MWANAE JACKIE CHAN AKAMATWA NA BANGI

Mwanawe muigazaji nyota wa Hollywood Jackie Chan amekamatwa kwa madai alitumia mihadarati.

Jaycee Chan, 31, ambaye mwenyewe ni msanii pamoja na muigizaji kutoka Taiwanese Kai Ko, 23, walikamatwa alhamisi iliyopita kwa mujibu wa taarifa ya polisi mjini Beijing.

Polisi wanasema kuwa wawilihao walipatikana wamevuta bhangi huku mwanawe Chan akikabiliwa na kosa zaidi la kupatikana na dawa hiyo haramu.

Kukamatwa kwa wawili hao kunawadia wakati polisi wamekuwa wakifanya misako ya dharura na kuwakamata wasanii nyota kadhaa.

Gao Hu, 40, aliyeigiza katika filamu ya mwaka wa 2011 Zhang Yimou "The Flowers of War", alikuwa miongoni mwa wasanii wengine wakutajika waliokamatwa mapema mwezi huu.

HU alipatikana ametumia Bhangi pamoja na madawa aina ya methamphetamines.

Operesheni hizi zinafuatia agizo la rais wa China Xi Jinping mwezi juni kwa polisi la kuwataka kuimarisha juhudi za kukabiliana na matumizi ya mihadarati nchini humo.

Duru zinaarifu kuwa Kukamatwa kwa mwanawe msanii maarufu zaidi nchini humo maafisa wa polisi wanajaribu kuwadhibitishia umma kuwa hakuna atakayeepuka mtego wao.

Mwandishi wa BBC mjini Beijing Martin Patience anasema kuwa watu wenye sifa kubwa wanalengwa na maafisa wa polisi kutokana na ushawishi mkubwa walionao miongoni mwa jamii nchini humo.

Hata hivyo kiongozi wa idara ya baraza la umma la Beijing inayopambana na matumizi ya mihadarati bwana Jin Zhihai amekanusha kuwa idara yake imekuwa ikilenga wasanii na waigizaji nyota katika kampeini yao dhidi ya matumizi ya mihadarati.

"ikiwa tutaendelea na kampeini hii dhidi ya matumizi ya mihadarati ninahakika waigizaji wengi nyota watakamatwa ''Juma lililopita miungano 42 inayowakilisha wasanii walitia sahihi maagano ya kukataa kuwasajili wasanii waotumia mihadarati katika maonesho yao.

Kampuni inayomwakilisha bwana Chan iliomba msamaha kwa uma kwa niaba yake.

Kampuni hiyo ya M'Stones International iliahidi kumpeleka hospitalini ilikukomesha matumizi ya dawa hizo.

Babake Jackie Chan hajasema lolote kufikia sasa.

JAJI MAKAME AFARIKI DUNIA

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Lewis Makame, amefariki dunia katika Hospitali ya Ami Trauma Centre iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Jaji Makame alifariki jana mchana katika hospitali hiyo, alikokuwa amelazwa ambapo pia Rais Jakaya Kikwete, alimtembelea kumjulia hali. Taratibu za mazishi zilikuwa zikiendelea jana nyumbani kwake Masaki.

Historia fupi iliyopatikana, inaonesha kuwa Jaji Makame alikuwa na Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza, ambapo baada ya kufanya mazoezi na kufanya kazi nchini humo, alirejea nchini Tanzania miaka ya 1960 na kutumikia Taifa mpaka alipofikia cheo cha Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

Mbali na cheo hicho, Jaji Makame pia alitumikia Taifa katika nafasi yaMwenyekiti wa NEC na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-ECF).

Wakati akiwa Mwenyekiti wa NEC kwa takribani miaka 19, Jaji Makame aliweka historia ya kusimamia uchaguzi kadhaa wa vyama vingi nchini.

Alistaafu wadhifa huo baada ya mkataba wake kuisha Julai mwaka 2011. Nafasi yake ilichukuliwa na Jaji mstaafu Damian Lubuva.

MAANDAMANO YA ALBINO YASAMBARATISHWA

MAANDAMANO ya walemavu wa ngozi kwenda Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar es Salaam jana, yalisambaratishwa kwa mabomu yamachozi na askari Polisi, baada ya waandamanaji hao kuzingira kituo hicho na kukaidi amri ya kutawanyika.

Waandamanaji hao walitokea Mahakama ya Mwanzo Buguruni kwenda katika kituo hicho, kulalamikia uamuzi wa Mahakama hiyo kutoa dhamana kwa mshitakiwa, Ombeni Swai, mkazi wa Tabata Matumbi, anayedaiwa kutishia kumuua mwenzao.

Kabla ya maandamano hayo, Swai alifikishwa mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mfawidhi, Benjamini Mwakasona na kushitakiwa kwa kosa la kutishia kumuua mlemavu wa ngozi, Mwinyisi Issa.

Karani wa mahakama hiyo, Edwin Mwandawanda alidai mahakamani hapo kwamba Swai alitishia kwa maneno kumuua Issa Agosti 16 mwaka huu, saa 7 mchana katika eneo la Buguruni Wilaya ya Ilala.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo ambapo Hakimu Mwakasona aliahirisha kesihiyo mpaka Septemba 3, mwaka huu na kumwambia mshitakiwa kuwa dhamana ya kesi yake ipo wazi, ambapo alitakiwa kuwa wadhamini wawili waliotakiwa wote kuwa na barua zinazotambulika na serikali za mtaa.

Pamoja na dhamana hiyo kuwa wazi, mshitakiwa hakufanikiwa kutimiza masharti hayo kwa wakati, hivyo akaendelea kushikiliwa wakati akisubiri wadhamini wake kutekeleza masharti hayo.

Vurugu

Kitendo hicho cha mahakama kutangaza dhamana kwa mshitakiwa, kiliamsha hasira kwa walemavu wa ngozi waliokuwa wamekusanyika nje ya mahakama kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, iliyotajwa kwa mara ya kwanza.

Baadhi ya walemavu hao walifanikiwa kupenya mpaka alipokuwepo mshitakiwa na kuanzakumpiga. Kitendo hicho kilifanya Polisi kumpakia haraka kwenye gari na kumpeleka kituoni Buguruni, kwa nia ya kumnusuru.

Hatua hiyo haikuwaridhisha albino hao, ambao walijikusanya na kuandamana kwenda katika Kituo cha Polisi Buguruni, kwa lengo la kutaka kumdhuru mshitakiwa.

Mashuhuda waliozungumza na gazeti hili, walidai kuwa waandamanaji hao walipotakiwa kutawanyika, walikaidi, hatua iliyosababisha Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Walisema baadhi ya albino walidiriki kupanda ndani ya gari la polisi aina ya Land Rover 'Defender' na kuanza kumshambulia kwa mateke na ngumi mshitakiwa, jambo lililowalazimu polisi kuondoka eneo hilo hadi kituo cha polisi Buguruni.

Albino hao pia walifuata kwa nyuma huku wengine walipanda ndani ya gari hilo hadi mahali hapo. Wananchi waliokuwepo nje ya kituo cha polisi, walikumbwa kwa taharuki.

Albino hao waliendelea kumshambulia mshitakiwa huyo hadi walipofika nje ya kituo hicho, huku wakizuiliwa na polisi hao, ambao baadae walilazimika kufyatua mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya.

Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marry Nzuki, ambaye alikiri kutokea kwa vuruguhizo. Alisisitiza kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa Polisi kwa kosa hilo.

"Baada ya kutawanywa pale kituo cha Buguruni, Mkuu wa Kituo aliwaambia waje katika ofisi zangu,lakini hadi hivi sasa sijamuona mtuyeyote wala kiongozi wao kuleta mashitaka yoyote," alisema Kamanda Nzuki.

Dau la Mengi

Wakati vurugu hizo zikitokea, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ametangaza kutoa Sh milioni 10 kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa watu walioshiriki kumkata mkono mlemavu wa ngozi, Susan Mungi (35) na kumuua mumewe wilayani Igunga, Tabora.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mengi alisema pia IPP itasomesha watotowa mlemavu huyo.

Katika mkutano huo uliohudhuriwapia na baadhi ya viongozi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Mengi alisema anafanya hivyo kama mwananchi wa kawaida ambaye ameguswa na vitendo hivyo vya kinyama, vinavyofanywa dhidi ya watu hao wenye ulemavu.

Aliomba Polisi kuwasaka wote waliohusika, kuwakamata na kuwapeleka mahakamani haraka.

Alisema albino ni watu kama wengine hivyo vitendo vyovyote vya kinyama dhidi yao lazima vilaaniwe na watu wote.

"Hakuna albino ambaye amependa awe hivyo, hakuna aliyemwomba Mungu ampatie ulemavu huo, hawa ni binadamu kama sisi, jamii na serikali kuendelea kukaa kimya juu ya unyama huu ni jambo linalosikitisha," alisema Mengi.

Mengi alisema waliotumwa kumkata albino huyo wakamatwe. Susan, mkazi wa Kijiji cha Buhelelekati ya Nsimbo wilayani Igunga, alikatwa kiwiko cha mkono wake nawahusika kutoweka nacho.

Katika tukio hilo, mumewe Mapambo Mashili aliuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kifuani na kichwani wakati akijaribu kumnusuru mkewe asikatwe mkono wake.

Mtoto huyo hadi sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo.

Katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa ametangaza dau la Sh 500, 000 kwa mwananchi atakayesaidia kukamatwa kwa watu wanaofanya vitendo hivyo.

Tukio hilo limekuwepo ikiwa ni wiki baada ya mtoto, Upendo Sengerema (15) mkazi wa Kijiji cha Usinge kata ya Uganza wilayani Kaliua mkoani Tabora, kukatwa mkono na watu waliokimbia nao.

Katibu Mkuu Chama cha Albino (TAS), Ziada Nsemo alisema kati yawatanzania milioni 45, Mengi ni mmoja wa watu waliojitokeza hadharani kukemea vitendo vya kinyama wanavyofanyiwa.

Alisema licha ya polisi kuahidi kuwalinda, wameendelea kuuawa.

Alitoa mwito kwa albino nchini, kujilinda na kukaa karibu na makundi ya watu ili wanapovamiwa iwe rahisi kupata msaada kwa sababu ulinzi kwao ni wa shaka na wanawindwa kila kona.

Chanzo: Habari leo

WATU WAWILI WAFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Land Cruser ilikuwa imebeba maiti 10 zikitokea hosiptali ya taifa muhimbili kwenda hospitali ya St Francis Ifakara kugonga wapanda pikipiki katika eneo la Mtego wa simba Mikese mkoani Morogoro.

Akizungumzia tukio hilo kwenye eneo la tukio mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Bonifasi Mbao amesema gari hiyo ikiendeshwana dereva Pankrasi Pasco mkazi wa ifakara iliwagonga wapanda pikipiki Shaban Rajab na Ally Benulo wakazi wa Mikese na kufariki dunia papo hapo na chanzo cha ajali mwendo kasi na dereva anashikiliwa na jeshi la polisi, kuhusu maiti 10 zilizokuwemo katika gari hiyo amesema zilikuwa zikipelekwa hospitli ya St Fancis Ifakar kwa lengo la kufanya utafiti na mafunzo ambapo wanafanya mawasilino ya kuzifikisha katika hospitali hiyo.

Nao wananchi walioshuhudia tukio hilo wameeleleza chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi huku wakilalamikia matukio ya ajali nyingi katika eneo hilo kutokana na kona na kuomba serikali kuweka matuta na vibao vya tahadhari.

AJIUNGUZA MWILI MZIMA KWA WIVU WA MAPENZI

MKAZI wa Igombe katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, jijini hapa, Tausi Juma (22)amelazwa katika Hospitali ya Rufaaya Bugando baada ya kujimwagia mafuta ya taa na kujiunguza mwili mzima kutokana na wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo ni la Agosti 9, mwaka huu saa 2 asubuhi nyumbani kwake.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime alipoulizwa, alisema ofisi yake haijapata taarifa juu ya tukio hilo.

Muuguzi wa zamu katika wadi hiyo, Pendo Muleta akizungumzia hali yamgonjwa huyo alisema si nzuri, kwani ameungua asilimia 60 ya mwili wake.

Alisema mpaka sasa wanaendelea kumpatia matibabu ikiwemo dawa za kupunguza maumivu na zinazozuia maambukizo kutokana na vidonda alivyo navyo.

Mwanamke huyo akizungumza kwatabu hospitalini hapo, alielezea kisa kwa kusema amefikia hatua hiyo baada ya kugundua mumewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine.

Alidai mwanamke huyo alituma ujumbe kwenye simu ya mkononi ya mumewe na akauona.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika hospitalini hapo jana, Tausi alisema aliona hana umuhimu wa kuendelea kuishi na mtu ambaye anampenda kwa dhati, lakini anakuwa na mwanamke mwingine.

Akielezea alivyojiunguza, Tausi alisema wakiwa nyumbani kwao namumewe aliyemtaja Hussein Yadunia ambaye ni polisi katika Kituo cha Polisi Igombe, wilayani Ilemela, jijini Mwanza, ujumbe wa maneno uliingia katika simu ya mume wake huyo.

Alisema hakumbuki maneno yote yaliyokuwemo kwenye ujumbe, lakini baadhi yalisomeka 'nakupenda sana honey wewe ndio chaguo la moyo wangu.'

Mwanamke huyo alisema alipomhoji mumewe ambaye pia hujishughulisha na uvuvi wa samaki, juu ya ujumbe huo, alidai kutofahamu namba iliyotuma.

"Nilipomuuliza alikataa kuwa mtu huyo hamjui na aliniambia nimpigie simu…na mie nilipopiga simu hiyo ilipokewa na mwanamke kwa hasira nilimuuliza tena mume wangu ambaye alikataa tena kwa kuniambia hamjui," alisema Tausi.

Huku akionekana kuwa na maumivu makali kutokana na sehemu kubwa ya mwili wake kuwa na majeraha ya kuungua, Tausi alisema ghafla mumewe alimbadilikia na kuanza kumgombeza kuwa amechoka na maswali yake na kumfuatilia kila siku maisha yake hivyo afungashe mizigo yake aende kwao.

"Baada ya maneno hayo, nilimuonamume wangu akiingia ndani na kuanza kunifungashia mizigo, akipakia nguo zangu kwenye mabegi nirudi kwetu na alifanya hivyo baada ya kumjua mwanamkealiyemtumia ujumbe wa maneno katika simu yake,"alisema.

Tausi ambaye aliwaambia waandishi wa habari kuwa mumewe ndiye anayemhudumia hospitalini hapo, aliendelea kusimulia, "nilimwambia mume wangu kuliko kuondoka wakati bado nakupenda bora nijiue."

Alisema moto mkubwa uliokuwa ukiwaka ulimshitua mumewe ambaye alimkimbilia na kumwagia mchanga na baada ya moto kuzimika alimvua nguo na kumkimbiza katika Kituo cha Afya cha Karume.

Kutokana na majeraha kuwa makubwa, iliamuliwa akimbizwe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure ambayo pia ilimpa rufaa kwenda Bugando.

Hussein Yadunia ambaye ni mume wa mke huyo, akizungumzia tukio hilo alisema, " Sina usemi.

Tayari tukio limetokea, yote namkabidhi Mungu lakini tukio hilolimenidhihirishia kuwa mke wanguananipenda."Aliendelea kusema, "hata vyombo vikiwa kabatini huwa vinagongana lakini uamuzi aliofanya mke wangu umenishangaza."

Akizungumzia ujumbe wa simu uliosababisha mtafaruku, alisema ulitoka kwa dadake na walikuwa wakitakiana heri.

"Haikuwa meseji ya mapenzi," alisema na kusisitiza akipona ataendelea kuishi naye na atazidi kumpenda.

Chanzo: Habari leo

HAKUNA MGONJWA WA EBOLA TANZANIA

Tanzania imesema haina mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.

Kauli hiyo inakuja baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.

Waziri wa Afya wa Tanzania Seif Rashid ameiambia BBC, wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizo kutokana na dalili za awali, ni wa kutoka Benin na Mtanzania, lakini vipimo vimeonesha hawana maambukizo hayo.

Amesema tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.

Mafunzo yametolewa pia kwa wataalamu watakao hudumia wagonjwa iwapo watatokea.

Vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa, vimewekwa pia.

Wizara ya Afya ya Tanzania inaongeza uwezo wa kufanya uchunguzi, katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.

NEC YATAJA MASHARTI YA DAFTARI LA WAPIGA KURA

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linalotarajiwa kuanza hivi karibuni linamhusu kila raia mwenye sifa yakupiga kura.

Ufafanuzi huo ulitolewa wakati kukiwa na mawazo tofauti ya nani hasa anatakiwa kushiriki katika zoezi hilo huku baadhi ya watu wakidhani kuwa jambo hili linawahusu ambao hawakuwahi kujiandikisha kupiga kura ama waliopoteza kadi na waliofikia umri wa kupiga kura.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema juzi jijini Dar es Salaam kuwa katika kufanya maboresho hayo na kupata daftari linaloaminika zaidi, Tume inatarajia kutumia mfumo mpya wa utambuzi wa watu kwa alama zabinadamu yaani "Biometric Voters Registration System".

Alisema kwa kutumia mfumo huu, mhusika atachukuliwa alama za vidole vyote 10 vya mikono, picha,saini yake na ni tofauti na mfumo uliokuwa unatumika wa "Optical Mark Recognition" (OMR) uliohitaji kujaza fomu na alama ya kidole kimoja tu.

"Watu wote wenye sifa watatakiwa kujiandikisha upya katika mfumo huu mpya na kupatiwa kadi mpya,"alisema na kuongeza kuwa uboreshaji wa daftari hilo unatokana na matakwa ya kisheria na malalamiko ya wadau mbalimbali.

Alisema tangu uchaguzi mkuu mwaka 2010 pamekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau kama vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na wapiga kura kuhusu haja ya kuboresha daftari hilo.

Sheria inataka liboreshwe mara mbili kati ya uchaguzi uliofanyika na ujao.

Akizungumzia matayarisho ya zoezi hilo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Mallaba alisema yanaridhisha na kuendelea vizuri.

"Sehemu kubwa ya maandalizi yamekamilika," alisema na kuongeza kuwa tayari ununuzi wa vifaa vya uandikishaji ikiwamo Biometric Voter Registration Kits umeshafanyika.

Alisema vituo katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa vimeongezeka kutoka vya awali 24,919 na kufikia vituo 40,015 nchinzima.

KAMATI ZASHAURI RAIS KUPUNGUZIWA MADARAKA

PAMOJA na Rasimu ya Katiba mpya ya Jaji Joseph Warioba kupunguza madaraka ya Rais, kamati zilizotoa taarifa ya mwenendo wake jana zimependekeza madaraka zaidi kupunguzwa.

Katika majadiliano kwenye kamati namba 10, 11 na 12, aidha imependekezwa watakaobaki kuwa wateule wa Rais ni lazima wapelekwe kuthibitishwa na Bunge au mamlaka nyingine.

Mwenyekiti wa kamati namba 12, Paul Kimiti, alisema wajumbe wengi wamejikita katika upunguzajizaidi wa madaraka ya Rais hasa katika mamlaka ya uteuzi.

Kwa kuangalia mwenendo wa majadiliano katika kamati hadi jana, inaonekana kwamba kasi ya kuchambua Rasimu ya Katiba ipo kiwango cha juu na kila Mwenyekiti aliyezungumza kuhusu akidi alisifia kutimia kwake.

Kimiti alisema wapo katika sura ya saba na wanaendelea na majadiliano na japokuwa vipengelevingi vimeshazungumzwa, wajumbe wengi wamejikita katika upunguzaji zaidi wa madaraka ya Rais.

Katika kikao hicho mjumbe wa kamati hiyo ambaye alikuwa mgonjwa kutokana na kipigo, Thomas Mgoli alisema aliomba kupiga kura kwa sababu alishiriki katika kujadili sura hizo na ilikuwa haki yake.

Alisema uamuzi huo ni tofauti na ilivyotafsiriwa kwamba ulitokana na kukosekana kwa akidi. Wakati huo huo, kamati nyingi zinaendelea kuzungumzia uraia pacha huku wakiwemo wanaopinga suala hilo.

Makamu Mwenyekiti wa kamati namba 10, Salmin Awadh Salmin alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba wameshaanza kupiga kura kwa kamati 2,3 na 4 huku wakiendelea na majadiliano katika sura namba 5.

Hata hivyo alisema jana waliacha majadiliano ya sura hiyo na kuingia sura namba saba ambapo wao watawasilisha maoni ya walio wengi na wachache kutokana na jinsi mambo yalivyojiri katika majadiliano.

Alisema katika kamati yake kulikuwa na mijadala mirefu hasa kwenye mazingira yanayosababisha haki, kiasi cha kuamini kwamba kuna hitajika sura nyingine.

Alisema sura hiyo itajikita zaidi katika haki za wakulima, wavuvi na wafugaji; pia haki za kimakundi kama wanawake.
"Tutapendekeza sura nyingine ili kila mtu apate haki zake..." alisema Salmin.

Aidha alisema katika kamati yake Sura ya 7 imekuwa na mvutano mkubwa na kulazimika kuweka viporo ibara 72 na 73 zinazojadili mamlaka.

ATUHUMIWA KUMLAWITI MTOTO WA MKEWE

MKAZI wa eneo la Majengo mjini Manyoni, Juma Saidi (32) anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumlawiti mtoto wa mkewe. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 14, anasoma Kidato cha Kwanza katika shule moja ya sekondari wilayani Manyoni na inadaiwa alifanyiwa kitendo hicho juzi saa 6 usiku nyumbani kwao.

Inadaiwa baba huyo wa kambo wa mtoto huyo ambaye jina na shule anakosoma vimehifadhiwa, alifanya kitendo hicho baada ya mkewe kusafiri.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alidai mwanamume huyo alimlawiti kwa nguvu kijana huyo na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani hapa inashikilia watu wengine watatu kwa tuhuma ya mauaji.

Kamanda alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Mlani Janila (55), Nchinja Ngaja (69) na Jagali Nchinja (37); wote wakazi wa Kijiji cha Mtavira wilayani Ikungi, mkoani hapa.

Wanadaiwa Agosti 9 mwaka huu saa1.00 jioni katika kitongoji cha Muguaghana, kijiji cha Mtavira, walimuua mwanakijiji mwenzao, Kwisu Funuki (30).

Inadaiwa siku ya tukio, Kwisu alionekana akinywa pombe ya kienyeji nyumbani kwa mtuhumiwa wa kwanza Mlani Janila.

Wakati akiendelea kunywa pombe, inadaiwa ulizuka ugomvi kati ya Funuki (marehemu) na Nchinja (mtuhumiwa) ambao uliamuliwa.

Hata hivyo, baada ya muda, Funuki aliokotwa na wasamaria wema akiwa amekufa karibu na nyumbani kwake huku pembeni kwake kukiwana kopo la kunywea pombe ya kienyeji ijulikanayo kwa jina la "mtukuru".

Uchunguzi wa awali kwa mujibu wa kamanda, unaonesha alichomwa kifuani na kitu chenye ncha kali. Hivyo watu watatu aliokuwa akinywa nao pombe wanashikiliwa kwa uchunguzi.

Chanzo: Habari Leo

BARAZA LA KIISLAMU WAMUUNGA MWIGULU MKONO

Baraza la Maadili la Kiislamu nchini (BAMAKITA), limeunga mkono kauli iliyotolewa na Mbunge wa Iramba Magharibi, mkoani Singida, Bw. Mwingulu Nchemba kutaka vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, viahirishwe ili kuokoa fedha za walipakodi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa baraza hilo, Shekhe Athuman Mkambaku, alisema kauli ya Bw. Nchemba inaonesha ni mzalendo halisi anayelipenda Taifa lake.

Alisema hivi karibuni, Bw. Nchemba alishauri Bunge hilo liahirishwe kwani wajumbe waliopo hawawezi kuwapatia Watanzania Katiba Mpya kutokana na theluthi mbili inayotakiwa kwa mujibu wa sheria, haiwezi kupatikana kwa sababu baadhi ya wajumbe kutoka upinzani hawashiriki vikao vya Bunge hilo.

“Kuendelea kuwalipa posho wajumbe wa bunge hili ni matumizi mabaya ya fedha za umma…Nchemba ameonesha ukomavu wa kisiasa na manenoyake hayapaswi kupingwa wala kupuuzwa bali aungwe mkono na kupongezwa,” alisema.

Aliongeza kuwa, baraza hilo linapinga vikali kitendo cha baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kuendelea kususia vikao wakiamini pengine wanatumiwa na kundi la watu wasiotaka Katiba Mpya ipatikane.

“Hoja za UKAWA zilizowafanya wagomee vikao hivyo hazina mashiko kwani wao wanataka rasimu ipite kama ilivyoandaliwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba…kama madai yao ni sahihi, kwa nini waende bungeni kuchukua posho tu?” alihoji.

Alisema lazima wajumbe wa Bunge hilo wabadili baadhi ya vifungu, waongeze na kuviboresha ndio maana ya vikao.

Shekhe Mkambaku wajumbe kutoka umoja huo hawapaswi kugoma kwa hofu kwamba, Katiba Mpya itatengenezwa kulingana na matakwa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na wingi wao bali watambue kuwa, chama hicho si waamuzi wa mwisho kwani mwisho wa siku rasimu hiyo itapelekwa kwa wananchi ambao ndio waamuzi wa mwisho.

“Kama rasimu hii itatoka kinyume na tulivyopendekeza, wananchi wataikataa, hivyo UKAWA wasijipe kazi ambayo siyao…kazi hiyo waiache kwa wananchi waitolee majibu kwa kupiga kura ya kuikataa au kuikubali,” alisema.

Baraza hilo pia limewapinga watu wanaomshambulia Rais wa Jakaya Kikwete wakidai amevuruga mchakato huo kutokana na hotuba yake alipolihutubia Bunge la Katiba kwani alichokisema ni ushauri tu.

“Kama Kiongozi Mkuu wa nchi, bado ana fursa ya kushauri si lazima wajumbe kufuata maoniyake ndio maana baada ya hotuba yake, vikao viliendelea,” alisema Shekhe Mkambaku

WATU WAWILI WAKAMATWA WIZI MAFUTA YA TRANSFORMER

Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro baada ya kupatikana na lita 30 za mafuta ya transfoma baada yakukata nguzo za umeme kuvunja transfoma na kuiba mafuta na kusababisha wakazi wa eneo la kola mjini Morogoro kukosa huduma ya umeme kwa muda mrefu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amethibitisha kukamatwa kwa watu hao ambapo amesema watuhumiwa walikamatwa katika eneo la kola kwa kamnyonge manispaa ya Morogoro wakihujumu miundombinu ya umeme ikiwemo kuiba mafuta ya trasfoma na kukata nguzo za umeme ambapo jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watu hao na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.

Naye afisa uhusiano wa shilika na umeme Tanesco mkoa wa Morogoro Ester Msaki amsema mafuta hayo yana thamini ya zaidi ya shilingi laki tatu ambapo amewataka wananchi kuendelea kuwa na ushirikiano kwa kuwafichua wanaohujumu miundombinu ya umeme kwani shirika linaendelea kupata hasara na kusababisha baadhi ya wananchi kukosa huduma ya umeme.

Kwa upande wao wakazi wa manispaa ya Morogoro wameiomba serikali kuongeza ulinzi na kuwachukilia hatua kali watakaobainika wakihujumu miundombinu ya umeme na kusababisha wananchi kuishi gizani kwakukosa huduma ya umeme.

URAIA PACHA PASUA KICHWA

SUALA la uraia wa nchi mbili, linaonekana kupasua vichwa vya wanakamati hasa wanaotoka Zanzibar, kutokana na historia ya nchi hiyo.

Kutokana na unyeti wa suala hilo imeelezwa na Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahya Khamis Hamad, kuwa Bunge liliruhusu mtaalamu mwakilishi wa watu waishio nje, Kadiri Singo kuwasilishawaraka ambao umejadiliwa na kamati hizo.

Akifafanua zaidi taarifa zilizoenea kwamba kulikuwa na majadiliano makali kwenye ibara inayohusu masuala ya uraia wa nchi mbili, Hamad alisema pamoja na majadiliano hayo raia walioko nje ya nchi walituma waraka maalumu ambao waliomba ujadiliwe.

"Juzi walimtuma mtaalamu wao, Singo alete waraka huo na niliomba kibali kwa mwenyekiti waraka huo uruhusiwe kujadiliwa ndani ya kamati na alipata ruhusa hiyo,'' alisema Katibu.

Alisema hadi juzi mchana kamati tatu zilikuwa zikiendelea kujadili ibara inayohusu uraia pacha na kamati nyingine zimekamilisha kujadili ibara hiyo.

Naye mwenyekiti wa kamati namba 12, Paul Kimiti alisema kamati yakeimekuwa ikijadili suala hilo la uraia pacha kwa kina, lakini kumekuwa namvutano hasa kwa upande wa Zanzibar ambapo baadhi ya wajumbe wamekuwa na hisia tofauti kuhusu uraia pacha kwa upande wao.

Kimiti alisema baadhi ya wajumbe wameonesha hofu kufuatia baadhi ya watu ambao walitoroka nje ya nchi wakati wa mapinduzi ambao wanaona kuruhusu uraia pacha kunaweza kuleta matatizo.

Lakini wajumbe walikubaliana kuwa uraia pacha kwa waliotoroka nje wakati wa mapinduzi unaweza kudhibitiwa katika sheria itakayotungwa.

Kwa maoni yake Kimiti alisema inaonesha kuwa sura zilizokuwa zikileta mgogoro ni zilizohusu muundo wa serikali kwani kwa sasa wamekuwa wakiendelea bila tatizo.

Wakati huo huo, imeelezwa kuwa majadiliano yanayoendelea kuimarika zaidi kutokana na kuzidi kuwasili kwa wabunge walikuwa wamesusia Bunge hilo.

Pamoja na kutojulikana idadi ya waliorejea, Katibu alisema kundi la wajumbe 201 waliosusia wanaendelea kurejea bungeni na kuendelea na majadiliano ya kamatikama kawaida.

ARSENAL WASAKA FURSA TANZANIA

DSC06091


Klabu ya Arsenal iliyopo kaskazini mwa jiji la London imeanza mkakati wa kujikita katika kutafuta ubia na kampuni Tanzania kwa lengo la kujitangaza na kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii.

Katika ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Mheshimiwa Peter Kallaghe aliyoifanya jana katika Uwanja wa Emirates, na kufuatiwa na mazungumzo rasmi na maofisa wa Klabu ya Arsenal, maofisa hao walieleza kutambua umuhimu wa Tanzania katika kukua kwa Arsenal.

Ofisa Miradi ya Jamii, Samir Singh alimweleza balozi baadhi ya takwimu juu ya wapenzi wa Arsenal walioko Tanzania, akisema kuwa mtandao wa www.arsenal.com unasomwa na watu zaidi ya milioni mbili kutoka Tanzania, huku wakirudia kuutembelea zaidi ya mara laki saba; kwenye face book wanafuatwa na watu zaidi ya 120,000.
DSC06097
Arsenal wamekuwa wakitoa msaada na makocha kwa mradi wa Tanzania Street Children ulioko Mwanza kwa karibu miaka minne sasa, ambapo kupitia mradi huu watoto zaidi 1,280 wamenufaika. Arsenal wamesema wangependa kuwa na ushirikiano na kampuni mbalimbali huko nyumbani ili kusaidiana katika kuinua michezo na kutambua vipaji vya wanamichezo.

Naye Ofisa Masoko wa Arsenal, Daniel Willey, alisisitiza umuhimu wa wanachama na wapenzi wa Arsenal kujisajili na kuwa na uongozi imara utakaotambuliwa na klabu na hivyo kutoa fursa mbalimbali kwa umoja huo wa wapenzi wa Arsenal Tanzania.

“Umoja wa wanachama unaotambuliwa kwa hivi sasa ni ule wa Kasulu,  Kigoma,  ambapo kumbukumbu zetu zinaonesha kuna wapenzi 150,000, lakini tuna imani wapo wengi zaidi, tunataka tufanye nao kazi, nitaenda Tanzania hivi karibuni, nitapenda kuonana nao Dar, sitakuwa na nafasi ya kwenda nje ya Dar kwa sasa,” alisema Willey.

Kwa upande wake Balozi Kallaghe, ambaye si mpenzi wa Arsenal, alisema hiyo ni fursa muhimu sana kwa wapenzi na mashabiki wa Arsenal kuchangamkia, na kuwataka kujisajili na kuwa na viongozi wanaotambulika.
Balozi Kallaghe, akiwa pamoja na maafisa wa Arsenal uwanhani Emirates
Balozi Kallaghe, akiwa pamoja na maafisa wa Arsenal uwanjani Emirates

“Unajua kubishana bishana masuala ya mpira bila kuwa na kadi ua uanachama kumepitwa na wakati, inapendeza upotumia pesa kidogo, kwa kuvaa fulana original ya timu yako,” alisema Balozi na kuwawataka wanachama hao kuisaidia klabu yao, kuwaunganisha na kampuni kama benki, viwanda vya bia na kampuni za simu.

Balozi Kallaghe alisema hiyo italeta changamoto itakayopelekea timu ya Arsenal kwenda Tanzania siku moja, ambapo Willey alionesha hamu kubwa sana ya kufanya mazungumzo na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), kuona jinsi gani wanaweza kushirikiana.

“Mna vivutio vikubwa sana vya utalii; Mlima Kilimanjaro, Serengeti, Manyara -  haya ni maeneo ambayo tungependa kuyafanyia mazungumzo.

“Tunafahamu kuwa Rais Kikwete ni mpenzi sana wa michezo, na hasa soka, tunamkaribisha sana, japo hatujui yeye ni shabiki wa timu gani hapa England,” alisema Willey.

Balozi Kallaghe aliwashukuru Arsenal na kuahidi kutoa msaada pale itakapobidi, na kuwataka wasisite kumwona wakati wowote, na aliwashukuru kwa mwaliko kwa Rais Jakaya Kikwete kutembelea Emirates  wakati wowote atakapo kuwa London.

Kazi kwenu sasa, mashabiki wa Arsenal, kutaneni, chaguaneni, mchangamkie fursa.


Source: Tanzania Sports

PADRI WA KIHISPANIA AFARIKI KWA EBOLA

Liberia imetangaza kuwa hivi karibuni itapokea dozi za dawa za majaribio ya kutibu ugonjwa wa Ebola kutoka Marekani, ambazo itazitumia kwa madaktari wawili walioambukizwa virusi hivyo.

Serikali ya Marekani ilithibitisha kuwa iliwaunganisha maafisa wa Liberia na kampuni inayotengeneza dawa hiyo iitwayo ZMapp. Katika taarifa yake, kampuni hiyo ya Mapp Biopharmarceutical yenye makao yake jimboni California, ilisema kuwa katika kujibu maombi kutoka kwa taifa la Afrika magharibi ambalo halikutajwa, ilikuwa imeishiwa na ugavi wa dawa hiyo.

Habari hizo zinakuja huku ghadhabu zikiongezeka kuhusiana na ukweli kwamba watu pekee waliopatiwa dawa hiyo ya majaribio ni kutoka mataifa ya magharibi - Wamarekani wawili na Mhispania ambao wote walirudishwa nyumbani kwao kutoka Liberia.

Idadi ya vifo yaongezeka

Jumatatu jioni, shirika la afya duniani WHO, lilisema watu 1,013 wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola katika mataifa ya Afrika ya Magharibi, huku serikali zikibainishawashukiwa wa ugonjwa huo 1,848. Idadi hiyo ya WHO inahusisha takwimu za kaunzia Agosti 7 hadi 9, ambapo watu 52 zaidi walikufa kutoka na ugonjwa huo, na 69 zaidi waliambukizwa.

Lakini mfanyakazi wa shirika la misaada la Madktari wasio na mipaka MSF nchini Liberia, Cokie Van Der Velde anasema hali ni mbaya kuliko inavyodhaniwa.

"Kiukweli idadi ya waliokufa na walioathirika haionyeshi hali halisi," alisema Van Der velde na kuongeza kuwa kuna vifo vijijini na nchini kote ambavyo havirekodiwi kwa sababu ukusanyajiwa data siyo mzuri kama unavyopasa kuwa.

"Nadhani nchini Liberia ugonjwa huo uko katika kaunti sita na unazidikusambaa. Na unaweza kuenea katika kanda nzima ya Afrika Magharibi, hivyo ni hali ngumu."

Bado hakuna tiba ya uhakikaHakuna chanjo wala tiba ya Ebola hadi sasa, lakini kuna dawa kadhaa za majaribio mbali na ZMapp. Tiba hiyo bado ni mpya sana kiasi kwamba haijafanyiwa majaribio ya usalama au ufanisi kwa binaadamu. Na kampuni inayoitengeneza imesema itachukuwa miezi kadhaa kutengeneza wingi wa kutosha.

Haikuwa bayana ni kiasi gani cha dawa hiyo kitapelekwa nchini Liberia. Wizara ya afya ya Marekani ilisema katika taarifa kuwa serikali ya Marekani ilisaidia kuiunganisha serikali ya Liberia na mtengenezaji wa dawa hiyo, na kuongeza kuwa kwa sababu inasafirishwa kutumiwa nje ya Marekani, taratibu zote za usafirishaji wa nje zilipaswa kufuatwa.

Taarifa ya Liberia iliyowekwa kwenye tovuti ya ofisi ya rais, ilisema nchi hiyo ilikuwa inapokea pia dawa ya majribio kutoka kwa shirika la afya duniani WHO, lakini haikubainika mara moja iwapo taarifa hiyo ilikuwa inamaanisha dawa ya ZMapp au nyingine.


*Usalama na ufanisi wa ZMapp

Katika wiki chache zilizopita, dawa hiyo ya majaribio imetumiwa kwa wafanyakazi wawili wa misaada wa Marekani walioambukizwa ugonjwa huo wakifanya kazi kwenye hospitali ya wagonjwa wa Ebola. Siku ya Jumatatu, maafisa wa Uhispania walisema tiba hiyo ilikuwa imetumika kwa Padri mmishonari wa Kihispania alieuguwa akiwa nchini Liberia.

Wamarekani wanasemekana kupata nafuu, lakini hakuna njia yoyte ya kubainisha iwapo dawa hiyo imesaidia, au wanapata nafuu kivyao kama walivyopata nafuu wengine. Karibu asilimia 40 ya walioambukizwa virusi vya Ebola wananusurika mripuko wa sasa.

BBC WAFUNGUA STUDIO DAR ES SALAAM

Wafanyakazi wa BBC wakiwa kazini kupeperusha matangazo ya Dira ya Dunia redio

Idhaa ya kiswahili ya BBC imezindua rasmi studio zake mjini Dar es Salaam kwa mbwembwe na haiba kuu.

Uzinduzi huo ni matokeo ya mkakati na uwekezaji wa miaka mingi wa shirika la BBC duniani kuhakikisha kuwa matangazo yake yanawafikia wasikilizaji katika hali ya ubora wa hali ya juu na ya kisasa zaidi.
Katika hafla hiyo iliyoandaliwa katika ofisi hizo hizo mpya zilizoko eneo la Mikocheni, mkuu wa kitengo cha uandishi wa habari katika BBC, Nicki Clarke, ameshukuru serikali ya Tanzania, kwa kuwaruhusu kujenga studio hizo za kisasa zitakazoinua tasnia ya habari nchini humo na uhuru wa habari kwa ujumla.

Naye mkuu wa ofizi ya Dar es Salaam, Hassan Mhelela mbali na kuwataka wafanyakazi wa BBC Tanzania, kuzidi kuonyesha ushirikiano pamoja na utendaji kazi wa pamoja, pia ametangaza kuanishwa rasmi kwa ushirikiano kati ya BBC na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha uandishi wa habari.
Eric David Nampesya akizipa taabu Tumba kwenye sherehe ya ufunguzi wa ofisi za BBC Dar es Salaam

Ushirikiano huo amesema kuwa unalenga kusaidia kutoa mafunzo kwa wandishi wa habari chipukizi walioko mafunzoni katika chuo hicho, ambao kwa nyakati tofauti, watakuwa wakijiunga na BBC ili kupata mafunzo katika uandaaji vipindi vya redio na televisheni pamoja na utangazaji.

Kwa upande wa BBC, kuanzishwa kwa ofisi hii, yenye studio za kisasa kabisa za redio na televisheni mbali na kuongeza ubora wa vipindi lakini pia kutawezesha matangazo ya redio na televisheni kufanyika moja kwa moja kutokea Dar es Salaam.

Na kuanzia sasa matangazo ya Amka na BBC yatakuwa yakiandaliwa Dar es Salaam.
Itakumbukwa kuwa Tanzania mbali na kuwa na wasikilizaji wengi wa idhaa ya kiswahili ya BBC, lakini pia ndiko kunakozungumzwa zaidi lugha ya kiswahili.

Tanzania pia ina rekodi ambapo mtangazaji wa kwanza au sauti ya kwanza iliyosikika mwaka 1957, ilikuwa ya mtanzania Oscar Kambona ambapo alikuwa mwanafunzi mjini London.

SUNGUSUNGU WAFANYA MAUAJI

Mauaji ya kutisha ya watu wawili yanadaiwa kufanywa na kundi la Askari wa jadi maarufu kama Sungusungu wilayani Manyoni mkoani Singida baada ya kuwatoa nyumbani kwao usiku na kuwapeleka kichakani ambako waliwashambulia kwa kipigo kisha kumchoma moto mmoja akiwa mfu na mwingine akiwa bado hajakata roho.

Marehemu hao wanajulikana kwa majina ya Lameck Joshua (31) na Doto Kindai ( 20), na taarifa zilizozagaa kijijini hapo ni kuwa watu hao wameuawa kikatili kwa madai kuwa ni weziwa mifugo hata hivyo serikali ya kijji haina taarifa za watu hao kujihusisha na vitendo vya wizi.

POLISI AINGIA MATATANI KWA KUCHEZA MUZIKI NA SHAH RUKH KHAN

Mgogoro umeibuka nchini India baada ya polisi mwanamke nchini humo kucheza densi ukumbini na muigizaji maarufu Shah Rukh Khan katika tamasha la polisi lililofanyika katika jimbo la Bengal Magharibi.

Wanasiasa wa upinzani wamekosoa densi hiyo, wakisema afisa huyo wa polisi kucheza densi akiwa avelia sare zake, imehujumu heshima kwa polisi.

Kiongozi wa jimbo la West Bengal,Mamata Banerjee, aliyehudhuria tamasha hilo, pia alishambuliwa kwa kuruhusu tamasha hilo kufanyika.

Polisi huyo mwanamke na muigizaji Shah Rukh Khan bado hawajatoa tamko lolote kuhusu sakata hiyo.

Densi hiyo, ilifanyika katika tamasha maalum la polisi lililofanyika siku ya Jumamosi.

Shah Rukh Khan ni mmoja wawaigizaji mashuhuri nchini India na duniani , na hivi maajuzi alitajwa kama balozi wa jimbo la Bengal Magharibi.

Rais wa chama cha upinzani cha Congress katika jimbo hilo, Adhir Ranjan Chowdhury, alituhumu mkuu wa jimbo hilo Bi Banerjee kwa kukiuka, katiba kwa kumruhusu afisaa hiyo kucheza densi akiwa amevalia sare yake.

"katiba hairuhusu mtu kucheza densi akiwa amevalia sare za kazi. Ni aibutupu kwamba sifa ya idara ya polisi ilivunjiwa heshima hivyo. Kwa kuruhusu afisa wa polisi kucheza katika hali ile, alivunja katiba ya India, '' alinukuliwa akisema afisa mkuu wa upinzani jimboni humo.

Taarifa zinasema kuwa kamishna mkuu wa zamani wa polisi Nirupam Som alisema, "wakati wa muhula wangu uongozini, singeruhusuhata kidogo polisi kucheza densi kama vile. ''Lakini baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii, walipuuza sakata hii iliyozua mgogoro huu wote kama kutokuwa kichekesho.

MWAKA MOJA TALAKA 1600, ZANZIBAR

TAKWIMU za Mahakama ya Kadhi Zanzibar, zimeonesha kuwa zaidi ya talaka 1,600 zimetolewa Zanzibar kati ya 2012 na 2013, huku wanawake wengi wakitelekezwa bila kupatiwa haki zao baada ya kutengana na wenza wao.

Akizungumzia hali hiyo juzi mbele ya waandishi wa habari, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Hassan Othman Ngwali, alisema kwa sasa peke yake kuna kesi 1,917 za talaka mbele ya Mahakama sita za Unguja.

Mbali na kuwa na kesi hizo, Ngwali alisema wanawake wamekuwa waathirika wakuu baada ya kuvunjika kwa ndoa, kwa kuwa hakuna hukumu ya kesi zilizopita, ambayo haki ya mgawanyo wa malikwa wanandoa imetolewa.

Alitaja baadhi ya sababu zinazochangia kuwepo kwa wingi wa talaka Zanzibar, kuwa ni pamoja na wanandoa wenyewe kukosa mafunzo ya ndoa na majukumu yake kwa ujumla.

"Moja ya tatizo la kuvunjika kwa ndoa katika jamii, ni wanandoa kukosa elimu ambayo itawafanya kujua haki na faida zinazopatikana katika ndoa," alisema.

Alisema Ofisi ya Mahakama ya Kadhi imeanza kutoa elimu kwa makadhi wote kuhusu haki za wanandoa katika kipindi chote wanapokuwa kwenye ndoa.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Bakari Mshibe, alisema marekebisho ya Sheria ya Mahakama ya Kadhi, yapo katika hatua za mwisho kuwasilishwa mbele ya Baraza la Wawakilishi.

Alitaja baadhi ya mambo yaliyofanyiwa marekebisho kwa lengo la kuimarisha Mahakama hizo, kuwa ni pamoja na kutoa uwezo wa kumshurutisha mwanamume kutoa matunzo ya mtoto wakati ndoa inapovunjika.

"Moja ya mambo yaliyopewa kipaumbele katika marekebisho yaSheria ya Mahakama ya Kadhi, ni kuwabana wazazi ambao hawatoi matunzo kwa watoto wakati ndoa inapovunjika," alisema.

Wanaharakati wengi Zanzibar, wanataka kuwepo kwa marekebisho makubwa katika Sheria hiyo ya Mahakama ya Kadhi,hasa katika mgawanyo wa mali kwa wanandoa wakati wanapotengana.

WANANDUGU WATANO WA FAMILIA MOJA WATEMBELEA MIKONO NA MIGUU

FAMILIA moja ya Uturuki inawapasua kichwa wanasayansi, kutokana na wanandugu watano kutokuwa na uwezo wa kutembea kama binadamu, na badala yake wanatembea mithili ya wanyama, wakitumia miguu na mikono.

Hata hivyo, katika uchunguzi wao waawali, wanasayansi hao wameeleza kuwa, hali iliyowakumba wanandugu hao haina uhusiano na mabadiliko ya binadamu, kwamba wanaanza kurudi katika zama za mwanzo ambako inaelezwa walitembea kwa miguu minne, wengine wakisema walianza kuwa nyani.

Ndugu hao watano ambao ni kaka na madada, wakiwa na umri wa miaka 16 hadi 34 kutoka kijiji cha Jimbo la Hatay, kusini mwa Uturuki,walianza kufuatiliwa na wanasayansi mwaka 2005 baada ya kugundulika na watu kutoka nje ya kijiji chao.

Wanatembea kwa mtindo wa kutambaa kama dubu kwa mikono na wanaweza kusimama tu kwa muda mfupi, kwa magoti yao.

Utafiti wa hivi karibuni ulifanywa na wanasayansi, Shapiro, Whitney Cole,Scott Robinson na Karen Adolph, wote wa Chuo Kikuu cha New York, Jessica Young wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Northeast Ohio na David Raichlen, wa Chuo Kikuu cha Arizona.

"Lakini hawa hawana uhusiano na mgeuko wa binadamu kwamba baada ya kupitia hatua kadhaa za mabadiliko, sasa wanarudi katika hatua za awali, hilo halipo," mmoja wa wanasayansi hao amenukuliwa akisema.

Nadharia za awali zilidai familia ya Ulas ilikuwa ikitembea kama nyani, na kupendekeza kuwa huenda ni hatua ya kurudi nyuma kwa mabadiliko ya binadamu.

Lakini sasa, wanasayansi wa Kimarekani wamethibitisha kwa kusema wanandugu hao wanakabiliwa na kasoro isiyoonekana na hutokea mara chache.

Katika ripoti iliyochapishwa na PLOSOne, watafiti walisema familia hiyo wanatembea kwa namna tofauti kama nyani, ambao wakitembea huweka mikono upande mmoja na miguu upande mwingine wakijirudia rudia.

Walidai kutembea kwa wanandugu hao ni matokeo ya hali ya kurithi ambayo husababisha uwiano wa akili kutatizika.

"Nilikuwa na hamu ya kuweka rekodi sawa, kwa kuwa haya madai ya asili na sababu ya kutembea kama mnyama wa miguu minne imechapishwa mara kwa mara, bila kuwepo uchambuzi wa kwa nini wanatembea hivyo, na watafiti ambao si wataalamu wa namna mamalia wa hali ya juu wanavyotembea," Mtafiti Kiongozi Liza Shapiro wa Chuo Kikuu cha Texas alilieleza gazeti la The Washington Post.

"Tumeonesha wanyama wa miguu minne wanavyofanana na mtu mzima mwenye afya njema ambaye ameambiwa atembee kwa miguu minne wakati wa kufanya majaribio.

Mwaka 2005, watafiti wa Uingereza walikubali katika utafiti tofauti kuwautembeaji wa ndugu hao unatofautiana na baadhi ya mamalia wengine, ikizingatiwa wenyewe hubeba uzito wao wote kwenye viganja vya mkono na kifundo cha mkono na sio kiungio.

Hata hivyo, Mtaalamu wa Bayolojia wa Uturuki, Uner Tan awali alidai wanandugu hao, ambao pia wanaonekana kuwa wameathirika kwenye ubongo wanakabiliwa na hali inayoitwa Uner Tan Syndrome.

Alisema watu wanaokabiliwa na halihiyo hutembea kwa miguu minne na mara nyingine huzungumza kama wanyama na huwa na mtindio wa ubongo.

"Ghafla nimegundua wanatembea kwa mtindo kama nyani kama walivyokuwa wahenga wetu… nilikuwa wa kwanza kupendekeza kuwa kuna uwezekano wa hali ya binadamu kugeuka na kurudi enzi za zamani za ubinadamu," alisema.

Wandugu hao ambao wazazi wao wanatembea kawaida, mara ya kwanza walirushwa mwaka 2006 kwenye dokumentari ya BBC2, dokumentari hiyo ikiitwa The Family That Walks On All Fours.

Wakati mabinti wawili na mtoto mmoja wa kiume wamekuwa wakitembelea mikono miwili na miguu miwili, mtoto mwingine wa kiume na kike mara nyingine huweza kutembea wakiwa wamenyooka sawa, ingawa si kwa muda mrefu.

Profesa Nicholas Humphrey, ambaye aliitembelea familia hiyo mara mbili wakati wa dokumentari hiyo, alisema,
"inashangaza kama mfano wa kitu cha ajabu cha maendeleo ya binadamu. Lakini kinachovutia ni jinsia wanavyoweza kuishi katika ulimwengu wa kisasa."

Alisema alifikiri familia hiyo imerudi katika silika ya mfumo wa tabia iliyojikita ndani sana kwenye ubongo, lakini aliachwa wakati wa mageuko.

"Sidhani kama walitakiwa kuwa wanyama wanaotembelea miguu minne kutokana na jeni zao, lakini mfumo wa utengenezaji jeni zao zinawaruhusu kuwa hivyo," alisema.

Wanandugu hao watano ambao wana kaka na dada zao wengine 14 ambao hawajaathirika na hali hiyo, hutumia muda mwingi kukaa nje ya nyumba yao ya familia iliyoko kijijini. Hata hivyo, mmoja wao hutembea kijijini, kuchanganyika na kuzungumza na watu.

NDEGE YAANGUKA NA KUUA 40

Ndege moja iliokuwa na abiria 40 imeanguka mjini Tehran nchini Iran.

Runinga ya taifa la Iran imesema kuwa abiria wote wamefariki.

Ndege hiyo ya kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makaazi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Maghribi mwa mji wa Tehran.

Ndege hiyo inayojulikana kama Iran 141 ilitengezwa nchini Iran kupitia teknologia ya Ukraine.

Uchunguzi umeanzishwa kuhusu ni nini kilichosababisha ajali hiyo.

Iran imekabiliwa na ajali kama hizo katika siku za hivi karibuni kutokana na ndege zake zilizozeeka mbali na marekebisho mabaya inazozifanyia.

MAREKANI YAENDELEZA MASHAMBULIZI IRAQ

Marekani imesema kuwa imetekeleza mashambulizi zaidi kazkazini mwa Iraq dhidiya maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa Jihad.

Taarifa kutoka Pentagon imesema kuwa ndege za Marekani pamoja na zile zisizo na rubani ziliharibu magari ya kijeshi ya wanamgambo hao likiwemo lile lilokuwa likiwashambulia raia wa Yazidi ambao wamekimbilia hifadhi katika mlima Sinjar.

Awali Rais Obama amesema kuwa kupitia washirika wake wa ulaya pamoja na wanajeshi wa Iraq watawakabili wanamgambo ambao wameuzunguka mlima huo.

Hata hivyo ameonya kuwa kampeni hiyo ya kijeshi itachukua miezi kadhaa na kwamba itachukua mda kwa jeshi la Iraq kujikusanya ili kutoa upinzani mkali dhidi ya wanamgambo hao.

Wakati huohuo Ndege za kijeshi za Marekani na zile za Uingereza zimeendelea kuangusha misaada kwa raia waliokwama katika Mlima Sinjar nchini Iraq,ijapokuwa viongozi wa mataifa hayo mawili wamekubaliana kwamba hatua hiyo sio suluhu ya kudumu.

Wamesema kuwa lazima njia ya kuwaondoa raia hao hadi katika eneo lililo salama itafutwe ili kuzuia mauaji ya kimbari.

Mfanyikazi mmoja wa shirika la Amnesty International kazkazini mwa Iraq, Donatella Rovera ameiambia BBC kwamba maelfu ya raia kazkazini na magharibi mwa mlima huo wamefanikiwa kutoroka, lakini wengi zaidi katika eneo la kusini la mlimahuo hawana mahala pa kwenda.

Amesema kuwa wale waliotoroka wako katika hali mbaya baada ya kukaa siku sita bila chakula na maji kidogo.

WATU NANE WAFARIKI KATIKA AJALI

Watu nane wamefariki dunia na tisa kujeruhiwa baada ya gari mali ya mfuko wa hifadhi ya jamii TASAF wilaya ya Masasi kumkwepa mbuzi na kuacha njia na kuua watu nane waliokuwa wamekaa pembezoni mwa barabara kuu ya Lindi Mtwara.

Akizungumza kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Tenatha Mzinga amethibitisha kufariki kwa watu hao ambapo saba walikufa papo hapo na mmoja amefariki asubui ya leo katika hospitali ya Nyangawa iliyopo jimbo la mtama wilaya ya Lindi vijijini.

Akizungumzia mazingira ya ajali kamanda Mzinga amesema imesababishwa na mwendo kasi wa dereva aliyefahamika kwa jina la Kesi Mwaijande ambapo amesema baada ya kumwepa mbuzi alikosa mwelekeo na kuwazoa.

Kwa upande wake daktari wa zamu Manfid Nyangali amethibitisha kupokea maiti zaba na majeruhi.

Wakizungumzia ajali hiyo wananchi wa kijiji cha Mtama jimbo la Mtama wanahaya ya kusema gari hiyo yenye namba za usajili STl 1615 Landrover iliyokuwa imebeba madiwani sita wa halmashauri ya mji wa Masasi ilikuwa ikitokea kwenye kilele cha maonyesho ya nanenane mkoani Lindi.

MZEE ARFI ATINGA BUNGENI

WAKATI Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, akisema kuwa anaamini idadi ya wajumbe wa bunge hilo wanaorejea bungeni baada ya kususa vikao itazidi kuongezeka, Mbunge wa Mpanda Kati, Said Arfi (Chadema) ametinga bungeni.

Amesisitiza kuwa yeye si msaliti, bali anachojali ni maslahi ya wananchi kwanza na maslahi ya vyama vya siasa, yanafuata baadaye. Pia, Arfi ameonya kwamba baadhi ya vyama vya siasa, hivi sasa vinataka kupora mamlaka ya wananchi, kuhusu mchakato wa katiba, kitu ambacho si sahihi na kinapaswa kuepukwa.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge jana, muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu za usajili kwa ajili ya kushiriki vikao vya Bunge hilo, Arfi alisema yeye anafuata maslahi ya wananchi wake waliomtuma na wala si vinginevyo.

"Bunge Maalumu la Katiba limeundwa kwa mujibu wa sheria, ambayo sote tulishiriki kuiandaa, ambayo inasema kutakuwa na makundi matatu, ambayo ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wateule 201 wa Rais kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.

"Hivyo mimi ni Mbunge wa Mpanda Kati, naingia kwa mujibu wa Katiba, nina haki kisheria kuwakilisha wananchi wangu, vyama visitake kupora mamlaka ya wananchi waliotutuma," alisema Arfi.

Alisisitiza kuwa kushiriki kwake vikao vya Bunge Maalumu la Katiba hakumaanishi yeye ni msaliti kama baadhi ya watu wanavyodai, bali wale wanaoshindwa kuhudhuria vikao, ndiyo wasaliti wa wananchi.

Alisema kwamba msimamo wake katika muundo wa serikali, unabakikuwa serikali tatu, na bado yeye ni mwanachama wa Chadema.

Alisema Bunge Maalumu la Katiba halina wajumbe wa chama tawala wala wa upinzani, kama ilivyo katika Bunge la kawaida la Tanzania.

"Bunge Maalumu la Katiba lina makundi ambayo naweza pia kusema mawili, wajumbe kutoka Tanzania Bara na wajumbe kutoka Zanzibar, hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani kama ilivyo katika lile bunge letu, hivyo mimi nimekuja kama Mjumbe wa Tanzania Bara," alisisitiza.

Alieleza kuwa jana alitarajia kuhudhuria vikao vya kamati yake Namba 10, kujadili rasimu hiyo. Alisema kwamba kinachotakiwa bungeni ni hoja na suala la wingi au uchache halina nafasi, kwani kuna wakati wakiwa wachache wanaweza kusikilizwa kama wakiwana hoja. Pia, alieleza kuwa suala la muundo wa serikali haliwezi kumfanya akae nje, kwani yapo mambo mengi ya kimsingi ya kwenda kujadili, ambapo yeye atatoa mawazo yake akiwa ndani bungeni na wala si vinginevyo.

Arfi, ambaye amepata kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema kabla ya kujivua nyadhifa zote alizokuwa nazo kwenye chama hicho mapema mwaka huu, anakuwa Mbunge wa tatu wa Chadema kujisajili kwa ajili ya kushiriki vikao vya Bunge hilo. Wengine ni Leticia Nyerere na John Shibuda.

Mjumbe mwingine ni Clara Mwatuka ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CUF).

Wakati huo huo, Sitta alisema idadiya wajumbe wa Bunge hilo kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) itazidi kuongezeka katika kuhudhuria vikao kadri siku zinavyoenda, kwa vile Rasimu ya Katiba ina mambo mengi ya msingi yanayojadiliwa.

Alitoa kauli hiyo jana mjini hapa, kutokana na swali aliloulizwa na waandishi wa habari, waliotaka maoni yake kuhusu wajumbe wa Ukawa, ambao wameanza kujisajili.

"Wataongezeka kadri siku zinavyoenda…unajua katika rasimukuna mambo mengi sana ya kujadili na utaonekana mtu wa ajabu kama haupo, mfano wewe mjumbe unatoka katika jimbo la wafugaji na suala hilo linajadiliwa halafu haupo, kuna mambo ya ardhi na mengine mengi.

"Kamati zetu mbalimbali tangu jana (juzi) zinaendelea kujadili Suraya Pili na ya Tatu, mijadala imekuwa mizuri sana na wajumbe wanatoa michango kwa nia ya kuboresha rasimu," alisema Sitta.

Mwenyekiti huyo alisema viongozi wa Ukawa wamekataa kuzungumza na yeye, Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo maalum, Samia Suluhu Hassan na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahaya Khamis Hamad, hivyo kama kuna wanaotafuta namna ya kuzungumza nao, basi ni nje ya ofisi yake.

"Kama kuna vyama huko vinazungumza sijui," alisema. Alisema anaamini mjadala wa kamati mbalimbali, zitakapokuwa zinawasilisha bungeni ripoti zao kuanzia Septemba 2, mwaka huu idadi ya wajumbe waliokuwa wamesusia, itakuwa imeongezeka kurejea bungeni, kutokana na kuwepo maslahi ya wananchi yanayojadiliwa.

Akizungumzia hali hiyo jana, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alisema mjumbe wa Ukawa atakayeshiriki vikao vya Kamati na Bunge, atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za chama." Msimamo wa Ukawa ni kuwa wajumbe wanaotoka Ukawa kutoshiriki vikao vya Bunge au kamati mpaka hapo tutakaporidhiana, na mpaka sasa hilo halijafanyika.

"Kutoa maelekezo ni jambo moja na kutekeleza ni jambo jingine, hivyo mjumbe atakayeshiriki vikaovya Bunge au Kamati, atakuwa ameshindwa kutekeleza agizo la chama, hivyo litakuwa ni suala la chama na atashughulikiwa kwa taratibu za chama," alisema.

Alisema jamii inatakiwa kuelewa kuwa wabunge ambao vyama vyao vimekataa kushiriki vikao vya Bunge Maalumu, hawana kosa kuonekana Dodoma, viwanja vya Bunge na kuwasiliana na wajumbe wa 201 na wale wa Chama Cha Mapinduzi."

Mbunge kuonekana viwanja vya Bunge au Dodoma si kosa, kwani Bunge Maalumu la Katiba linatumia majengo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ambayo pia shughuli zingine za Bunge zinaendelea.

"Hata mimi (Mbowe) ukiniona viwanja vya Bunge si kosa, ofisi zangu ziko katika majengo ya Bunge, pia kuna masuala mbalimbali ya maslahi ya wabunge, mishahara, majalada na masuala ya utumishi wa wabunge yanafanyika hapo," alisema.

Akizungumzia tamko la Mbowe kwamba watakaohudhuria Bunge hilo, watachukuliwa hatua kulingana na taratibu za chama, Arfi alisema ifike mahali unapofanyika uamuzi, uzingatie hoja.

Alisisizita kuwa ni haki yake, kufanya hivyo na ikiwa vipo vyama visivyozingatia demokrasia, ni jambo la kushangaza katika uendeshaji wa nchi.

Alisema mgogoro uliopo ni juu ya tafsiri ya Kifungu Namba 25 cha Sheria, ambayo waliitunga wabunge wenyewe.

Arfi alisema kwa kuwa wabunge ndiyo waliotunga sheria husika, hakuna mahali pengine ambako tafsiri ya sheria hiyo, inaweza kupatikana isipokuwa mahakamani.

"Njia pekee ni mahakamani na si kujadili nje ya Bunge au kususa," alisema Arfi.

MAREKANI WASHAMBULIA IS IRAQ

Wizara ya ulinzi nchini Marekani inasema kuwa ndege za jeshi la Marekani zimefanya mashambulizi ya angani dhidi wanamgambo wa kundi la Islamic state kaskazini mwa Iraq.

Pentagon ilisema kuwa ndegezilishambulia vituo vilivyokuwa vikitumiwa kushambulia vikosi vya kikurdi vinavyopigana kulindangome ya mji wa mji wa Irbil.

Siku ya Alhamisi rais wa marekani Barack Obama aliamrisha kufanyika kwa mashambulizi ya angani dhidiya wanamgambo wa kisuni ambao wameteka kiasi kikubwa cha ardhi ndani ya Iraq na pia ndani ya Syria.

Rais Obama alisema kuwa wapiganaji wa kundi la Islamic State watalengwa iwapo wataelekea kwenye mji wa kikurdi wa Irbil au kwalengo la kuzuia kile alichokitaja kama vitendo vya mauaji ya halaiki dhidi ya wakristo na jamii za Yazidi.

Hatua ya Marekani inajiri kukiwa na wasiwasi mkubwa wa uwezo wa wanamgambo hao kuteka sehemu kubwa zaidi ya Kaskazini mwa Iraq mbali na sehemu kubwa ya Syria.

Rais Obama amewashutmu wanamgambo wa Islamic State kwa kujaribu kuiangamiza jamii nzima na ya Yazidi akisema kuwa serikali yake itachukua hatua za kuzuia kutokea kwa mauaji ya halaiki.

Ndege za jeshi la marekani zimekuwa zikiangusha misaada huku nayo Uingereza ikisema kuwa itajiunga kwenye jitihada za kutoa misada.

Kiongozi wa dhebu la shia nchini Iraq Ayatollah Ali al Sistani amewataka wanasiasa nchini Iraq kungana na kumaliza ghasia huku naye kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis akisema kuwa atatuma mmoja wa viongozi wa kanisa hilo kama njia ya kuonyesha umoja.

Mnamo mwezi juni IS, awali ikijulikana kama Isis, iliteka mji wa Mosul kisha kundi hilo likauteka mji wa wenye wakristu wengi Qaraqosh.

Kulingana na Idara ya usalama ya Marekani Pentagon ndege mbili za F/A-18 zilidondosha mabomu yenye paundi 500 ilikukaharibu ngome ya mashambulizi ya IS inayotumika kuishambulia mjiwa Irbil.

Mji huo wa Irbil ni mwenyeji wa kikosi cha wanajeshi wa Marekani.Hii ndiyo mara ya kwanza kwa jeshi la Marekani kujihusisha katika mapigano ndani ya Iraq tangu mwaka wa 2011.

Waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry ameonya jamii ya kimataifa kugutuka na kutahadhari dhidi ya ufanisi wa kundi hilo la wanamgambo wa IS.

WAKILI WA PISTORIUS ASEMA KESI IMEVURUGWA

Kundi la mawakili wanaomtetea mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius wanasema kuwa viongozi wa mashitaka wamevuruga kesi hiyo kwa minajili ya kumfanya kuwa namakosaKwenye taarifa yake ya mwisho wakili wa Pistorius Barry Roux amesema kuwa bwana Pistorius angefunguliwa mashitaka ya kuua bila kukusudia bali si ya mauaji baada ya kumpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

Bwana Pistorius anasema kuwa alimpiga risi kimakosa akidhani kuwa alikuwa ni jambazi.

Lakini bwana Roux alikiri kwamba Pistorius anapaswa kupatwa na hatia kwa kosa la kutumia silaha yake katika mgahawa.

Wakati kila upande utakapo kamilisha kutoa kauli zao ya mwisho jaji ataahirisha kesi hiyo kwa takriban wiki moja kufanya uamuzi.

Mwanariadha huyo amekanusha makosa yake dhidi yake ikiwemo kosa la kutumia silaha yake katika sehemu ya umma pamoja na kumiliki silaha haramu.

ISRAEL WASHAMBULIA GAZA

Israel imeanza kufanya mashambulizi ya angani dhidiya Gaza katika hatua yake ya kujibu mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa kipalestina dhidi ya Israel.

Mashambulizi haya yametokea baada ya makubaliano ya siku tatu ya kusitisha vita kuvunjika.

Serikali ya Israel imesema kuwa iliamuru jeshi kujibu mashambulizi hayo kwa ukali.

Jeshi la Israel linasema linashambulia maeneo yanayotumiwa na wapiganaji hao katia ukanda wa Gaza.

Kuna taarifa za kutokea mlipuko mkubwa katika ukanda wa Gaza na wakazi wa Palestina wamekuwa wakiondoka katika maeneo hayo.

Hamas ilikanusha madai ya kuongezwa muda wa makubaliano ya kusitisha vita ikisema kuwa Israel ilikataa kukubaliana kufanya mkutano kulingana na matakwa yao kwa masharti ya Misri ikiwemo kumaliza.

WAJUMBE WA UKAWA WATINGA BUNGENI

Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahya Khamis Hamad Amethibitisha kuwepo kwa wajumbe wa Bunge hilo kutoka kundi la Ukawa ambao wanashiriki vikao na wengi wamejisajili lakini hawajashiri kikatika kamati yoyote.

Amesema katika uchunguzi alioufanya wajumbe waliojisajili na kutoshiriki vikaoni pamoja na Leticia Nyerere, Clara Mwituka Pamoja na John Shibuda wote kutoka chadema.

Aidha amewataja wajumbe wengine kutoka Ukawa ambao wanashiriki vikao ni pamoja na Fatuma Ally, Jamila Abed na Omary Alyla Katiba kamati namba 2 wanasema majadiliano yanaendelea vizuri licha ya kuwepo na changamoto mbalimbali Miongoni mwa wajumbe Kutoka ukawa walionekana Mjini Dodoma ni pamoja na Chiku Abwao ambaye anasema amekuja kwa kazi zake binafsi na kamwe hawezi kushiriki vikao hivyo.

Shamsi Vuai Nahodhani mwenyekiti kamati namba 3 na Dk Francis Michael ni mwenyekiti kamati namba mbili wanasema kwasasa tayari wamekwisha anza kujadili sura ya 3,4,5 na tano,licha ya changamoto mbalimbali zinazojitokeza.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wameanza kukaa kwenye kamati katika kumbi mbalimbali zilizopo Mkoani humo tarehe 6 mwezi huu kwaajili ya kujadili sura 15 za Rasimu ya Katiba zilizokuwa zimeb aki na kazi hiyo itafanyika kwa siku 15, ambapo watarejea tena ndani ya bunge.

WAKRISTO WATOROKA MJI WA QARAQOSH IRAQ

Maelfu ya Wakristu wanatorokea maisha yao katika mkoa wa Nineva baada ya wapiganaji wakiislamu waThe Islamic State kuuteka mji wa Qaraqosh.

Afisa wa ngazi ya juu wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq ameonya kuwa watu 50,000 wa jamii ya Yazidi watakabiliwa na njaa ikiwa hawatapata msaada wa dharura.

Jamii ya Yazidi ilikimbilia maeneo ya milima ikiwa na chakula kidogo na maji baadaya wapiganaji wa jihad kutoka kwa kundi la Islamic State kuvamia mji wa Sinjar mwishoni mwa wiki.

Wapiganaji wa Kikurdi Peshmerga awali wakidhibiti mji huo wa Mosul.

Jabbar Yawar, ambaye ni kiongonzi wa wapiganaji wa kikurdi anasema kuwa tayari wengi wao wameaga dunia

Kutekwa kwa mji wa Qaraqosh kumesababisha kukimbia kwa maelfu ya watukaskazini mwa Iraq kutokana na vitishovya makundi ya Jihad.

Kushindwa kwa vikosi vya kikurdi kudhibiti mji huo na mji mingine kutoka kwa mikono ya wapiganaji wa Islamic State kutasabaisha mengi..

Wapiganaji wa Kikurdi wa Peshmerga walikimbia mji huo bila kupingwa.

Kasisi mmoja mkuu wa eneo hilo ameliambia shirika la Habari la Ufaransa kuwa, maelfu ya watu wanaonekana wakikimbia kwa hofu.

Kuondoka kwa watu hao kunafutia kuondoka kwa wakrito wengine kutoka mji wa Mosul baada ya kuamrishwa kundoka , kubadili dini au kuawa na wapiganaji wa Jihad.

Wapiganaji wa The Islamic State wameteka kiasi kikubwa tu cha ardhi kutoka Iraq na Syria ambayo wametangaza kuwa taifa la kiislamu.

Inakisiwa kuwa wakaazi laki moja wameshatorokea maeneo ya Kurdistan.

URUSI YALIPIZA KISASI MAREKANI NA ULAYA

Urusi imetangaza marufuku ya vyakula kutoka kwa muungano wa Ulaya, Marekani na nchi zingine kadha za magharibi ambazo zilikuwa zimetangaza vikwazodhidi ya Urusi kutokana na sera zake nchini Ukraine.

Waziri mkuu nchini Urusi Dmitry Medvedev aliuambia mkutano wa serikali kuwa Urusi haitaruhusu tena uingizwaji wa Nyama, Samaki, Matunda na bidhaa zingine kutoka mwa jumuiya ya Ulaya, Marekani, Australia,Canada na Norway.

Medvedev amesema kuwa vikwazo hivyo vitadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Amesema kuwa Urusi inatathmini kupiga marufu mashirika ya ndege ya nchi za magharibi yanayotumia anga ya Urusi kuingia barani Asia.

Wadadisi wanasema kuwa Urusi inategemea zaidi chakula kutoka nje asilimia kubwa ikiwa ni kutoka kwa nchi za magharibi.

KITUO CHA POLISI CHACHOMWA MOTO

WATU tisa w a n a o d a i wa ni waendesha bodaboda (pikipiki), wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kuchoma moto Kituo cha Polisi Mkuyuni na kusababisha majeruhi kwa watu wawili, akiwemo askari polisi na kumtorosha mtuhumiwa aliyekuwa anashikiliwa kituoni hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema tukio hilo lilitokea Agosti 3, mwaka huu, saa11:45 alfajiri katika Tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro.

Aliwataja waliojeruhiwa katika tukio hilo ni askari mwenye namba G 7012, PC Edson ambaye alitibiwa na kuruhusiwa, Hamad Kimolo(26), mwendesha pikipiki na mkazi wa Kinole ambaye alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Kamanda Paulo aliwataja waliokamatwa ni Valentino John (18), Jafari Hussein (20),Kulwa Kesi (32) na Rashidi Iddi(22), wote wakiwa ni wakazi wa eneo la Kinole, Mashaka Degeresa (20) na Juma Ally(19), wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji cha Kalundwe.

Aliwataja wengine ni Hamisi Juma mkazi wa Dar es Salaam, Sheuna Hassan na Bilali Tamimu (19), wote wakiwa ni wakazi wa Kinole.

Kamanda alisema siku ya tukio askari wakiwa kazini walimkamata mwendesha pikipiki, Ally Musa (19), mkazi wa Kinole akiwa amepakia abiria watatu kwenye pikipiki namba T 162 CSC aina ya Fecon, ambapo mtuhumiwa alikataa kwenda polisi na kutelekeza pikipiki yake.

Paulo alisema baada ya kuondoka, polisi waliichukua pikipiki hiyo na kumfungulia kosa la kupakia watu watatu(mshkaki).

Alisema saa 12: 45 asubuhi waendesha bodaboda zaidi ya 30 walivamia kituo hicho, huku wakiwa na marungu, matofali na fimbo na kuanza kufanya vurugu wakitaka kumtoa mwenzao aliyekamatwa na kukiweka kituo hicho katika hali ya hatari, ambapo walifanikiwa kumtoa mwenzao na kuondoka na pikipiki yake.

Kamanda aliongeza kuwa, bodaboda hao waliamua kuchoma moto kituo hichona kumjeruhi askari namba G7012.

Aliwataka raia kutambua kuwa, polisi haihitaji uhuni katika maisha ya binadamu, bali inahitaji kuheshimu sheria ili waweze kuishi katika mazingira ya amani.

WANAOFUGA NDEVU NA KUVAA HIJAB MARUFUKU CHINA

Wanaume wanaofuga ndevu pia wameambiwa wasipande kwenye usafiri wa umma.

Mji mmoja wa China wa mkoa wa Xinjing umekataza wale wote wanaovaa nikab na kufuga ndevu kupanda kwenye usafiri wa umma, limeeleza gazeti moja nchini humo.

Maafisa wa Karamay walisema katazo hilo, ambalo linakataza uvaaji wa hijab, nikab na burka kuwa utaisha Agosti 20 kutokana na matukio ya michezo.

Xinjiang, ni makazi yenye Waislamu wa Uighur wachache, umekumbwa na ghasia miezi ya karibuni.

Wanawake wanaovaa nikab, hijab na burka wamekatazwa kupanda usafiri wa umma katika jimbo hilo.Uongozi umeilamu Uighur wanaotaka kujitenga kwa kufanya ghasia hizo.

Katika ripoti iliyotolewa na gazeti la Karamay Daily ambalo huendeshwa na chombo cha habari cha taifa hilo, maafisa hao walitaja "watu wa aina tano" ambao wamekatazwa kupanda usafiri wa umma.

RAGE, TAMBWE WAPATA AJALI

WABUNGE Wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Tabora kwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba kupata ajali.

Wabunge hao ni Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage na Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe. Majeruhi wengine katika ajali hiyo ni Issa Chimwaga (31), Mwanahamisi Ramadhani (34), John Hoya (32) ambaye ni dereva ambapo pia hakuumia katika ajali hiyo.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ezekiel Mpuya alisema jana mchana walipokea majeruhi wannewa ajali hiyo wakiwemo Wabunge Rage na Munde.

Alisema majeruhi hao walitokana na ajali waliyoipata katika eneo la Chigongwe Manispaa ya Dodoma walipokuwa wakisafiri kwenda Dodoma kwa gari binafsi.

Dk Mpuya alisema vipimo vimeonesha Munde pamoja na kupata majeraha usoni na kichwanipia amevunjika mkono wakati Rageameteguka bega la kushoto. Hata hivyo, alisema hali zao zinaendelea vizuri na wanaendelea na matibabu.

Hata hivyo, Rage na Munde wamelazwa katika Wodi namba 18 Grade One chumba namba moja na mbili wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini. Akizungumza akiwa wodini Rage alisema amepata majeraha katika bega la kushoto na eneo la nyuma ya mgongo.

Alisema ajali hiyo ilitokea baada yadereva wa gari lao anataka kulipita lori lakini ghafla dereva wa lori hilo akaingia katikati ya barabara.

Alisema dereva wao alipoona hivyo badala ya kuligonga lori aliamua kwenda pembeni ndipo gari lao likaruka na kuingia kwenyekorongo na kupinduka.

Alisema kilichowasaidia walikuwa wamefunga mikanda jambo ambalo. Kwa upande wake Tambwe alikuwa akilalamikia maumivu katika sehemu za kichwani na mkono.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Dodoma, Peter Sima alipotakiwa kuzungumzia ajali hiyo alisema bado anakusanya taarifa na kuahidi kutoa taarifa baadaye.

Hata hivyo, taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu wa familia za wabunge hao iliyopatikana baadaye jana, ilisema wabunge hao walichukuliwa kwa ndege maalumu jana jioni kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar kwa matibabu zaidi.

DAKTARI AAMBUKIZWA EBOLA NIGERIA

Daktari mmoja jiji Lagos Nigeria amepatikana ameambukizwa na maradhi ya homa ya Ebola.

Daktari huyo ambaye alimtibu mfanyikazi wa wizara ya hazina nchini Liberia aliyepatikana na homa hiyo ya Ebola na kuwa mtu wa kwanza kuaga dunia nchini Nigeria sasa amedhibitishwa kuambukizwa.

Waziri wa afya nchini humo Onyebuchi Chukwu amesema kuwa daktari huyo pamoja na watu wengine 70 waliokutana na marehemu wametengwa kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Patrick Sawyer alitua nchini Nigeria Julai tarehe 20 na akafa tarehe 25 katika hospitali moja mjini Lagos.

Mlipuko huu wa ugonjwa wa ebola katika ukanda wa magharibi mwa Afrika umesababisha vifo vya watu zaidi ya 826 katika mataifa ya Guinea, Liberia na Sierra Leone.

MAHASIMU WA SUDAN KUSINI KUKUTANA TENA

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na waasi yameanza tena katika nchi jirani ya Ethiopia.

Mazungumzo hayo, yalikuwa yameahirishwa kwa wiki kadhaa Vita vimeendelea nchini Sudan Kusini licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufikiwa kati ya pande husika.

Zaidi ya watu milioni moja unusu, wameachwa bila makazi kutokana na vita hivyo.

Umoja wa Mataifa na mataifa mengine ya Magharibi yameonya kua Sudan Kusini inakabiliwa na tisho la kukumbwa na njaa.

Maafisa wa baraza la usalama la Umoja huo, wanatarajiwa kuzuru nchi hio wiki ijayo.

Katika mazungumzo hayo, serikali na waasi wanatarajiwa kuzungumzia swala la kubuni serikali ya mpito pamoja na muundo wake Makataa ya makubaliano hayo ni chini ya wiki moja na huenda muda huo usifikiwe.

DAKTARI FEKI ADAKWA MANYARA

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa ya mkoani Manyara kwa kushirikiana na polisi wamefanikiwa kumnasa mkazi wa jijini Dar-es-salaam Bw Godlove Sozigwa akituhumiwa kuomba kufanya mazoezi ya kutibu kwa muda kama daktari wa magonjwa ya moyo na figo kwa kutumia vyeti bandia wakati akitambua kuwa yeye si mtaalam wa tiba.
Bw Godlove Sozigwa kabla ya kukamatwa kwake asubuhi kufuatia jopo hilo la madaktari kubaini kuwa vyeti alivyoviwasilisha katika hospitali hivyo julai 31 ni bandia na hata hivyo alipoitwa na kufanyiwa mahojiano amedai huku akionyesha ukomavu wa kujieleza taaluma hiyo aliipatia katika chuo cha sayansi, tiba na utafiti cha Muhimbili na kufuzu hata hivyo alibahatika serikali kumpeleka nchini India kwa mafunzo zaidi kusomea dawa zaidi.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoani Manyara Dr Peter Mshali akizungumza na ITV baada ya kukabidhiwa kwa polisi ili kufanyiwa upelelezi amesema katika mahojiano na jopo la madaktari walibaini vyeti hivyo ni bandia aidha pia mtuhumiwa Dr huyo Godlove Sozigwa si mtaalam kulingana na maelezo yake bali ni tapeli na hatari endapo angebahatika kupata nafasi hiyo.

Nae kamanda wa polisi mkoani hapa afande Deusdedit Nsimeki amekiri na katika mahojiano amesema polisi imebaini baada ya kumfanyia mahojiano na upekuzi kumkuta na kompyute mpakato(laptop) muhuri wa kuchonga wa hospitali ya rufaa ya Muhimbili, koti na vyeti mbalimbali,lakini wanafanya upelelezi zaidi kabla ya kumfikisha mahakamani.

Tangu awali ITV iliyoshughudia mtego huo mapema asubuhi na baada ya mtuhumiwa Godlove Sozigwa kufikishwa polisi amekiri kuwa yeye si daktari aliyesoma chuo hicho cha Muhimbili bali anafanya hivyo kutokana na mazingira magumu, hasa kwa kuipenda taaluma ya udaktari baada ya kujifunza katika kituo cha tiba cha Neptune cha matabibu ya kichina kilichopo Ubungo Plaza jijini Dar-es-salaam na kupata uzoefu.

Chanzo: ITV

RAIS KIKWETE AKANUSHA KUMUOKOA RIDHIWANI CHINA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Sina muda kujadili upuuzi huu kuhusu Ridhiwani–Rais Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni mkusanyiko wa upuuzi mtupu madai kuwa yeye Rais alishiriki kumwokoa mtoto wake, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ambaye alikuwa amekamatwa na madawa ya kulevya nje ya nchi.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Urais ni taasisi kubwa sana nchini na hivyo yeye akiwa Rais hawezi kujiingiza katika ubishani na watu wa mtaani, kama ambavyo wanataka baadhi ya watu wanamsukuma ili ashiriki katika maneno hayo ya mitaani.


"This is nonsense–ni mkusanyiko wa upuuzi. Sina muda wala siwezi kupoteza nguvu yangu kujadili upuuzi na ujinga wa namna hiyo,"amesema Rais Kikwete usiku wa Jumamosi, Agosti 2, 2014, wakati alipozungumza na Watanzania wanaoishi katika Marekani kwenye Hoteli ya Marriot Washington, mjini Washington D.C.
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa katika Marekani alitoa majibu hayo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu madai yaliyotolewa Julai Mosi, mwaka juzi, 2012 na Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA, Wilbroad Slaa, madai hayo yamempeleka mahakamani.
Amesema Rais Kikwete:"

Hatuwezi sisi kujiingiza katika shughuli ya kupoteza muda kwa kushiriki upuuzi na ujinga.

Haya ni maneno ya kipuuzi yanayosemwa na watu ambao kazi yao usiku na mchana ni kuota jinsi ya kuyumbisha ajenda yetu ambayo imefanikiwa sana katika kubadilisha hali ya maisha ya Watanzania.'

Amesisitiza Rais Kikwete:
"Urais ni taasisi kubwa sana. Rais wa nchi yetu hawezi kujiingiza katika ubishani na watu wa mitaani. Kwanza huyo Ridhiwani amemfikisha Slaa kortini na mpaka leo hata kesi yenyewe haijatajwa."


Kuhusu swali jingine aliloulizwa kuhusu suala hilo, kuwa Rais Kikwete alitia saini mikataba 12 na uongozi wa Jamhuri ya Watu wa China kama sehemu ya masharti ya kuachiwa kwa Ridhiwani, Rais Kikwete amesema:

"Naipenda nchi yangu kiasi cha kwamba siwezi kufikiria hata kuiweka rehani. Haya ni maneno ya kipuuzi tu, yenye kutafuta kututoa kwenye ajenda zetu nzuri. Hatuna muda nayo, sisi tunaelekeza nguvu zetu kwenye mambo ya maana ya kuleta mabadikio katika ustawi wa Watanzania."


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu–Dar es Salaam.
04 Agosti, 2014

JK, OBAMA KUKUTANA NA MARAIS WA AFRIKA

RAIS Jakaya Kikwete yuko Marekani kwa ziara ya siku tisa nchini humo ambako miongoni mwa mambo mengine, atahudhuria Mkutano waKwanza wa Kihistoria wa Viongozi wa Bara la Afrika na Marekani ulioitishwa na Rais Barack Obama.

Mkutano huo wa siku mbili unafanyika kuanzia leo ukianza na mkutano wa biashara kati ya Afrikana Marekani. Unafuatiwa na mkutano wenyewe wa Marekani naAfrika utakaofanyika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles mjini Washington, Rais Kikwete alipokewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Kwenye ziara hiyo, Rais Kikwete ameongozana na mkewe, Mama Salma Kikwete ambaye naye atakuwa na programu tofauti wakati wa ziara hiyo, kama watakavyokuwa wake wa viongozi wengine wa Afrika wanaohudhuria mkutano huo.

Mkutano huo wa kwanza wa aina yake kati ya kiongozi wa Marekani na viongozi wa Afrika umepangwa kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi 47 ambazo zote zimealikwa naRais Obama kushiriki mkutano huo.

Mbali na shughuli zake nyingi za mjini Washington, Rais Kikwete atasafiri kwenda Dallas, Jimbo la Texas, ambako atakutana na Rais wa 43 wa Marekani, George W. Bush, kabla ya kuendelea na safari katika mji mwingine mkubwa wa jimbo hilo wa Houston.

Mjini Houston, Rais Kikwete atafanya mkutano wa kimkakati wakibiashara na wafanyabiashara maarufu mbalimbali hasa wa sektaya gesi na mafuta kabla ya kumaliza ziara yake.

Miongoni mwa shughuli zake, Mama Salma Kikwete atahudhuria mkutano wa wake wa marais wa Afrika na mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama utakaofanyika kwenye Kituo cha John F Kennedy.

Mkutano huo utahudhuriwa pia na mke wa Rais George W. Bush, Mama Laura Bush.

''UKAWA WAMEPOTOSHA'' JK

RAIS Jakaya Kikwete amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, waliojiundia kundi la Umojawa Katiba ya Wananchi (UKAWA), warudi katika Bunge hilo, watumie mifumo maalumu waliyojiwekea na kanuni walizojitungia wenyewe, kutafuta maridhiano.

Ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati wa hotuba yakealiyoitoa kwa Taifa katika utaratibu aliojiwekea wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi.


Rais Kikwete amewataka wajumbe hao, watafute maridhiano kwa kutumia mifumo hiyo rasmi, na yeye yupo tayari kusaidia pale watakapohitaji msaada wake kuhusu suala hilo, ili Watanzania wapate Katiba bora wanayoihitaji.Ameonya kuwa ikiwa maridhiano wanatafuta nje ya mifumo hiyo, watakuwa wakitumia mitandao tu isiyokuwa na faida kwao wala jamii.

Mbali na kuwapa onyo hilo, pia aliwakumbusha kuwa Bunge Maalumu la Katiba lina mamlaka ya kutunga Katiba, na kama isingekuwa hivyo kusingekuwa na haja ya kuwa na siku 70 za awali nayeye kupewa mamlaka ya kuongeza siku 60 kujadili.

Alionesha kuwashangaa wajumbe hao kwamba, kanuni na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba waliitunga wenyewe na sasa katika utekelezajiwa sheria hiyo, wanasusia vikao jambo alilosema si haki kwa ummawa Watanzania.

Kikwete alisema yeye si Mwanasheria hivyo anakiri kwamba anaweza kuwa na upungufu katika kuelewa maana yabaadhi ya maneno ya kisheria, lakini akasema hakumbuki kuwepokwa kifungu chochote katika Sheria, kinachosema kuwa Bunge Maalumu la Katiba halina mamlakahayo.

"Tangu tuliposikia maneno hayo yakisemwa (kwa Bunge Maalumu haliwezi kubadilisha rasimu ya Katiba), nimeuliza nithibitishiwe ukweli wa madai hayo lakini bado sijaambiwa vinginevyo. Kama ukweli huo upo naomba wanisaidie," alisema Rais Kikwete.

Alisema badala yake ameambiwa kuwa maneno yaliyotumika katika Sheria, hayaakisi dhana inayotolewa kuwa kazi ya Bunge Maalumu la Katiba ni kubariki Rasimu na si kufanya vinginevyo."Nimeambiwa kuwa sheria inasema Tume itaandaa Rasimu ya Katiba na Bunge Maalumu la Katibalitatunga Katiba iliyopendekezwa," alifafanua Kikwete.

Akielezea hatua iliyofikiwa kabla yakuahirishwa kwa Bunge hilo Aprili 25 mwaka huu kupisha Bunge la Bajeti na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Rais Kikwete alisema wakati baadhi ya wajumbe wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, wakisusia vikao Aprili 16, kazi kubwa ilikuwa imefanyika."Tayari kamati zote 12 za Bunge hilo zilikuwa zimekamilisha kujadiliSura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Sura hizo zinazungumzia utambulisho wa nchi na muundo wa Muungano.

"Kamati zote zilipiga kura ya kupitisha uamuzi wao kuhusu sura hizo mbili. Kamati kadhaa ziliweza kupata theluthi mbili ya kura kwa wajumbe wa pande zote mbili za Muungano, jambo lililoonesha dalili njema kwamba Katiba mpya inaweza kupatikana," alisisitiza Kikwete.Alisema kazi iliyobaki baada ya taarifa ya kila Kamati kuwasilishwa kwenye Bunge zima, ni Kamati ya Uandishi kukamilisha taarifa yake na kuiwasilisha kwenye Bunge zima kwa ajili ya kujadiliwa.

Alisema ikijadiliwa wajumbe watapiga kura kuamua kuhusu Sura hizo mbili kwa kutumia theluthi mbili ya kura za kila upande wa Muungano.

Kuhusu Ukawa kususia vikao vya Bunge hilo, Rais Kikwete alisema sababu walizotoa zimekuwa zikiongezeka na kubadilika kadri siku zinavyosonga mbele na upepowa kisiasa unavyokwenda.

"Hivi sasa wanazungumzia mambo mawili. Kwanza, kwamba Bunge Maalumu halina mamlaka ya kuifanyia mabadiliko yoyote Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa naTume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa maoni yao, kazi ya Bunge Maalumu la Katiba ni kujadili na kupitisha tu Rasimu ya Katiba ya Tume na siyo kubadili chochote.
Pili, wametoa sharti la wao kurudi bungeni ni kuhakikishiwa kwamba, kitakachojadiliwa bungeni ni Rasimu ya Tume. Bila ya sharti hilokukubaliwa, wamesisitiza kutorudi bungeni," alieleza Kikwete.

Akifafanua suala hilo, Kikwete ambaye alihusika kubuni wazo la kuwa na mchakato wa kuandika Katiba mpya, na katika maandalizi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ya kuongoza na kuendesha mchakato huo, alisema hakuna popote katika vikao vya Baraza la Mawaziri kujadili Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba walipozungumzia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kuwa haiwezi kufanyiwa marekebisho na Bunge Maalumu la Katiba.

Alisema ndio maana suala hilo limewekwa kisheria kwa uwakilishi mpana kupitia ngazi nne muhimu za mchakato wa kutunga Katiba hiyo ikiwamo wananchi kutoa maoni, Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Mabaraza ya Kitaasisi kutoa maoni yao kuhusu Rasimu yakwanza ya Katiba iliyotayarishwa naTume.

Bunge Maalumu na Kura ya Maoni itakayoshirikisha wananchi wote ambao ndio wenye kauli ya mwisho kuhusu Katiba wanayoitaka.

Alisema mamlaka ya kutunga Katiba kwa mila na desturi za mabaraza ya kutunga sheria, ni uwezo wa kurekebisha, kubadili, kufuta na hata kuongeza kilichopendekezwa. Alisema kama ingekuwa kilichokusudiwa ni kubariki tu, kusingekuwa na haja yaneno "kutunga Katiba" wala kura inayohitaji theluthi mbili.

Kikwete alisema anapata shida kuelewa mkanganyiko unatokea wapi kutokana na ukweli kwamba wale wanaoongoza kuhoji mamlakaya Bunge Maalumu, ni wale wale waliotunga Sheria ya Mabadiliko yaKatiba tena hatua kwa hatua.

Alisema siku zote za mjadala kilichokuwa kikijadiliwa ni Sura ya Kwanza na Sura ya Sita hivyo haiingii akilini kudai kuwa kinachojadiliwa bungeni humo si Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba.

Aliwataka Ukawa kuwa wakweli kwaWatanzania na kueleza kabla huenda katika Kamati kumefanyikamarekebisho kwenye Rasimu ambayo hayakuwapendeza kuliko kusema mambo yasiyowakilisha ukweli halisi wa Rasimu inayojadiliwa na kuwafanya watu waamini kinachojadiliwa si rasimu hiyo ya Jaji Warioba na kwamba ni matakwa ya CCM.

Kikwete alisema kama Ukawa hawakuridhishwa na yaliofanyika, walipaswa kutumia mifumo waliyojitengenezea wenyewe kwenye Kanuni kumaliza tofauti zao.

"Kanuni zinaelekeza kuwa mambo wasiyoridhika nayo yajadiliwe kwenye Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Ukiacha mifumo ya maridhiano ndani ya Bunge ukaenda nje kwa wananchi au vyombo vya habari na mitandao si jawabu la tatizo," alisema Kikwete.Aliwasihi Ukawa warejee bungeni na watumie mifumo maalumu ya Bunge iliyowekwa na Kanuni kutafuta maridhiano na wasichoke kuwa na mawasiliano na vyama vingine vya siasa na hasa CCM kutafuta maelewano.

"Mimi niko tayari kusaidia pale watakapoona inafaa kufanya hivyo kama ambavyo nimekuwa nikifanya siku za nyuma," alisema Kikwete.Alisisitiza kuwa ili kupata Katiba mpya inayohitajika, maelewano baina ya wadau wakuu wa kisiasa nijambo lisilokuwa na badala yake. Vinginevyo kupata theluthi mbili kwa pande zote mbili za Muunganohaitawezekana.Alimpongeza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa uamuzi wa kuvikutanisha vyama vinne vikuu vya siasa kujadili suala hilo.

"Ombi langu kwa viongozi wa vyama hivyo ni kuitumia vyema fursa ya majadiliano kuukwamua mchakato kwa maslahi ya nchi yetuna watu wake," alisisitiza Kikwete na kumpongeza Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kwa juhudi za kusaka maridhiano ingawa wajumbe waliosusia vikao hawakushiriki, alimtaka asikate tamaa.Kikwete alisema amesikia madai kwamba hotuba yake ya ufunguzi ndio iliharibu mchakato na kwamba ameikana Rasimu ya Katiba ambayo na yeye ni mmoja wa watu waliotia saini.

Nadhani ndugu zetu wanaotoa madai haya wameitafsiri isivyo, saini yangu katika Gazeti la Serikali lililotangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Alisema katika kutangaza katika Gazeti la Serikali sharti linamtaka anayetangaza ajitambulishe kuwa yeye ni nani na atie saini yake. Kwa kufanya hivyo, hakumfanyi yeye kuwa naye ni mhusika na maudhui ya kila kinachopendekezwa na Tume.Jambo lingine linalofanana na hilo ni yale madai kwamba nilikuwa napata taarifa ya maendeleo ya mchakato ndani ya Tume mara kwamara, iweje leo nitoe maoni tofauti kama niliyoyatoa katika hotuba yangu kwenye Bunge Maalumu.

Ni kweli kabisa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, Makamu wake, Mheshimiwa Jaji Agustino Ramadhani na Mheshimiwa Dk Salim Ahmed Salim wamekutana na mimi kwa nyakati mbalimbali kuzungumzia mwenendo wa mchakato. Lakini, hayakuwa mazungumzo ya kina kuhusu nini kiwe vipi katika maudhui na mapendekezo ya Tume, alieleza Kikwete.

Alisema Rasimu zote mbili nilizipata mara ya kwanza alipokabidhiwa rasmi, tena kwa uwazi na kwamba watu wasijenge dhana kuwa alipewa Rasimu na kuisoma kabla ya kukamilika na hivyo nilitoa maoni yake Tume hii ilikuwa huru na niliiacha iwe hivyo.

Sikuiingilia kwanamna yoyote ile kupenyeza mambo ninayotaka yawemo. Kuthibitisha dhamira yangu ya kutaka Tume iwe huru katika kufanya kazi zao hata pale waliponitaka nitoe maoni niliwaomba tusifanye hivyo ili nisiwakwaze katika kufanya kazi zao, wakapata taabu ya kuwianisha wanayofikiria na mawazo yangu, alisema Kikwete. Kuhusu hotuba yake kuvuruga mchakato, Kikwete alisema madai hayana ukweli wo wote wala msingi kwani hakuna chaajabu alichofanya siku alipohutubiaBunge hilo.

Ukweli ni kwamba nilisema yale yale ambayo Tume yenyewe imeyasema katika Rasimu ya Katiba na Taarifa za Tume.

Niliyoyasema kuhusu malalamiko ya watu wa pande zetu za Muungano na uzuri na changamotoza miundo ya serikali mbili na serikali tatu ni yale yale yaliyomo kwenye taarifa za Tume.

Nimetumia takwimu zile zile za Tume.

Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume, alisema Kikwete.Alisema haoni kosa lake kutoa maoni kuhusu baadhi ya vipengele vya Rasimu hususan uandishi na dhana mbalimbali zilizokuwamo kwa kuwa ilitolewa hadharani ili ijadiliwe.

Lakini, pia mimi ndiye Rais wa nchi yetu, ninayo dhamana ya uongozi na ulezi wa taifa letu. Itakuwaje kwa jambo kubwa la hatma ya nchi yetu nilinyamazie kimya. Watanzania wangeshangaa na wangekuwa na haki ya kuhoji Rais wao ana maoni gani. Bahati nzuri nilitoa maoni yangu mahali penyewe hasa, na kwa uwazi, kwenye Bunge Maalumu la Katiba.Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kuwa namna nilivyotoa maoni yangu sikuwa natoa maagizo wala kushurutisha, ndiyo maana kila wakati niliwakumbusha Wajumbe kuwa mamlaka ya uamuzi ni yao.

Yangu yalikuwa maoni tu wanahiariya kuyakubali au kuyakataa, alisema Kikwete.Kuhusu muundo wa serikali tatu, nilieleza wazi kuwa sina tatizo nao kama ndiyo matakwa ya Watanzania. Lakini, nilieleza hofu yangu kuhusu mapendekezo ya Tume na kuwataka Wajumbe wafanye kazi ya ziada kuondosha udhaifu iwapo wataukubali muundo unaopendekezwa.

Nilieleza nia yangu ya kutaka tuwe na Serikali ya Muungano yenye ukuu unaoonekana, yenye nguvu ya kuweza kusimama yenyewe, inayoweza kuwa tegemeo kwa nchiwashirika, Serikali isiyokuwa tegemezi wala egemezi kwa nchi washirika na ambayo inavyo vyanzo vya uhakika vya mapato.

Hivi kwa kutoa ushauri huo kwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba inageuka kuwa nongwa. Kwakweli sielewi lawama ni ya nini, alibainisha Rais. Alisema anachoamini hastahili lawama bali pongezi kwa kuwa muwazi na kutoaushauri wa msingi ambao utasaidianchi kupata Katiba nzuri inayojali maslahi ya watu wa nchi yetu na yanchi zetu mbili zilizoungana miaka 50 iliyopita.

Rais alitaka mgogoro uliopo sasa katika mchakato wa Katiba usiendelee kwani malalamiko ya wajumbe wa Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi yanaweza kushughulikiwa kwa ukamilifu katika mifumo ya Bunge hilo. Nawasihi waitumie. Hali kadhalika, kwa kupitia mazungumzo wanayofanya na wenzao wa CCM wanaweza kutengeneza nguvu ya pamoja kutatua changamoto za sasa na zitakazojitokeza baadaye.

Kilicho muhimu ni kwa pande zote kuwa na dhamira ya dhati ya kutoka hapa tulipo sasa. Kama utashi wa kisiasa upo kwa kila mmoja wetu, hilo ni jambo linalowezekana kabisa. Narudia kuahidi utayari wangu wa kusaidia kadri inavyowezekana tusonge mbele, alihitimisha Rais Kikwete.

MVIETNAM ADAKWA NA KUCHA NA MENO YA SIMBA

RAIA wa Vietnam, Dong Van (47) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na meno 65 na kucha 447 za simba zote zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 189.

Kamanda wa Polisi Makao Makuu ya Viwanja vya Ndege, Hamisi Seleman alisema Van alikamatwa juzi saa 10 jioni akijiandaa kusafiri kwa ndege ya Shirika la Qatar kwenda Vietnam.

Alisema Polisi ilimkamata raia huyo wa nje mwenye hati ya kusafiria No.B 9306216 iliyotolewaVietnam, akiwa katika eneo la kuondokea abiria.

Baada ya kupekuliwa, inadaiwa alikutwa akiwa amehifadhi nyara hizo kwenye pakiti saba za kahawa na moja ya mchele aina ya 'Pure Basmati'.

Inadaiwa alichanganya na pakiti zingine 15 za vyakula mbalimbali.

"Baada ya kupekuliwa raia huyo alipatikana na meno 65 na kucha 447 za simba akiwa amevihifadhi katika hali ya umaridadi katika begilake la nguo ambapo ndani yake pia kulikutwa suruali mbili," alisema Selemani.

Aidha alisema uchunguzi wa suala hilo unaendelea ukihusisha vyombo mbalimbali vya usalama pamoja na watu kutoka Idara ya Maliasili kubaini mahali alipotoa nyara hizo.

Kulingana na tathmini iliyofanywa, inaonesha simba 21 wameuawa. Kwa mujibu wa Kamanda, mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Kwa sasa wanaendelea na taratibu za kuandaa mashitaka kabla ya kuwasilisha jalada la kesi yake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DPP).

"Tunawaomba Watanzania kuwa makini katika suala zima la ulinzi wa maliasili kwa kuwa sasa inaonekana ujangili haufanyiki kwa tembo peke yake bali hata kwa wanyama wakali kama simba ambao hapo awali hatukuwahi kuusikia," alisisitiza Selemani.

Pi alitaka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kwa pamoja waweze kuzuia uhalifu unaofanywa kupitia maeneo mbalimbali ya mipaka.

WATUHUMIWA ULIPUAJI MABOMU ARUSHA WATAJWA

WATUHUMIWA 19 wa ulipuaji mabomu mkoani Arusha, majina yao yamewekwa hadharani jana na leo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.

Watuhumiwa hao ni pamoja wanaodaiwa kuhusika katika ulipuaji wa bomu katika viwanja vya Soweto, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo (Chadema) uliofanyika Juni 15, 2013.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema askari Polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa watuhumiwa wengine akiwemo mtuhumiwa Yahaya Hella, ambaye anatafutwa sana na polisi akihusishwa na matukio mbalimbali ya ulipuaji mabomu.

Alifafanua kwamba mahojiano kati ya polisi na watuhumiwa hao, ndiyo yaliyotoa mwanga wa kukamatwa kwa watuhumiwa wengine na kuunganishwa katika kesi mbalimbali ambazo tayari zilishapelekwa mahakamani.

Mbali na mashitaka ya kulipua mabomu, Kamanda Sabas alisema watuhumiwa hao leo watakabiliwa pia na mashitaka ya kumwagia watu tindikali na kuhamasisha vitendo vya kigaidi kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Kamanda Sabas, baadhi ya watuhumiwa walishiriki katika tukio zaidi ya moja hali inayoonesha ulikuwa mtandao.

Hata hivyo tofauti na ilivyotarajiwa, Chadema iliposhirikishwa katika kuwapata watuhumiwa, kutokana na madai kwamba ina ushahidi wa aliyetupa bomu katika viwanja vya Soweto, viongozi wa chama hicho walishindwa kutoa ushahidi.

Akizungumza jana katika utaratibu aliojiwekea wa kuzungumza na Taifa kila mwisho wa mwezi, Rais Jakaya Kikwete, alisema watuhumiwa waliokamatwa safari hii, wanaelekea kutoa sura nzuri zaidi ya mtandao wa watu wanaofanya vitendo hivi vya kikatili jijini Arusha na kwingineko nchini. Alipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri ya kukamata watuhumiwa wa mashambulio ya mabomu.

"Kila lilipotokea shambulizi uchunguzi ulifanyika na watuhumiwa kukamatwa. Lakini, watuhumiwa waliokamatwa safari hii wanaelekea kutoa sura nzuri zaidi ya mtandao wa watu wanaofanya vitendo hivi vya kikatili pale Arusha na kwingineko nchini," alisema Rais Kikwete.

Alisema watu 38 wameishafikishwa Mahakamani, wengine watafikishwa mahakamani kesho na uchunguzi na msako unaendelea kote nchini kuwapata watuhumiwa wengine.

Ameomba vyombo hivyo viongeze bidii, maarifa na ushirikiano mpaka wote waliohusika wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Aidha Rais Kikwete alishukuru wananchi waliotoa taarifa zilizowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa.

"Napenda kutumia nafasi hii kuwasihi wananchi wenye taarifa kuhusu wanaotafutwa au yeyote anayejihusisha na vitendo hivi viovu watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama ili hatua zipasazo zichukuliwe," alisema Rais Kikwete.

Tukio la kwanza ni la mlipuko wa bomu uliotokea nyumbani kwa Shekhe Abdulkarim Jonjo, Oktoba 25 mwaka 2012, ambapo watuhumiwa wanne walikamatwa.

Watuhumiwa hao ni Yusuph Huta (30), mkazi wa Ngusero, Kassim Ramadhan (34), mkazi wa Kaloleni na Shekhe wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa na Abdul-Aziz Mohamed (49), ambaye ni mkazi wa Faya ambaye pia alikuwa ni Imamu wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa.

Tukio la pili ni la mlipuko wa bomuuliotokea katika Kanisa Katoliki la St, Joseph Mfanyakazi Olasiti Mei 5 mwaka jana ambapo watuhumiwa 12 wanadaiwa kuhusika.

Watuhumiwa hao ni Huta (30), ambaye anadaiwa kuhusika katika ulipuaji wa bomu nyumbani kwa Shekhe Abdulkarim Jonjo na Ramadhan Waziri (28) ambaye ni mkazi wa Kwa mrombo.

Wengine ni Abdul Humud (30) ambaye ni wakala wa mabasi ya Mohamed Trans ambaye pia aliwahi kufikishwa mahakamani akishitakiwa kuhusika katika ulipuaji wa bomu katika mgahawa wa Vama.

Pia yupo Jafar Lema (38) aliyekuwa Imamu wa Msikiti wa Quba, ambaye pia alifikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na tukio la bomu katika mgahawa wa Vama, Said Ramadhan (34) ambayeni mwendesha bodaboda Standi Kuu Arusha na Kassim Ramadhan (34) ambaye ni dereva wa bodaboda eneo la Friends Corner, Arusha.

Watuhumiwa wengine ni Abashar Omar (24) ambaye ni dereva wa bodaboda Stendi Kuu Arusha, Abdulrahaman Hassan (41), mfanyakazi wa Benki ya Stanbic Arusha na Morris Muzi (44) mkazi wa Kilinzi mkoani Kigoma.

Pia yupo Niganya Niganya (28) mkazi wa Businde Ujiji mkoani Kigoma, Baraka Bilango (40), ambaye ni mkazi wa Kalinzi mkoani Kigoma na Hassan Omar (40) mkazi wa Ilongero mkoani Singida.

Tukio la tatu ni la mlipuko wa bomu Viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa Chadema Juni 15 mwaka jana, ambalo viongozi wa kitaifa wa chama hicho walidai kuwa na ushahidi wa mhusika wa bomu hilo.

Watuhumiwa waliokamatwa na Polisi, baada ya Chadema kukataa kutoa ushirikiano ni Huta (30) mkazi wa Ngusero, ambaye pia anadaiwa kushiriki katika ulipuaji wa bomu nyumbani kwa Shekhe Abdulkarim Jonjo na katika Kanisa la St Joseph Mfanyakazi Olasiti.

Mwingine ni Humud (30) ambaye ni wakala wa mabasi ya Mohamed Trans, ambaye pia aliwahi kufikishwa mahakamani akishitakiwa kuhusika katika ulipuaji wa bomu katika mgahawa wa Vama, na pia anadaiwa kuhusika katika ulipuaji wa bomu katika Kanisa la St, Joseph Mfanyakazi Olasiti.

Wengine ni Jafar Lema (38) mkazi wa Ngulelo, Arusha, Said Temba (42), ambaye ni mfanyabiashara katika Soko la Kilombero, Morogoro ambaye pia alifikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na ulipuaji wa bomu katika mgahawa wa Vama.

Pia yupo Kassim (34) mbaye ni dereva wa bodaboda eneo la Friends Corner na anatuhumiwa pia kuhusika katika ulipuaji wa bomu katika Kanisa Katoliki la St, Joseph Mfanyakazi Olasiti na Ramadhan Omar (24), mkazi wa Arusha.

Wengine ni Hassan (41) ambaye ni mfanyakazi wa Benki ya Stanbic na Muzi (44), Niganya (28) na Bilango (40) wanaotokea Mkoa wa Kigoma na Omar (40) anayetokea Singida, ambao pia wanadaiwa kushiriki ulipuaji bomu katika Kanisa Katoliki la St, Joseph Mfanyakazi Olasiti.

Tukio la nne ni la kumwagiwa tindikali kwa Shekhe Said Makamba, lililotokea katika Msikiti wa Kwamrombo Julai 11/2013. Watuhumiwa wapo wanne ambao ni Huta (30) anayedaiwa kushiriki katika mlipuko wa bomu uliotokea nyumbani kwa Shekhe Abdulkarim Jonjo, mlipuko wa bomu uliotokea katika Kanisa Katoliki la St Joseph Mfanyakazi Olasiti na mlipuko wa bomu katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa Chadema.

Mwingine ni Waziri (28) anayedaiwa pia kushiriki katika ulipuaji wa bomu katika Kanisa Katoliki la St Joseph Mfanyakazi Olasiti.

Mtuhumiwa mwingine ni Kassim (34) mbaye ni dereva wa bodabodaeneo la Friends Corner na anatuhumiwa kuhusika katika ulipuaji wa bomu katika Kanisa Katoliki la St Joseph Mfanyakazi Olasiti na mlipuko wa bomu katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa Chadema na Jafar Lema (38)Tukio la tano ni la kumwagiwa tindikali kwa Shekhe Mustapha Kiago wa Msikiti Mkuu Februari 28 mwaka huu, ambapo watuhiwa wanne wametajwa ambao ni Huta (30), Kassim Ramadhan (34), Jafar Lema (38) na Hassan Mfinanga (57).

Tukio la sita ni la bomu Arusha Night Park lililotokea Aprili 13 mwaka huu, ambapo watuhumiwa wawili ambao ni Jafar Lema (38) naIbrahim Lenard maarufu kwa jina la Shekhe Abuu Ismail (37) mkazi wa mabatini Mwanza watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka.

Katika tukio la sita ni bomu nyumbani kwa Shekhe Sudi Ally Sudi, lililotokea Julai 3 mwaka huu,ambapo watuhumiwa nane watafikishwa mahakamani akiwepo Yahaya Twahir (37) ambaye ni mfanyabiashara mtaa wa Bondeni na Idd Yusuph (23), mkazi wa mtaa wa Jaluo.

Wengine ni Said Temba (42), ambaye ni mfanyabiashara katika Soko la Kilombero, Morogoro ambaye pia alifikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na ulipuaji wa bomu katika mgahawa wa Vama na pia ametajwa katika tukio la bomu Viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa Chadema.

Mwingine ni Anwar Hayael (29) ambaye ni mfanyabiashara, Jafar Lema (38), Hassan Mfinanga (57) ambaye pia ametajwa katika tukio la kumwagiwa tindikali kwa Shekhe Mustapha Kiago wa Msikiti Mkuu.

Wengine ni Yusuph Ramadhan (23) mkazi wa Ngusero na Omar (24) ambaye ametajwa pia katika tukio la mlipuko wa bomu Viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa Chadema.

Kukutwa na mabomu Tukio la nne ni la kupatikana kwa mabomu Julai 21 mwaka huu, ambapo watuhumiwa 10 watafikishwa mahakamani wakiwemo mume na mke.

Watuhumiwa hao ni Huta (30) ambaye anatajwa katika matukio mengi na mkewe Sumaiya Ally (19)wakazi wa Ngusero na Waziri (28) anayedaiwa pia kushiriki katika ulipuaji wa bomu katika Kanisa Katoliki la St Joseph Mfanyakazi Olasiti na kumwagiwa tindikali kwa Shekhe Said Makamba.

Pia yupo Mfinanga (57) na Omar (24), Muzi (44) na Niganya (28) ambao wametajwa katika matukio kadhaa, Kimoro Mchana (25) mkaziwa Itolwa Kondoa, Hassan Omar (40) mkazi wa Mkoa wa Singida na Baraka Ntembo (40) mkazi wa Arusha.

Kosa la tisa ni la kuhamasisha vitendo vya kigaidi kupitia mitandao ya kijamii, ambalo watakaotakiwa kujibu mashitaka yake ni Lenard (37), anayetajwa katika tukio la bomu la Arusha Night Park, Hayel (29) anayetajwa katika tukio la bomu nyumbani kwa Shekhe Sudi na Yasin Shaban (20), mkazi wa Arusha.

Kamanda Sabas alisema operesheni ya kukamata watuhumiwa wengine bado inaendelea nchi nzima, na tayari wanayo majina ya watuhumiwa kadha ambao wametoweka Arusha kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.