mara kwa mara zimekanusha tuhuma za kuwasaidia waasi wa M23, kikundi ambacho hivi karibuni kilipigwa na majeshi ya Congo yakisaidiwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyolinda amani nchini Congo.

Askari wapatao 22,000 wapo nchini Congo,kikiwa ni kikosi kikubwa zaidi cha Umoja wa Mataifa katika shughuli za kulinda amani duniani.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kulinda amani Herve Ladsous ameiambia BBC kuwa ndegehizo zisizo na rubani, zitatumika kama njia mojawapo ya kufuatilia harakati za makundi yenye silaha na mienendo ya raia katika eneo la mashariki mwa Congo.

"Tunatakiwa kuwa na picha halisi ya kile kinachotokea," amesema.

Amesema kama watafanikiwa nchini DR Congo, ndege hizo zinaweza pia kutumika katika maeneo mengine ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.

MWENYEKITI CHADEMA MKOA WA SINGIDA AACHIA NGAZI

WILFRED NOEL KITUNDU MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013

KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA

YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA

Somo hapo lahusika,Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua kujiuuzuru nafasi yanguya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli ndani ya chama.

Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA nani mwanachama wa 300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitilizaMaamuzi na vitendo vinavyoendelea ndani ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa demokrasia ya kweli tunayoihubiri mbele ya umma.

Kwa barua hii basi, nimeonelea bora upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na dhamira yangu inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.

Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu tayari.

Ninatanguliza shukrani zangu za dhati kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywana kamati kuu ya chama.

Kusimamia haki, katiba na misingi ya chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba macho pindi ujinga wa namna hii unapoendeleakutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.

Nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako.
………………………………………………….

Wilfred N. Kitundu

MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013

OFISI YA CHADEMA ARUSHA YACHOMWA MOTO

Ofisi ya chadema mkoani Arusha imeponea chupuchupu kuteketea kwa moto baada ya watu wasiofahamika kuichoma moto asubuhi ya leo.Katibu wa Chadema mkoani Arusha.

Bw. Amani Golugwa amesema lengo la mtu huyo inaonekana lilikuwa kuteketeza vifaa na nyaraka zao za kiofisi ila alivyoona muda umeenda ndipo aliamua kuchoma (ceiling board) akiamini kuwa moto huo utasambaa mahali kote lakini wao waliweza kuwahi na kuuzima.

Ceiling board ya chumba kimoja nachoo ndio maeneo yaliyoathiriwa ila maeneo yaliyobaki na vifaa vyote ni salama.