BABU WA MIAKA 62 AMBAKA MJUKUU WAKE WA MIAKA MITANO(5)
NDUGU WADAIWA KUNYONGWA
UPINZANI WAANDIKA UKURASA MWINGINE WA HISTORIA
Chanzo: Mwananchi
WENYE VICHWA VIKUBWA WANYANYAPALIWA
Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya afya, tatizo la kujifungua mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi linaepukika. Kinachotakiwa kwa kina mama wajawazito ni kupewa uelewa wa kutosha kuhusu lishe hasa katika kipindi cha ujauzito.
Hata hivyo, inaonekana kunahitajika kazi ya ziada kwa sababu uelewa miongoni mwa kina mama bado ni mdogo. "Sisi tunahisi kwamba uelewa ni mdogo sana, na tunatakiwa sasa hivi kueneza hii elimu kwamba ni lazima mama ambaye anatarajiwa kushika ujauzito au msichana mdogo ambaye anatarajia kuolewa na kuja kuzaa basi aanze kutumia hizi folic acid tangu wakati huo na asingojee mpaka apate ujauzito.
Mtoto wakati ule anaumbika siku za mwanzo mwanzo anaweza kupatwa na hali hii," amesema Abdulhakim Bayakubu ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.Ingawa watoto wanaozaliwa na matatizo haya wanatoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania, lakini takwimu zinaonyesha kuwa wagonjwa wengi wanatokea katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Mwanza.
Mbali na tatizo la lishe, Dr. Marks Mwandosi ambae ni mtaalamu wa upasuaji katika hospitali ya Muhimbili anasema mtoto pia anaweza kuzaliwa katika ule mfumo wake wa maji ya kwenye ubongo ambayo yanalinda ubongo, yakawa hayazunguki katika mfumo wa kawaida.
Hii inatokana na mtoto jinsi alivyoumbwa tumboni. Inawezekana ikawa kuna kuzibwa au yakawa hayanyonywi vizuri au yanatengenezwa mengi.
Baadhi ya kina mama ambao ndio walezi wa watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi wamemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar Famau kwamba wanakabiliwa natatizo la unyanyapaa katika jamii huku miongoni mwao wakikiri hata kuvunjika kwa ndoa zao baada ya kujifungua watoto wenye matatizo hayo.
Mwajuma Hassan Makame amelazimika kulea mtoto mchanga katika wodi ya hospitali ya Muhimbili huku akimuuguza binti yake wa miakakumi. Katika mazingira ya kawaida, hairuhusiwi mtoto mdogo kuingia hospitalini hasa anapokuwa hana tatizo la kiafya kwa kuhofia kuhatarisha maisha yake.
"Sina wa kunisaidia huyu mtoto.
Ninao jamaa zangu lakini huruma ni ndogo. Nina dada zangu baba mmoja mama mmoja hapa Dar es Salaam, lakini hawaji hata kuniangalia. Yaani nisipokuwa na chakula chahospitali, basi nimelala. Siletewi chakula na ndugu, Huu ni mzigo wangu pekee yangu. Babake yuko, lakini amenisusia muda mrefu, nahangaika pekee yangu," amefafanua Mwajuma huku machozi yakimlengalenga.
Tatizo la watoto wanaozaliwa na ugonjwa huu linaonekana kuwa kubwa nchini Tanzania.
Kila watoto elfu nne wanaozaliwa kwa mwaka, wawili au watatu miongoni mwao wana tatizo hilo. Takwimu zinaonyesha kwamba hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania inapokea watoto takriban 5 mpaka 6 kwa wiki. Hata hivyo, licha ya tatizo hilo kuwepo katika jamii, imedhihirika kwamba nchini Tanzania, kuna vituo vinne tu vya matibabu hayo.
Hali hii ndiyo iliyofanya maadhimisho ya siku ya mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi ya mwaka huu ambayo yanatarajiwa kufanyika hapo kesho kupewa kauli mbiu ya 'matibabu kwa wote,' ikiwa na lengo la kuitaka serikali angalau kuongeza vituo vya matibabu nchini kwa wagonjwa hao.
KIJANA APIGWA MAWE KWA UBAKAJI
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 alipigwa mawe Jumanne eneo la Lower Shabelle Kusini mwa Somalia.
Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya ubakaji iliyomhusisha mwanamume huyo alisema alipatikana na hatia ya kumbaka mwanamke akiwa amejihami kwa bunduki.
Al-Shabaab hutumia sheria kali ya kiisilamu au Sharia kutekeleza sheria na mwezi janamwanamke mmoja pia alipigwa mawe hadi akafariki kwa kufanya zinaa mjini Barawe.
MCHINA MBARONI KWA KUMTEKA MWENZAKE
Mtuhumiwa huyo alitoa sharti na kumtaka mlalamikaji atoe fedha kiasi cha dola za Kimarekani 350,000 (sawa na Sh milioni 584.5)ili amwachie huru.Akizungumza ofisini kwake mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 19 mwaka huu majira ya saa 4.00 usiku wilayani Mkuranga.
Kamanda Matei alisema kuwa baada ya kupekuliwa kwenye gari lake aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 554 BAJ alikutwa na bunduki aina ya Short gun namba 006085010, risasi 98 na visu viwili.
Kwa mujibu wa Kamanda Matei, Polisi walikwenda kupekua nyumbani kwa kijana huyo wakakuta nyaraka zinazoonesha kuwa, amewahi kumiliki risasi 300,hivyo haijafahamika risasi 202 amezitumia wapi.Amesema, Ubalozi wa China umewafahamisha polisi kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa akishiri kikufanya uhalifu nchini humo.
Kamanda Matei alisema , polisi wanawasiliana na wenzao wa Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) ili kupata taarifa zaidi kuhusu kijana huyo.
Katika tukio lingine, watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamekamatwa wakiwa na bunduki aina ya Short gun yenye namba 07019302 ikiwa na risasi nane.Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mohamed Kalipa (20) dereva wa Bajaji mkazi wa Mbagala Rangi Tatu, Salum Shekivui (20) mkazi waBuza na Seuli Lucas (18) mkazi wa Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam.
Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 20 mwaka huu majira ya saa 2:30 Mlandizi wilaya ya Kibaha. "Mbali ya silaha pia walikutwa na fedha taslimu kiasi cha Shi milioni 6,611,800, vocha mbalimbali za simu zenye thamani ya Sh milioni 2,185,500 na simu za mkononi sitaza aina mbalimbali ambazo thamani yake bado hazijafahamika," alisema Kamanda Matei.
Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walifanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha katika kijiji cha Mbwewe wilaya ya Bagamoyo kwenye duka la Twaha Mbuta, Oktoba 19 saa 1:30 usiku na kupora kiasi cha Sh milioni 30.
"Baada ya kukamatwa walimtaja mtuhumiwa mwenzao ambaye walikuwa wakishirikiana naye Samwel Joseph mkazi wa Kongowe,Kibaha ambapo baada ya upekuzi walimkuta na risasi sita za Short gun ambazo alikuwa akizimiliki bilaya kibali. Hata hivyo mtuhumiwa huyo alitoroka," alisema Kamanda Matei.
Katika tukio lingine watu wawili walikamatwa kwa tuhuma za wizi wa ng'ombe 61 wenye thamani ya Sh milioni 27.4 mali ya Keke Furaha (37) kwa kutumia silaha aina ya sime.
Alibainisha kuwa tukio hilo limetokea Oktoba Mosi mwaka huumajira ya saa 5.00 asubuhi eneo la Lulenge kata ya Ubena wilayani Bagamoyo. Watuhumiwa katika tukio hilo ni Sadala Lupoto (25) mkazi wa Kimamba Kilosa na Luseky Sogoyo (25), na juhudi za kuwatafuta ng'ombe wengine 39 zinaendelea.
Chanzo:Habari Leo
MAHABUSU AFIA MIKONONI MWA POLISI
Chanzo: Mwananchi
OSCAR PISTORIUS ATUPWA MIAKA MITANO (5) JELA
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.
Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
Jaji alisema kuwa Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani kwani hukumu kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu.
ANYWA SUMU BAADA YA KUNUSURIKA KUBAKWA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Frasser Kashai alibainisha hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kupitia mkutano uliofanyika ofisini kwake jana.
Alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 18, mwaka huu nyumbani kwao mtaa wa barabara ya 20 uliopo Kata ya Ngamiani Kusini wakati baba huyo aitwaye Richard Leonard (39) alipokuwa akimvizia ili kutekeleza ubakaji huo.
"Uchunguzi wetu wa awali umebaini kwamba sababu ya chanzo cha mtoto huyo kutaka kunywa sumu ili kujiua ni baada ya kuponea chupuchupu kubakwa na mtuhumiwa ambaye hata hivyo inadaiwa kuwa ni baba yake wa kambo," alisema.
Aidha, aliongeza, "Leonard tayari tumemkamata na huyu mtoto naye kadhalika ingawa kwa sasa yeye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo kwa matibabu na taratibu za kuwafikisha mahakamani wote wawili zinaendelea."
MTU MMOJA AFARIKI NA DALILI ZA EBOLA, SITA WAWEKWA KARANTINI
Mtu aliyefariki alitajwa kuwa ni Salome Richard (17), anayetoka katika kijiji cha Kahunda wilayani Sengerema.
Akithibitisha kuwapo kwa hali hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema, Dk. Mary Jose, alisema mgonjwa huyo alifikishwa katika hospitali hiyo na ndugu zake watatu akiwa na homa kali huku akitokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema vipimo vya mgonjwa huyo vimepele kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
"Tulimpokea juzi saa 7 mchana kutoka katika kijiji cha Kahunda wilayani hapa akiwa na homa kali akitokwa damu mwilini, lakini kwa tahadhari tulimweka wodi maalum peke yake akipatiwa matibabu na ilipotimu saa 8 usiku alifariki dunia," alisema.
Alisema kutokana na tahadhari ya ugonjwa huo, watumishi watatu wa idara ya afya na ndugu watatu wa marehemu huyo, wamezuiliwa kwa kuwekwa katika uangalizi maalum hadi matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa vitakaporejeshwa toka Muhimbili.
Akizungumzia tukio hilo, muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo, Daniel Mihayo, alisema timu maalum ya watalaam na viongozi wa mkoa walienda hospitalini hapo juzi na kuondoka na vipimo vya mgonjwa huyo kabla hajafariki dunia kwa kuzingatia maelekezo ya serikali ya kuchukua tahadhari linapotokea tukio kama hilo.
"Kwa sasa jamii inatakiwa kuepukana na uzushi uliozagaa kila kona kuhusu mgonjwa huyo kufarikikwa ebola…tunawamba wasiwe na wasiwasi kwani hatua stahiki zinachukuliwa kwa wagonjwa wa aina hiyo kama tahadhari," alisema Mihayo.
Mhudumu aliyempokea mgonjwa huyo katika hospitali hiyo, Fungameza Majula, alisema ndugu watatu walimpeleka mgonjwa huyo kwa taksi lakini alipobaini dalili hizoaliujulisha uongozi wa hospitali na mara moja hatua za tahadhari zilichukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwazuia ndugu kurudi nyumbani.
Hata hivyo, juhudi za kumpata mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Careen Yunusu, kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa.
Akizungumzia tukio hilo, mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza, Valentino Bangi, alisema alipokea taarifa za mgonjwa huyo kufariki kwa homa inayofanana na ugonjwa wa ebola au maburgh.
Akizungumza na NIPASHE jana, Bangi alisema ofisi yake imetuma timu ya wataalam wa afya katika Hospitali ya Wilaya Sengerema na kuchukua sampuli ya vipimo vya mgonjwa na kupeleka Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
"Ni kweli nimepata taarifa hizo tangu juzi, ila vipimo vimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi kubainisha iwapo amefariki kwa ebola au arburg…nimefahamishwa alikuwa na dalili zote za magonjwa hayo," alisema Bangi.
Bangi alisema ili kukabiliana na mlipuko wa magonjwa hayo, tayari taifa, uongozi wa mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na ofisi yake, wameweka vituo vya kupima magonjwa katika mipaka ya Sirari, Mutukula na uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Alisema tayari wataalam wa afya wamepewa mafunzo ya kukabiliana na ugonjwa huo na kusambazwa katika mipaka hiyo.
"Natoa wito kwa wananchi wote kujiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima kwani magonjwa haya yanaambukiza kwa haraka kwa kugusana na mgonjwa aliyeambukizwa au kushika majimaji na damu ya mgonjwa," alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza na Kamati ya Afya ya Msingi mkoa wa Mwanza alisema ni wakati muafaka kwa jiji na halmashauri zake kutoa elimu juu ya magonjwa hayo ili wananchi wajue dalili na namna ya kujikinga na ugonjwa huo.
Ndikilo alisema mkoa wake unapata wageni kutoka Uganda hususani wafanyabiashara wanaoleta bidhaa zao nchini kupitia Mutukula, na Watanzania wengi kwenda huko kwa sababu mbalimbali.
KAMATI NDOGO YAUNDWA KAGERA
Katika kukabiliana na hilo, Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Kagera, umeunda kamati ndogo ya watu 19 kwa ajili ya kufuatilia magonjwa ya maburg na ebola.
Dk. Rutachunzibwa Thomas, alisemakamati hiyo itakuwa inashughulikia masuala mbalimbali ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi.
SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa mlipuko wa ugonjwahuo umeongezeka kwa asilimia 70 na wagonjwa wapya wanaweza kuongezeka hadi kufikia 10,000 kwawiki kwa kipindi cha miezi miwili.
Taarifa hii imeandaliwa na Renatus Masuguliko, Sengerema, Pendo Paul, Mwanza Na Lilian Lugakingira, Bukoba.
Chanzo: Nipashe
KIJANA APIGISHWA MBIZI KWENYE DIMBWI LA MAJI
Kijana huyo alikutana na adhabu hiyo kali kutoka kwa mjeda huyo baada ya kumbaini kuwa si askari halisi ya jeshi la Tanzania wakati alipokamatwa na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusiana na swala zima la kijeshi, na hapo ndipo alipoanza kuamuliwa kuvua mavazi hayo na kisha kuaza kutumikia adhabu hiyo.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.
VIFO VYA LORI LA MAFUTA VYAFIKIA SITA
Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 347 BXG mali ya Moil Transporter lililokuwa likitarajiwa kusafirisha mafuta kuelekea Kampala, Uganda likiwa na kemikali aina ya petroli lita 38,000 inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola 36,000 (Sh milioni 60).
Aliwataja waliokufa kuwa ni Hassan Mohammed (25), mkazi wa MbagalaKimbangulile, Masoud Masoud (33), Mohammed Ismail (19), RamadhaniKhalfan (36) na Maulid Rajabu, wakazi wa Mbagala Charambe.Majeruhi waliotambuliwa ni Hamis Ally (35), mkazi wa Mbagala Kiburugwa, Rajabu Selemani (28), mkazi wa Tandika, Idd Said (28), Janney Mathayo (25), mkazi wa Mbagala Kizuiani, Mathayo Daniel (21), mkazi wa Mbagala Charambe na askari polisi, Koplo Thomas aliyejeruhiwa na jiwe kwenye paji lauso wakati akijaribu kuzuia vibaka kuchota mafuta kabla ya kulipuka.
Alisema majeruhi wengine 10 wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Wilaya ya Temeke wakiendelea na matibabu na wengi wao hali zao siyo za kuridhisha.Kamanda Kova aliongeza kuwa, mbali ya kusababisha vifo na majeruhi, ajali hiyo pia ilisababisha kuungua kwa nyumba ya kulala wageni iitwayo United yenye vyumba 32, mali ya Deus Kasigwa (42), mkazi wa Mtoni Mtongani.
Moto huo uliteketeza pia maduka matano yenye vitu vyenye thamani ya Sh milioni 197 na pipikipiki saba ziliteketea kabisa na moto.Naye Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya taifa ya Muhimbili, Doris Ishendaalisema majeruhi 11 wanaoendeleakutibiwa hospitalini hapo, huku akiongeza kuwa, hali zao sio nzuri kwa kuwa waliunguzwa vibaya na moto na kwamba madaktari wanaendelea kuwapatia matibabu.
''Majeruhi wote wamelazwa katika wadi namba 22 ya Sewa Haji wanaendelea na matibabu, lakini hali zao sio nzuri kabisa kwani waliungua sana,'' alisema Ishenda.
Wakati huo huo, Paulo Milanzi (35), mkazi wa Chanika katika manispaa ya Ilala anayetuhumiwa kushiriki katika mauaji ya Ofisa Usalama wa Taifa, Sylvanus Mzeru, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katikamajibizano na polisi.
Kova alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu kuhusu matukio mbalimbali ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
BINTI WA MIAKA 7 ABAKWA NA KUUAWA KINYAMA
Mwanafunzi huyo wa darasa la kwanza (jina linahifadhiwa), mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye shamba karibu na nyumbani kwao jana maeneo ya Mbezi Temboni, kata ya Saranga.
Akisimulia tukio hilo, mama wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa), alisema kuwa juzi baada ya mwanawe kurejea toka shuleni alimuogesha na kumpa chakula majira ya saa 12 ya jioni.
Alisema baada ya kumtayarishia chakula hicho, alitoka kidogo kuelekea Temboni na aliporejea nyumbani hakumkuta mtoto wake na ndipo alipokwenda kwa majirani kumtafuta.
Alisema mpaka saa 1 usiku hawakufanikiwa kumuona mtoto huyo licha ya kuambiwa mara ya mwisho alionekani akiwa anacheza na mtoto wa jirani yake.
Hata hivyo, alisema alipokwenda kwa jirani kumuulizia kama wamemuona, alijibiwa kuwa alionekana akiwa anacheza pembeni ya banda la nguruwe.
Alisema baada ya kufanya jitihada zote bila mafanikio aliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.
Aliendelea kusimulia kuwa jana majira ya saa 2 asubuhi, alipata taarifa ya kuonekana kwa mwili wa mtoto wake kwenye shamba moja lililopo karibu na nyumbani kwake.
Alisema mwili wa mwanawe umekutwa ukiwa umepandishwa nguo alizovaa juu huku nguo ya ndani ikiwa imevuliwa.
Aidha, sehemu zake za siri zilikutwa zikiwa na uwazi kitendo kinachoonyesha kuwa aliingizwa kitu na kunyofolewa baadhi ya viungo.
"Roho inaniuma sana mwanangu jamani wamembaka na kisha kupanua sehemu zake za siri inaonyesha kuna vitu vimechukuliwa na shingo yake wamemkata hata kwenye kichwa chake karibu na paji la uso wamempiga kwa tofali,"alisema.
MMOJA WA WATUHUMIWA AKAMATWA
Baba wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) akizungumza huku akitokwa na machozi alisema mmoja kati ya watu waliofanya unyama huo amekamatwa.
"Pamoja na kukamatwa kwa mtuhumiwa lakini wameniachia kovu la huzuni,"alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo amewataja na wenzake wawili walioshiriki kufanya unyama huo ambao wanatafutwa na polisi.
Mwili wa mtoto huyo umehidhiwa katika Hospitali ya Tumbi na umeshafanyiwa uchunguzi.
Habari za uhakika ambazo NIPASHE imezipata ni kuwa mtuhumiwa aliyekamatwa alikutwa na damu kwenye chupi yake baada ya kukaguliwa na askari.
Mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuonekana mara ya mwisho na marehemu, aliwataja wenzake baada ya kubanwa na askari.
MAJIRANI WAZUNGUMZA
Akizungumza kwa niaba ya majirani, Halima Omary, alisema taarifa za kuonekana kwa mwili wa mtoto huyo walizipata kutoka kwa mmiliki wa shamba hilo baada ya kufika shambani kwake asubuhi na kuona kishimo cha damu.
Anasimulia kuwa baada ya kuona shimo hilo la damu alifuatilia michirizi ya damu hiyo shambani hapo ambayo ilikuwa ikionyesha kama kuna mtu kaburuzwa.
"Baada ya mama huyo kufuatilia damu hizo shambani kwake, ndipo alipokutana na maiti hiyo na kuondoka kwenda kutoa taarifa kwa majirani na watu walipofika wakagundua ni yule mtoto aliyekuwa akitafutwa baada ya kupotea,"alisema.
Alisema baada ya kufika katika tukio hilo walimkuta mtoto huyo akiwa amejeruhiwa katika maeneo ya sehemu zake za siri, kifuani, shingoni na kichwani.
Omary alisema kuna haja ya serikali kuwachukulia hatua watu wenye mapori ambao hawayaendelezi ili yasitumike kufanyia matukio kama hayo.
Naye Marry Machange ambaye ni jirani wa marehemu aliitaka serikali iingilie kati suala hilo, kwani katika Kata ya Saranga kuna mapori makubwa ambayo yanatakiwa kuendelezwa hata kwa kujengwa zahanati kuliko kuachwa kuwa sehemu za kufanyia mauwaji.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kata ya Saranga, Godwin Muro, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema alipata taarifa za kupotea kwa mtoto huyo saa 12 jioni na kuamua kusambaza taarifa hiyo katika kituo cha polisi cha Mbezi na kwa wananchi.
Mjumbe wa nyumba 10 shina namba 25 katika eneo hilo, Asibwene Mwaipopo, alisema tukio hilo ni la kinyama na halijawahi kutokea katika eneo hilo.
Naye Diwani wa kata ya Saranga, Efyemu Kinyafu, alisema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa na kuwataka wananchi wasubiri majibu kutoka kwa polisi ambao wanaufanyia uchunguzi mwili wa marehemu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtoto huyo katika maeneo ya shingoni amekatwa na kitu chenye ncha kali.
"Kuna tatizo limeonekana huenda ameingiliwa sana hivyo siwezi kuthibitisha kama sehemu zake zimekatwa kuna mambo mengine hayapaswi kuzungumzwa ni ya kidaktari zaidi,"alisema.
Kamanda Wambura alisema mpaka sasa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja na wengine wawili wanaendelea kuwasaka ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Chanzo: Nipashe
CHRIS BROWN ACHAFUA HALI YA HEWA TWITTER
''Sijui , lakini nadhani Janga la Ebola ni njia moja ya kudhibiti idadi ya watu duniani...janga hililinatisha kweli,'' aliandika Brown.
Saa chache baadaye alionekana kufahamu uzito wa kauli yake naambavyo uliwakera watu kwenye mtandao huo na baadaye kusema....''afadhali nikimye.
Ujumbe wa Brown ulisambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet.
Hata hivyo watu hawahukufurahia matamshi ya Chris Brown kwani walaionekana wakimjibu kwa ukali baadhi wakisema, mwimbaji huyo anapaswa kunyamaza ikiwa hana cha kusema.Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000 katika kanda fa Afrika Magharibi.
Ugonjwa huo umeenea hadi Uhispania na nchini Marekani ambako mgonjwa mmoja aliyueingia nchini humo akiwa ameambukizwa Ebola alifariki wiki jana.
MAASKOFU KATOLIKI KUJADILI USHOGA
Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja, lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa jamii zao.
Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti.
Zaidi ya maaskofu 200 wa kanisa katoliki wanakutana kwenye mkutano wa synodi tangu mapema mwezi huu, katika mkutano huo ni papa Francis aliyetoa mwito wa kujadili masuala ya utoaji wa mimba,vidonge vya uzazi wa mpango,mapenzi ya jinsia moja na talaka.
Papa Francis amewataka viongozi wa juu wa kanisa hilo kuzingatia Zaidi suala la wapenziwa jinsia moja chanya kuliko kuwa kinza na amefanikiwa kuwateka maaskofu wanaohudhuria mkutano huo wa sinodi.
Mwaka uliopita katika ripoti aliyo itoa papa Francis kuhusiana na mwenendo wa kanisa katoliki kuwa waumini walio wengi waliliacha mkono kanisa hilo kutokana na mafunzo yahusianayo na ngono na dawa za uzazi wa mpango.
Papa huyo anazichukulia ndoa hizo za jinsia moja kama zisizo na utaratibu akiinukuu ripoti ya kanisa katoliki iliyochapishwa mwaka 1986, wakati Papa Francis alipokua mshauri mkuu wa masuala ya teolojia ya kanisakatoliki wa hayati papa John Paul wa pili.
Nguvu kubwa ya vikundi vya kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja ni juu yakauli ya papa Francia aliyoitoa mwishoni mwa mwaka wa jana alipokuwa kwenye kambi ya vijana wa kanisa hilo huko Rio de Jeneiro alitoa kauli kua kamamtu anamtafuta Mungu na ana nia njema ,yeye ni nani wa kuhoji? Papa Francis anaingia katika historia ya kanisa katoliki ulimwenguni kutumia jina (hasha kum si matusi) WASENGE hadharani kuliko kutumia neno wapenzi wa jinsia moja.
JESHI LA POLISI ZANZIBAR LANASA RISASI 123
Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini unguja kamishna msaiidzi Juma Saadi Khamis ambaye alifika kwenye tukio amethibitisha kupatikana kwa risasi hizo amabzo zilikuwa ndani ya magazini nne na zilikuwa zimezongwa ndani ya majani ya mgomba ambapo wachimba kisima waliokuwa wakikisafisha ndio walioziibua na kuzitoa ambapo awali hawakuzieelewa kama ni risasi ambapo mmoja yao mchimbaji Gefrey Silas amesema wao waliziweka juu na wakaja vijana wawili wakazichukua baadhi yake na ndipo wakatoa taarifa kwa Polisi jamii.
Akitoa maelezo ya ziada kamanda juma amewataja watu wawili Abdullah Suleiman na Mateo Makungu maarufu dilli wote wakazi wa kizimbani ambao walizichukua na kuzifikia eneo lengine huku akithibitisha risasi na magazine zote zimepatikana na upelelzi bado unaendelea huku risasi hizo zikionekana ni za muda.
Hili ni tukio la pili la Polisi kukamata shehena kubwa za risasi za vita katika kipindi cha miezi mitatu ambapo risasi hizo zimekutwa katika shamba linalomilikiwa na mmoja ya mwananchi na eneo hilo halina makazi ya watu ilawalinzi tu na kisimaa hicho kimekuwa hakitumiki kwa muda mrefu.
RAIS WA ZAMANI WA MADAGASCAR AKAMATWA
Mwandhi wa bbc mjini Antananarivo amesema kuwa vitoa machozi vilirushwa na badaye vikosi vya usalama vikaonekana nje ya nyumba yake.
Serikali ya kisiwa hicho cha bahari Hindi mara nyingi imezuia kurudi kwake nyumbani tangu mpinzani wake Andry Rajoeline amuondoe madarakani kwa njia ya kijeshi.
Miaka minne iliyopita rais huyo wa zamani alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani bilaya yeye kuwepo mahakani kutokana na mauaji ya watu 30 wafuasi wa upinzani.
TAIFA STARS YAITWANGA BENIN GOLI 4 KWA 1
Kabla ya mchezo uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya115 katika viwango vya ubora vya Fifa duniani, ikishika nafasi ya 34 barani Afrika, huku Benin ikiwa katika nafasiya 78 duniani na 18 barani Afrika.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na Nadir Haroub Cannavaro, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu na Juma Luizio akiifungia timu ya stars huku la kufutia machozi la Benin likitumbukizwa wavuni dakika ya 90 ya mchezo na Ssegnon Stephane anayechezea timu ya West Bromwich Albion ya England.
Katika uwanja huo huo wa Taifa kabla ya mchezo wa Tanzania na Benin, mchezo mwingine wa kuvutia ulizikutanisha timu za viongozi wa dini waliochanganyika katika timu mbili wakiwemo Mashekhe na Maaskofu.
Viongozi hao waliunda timu za Amani na Mshikamano, ambapo Amani waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mchezo huo ulilenga kuonyesha ushirikiano wa kijamii kati ya waumini wa dini kubwa mbili nchini Tanzania za Waislam na Wakristo.
BOTI YAZAMA, YAUA WATATU MAHARUSI WAOKOLEWA
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohammed zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Kalalangabo Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.Akielezea tukio hilo, Kamanda Mohammed amesema kuwa hadi sasa haijafahamika ni watu wangapiwalikuwa wamepanda kwenye boti hiyo kwani haikuwa imesafiri katika taratibu za kawaida ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya usalama wa nchi kavu na majini (SUMATRA).
Kamanda huyo wa Polisi alisema kuwa vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na wavuvi waliowahi kufika katika eneo hilo walifanikiwa kuokoa watu 20 ambao walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Kigoma ya Maweni kwa matibabu na wengine inawezekanawalikimbia ili kupoteza ushahidi waidadi ya abiria waliokuwa kwenye boti hiyo.
Kwa upande wake Mganga wa Zamu katika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni, Haika Masula amethibitisha kupokelewa kwa miili mitatu ya watu waliofariki kwenye tukio ambapo mmoja ametambuliwa kwa jina la Salama Juakali huku maiti wawili watoto wakiwa hawajatambuliwa hadi sasa.
Masula alisema kuwa katika idadi ya majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo hadi kufikia jana mchana watu 11 waliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na hali zao kurejea katika hali ya kawaida.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Wavuvi kwenye Mwalo wa Kibirizi mjini Kigoma, Sendwe Ibrahim alisema kuwa walipokea taarifa za kuwepo kwa ajali ya boti juzi kuanzia majiraya saa tisa mchana na boti zikaanzakuelekea eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada.Mwenyekiti huyo alisema kuwa hiyo haikuwa boti ya kubeba abiria ilikuwa ni boti ya uvuvi ambayo kwa idadi inayopaswa kubeba haipaswi kuzidisha abiria 20 na ndiyo maana boti hiyo ilipandisha watu kinyemela katika Kijiji cha Kalalangabo badala ya bandari ndogo ya Kibirizi mjini Kigoma.
Ajali hiyo imetokea wakati ShaabanHussein na Mariam Juma (18) wakazi wa Kijiji cha Mtanga wakitoka kufunga ndoa kwenye Kijiji cha Mwandiga Kigoma vijijini nyumbani kwa bibi harusini na ambapo hali za maharusi hao ambao walikuwemo ndani ya boti wakisindikizwa na ndugu na jamaa zao zinaendelea vizuri.Bwana harusi aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo jana asubuhi wakati hali ya bibi harusi ikiendelea vizuri huku akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitaliya Maweni.
Chanzo: Habari Leo
MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO MZUMBE UNVERSITY
Chuo kikuu cha Mzumbe kimetoa majina ya wanafunzi watakao jiunga mwaka wa kwanza wa masomo ya shahada ambao wameweza kupata mkopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania.
Kwa wanafunzi wa vyuo vingine Bofya hapa na fuata maelekezo jinsi ya kuangalia kama inavoonesha hapa chini.
WATUMISHI 1,360 WAKUTWA NA VYETI FEKI
UDANGANYIFU katika vyeti wakati wa kuomba ajira umeendelea kukithiri nchini, ambapo ndani ya mwaka mmoja tu, kuanzia Julai mwaka jana mpaka Juni mwaka huu, watumishi 1,360 wamekutwa na vyeti visivyo halali. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, alisema hayo jana mbele ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk ShukuruKawambwa, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya baraza hilo.
Katika uhakiki huo, baadhi ya watumishi wakiwemo wa Serikali walikutwa wakitumia vyeti vya kughushi ambavyo imebadilishwa matokeo, wengine walikutwa na vyeti vyabandia huku wengine wakitumia vyeti vya watu wengine.
Hii si mara ya kwanza kwa Serikali kuelezea uozo huo katika elimu, ambapo Julai mwaka jana Msemaji wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Riziki Abraham, alitoa taarifa ikielezakuwa Sekretarieti hiyo ilibaini kuwepo kwa udanganyifu wa vyeti 677, kwa watumishi serikalini.
Aidha, Oktoba mwaka jana Ofisa Habari na Mawasiliano waOfisi ya Sekretarieti hiyo, Kasim Nyaki, alieleza kuwa vyeti vya Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi (Veta) ni miongoni vyeti vinavyoongoza kutumiwa katika udanganyifu kwa watu wanaoomba kazi kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Nyaki alisema kuwa kati ya watu 517 waliotumia vyeti vya Veta kuomba ajira kupitia sekretarieti hiyo, watu 304 walitoa vyeti halali, lakini watu 213 walighushi.
Mbali na hao, alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa kati ya watu 13,554 walioomba ajira katika miaka mitatu yaani 2010, 2011 na 2012, watu 816 walibainika kudanganya kwa kutumia vyeti vya taasisi mbalimbali za elimu, vyeti vya kuzaliwa na vinginevyo.
Kutokana na hali hiyo, Dk Msonde alisema Baraza hilo limeamua kushirikiana kwa karibu na mamlaka za ajira na udahili, ili kuhakikisha uhakiki wa vyeti vinavyotolewa na baraza hilo, unafanyika kabla ya mtahiniwa kuajiriwa au kudahiliwa.
Mbali na ushirikiano huo, Baraza hilo limeazimia kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya kutumia udanganyifu katika vyeti.
Aidha, Baraza hilo pia limeanzakutoa vyeti vyenye picha ya mmiliki kuanzia 2008, ili kupunguza kasi ya udanganyifu huo.
Katika hatua nyingine, Baraza hilo limeanza utaratibu wa kutoa vyeti mbadala kwa watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa waliohitimu kuanzia mwaka 2008 ambao vyeti vyao vilikuwa na picha.
Dk Msonde alisema hatua hiyo ya kutoa vyeti kwa waliopoteza,inatarajiwa kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa sababu mbalimbali kwa kupata vyeti mbadala, huku likiweka utaratibu madhubuti kuhakikisha fursa hiyo haitumiwi vibaya.
Akizungumzia kudhibiti wizi na udanganyifu katika mitihani, alisema Baraza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na kwa kiasi kikubwa na kudhibiti udanganyifu wakati wa ufanyaji mitihani.
Alisema Baraza hilo linakabiliwa na upungufu wa fedha za kuendesha mitihani yataifa, ambao usipofanyiwa kazi,utaathiri uendeshaji wa mitihani ya kidato cha sita na ualimu.
Ukata huo alisema pia utaathiriuongezaji wa viwango vya posho za wasahihishaji kwa mitihani ya kidato cha nne, sitana mitihani ya ualimu kama ilivyokuwa imepangwa.
Alisema katika mwaka wa fedha 2014/15, kulikuwa na umuhimu wa kuongeza posho ya wasahihishaji kwa kuwa posho hiyo imekuwa ikilalamikiwa na washiriki kwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na posho zinazolipwa na mamlaka nyingine, ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa shughuli za mitihani.
Akizindua bodi hiyo, Waziri Kawambwa alisema wakati matokeo ya kidato cha nne mwaka huu yakianza kutolewa kwa mfumo mpya wa Wastani wa Pointi (GPA) ni vema kutoa elimu wakati huu kabla na baada ya mtihani, ili kuzuia mtafaruku.
Alisema utoaji wa elimu kwa wadau wote wa elimu, wanafunzi na wazazi utasaidia kudhibiti upotoshaji mara utekelezaji utakapoanza.
“Hili lifanywe kwa juhudi na umakini ili kuepusha upotoshaji unaoweza kufanywa na baadhi ya watu, elimu kuhusu mfumo mpya wa kutunuku matokeo itolewe kwa kutumia aina zote za mawasiliano na umma kabla, wakati na baada ya mitihani.
Bodi hiyo mpya inaongozwa na Mwenyekiti wake, Rwekaza Mukandala na wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma), Profesa Makenya Mabhoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Benedict Misani na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi, Mahmoud Mringo.
Wengine ni Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani la Zanzibar, Ameir Selemani Haji, Mkuu wa Skuli ya Ualimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Dk Maryam Jaffar Ismail, Mkurugenzi wa Idara ya Sekondari, Asia Iddi Issa, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Shaban Kamchacho, Mkuu wa Sekondari ya Kisimiri Meru, Emmanuel Kasongo na Mwalimu Mkuu Shule ya MsingiKimara Baruti, Rehema Ramole.
TCU YATOA ONYO KWA WANAFUNZI WANAODAHILIWA MOJA KWA MOJA NA VYUO
TAARIFA KWA UMMATume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ina mamlaka kisheria kusimamia na kuratibu udahili wa Wanafunzi wote wanaojiunga na Vyuo Vikuu vyote nchini Tanzania.
Tume imebaini kuwa, hivi karibuni baadhi ya Vyuo Vikuu vimekuwa vikitangaza kudahili Wanafunzi moja kwa moja kupitia Vyuo vyao kwa mwaka wa masomo 2014/2015.
Ifahamike kuwa, utaratibu unaotambulika kisheria ni wa kudahili Wanafunzi kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania na si vinginevyo.
Hivyo mwanafunzi atakayeomba na kupatiwa udahili kupitia Chuoni moja kwa moja, udahili wake hautatambulika.
Tume inapenda kusisitiza kuwa waombaji wote wenye sifa za kujiunga na Vyuo Vikuu wanapaswa kufuata tartibu na miongozo iliyowekwa na Tume.
Taarifa hii imetolewa na KatibuMtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu.
Kwa mawasiliano zaidi, barua pepe es@tcu.go.tz na/au simu +255 222772657
MELI YA MV VICTORIA YANUSURIKA KUZAMA
Baadhi ya abiria waliokuwa wanasafiri na meli hiyo kutoka mjini Bukoba kwenda mwanza wamesema meli hiyo imekuwa ikipata hitilafu za mara kwa mara bila kuchukuliwa hatua na kwamba katika safari ya jana meli hiyo iliondoka mjini bukoba saa tatu usiku lakini ilizima mara tatu ndani ya maji na hivyo ikachelewesha safari ya meli hiyo ambayo ilifika katika bandari ya kemondo saa tisa usiku na kuleta usumbufu na wasiwasi kwa abiria waliokuwa wanasafiri na meli hiyo.
Kwa upande wake nahodha wa meli hiyo John Mwita amesema meli hiyo ilipata hitilafu kutokana na usukani kuwa mbovu hali ambayo ilisababisha meli hiyo kuzimika mara kwa mara na kwamba tayari kampuni ya huduma za meli imeagiza vipuri kwaajili ya matengenezo ya meli hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea na safari baada ya matengenezo kukamilika ambapo meneja wa bandari ya kemondo joashi miso amesema meli hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya mia nne na hamsini na tani mia moja na hamsini za mizigo na amewataka abiria kuwa watulivu wakati taratibu za kutatua tatizo hilo zikiendelea.
Kufuatia tukio la kukwama kwa meli hiyo ya mv victoria katika bandari ya kemondo, wengi wa abiria wa meli wakiwa na hasira walifunga barabara kutoka mjini bukoba kwenda muleba inayopita karibu na bandari ya kemondo kama njia ya kushinikiza uongozi wa bandari kuwarudishia nauli ili waweze kuendelea na safari yao kwa njia ya barabara ingawa baadae jeshi la polisi mkoani kagera lilifanikiwa kudhibiti hali hiyo na kuruhusu magari kuendelea na safari zao.
JESHI LA POLISI LAWAFUTA KAZI ASKARI WATATU WALIOPIGA PICHA ZA KULIZALILISHA JESHI HILO.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe, alisema kitendo kilichofanywa na askari hao kimeshusha hadhi ya jeshi.
Aliwataja askari hao waliofukuzwa ni F.7788 PC Mpaji Mwasumbi, G 2122 PC Fadhili Linga na WP.8898 Veronica Mdeme ambao wote ni wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Misenyi.
Alisema PC Mpaji na WP Veronica walipiga picha inayokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi wakiwa kazini, huku PC Fadhili akiingia matatani kwa kuwapiga picha hiyo chafu askari wenzake na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Kamanda Mwaibambe alisema picha hiyo ilianza kuonekana katika mitandao mbalimbali ya kijamii mapema wiki hii.
Alisema askari PC Fadhili alipiga picha hiyo mwaka 2012 kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kuitunza, lakini wiki hii aliamua kuisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume na kazi yake.
“Napenda kuthibitisha kuwa picha hii iliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa kabisa.
“Maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari wetu wanafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi na si vinginevyo.
“Jeshi halikubaliani na vitendo hivi, ikitokea askari kwenda kinyume lazima achukuliwe hatua kali,” alisema Kamanda Mwaibambe.
Taarifa zaidi kutoka mkoani Kagera, zinaeleza baada ya kusambazwa kwa picha hiyo na kuonekana katika mitandao ya kijamii, WP Veronica alianguka ghafla na kupoteza fahamu kwa mshtuko wa tukio hilo.
Kutokana na hali hiyo, majirani waliokuwa karibu na nyumbani kwake walilazimika kumpatia msaada na kumkimbiza hospitali kwa matibabu, ambako aliruhusiwa juzi jioni kabla ya kutiwa mbaroni.
DAR ES SALAAM
Wakati hayo yakiendelea, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewahamisha askari wake, WP 5863 Quine na WP 3548 Koplo Maeda kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ilala kwa kukiuka maadili ya kazi.
Taarifa ya ndani ya Oktoba 2, mwaka huu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Dar es Salaam iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, imesema askari hao walisimamisha gari dogo na baada ya dereva kujitetea, waliendelea kutafuta makosa hali iliyosababisha abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki.
Kutokana na tukio hilo, makamanda wa polisi wa wilaya zote za Mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam wametakiwa kuwakumbusha askari wao kuepuka kutolazimisha kutafuta makosa ambayo hayana madhara.
“Makosa ambayo hayana madhara katika kusababisha ajali mfano ni vifaa vya kuzimia moto, rangi, kadi kutoandika anuani, motor vehicle, leseni chini ya siku 30 na kadhalika,” lilisomeka agizo hilo kwa makamanda hao wa polisi
WATU SABA WA FAMILIA MOJAWAUAWA NAKUCHOMEWA NYUMBA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA
KENYATTA ANA KWA ANA NA ICC
![]() |
| Rais Kenyatta akiwa ICC |
Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi muhimu.
Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.
Kikao cha leo kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi mahakama hiyo ushahidi unaohitajika kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.
Upande wa utetezi nao unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea.
Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda, amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko katika awamu muhimu sana.
Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea kwa niaba yake.
RAIS KIKWETE KUKABIDHIWA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA
Tukio hilo la kihistoria linafanyika mjini Dodoma likitarajiwa kuhudhuriwa na watu wa kada tofauti wakiwamo mabalozi wa nchi karibu zote ambao wamealikwa.
Kwenye sherehe hizo ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ally Mohamed Shein watakabidhiwa Katiba hiyo huku polisi mkoani Dodoma ikiwahakikishia umma usalama wa kutosha.Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema "Tumealikamabalozi wa nchi karibu zote…sijajua waliothibitisha kufika ingawa hakuna aliyetoa udhuru.
"Licha ya mabalozi wanaotarajiwa kutoka nchi mbalimbali, kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi, sherehe hizo zitahudhuriwa pia na viongozi kutoka nje ya nchi. Pia kutakuwa naviongozi wakuu wastaafu, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla.
Usalama Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya mji.
Alisema zinafanyika doria kwa miguu, mbwa, farasi, magari na pikipiki kuhakikisha sherehe hizo zinafanyika kwa utulivu mkubwa.
Pia wamiliki wa nyumba za wageni wametakiwa kuimarisha ulinzi. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kamanda alisema ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali nakuzifanyia kazi umeimarishwa zaidi.
Kamanda Misime alisema vyombo vyote vya dola vimeimarisha zaidi ushirikiano hasa kubadilishana taarifa mbalimbali na kufuatilia tukio hilo muhimu kwa kutumia mbinu zote walizo nazo.
"Niwahakikishie wananchi wa Mkoawa Dodoma na wageni wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa; Tunachowaomba ni ushirikiano wao pale watakapomtilia mashaka mtu yeyote au jambo lolote wajulishe Polisi haraka nasi tutalifanyia kazi," alisema Misime.
Pia wenye nyumba za kulala wageni, pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yao, wameelekezwa wakitilia mashaka mgeni yeyote watoe taarifa Polisi.
Alihadharisha kwa kusema anayepanga kukiuka sheria kwa lengo la kuvunja amani na utulivu, atashurutishwa kwa nguvu kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa mamlaka iliyopewa jeshi lake.
Safari ya Katiba mpya Hatua mbalimbali zimepitiwa kabla ya kupatikana Katiba Inayopendekezwa Oktoba 2, 2014 iliyopitishwa kwa kura zinazostahili. Mchakato wa kupata Katiba mpya ulianza na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa mabadiliko Februari, 2012.
Rais Jakaya Kikwete aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa mujibu wa Kifungu 6(1) cha sheria hiyo.
Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na kuapishwa na Rais Kikwete, Aprili, 2012 na ikapewa miezi 18 kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo ilikuwa Mei 2, 2012. Uzinduzi wa Rasimu ya Katiba Mpya ulifanyika Juni 3, mwaka jana katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Bunge Maalumu la Katiba lilianza Februari mwaka huu. Lilikwenda hadi Aprili kabla ya kuahirishwa kupisha Bunge la Bajeti na kisha kuanza awamu nyingine Agosti 5 mwaka huu.
Hata hivyo, sehemu ya wajumbe wa bunge hilo wanaojiita Umoja wa Wabunge wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walisusa ingawa mchakato ulioendelea hadi Oktoba 2, mwaka huu ilipopatikana Katiba Inayopendekezwa.
Kususa kwa kundi hilo, hakukuathiri mchakato huo kuendelea lakini umechelewesha hatua inayofuata kwa kuwa baada ya kupatikana Katiba Inayopendekezwa, hatua nyingine ingekuwa Kura ya Maoni.
Lakini kulingana na makubaliano yaliyofanyika hivi karibuni kati ya Rais Kikwete na viongozi wa vyama vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), mchakato wa kura ya maoni utafanyika baada ya uchaguzi mkuu mwakani; kwa maana utategemea utashi wa rais ajaye.
Walikubaliana kwamba kwa mujibuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, baada ya bunge hilo kumaliza kutunga Katiba, ingefuata hatua ya kura ya maoni kuthibitisha Katiba.
Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo alisema walikubaliana kwamba kwakutambua kuwa hatua ya kura ya maoni italazimisha uchaguzi mkuu 2015 kuahirishwa, basi hatua hii iahirishwe na mchakato wa Katiba uendelee baada ya uchaguzi mkuu.
Wakati huohuo, msemaji wa Ukawa ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema:
"Hatutahudhuria, kwa sababu hatuna mwaliko, sisi ni taasisi, kama mabalozi wamealikwa na watu wengine kwenye sherehe hiyo, na sisi tungealikwa kwa barua".
Hata hivyo, alipoulizwa ikiwa wangepata mwaliko kama wangehudhuria, Mbatia alisema ingetegemea na maudhui ya baruaya mwaliko na kwamba hawezi kuzungumzia zaidi kwa kuwa hana huo mwaliko.
Kwa upande wao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa kimesema kinachambua Katiba Inayopendekezwa na nyaraka nyingine kwa ajili ya kuzunguka nchi nzima kuipinga kwa wananchi.
Dk Slaa alisisitiza chama chake pamoja na vyama vingine vinavyounda Ukawa, kutohudhuria sherehe hizo za kukabidhiwa kwa Katiba Inayopendekezwa.
"Hatuko tayari sisi Chadema wala Ukawa kuhudhuria sherehe hizo Dodoma," alisema.
Chanzo: Habari Leo
ALIYEBADILI JINSIA ASHINDA KESI
Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa.
Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti hicho kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi la serikali.
Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti hicho haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake vile vile hakuna athari yoyote.
Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa.'Audrey ni mwanadamu ambaye anajitambua kwama mwanamke wala sio kama mwanamume jinsia aliyozaliwa nayo,'' alisema jaji.
Jaji alisema kuwa katiba ya nchi inaamrisha watu kuwaheshimu wengine kama ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo inahusu mambo mengi ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa.
Aliongeza kuwa ili Audrey kuhisi kuwa sawa anapaswa kukubalika kama alivyo na kumyima haki hiyo ya kubadilisha jina lake katika chati chake itakuwa ukiukwaji wa haki zake za kibinadamu.
Wakili wa Audrey, aliambia mahakama kuwamteja wake alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea matibabu.
AL SHABAAB WAPOKONYWA MJI MUHIMU
Wanajeshi hao waliingia mji wa Barawe ulio kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu siku ya Jumatatu baada ya kuuzingira tangu siku ya Jumapili.
Sauti za risasi zilisikika mapema Jumatatu wakati wanajeshi walikuwa wakiingia mji huo. Ripoti zinasema kuwa kwa sasa mji huo umetulia na magari ya kijeshi kwa sasa yanapiga doria.
Mji wa Barawe haujakuwa chini ya serikali kwa miaka 23 na umekuwa chini ya udhibiti wa al Shabab kwa miaka sita iliyopita.
Gavana na maafisa wa kijeshi waliwahutubia wenyeji leo ambapo walitoa wito wa kuwepo kwa utulivu wakisema kuwa nyakati za al-Shabab zimekwisha.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay alipongeza jeshi hilo la pamoja na kusema kuwa sasa Somalia ina mazuri siku za usoni.
Kutwaliwa kwa mji huo ni pigo kwa kundi la al-Shabab lililo na uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.
Al Shabab wamekuwa wakiutumia mji huo kupitisha silaha na chakula na pia kama kituocha biashara ya makaa.
Muungano wa Afrika pia unasema kuwa al-Shabab waliutumia mji wa Barawekupanga mashambulizi yao dhidi ya mji mkuu Mogadishu.
UMASIKINI BADO JINAMIZI DUNIANI
Katika ripoti yake ya kila mwaka, kundi hilo linasema katika baadhi ya mataifa yaliopo Kusini mwa jangwa la sahara bado kuna tatizo kubwa la serikali kutumia kiwango kidogo sana cha pesa kupambana na umasikini na kwamba tatizo hili ni sugu ila linahitaji kutatuliwa.
Pia kundi hilo linasema ufadhili mkubwa bado utahitajika kusaidia juhudi hizo dhidi ya umasikini.
Ripoti hiyo inasema kwamba mataifa yamo katika njia panda katika kukabiliana na umaskini.
Kumekuwa na jitihada nyingi Katika sehemu nyingi. Lakini maendeleo ya siku zijazo, yanatishiwa, kutokana na ukosefu wa usawa, ukosefu wa ajira na jitihada zilizositishwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kundi hilo linasema kuwa wafadhili wengi wanashindwa kulenga na kutoa misaada kwa nchi zilizo maskini Zaidi na zilizomo kwenye hatari.
Ripoti hiyo pia inasema serikali nyingi za Kiafrika hazitimizi ahadi zao za matumizi katika sekta muhimu kama vile za afya, kilimo na elimu.
Ripoti ya ONE inasema mwaka ujao wakati malengo mapya yatatangazwa ya kukabiliana na umaskini wa hali ya juu na maamuzi yatakapo chukuliwa kuhusu ufadhili wa kuyafikia malengo hayo, huenda yakatoa nafasi murwaa na ya kihistoria kwa mataifa hayo.
WANANCHI WA URAMBO WATANGAZA MAANDAMANO YASIYO NA KIKOMO
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kwaniaba ya wakazi wenzao wa Urambo Mashariki; wakazi hao wamesema watachukua hatua hiyo kupinga kile walichokiita kuwa ni hatua ya mbunge wao Mh. Samuel Sitta, kuvuruga mchakato wa katiba kwa kuacha maoni ya Watanzania na kuweka yale yenye maslahi yao ya kisiasa.
Akisoma tamko kwa niaba ya wakazi wenzake, mmoja wa wakazi hao, Bw. Isack Gerald amesema Mhe Samuel Sitta ameongea uongo pale aliposema kuwa maoni yaliyomo ndani ya katiba inayopendekezwa yamejali pia matakwa ya wakazi wa Urambo huku akijua kuwa hajawahi hata siku moja kwenda jimboni kwake kuhoji wapiga kura wake kuhusu maoni wanayotaka yaingie katika katiba mpya.
Katika hatua nyingine, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amewataka wakuu wa wilaya kuzingatia na kufutatilia kwa ukaribu ujenzi wa Maabara katika shule za kata ili kukamilisha Agizo alilolitoa.
Rais Kikwete ameyasema jana mjiniDodoma wakati wa mkutano wa kujadili muelekeo wa Elimu ya msingi na sekondari nchini na kuongeza kuwa hayuko tayari kuonaagizo lake hilo kuupuza kwa kuwa lina lenga kukuza ufaulu wa masomo ya Sayansi nchini Tanzania.
Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu (TAMISEMI).
Bi.Hawa Ghasia amesema mkutano huo utawasaidia wakuu hao wa wilaya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu.
KADI KUTUMIKA KATIKA USAFIRI WA TRENI
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesisitiza ni lazima kufanya haraka kwani mwekezaji, Kampuni ya Ms Shimoja ya Marekani, iko tayari hata sasa kuleta treni hizo aina ya Diesel Multiple Unit (DMU) ambazo ni za kisasa, itakayopita kila baada ya nusu saa.
Usafiri huo wa treni kwenye njia ya umbali wa kilometa 13 kutoka uwanja wa ndege hadi katikati ya jiji, unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu au mapema mwakani ukilenga kubeba abiria kati ya 800 na 1,000.
Katika hafla ya kutia saini kati ya mwekezaji huyo na Shirika la Reli Tanzania (TRL) jana jijini Dar es Salaam, Waziri Mwakyembe aliwaambia watendaji kwamba ikiwa watafanya haraka, baada ya wiki mbili watasaini makubaliano ya mwisho na kuanza urekebishaji na ujenzi wa vituo sita vya kupandia treni kwa kadi.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Ms Shimoja, Dk Robert Shumake na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu walitia saini jana katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri Mwakyembe na Katibu Mkuu wake, Dk Shaaban Mwinjaka.
Waziri Mwakyembe alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kusafisha njia ya kupata wawekezaji, akiwemo mfanyabiashara huyo mkubwa ambaye ametajwa kuwa na imani kuwekeza katika mradi huo utakaogharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 35.
Kwa mujibu wa waziri, waliamua kuanza mradi huo baada ya kuhamasisha mashirika makubwa yandege kufanya safari katika kiwanja hicho cha ndege. Hata hivyo, alisema wasafiri wanapata kero ya usafiri kufika katikati ya jiji jambo wanalotegemea mradi kuondoa kero hiyo.
"Mabehewa hayo yataunganishwa kulingana na idadi ya abiria waliopo na muda, huku mwekezaji akiwekeza bila masharti kama walivyo wengine; kama vile kutaka dhamana ya serikali," alisema Mwakyembe.
Hata hivyo alisisitiza, "lakini ni lazima watendaji waache ukiritimbakwa kufanya utaratibu haraka ili kazi zianze."
Alisema katika utaratibu wa PPP, uwekezaji na idara nyingine lazima wafanye haraka. Aidha alitaka watendaji TRL kumsihi mfanyabiashara huyo kuleta treni nyingine mbili za Ubungo mpaka Stesheni na kwingineko.
Treni hiyo itasaidia kupunguza adha kwa abiria wanaosafiri kwa ndege, ambapo katika kituo cha Karakata, itajengwa njia ndogo ya treni mpakabarabarani. Pia litajengwa daraja kwa ajili ya wasafiri kuvuka na mizigo yao.
Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji waTRL, Kisamfu alisema watafanya kaziusiku na mchana kuhakikisha usafirihuo unaanza mapema iwezekanvyo kutoka katikati ya jiji hadi Pugu kupitia maeneo ya Karakata, kwenye Uwanja wa Ndege kwa kutumia Reli ya Kati.
Mwekezaji Dk Shumake ambaye ni Balozi wa Heshima Tanzania nchini Marekani, alisema wako tayari kuanza mradi huo hata leo kama utaratibu utakamilika.
Alisisitiza kwamba uwekezaji huo utaondoa tatizo la foleni barabaranikutoka uwanja huo wa kimataifa wa ndege hadi katikati ya jiji.
BINTI ATOLEWA KIAZI KILICHOKUWA KINAOTA UKENI
"Mama yangu alinambia ikiwa sitaki kushika mimba niweke kiazi huko na nilimuamini" alisema binti huyo ambaye hakutajwa jina.
Baada ya kiazi hiyo kukaa huko kwa majuma mawili (wiki mbili) mgonjwa alianza kuhisi maumivu makali sana sehemu za chini ya tumbo kwani kiazi kiliota mizizi ndani yake chanzo kimeeleza, madaktari waliomtibu walikuta mizizi ya kiazi kiliyoota ndani ya uke na kiazi kile kiliweza kuondolewa bila kufanya upasuaji wowote na kuwa na uhakika kuwa kufanya hivyo kusingeleta madhara yoyote kwa binti huyo.
Carolina Rojas, nesi wa zamu hospitalini hapo alimshutumu moja kwa moja mama wa binti huyo kwa kumshauri ushauri mbaya wa kuzuia uzazi, tukio hili linaonyesha wazi kuwa kuna uhaba wa elimu ya uzazi miongoni mwa jamii kubwa ya America ya kusini.
Ripoti kutoka katika serikali ya Colombia katika wizara ya afya na uzazi inayoongozwa na Bibi maria Eugenia Rosseli inasema"hakuna mazungumzo ya afya ya uzazi baina ya vijana na wazazi wao inasababisha taarifa potovu na kusababisha ongezeko kubwa la mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa (STD's)
RAIA MWINGINE WA UINGEREZA ACHINJWA NA ISLAMIC STATE
Henning mwenye umri wa miaka 47 ambaye ni dereva wa texi kutoka kaskazini mwa Uingereza alitekwa nyara mwezi Disemba mwaka uliopita alipokuwa akilifanyia kazi shirika moja la kutoa huduma za misaada kwa wakimbizi nchini Syria.
Kundi la Islamic State ambalo limechukua udhibiti kwenye maeneo ya mpaka kati ya Syria na Iraq tayari lishawaua waandishi wa habari raia wa Marekani James Foley na Steven Sotlof pamoja na mfanyikazi wa kutoa huduma za misaada kutoka Scotland David Haines.
Mapema babake John Cantlie raia wa Uingereza ambaye anashikiliwa mateka na wanamgambo wa Islamic State aliomba kuachiliwa kwa mwanawe.
TAHLISO YALIA ADA KUPANDA KIHOLELA
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa TAHLISO, Musa Mdede, alisema kumekuwa na utaratibu mbovu wa vyuo binafsi kupandisha ada, jambo ambalo linawanyima fursa masikini kupata elimu.
Mdede, alivitaja vyuo ambavyo vimeongezaada kuwa ni KCMC Moshi, Bugando Mwanza na St Francis kutoka sh milioni 2 zaawali hadi milioni 5 kwa mwaka.
"Kuna baadhi ya vyuo kama KCMC, kimezuia wanafunzi kuingia chuoni hadi waoneshe stakabadhi inayoonyesha kuwa amelipa ada mpya, japokuwa TCU imekwisha waandikia barua wasitishe ongezeko hilo kwa mwaka wa masomo 2014/15," alisema Mdede.
Aliongezea kuwa asilimia 50 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu nchini kwa mwaka wa masomo 2014/15, watakosa mikopo japokuwa wana sifa ya kukopeshwa.
Mdede, alisema ili kumsaidia kila mtanzania kupata elimu ni vyema serikali ikatoa mikopo kuanzia ngazi ya cheti na stashahada kwa wanafunzi wote wenye sifa.
"Tumefurahi kuona kwa mara ya kwanza nchini, Chuo Kikuu cha Dodoma kuna baadhi ya wanafunzi ngazi ya stashahada wamepewa mikopo, kwa mfano huo serikali ijipange kuwapa mikopo ili tuweze kuwa na taifa la wasomi," alisema Mdede na kuongeza.
Pia, kutokana na kupanda kwa gharama za maisha, serikali inatakiwa kuwapandishia fedha za kujikimu kutoka sh7,500 ya sasa hadi 15,000 kwa siku.
KINSHASA: CHIMBUKO LA UGONJWA WA UKIMWI
Ugonjwa wa ukimwi uligunduliwa miaka ya 1920 mjini Kinshasa, nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo. Wanasayansi wameeleza.
Wanasayansi wa kimataifa wanasema ongezeko la watu, vitendo vya kukutana kimwili na shughuli za usafirishaji kwa njia ya reli zilifanya virusi vya ukimwi kuenea.
Ripoti inasema kuwa biashara ya ngono, ongezeko kubwa la watu na vitu vyenye ncha kali kama sindano kwenye zahanati huenda kulichangia kusambaa kwa ugonjwa huo DRC.
Wakati huo huo reli ilikuwa ina watu takriban milioni moja waliokuwa wakiingia na kutoka kwa wingi jijini Kinshasa kwa mwaka, wakisambaza virusi kwenda kwenye miji mingine.
Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.
Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.
Inaarifiwa virusi vya HIV ni sawa na virusi vya Sinium vinavyopatikana katika Sokwe Ukimwi ulitambulika kuwajanga kimataifa mwaka 1980 na uliathiri takriban watu milioni 75.
Ugonjwa huu una historia ndefu barani Afrika , lakini ulipotokea ugonjwa huu bado ni mjadala mrefu.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Oxford nachuo cha Leuven, nchini ubelgiji walitafiti chanzo cha ugonjwa wa ukimwi wakisema kuwa ulianzia kwa Sokwe.
Virusi vya HIV ni sawa na virusi vinavyopatikana kwa Sokwe ambavyo vinajulilkana kama Simian ambavyo vinadhaniwa vilitoka kwa Sokwe na kuambukizwa binadamu kupitia kwa damu wakati wakitafuta nyama ya wanyamapori.
Virusi hivyo vilikuwa na muundo tofauti na muundo huo ulikuwa unabadilika kila wakati. Virusi vya kwanza viliwaathiri maelfu ya watu nchini Cameroon.
Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.
Idadi kubwa ya wanaume waliokuwa wanafanya kazi mijini na idadi ya wanaume ndio ilikuwa kubwa kuliko wanawake na hivyo biashara ya ngono ikawa kubwa sana.
Mmoja wa watafiti Profesa Pybus anasema kuwa mambo mawili yanesaidia kupunguza maambukizi.
Kwanza hamasisho la serikali kuwatibu wagonjwa kwa maradhi tegemezi.
Jambo la pili ingekuwa mfumo wa usafiri ambao uliwawezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine huku ugonjwa ukienezwa zaidi.
Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.
Virusi vielendelera kuenezwa kwa nchi jirani ya Brazzaville na mkoa wenye madini wa Katanga ambao ulikuwa kitovu cha ugonjwa huo.
Virusi havikukomea tu nchini Congo bali vilianza kuenezwa kote duniani.
ASKARI WA JWTZ APIGWA RISASI NA POLISI
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Kamishna Msaidizi Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jana kwa njia ya simu.
Mambosasa alisema pamoja na private Nassoro, pia askari mwingine wa JWTZ MP 104464 Private Aloyce Engbert alipata majeraha puani na raia mwingine ambaye alikuwa anashuhudia tukio hilo alijeruhiwa.
Kamanda huyo alisema tukio hilo lilitokea baada ya askari huyo wa JWTZ kukiuka sheria na taratibu za barabara ambapo alisimamishwa kwa kosa la kutovaa 'helmet' jambo ambalo liliibua mtafaruku baina yao.
Alisema baada ya askari wa usalama kusimamia sheria askari wa Jeshi la Wananchi aliwasiliana na wenzake hivyo kusababisha mapigano ya ngumi baina ya askari Polisi na wa JWTZ ndipo mmoja wao akapigwa risasi katika kuleta amani.
Kamishna Msaidizi alisema baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi liliwashilikia askari hao ambao walipatiwa matibabu na baadae kupelekwa kwenye mamlaka zinazowahusu.
Mambosasa alisema Kamati yaUlinzi imekutana na kuhakikisha kuwa vyombo hivyo vinakuwa na umoja ili kuondoa tafsiri potofu kwa jamii.
Chanzo: Jambo Leo
VIJANA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KULAWITI WANAFUNZI
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba Mosi, mwaka huu katika Kijiji cha Longuo B, Tarafa ya Moshi Magharibi wilayani Moshi.
Moita alisema wanafunzi waliolawitiwa mmoja wa miaka 10 na wengine wana miaka kati ya 12 na 13. Aliwataja vijana waliofanya kitendo hicho ni Musa Selemani (13) na Daudi Raphael (15).
Alisema chanzo cha tukio ni wakati watoto hao walipokuwa wakielekea shuleni, walipofika njiani watuhumiwa waliwaita pembeni ya kichaka watoto hao, na kuwafanyia kitendo hicho cha kinyama kwa nguvu.
Kutokana na kitendo hicho, wanafunzi hao walipelekwa Hospitali ya Rufaa KCMC kwa matibabu zaidi na wanaendelea vizuri, huku watuhumiwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi na uchunguzi zaidi unaendelea.
KIJANA AACHA SHULE KWA KUNOGEWA NA PENZI LA NGURUWE
Amelalamika akidai kuwa kijana huyo amenogewa `penzi' la mnyama huyo maarufu hapa kama"kitimoto au noah", kiasi cha kumfanya aache masomo na kuwa mtoro sugu shuleni.
Nguruwe huyo jike, inadaiwa anafugwa na familia ya mwanafunzi huyo anayesoma katika shule moja ya umma ya sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga.
Hayo yalithibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii mkoani Rukwa, Sixmund Kibassa aliyemweleza mwandishi wa habari hizi jana kuwa mama mzazi wa mtoto, ameripoti tukio hilo katika jeshi polisi.
Kibassa alisifu uamuzi huo, akisema ni mafanikio makubwa yanayotokana na Mpango Shirikishi wa Kitengo hicho wa kuwarejesha shuleni watoto, ambao ni watoro sugu.
Alisema mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) ni miongoni mwa watoro sugu 70 kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga, waliorejeshwa hivi karibuni kupitia mpango huo shirikishi wa kuwarejesha watoro shuleni, unaotekelezwa na Kitengo cha Polisi Jamii mkoani humo.
Kibassa alisema wazazi na walezi wenyewe wanafika katika kitengo hicho cha polisi jamii na kuripoti kuhusu watoto wao ambao wamekatiza masomo.
Alisema wazazi na walezi hao, wanafichua kwamba watoto wao hao licha ya kutokwenda shuleni, pia nyumbani hawaonekani na kwamba baadhi yao wamebainika kutumia muda wao mwingi kunywa pombe vilabuni badala ya kusoma.
"Ni juzi tu mama mmoja alinifuata na kuripoti kisa cha mwanawe wa kiume anayesoma Kidato cha Pili katika shule moja ya sekondari, kwamba licha ya kuwa mtoro sugu shuleni, lakini pia amekuwa na tabia chafu ya kufanya mapenzi na nguruwe wao jike mara kwa mara…Nilipomhoji kijana huyo alikiri kufanya hivyo …basi tulimsihi,"alieleza.
Kwa mujibu wa Kibassa, baada ya kumsihi mwanafunzi huyo, alikubali kuendelea na masomo, ambapo alirejeshwa shuleni kwakena kupokewa na walimu na wanafunzi wenzake kwa furaha.
Akizungumzia tukio hilo, Daktari wa Tiba ya Binadamu, Dk Paulo Maiga alisema mwanadamu kufanya mapenzi na mnyama, kunamadhara makubwa, ikiwemo kuambukizwa virusi ambavyo vikiingia katika mwiliwa binadamu,kuna uwezekano mkubwa visiweze kutibiwa.
"Hili ni tatizo kubwa, madhara yake ni makubwa, huyu nguruwe anaweza kuwa ameshambuliwa na virusi vya ugonjwa ambao ukiingia na kumshambulia mwanafunzi huyo, upo uwezekanao mkubwa kusiwepo na tiba," alisisitiza Dk Maiga.
Chanzo: Habari Leo
'SIJAFA' ADAI KIONGOZI WA BOKO HARAM
Katika kanda hiyo,Abubakar Shekau anasema kuwa wapiganaji wake waliitungua ndege ya wanajeshi wa angani iliotoweka wiki tatu zilizopita.
Wiki iliopita jeshi lilidai kuwa mtu anayejionyesha katika kanda ya video ya Boko Haram aliuawa na mwezi Agosti 2013 likadai kwamba huenda Shekue amefariki.
Wachanganuzi wametilia shaka kuhusu uthabiti wa madai hayo ya jeshi.
Wapiganaji wa Boko Haram Mwandishi wa Nigeria Ahmad Salkida ,ambaye ana mawasiliano mazuri na Boko Haram alisema kuwa katika mtandao wake wa Twitter wiki iliopita ana hakika kwamba Shekue yu buheriwa afya na kwamba hajafariki.
Haijabainika ni lini ama wapi kanda hiyo iliopatikana na shirika la habari la AFP ilitengezwa.
Lakini muhariri wa Idhaa ya BBC ya Hausa, Mansur Liman ,amesema kuwa mtu aliyezungumza katika kanda hiyo ya video alikuwa Abubakr Shekue yule yule anayeonekana katika kanda nyengine za video za kundi la Boko Haram.
ARSENE WENGER AMSIFIA WELBECK
Welbeck sasa amefunga mabao manne katika mechi tatu na Kocha Wenger amesema kuwa alidhani mchezaji huyo ana kasi lakini sasa amebaini kwamba ana kasi ya umeme.
Amesema kuwa ana matumaini kwamba mabao hayo matatu yatampa motisha zaidi.
Danny Welbeck sasa ni mchezaji wa sita nchini Uingereza kufunga mabao matatu katika mechi moja ya kombe la kilabu bingwa barani Ulaya.
Welbeck alicheza kama mshambuliaji mkuu dhidi ya Galatasaray ,huku Alex Sanchez,Mesut Ozil na Alex Oxlade-Chamaberlain wakiwa nyuma yake.
Wanne hao walishirikiana vyema,huku Welbeck akionekana kufanya mashambulizi makali baada ya kupata pasi murua kutoka kwa Sanchez na Oxlade Chamberlain.
BUNGE LAPITISHA KATIBA ITAKAYOPIGIWA KURA NA WANANCHI
Ili katiba hiyo iliyopendekezwa ipite ilitakiwa kuungwa mkono na kura za ndio theluthi mbili kutoka Tanzania bara na theluthi mbili za ndio kutoka Zanzibar.
Jumla ya wajumbe wote wa bunge hilo la Katiba ni 629, huku 419 wakitoka Tanzania bara na 210 kutoka Zanzibar.
Zoezi hilo la upigaji kura ambalo lilianza Septemba 29 mpaka Oktoba 2, siku matokeo yalipotangazwa, lilisusiwa na wabunge wengi wa upinzani, kwa madai kuwa baadhi ya vipengele vya awali vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa mwananchi, vilikuwa vimeondolewa.
Kabla ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, bunge hilo maalum la katiba lilikaa kama kamati kujadili mapendekezo katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.
Baada ya kamati hizo za bunge hilo kutoa mapendekezo yao, kamati ya uandishi ilikuwa na jukumu la kuandika upya Ibara za Sura za Rasimu ya Katiba zilizojadiliwa na Bunge Maalum na hatimaye kutoa taarifa kwa Mwenyekiti baada ya kukamilisha kazi hiyo.
Hivyo, Kamati ya Uandishi ilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko katika Rasimu ya Katiba yanakidhi matakwa na masharti ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014.
Hatma ya katiba hiyo itahitimishwa kwa kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa na wananchi
RAIS KENYATTA ATAKIWA THE HAGUE
Majaji hao wamekatalia mbali ombi la mawakili wa rais Uhuru Kenyatta la kutaka aruhusiwe kuhudhuria kikao hicho kupitia kwa njia ya Video ama kikao hicho cha ana kwa ana kiahirishwe hadi siku nyingine kwani alikuwa amekabwa na kazi na majukumu kama rais wa Kenya.
Majaji hao wanasema kuwa Rais Uhuru Kenyatta hakutoa sababu madhubuti ya kukosa kuhudhuria kikao hicho maalum.
Majaji hao aidha wanasema kuwa Bwana Kenyatta lazima awe hapo ilikujibu maswali muhumi kuhusu ushirikiano wa serikali yake na kujadili maswala muhimu yatakayo jadiliwa katika kikao hicho.
Kenyatta alikuwa ameiamboa mahakama kuwa ameratibiwa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha uhuru wa Uganda.
Kauli hiyo inawadia wakati ambapo mwendesha mashataka wa mahakama hiyo Fatou Bensouda alikuwa amepinga ombi la rais Kenyatta la kuahirisha kikao hicho ama kuruhusiwa kushiriki kikao hicho kwa njia ya video.
Bi Bensouda alikuwa ameilalamikia mahakama hiyo akidai kukosa ushahidi wa kutosha baada ya serikali ya Bw Kenyatta kumnyima stakabadhi alizotaka ilikuimarisha kesi dhidi ya kiongozi huyo wa Kenya.
Bw Kenyatta kwa upande wake naye alikuwa amewasilisha ombi mahakamani ya kutaka kesi dhidi yake itupiliwe mbali baada ya bi Bensouda kukiri kuwa hakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yake.
EBOLA YATUA MAREKANI
Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.
Mgonjwa huyo anasemekana kuwa ni mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia kabla ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 3,000 tayari wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi na idadi ndogo ya wafanyakazi wa Marekani wa mashirika ya misaada wamepata nafuu baada ya kupelekwa kutibiwa Marekani.
Jumatatu, maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.
Nchini Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19 waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watuwa nane wamekufa tangu mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai..
Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.
Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.











