Shaffih Kujibu Tuhuma za TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih
Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti
ya www.shaffihdauda.com kutoa
maelezo kuhusiana na barua ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye
mtandao wake huo.

FIFA ambayo ilisimamisha mchakato
wa uchaguzi wa TFF baada ya
baadhi ya wagombea kuulalamikia,
baadaye ilitoa maelekezo kuhusu
mchakato huo kwa barua ambayo
iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar
Lenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na
waandishi wa habari ambao Dauda
alihudhuria alibainisha kuwa barua
hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu,
na kuruhusu waandishi kuisoma
kwa Ofisa Habari wa TFF bila
kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na
waandishi wa habari (Mei 2 mwaka
huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA
ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF
pekee, na viongozi wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.

Hivyo TFF imemtaka Dauda
kutoa maelezo ya mahali alipoipata
barua hiyo ndani ya siku saba.

Chanzo:shaffihdauda.com

Aston Villa Kutupa Karata Yake leo

Timu ya mpira wa miguu Katavi Warriors hali maarufu kama Aston Villa ikifahamika hivyo katika viunga vya mji wa mpanda.

Ambayo imefanikiwa kupanda daraja baada ya kuibuka bingwa wa mkoa wa katavi na kufanikiwa kuingia ligi ya TFF ngazi ya kanda Inatarajia kutupa karata yake leo 12 May dhidi ya timu kutoka mkoan Rukwa, Rukwa United katika Uwanja wa Azimio mjini mpanda muda ni kuanzia saa kumi jioni kwa saa za afrika mashariki.

Katavi inawakilishwa na timu mbili katika mashindano haya, timu hizo ni Katavi Warriors(Aston Villa) na Small kids(kotaz).  Small kinds inashiriki mashindano haya baada ya kushuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza ngazi ya taifa. Kila la heri timu kutoka katavi

"Burundi Mpaka Dar Kwa Bajaj" Dr. Magufuli

WAZIRI wa Ujenzi, Dk John
Magufuli amesema serikali
inaendelea kujenga barabara
kwa kiwango cha lami ifikie
hatua ya watu wasafiri kutoka
Burundi hadi Dar es Salaam
kwa teksi na ikiwezekana kwa
bajaj.

Dk Magufuli alisema hayo jana
bungeni wakati akijibu
maswali bungeni likiwemo la
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Kabwe Zitto aliyesema Kigoma
imefaidika na barabara lakini
hazina maana kama barabara
za kuiunganisha na Tabora
hazitengenezwi.
“Namshukuru Zitto kwa
kupongeza Serikali ya CCM.
Ni
kitendo cha ushujaa kwa
mbunge wa kambi ya upinzani
kupongeza…barabara (za
Tabora) zimeshawekewa jiwe
la msingi, zitaendelea
kujengwa watu watoke
Burundi hadi Dar es Salaam
kwa teksi na ikiwezekana kwa
bajaj,” alisema Magufuli.
Akielezea kusimama kwa
ujenzi wa barabara za Tabora-
Nzega, Tabora-Urambo na
Kaliua, Waziri Magufuli
alisema miezi miwili iliyopita
kulikuwa na mvua nyingi
ambazo ziliathiri matengenezo
yake. Akizungumzia maeneo
ya barabara yaliyoharibika
baada ya ujenzi, Magufuli
alisema wizara inachukua
hatua.

Mojawapo ni mkandarasi
aliyerudishwa katika eneo la
Sekenke kurudia ujenzi kwa
gharama zake na amepewa
mwaka mmoja wa uangalizi
wa barabara hiyo.
Hata hivyo, Waziri Magufuli
alisema serikali iko katika
mchakato wa kupitia sheria
kudhibiti uzidishaji wa mizigo
kutokana na ukweli kwamba
Tanzania ndiyo inaruhusu tani
nyingi kupitishwa barabarani
ikilinganishwa na nchi
nyingine zikiwemo
zilizoendelea.

Kwa mujibu wa Magufuli,
kiwango cha tani
zinazoruhusiwa nchini ni 56
wakati nchi kama vile
Marekani, kiwango chao ni
tani 40, Uingereza ni 44,
Denmark tani 48; Uganda na
Kenya zinaruhusu tani 54.
Awali katika swali la msingi,
Mbunge wa Viti Maalumu,
Martha Mlata (CCM) alihoji
utekelezaji wa ahadi ya
Serikali kwamba katika
awamu ya nne wananchi
wataweza kusafiri kwa teksi
kutoka Mtwara hadi Bukoba.

Akijibu swali hilo, Naibu
Waziri wa Ujenzi, Gerson
Lwenge alisema lengo hilo
limetekelezwa kwa mafanikio
makubwa hadi kufikia asilimia
99 ya barabara yote kutoka
Mtwara hadi Bukoba.

Alisema barabara yote kuanzia
Mtwara-Dar es Salaam-
Dodoma-Singida-Nzega-Tinde-
Usagara-Geita-Bwanga-
Kyamyorwa hadi Bukoba
yenye urefu wa kilometa
zipatazo 1,989 imejengwa kwa
kiwango cha lami isipokuwa
eneo la urefu wa kilometa 26
katika barabara ya Ndundu-
Somanga litakalokamilika
Desemba mwaka huu.

Shekhi Ponda Apata hukumu ya Kifungo cha Nje

Makahama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar Es
Salaam, imemfunga kifungo cha nje
cha mwaka mmoja katibu wa Jumuiya
na Taasisi za Kiislam Tanzania Shekhe
Ponda Issa Ponda,huku washtakiwa
wengine wote 49 wakiachiwa huru

Babu Wa Loliondo Ashitakiwe

KAMBI rasmi ya upinzani
imeibua upya hoja ya tiba ya
asili maarufu kama Kikombe
cha Babu wa Loliondo, ikihoji
kwamba Serikali haijatoa kauli
wala kuchukua hatua dhidi ya
Mchungaji mstaafu wa Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Ambilikile Mwaisapile
aliyekuwa akitoa tiba hiyo.
Msemaji Mkuu wa kambi hiyo,
Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk Antony Mbassa
alihoji jana bungeni katika
hotuba yake kuhusu makadirio
ya mapato na matumizi kwa
mwaka 2013/14.

Alisema kwa mujibu wa
aliyekuwa Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk Hadji
Mponda, watu 116 walifariki
dunia kutokana na sababu
mbalimbali wakiwa kijiji cha
Samunge, ilikokuwa ikitolewa
tiba hiyo na mchungaji
Mwaisapile.

“Mpaka leo Serikali haijasema
chochote kuhusu uchunguzi
wa dawa ya babu. Mpaka leo
Serikali haijatoa kauli yoyote
wala kuchukua hatua yoyote
dhidi ya Mzee Mwaisapile
ambaye Februari hii alitoa
kauli nyingine juu ya ugunduzi
wa dawa nyingine,” alisema
Mbassa.

Kwa mujibu wa Mbassa, timu
ya uchunguzi iliyoundwa
mpaka Machi 2011 ilikuwa
imeandaa kukamilisha
taratibu , ili kufuatilia
maendeleo ya kiafya ya
wagonjwa 200 ambao
wamekubali kwa ridhaa yao
kushiriki katika utafiti huo
kuona maendeleo yao kiafya
baada ya kunywa dawa hiyo.

Wakati huo huo, kambi hiyo ya
upinzani imeishauri Serikali
kutoa taarifa rasmi kwa
wananchi juu ya dawa bandia
za kupunguza makali ya
Ukimwi (ARVs) makopo 4,000,
ambazo hazijakusanywa ili
kuwaondolea mashaka na
kuwajengea imani watumiaji.

Kambi hiyo imesema sakata la
kuwepo ARVs bandia
lililochukua miezi minane sasa,
limekuwa na sura tofauti
hususan juu ya nani anahusika
moja kwa moja baada ya
kiwanda cha Tanzania
Pharmaceticals Industry (TPI),
kukanusha kuhusika wakati
Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA) na Bohari Kuu (MSD )
wakisisitiza zimetoka
kiwandani hapo.

“Wakati taratibu za kitaalamu
na kisheria zikiendelea
tunaishauri Serikali kutoa
taarifa rasmi kwa wananchi
juu ya dawa ambazo
hazijakusanywa. Je, ziko
vituoni au zilishatumiwa na
wananchi? Kama
zilishatumiwa, je, serikali ina
taarifa zozote juu ya
waliozitumia dawa hizo? Je,
kuna madhara yoyote
waliyoyapata kutokana na
kuzitumia,” alisema.

Kulingana na taarifa ya kambi
ya upinzani, jalada la kesi ya
ARVs bandia limepokewa na
linashughulikiwa na
Mkurugenzi wa Mashitaka
(DPP) ili kupata mwelekeo wa
nani ahusishwe na kwa kosa
gani kabla ya kuachia mamlaka
husika jukumu la uchunguzi
wa kina.

Taarifa hiyo ya kambi inasema
ofisi ya DPP ilitoa maelezo
kwamba suala hilo limechukua
muda mrefu wa zaidi ya miezi
miwili tofauti na muda wa
kawaida wa siku 14
unaotumiwa na ofisi hiyo
kushughulikia kesi mbalimbali
zinazofikishwa kutokana na
uzito na unyeti wa suala hilo.

Picture Of the Day| Picha Ya Siku

Unazani Mr Arsene Wenger Aliwaza nini hapo.

FBI Watua Arusha

Makachero wa FBI kutoka Marekani
wamewasili nchini Tanzania kusaidia
katika upelelezi wa shambulizi la
bomu lililotekelezwa katika kanisa
katoliki mjini Arusha siku ya jumapili.

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza
akiwa mjini Arusha anasema
makachero hao wa FBI wako Tanzania
kusaidiana na Jeshi la wananchi wa
Tanzania na Polisi kutafuta undani wa
tukio hili ambalo limeishtua na
kuiweka serikali ya Tanzania katika
wakati mgumu.

Baruan Muhuza anaongezea hali
inaonekana kuwa ngumu zaidi hasa
kutokana na aina ya matukio ambayo
yamekuwa yakitokea katika siku za hivi
karibuni yakihusisha viongozi wa dini
ambapo wengi ya wanaodhurika
huwa ni wa imani ya kikristo.

Wakati huo huo wakuu wa serikali
wakishirikiana na viongozi wa kidini
wameandaa mkutano
utakaojumuisha viongozi wapatao
200.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Said Meck Sadiq amewaambia
wanahabari kuwa wamelazimika
kuandaa mkutano huo wa siku mbili
kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete.

Mkutano huo utajadili uhusiano bora
baina ya wakrito na waislamu.

Chanzo: BBC

Majambazi Yapora na Kuuwa Jijini Dar

Majambazi yapora mama mmoja kiasi
cha shilingi milioni kumi na kutokomea
kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea leo
saa 11 jioni inavyosemekana mdada
huyo alikua akitoka benki ya CRDB
tawila
Uhuru ambapo majambazi yakiwa na
pikipiki yalikua yakimfuatilia, alipotoka
tu wakaligonga gari lake makusudi
ndipo dada huyo
aliposimama ili angaalie nani kagonga
gari yake ambapo jambazi mmoja
alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na
kutokomea na kiasi hicho cha pesa.

Raia Wanne Wa Saudia Wakamatwa Mlipuko Wa Arusha

Polisi nchini Tanzania inawashikilia
watu wa nane kwa madai ya kuhusika
na mlipuko wa siku ya jumapili katika
kanisa Katoliki la Olasit viungani mwa
mji wa Arusha.

Miongoni mwa washukiwa ambao
wako mikononi mwa polisi ni raia
wanne wa Saudi Arabia, na wengine
wanne ni raia wa Tanzania.

Wakati mwandishi wa BBC Baruan
Muhuza akuzungumza akiwa
hospitalini mjini Arusha amesema
idadi ya watu waliofari dunia kufuatia
mlipuko huo ni wawili na wala sio
watatu kama ilivyoripotiwa hapo
awali.

Polisi mjini Arusha vile vile
wamethibitisha kuwa waliokufa wakati
wa tukio hilo la kigaidi ni wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza
ni kulipuzi aina gani kilitumika wakati
wa shambulizi hilo.

Lakini Baruan Muhuza ambaye
alitembelea eneo la tukio mbali na
majeruhi hakuna hasara kubwa
iliyotokea mahali hapo pia sakafi na
kuta za kanisa hilo hazikuchimbika
sana.

Kutoka Dar es Salaam Leornad
Mubali anaongezea kuwa watu wawili
sana wamethibitishwa kufariki dunia
katika mlipuko huo uliotokea majira ya
saa tano asubuhi katika kanisa katoliki
la Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha
nchini Tanzania na wengine kadhaa
kujeruhiwa huku balozi wa papa na
watawa waliokuwa katika shughuli
hiyo maalumu ya uzinduzi wa parokia
mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi
wakinusurika pia .

Kwa mjibu wa Padri Festus
Mangwangi ambaye ni paroko
msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la
Arusha mlipuko huo unapotokea
walikuwa tayari katika hatua ya
kubariki maji kwaajili ya uzinduzi wa
kanisa ulikuwa ukiongozwa na balozi
wa Papa Fransis.

Hata hivyo Padre Mangwangi
ameiambia BBC kuwa taarifa
walizonazo muda mfupi baada ya
majeruhi kukimbizwa hospitali watu
kati yao wamefariki huku wengine
wakiendelea kupatiwa matibabu katika
hospitali ya Mount Meru mjini
Arrusha.

Shughuli zote kuhusiana na ibada
hiyo zimesitishwa huku watalaalamu
wa milipuko na polisi wakiendelea na
uchunguzi kuhusiana na mlipuko
huo.

Bado hakuna taarifa zozote kuhusiana
na chanzo halisi cha bomu hilo ama
kundi lolote linalodaiwa kuhusika na
utegaji wa bomu hilo.

Hili ni shambaulio la kwanza la bomu
nchini Tanzania japo kuwa mwaka
huu pia kulikuwa na mtukio ya mauaji
ya Padre wa kanisa hilo visiwani
Zanzibar ambaye alipigwa risasi
wakati akiwa anajiandaa kuingia
kanisani.

Chanzo:BBC

Samatta, Kapombe na Yondani Wagombania Tuzo


WACHEZAJI mahiri wa timu ya
soka ya Taifa ya Tanzania
‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta
wa TP Mazembe, Kelvin
Yondani wa Yanga na Shomari
Kapombe wa Simba ya Dar es
Salaam, wametajwa katika
orodha ya wanaowania tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Tanzania
mwaka 2012.

Taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari jana na
Mwenyekiti wa Kamati ya
Tuzo za Wanamichezo Bora
wa Tanzania mwaka 2012
zinazotolewa na Chama cha
Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA),
Haji Manara, ilieleza kuwa
majina hayo ni mapendekezo
kutoka vyama mbalimbali kwa
ajili ya kuwania tuzo hizo kwa
kila mchezo.

Alisema hatua itakayofuata ni
kuchambua majina hayo kwa
ajili ya tuzo hizo ambazo awali
ilikuwa zifanyike Aprili 27
mwaka huu na sasa zitafanyika
mwezi ujao. Orodha kamili ya
wanaowania tuzo kwa mpira
wa magongo wanaume ni
Sylvester Kigodi, Casto
Mayuma, Gurtej Bilu Singh,
Vendri Bhamra na Elias
Samala.

Gofu ya kulipwa wanaume ni
Hassani Kadio, Yassin Salehe,
Fadhili Nkya, Salimu
Mwanyenza na Rajabu Iddy,
wakati gofu ya ridhaa
wanawake ni Madina Idd,
Angel Eaton, Hawa Wanyeche
na Ayne Magombe.

Wanaume ni Jimmy Mollel,
Frank Roman, Nuru Mollel,
Martin MacDonald na John
Said. Ngumi za ridhaa
wanaume ni Ismail Isack
Galiatano, Said Hofu, Selemani
Kidunda, Victor Njaiti,
Mohamed Chibumbui na
wanawake ni Sara Andrew,
Irene Kimaro, Easter Kimbe,
Mather George na Mariam
Nyerere.

Manara aliwataja wanaowania
upande wa ngumi za kulipwa
kuwa ni Francis Miyeyusho,
Ramadhan Shauri, Thomas
Mashali, Said Mbelwa na
Francis Cheka, huku judo kwa
Tanzania Bara wanaume ni
Ahmed Magogo, Andrew
Mlugu, Geophrey Mtawa,
Gervas Chilipweli, Abuu
Mcheteko na Abuubakar Nzige
na wanawake ni Matrida
Temba na Amina Mohamed.

Judo kwa wanaume Zanzibar
ni Mohammed Khamis Juma,
Masoud Amour Kombo na
Mbarouk Suleimani Suleiman,
wakati wanawake ni Grace
Alphonce na Laylati
Mohammed, huku tenisi
wanawake ni Rehema
Athumani, Vailety Peter,
Mkunde Iddi, Edna John na
Zuhura Baraka na wanaume ni
Omary Abdalah, Yassini
Shaabani, Hassan Kassim,
Kiango Kipingu na Lebric
Jacobu.

Mpira wa mikono kwa
wanaume na timu zao katika
mabano ni Faraji Shaibu
(Nyuki Zanzibar) Hemedi
Salehe na Abinery Kusena
(JKT), Ally Khamis (Ngome) na
Hassan Yusufu (Magereza),
wakati wanawake ni Catherine
Mapua (Ngome), Doris
Mangara (Magereza), Zakia
Mohammed (Ngome), Happy
Mahinya (JKT) na Mary Kimiti
(Magereza).

Riadha wanawake ni Zakia
Mrisho, Mary Naali, Jackline
Sakilu, Sarah Ramadhani,
Anjelin Tsere, Sara Maja,
wanaume ni Dickson Marwa,
Faustine Musa, Augustino Sule,
Bazil John na Samson
Ramadhan.

Kriketi wanaume
ni Abhik Patwa, Benson Mwita,
Sefu Khalifa, Issa Kikasi na
Riziki Kiseto, wakati
wanawake ni Monica Pascal,
Mwanaiddi Ibrahim, Hadija
Nasibu, Esther Wales na
Mwanaidi Ammy.

Soka wanawake ni Fatuma
Mustapha, Asha Rashid,
Mwanahamisi Omary, Sophia
Mwasikili na Ester Chabruma,
wanaume ni John Bocco
(Azam), Kelvin Yondani
(Yanga), Shomari Kapombe
(Simba), Mcha Khamisi
(Azam), Mbwana Samatta (TP
Mazembe).

Wachezaji wa nje wanaocheza
Tanzania ni Emmanuel Okwi-
Simba (sasa Etoile du Sahel),
Kipre Tchetche-Azam, Haruna
Niyonzima na Hamisi Kiiza,
wote Yanga na Mary Waya
(netiboli-alikuwa kocha
mchezaji).

Upande wa kikapu ni Faraja
Malaki (Jeshi Stars), Evodia
Kazinja (JKT Stars), Doritha
Mbunda (JKT) na Sajida Ahmed
(Don Bosco) wakati wanaume
ni Mussa Chacha, Lusajo
Mwaipopo na Erick Mchemba.

Netiboli ni Lilian Sylidion
(Filbert Bayi), Mwanaidi
Hassan (JKT), Irene Kanile
(Filbert Bayi), Jacqueline
Sikozi (Filbert Bayi), Faraja
Malaki (Jeshi Stars).

Wachezaji Bora Chipukizi ni
Salum Abubakari (Azam),
Frank Domayo (Yanga),
Edward Cristopher (Simba) na
Emmanuel Malya tenisi Arusha,
wakati Watanzania
wanaocheza nje ni Mbwana
Samatta (TP Mazembe), Ivo
Mapunda (Gor Mahia),
Hasheem Thabeet (Oklahoma),
Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe), Soud Abdulrazak
na Mohammed Abdallah
‘dulah’ (wote Uganda).

Chanzo:Habari Leo

Waziri Membe: Movement 23 Hawatutishi

Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano na Kimataifa Bernard Membe,
amesema kuwa kamwe Tanzania  haitaogopa
vitisho vinavyotolewa na Kikundi cha Waasi cha
M23 cha DRC, huku akitoa masharti matatu kwa
kikundi hicho kama hakitaki majeshi ya
Tanzania yaende nchini humo.

Membe alisema hayo, akijibu hoja iliyotolewa na
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa kikundi hicho kimeandika barua ya wazi ikieleza kuwa,
kisilaumiwe kama raia wa Tanzania watapatwa na mauaji ya halaiki ikiwa vikosi vya majeshi yake
vitaenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Katika barua hiyo kiongozi huyo ametishia kwamba kikundi cha M23 kisilaumiwe kwa mauaji ya halaiki
yatakayotokea kwa raia wa Tanzania endapo Serikali itaendelea na mpango wa kupeleka askari wake
kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Congo DRC,” ilisema hotuba ya
kambi ya upinzani.
“Katika barua hiyo kiongozi huyo ametishia kwamba kikundi cha M23 kisilaumiwe kwa mauaji ya halaiki
yatakayotokea kwa raia wa Tanzania endapo Serikali itaendelea na mpango wa kupeleka askari wake
kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Congo DRC,” ilisema hotuba ya
kambi ya upinzani.

Akijibu hoja hiyo, Membe alikiri kuiona barua hiyo, aliyosema ilielekezwa kwake pamoja na Bunge na
kusema kuwa lengo lake ni kutoa vitisho kutokana na kuogopeka kwa vikosi vya Tanzania.

“Kuhusu M23 nimepata barua wizarani na bungeni imeletwa, hiyo barua wanasema imeandikwa kwangu
na Mungu na kuwa imesainiwa na Mungu, hawa wanatutisha kama  tulivyotishwa na Kanali Mohamed
Bakari alipokuwa ameiteka Anjwani, pamoja na vitisho vyote alivyotoa yeye ndiye aliyeishia kutoroka
akiwa amevaa baibui,” alisema na kuongeza:
“M23 wanaua, wamebaka, wamedhalilisha wazee na mama, wameleta wimbi la wakimbizi zaidi ya
220,000, halafu wanamnukuu Mwalimu Nyerere wakisema binadamu wote ni sawa, huko ni kukufuru
Kama wangekuwa wanathamini kauli ya Mwalimu wasingeliua, wasingebaka, wasingedhalilisha wazee.”
Alibainisha kuwa, waasi wa kikundi hicho wamefanya uhalifu wa kutisha hadi kiongozi wao Bosco
Ntaganda akaamua kujisalimisha kwenye vyombo vya usalama na kwa sasa amepelekwa katika
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC.

“Kwa hiyo M23  hawawezi kutufundisha ubinadamu, hawawezi kutufundisha amani na wala hawawezi
kutumia jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kutuambia kitu kuwa binadamu wote ni sawa,”
alisema.

Alisema kuwa, vikosi vitakavyokwenda DRC vitakuwa na kazi ya kutekeleza mambo matatu akitaja la
kwanza kuwa ni  kuhakikisha M23 hawajipanui kutoka idadi ya 600 waliopo sasa,  kudhoofisha kundi hilo
kwa kuondoa silaha mikononi mwao pamoja na kutengeneza uhusiano.
“Ni vizuri,  wale askari  tutakaowaona wapo bora waingie kwenye Jeshi la Taifa la DRC ili kuleta amani
pale na tutalinda amani pale. Wakituchokoza tutajibu mapigo, lakini lengo la kwenda pale siyo kupigana
vita.

Sisi tunaenda na mandate (mamlaka) ya Umoja wa Mataifa ‘chapter’ 7 ya Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa,” alisema.
Aliongeza: “Jeshi letu ni imara sana, lenyewe halishindwi lipo Lebanon linafanya kazi nzuri na ya
kusifiwa. Lipo Darfur la linafanya kazi nzuri ya kustahili kusifiwa; na Watanzania wajue kuwa ‘United
Nation Mission ya Darfur’ sasa inaongozwa na jenerali Mtanzania kuanzia mwezi huu, kutokana na rekodi nzuri ya jeshi letu la Tanzania

Ndiyo maana hao wanaobaka na kuua wakisikia
tu Tanzania wanakwenda wanamsingizia Mungu,
eti Mungu anawaunga mkono na Mwalimu
Nyerere anawaunga mkono!”

“Wanataka Bunge hili liseme Serikali isipeleke
askari. Nalipongeza Bunge kwa uelewa mpana
na kuungana kuwa kitu kimoja tunapokabiliana
na vitisho vya aina hii.

Tanzania tuna nguvu, tuna historia, wakitaka M23 tusiende kule Alitaja mambo hayo kuwa ni; “Moja,
wafanye kama walivyofanya jana,(juzi) waanze kujitoa kwenye jeshi lile na kujisalimisha.
Pili,  yapo mazungumzo yanayofanywa na Rais Museveni Kampala ya kuitaka M23 pamoja na majeshi na
Serikali ya DRC kukaa na kumaliza tofauti zao basi wamalize tofauti zao na kisha watupigie simu
kwamba wameshayamaliza matatizo yote.”

Sharti la tatu ambalo Membe alitoa kwa kikundi hicho ni kutaka kikundi hicho kuacha mara moja vitendo
vyao vya  kubaka, kuua na kuwafanya wananchi kuwa wakimbizi Kuhusu suala la Malawi, alisema:

“Mazungumzo yataanza rasmi kwa maana ya kuitwa kuhojiwa sisi akiwemo Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.

Mwishoni mwa mwezi huu ataenda Maputo, watakuwa wanahojiwa, ni imani  yetu Watanzania
kwamba jopo  la marais wastaafu linaloongozwa na Joachim Chisano litafikia uamuzi.”
“Lakini ikishindikana itabidi tusonge mbele kwenda ICJ, Tanzania hatutasita kufanya hivyo na tuna kila
aina ya ushahidi wa kuhakikisha kwamba tunashinda kesi hiyo,” alisema Membe.

Source:Mwananchi.co.tz

Tamko La Rais Jakaya Kikwete Juu Ya Mlipuko Wa Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amepokea kwa
mshtuko na masikitiko makubwa
taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei
5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa
Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la
Olasiti Jijini Arusha.

Tukio hilo la
kigaidi limesababisha mtu mmoja
kupoteza maisha na wengine 40
kujeruhiwa. Rais Kikwete analaani
vikali shambulio hilo lililofanywa na
mtu au watu katili, waovu na wenye
dhamira mbaya na nia mbaya kwa
Tanzania na watu wake.

Rais Kikwete ameagiza vyombo vya
usalama nchini kumsaka mtu au
watu waliohusika na kitendo hicho
kiovu na kuwafikisha kwenye
vyombo vya sheria.

Vile vile Rais
Kikwete amewataka wananchi wote
kuwa watulivu wakati Serikali na
vyombo vyake inaendelea kufuatilia
tukio hili. Tutawasaka popote walipo
na kupambana nao bila huruma.

Aidha, tutakabiliana na aina yoyote
ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au
aina yoyote ya uhalifu wa namna
hiyo au wa namna nyingine, uwe na
chimbuko lake ndani ya nchi ama
nje ya nchi yetu.

Kamwe
hatutakubali kuwaacha wavuruge
amani na usalama wa Tanzania na
watu wake. Rais anaamini kuwa
Serikali, kwa msaada na ushirikiano
wa wananchi, watu hao
watapatikana na kuadabishwa
ipasavyo.

Aidha, Rais Kikwete anatoa
rambirambi za dhati ya moyo wake
kwa wafiwa na wale wote ambao
wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Anaungana nao katika machungu
na msiba.

Rais pia anawaombea
wote walioumia katika tukio hili
wapate nafuu ya haraka na
waendelee na shughuli zao za
ujenzi wa taifa.

Rais Kikwete vilevile anatoa pole
nyingi kwa viongozi na waumini wa
Kanisa Katoliki kwa tukio hili la
kusikitisha na kuvurugika kwa ibada
na shughuli yao muhimu ya
uzinduzi wa Kanisa lao.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
5 Mei, 2013

Babu Wa Loliondo anaswa Bank

Katika kuonesha kuwa Mchungaji
Mstaafu, Ambilikile Mwasapile ‘Babu
wa Loliondo’ bado ana fedha baada
ya kuzikusanya kutoka kwa wateja
wake wa huduma ya kikombe, hivi
karibuni alinaswa ndani ya Benki ya
NMB akipata huduma.

Babu alibambwa ndani ya benki
hiyo Tawi la Loliondo mkoani
Manyara akihudumiwa na mmoja
wa wafanyakazi aliyefahamika kwa
jina la Lembris Lesion ambapo
inaelezwa alikuwa akielekezwa jinsi
ya kujiunga na huduma mpya ya
Jisevie.

Akiwa benki hapo, Babu alionekana
akijaza fomu huku akiwa na begi
ambalo linashukiwa kuwa na fedha
ndani yake ambapo baadhi ya watu
waliokuwa wakimpiga chabo
hawakuonesha kumshangaa
wakiamini bado ana mkwanja wa
kutosha kutokana na ile tiba
ailiyokuwa akiitoa kwa watu wengi
hivi karibuni.

“Unajua Babu alipata pesa nyingi
sana na bado anaendelea
kuzikusanya, kimsingi ana pesa
ndefu benki,” alisema mmoja wa
wateja aliyekuwa eneo hilo.

Source: udakuspecial

Mlipuko Wa Arusha

Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa mtu mmoja amekufa kwenye mripuko uliotokea katika ufunguzi wa kanisa la Katoliki la Olasiti, kwenye kitongoje cha Arusha, Tanzania.
Watu kama 50 wamejeruhiwa. Makamo wa rais wa Tanzania, Dr. Mohamed Gharib Bilal amewasili Arusha kwenda kupeleka pole ya serikali kwa viongozi wa kanisa na majeruhi.
Dr. Bilal alisema serikali ya Tanzania itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa inawapata watu waliohusika na mripuko huo. Mtu mmoja amekamatwa lakini haikuelezwa ni nani au kama amehusika na kundi lolote.

Mchina Agongwa na Gari na Kufariki

RAIA wa China aliyetambuliwa kwa jina la Ruo Yaowu (34) amekufa papo
hapo baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela
alithibitisha hayo jana na kusema kuwa, ajali hiyo ilitokea juzi saa
7:00 usiku katika barabara ya Bagamoyo eneo la Boko, Kinondoni.

Alisema gari namba T865 AHB aina ya Toyota Canter, likiendeshwa na mtu
asiyefahamika akitokea Bunju kwenda Tegeta, alimgonga mtu huyo ambaye
alikufa papo hapo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili na msako wa kumtafuta dereva aliyekimbia baada ya
ajali unaendelea.

Katika tukio jingine, maiti moja ya mwanaume aliyetambuliwa kwa jina
moja la Chalii anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 15 ba 20,
imekutwa ikiwa imelala pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi alisema tukio
hilo ni la juzi saa 4:10 usiku katika eneo la Ferry, wilaya ya Ilala.

Maiti hiyo ilikutwa ikiwa pembezoni huku ikiwa haina jeraha lolote
isipokuwa ilikuwa inatoka damu mdomoni na puani. Chanzo cha kifo chake
hakijafahamika na maiti imehifadhiwa hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wanafunzi Waua Mwizi

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Ntuchi wilayani Nkasi mkoani Rukwa
wanadaiwa kumuua kwa kumpiga mkazi wa kijiji cha Ifundwa wilayani
hapa, Ignas Maruku (29) wakimtuhumu kuingia kwenye bweni la wanafunzi
wa kike na kuiba nguo zao mbalimbali, zikiwemo nguo za ndani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda amemweleza mwandishi wa habari
hizi kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 25 mwaka huu saa 6.00mchana
wakati wanafunzi hao wakiwa darasani.

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Mwaruanda alisema siku hiyo, mmoja wa
wanafunzi hao wakike ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja
akiwa nje ya madarasa karibu na bweni lao alimwona kijana huyo
akiingia bwenini mwao hivyo alimshtukia na kuanza kupiga kelele.

Inadaiwa ndipo wanafunzi hao wa kike na wa kiume walipotoka darasani
na kuanza kumfukuza mwizi huyo kisha kumkamata na kuanza kumshambulia
kwa mawe, marungu na fimbo hadi akazimia.

Wakati wanafunzi hao wakimsulubu mwizi wao huyo ndipo walimu wao
walipoacha shughuli zao zote shuleni hapo na kukimbilia eneo la tukio
na kuamuru wanafunzi hao watawanyike na kuacha kumpiga mtuhumiwa huyo,
warejee madarasani.

Kwa mujibu wa Mwaruanda, walimu hao walitaarifu polisi ambao kwa
kushirikiana nao walimkimbiza mtuhumiwa huyo katika Hospitali Teule ya
Wilaya hiyo mjini Namanyere, lakini alifariki dunia wakati akipata
matibabu hospitalini hapo.

Kamanda Mwaruanda amedai kuwa mwalimu wa shule hiyo aliyetambuliwa
kuwa Thobias Ndunguru (26) na mkazi wa kijiji hicho cha Ntuchi, Simon
Osayi wanashikiliwa na Polisi kwamahojiano kuhusu mauaji hayo, lakini
hakuna mwanafuzi yeyote anayeshikiliwa hadi sasa huku uchunguzi zaidi
wa tukio hilo ukiendelea.

Azikwa Akiwa Hai

Mbeya. Msaidizi wa zamani wa Padri (Katekisita) katika Kigango cha
Kanisa Katoliki Kijiji cha Mkwajuni, Florian Mwamosi (70) amekufa
baada ya kuzikwa akiwa hai katika kaburi moja na mtu anayedaiwa kumuua
kwa njia ya kishirikina.
Tukio hilo limetokea katika Kitongoji cha Maweni kijijini hapo
wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alikiri kutokea kwa
tukio hilo akieleza kuwa lilitokea saa 9:00 mchana katika kijiji
hicho cha Maweni Mkwajuni wilayani Chunya.

"Marehemu aliuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa na mawe
kwa tuhuma za kuhusika na uchawi na kusababisha kifo cha Peter
Robert," alisema.

Kamanda Athumani alisema kuwa uchunguzi kuhusiana na tukio hilo
unaendelea na kwamba wahusika wote wa tukio hilo wamekimbia na
kuzihamanyumba zao, hivyo polisi wanaendelea na msako wa kuwatia
mbaroni watuhumiwa na kwamba tayari kaburi hilo limefukuliwa jana
kutenganisha maiti hizo.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa marehemu huyo ambaye alikuwa
akituhumiwa kwa ushirikina aliwahi kuwa Katekista wa kigango hicho
hadi mwaka 2007.

Wameeleza kuwa Mwamosi alikwenda kuhudhuria mazishi ya Peter Robert
(28) katika kitongoji hicho cha Maweni, baada ya kufuatwa nyumbani
kwake na watu wakitaka aende kwa sababu yeye ni mmoja wa wazee wa mila
katika kitongoji hicho.

"Bwana Mwamosi alikuwa akituhumiwa kwa uchawi kwa muda mrefu na wenzie
wawili, hivyo alipofika makaburini ilianza minong`ono ya watu na huku
wengine wakiguna na ndipo alipoombwa aingie kaburini kwa ajili ya
kupokea jeneza lililobeba mwili wa marehemu Peter Robert," alisema
mkazi mmoja wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Joseph.

Alisema kuwa baada ya kuingia kaburini akiwa na watu wengine watatu
wenzake walitoka kwa haraka na kumwacha Mwamosi peke yake ndipo kundi
la watu waliokuwa eneo hilo la makaburi walianza kumshambulia kwa
kumpiga mawe huku wakimwamuru akae chini.

Shuhuda huyo alisema kuwa baada ya kukubali kukaa chini akiwa ndani ya
kaburi hilo, walianza kumfukia naalipofukiwa nusu ya mwili wake
waliingiza jeneza la marehemu Peter na kuliweka juu yake na kuanza
kulifukia kaburi hilo.

"Baada ya kukaa chini ndani ya kaburi hilo ndipo walianza kumfukia kwa
udongo na baadaye wakachukua jeneza la marehemu na kuliweka juu yake,
kisha kumfukia na udongo na taratibu za mazishi ziliendelea kwa ajili
ya marehemu Peter,"alisema.

Alidokeza kuwa chanzo cha tukio hilo ni marehemu Robert kuugua ghafla
tumbo, ndipo ndugu zake walipoamua kumpeleka kwa mganga wa jadi kwa
ajili ya kupata matibabu na baada ya siku tatu alifariki dunia.

Kamanda huyo amewasihi wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuacha tabia kama hizo
kwani kufanya hivyo ni kuuchafua mkoa na kuwa na sifa mbaya, hivyo
kusababisha maendeleo ya mkoa kurudi nyuma.
Januari 12, mwaka huu wakazi wawili wa Kijiji cha Karungu, Kata ya
Ivuna, Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya walikufa baada ya kufukiwa wakiwa
hai katika kaburi moja na marehemu wanaodaiwa kumuua, tukio
linalohusishwa na imani za kishirikina.

Chanzo:Mwananchi

Godbless Lema Akamatwa

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekamatwa na Polisi usiku wa
kuamkia jana, eneo la Njiro jijini hapa. Ukamataji huo haukuhusisha
matumizi ya nguvu dhidi ya Mbunge huyo, bali mkewe alimsindikiza hadi
makao makuu ya Polisi kutoa maelezo kuhusu tukio la vurugu katika Chuo
cha Uhasibu juzi.

Kukamatwa kwa Lema ambaye ni Mbunge wa Chadema, kulithibitishwa jana
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas, akisema polisi
walimkamata saa 9 alfajiri na hadi jana alikuwa akiendelea kuhojiwa na
kesho kutwa atafikishwa mahakamani kwa madai ya kusababisha
vuruguhizo.

"Tumemkamata na anahojiwa kuhusu vurugu zilizotokea chuoni juzi na
bado tunaendelea na uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi Henry Koga (22)
aliyeuawa, lakini hatukutumia nguvu kumkamata na naomba watu watii
sheria bila shuruti," alisema Kamanda.

Aliongeza kuwa baadhi ya watu wanaojikusanyakwenye vikundi eneo la
Polisi ni vema watii sheria bila shuruti badala ya kuleta fujo hivyo
watulie ili polisi wafanye kazi zao.

Awali wafuasi wa chama hicho walionekana maeneo ya makaburini wakiwa
makini kusikilizakama Lema atapewa dhamana au la, lakini hadijana
mchana alikuwa akiendelea kuhojiwa na Polisi akiwa na wakili wake
ambaye polisi hawakumtaja jina.

Juzi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alisisitiza kuwa hawezi
kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Lema wa kutaka kumbambikiza kesi bali
yeye ni kiongozi wa wananchi na anatimiza wajibu wake
kuhakikishausalama unakuwapo.

Mulongo alitoa kauli hiyo kutokana na madai ya Lema kwake kuwa
alimtumia ujumbe huo wa maandishi kwa njia ya simu ukimtishia
kumbambikia kesi. Mkuu wa Mkoa aliwapa polewanafunzi wa chuo hicho
ambao walikusanyika katika hospitali ya Mount Meru kuaga mwili wa Koga
na kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa maziko.

Mbowe ahadharisha Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,
ameihadharisha Serikali juu ya kukamata viongozi kwamba hali hiyo
isipodhibitiwa nchi inaweza kuchafuka. Alikuwa akizungumzia kukamatwa
kwa Lema na kufunguliwa mashitaka ya uchochezi na kuongeza kuwa
kukamatwa huko hakukuwa halali, kwa kuwa alikuwa akitimiza wajibu wake
wa ubunge.

"Napenda kuwasilisha masikitiko ya chama changu kwa Polisi Arusha
kwanza kutumia nguvu kwa kuzingira nyumba ya Lema usiku wamanane na
kumkamata kwa nguvu kama jambazi jambo ambalo halikuwa la lazima,"
alisema.

Alisema Lema alikumbwa na kadhia hiyo baadaya kuingilia kati vurugu
katika chuo cha Uhasibuambazo chanzo chake ni kuuawa na vibaka na
kuporwa kwa mwanafunzi wa chuo hicho.

"Kulitokea vurugu wanafunzi waliandamana wakitaka kuongezwa ulinzi,
Lema akiwa mbunge wa Arusha, alikwenda kuwatuliza na akiwa huko
akamwita Mkuu wa Mkoa wa Arusha wasaidiane, sasa Mkuu huyo akaharibu
wanafunzi wakazidisha jazba, wao sasa wanamkamata mbunge!" alishangaa.
Alisema pamoja na kukamatwa Lema, chama kinasikitishwa na polisi
kumvamia nyumbani usiku.

"Huyu hakuwa jambazi, kulikuwa na umuhimu gani wa kuzingira nyumba
yake na kumtaka atoke, huyu mbunge jamani ana watoto tena mmoja ana
mwaka mmoja na nusu, huku ni kumdhalilisha."

Alilitaka Jeshi la Polisi Arusha, kumpa Lema haki yake kwa kuwa
mashitaka yanayomkabili yanaruhusu dhamana na si haki kuzuia watu wake
wa karibu hadi wanasheria kumsaidia.

"Mimi naomba tu, huu utaratibu wa kukamata viongozi mara kwa mara
uangaliwe kwani utaligharimu Taifa, tuepuke kuingiza masuala ya
itikadi kwenye mambo ya usalama wa taifa, tukiendelea hivi nchi
inaweza kuchafuka," alisisitiza.
Taarifa zilizopatikana baadaye kutoka kwa Kamanda Sabas zilisema Lema
anatarajiwa kufikishwa mahakamani keshokutwa ambapo ataunganishwa na
watuhumiwa wenzake 14 waliofikishwa mahakamani juzi.


chanzo: habarileo

Vigogo Ardhi Wafikishwa Mahakamani

Dar/Korogwe. Maofisa waandamizi serikalini wamefikishwa katika
Mahakama tofauti Dar es Salaam na Korogwe jana wakituhumiwa kwa
makosa ya matumizi mabaya ya ofisi na kuhujumu uchumi.
Maofisa hao wanatoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri ya Wilaya ya
Korogwe.
Kesi ya Dar
Mpimaji wa Wizara ya Ardhi, Revocatus Wachawendera na Mpimaji wa
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Steven Kongwa walifikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka
mawili, likiwamo la matumizi mabaya ya ofisi. Kongwa aliwahi kuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke na alistaafu miaka miwili
iliyopita.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Wakili Hussein Mussa jana alidai mbele ya Hakimu Mkazi,
Augustina Mmbando kuwa washtakiwa hao walifanya makosa hayo kati ya
Januari 2000 na Desemba 2001. Akisomahati ya mashtaka yanayowakabili
washtakiwa hao, Wakili Mussa alidai kuwa washtakiwa hao kwa
pamojawakiwa waajiriwa wa ofisi ya umma, walitumia madaraka yao
vibaya.
Alisema walikiuka mamlaka ya ofisi zao kwa kugawa eneo la wazi
lililopo Mbezi ambalo lilitengwa kwa ajili ya bustani kinyume cha
sheria. Wakili Mussa alidai katika shtaka jingine kuwa maofisa hao kwa
pamoja walikiuka Kifungu cha 35 cha Sheria ya Mipango Miji Sura ya 355
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kuligawa eneo hilo.

Alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja katika kipindi hicho cha Januari
2000 na Desemba 2001 wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es
Salaam, kwa makusudi walikiuka sheria hiyo ya mipango miji na kugawa
eneo la Mbezi Kitalu L bila ya kupata kibalikutoka mipango miji. Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana na Wakili Mussa
alisema upelelezi umekamilika, hivyo aliiomba Mahakama kuipangia kesi
hiyo siku nyingine ili kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Ili kupewa dhamana, Hakimu Mmbando aliwataka kila washtakiwa kila
mmoja wao kuwa na mdhamini anayeaminika ambaye anafanya kazi katika
taasisi inayotambulika kisheria.
Sharti jingine ni la kila mdhamini kusaini bondi ya Sh10 milioni.
Washtakiwa walikamilisha masharti hayona kesi yao imeahirishwa hadi
Mei 20, mwaka huu.
Kesi ya Korogwe
Takukuru wilayani Korogwe imewashtaki vigogo watatu kwa makosa manne
likiwamo la kuhujumu uchumi na kusababishia hasara ya Sh56 milioni
kwenye Halmashauri ya Korogwe mkoani Tanga.
Mwendesha mashtaka wa Takukuru, George Magoti alimsomea mashtaka
mshtakiwa wa pili tu, Declley Nyato.
Mshtakiwa wa kwanza, ambaye ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri wa
wilaya hiyo, Christine Midello na mshitakiwa wa tatu, Ofisa Ardhi wa
Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Emmanuel Ntatiye hawakuwapo mahakamani.
Mbali na kumsomea mashtaka, Magoti aliiomba Mahakama ya Wilaya ya
Korogwe kutoa hati zitakazowezesha kukamatwa kwa washtakiwa hao
wengine.
Magoti aliiambia Mahakama kuwa kati ya Julai na Agosti mwaka 2011,
Nyato na wenzake walitumia nyadhifa zao vibaya kwa kuidhinisha malipo
ya Sh15 milioni kwa Kampuni ya Concise pasipo kuishirikisha Bodi ya
Zabuni.
Katika kosa la pili, Nyato anadaiwa kuruhusu kufanyika kwa malipo ya
Sh41,050,000 kwa Kampuni ya Concise Geo Solution bila ya kuishirikisha
bodi ya zabuni na shtaka la tatu, wote wanatuhumiwa kupanga njama za
kutenda kosa namba moja na mbili.

Shitaka la nne ni la kuhujumu uchumi. Wote kwa pamoja wanadaiwa
kuisababishia Halmashauri ya Mji wa Korogwe, hasara ya Sh56,185,000 na
kuvunja Sheria ya Kuhujumu Uchumi.
Nyato aliyakana mashtaka yote. Hakimu Arnold
Kirekiano aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 7, mwaka huu baada ya kutoa
masharti likiwamo la kuwa na mdhamini mmoja, ambaye ni mwajiriwa wa
umma au shirika linalotambuliwa ambaye ana makazi ya kudumu Korogwe au
fedha taslimu Sh9.4 milioni au hati ya mali isiyohamishika au maelezo
yatakayothibitisha mali hiyo aliyonayo mdhamini ina thamani sahihi
iliyotajwa na kusalimisha pasi za kusafiria mahakamani.



Chanzo: Mwananchi.co.tz

Vurugu zazuka Liwale Na Arusha

Liwale/Arusha. Uharibifu mkubwa wa mali ulifanywa juzi usiku Mjini
Liwale, Lindi baada ya wananchi wenyehasira kuchoma moto nyumba za
viongozi waandamizi, makao makuu ya Halmashauri ya Wilayana maghala ya
mazao kutokana na kuchukizwa kushushwa kwa bei ya korosho.
Nyumba zilizochomwa moto ni za Mbunge wa Liwale (CCM), Faith Mtambo,
Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Umoja, Hassan Myao na Makamu wake,
Hassan Mpako, Diwani wa Viti Maalumu (CCM) Liwale,Amina Mnocha,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Abbas Chigogola ambaye
pia ng'ombe wake tisa walikatwakatwa mapanga na kuachiwa ndama watatu.
Nyingine ni nyumba ya Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Liwale, Mohamed
Ng'omambo, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Lindi, Mwenyekiti wa Chama
cha Msingi Minali, Mohamed Limbwilindi na Katibu wa chama hicho, Juma
Majivuno.
Wakati hayo yakitokea Lindi, huko Arusha, vurugu kubwa za wanafunzi wa
Chuo cha Uhasibu zilizuka jana baada ya kuuawa kwa mwanafunzi Henry
Kago (22), juzi usiku.
Kago, ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili,anadaiwa kuwa
alifariki juzi saa nne usiku baada ya kuchomwa kisu na watu
wasiojulikana, akiwa njiani eneo la Kanisa la Wasabato akitokea chuoni
hapo kujisomea.
Ghasia za Liwale
Ghasia hizo zilianza juzi mchana katika Kijiji cha Liwale B na
ziliendelea usiku kucha hadi jana asubuhi.
Watu walioshuhudia ghasia hizo walisema chanzo ni wakulima kudai
kulipwa Sh600 na siyo Sh200 za mauzo ya korosho kwenye Chama cha
Msingi Minali.
Bei ya kilo moja ya korosho waliyokubaliana wakulimana chama hicho ni
Sh1,200 na mara ya kwanza kiliwalipa Sh600 kwa kilo na kuahidi kulipa
nusu nyingine baadaye.
Hata hivyo, viongozi wa Ushirika walibadili uamuzi na kulipa Sh200 kwa
maelezo kuwa mauzo hayakuwa mazuri kitendo ambacho kiliwakasirisha
wakulima haoambao waligoma kupokea fedha hizo.
Baadaye ilielezwa kuwa viongozi wa Minali walipeleka fedha hizo polisi
ili malipo yafanyike huko, lakini ghasia zikaibuka na wakaamua
kusitisha malipo hayo na ndipo wananchi wakaamua kuingia mitaani.
Mmoja wa mashuhuda alisema "Polisi walijaribu kuwadhibiti watu hao,
lakini walipoona wanazidiwa nguvu, wakawaachia wafanye wanavyotaka
ndiyo maana kumekuwa na uharibifu mkubwa."
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga alisema kwa kifupi:
"Hali imetulia na vurugu zimemalizika lakini bado tuko kwenye kikao
kuzungumzia suala hili."
Wakulima hao walikerwa na tamko la Limbwilindi ambaye ndiye aliyetamka
kwamba watalipwa Sh200 kwa kilo na kuamua kwenda kuchoma moto nyumba
yake na baadaye ya Katibu wake Majivuno.
Limbwilindi hakupatikana kuzungumzia tukio hilo lakini, Majivuno
alipohojiwa alisema: "Tulikubaliana kuwalipa Sh1,200 kwa kila kilo,
lakini kwa awamu.
tuliwapa Sh600 awali na nusu yake imeshindikana kwakuwa mauzo hayakuwa
mazuri. Biashara haikwenda vizuri, ndiyo maana tukawaambia tutawalipa
Sh200 lakini wakakataa wanataka fedha zote Sh600, sasa sisihatuna
fedha hizo. Kama biashara ingefanyika kwa faida tungewalipa."
Habari zilizopatikana baadaye jana zilidai kuwa mke wa Mkungura, Amina
Mmoto amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Liwale baada ya kupata
shinikizo la damu kutokana na sakata hilo.
Akizungumza kwa simu kuelekea Liwale, Mbunge Mtambo alisema:
"Nimesikitishwa na ghasia hizi... wamenitia hasara kubwa. Nyumba zangu
zote mbili zimechomwa, sijui nitaishi wapi. Hakuna kingine hizi
nisiasa tu...hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo. Kama ni kulipwa
Sh200, mbona vyama vingine wamelipwa fedha hizo na hakukuwa na vurugu?
Jana kutwa nzima, Mji wa Liwale ulikuwa na utulivu huku polisi
wakitawanya makundi ya watu waliokuwa katika vikundi kwa mabomu ya
machozi na shughuli za biashara zilisimama na hakuna maduka wala
magenge yaliyofunguliwa.

Vurugu Arusha
Kutokana na vurugu hizo, Chuo cha Uhasibu cha Arusha, kimefungwa kwa
muda usiojulikana kwa usalama huku wanafunzi wakitakiwa kuondoka
chuoni hapo hadi watakapotangaziwa tena.
Licha ya kuelezwa kwamba aliuawa kwa kisu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Magesa Mulongo alisema taarifanyingine, zinaeleza kuwa aliuawa
akitokea katika Ukumbi wa Disko wa Bugaloo jirani na chuo hicho.
Baada ya taarifa za kifo hicho, wanafunzi wa chuo hicho walikusanyika
jana asubuhi na kuanza maandamano hadi Kituo Kikuu cha Polisi
wakilalamikia ulinzi duni.
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alifika na kuwatuliza
wanafunzi hao na kuzungumza nao, kwa zaidi ya saa tatu wakati
wakimsubiri Mkuu wa Mkoa.
Hata hivyo, baada ya kufika chuoni hapo, mkuu huyo wa mkoa alishindwa
kuzungumza kutokana na kutokuwa na kipaza sauti na kusababisha
wanachuo kumzomea kabla ya uongozi wa chuo kubadili eneo la mkutano.
Hata hivyo, zomeazomea iliendelea na mkutano kuvunjika na FFU kufika
na kurusha mabomuya machozi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kumalizika kwa
Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na uongozi wa chuo hicho, mkuu
huyo wamkoa alisema polisi wanafanya uchunguzi wa suala hilo.

"Baada ya kuletewa taarifa za tukio hili na Mbunge
Lema, niliondoka na kwenda kuwasikiliza wanachuo lakini tayari nilijua
mazingira yalikuwa yamebadilishwana pale nikagundua Lema ndiyo amekuwa
msemaji mkuu badala ya uongozi wa chuo au Serikali ya wanachuo. Ndiyo
maana mkaona na zomeazomea ile," alisema Mulongo.
Alimtuhumu mbunge huyo uchochezi na ameamuru kukamatwa kwake na
wanafunzi waliohusika na vurugu zile.

Lema alieleza kusikitishwa na agizo la kutakiwa kukamatwa akisema
alizuia maandamano kufika mjini...
"Nyie waandishi wa habari mlikuwepo nimezungumza zaidi ya saa mbili na
wale wanafunzi kuwasihi watulie wasiandamane na mimi ndiye nilimpigia
simu Mkuu wa Mkoa aje kuwasikiliza wanafunzi iweje niwachochee kufanya
fujo? Ninawasubiri waje wanikamate."


Chanzo: Mwananchi

Ubalozi Wa Ufaransa Washambuliwa

Bomu limelipuka nje ya ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa Libya,
Tripoli na kuwajeruhi walinzi wawili huku ikisababisha uharibifu
mkubwa.
Mlipuko huo ulisababisha uharibifu katika sehemu moja ya ofisi hizo na
pia kuharibu nyumba jirani.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli, Rana Jawad anasema kuwa inaaminika
kuwa mlipuko huo ulisababishwa na gari lililokuwa na mabomu.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, aliitaka serikali ya Libya
kuchukua hatua za haraka kukabiliana na waliosababisha shambulio hilo.
Aliongeza kwamba shambulizi hilo lililenga nchi za kigeni
zinazopambana dhidi ya ugaidi.

Balozi za kigeni nchini Libya zimewahi kushambuliwa katika siku
zanyuma, lakini hili ndilo shambulizi la kwanza kubwa dhidi ya ubalozi
wa kigeni mjini Tripoli.

Shambulizi liliwahi kufanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini
Benghazi mwezi Septemba mwaka jana na kusababisha kifo cha balozi
Christopher Stevens pamoja na maafisa wengine wamarekani.
Shambulio la leo lilifanyika muda mfupi baada ya saa kumi na
mojaasubuhi katika mtaa wa kifarahari mjini Tripoli.

Wakaazi wa eneo hilo walighadhabishwa sana na shambulizi hilo na
kulalamikia ukosefu wa ulinzi mzuri wa sehemu hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Libya, Mohammed Abdel Aziz alilaani vikali
shambulizi hilo, ingawa hawajaeleza ni nani wanayemshuku kulifanya.

Chanzo:BBC

Ubovu Wa MiundoMbinu

Hii ni barabara Inayounganisha Mkoa wa Tabora na Katavi, Hali imekuwa
korofi baadhi ya maeneo na kusababisha magari kushindw kupita na
kusababisha msururu kusubiri kukwamua Magari yaliyo Kwama, Kabla ya
Eneo la Ipole ambako ujenzi wa Daraja Unaendelea hali ni mbaya na pia
katika Eneo mbele kidogo ya Mji wa Inyonga mkoani Katavi. Juhudi za
Hali zinahitajika kuokoa usafiri wa unaunganisa Mikoa hii ya
Magharibi. Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa

Wamaasai Wa Loliondo, Serikali Inafikiria Nini?

Katika kijiji kimoja Kaskazini mwa Tanzania, ndege aina ya Boeing 747
zinatua kwenye kiwanja binafsi, magari yenye nambari za usajili za
milki za kiarabu, zikiendeshwa katika eneo hilo na yeyote mwenye simu
ya mkononi anapotua hapo hupokea ujumbe ambao haukutarajiwa:
''Hujambo mgeni na karibu UAE.''

Kwa karne nyingi, (Savanna) katika eneo la Arusha lilikuwa makao kwa
watu wa jamii ya wamaasai lakini siku hizi mtu sasa anaweza kudhania
yuko Dubai moja ya nchi za milki za kiarabu.

Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya ardhi mjini Arusha hasa katikaeneo
la Loliondo karibu na mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Serengeti
imekodishwa kwa kampuni ya uwindaji ya Emirati iitwayo Ortello
Tangu mwaka 1992, kampuni hiyo imekuwa ikiwapeleka kwa ndegewatalii
matajiri zaidi kuwinda simba na wanyama wengine hali
iliyowaghadhabisha wenyeji wa eneo hilo ambao ni wamaasai ambao
wamezuiwa kuwalisha mifugo wao katika maeneo ya kuwinda.

Sasa serikali ya Tanzania inataka kutoa ardhi zaidi kwa wawindaji hao
kwa lengo la kujenga barabara ya umbali wa kilomita 1,500 ambako
wanyamapori watakuwa wakipita kwa manufaa ya kampuni hiyo ya uwandaji.
Mpango huo utawaathiri takriban watu 30,000 watakaoachwa bila makao na
pia kuwaathiri maelfu ya wengine, ambao huwalisha mifugo wao katika
maeneo hayo wakati wa msimu wa kiangazi.
Wamaasai wameghadhabishwa mno na hata kufanya maandamano, wakisema
kuwa maisha yao yataathirika pakubwa.

Zaidi ya asilimia ya 90 ya wakaazi wa Loliondo ni wa Maasai
ambaohutegemea kuwalisha mifugo wao nyasi kutoka eneo ambalo serikali
inanuia kuwakodishia waarabu.
"bila Ardhi hatuwezi kuishi,'' anasema mama Naishirita Tenemeri,
mwenye watoto watatu.
Bi Tenemeri anafuga Ng'ombe na Mbuzi eneo la Loliondo, ili kuwanunulia
chakula na kuwalipia karo ya shule wanawe.

Wa Maasai wana historia ya kupoteza ardhi yao nchini Tanzaniatangu
wazungu walipowahamisha kutoka mbuga ya Serengeti mwaka 1959.

Mapema mwezi huu, Bi Tenemeri, akiwa amejifunga shuka yake nyekundu,
alijiunga na watu 1,000 wengi wao wakiwa wanawake chini ya miti ya
mivule, katika kijiji cha Olorien kupinga mipango ya serikali kuuza
ardhi yao.
Wengine walitembea kwa siku nyingi kuonyesha ghadhabu yao kwakujiondoa
katika chama tawala cha CCM kama wanachama.

"ikiwa sina ardhi, sina mahala pa kujifungulia watoto wangu,'' alisema
Bi Morkelekei Gume,akitupa kadi yake ya uwanachama wa CCM chini .
"mwanangu yuko katika shule ya upili, kwa sababu ya nyasi zinazotoka hapa.''
''Ikiwa wanataka ardhi yangu wanaweza kuniua.''
Mwanamke mmasaai anashikia bango linalosema "tutapigania ardhiyetu
hadi mwisho wake.'' Wanawake hapa ndio wamekuwa wakisikika zaidi
katika maandamano yao.
Wanawake wamekuwa wakisikika zaidi, wameathirika zaidi kutokana na
hatua ya serikali kuwafukuza, wakiachwa bila kazi kuwalea watoto wao
kwa hali ngumu wakati wanaume wakienda katika sehemu za miji ambako
wanapata kazi kama walinzi.
Pia wameongoza maandamano tangu viongozi wao wa kisiasa waliopinga
mpango wa ujenzi wa barabara waliokuwa wamesema wataondoka katika
chama tawala kukosa kutimiza ahadi zao.
Eneo la Loliondo lina wanyama wengi wa porini na hivyo kuvutia watalii
ingawa sio wengi. Linapakana na mbuga ya wanyama ya Maasai Mara
iliyoko Kenya pamoja na hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro.
Waziri wa utalii Khamis Kagasheki anatetea hatua ya serikali kutaka
kuwaondoa wamasaai katika eneo hilo akisema kuwa mradi huo utasaidia
katika kuendeleza uhifadhi kwani Maasai wametumia ardhi hiyo vibaya.
Lakini wasomi wanasema kuwa jamii ya wamaasai kawaida hawaathiri wanyamapori.
"nina swali moja kubwa kwa wanaosema kuwa wamaasai ni tisho kubwa kwa
wanyamapori kuliko kampuni hiyo ya kiarabu ya OBC," alisema Benjamin
Gardner wa chuo kikuu cha Washington na ambaye amesomea maswala ya
ardhi miongoni mwa wamaasai kwamiongo miwili.
Ni nadra kwa wamaasai kuwinda wanyama na hutumia ardhi kuzuiabaadhi ya
wanyama kujifungulia huko kwani ni tisho kwa mifugo wao.
Mashirika 13 ya kijamii kutoka kote nchini Tanzania, yamesema kuwa
wamaasai, wana vibali vichache sana vya kumiliki ardhi, na kuwa
serikali inawapotosha watu
Viongozi wa jamii hiyo wanapanga kwenda mahakamani kuishtaki serikali,
lakini wanahofia kuwa huenda swala hilo likakosa kutatuliwa haraka
kwani kuna kesi moja iliyowasilishwa mwaka 2009 na haijapata ufumbuzi
hadi wa leo.

Ahukumiwa Maisha Jela Kwa Kumbaka Mwanae

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,
imemuhukumu Abisai Joseph (40) mkazi wa Mtaa wa Kigamboni, Kata ya
Shanwe mjini hapa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto
wake wa miaka sita.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya
wilaya hiyo, Chiganga Tengwa ambapo Joseph anadaiwa kutenda kosa hilo
Desemba 18 mwaka jana, saa tano usiku akiwa nyumbani kwake.
Awali, Mwendesha Mashtaka Ally Mbwijo, aliieleza mahakama kuwa siku
hiyo ya tukio Joseph alimbaka mwanaye baada ya kumvizia wakati alipo
toka kujisaidia haja ndogo.

Alidai kuwa baada ya kumkuta nje, alimvua nguo kisha alimweka sehemu
ya mapaja yake na kuanza kumfanyia kitendo hicho, na kwamba pamoja na
mtoto huyo kupiga kelele za kuomba msaada, mama yake aliyekuwa amelala
ndani hakuweza kusikia.

Mbwijo aliongeza kuwa baada ya kumaliza kufanyiwa kitendo hicho, mtoto
huyo aliingia ndani akilia, hali iliyomfanya mama yake amuulize,
lakini baba yake alijibu upesi kuwa alimkuta nje akibakwa na balozi
waowa nyumba kumi.
Alidai kuwa baada ya maelezo hayo, mama wa mtoto, Sauda Rajabu
alikwenda kwa majirani kuwapa taarifa ya kitendo hicho, lakini
walimshauri ende kutoa taarifa polisi.
"Akiwa hapo polisi mtoto huyo alikana kubakwa na balozi wao, bali
alisema aliyembaka ni baba yake mzazi," alidai.
Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne
akiwemo mtoto mwenyewe aliyebakwa na mshtakiwa hakuwa na shahidi
yeyote.

Hakimu Chiganga katika hukumu hiyo alisema mahakama imeridhika na
ushahidi uliotolewa na kwamba imemtia hatiani mshtakiwa kwa kuvunja
sheria namba 130 (1) (e) na 131 (3) kifungu cha marekebisho ya sheria
ya mwaka 2009.

Alisema kutokana na kosa hilo mahakama inamuhukumu Joseph kifungo cha
maisha jela ili liwe funzo kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.




Chanzo: Nassor Wazambi(fb)

Tundu Lissu Na Wabunge Watano Wa Cha Wapigwa Stop Bungeni

MNADHIMU wa Upinzani na Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu na
wabunge wengine watano wa Chadema wameamriwa na kiti cha
Spikakutoingia bungeni kwa siku tano kutokana na utovu wa nidhamu.
Wabunge wengine ambao wamepewa amri ya kutohudhuria kwa siku tano ni
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi; Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa
Ilemela, Highness Kiwia na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje.

Wakati wabunge hao watano wamepewa adhabu hiyokutokana na utovu wa
nidhamu wakimkinga Tundu Lissu asitolewe nje na askari, Tundu Lissu
adhabu yake inatokana na kukaidi kukaa chini, Kiti kilipomuaru kufanya
hivyo na kukataa kutoka nje alipoamriwa kutoka.

Kutolewa nje huko kulitanguliwa na kizaazaa cha dakika kadhaa katika
ukumbi wa Bunge wakati likikaribia kuahirishwa ambapo Tundu Lissu
ambaye alitaka kutoa mwongozo wakati Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM),
Mwigulu Nchemba akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma kuamriwa na Naibu Spika Job Ndugai kukaa na kukaidi.
Wakati tukio hilo likitokea muda wa saa moja na dakika 35 usiku,
Nchemba alikuwa anaeleza kuwa kiongozi wa Chadema Willibrod Slaa
alifanya mkutano wa ndani na viongozi wa kidini, kauli ambayo
ilimfanya Lissu aamke na kutaka mwongozo ambapo Naibu Spika Ndugai
alimkatalia kwa kumwambia kwamba anaingilia muda wa wachangiaji
wengine na ameshasimama mara 20 kuomba mwongozo na kutoa taarifa.
Hata hivyo, Mbunge huyo alikaidi amri hiyo ya kukaa chini ndipo Ndugai
alipoamuru: ''Askari toa nje Tundu Lissu .. nasema toa nje'' lakini
Lissu aliendelea kugoma ndipo hali ilipobadilika katika ukumbi huo na
kuanza kusikika maneno..
" watu katika Tv wanacheka... uonevu... " na wabunge wa Chadema
wakatoka kwenda kuzuia Lissu kuondolewa katika ukumbi wa Bunge, licha
ya kwamba askari watatu walikuwa tayari wamesogea kwenda kumuondoa
Lissu.
Wabunge hao ni Msigwa, Mbilinyi , Lema , Kiwia na Wenje . Wakati
wabunge hao wakiendelea kuzozana na askari hao, Ndugai akatangaza
kuongeza adhabu nyingine kwa Tundu Lissu ya kutohudhuria Bunge kwasiku
5 baada ya kukaidi ile ya awali ya kumtaka atokenje ya Bunge na kuita
askari zaidi kutoka nje.
Wakati askari hao wakiingia kuongeza nguvu Naibu Spika alitoa adhabu
ya kutohudhuria Bunge kwa siku tano kwa wabunge watano ambao ni
Mbilinyi, Lema, Msigwa, Kiwia na Wenje kwa utovu wa nidhamu.
Kuongezeka kwa askari kuliwafanya wabunge hao waChadema kushawishi
wenzao ambao walitoka nao njeya Bunge saa moja na dakika 42, dakika
tatu kabla yakuahirishwa kwa Bunge.
Lissu akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge alisema kwamba hakubaliani na
uamuzi wa Naibu Spika na kwamba leo atakuja bungeni kwani hakuna
kifungu cha kanuni kinachoruhusu atolewe bungeni kwa siku tano na
kinachozuia asisimame na kuongeza:
"hata kusimama mara 30 naruhusiwa". Akichangia hoja ya bajeti ya Ofisi
ya Rais, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema Dk Slaa
alikusanya viongozi wa dini katika mkutano wa ndani badala ya
wanachama wa Chadema.
Hata hivyo, Susan Kiwanga alisimama kumpa taarifa Nchemba kuwa mkutano
huo haukuwa wa viongozi wa dini bali wa wadau wa Chadema.

Serukamba (MB) Afumua F***k(!!!!!!!!!!!) Bungeni, Spika kutumia Askari Kuwatoa Wabunge watumizi wa Lugha chafu.

PAMOJA na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutishia kutumia Polisi
kudhibiti wabunge wanaotukana bungeni, jana Mbunge wa Kigoma Mjini,
Peter Serukamba (CCM), alijikuta akitukana matusi ya nguoni bungeni.
Mbunge huyo alijikuta akitukana wakati wa mjadala kuhusu kusitishwa
kwa hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kuingilia Mhimili wa Mahakama.
Awali kabla ya Serukamba kutoa tusi hilo kwa Kiingereza, akisema
'F***'(haliandikiki hapa), hotuba hiyo kuhusu makadirio ya mapato na
matumizi ya ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ilizua
mabishano miongoni mwa wabunge.
Ubishi huo ulitokana na hoja kwamba sehemu yake, inaingilia kesi
inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred
Lwakatare.
Kutokana na hali hiyo, hotuba hiyo ilizuiwa kusomwa jana mchana katika
muda uliokuwa imepangiwa; badala yake ililazimika kusubiri kwanza
Kamati ya Bunge ya Kanuni, kwenda kuijadili na kutoa uamuzi,
ilikukisaidia Kiti cha Spika kutoa uamuzi.
Awali Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Profesa Kulikoyela Kahigi
alipoanza kusoma hotuba hiyo, Serukamba alisimama na kusema kurasa nne
za kwanza za hotuba hiyo, zinaingilia uhuru wa Mahakama.
Serukamba alisema katika hotuba hiyo, kunatajwa kesi ya Wilfred
Lwakatare, suala ambalo liko mahakamani na kuongeza, kwamba Mbunge wa
Mbulu, Mustafa Akunay (Chadema), wakati wa kujadilihoja ya Waziri
Mkuu, alionya kuwa kuzungumza sualahilo ambalo liko mahakamani ni
kuingilia uhuru wa Mahakama.
Kwa hoja hiyo, Serukamba aliomba Naibu Spika, Job Ndugai, amwamuru
Msemaji wa Kambi ya Upinzani, asisome kurasa za kwanza hadi nne, kwa
maelezo kuwa zina mambo mengi yanayoingilia mhimili mwingine wa Dola.
Mpambano wa hoja Wakati mjadala huo ukianza, Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, Tundu
Lissu, walikuwa wakishuhudia majadiliano wakiwa nje ya ukumbi wa
Bunge, wakaamua kurudi ndani ya ukumbi haraka, kuwahi mjadala.
Wakati Mbowe na Lissu wakiingia kwa mwendo wa haraka ndani ya ukumbi
wa Bunge, Mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema), alitetea hotuba
hiyokwa maelezo kuwa hakuna suala ambalo liko kwenye hotuba hiyo
lililoko mahakamani.
Mnyika, ambaye alikuwa anatoa taarifa kwa Serukamba, alisema mambo
kwenye hotuba hiyo yanahusu vitendo vya utekaji wa Dk Steven Ulimboka
na Absalom Kibanda, ambavyo haviko mahakamani, ila vinafanywa na Idara
ya Usalama wa Taifa.
Mnadhimu Mkuu wa Serikali, William Lukuvi, alisimama kumpinga Mnyika,
akieleza kuwa kurasa zahotuba hiyo zinataka kuifanya kesi ya Lwakatare
iwe ya kisiasa, badala ya kuiachia Mahakama ifanye kazi yake.
Baada ya hoja hizo, Ndugai, alitoa uamuzi akikubaliana na hoja za
Serukamba na Lukuvi kuwa nikweli hotuba hiyo ina mambo ambayo yako
mahakamani.
"Ndugu zangu wa Chadema haya mambo mnayoleta hapa tumeshahadharishwa
kuwa yako kortini, lakini pia yanaweza kuleta mjadala wa ajabu hapa
bungeni,hivyo naomba yasisomwe," alisema Ndugai jambo ambalo
lilimfanya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee naMbunge wa Singida Mashariki,
Lissu kusimama kupinga uamuzi huo.
Lissu katika maoni yake, alionesha Sheria ya Usalamawa Taifa namba 15
na akamtaka Lukuvi aeleze hoja zake amezitoa wapi. Alisema sheria hiyo
inakataza kuandika jina nje ya Bunge na si bungeni.
"Haya maneno ya Lukuvi ni ya kuokoteza tu mitaani, hakuna sheria
inayokataza Bunge lisijadili majina ya usalama," alisema.
Mnadhimu huyo wa Kambi ya Upinzani, alisema itakuwa ni hatari kwa
Bunge kukatazwa kujadili suala la Idara ya Usalama wa Taifa, wakati
kuna waziri anayesimama na kuomba fedha za wananchi kwa ajiliya idara
hiyo. Hoja za ajabu ajabu Lissu alisema kama kuna 'madudu' yanafanywa
na idara hiyo, Bunge linamwajibisha waziri husika, "Hivyo hizi hoja za
ajabu ajabu zinazotolewa hapa bungeni naomba Naibu Spika uzikatae,"
alisema.
Naibu Waziri wa Sheria, Angela Kairuki, alisema Lissu anapotosha Bunge
na akasoma sheria inayokataza kuwa hairuhusiwi hadi kupata kibali cha
waziri mwenye dhamana, kutangaza majina ya maofisa wa Idara ya Usalama
wa Taifa.
Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), alisema hotuba ya
upinzani inazungumzia mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa,
anayedaiwakughushi ushahidi dhidi ya Lwakatare, jambo ambalo liko
mahakamani.
"Bunge lijiheshimu kwa kutojadili mambo yanayoingilia uhuru wa mhimili
mwingine wa Dola, haya mambo ya kughushi ushahidi ni kuingilia
Mahakama," alisema Sendeka.
Baada ya malumbano hayo, Ndugai alisema kwa kuwa suala hilo ni la
kikanuni, akaamuru Kamati hiyo ikae na kulitolea ufumbuzi suala hilo.
Serukamba aomba radhi Bunge liliporejea jioni, Serukamba alisimama na
kuonwa na Naibu Spika ambaye alimpafursa ya kuzungumza, naye akaomba
radhi kwa kauli aliyoitoa asubuhi akisema imemfedhehesha na kwamba
ilimtoka kwa bahati mbaya.
Hata hivyo, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje alisimama na kutaka
agizo la Kiti la polisi wa Bunge kutumika kumtoa nje mbunge
atakayetukana, lianze kutekelezwa kwa Serukamba.
Ndugai aliahidi kulitolea uamuzi suala hilo, lakini akaruhusu Kambi ya
Upinzani kuendelea na hotuba yake, baada ya kufanyiwa marekebisho kwa
maagizo ya Kamati ya Kanuni ya Bunge.
Hilo lilifanyika. Wakati huo huo, Naibu Spika wa Bunge, amempa siku
saba Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, athibitishe kauli yake
kwamba Rais Jakaya Kikwete, ndio kinara wa udini nchini.

Bi Kidude Afariki

Mwimbaji nguli wa muziki wa tarabu nchini Tanzania Fatma binti Baraka,
maarufu kama Bi Kidude amefariki Jumatano kisiwani Zanzibar akiwa na
umri wa zaidi ya miaka 100.
Taarifa ya kifo chake ilitolewa na mjukuu wake Fatuma Baraka ambaye
pia ni muimbaji wa Taraabu. Alisema Bi Kidude alifariki hospitalini
kutokana na maradhi ya kisukari na uvimbe kwenye Kongosho.
Bi Kidude amekuwa katika fani ya muziki wa taarab ya kiasili pamoja na
ngoma za unyago kwa zaidi ya robo tatu ya umri wake.

Katika miaka ya karibuni afya yake imekuwa ikizorota kiasi cha
serikali ya Zanzibar kumzuia kupanda majukwaani kuburudisha japokuwa
alionekana katika tamasha la Sauti za Busara mwezi Februari mwaka huu.
Mipango ya mazishi ya nguli huyu inafanywa nyumbani kwake Zanzibar.

Wengi, hasa vijana wa kizazi kipya wanamfahamu Bi. Kidude kwa uwezo
wake mkubwa wa kuimba taarabu kwa kuchanganya lugha ya kiswahili na
ile ya kiarabu. Nyimbo zake za kiarabu mara nyingi zimekuwa na ladha
kama ile ya aliyekuwa mwimbaji gwiji wa Misri Ummu Kulthumu.
Sio uimbaji tu uliomfikisha Bi. Kidude alipofika, bali uwezo wake pia
wa kutunga mashairi, kutumia ala za mziki kama vile kupiga ngoma na
hata ngoma za unyago, vyote hivi vilimuweka Bi. Kidude katika nafasi
tofauti katika jamii.
Alikuwa na tabia ya kumwita kila mtu 'mwanangu,' ingawa yeye mwenyewe
hakubahatika kupata mtoto. Katika mahojiano aliyofanyiwa na vyombo
mbali mbali vya habari, mwenyewe alisikika akisema, ingawa alikuwa na
hamu ya kupata mtoto, lakini Mwenyezi Mungu hakumjaalia.
Katika miaka ya hivi karibuni, Bi. Kidude alishirikishwa sana na
wasanii wengine katika kazi zao. Miongoni mwao ni Ahmada Amelewa, Fid
Q Juhudi za Wasiojiweza.
Mbali na hayo, mashirika mbali mbali yakiwemo ya kibiashara na yale
yasiyo ya kiserikali yaliona mvuto aliokuwa nao Bi. Kidude katika
jamii, hivyo wakamtumia katika matangazo mbali mbali maarufu likiwa
lile la kutokemeza Malaria.
Ni bibi aliyebahatika kusafiri takriban duniani kote, na vilevile
katikamaisha yake alijinyakulia tuzo lukuki. Miongoni mwa hizo ni ile
ya 2005 WOMEX ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika tasnia ya
muziki.
Katika siku zake za mwisho, Bi. Kidude alikuwa akiumwa, lakini wengi
wanahusisha kuumwa kwake na utu uzima aliokuwa nao.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa wote, lakini zaidi ni wanamziki wa kizazi
kipya waliokuwa wakimuona Bi. Kidude ni nyanya yao.

Aliyefariki Miaka Mitano Iliyopita Afufuka

Mji wa Geita na maeneo ya jirani juzi ulikumbwa na taharuki ya aina
yake, pale mwanamke ambaye anadaiwa kwamba alifariki miaka mitano
iliyopita alipoonekana akiwa hai katika eneo la Kasamwa.
Inadaiwa kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika
Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya,
Kata ya Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba
ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.
Aliyekuwa wa kwanza kumwona Flora ni mdogo wake aitwaye Monica Onesmo
ambaye baada ya kuamka saa 11:00 alfajiri nyumbani kwa dada yake,
alimwona mwanamke aliyekuwa ameketi nje ya nyumba hiyo, lakini
alimfananisha mwanamama huyo na marehemu dada yake.
"Baada ya kumwona nilimwita mtoto wake tunayekaa naye na nikampigia
simu dada (Monica) ambaye alikuwa amelala chumba kingine nikamwambia
kwamba nimeamka na kumkuta mwanamke amekaa hapa nje, lakini kila
nikimwangalia anafanana na marehemu dada yetu,"alisema Jubili na
kuongeza kwamba alipowaita wote walitoka nje.
Alisema mtoto wa Flora (marehemu anayedaiwa kufufuka) anaitwa Rebeka
Elisha (16) na kwamba walimchukua tangu 2008 wakati mama yake huyo
alipofariki dunia katika Hospitali ya Geita ambako alikuwa amelazwa
kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ini.
Rebeka ambaye ni mtoto wa nne wa Flora alisema: "Mama mdogo alituita
sisi tulikuwa tumelala akasemakwamba nje kuna mwanamke ambaye
anafanana na marehemu mama yetu, ndipo na sisi tukatoka na kweli
kumwangalia alikuwa ni yeye kabisa."
Alisema walipomuhoji mama yake huyo kwamba ametokea wapi, aliwaeleza
kuwa ametoka eneo la Katoro kwa mganga na aliletwa na watu ambao
hakuwatambua Alhamisi saa 1:30 usiku ndani ya gari na watu hao
walimshusha kwa mtu aitwaye Juma Luchunga ambaye ni jirani na dada
zake hao.
Kauli ya Flora
Akizungumza na waandishi wa habari, Flora alisema yeye ni mkazi wa
Katoro na kwamba alitokea Katoro nyumbani kwa mganga wa jadi ambaye
hata hivyo hakumtaja kwa maelezo kwamba wataalamu wake (majini)
wamemkataza.
"Nilikuwa naishi kwa mganga wa kienyeji ila alikuja mwanaume wakati
nikiwa pale akaninywesha dawa kisha tukapakizwa kwenye gari na watu
wawili ambaosikuwatambua, mmoja mwanamke na mwingine mwanaume mpaka
hapa Kasamwa tukashushwa saa 1:00 jioni,"alisema Flora.
Alisema alipofika Kasamwa alikwenda kunywa uji kwamama mmoja ambaye
pia hakumtaja na kwamba baadaye alipelekwa nyumbani kwa mtu mwingine
saanne usiku, lakini watu wa nyumba hiyo walipomwona walimwambia:
"Hapa si kwako twende tukupeleke kwa ndugu yako" na ndipo wakampeleka
kwa dada yake ambako aliketi nje hadi alfajiri.
Flora alisema kabla ya kuishi kwa mganga alikuwa akiishi porini ambako
alitupwa na watu asiowafahamuna baadaye aliokotwa na wasamaria wema
ambao ndiyo walimpeleka kwa mganga ambako alikuwa akiishi muda wote.

Ndege Yaanguka Arusha

Arusha: Ndege ya Marehemu Wakili Nyaga Mawalla yaanguka na kuharibika
'write-off'
- Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba ndege iliyokuwa
inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawalla aliyefariki wiki
3 zilizopita na kuzikwa huko Nairobi, imeanguka ikiwa katika hatua za
mwishoza kutua (final approach) katika kiwanja cha ndege chaArusha.
- Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee
anayejulikana kwa jina la Jamal B S, au maarufukama "Bob Sambeke"
aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro ambaye naye kapoteza maisha
(kafariki)!
- Inadaiwa kuwa ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida
ya kufunga kiwanja (saa 12.30 jioni)kupita.



Chanzo:JamiiForum

President Uhuru After Inauguration

Hapo Juu ni baadhi ya picha za Rais wa Jamuhuri ya Kenya Mh. Uhuru
Kenyatta siku chache baada ya Kuapishwa Akiwa na Makamu wake Mh.
William Ruto, Mpinzani mkuu katika Uchanguzi wa Kenya Mh. Raila Odinga
pamoja na mgombea mwenza Mh. Karonzo Musyoka.
Pia Rais wa Burundu Mh. Nkurunzinza na Mkewe na Pamoja na First lady
wa Kenya Mrs. Kenyatta

Ambwene Yesaya Awa Verified Twitter

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nchini Ambwene Yesaya (AY) Amekuwa
verified katika mtandao wa kijamii wa Twitter, Amekuwa msanii wa
kwanza wa Muziki Tanzania kutambuliwa na Twitter, Kwa Upande mwingine
Watanzania ambao wako verified katika Twitter ni Raiswa Jamhuri ya
Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete (@jmkikwete), January Makamba
(@JMakamba), Hasheem Thabiti (@hasheemthedream), Flaviana Matata
(@Flavianamatata), Ambwene Yesaya (@AyTanzania)
Kwa kitendo Hicho kinaifanya Tanzania kuendelea kutambulika Duniani
Hasa kwa uwakilishi Unaofanywa na AY

Zombie Gangnam Style

Lol! Oppa Gangnam style watu na ujuzi wao now ni kw zombie style cheki video hapo juu.

CAG: Aagiza Kumbi za Harusi, M-Pesa,Tigo Pesa na Zinginezo Kutozwa Kodi

MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh,
ameshauri kampuni za simu zinazotoa huduma ya utumaji fedha na kumbi
za harusi vitozwe kodi. Sambamba na hilo aliutaka uongozi wa Bunge,
kurejesha Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).
Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha
taarifa yake bungeni mjini hapa jana akisema uamuzi wa kufuta kamati
hiyo na kazi zake kuunganishwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),
hautakidhi matarajio ya wadau wa uwajibikaji.
Kwa upande wa kodi, alishauri kodi kutoka kwa wafanyabiashara wadogo,
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ihusishe kikamilifu makatibu kata
kutambua walipa kodi wakiwamo wamiliki wa kumbi za harusi na mikutano.
Akifafanua kuhusu kodi kwenye kampuni za simu za mkononi alitaka
zitozwe kodi ya zuio la malipo ghafi ya kamisheni, inayolipwa kwa
wanaofanya biashara hiyo ya kuhamisha fedha kwa niaba ya kampuni.
Uhamishaji fedha hizo unafaywa kwa kupitia mifumo ya M-pesa, Tigo
Pesa, Airtel Money na Easy Pesa.
Alishauri kodi hiyo ya zuio, ipunguzwe kutoka kodi ya mwisho
inayotakiwa kulipwa na kampuni za simu.
Kamati ya POAC Utouh alisema PAC itazidiwa na wingi na ukubwa wa
majukumu na akatoa mfano, kuwa hata kabla ya kamati hizo kuunganishwa,
kamati hizo mbili zilikuwa zinazidiwa.
Alisisitiza kuwa ni jambo jema POAC irejeshwe kwa jina lolote, lakini
kazi zake zibaki zile zile.
"Kuna mashirika 176, ukiweka na taasisi za Serikali mzigo unakuwa
mkubwa na PAC hii ya Zitto (Kabwe ambaye ni mwenyekiti), kama
atafanikiwa hata nusu ya kazi zake, itakuwa ni muujiza.
"Hivyo nashauri tuone uwezekano wa kurudishakamati hii hata kama
itakuwa na haja ya kubadilisha jina, iitwe ya mashirika ya umma auya
uwekezaji, lakini ifanye kazi za POAC," alisema Utouh. Wabunge na CAG
pia alisisitiza kuwa licha ya Serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya
ukaguzi wa umma, mabadiliko hayo hayajaingilia uhuru wa ofisi yake
kutimiza wajibu wake.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa PAC, alilalamikia sheria hiyo kuwa inawaziba
midomo wabunge kwa vile wanazuiwa kujadili ripoti ya CAG.
Zitto alisema mfumo uliokuwapo wa kuwasilisha ripoti za kamati za
Bunge, umefutwa na Serikali baada ya kutunga sheria, na Serikali
inachotaka ni Bunge kujadili ripoti hizo kupitia kamati zake kabla ya
kujadiliwa na Bunge zima.
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe alisema Serikali imetunga
sheria hiyo kwa vile haitaki kusimamiwa na Bunge, ila inataka Bunge
kiwe chombo cha kujadili tu. Alisema hilohalikubaliki na akasisitiza
kuwa kamwe hawataruhusu ripoti za kamati ya CAG isijadiliwe bungeni.
"Tunatumia miezi mitatu kuomba fedha za Watanzania, lakini linakuja
suala la kuhoji matumizi yake kwa sasa tunanyimwa fursa
hii…hatuikubali ni lazima ripoti hizi zijadiliwe namwenye kuwajibika
awajibike kama ilivyotokea mwaka jana," alisema Filikunjombe.
Mwenyekiti wa PAC wa zamani John Cheyo alisema sheria hiyo mpya ya
Ukaguzi wa Umma, inaifedhehesha Serikali na akashauri marekebisho hayo
yafutwe na Bunge ili kutoa fursa ya ripoti ya CAG kujadiliwa.
"Tulikuwa tunakwenda mbele sasa na mabungemengine yalikuwa yanakuja
hapa kujifunza namna tunavyoshirikiana na CAG kusimamia fedha za umma,
lakini sheria hii ya sasa inaturudisha nyuma, tusikubali ni lazima
ripoti hii ijadiliwe bungeni," alisema Cheyo.
Misamaha ya kodi Wakati huo huo, CAG alisema ataanza ukaguzi kwenye
misamaha ya kodi kwa vile fedha ambazo zingelipwa kutokana na
misamaha, ni za Serikali ambazo zinatolewa kama ruzuku kwa wanaopewa
misamaha hiyo.
"Tumeamua kuikagua kwa kina misamaha yote ya kodi kuanzia mwaka ujao
wa fedha kwa madhumuni ya kuangalia manufaa ya misamaha hiyo kwa
uchumi wa Taifa," alisema Utouh.
Lakini CAG alitaka hati za misamaha ya kodi, ziwekwe bayana kuwa
msamaha wa kodi ni wa muda gani, unaanza lini na kumalizika lini.
Alitaka misamaha ya kodi ianishwe ikionesha malengo yanayokusudiwa na
kuwa na utaratibuwa Serikali kusimamia utekelezaji wa misamaha hiyo.
Ameshauri pia mikataba yote yenye vipengele vya misamaha ya kodi,
ipitiwe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya ushauri kabla ya
kusainiwa na pande husika.
Pia alishauri mikataba ya kuchimba madini, ijadiliwe na Kamati ya
Bunge inayoshughulikia masuala ya madini, na ushauri utolewe kwa
waziri husika kabla ya kusainiwa.



Chanzo:HabariLeo

Serikali Yagomea Ushauri Wa Wabunge

Serikali imekataa ushauri wa wabunge na kusema kuwa itaendelea
kuwaajiri wastaafu mbalimbali nchini hadi hapo soko la ajira
litakapojitosheleza.
Mbali na hilo, jana Serikali ilitangaza bungeni kuwa kazi za wakuu wa
mikoa siyo ajira rasmi, bali ni ajira za kisiasa ambazo hazipaswi
kuhesabiwa.
Akijibu swali bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti
ya Utumishi wa Umma) Celina Kombani, alikiri kuwa bado Serikali
inaendelea kutoa ajira kwa watu ambao wamestaafu na kuwa itaendelea
kufanya hivyo kwa siku za usoni.
Alikuwa akijibu swali la Vicent Nyerere (Musoma-Chadema) ambaye
alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kusitisha kutoa mikataba kwa
wastaafu ili wahitimu wanaotoka vyuoni wapate ajira na kujenga nchi
yao.
Mbunge huyo pia alihoji nafasi za wakuu wa mikoa nchini ambao wengi
hufanya kazi wakiwa katika umri mkubwa, huku baadhi wakiwa wamestaafu
utumishi wa umma. Waziri alisema ni kweli kuwa wako wataalamu wengi
wanaohitimu vyuo vikuu hapa nchiniambao wanahitaji kuingia katika soko
la ajira, lakini hupatiwa ajira kulingana na uwezo na bajeti ya
Serikali.
Kuhusu wastaafu kuendelea kupewa ajira, alisema "Hilo linatokana na
utaalamu walionao ambao ni vigumu kuziba nafasi zao kwa kipindi cha
haraka."
Kombani alizitaja kada ambazo Serikali inatoa mikataba kwa wastaafu
kuwa ni walimu, waganga, wahandisi na wahadhiri wa vyuo ambao alisema
nafasi zao ni adimu.



Chanzo:Mwananchi.co.tz

Tanzania Yazidi Kufukuzia Namba za Juu

Tanzania na Timu ya taifa ya mpira wa miguu imeendelea kujichukulia
nafasi kupanda juu katika viwango vya FiFa na sasa Kukwea mpaka
kufikia Nafasi ya 116 kutoka 119 katika takwimu zilizotolewa mwezi
uliopita wa March. Tanzania Imepata Points 3 baada ya Kuichabanga Timu
ya Taifa ya Morocco kwa goli Tatu kwa moja Katika uwanja wa Taifa
Jijini Dar es salaam mwenzi March, ambapo ulikuwa na Mchezo wa
kutafuta Nafasi ya kufuzu Kucheza final za kombe la Dunia , Michuano
hiyo Itafanyika Nchini Brazili mwakani(2014). Tanzania Katika michuano
Hiyo Ipo Kundi moja na timu za taifa za Ivory coast Vinara wakiwa na
Points 7, Tanzania Yenyewe Points 6, Morocco points 2 na Gambia point
1 Huku zote zikiwa zimecheza Mechi Tatu kila mmoja.

Kwa Siku za Hivi Karibuni Taifa stars imekuwa wazuri zaidi katika
uwanja wa nyumbani kwa kuzifunga timu vigogo. Cameroon, Zambia na
Morocco

Picture of The Day | Picha Ya Siku

Hiyo Wikiend tayari ishafika sasa wale wa bata batani, wale wa kula
bata mpaka bata aseme bata ndo muda sasa. Enjoy Responsibly

KumbuKumbu Ya Marehemu Edward Moringe Sokoine

LEO NI KUMBUKUMBU YA MAREHEMU EDWARD MORINGE SOKOINE ALIYEFARIKI KWA
AJALI YA GARI 12/04/1984 LEO ANATIMIZA MIAKA 29

Ufuatao ni miongoni mwa maneno aliyowahi kuyatoa wakati wa Uhai wake.

"Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka
thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize
mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, 'mali
hii umeipata wapi?'" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1983"Aliwahi
kuwa Waziri Mkuumara mbili, tangu tarehe13 Februari 1977 hadi 7
Novemba 1980, tena tangu tarehe 24 Februari 1983 hadi kifochake,
alipofariki kufuatana na ajaliya gari.
Uongozi wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na
uadilifuna kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulajirushwa na
ubadhirifu wa mali za umma.
Sokoine alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha
bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam. Wengi wanashuku ajali hiyo kuwa
ilipangwa.
Kifo chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao
walikuwa wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao.
Mwiliwa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwaoMonduli, mkoaniArusha.
Chuo cha Kilimo na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo
cha Sokoine" ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.