Mikopo ya Wanafunzi Elimu Ya Juu Wiki hii Kutolewa na HESLB


   Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itaanza kupeleka fedha za wanafunzi katika vyuo kuanzia wiki hii.
   Ahadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, George Nyatega, alipozungumza na NIPASHE.
   Nyatega alisema jumla ya wanafunzi 29,113 wa elimu ya juu nchini kutoka vyou mbalimbali waliochaguliwa kupata mkopo, fedha zao zitaanza kupelekwa kuanzia wiki hii.
   Nyatega alisema baada ya kutoa majina hayo,bodi ya wakurugenzi ilitarajiwa kukutana Jumamosi kufanya tathmini kisha fedha zao zianze kupelekwa vyuoni.
   Hata hivyo alisema kwa mwaka huu idadi ya walioomba mikopo imeongezeka tofauti na mwaka jana na kuongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ufinyu wa bajeti.
   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandara, jana aliiambia NIPASHE kuwa chuo hichi kimekubaliana na HESLB kwamba kuanzia Alhamisi wiki hii fedha zitapelekwa.
Chanzo:NIPASHE
chuotanzania.blogspot.com

Shilole Achafua Mashabiki Wake

Hii ndiyo post ya Shilole
Comment ya moja wa mashabiki wake
Jibu alilotoa Shilole
Katika pita pita zangu leo kwenye mitandao ya kijamii leo nimekutana
na kali ya Msanii Shilole kutukana mashabiki wake katika Facebook.
Swali lilibaki kwangu kuwa ile account ya Shilole Facebook ni yake au?
Lakini baada ya mashabiki kumjibu alijaribu juomba ladhi.
Kweli ni Kioo cha jamii????????????

Serengeti Fiesta 2012

Na hatimae Rick Ross kutua Bongo kuja kukamua show ya Fiesta 2012 Dar
es salaam Viwanja vya Leaders tarehe 6 October 2012
Kiingilio: Tsh 20,000 Ukiwahi tiketi yako mapema na Tsh 25,000 Mlangoni
Bhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaas!

Pamoja FM

Neema yazidi kuufikia mkoa wetu wa Katavi na Sasa Pamoja Fm imeanza
kurusha matangazo yake Rasmi kwa masafa ya fm 98.5 Tune radio Yako
mpaka hapo kwa Wakazi wa Mpanda uweze kusikiliza Radio ya nyumbani.
Kuongezeka kwa Radio ya Tano (5) Pamoja Fm baada ya hapo mwanzo kuwa
na RFA, TBC Taifa, TBC fm na Radio Maria. Sasa kutazidi kufungua
mianya ya uwekezaji na Kufahamika kwa Mkoa mpya wa katavi
Ni Pamoja FM 98.5

Wananchi Wa Rukwa na Katavi Kukutana

Kwa Wale Wananchi wote wenye asili au wanaotokea Mkoa Wa Rukwa na mkoa
Mpya wa Katavi ambao wanaishi Dar na mikoa ya Karibu, Kutakuwa na
mkutano katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar Es Salaam Ili kupanga
mikakati ya Uzinduzi wa Mkoa mpya wa Katavi. Kikao hicho kitafanyika
siku ya Jumapili tarehe 23/9/2012 Muda ni kuanzia Saa nane mchana
mpaka saa Kumi Jioni
Fika bila kukosa.

TCU yatoa Majina Ya Waliochaguliwa kujiunga na vyuo viwango vyao vya mkopo pamoja na Waliokosa

SELECTED APPLICANTS FOR THE 2012/2013ADMISSIONSThe Tanzania Commission
for Universities(TCU) in Collaboration with the NationalCouncil for
Technical Education (NACTE) isannouncing the names of Applicants who
were seleted into various programs forthe 2012/2013 Admissions.
However, weshall announce the list of  someapplicants who were
selected into variousprograms but obtained no loan,applicants who were
returned by some institutions, and selected applicants whoasked for
transfer, will be announcedbefore 21 September 20121.

1. To view selectedApplicant with no loan/Waliochaguliwa wakakosa
mkopo http://www.tcu.go.tz/uploads/file/SELECTED%20APPLICANTS.pdf

2. To view selected Applicant with loan but subject to verification
with heslb/ Waliochaguliwa wakapata mkopo
http://www.tcu.go.tz/uploads/file/LOANS%20SUBJECT%20TO%20VERIFICATION.pdf

Source: www.heslb.go.tz

Waandishi wa Habari wafanya Maandamano.

Waandishi wa Habari jijini Dar-es-salaam leo wanafanya maandamano
asubuhi hii kuonesha masikitiko yao kwa kuuwawa kwa Mwandishi wa
habari Daudi Mwangosi aliyeuwawa na polisi mjini Iringa

Picha:EARadio

Kifo Cha Mwandishi wa Habari

Vurugu kubwa zilizuka jana katika eneo la Nyororo wilayani Mufindi
kati ya polisi na wafuasi wa Chadema, baada ya askari hao
kusambaratisha mkutano wa chama hicho nakusababisha kifo cha mwandishi
wa habari na watu kadhaa kujeruhiwa.
Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi
anadaiwa kuuawa kwa bomu lililorushwa na polisi katika vurugu hizo.
Awali, inadaiwa kuwa mwandishi huyo alishambuliwa kwa marungu na
Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kabla ya bomu hilo
kumjeruhi vibaya tumboni na kusababisha kifo chake.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio, alisema wakati mwandishi huyo
akishambuliwa na polisi, mmoja wa askari wa jeshi hilo aliwazuia
wenzake kuendelea kumpiga akiwaeleza kuwa anamfahamu kuwa ni mwandishi
wa habari, huku akimkumbatia.
Shuhuda huyo alidai kwamba jitihada za askari huyo hazikusaidia, kwani
baada ya kutupwa kwa bomu hilo lililosababisha utumbo wa mwandishi
huyo kutoka nje, polisi huyo naye alijeruhiwa mguu.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alikana polisi
kumuua mwandishi huyo akidai kwamba kilichosababish a kifo chake
nikitu kilichorushwa na wananchi ambapo alisema polisi inakichunguza.
Vurugu hizo ziliibuka baada ya polisi kufika Nyororo na kuwataka
viongozi wa Chadema pamoja na wafuasi wao kutawanyika kwa kuwa
walikuwa hawaruhusiwi kufanya mkusanyiko wowote kutokana na amri
iliyotolewa na jeshi hilo awali.
Polisi mkoani Iringa jana asubuhi walilipiga marufuku kufanyika kwa
maandamano na mikutano yote ya halaiki ya kisiasa mpaka hapo Sensa ya
Watu na Makazi itakapokamilika baada ya kuongezwa wiki zaidi.
Hata hivyo, pamoja na amri hiyo Chadema kilifanya mkutano wilayani
Mufindi kitendo ambacho polisi walisema ni kinyume cha sheria.

Source: Star Tv

Ajari ya Bodaboda agonga(samahani kwa picha)

Dereva bodaboda agonga na kukimbia, ajali hiyo ilitokea maeneo ya
shule ya sekondari Istiquama kijana aliyegongwa alifaliki papo hapo.
Hakika bodaboda zimekuwa chanzo kikubwa cha vifo hapa kwetu.

Ajali Ya Lori.

Ajali ya lori kubwa lilobeba magogo imetokea maeneo ya mgahawa wa
Bismillah karibu na kanisa la Anglican. Taarifa zaidi zitafuata

Picha kwa hisani ya: Majaliwa Rubuye

PICHA ZAIDI KIFO CHA ASKOFU KIKOTI WA JIMBO KUU LA KATOLIKI MPANDA



Makamu wa  Askofu Jimbo Katoriki Mpanda Padre Patrick Kasomo akiwatoa taalifa kwa waumini ya kuwafahamisha kifo cha Askofu wao Paschal Kikoti kilichotokea hapo jana katika Hospitari ya Bugando Jijini Mwanza ambapo mazishi yatafanyika siku ya juma mosi wiki hii ndani ya Kanisa la Parokia kuu Jimbo la Mpanda.
 Waumini wa Kanisa Katoriki Jimbo la Mpanda wakimlilia Askofu wao Paschal Kikoti mara baada ya kutangaziwa na makamu wa Askofu wa Jimbo la Mpanda Padri Patrick Kasomo kuwa Askofu Paschal Kikoti amefariki majira ya saa 2:30 usiku katika Hospitari ya Bugando hapo jana. Picha na Walter Mguluchuma Katavi Yetu.
Blogzamikoa
Chanzo: kataviyetu.blogspot.com


WACHINA WAFUMWA WAKICHIMBA MADINI KATAVI NATIONAL PARK

MKUU wa mkoa wa Katavi, Dr Rajabu Rutengwe amewataka wawekezaji wanaokwenda kuwekeza katika sekta ya madini katika mkoa wa Katavi wawasiliane na ofisi za serikali mkoani humo kabla ya kuingia katika mikataba ya uendeshaji wa shughuli za uzalishaji katika maeneo husika
Mwandishi wa habari hii kutoka Katavi Willy Sumia anaripoti kuwa wito huo umetolewa na mkuu kufuatia utapeli waliofanyiwa wawekezaji wa kutoka nchi ya China na kampuni yao ya Red Ore Mining Co. Ltd ya DSM na kupelekwa eneo la pori la akiba la Luafi mpakani na hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji wa madini ya chuma na shaba.
Taarifa zinasema kuwa kampuni hiyo yenye makao yake jijini DSM inayoendeshwa na Raia wa nchi ya China ilianza shughuli katika eneo hilo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita hadi jana walipofika askari wa wanyamapori wa Pori la akiba la Rukwa / Lukwati/ Luafi na hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwaamuru waondoke katika eneo hilo kwakuwa ni eneo lilitengwa kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na ustawi wa wanyama pori.
Askari hao walipozungumza na waandishi wa habari walisema kuwa awali walipowakuta raia hao wa China waliweza kuwahoji na kubaini kuwa walikuwa wameingizwa eneo hilo kimakosa na ofisi ya hifadhi hiyo iliwaandikia barua yenye Kumb Namba RLLGR/LGR.1/72/14 ya tarehe 06/06/2012 iliyokuwa akiwapa amri ya kuondoka eneo ndani ya siku saba tangu tarehe ya barua hiyo lakini hawakuweza kutekeleza agizo hilo
Askari hao wa wanyamapori walisema kutokana na kushindwa kutii agizo hilo waliamua kufika eneo husika kuwachukua viongozi wa kampuni hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa kwa maamuzi zaidi kwani walibaini kuwa walipewa taarifa za uongo na mtu aliyewauzia hilo eneo kwani hilo eneo na eneo lisilotakiwa kufanyiwa shughuli yoyote ile
Walisema hata barua walizojibiwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii yenye kumbukumbu namba HB 178/286/01/102 iliyosainiwa na ndugu J. Muya kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara hiyo ya tarehe 20/06/2012 pamoja na ile iliyotoka kwa wakala wa misitu Tanzania (TFS) yenye kumbukumbu namba TFSC.166/286/01/29 ya tarehe 25 Juni, 2012 ikieleza kuwa eneo hilo waliloomba kwa barua siyo eneo linaloruhusiwa kwa kufanya shughli yoyote ya kibinadamu isipokuwa kwa utafiti wa mafuta, gesi au madini ya uraniamu tu
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao na Wachina wamiliki wa Kampuni ya RedOre Mining Co. Ltd, mkuu wa mkoa wa Katavi, Dr Rajabu Rutengwe alisema kuwa katika mazungumzo na wawekezaji hao alibaini kuwa walitapeliwa na mtu aliyewauzia eneo hilo baada ya kuona kuwa eneo hilo haliruhusiwi kwa shuguli yoyote.
Alisema kutokana na hali iliyojitokeza inabidi sheria ichukue mkondo wake na huku wawekezaji hao wakiwa nje ya hifadhi kwani tayari eneo hilo limeshaharibiwa na kuingiza hasara kubwa Taifa hivyo ili kuepusha malalamiko ya kuwa wageni hao wameonewa na Watanzania hivyo mahakama ndiyo itakayoamua nani kakosea, wapi na namna gani kakosea ili kulinda utawala bora.


Akizungumzia juu ya aliyewatapeli wawekezaji hao mkuu wa mkoa alisema wao ndio wanamfahamu aliyewauzia na wanafahamu watampata wapi hivyo ni jukumu la wawekezaji kumtafuta wamuawajibishe kwa kuwatapeli ambapo mkuu huyo wa mkoa alitoa ushauri kwa wawekezaji wengine wasiingie mkataba na mmiliki yeyote wa ardhi katika mkoa wa Katavi bila kuwasiliana na Halmashauri au ofisi ya madini ya kanda ya Magharibi iliyoko mjini Mpanda kwa ushauri na msaada wa taarifa za eneo husika. 
Chanzo: kataviyetu.blogspot.com

Ukusanyaji Maoni ya Katiba Mpya

Kijana akichangia maoni yake kwa njia ya maandishi.
Wananchi wakifuatilia mchakato mzima wa utoaji maoni.
Wananchi wa mpanda wakitoa maoni katika mchakato wa kukusanya maoni ya
uundwaji wa katiba mpya ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Mchakato huu umefanyika katika viwanja vya Kashaulili.

Kwa taarifa zaidi tembelea www.katiba.go.tz

Tanzia: Askofu Mkuu William Pascal Kikoti wa jimbo la Mpanda Katoriki Afaiki

Mpanda_KATAVI

Usijiulize sana Mpanda Katavi iko wapi? Inapatikana Magharibi mwa Tanzania
Kwa upande wa Kaskazini inapakana na mkoa wa Tabora, Kaskazini
magharibi Inapakana na Kigoma
kwa Upande magharibi inapakana na Ziwa Tanganyika. Kusini Mkoa wa
Rukwa, Mashariki Mkoa wa Mbeya.
Karibu Mpanda Katavi

Maisha Plus ndani ya Mkoa wa Katavi.

MAISHA PLUS 2012:
JE UNGEPENDA KUSHIRIKI MAISHA PLUS? UWE NA UMRI KATI YA MIAKA 21-26,
KWA MARA YA KWANZA MKOANI KATAVI. USAILI UTAFANYIKA TAREHE 14/09/2012
SAA 2:00 ASUBUHI MPANDA MJINI. ILI KUJUA IDADI YA WASHIRIKI
TUNAANDIKISHA MAJINA YA VIJANA BURE KUANZIA SASA FIKA NEW TANGANYIKA
CAFE KARIBU NA KANISA LA MORAVIAN - MPANDA. KWA MAELEZO ZAIDI PIGA
SIMU NA. 0712 552211 HII NI NAFASI YA PEKEE KWA VIJANA WA JINSIA ZOTE
NI WAKATI WA KUPATA MWAKILISHI WA KUTANGAZA MKOA WETU MPYA. NYOTE
MNAKARIBISHWA

Siku ya May Mosi kama kawaida Mpanda_Katavi hatukuwa nyuma

 Wanafunzi wa chuo cha ufundi stadi(Veta) wakiwa kwenye maandamano.

Huku mmoja akiwa na bango lenye ujumbe usemao UFUNDI STADI Ni AJIRA KWA VIJANA

Wafanyakazi wakiwa kwenye maandamano ya siku yao ya wafanya kazi.




Wanafunzi nao hawa kuwwambali kuonesha ushilikiano wao katika siku hii ya wafanyakazi duniani.







                     Kama kawaida ya VETA hawakuwa mbali kuonesha zana zao za kufanyia kazi


Kitaifa sherehe hizi zilifanyika Jijini Tanga katiaka uwanja wa Mkwakwani huku Mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dk J.Kikwete


Picha:

  • Alex Milwano

Sherehe za Kumkabidhi mkoa mkuu mpya wa mkoa mpya wa katavi!

Hapa ni mkuu wa mkoa akiwa anaingika katika viwanja vya kashaulili na hapo alikuwa akisalimiana na wananchi.















Hapa mheshimiwa mkuu wa mkoa akiwa anaingia katika viwanja vya kashaulili kuendelea na sherehe.







Mambo ya kimila pia yalikuwepo katika makabidhiano ya mkoa kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Eng. S. Manyanya kwa Mkuu wa mkoa wa KAtavi Mh. R. Rutengwe.

Hapa Mh. ndugu R. Rutengwe akiwa amekalisha kuombewa dua na wazee.

Picha: 
  • Alex Milwano
  • Oswald Kikwala

Mkuu wa Mkoa wa Katavi.



 Hapo awali alikuwa mkuu wa wilaya ya Mpanda, ambapo baada ya uteuzi wa wakuu wapya wa mikoa na yeye aliteuliwa kuongoza mkoa Mpya wa katavi.
 Hapa ni picha ya pamoja Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kuapishwa. Kutoka kushoto ni Dk. Rajabu Rutengwe.
Akiwa na wakuu wa miko mipya ya, Geita Mh. Magalila S. Magalula,  Pascal Mabiti(Simiyu), na  Mh. Aseri masangi(Njombe).




Hapa Mkuu wa Mkoa Dk. R. Rutengwe akiwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda










Dk. Rutengwe Akiwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Eng. S. Manyanya

Cheki Video ya Moi G_hivi ni nini?

                                           Video imetengenezwa na Viper Empire Production.

Moi G ni msanii chipukizi kutoka Mpanda mjini. Ambaye amepata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi ya Azimio iliyopo mpanda mjini alimaliza darasa la saba mwaka 2006 baadae aliweza kujiunga na shule ya sekondari ya mwese ambapo alikuwa na mazingira magumu ya kusoma na hakuweza kumaliza elimu yake hapo.
Lakin Viper Empire Production ikiongozwa na CEO Michael Mazalla wameamua kuinua kipaji chake. kwa uweza wa mungu natumaini mafanikio yatapatikana.

Wananchi wa wilaya ya Mpanda wakiwa kwenye shughuli za kimaendeleo


Hapa ni katika soko kuu la mpanda upande wa vijana wanakouzia Mitumba.
 Huku ni katika upande wa kuuzia samaki, Kuna haja ya kuboresha kwa hali ya juu eneo hili, Sababu wafanya biashara katika mazingira magumu hasa wakati wa masika. Kuna haja ya kuwajengea soko la kisasa.
 Hapa ni upande wa wauza dagaa wakavu katika soko kuu la Mpanda mjini.
Ubovu wa barabara kutoka Mpanda mjini kuelekea karema ambako huzalishwa kwa wingi husababisha Kupanda kwa bei ya dagaa mara kwa mara.
Huduma za kisoko zikiwa zinaendela hapo. katika eneo la wauza dagaa

Hali ngumu ya kiwanja kikuu cha Mpira wa miguu(football) wa AZIMIO STADIUM Wilayani Mpanda Mkoa wa katavi.

 Hapo ni Mashabiki wakiangalia moja ya mechi katika uwanja wa Azimio wilayani mpanda
 Hili ni eneo la nje ya uwanja kwa upanda wa mashariki ya uwanja

 Ndani ya uwanja.











  

Huku ni ndani ya uwanja sehemu ya ukaguzi wa wachezaji kabla ya mechi.

 Huu ndo muonekano wa uwanja kwa juu.
 Pitch inahali nzuri sana lakini nyasi zilizopo pembeni yake zinatia wasiwasi. kunaweza kuwa Nyoka hata na wadudu wengine wenye sumu.
 Huo ndiyo muonekano wa Pitch
                                        Huu ni ubao wa matangazo
ambao hutumika kutoa taarifa mbali mbali.
 Hili ndo lango kuu.


Hapa ndipo dirisha la kukatia tiketi lilipo
Kutoka kana na hali ya uwanja ilivyo, je?? Wananchi kweli hata wachezaji watakuwa na moyo wa kujitolea kweli
Hiii ni changa moto kwa TFF na MUFFA ambao ndiyo wahusika wakuu katika swala zima la kusimamia michezo hapa nchini(TFF), na MUFFA(Wilaya).
Kwa hali iliyopo inabidi kuongeza bidii katika kuboresha viwanja vya michezo, hapa katika wilaya ya Mpanda na mkoa wa katavi kwa ujumla.