NGO YA USHOGA YAFUNGIWA

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imelifutia usajili Shirika la Tanzania Sisi kwa Sisi Foundation (TSSF), kwa tuhuma ya kujihusisha na kuhamasisha ushoga nchini.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wizarani hapo katika gazeti la jana, ilieleza kuwa shirika hilo limefutiwa usajili kuanzia Aprili 4, mwaka huu.

Ilieleza kuwa kufungiwa huko, kunatokana na kukiuka masharti ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 na sheria mbalimbali za nchi.

"Taarifa inatolewa kwa umma kuwashirika la Tanzania Sisi kwa Sisi Foundation (TSSF) lililosajiliwa chiniya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mwaka 2011, limefutiwa usajili kuanzia tarehe 04.04.2014 kutokana na kukiuka masharti ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 na sheria mbalimbali za nchi.

Kwa taarifa hii, utendaji kazi wa shirika hili unasitishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya mwaka 2002 na utendaji kazi wake baada ya taarifahii, utakuwa ni kinyume cha sheria," ilieleza taarifa hizo ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Mmoja wa viongozi wa wizara hiyo, alieleza kuwa shirika hilo limefungiwa kutokana na vitendo vya ushoga, lakini hana taarifa zaidina kutaka watendaji waulizwe.

Baada ya taarifa hiyo, mtu mmoja ambaye namba zake zinaonekana katika mtandao wa kijamii wa shirika hilo, ukielekeza wanaume wanaojihusisha na vitendo vya kishoga kumuandikia taarifa kwa ajili ya semina, alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, kwamba wamefutiwa leseni alisema hawana taarifa.

Akizungumza na gazeti hili, mtu huyo aliyesema ofisi zao ziko Ilala jijini Dar es Salaam, aliyekataa kutaja jina lake, alisema hawajapewa barua ya kusitisha huduma zao, hivyo wataendelea na huduma zao mpaka wapewe taarifa.

Mtu huyo ambaye awali alijitambulisha kwa jina la Dk John, ambaye namba zake zinaonekana katika maelezo ya taasisi hiyo katika mitandao, alisema hana taarifa zozote na yuko nje ya nchi.

Alisema namba hiyo ni kwa ajili ya huduma za wateja. Alisema hajaliona tangazo wala hana taarifa.

Hivi karibuni katika mitandao ya jamii, watu kadhaa walililalamikia shirika hilo, lililosajiliwa na serikali kujihusisha kudai haki, wakidai linahamasisha ushoga nchini. Mtandao wa kijamii wa shirika hilo, una tangazo linalowaalika wanaume wanaojihusisha na vitendo hivyo.

"Je, wewe ni mwanaume unayejihusisha katika mapenzi ya jinsia moja?TSSF inakualika katika semina fupi, itakayofanyika kesho Ijumaa ya tarehe 21 Februari 2014 kuanzia saa 4 asubuhi."

Mada zitakazo ongelewa ni: Magonjwa ya ngono yanayowaathiri kuchu; Namna ya kujilinda na magonjwa hayo, Kujiepusha na magonjwa hayo na tiba. Kwa maelezo ya jinsi ya kuhudhuria tupigie katika 0752648253 au tutumie meseji.


Chanzo: Habari leo

MUSTAKABALI WA UKRAIN KUAMULIWA NDANI YA SAA 48

Waukraine wanaoishi mashariki mwa taifa hilo wanatakriban saa 48 kuamua mustakabal wao la sivyo wakabiliane na vyombo vya usalama vya dola.Waziri wa masuala ya ndani nchin Ukrain Arsen Avakov amewaambia waandishi wa habari mjini Kiev kuwa hali iliyo mashariki mwa nchi itatatuliwa kstika masaa 48 yajayo aidha kwa mazungumzo au kwa kutumia nguvu.

Wanaharakati wanaoiunga mkono Urusi bado wameyateka majengo ya serikali kwenye miji miwili iliyo mashariki mwa Ukrain

Duru zinaarifa kuwa baadhi ya waandamani ambao walikuwa wameteka majengo ya serikali katika mji wa Luhansk wameondoka.

Mapema juma hili utawala nchini Ukrain uliendesha kile ulichokiitakampeni dhidi ya ugaidi ukilenga makundi yaliyotenga.

Ukrain inaishutumu Urusi kwa kuchochea ghasia.

Maafisa wa ngazi za juu kutoka Urusi, Marekani , Ukrain na Jumuiya ya Ulaya wamekubalina kufanya mazunguzmo juma lijalo.

Mazungumzo hayo yanalenga kuleta uwiano baada ya Urusi kuteka eneo la Crimea mwezi February.

Majeshi ya Urusi yangali karibu na mpaka wa Ukraine.

Taharuki imetanda mijini Luhansk, Donetsk na Kharkiv tangu watu wanaounga mkono hatua ya Urusi kuchukua Crimea kudai wanataka Urusi itawale mijihiyo iliyoko mashariki mwa Ukraine.

Serikali ya Kiev tayari imewataja kuwa magaidi na kuwa inapanga operesheni dhidi ya magaidi hao katika kipindi cha siku mbili zijazo.

Bwana Avakov amesema kuwa afua ni mbili mazungumzo ya amani ama vita.

Kiongozi wa waandamani mjini Luhansk amemuomba rais wa Urusi Vladimir Putin kuwasaidia wasidhulumiwe na Kiev.

Wakati huohuo serikali ya Kiev imetangaza kuwa imewaachia watu 56 waliokuwa wamekamatwa kwa kuvamia majengo ya Umma.

Huko Kharkiv viongozi wa maandamano wamelaumu serikali ya Kiev kwa matatizo mengi yanayowakumba na wakaitisha kura ya maoni ya kuamua iwapo wangependa kusalia Ukraine ama kujiunga na Urusi.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa kiev imetwaa majengo yaliyokuwa yametekwa na waandamanji ingawaji hali ingali tata katika mji ulioko karibu wa Donetsk.

KENYA YAWARUDISHA WASOMALI KWAO

Serikali ya Kenya imewarudisha nyumbani Wasomali 82 waliokuwa miongoni mwa wageni3000 walioshikwa katika msako mkubwa unaoendelea mjini Nairobi kukabiliana na tishio la ugaidi.

Mwandishi wa BBC mjini Nairobi, Paul Nabiswa, ambaye yuko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ameshuhudia zaidi ya Wasomali 82 wakiingizwa katika ndege moja ambayo imekodishwa maalum kwa shughuli hiyo.

Balozi wa Somalia nchini Kenya , Mohammed Nur amesema kuwa ndege hiyo imekodishwa na serikali ya Somalia baada ya watu hao kuamua kwa hiari yao wenyewe kurejea nyumbani baada ya kukamatwa katika msako unaoendelea mjini Nairobi wakiwa hawana vibali rasmi ya kuishi nchini Kenya.

Balozi huyo anasisitiza kuwa wasomali wengi wakimbizi walionaswa wakiwa na stakabadhi rasmi za Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR wataregeshwa katika kambi za wakimbizi baada ya uchunguzi wa serikali ya Kenya.

Msako huu unaoendelea sasa mjini Nairobi ulianza ijumaa iliyopita baada ya kutokea milipuko ya grenadi mtaani Eastleigh.

Watu sita waliuawa katika matukio hayo ya mwisho yaliyoibua hasira miongoni mwa wakenya na kuchochea serikali kuanzisha msako huu.

Kufikia jana Polisi ya Kenya ilidhibitisha kuwa imewanasa wahamiaji 3,000 na kuwaachilia huku ikiwa imesalia na wahamiaji 447.

AMTUPA MWANAE ILI ALIWE NA FISI

JESHI la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mkazi mmoja wa kijijicha Songambele wilayani Maswa mkoani hapa, kwa tuhuma za kutaka kumuua mtoto wake kwa kumtupa na kumtelekeza nje ya nyumba ili aliwe na fisi.

Kamanda wa polisi mkoani Simiyu, Charles Mkumbo alisema ofisini kwake mjini hapa jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nane za usiku wakati mtuhumiwa Baya Seni (30) akiwa amelala na familia yake kijijini hapo, ndipo alipokurupuka ndani akampiga mtoto wake Amos Baya (3) na kisha kumtupa na kumtelekeza njeya nyumba.

Alisema, Seni katika maelezo yake kituo cha polisi alisema alifikia uamuzi huo kwa kuwa hakuona thamani ya mtoto wa kiume kwenye familia yake kwani uzoefu umeonesha kuwa watoto wa kiumewakikua hudai kupata mirathi kutoka kwa wazazi wao.

Alisema kinyume chake watoto wa jinsia ya kike wakikua watamuongezea utajiri wa mifugo atakapolipwa mahari ili waolewe na baada ya kuolewa hawawi mzigotena kwenye familia yake bali mzigo huo huhamia kwenye familia atakayoolewa. Mtoto huyo aliokolewa na majirani baada ya kusikia kilio.

Mama wa mtoto huyo Elizabeth Paulo alisema, mume wake alikuwa akimtesa sana mtoto wake akimbagua kwa vile yeye ni wa jinsia ya kiume na kwamba hana faida kwake.

JK AKUBALI KUONGEZA MUDA WA BUNGE LA KATIBA

RAIS Jakaya Kikwete amekubali kuongeza muda wa Bunge Maalumula Katiba katika mazungumzo aliyofanya na mwenyekiti wake, Samuel Sitta.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti huyo wakati akijibu swali la waandishi wa habari katika mkutanowake jana, Dar es Salaam, baada ya kumaliza mkutano wake na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu.

Ziara hiyo ambayo amesema ni utaratibu aliouanza kukutana na viongozi wa dini, pia ilimkutanisha na Mufti wa Baraza la WaislamU Tanzania (BAKWATA), Shekhe Issa Bin Shaaban Simba. Sitta alikutana na Rais Kikwete juzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Sitta, Rais Kikwete hajataja ni lini Bunge hilo litaanza tena kwa nyongeza ya siku 20 kwa mujibu wa sheria, baada ya siku 70 zinazomalizika mwezi huu, kuisha ili kufanya jumlaya siku 90. Lakini amesema uongoziwa Bunge umekusudia lianze tena Agosti mwaka huu.

Alisema lengo la kukutana na viongozi hao wa kidini ni kuwaeleza kinachoendelea Dodoma, kwa kile alichodai viongozi hao wana ushawishi na wafuasi wengi nyuma yao, hivyo si busara kusikia mitaani.

Katika mkutano huo Sitta alikanusha habari ya gazeti moja lililodai anakwenda kuwaangukia viongozi hao na kusema hana dhambi za kufanya hivyo.

"Leo (jana) nimepanga kukutana na viongozi wa dini zetu na si hawa tu nitakaokutana nao, nitaendelea na utaratibu huu kwa viongozi wengi hata wenye wafuasi wachache, hawawana ushawishi japo hawahusiki sana na siasa lakini ni viongozi wa jamii, wanapaswa kupata taarifa sahihi ya nini kinachoendelea Dodoma," alisema Sitta.

Alisema katika mazungumzo yake na Kardinali Pengo jana asubuhi, amemweleza kwa kifupi mchakato unavyoendelea Dodoma na yeye (Pengo) alimhakikishia kuwa Kanisa Katoliki linaliombea Bunge Maalumu la Katiba na wajumbe wote ili lengo lifikiwe na Watanzania wapate Katiba mpya na yenye ubora.

Baada ya kutoa maelezo hayo mafupi ya mkutano wake na Pengo, Sitta akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa Bunge hilo, ikiwemo kama muda watakribani wiki tatu uliobaki unatoshakumaliza kazi iliyo mbele yao, alisema muda huo hautoshi.

"Ni dhahiri mpaka Aprili 28 tutakuwa hatujamaliza Bunge, itabidi tupishe Bunge la Bajeti la Muungano, Wawakilishi watarejea Zanzibar na sisi wengine tutabaki Dodoma, bajeti itafanyika si chini yamiezi miwili, yaani Mei na Juni," alisema na kuongeza: "Jana nilionana na Rais Jakaya Kikwete nikamweleza hali halisi ilivyo, kimsingi alikubali ataongeza muda ingawa hatukufikia kutaja ni lini. Ila sisi tunakusudia tuanze tena Agosti, nimemweleza kwa undani maana hata baadhi ya nchi nyingi zimechukua muda kuandika Katiba, akaona ukweli huu akatuongezea".

Sitta alisema Bunge litatangaza rasmi utaratibu huo utakapo kamilika ila alisisitiza kuwa, kwa hali inavyoendelea hawawezi kuendelea kubaki Dodoma kwa ajili ya Katiba kwa kuwa kisheria siku zitakwisha na pia mwingiliano wa sikukuu za Pasaka na Muungano Aprili 26, zitapunguza siku.


Muundo wa Muungano:

Awali, akizungumzia kuhusu muundo wa muungano hasa baada ya kuibuka kwa madai ya kutaka Hati ya Muungano wakati wa mjadala wa sura ya kwanza ya sita ya Rasimu ya Katiba uliofanyika katika kamati, Sitta aliwataka wabunge kutopoteza muda kujadili serikali ngapi ziwepo.

Aidha, Sitta amesema ipo hatari ya kupoteza muda mwingi kuzungumzia muundo wa serikali uweje, jambo analoona kwa baadhi ya watu, wanataka serikali nyingi kwa uchu wa madaraka wakijua wakikosa uongozi upande mmoja, watapata upande mwingine.

Alisema ingawa suala la serikali ni muhimu kwa kuwa ndio linalotoa dira, ila haja kubwa ipo katika kuipitia rasimu Ibara kwa Ibara kama alivyoagiza Rais Kikwete.

Alitolea mfano suala la uadilifu na kushauri wajumbe wakipitia vizuri, watashauri mfumo gani uwekwe kuwabana zaidi viongozi.

"Kiongozi anapaswa ajue anaingia katika utumishi wa umma si kuchota fedha na kufanya ufisadi bali suala kubwa ni maendeleo ya nchi, ustawi wa wafanyakazi, wakulima na vijana, kuhakikisha sheria zinakuwepo kuzuia mikataba mibovu, kwa mfano Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) inavyopandisha umeme, wananchi wanaumia."

"Tukiingia katika sura nyingine za rasimu, Katiba lazima ibane tutungesheria zilizo wazi, angalia suala la Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, tunajaza fomu kisha zinakuwa siri, sasa zina haja gani, ni za nini, si bora tuache, maana naweza kujaza nina kijumba kibovu kimoja, kumbe nina majumba," alitoa mfano Sitta.

Alisema, "Ili kuzuia viongozi kujitajirisha, ni lazima sheria ziwe kali la sivyo wizi utaendelea, sheria inapaswa kuwakwamisha wanaopenda madaraka…., maombi yangu kuhusu mchakato, pamoja na purukushani, kutaka kuonekana, vijana machachari, lakini wengi wanataka Katiba mpya ipatikane."

Sitta akifafanua kuhusu ama serikali tatu ama mbili, alinukuu alichowahi kusema mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale- Mwiru kuhusu suala hilo kwamba ni kama wanaotaka serikali tatu wanataka madaraka, kwamba akikosa uongozi katika upande mmoja, apate kwingine.


Hati ya Muungano;

Sitta aliwaambia waandishi wa habari kumekuwepo na madai ya hati ya Muungano katika kamati na kwamba, ni ajabu kuona ndoa iliyodumu kwa miaka mingi, wahusika sasa wamekuwa vikongwe, anatokea mtu anadai cheti cha ndoa.

"Ni kama haamini kwamba hiyo ndoa ilifungwa ama! Ni ajabu kweli, vielelezo ni pamoja na Sheria ya Bunge ya Aprili 5 mwaka 1964, Msekwa akiwa Katibu wakati huo alikwenda katika kamati kueleza yaliyotokea wakati ule, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amekwenda kueleza." "Ndoa watu wamefunga miaka, wamekuwa vikongwe, wajukuu leo wanadai cheti cha ndoa, ni upuuzi, mtu anayehitaji utafiti aendelee, hakuna anayemzuia ila haituzuii sisi kuendelea," alieleza Sitta.


Ripoti za Kamati;

Kwa mujibu wa Sitta, Alhamisi na Ijumaa wiki hii, taarifa za kamati zitatolewa bungeni na maoni ya wengi na ya wachache yataelezwa ilikuruhusu mjadala kuanza ndani ya ukumbi na kwamba katika sura ya kwanza hadi ya sita, kila mjumbe atachangia."

Baada ya hapo kazi itakuwa nyepesi, siwezi kutabiri kitakachotokea lakini hoja yenye maana itashinda, ukiacha wachache wenye utamaduni wa fujo, wengi wanataka ifike mahali tupate Katiba mpya, tusichezee mabilioni ya Watanzania bure.


Uzoefu wa Kenya;

Sitta alitumia nafasi hiyo kutolea uzoefu wa nchi jirani ya Kenya mwaka 2007 walipoingia katika machafuko ya kisiasa baada ya kushindwa kufanya mabadiliko katika Katiba yao na kufanya uchaguzi.

Alisema kazi inayofanyika Dodoma ni kubwa hivyo inapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa vile vile. Akiwa na Mufti Mkuu Akizungumza mara baada ya kukutana na Mufti wa Tanzania, Shekhe Issa Bin Shaaban Simba, Sitta alisema ujumbe wake ulipokewa vizuri katika Ofisi za Bakwata, Dar es Salaam na kwamba Mufti alishukuru hatua hiyo ya Waislamu kushirikishwa.

"Ukweli Mufti amefurahia huu ujio wangu hapa na kuueleza kuwa anafuatilia kwa makini kile kinachoendelea kwa sasa kule Dodoma na zaidi ameuombea mchakato huu uweze kuisha kwa amani na utulivu hadi katiba mpya itakapopatikana" "Zaidi ametutaka wajumbe wote kuvumiliana na kufanya kazi yetu tukitanguliza maslahi ya Taifa na kuachana na misuguano ili hatimaye katiba iweze kupatikana," alisema Sitta.


Chanzo: Habari leo

JELA MIAKA NANE KWA KUJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Mahakama moja nchini Misri imewahukumu watu wanne kifungo cha hadi miaka minane jela kwa kosa la vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Watu hao wanashutumiwa kuhudhuria au kupanga tafrija za vitendo vya ngono, na kuvaa mavazi ya kike na kujipodoa.

Sheria ya Misri haitamki kupiga marufu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, lakini waendesha mashitaka wametumia sheria ya Misri inayokataza mambo fulani kufanyika hadharani kuwahukumu wapenzi wa jinsia moja.

Hukumu hiyo imeshutumiwa na wanaharakati wa haki za binadamu.

Mmoja wa watu hao amehukumiwa na mahakama mjini Cairo, kifungo cha miaka mitatu jela na kazi ngumu.

Kikundi cha kutetea haki za binadamu chenye makao yake nchini Marekani, Human Rights First , kimesema hukumu hizo zinasikitisha na kukatisha tamaa.

"Misri ni taifa linalobadilika katika eneo la nchi za Kiarabu; kinachotokea Misri kinaweka hali ya kuenea katika ulimwengu wote wa nchi za Kiarabu," kimesema kikundi hicho katika taarifa yake.

Kikundi hicho kimesema tangu kung'olewa madarakani Rais Mohammed Morsi mwezi Julai 2013 kumekuwa na ongezeko la watu kukamatwa kwa misingi ya jinsia zao.

Hukumu ya sasa inakumbushia kesi ya mwaka 2001 ya watu 52 kushutumiwa kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na makosa mengine chini ya sheria ya Misri.

Watu ishirini na watatu walihukumiwa kifungo cha kufikia miaka mitano jela pamoja na kazingumu, hukumu ambayo ilishutumiwa kimataifa.

Kikundi kimoja cha kutetea haki za binadamu nchini Misri kimesema adhabu kali zilizotolewa kwa watu hao Jumatatu ni sehemu ya msako unaoendelea dhidi ya uhuru binafsi.

CHADEMA KATAVI WABARIKI KUNG'OREWA MWENYEKITI

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chadema mkoani Katavi wameridhia kwa kauli moja na kubariki uamuzi wa kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama hicho, John Malack na viongozi wengine watatu waandamizi wa chama hicho, Jimbola Mpanda Mjini.

Viongozi hao watatu ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Mpanda Mjini, Seif Sipia, Katibu wa jimbo hilo, Joseph Mona ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Said Arfi.

Katika orodha hiyo yupo pia KatibuMwenezi wa chama hicho, Godfrey Maufi ambaye ameshavuliwa uanachama wa chama hicho akidaiwa kuiba nyaraka za siri za chama hicho na kuzisoma katika mkutano wa hadhara.

Pia mkutano huo umependekeza kuvuliwa uanachama wa chama hicho watu kadhaa akiwemo Iddi Nziguye ambaye ni Diwani kwa tiketi ya chama hicho Kata ya Makanyagio na Diwani wa Kata ya Kashaulili, John Matongo.

Uamuzi huo ulifikiwa juzi na wajumbe wa mkutano huo mkuu wa chama hicho uliofanyika mjini hapa ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema wa Kandaya Magharibi, Masanja Mussa Katambi.

Februari 22 mwaka huu kikao cha mashauriano cha chama hicho ngazi ya mkoa kiliwasimamisha viongozi hao, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa, Malack akituhumiwa kufungua na kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Februari 2, mwaka huu ambao unadaiwa uliwakashifu viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa.

RWANDA YAKUMBUKA MAUWAJI YA KIMBARI

Rwanda inaadhimisha miaka 20 tangu kutokea mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Watu laki nane waliuawa wengi wakiwa wa kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri. Wote waliuawa na watutsi wenye msimamo mkali.

Hii leo Rais Paul Kagame anatarajiwa kuwasha mwenge ambao utasalia hivyo kwa siku 100 ,kipindi ambacho mauaji ya kimbare yalifanyika.

Mgogoro wa kidiplomasia umesababisha Waziri wa sheria wa Ufaransa, kujiondoa katika shughuli za kumbukumbu ingawa Ufaransa inasema kuwa balozi wake ataiwakilisha nchi hiyo.

Wengi wa waathiriwa wa mauaji ya Rwanda, walishambuliwa kwa mapanga kwa siku 100. Mauaji hayo yalianza Aprili mwaka 1994, punde baada ya kufariki kwa hayati Rais Juvenal Habyarimana.

Mauaji ya kimbari Rwanda

¤6 Aprili: 1994: Rais Habyarimana afariki katika ajali ya ndege

¤7 Aprili: Wanajeshi wa Rwanda pamoja na waasi wawaua wananchi

¤8 Aprili:Kundi la waasi la (RPF) laanza kupambana

¤11 Aprili: Maelfu wauawa

¤17 Mei: Baraza la usalama la umoja wa mataifa lasema mauaji ya kimbari yametokea

¤22 Mei: RPF yadhibiti uwanja wa ndege wa Rwanda

¤22 Juni: Mauaji ya watutsi yaendelea licha ya kuwepo wanajeshi wa Ufaransa nchini humo

¤4 Julai: RPF yadhibiti KigaliAlifariki wakati ndege yake iliposhambuliwa katika anga ya Kigali na kudunguliwa.

Baadhi ya viongozi wa kidini walihusishwa na ghasia zilizofuata kifo cha Habyarmana.

Mauaji ya kimbari yaliisha mwezi Julai 1994 wakati chama cha RPF, kilichokuwa cha waasi wa Tutsi wakati huo, kilipoingia nchini humo kutoka Uganda na kuchukua uongozi wa nchi hiyo.

Kumbukumbu zinaanza kwa kuwekwa mauwa katika eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo na kufuatiwa na kuwashwa kwa mwenge katika uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali.

Mwenge huo umekuwa ukitembezwa katika nchi hiyo kwa miezi mitatu iliyopita

Viongozi wa kimataifa akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, aliyekuwa Raiswa Afrika Kusini Thabo Mbeki na katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

Mnamo Jumapili mamia ya watu walihudhuria maombi kuwakumbuka maelfu waliouawa .

TANZANIA YASHINDA KOMBE LA DUNIA KWA WATOTO WA MITAANI

Timu ya Taifa Ya Tanzania kwa Watoto wa Mitaani hatimaye Yanyakua Kombe la Dunia Kwa Watoto wa Mitaani, (Street Child World Cup 2014) Rio de Janeiro, Brazil Ikitinga fainali za Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani kwa mara yapili mfululizo, hatimaye Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro.

Tanzania leo imeweza kuchachanya Burundi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kulinyakua Kombe hili kwa Kuinyuka magoli 3 kwa moja huku mchezaji kiungo mshambuliajiwa Tanzania Frank William akipiga magoli matatu na kuwa nyota wa mchezo, Tanzania iliweza kufunga magoli mawili kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuongeza goli latatu kipindi cha pili. Burundi iliweza kufunga goli lake la pekee zikiwa zimebaki daika nne mpira kuisha.

Tanzania imeweza kufika fainali baadaya kuonyesha kiwango cha juuhata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino na Argentina.

Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipabowa wa michuano hii ya kombe la dunia. Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za michuano hii Kule Durban Afrika Kusini Tanzania ilifikafainali na kufungwa na India.

Timu ya Tanzania itaondoka Brazil kesho Jioni ikipitia Dubai na kuwasili Dar es salaam siku ya tarehe 10 kwa Shirika la Ndege la Emirates.

WAASI WAKUBALI MAFUTA KUUZWA

Makubaliano yameafikiwa kuondoa kizuizi cha kusafirisha mafuta mashariki mwa Libya.

Mauzo ya mafuta katika nchi za ng'ambo nchini humo yaliathirika pakubwa katika kipindi cha miezi minane iliyopita baada ya kufungwa kwa bandari zilizo katika eneo la mashariki linalotawaliwa na makundi ya wanamgambo.

Katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyiwa katika jiji la Beghazi, Waziri wa Maswala ya Haki wa Libya, Salah Al-Maghani, alithibitisha kuondolewa kwa muda kwa vizuizi vya kuuza mafuta.

Vituo vya mafuta vya Hureiga na Zuetina vilivyo na uwezo wa kuzalisha mafuta mapipa 200,000kwa siku hivi sasa vimesimamiwa na Serikali.

Vituo viwili vilivyo vikubwa zaidi nchini humo vya Mashariki mwa nchi vya Ras Lanuf na Sidra vitafunguliwa kwa muda wa majuma machache yajayo, kulingana na Waziri.

Mapatano yaliafikiwa kati ya makundi ya wapiganaji yaliyosababisha kufungwa kwa vituo hivyo na kundi ambalo Serikali ililitaja kama"wapatanishi".

Msemaji wa Waziri Mkuu ameambia BBC kuwa Serikali imekubali kuwalipa mishahara walinzi wa vituo hivyo vya mafuta.

Juhudi za mwezi uliopita za kufikia mapatano ya kuanza kuuza mafuta tena katika vituo hivyo hazikufaulu.

Wale wanaozuia mafuta kuuzwa katika vituo hivyo wamekuwa wakilalamika kuwa sekta ya mafuta nchini Libya inakabiliwa na ufisadi mkubwa, lawama ambayo imekanushwa na maafisawa Serikali.

Wapiganaji hao pia wamekuwa wakisema kuwa wakaazi wa Mashariki wanahitaji mapato makubwa zaidi kutoka kwa mauzo ya mafuta. Waziri wa Haki sasa anasema kuwa Serikali itachunguza lawama za ufisadi.

Libya imepata hasara ya zaidi ya Dola Bilioni tisa tangu kufungwa kwa vituo hivyo vya mafuta. Eneola Mashariki ndilo linalozalisha kiwango kikubwa cha mafuta.

SIR ALEX FERGUSON ATUA HARVARD UNIVERSITY KUFUNDISHA

Kocha aliyestaafu Manchester United, Sir Alex Ferguson amejiunga na Chuo Kikuu cha Harvard ambako alikoingia mkataba wa kufundisha kwa muda mrefu.

Ferguson (72) ataanza kazi yake hiyo mpya mapema mwezi ujao katika programu mpya chuoni hapo inayohusu Biashara, Burudani, Vyombo vya Habari na Michezo katika moja ya vyuo vinavyoheshimika zaidi duniani.

Fergie ndiye kocha aliyepata mafanikio makubwa zaidi nchini Uingereza na alifikia makubaliano ya kazi hiyo nchini Marekani, na anatarajiwa kurejea huko mwezi ujao kwa ajili ya kutoa mhadhara kwa maofisa watendaji waandamizi kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Mskochi huyo ameona ni bora kuchukua kazi hiyo badala ya kuendelea kuketi kwenye jukwaa la watu maarufu au viongozi kutazamatimu yake aliyomwachia David Moyes inavyofanya kazi. Alikaa Old Trafford kwa miaka 26 yenye mafanikio makubwa.

"Nimefurahishwa sana kupata fursa kama hii ya kuchangia nilicho nachokatika chuo chenye sifa kubwa miongoni mwa wasomi duniani. Muda niliokaa hapa tayari umenichochea uzoefu wangu na natumaini kuendeleza uhusiano mzuri katika shughuli za wanafunzi, vitivo na marafiki katika chuo hiki," akasema Fergie akiwa Marekani.

Ferguson aliwawezesha Man U kutwaa jumla ya vikombe 38, kati ya hivyo 13 vikiwa ni vya ubingwa wa ligi kuu, viwili vya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia kuna vinginevya mashindano tofauti ndani na nje ya nchi. Kwa sasa ni balozi na mmoja wa wakurugenzi wa klabu hiyo.

Profesa wa Harvard, Anita Elberse amesema wamefurahishwa na Fergie kukubali kuchukua jukumu hilo jipya na kwamba wanasubiri kwa hamu ili aianze rasmi kazi yakehiyo, ambapo watapata uzoefu wake kwenye uongozi.


Chanzo: Tanzania sports

DENI LA TAIFA LAZIDI KUPAA

Mtandao wa Madenina Maendeleo Tanzania (TCDD), umebaini ongezeko la madeni ya ndani, ambayo sasa yamefikia Sh6.8 trilioni na kusababisha athari kubwa kwa jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa TCDD, Hebron Mwakagenda alisema hayo wakati akitoa taarifa za matokeo ya utafiti wa usimamizi wa deni la ndani.

Alisema deni hilo limeongezeka kutoka Sh811 bilioni mwaka 2002 hadi kufikia Sh6.8 trilioni Desemba mwaka 2013.

Alisema ingawa deni hilo ni dogo ikilinganishwa na deni la nje, lakini madhara yake ni makubwa kwa jamii ya Watanzania. Deni la nje kwa mujibu wa utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 2012-13, limefikia Sh20.2 trilioni na kwamba jumla ya deni la taifa ni Sh27 trilioni.

"Malipo ya riba kwa madeni ya ndani yamegharimu sehemu kubwaya rasilimali za Serikali katika kuyalipa ikilinganishwa na madeni ya nje," alisema.

Mwakagenda alisema asilimia 73 ya deni la ndani inatokana na benki ambazo zinatoza riba kubwa na kwamba dhamana za Serikali zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa.

Alisema hicho ni kiashiria kwamba, gharama za madeni ya ndani ni kubwa kuliko madeni ya nje ambayo yana masharti nafuu.

"Ukiangalia unaona wazi kuwa hali hiyo ni ongezeko la madeni ya ndani kwa kiasi kikubwa. Deni linaongezeka kila mwaka," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema Serikali inatumia fedha nyingi kulipa riba zamadeni ya ndani na kusababisha kuzorota kwa huduma za jamii.

"Unaweza kuona kwamba, Serikali inatumia pesa nyingi kama riba kulipa madeni yake ya ndani," alifafanua.

Alipendekeza Serikali kuondoa misamaha ya kodi ili fedha zinazokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ziweze kutumika katika uendeshaji wa Serikali.

Taasisi hiyo ilipendekeza Serikali kuomba kibali cha Bunge kila inapotaka kukopa ili sababu za kufanya hivyo ziweze kujulikana na kusimamia utekelezaji wa fedha zinazokopwa.

Pia ilipendekeza madeni ya Serikali na taasisi zake yawekwe wazi ili vyombo vya usimamizi vipate fursaya kuyafuatilia kwa ukaribu ili kubaini maendeleo na matokeo ya madeni hayo.

MSEKWA ALONGA, ASEMA SITTA ANA LAKE JAMBO

Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta kukiri kuchezewa kwa saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Msekwa amesema, 'mzungumzaji huyo ana lake jambo'.

Sitta akizungumza na gazeti hili juzimjini Dodoma alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa,Aprili 25, 1964, yameongezwa.

Alifafanua kuwa saini ya Nyerere imeongezwa herufi 'us' kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno 'Msekwa' kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.

Msekwa akizungumza na gazeti hili jana alisema: "Saini iliyo katika hati original (halisi) ni ya kwangu mimi, lakini huyo anayesema zimechezewa muulizeni atakuwa nalake jambo. Kama kompyuta imekosea ni leo kwa kuwa kipindi hicho kompyuta hazikuwapo."Aliongeza:

"Ana lengo gani la kutiliashaka, ana lengo gani la kusema imechakachuliwa, kinachotakiwa ni hati original ambayo iko ofisi ya Katibu wa Bunge itolewe, kwanini tuendelee kuandikia mate wakati wino upo?"


Maoni mengine

Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Taarifa kwa Wananchi Umma (TCIB), Hebron Mwakagenda alisema yote hayo yanatokea ni kuvuruga hoja iliyopo mezani.

Alisema kitendo cha kupoteza muda kuzungumzia suala la kuchezewa kwa saini halitakiwi kwani kama maudhui yake hayakuchezewa basi hoja ya muundo wa Muungano uamuliwe na wananchi wenyewe.

"Tusianze kupoteza muda kwa mambo ambayo hayapo cha msingi wananchi wenyewe waulizwe wanaupenda Muungano au la lakini tusianze kumtafuta mchawi kuwa saini zimechezewa wananchi waamue wenyewe kuhusu Muungano," alisema Mwakagenda.


Sakata lilivyoanza

Utata huo ulianza wiki hii baada ya kamati za Bunge Maalumu la Katibakuanza vikao vyake vya kujadili suraya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba, zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wake.

Hali hiyo ilitokana na kutopatikana kwa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ile ya Sheria ya Baraza la Mapinduzi ya kuridhia Mkataba wa Muungano.

Aprili 2 mwaka huu, Kamati namba 2 ilimwalika, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Pius Msekwa kutoa ufafanuzi kuhusu hati hizo, lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali. Msekwa aliitwakutokana na kwamba ndiye aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati huo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Shamsi Vuai Nahodha, alithibitisha kutokea utata huo na kwamba walilazimika kumuita Msekwa ili kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa na Msekwa alisema saini zilizopo katika hati hiyo ni ya kwake.

Nahodha alisema kwa maelezo ya Msekwa, inaonekana hati ya Muungano ipo Umoja wa Mataifa (UN), kwani kabla ya Muungano, Tanganyika ilikuwa na kiti chake UNna Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hali kadhalika.

Aliongeza kuwa baada ya UN kuomba uthibitisho wa Muungano, ndipo walipelekewa hati hiyo na kwamba haijawahi kurejeshwa.

Kwa upande wake Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Hamis Hamad alisema hati hiyo ipo Dar es Salaamn a ni moja tu, hivyo siyo rahisi kuipeleka bungeni Dodoma.


Chanzo: Mwananchi

BERANIHO ASEMA HANA BIFU NA MTU, RAMSEY AREJEA DIMBANI BENTEKE NJE MIEZI SITA

Raia wa Burundi, Saido Beraniho anayekipiga West Bromwich Albion amesema hana bifu na wachezaji wenzake waliomzonga na hata kufikia kupigwa baada ya kusababisha kufungwa bao la kusawazisha na Cardiff hivi karibuni.

Beraniho (20) ambaye emepewa pia uraia wa England amesema kwamba hana nia ya kufungua mashitaka dhidi ya mchezaji mwenzake, James Morison aliyempiga na kwamba wawili hao walikutana, kuzungumza kidugu na kumaliza mambo.

Kocha Pepe Mel amesema anaamini kwamba kinda huyo atakuwa na msaada mkubwa katika mikakati ya klabu hiyo kuinusuru timu kushuka daraja msimu huu. West Brom walikuwa wakiongoza hadi dakika za majeruhi ambapo Beraniho alipokonywa mpira na kuzaa bao la Cardiff Jumamosi iliyopita.

Baada ya mechi hiyo lilizuka zogo kubwa hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo ambapo wachezaji kadhaa walimvaa Beraniho kwa madai kwamba alicheza kizembe. Hata hivyo, Beraniho ndiye aliifungia timu bao muhimu la ushindi dhidi ya Manchester United na pia bao muhimu dhidi ya Arsenal.

Beraniho alikuwa na uamuzi wa kufuatilia suala hilo kisheria ili apate haki yake na Morrison aadhibiwe kwa ngumi aliyomtwanga.

"Beraniho atakuwa muhimu sana kwetu katika mechi saba zinazokuja," akasema Mel na kuongeza kwamba hakuna hatua zozote za kinidhamu zilzochukuliwa kuhusiana na tukio hilo.

Msemaji wa klabu alisema kutokea zogo kama hilo ni kawaida baada ya mechi kwa klabu nyingi, na kwambahiyo inaonesha kwamba wachezaji wanajali na wasingependa kuona wanapoteza mechi.

"Wachezaji walimalizana wenyewe kama walivyolianzisha na sasa mambo yanaendelea vyema na kwa Beraniho na Morrison ni kana kwamba ni ndugu wa familia moja.

Nimezungumza na Beraniho na anaonesha kujali kuliko watu wengine wa umri wake mdogo.
Nimemweleza kwamba namwamini na kumtegemea kwa mafanikio ya timu yetu," akasema kocha huyo.


AARON RAMSEY AREJEA DIMBANI

Kiungo Aaron Ramsey aliyewabeba Arsenal tangu mwanzo wa msimu hadi alipoumia Desemba 26 mwakajana, anarejea uwanjani.

Ramsey (23) ni moja ya sababu za Arsenal kupanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi, lakini mambo yalibadilika tangu kuumia kwake na wenzake wakiwamo Theo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain ambapo timu ilianza kuporomoka.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema nyota huyo ambaye msimu huu ameshafunga mabao 13 licha ya kuwa nje kwa mechi nyingi, atakuwa kwenye kikosi kinachosafiri kukabiliana na Everton kwenye dimba la Goodison Park Jumapili hii.

Mchezaji huyu wa Timu ya Taifa ya Wales alikuwa anasumbuliwa na nyonga, na aliumia wakati timu yake ikipata ushindi wa 3-1 dhidi yaWest Ham. Wenger amesema kuwa na mtu kama Ramsey anayeweza kuisaidia timu ni muhimu sana.

Arsenal sasa wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 64 huku Everton wakiwafuatia kwa pointi 60 na bado wana mchezo mmoja mkononi. Liverpool wanaongoza ligikwa pointi 71, Chelsea wana pointi 69 na Manchester City wanazo 67 na michezo miwili mkononi.

Nafasi ya sita inashikwa na Tottenham Hotspur ambao kama Everton wanagombea kuwapokonya Arsenal nafasi ya nne ili kuwa moja ya timu nne zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Spur wana pointi 56 hivyo bado wapo mbali.


BENTEKE NJE MIEZI SITA

Wakati Ramsey akirejea, Aston Villa wamepata pigo kubwa baada ya mpachika mabao wao, Christian Benteke kuumia mazoezini na imeelezwa kwamba hatacheza kwa miezi sita ijayo.

Benteke (23) aliumia kwenye mazoezi ya timu hiyo, na inamaanisha pia kwamba hataweza kuiwakilisha nchi yake ya Ubelgiji kwenye michuano ya Kombe la Dunia Brazil inayoanza Juni 12 mwaka huu.

Kocha wa Villa, Paul Lambert alisema habari hizo ni za kusikitisha sana kwa Benteke mwenyewe na klabu kwa sababu alihitaji na kuhitajiwa kucheza wakati huu kuliko mwingine wowote.

Benteke aliyezaliwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kabla ya kupata uraia wa Ubelgiji alijiunga na Villa Agosti 2012 kwa kitita cha pauni milioni saba akitoka klabu ya Genk ya Ubelgiji.

Msimu uliopita aliifungia timu yake mabao 23 kwenye mashindano yotelakini baadaye alitikisa kibiriti kuondoka kabla ya kupozwa na kukubali kubaki. Msimu huu amefunga mabao 11 tu na amekwenda miezi mine bila kufunga hata moja.

TANZANIA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA

Timu ya Taifa ya Tanzania ya watoto wanaoishi mitaani – Tanzania Street Star kwa mara nyinginge imeweza kufika katika nusu fainali za mashindano ya Kombe la Dunia kwa vijana wanaoishi mitaani ( Street Child World Cup 2014) yanayofanyika kwa mara ya pili toka kuanzishwa na safari hii yakifanyika katika Jiji la Rio de Janeiro.

Tanzania leo imeweka kufika fainali baada ya kuifunga moja ya timu ngumu kabisa katika mashindano haya timu ya Indonesia kwenye mechi ya Robo fainali iliyochezwa majira ya asubuhi hapa Rio de Janeiro.

Katika mechi hii ya robo fainali Tanzania ilikuwa ya kwanza kupachika magoli ya mapema katika kipindi cha kwanza yakifungwa na Michael pamoja na Hassan. Baada ya magoli hayo Indonesia waliweza kuishambuli Tanzania kwa takribani muda wote wa mchezo wakisaka kurudisha magoli.

Indonesia waliweza kusawazisha magoli katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza na mwanzoni mwa kipindi cha pili na kuufanya mchezo kumalizika kukiwa na sare ya magoli mawili kwa mawili hivyo kulazimika kucheza muda wa nyongeza ambao pia ulimalizika magoli yakiwa mbili kwa mbili. Kufuatia matokeo hayo na sheria za mchezo wa wachezaji saba uwanjani( 7 aside) ziliamuliwa penati kupigwa. Penati 3 ziliamuliwa kupigwa kwa kila timu na Tanzania ikafunga penati 3 Indonesia ikafunga 1 na kufanya matokeo ya mchezo kuwa 5 kwa Tanzania na 3 kwa Indonesia.

Penati za Tanzania zilipigwa na Michael, Emmanuel (golikipa) na Hassan penalt ya mwisho. Na nyota wa mchezo alikuwa golikipa wa Tanzania Emmanuel aliyeokoa michomo mikali golini kwa timu ya Tanzania. Na kuweza kuibeba timu hadi nusu fainali, Emmnauel amekuwa gumzo kweli kweli katika mashindano haya akidhaniwa kuwa ndiye goalikipa bora wa mashindano mpaka sasa.

Kwa matokeo hayo Tanzania imefuzu kwenye nusu fainali hizi na hivyo itacheza na USA katika kusakatiketi ya kucheza fainali na mshindi wa 3 na 4 siku ya Jumapili mechi zitakazo chezwa kwenye Uwanja wa Klabu maarufu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro. Timu nyingine zilizoingia nusu fainali na mechi zake zitachezwa kesho ni Burundi vs Pakistani, timu hizi mbili pamoja na USA zimesheheni vijeba, wachezaji wao wanaomekana dhahili kuwa na umrimkubwa sana kama kama U20 wetuwa Tanzania hivyo kuipa Tanzania wakati mgumu kushindana na wachezaji wenye umri mkubwa sana.

Mashindano ya mwaka huu yamekuwa magumu na makubwa sana, na ushani umekuwa mkubwa na timu kukamiana. Tanzania imekifa nusu fainali ya mashindano baada ya kucheza na timu za Burundi 2 – 2 Tanzania, Tanzania 3 – 0 Argentina, Tanzania 2 – 0 Nicaragua, Philippines 2 – 0 Tanzania, na robo fainali Tanzania 5 – 3 Indonesia.


Chanzo: Tanzania sports

MICHAEL SCHUMACHER AANZA KUPATA FAHAMU

Bingwa wa zamani wa mbio za magari ya langalanga ya F1, Michael Schumacher ameanza kuonyesha hali ya kupata fahamu baada ya miezi kadha ya kuwa katika hali ya kutojitambua.

Wakala wake Sabine Kehm amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema Schumacher "anaendelea vizuri", akisema kwamba wana "uhakika"wa kupona kwake.

Madaktari nchini Ufaransa wanafanya jitihada za kumwondoa katika hali ya kutojitambua, bingwa huyo mara saba wa F1.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 45-alipata majeraha makubwa ya kichwa baada ya ajali wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps nchini Ufaransa Desemba 29,2013.

"Tuko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake, sisi na timu nzima ya madaktari na wauguzi wa hospitali ya Grenoble," amesema BiKehm.

MUDA WA BUNGE LA KATIBA HAUTOSHI

Wajumbe wa Bunge la Katiba wametofautiana kuhusu muda wa siku 70 na nyongeza ya siku 20 ambao umetengwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya Bunge hilo kufanya kazi zake.

Amon Mpanju, ambaye ni mjumbe anayetoka kwenye kundi la wateule201, alisema mpaka wakati Bunge hilo linamaliza kutengeneza na kuthibitisha kanuni zake, kisheria lilikuwa limebakiwa na siku 32 tu.

Mpanju alisema hata hivyo, marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yalitoa mamlaka kwa Rais wa Jamhuri baada ya kushauriana na kuafikiana na Rais wa Zanzibar, kuongeza muda wa Bunge hilo kufanya kazi, siyo kwa siku 20 bali kwa mujibu wa itakavyoonekana inafaa.

Ingawa hakupendekeza siku ngapi zinafaa kuongezwa, Mpanju alieleza kuwapo umuhimu wa Bunge hilo kuongezewa muda akisema muda uliyopangwa ni finyu mno.

Naye Kangi Lugola alisema ni muhimu kuongeza muda wa kazi zaBunge la Katiba ili mijadala ifanyike kiufasaha.

"Mimi naona tungeongezewa mara mbili ya muda uliopangwa awali (wa siku 70) angalau ingesaidia kufanya kazi kwa kiwango kizuri kidogo, kwa kuwa aina ya Katiba tunayofanyia kazi ni ngumu ikilinganishwa na nyingine nyingi duniani, kutokana na aina ya Muungano wetu," Lugora alieleza.

Tofauti na wajumbe hao, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuongezwa muda bila utashi wa kisiasa hakutasaidia kitu.

"Hata wakiongeza muda hadi kufikia miezi sita, haitawasaidia kwa kuwa kuna kila dalili zinazothibitisha kuwa CCM ambao ni wengi na wenye dola hawako tayari na hawana utashi wa kisisasa," alisema Mbowe.

SITTA AKIRI KUCHEZEWA SAINI YA BABA WA TAIFA NA YA P. MSEKWA

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amekiri "kuchezewa" kwa saini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na sehemu ya saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa zilizopo kwenye hati ya sheria ya kuridhia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ni kweli kuna manenokatika hati hiyo ya sheria namba 22ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.

Alisema katika saini ya Nyerere kumeongezwa herufi "us" kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno "Msekwa" kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.

"Wale vijana walipoona document (nyaraka) haisomeki waliongeza "us" mwisho kwa kompyuta kwenyesaini ya Nyerere, ila walifanya makosa maana bora kitu kionekane kufifia hivyo hivyo lakini kibaki na maana yake," alisema.

Hata hivyo, Sitta alisema kwa waliofanya kazi na hayati Baba wa Taifa wanatambua saini iliyopo kwenye hati ya sheria hiyo ipo sawaukiondoa makosa ya kuwekwa herufi hizo.

Kuhusu saini ya Msekwa, alisema pia kulifanyika makosa katika sehemu ya saini hiyo, kuandikwa kwa kompyuta "Msekwa".

"Ni saini ya Msekwa, lakini vijana wa chamber kwa AG waliongeza neno "Msekwa" kwa kompyuta. Ni mtu asiyejua thamani na uhalisia wa saini ni kubaki ilivyo hata kama kwa miaka 100 hata mtu aje kuisoma kwa darubini," alisema.

Hata hivyo, alisema maudhui ya hati ya sheria hiyo, iliyosainiwa rasmi Aprili 25, 1964 ni sahihi kama ambavyo walikubaliana waasisi wa Muungano, Nyerere na Karume.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alisema kwamba hafahamu kama ofisi yake inahusika na kuchezewa kwa saini hizo, tofauti na madai ya Sitta.


Sheria iliyopitishwa Z'bar

Sitta alisema ili kuondoa utata, ameagiza kupatiwa hati ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume(Presidential Decree) aliyotoa kusaini makubaliano kwani wakati huo, hakukuwa na Bunge.

"Karume alitumia Baraza la Mapinduzi akatumia amri ya Rais akasaini. Tunatarajia kuipata hiyo, sasa tutakuwa tumepata nyaraka za Bara na Zanzibar," alisema Sitta.

Hata hivyo, alisema kisheria kilichopitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Zanzibar ni yaleyale yaliyopo kwenye mkataba wa Muungano.

"Unajua kuhoji sasa mambo haya nikupoteza muda, ni kama kuulizana na mke wako cheti cha ndoa baada ya kuishi pamoja miaka mingi, jana (juzi) nilikuwa nawaomba wajumbe kujua tunachotakiwa ni kutengeneza Katiba ambayo, inajibu matatizo yetu," alisema Sitta.


Hati ipo UN

Akizungumzia hati ya Muungano, alisema kuwa ni kweli kupata hati hiyo kuna umuhimu, lakini mambo yote muhimu yanayohusu Muungano yamewekwa katika sheria hizo mbili zilizoridhiwa na pande zote.

Alisema kwa muda walionao wajumbe wa bunge hilo, lazima wautumie vizuri kuliko kwenda hadi Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kuchukua hati hizo.

"Bunge la Tanganyika lililetewa muswada unaoonyesha mambo waliyokubaliana Nyerere na Karume, na Baraza la Mapinduzi likapelekewa hivyohivyo," alisema na kuongeza: "Sasa ubishi wa hiyo hati ya kwanza kabisa ambayo wengi wanasema ipo Umoja wa Mataifa ilikopelekwa kuthibitisha nchi imebadili jina, hiyo ni ya nini? Ni ubishi wa bure tu."

Sitta alisema kisheria kilichopitishwa na Bunge kinatambua yaliyomo katika hati hiyo na hali ndivyo ilivyo pia kwa Baraza la Mapinduzi.

Kwa takriban siku tatu, kamati kadhaa za Bunge zinazojadili Rasimu ya Katiba, zimekuwa na mgongano juu ya hati za muunganona uhalali wa saini za Nyerere na Msekwa.


Kanuni kutenguliwa

Alisema pia, Bunge la Katiba itabidi kubadili kanuni na ratiba yake katika kikao cha leo.

Sitta alisema kwa utaratibu uliokuwapo, leo kamati ndio zilipaswa kuanza kuwasilisha taarifazake, lakini imeonekana haiwezekani.

"Ni kamati moja tu Namba 5, kati ya kamati 12 ndio ambayo ilikuwa imekamilisha kujadili na kupiga kura walau Sura ya Kwanza tu ya Rasimu, hivyo kwa hali ilivyo lazima tupitie upya kanuni zetu," alisema Sitta.

"Tuliweka siku moja kwa ajili ya uandishi na kuandika ripoti, lakini haiwezekani, imebidi tuongeze siku nyingine moja ili wajumbe waweze kuipitia tena taarifa ya kamati ambayo itasomwa bungeni, vinginevyo itasababisha ubishi," alisema.

Alisema marekebisho yote ya kanuni, yatafanyika leo bungeni na baadaye ndio itatolewa Ratiba ya Bunge katika siku zijazo.

Hata hivyo, alisema katika ratiba hiyo, kutakuwa na mapumziko ya Bunge Aprili 7, kupisha maadhimisho ya Siku ya Karume, baadaye Ijumaa Kuu, Sherehe za Pasaka na pia maadhimisho ya Sokoine na Muungano.

Chanzo: Mwananchi

SAMANTHA LEWTHWAITE KULIPIZA KIFO CHA MAKABURI

White Widow Samantha Lewthwaite was last night feared to be planning a new wave of attacks against Westerners in revenge for the killing of her terror teacher.

Sheikh Abubakar Shariff Ahmed is believed to have recruited hundreds of Brits - including Lewthwaite, her pal Jermaine Grant, who is on trial accused of bomb plots, and Lee Rigby's killer Michael Adebolajo.

But Ahmed also known as Makaburi, meaning "graveyard" – was gunned down in Mombasa, Kenya, on Tuesday, just moments after he appeared in public to support five youths accused of being part of the terror group al-Shabaab.

Today we can also reveal how the hate preacher exclusively spoke to the Mirror last year and predicted his own death at the hands of the Kenyan government.

Intelligence sources fear mum-of-four Lewthwaite also blames the Kenyan authorities for the death of her mentor and will retaliate with attacks on Western targets across Africa.

A senior security source said:­

"International security services areon high alert after this latest bloody development.

Makaburi was always believed to be at the very top of the hierarchy of terror organisation al-Shabaab.

AFGHANISTAN KUFANYA UCHAGUZI MKUU

Vyombo vya usalama nchini Afghanistan viko katika hali ya tahadhari kuu siku moja tu kabla ya uchaguzi mkuu wa urais katika taifa hilo lililosakamwa na vita.

Zaidi ya askari laki mbili wametumwa kote nchini kulinda raiya dhidi ya mashambulizi ya taliban wakitekelza jukumu lao la kikatiba ambalo kundi hilo la kislamu inapinga.

Tume huru ya uchaguzi ya afghanistan imesema kuwa imekwisha wasilisha vifaa vya kupigia kura.

Msemaji wa wa tume hiyo Noor Mohammad Noor, amesema kuwa maandalizi ya uchaguzi yamekamilika.

Wagombea urais wana chini ya saa 12 kukamilisha kampein zao tayari kwa uchaguzi huo utakao andaliwa kesho.

Mshindi atatangazwa katika raundi ya kwanza iwapo mgombea atasajili takriban asilimia hamsini ya kura zitakazopigwa.

Mkondo wa pili utaandaliwa tu iwapo hakutakuwa na mgombea atakayefikisha asilimia hamsini.

Rais anayeondoka Hamid Karzai hawezi kugombea kwani amekwisha ongoza kwa vipindi viwili.

Viongozi 8 Wanagombea kumrithirais Karzai ambaye ameongoza tangu mwaka wa 2001 utawala wa Taliban ulipoondolewa mamlakani.

Wagombea wakuu ni Abdullah Abdullah na Zalmai Rassoul, ambao wamewahi kuhudumu kama mawaziri wa maswala ya Kigeni na Ashraf Ghani Ahmadzai ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa fedha..

CIA KUBADILISHWA MBINU ZAKE

Kamati ya bunge la Marekani kuhusu ujasusi imeidhinisha kuwekwa wazi kwa sehemu mojawapo ya ripoti iliyoiita ya"ukatili" ilioelezea jinsi maafisa wa shiriki la upelelezi la Marekani CIA linavyowahoji wanatuhumiwa wa ugaidi.

Lakini wanakamati wanasema kuwa itachukua muda kabla ya uchunguzi huo kuwekwa wazi kwa umma.

Sehemu ya ripoti iliyofichuliwa inasema kuwa idara ya CIA kila mara ilipotosha serikali kuhusiana na mtindo wake wa kuhoji washukiwa wa ugaidi wakati wa utawala wa Rais George W Bush.

CIA inapinga baadhi ya matokeo ya taarifa hiyo huku ikikiri kutenda matendo ambayo hayakuafikiana na sera za Marekani.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya baraza la Senate Dianne Feinstein anasema matokeo ya kura iliyopigwa kuhusu ripoti hiyo inaonesha wabunge 11-3 waliipigia mswada huo kura huku akisema ni uchunguzi wa matokeo yanayotamausha.

Stakabdhi za CIA Kufichuliwa kwa umma

"Ripoti hiyo inaonyesha dhuluma inayoenda kinyume na hadhi ya taifa letu,''alisema Dianne

Hii inatia doa historia ya taifa letu na ambayo hairuhusiwi kamwe kufanyika. ''Hivi sivyo wamarekani wanavyofaa kufanya." Mwanasiasa huyo wa chama cha Democrat kutoka Carlifonia amesema.

Taarifa ya wanahabari inasema kuwa japo baadhi ya wanakamati wa chama cha Republican walikashifu ripoti hiyo kwa pamoja na wa Democrats, kulionyesha waziwazi mgawanyiko uliopo ndani ya wajumbe hao.

Matokeo ya uchunguzi huo uliyomo katika kijitabu cha ukurasa 500, yatatumwa kwa Rais Barack Obama ili kuchunguzwa, kutiwa saini, kisha kutolewa kwa umma.

MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA MPANDA KUHAMISHWA

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi limepitisha uamuzi wa kuhamisha Ofisi za Makao yake makuu ya Halmashauri wilaya hiyo kutoka Mjini Mpanda na kuhamishia makao makuu yake mapya katika Tarafa ya Kabungu Wilayani

Uamuzi huo ulitolewa hivi karibuni katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilayani ya Mpanda kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Maji kilichoongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Yassin Kiberiti

Katika kikao hicho baadhi ya madiwani walimtaka Mwenyekiti wao wa Halmashauri hiyo awape maelezo ya kina kuhusiana nataarifa zilizoenea kuwa kuna mapendekezo yamekuwa yakitolewa kwenye vikao mbalimbali yanayopingana na uamuzi wa Baraza la Madiwani la kuhamisha ofisi za Makao yao makuu na kuhamishia Kabungu

Diwani wa Kata ya Kabungu Nassor Kasonso ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhoji na kutaka kujua ni utaratibu upi ambao unataka kutumuka kutengua maamuzi yaliyopitishwa na Baraza la madiwani kwenye kikao chao Baraza la madiwani walioamua kuhamishia makao yao makuu Kabungu na badala yake wahamii Katuma Tarafafa ya Mwese

Mwenyekiti wa Halmashauri Yassin Kibiriti alilieleza Baraza hilo kuwa ni kweli kuna baadhi ya vikao vimekuwa vikipendekeza makao makuu yahamishiwe Kata ya Katuma bila kuwashirikisha madiwani ambao ndio wenye Halmashauri.

Aliwafafanulia maamuzi ya kikao cha Baraza la madiwani kiliisha amua makao makuu yawe Kabungu si kwinginepo labda kama baraza hilo litatengua uamuzi wao wa ambao walikuwa wameutowa hapo awali.

Baraza hilo la madiwani baada ya kupata maelezo ya mwenyekiti wao wote kwa pamoja walipitisha kwa kauli moja uamuzi wao wa kuhamishia makao yao makuu Kabungu uendelee kama ambavyo walivyokuwa wameamua toka awali na sivinginevyo.

Pia katika kikao hicho walijadili ombi la SUMA JKT ambao wameomba wapatie zaidi ya Ekari 5000 za ardhi kwa ajili ya ujenzi a kambi katika eneo la Kijiji cha Kamama Kata ya Mpanda Ndogo.

Madiwani hao walishauri kuwa kabla ya ya Halmashauri hiyo kuwapatia eneo hilo Suma JKT ni vizuri kwanza madiwani wakaenda kwenye eneo hilo na kulikaguaili kuepukana na migogoro ya ardhi ambayo inaweza kuja kujitokeza hapo baadaye.

Chanzo: Katavi Yetu

ZAIDI YA WATU 10 WATAPELIWA KWA NJIA YA KUDAI KUPATIWA MKOPO

WATU zaidi ya 10 wametapeliwa fedha, walizotuma kwa mtandao baada ya kurubuniwa kuwa wangepata mikopo katika taasisi, iliyojitambulisha kwa jina la Savings Foundation Loans na kudai ofisi zake ziko katika Jengo la Utumishi.

Wanadaiwa kutoa kati ya Sh 50,000na 100,000 kwa watu hao, wanaodaiwa ni matapeli, wakitumia jina la Menejimenti ya Utumishi wa Umma Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Florence Temba alimwambia mwandishi watu waliotapeliwa, wamekuwa wakifika ofisini hapo kufuatilia mikopo hiyo.

Kwa mujibu wa Temba, miongoni mwa waliotapeliwa, wamo wakazi wa mikoa mbalimbali nchini, ambao wamekuwa wakipiga simu, kuulizia mikopo hiyo baada ya kutakiwa na watu hao kutoa fedha.

Taasisi hiyo ya kitapeli, ilielekeza watu kuwa makao makuu yake yako Dar es Salaam, Jengo Kuu la Utumishi wa Umma "Ofisi ya Rais" kitengo cha Mikopo na Uwekezaji, Jengo Namba 360, ghorofa namba moja Customer Service fund.

Temba ambaye ofisi yake jana ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari, kuonya wananchi juu ya utapeli huo, alisema hiyo ni mara ya pili kuhadharisha, lakini wamekuwa wakipokea maswali kutoka kwa wananchi huku taasisi hiyo ikiendelea kuwatapeli kwa kutoa namba zaidi kwa ajili ya kutuma fedha.

Wakati huo huo, polisi imesema utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti, umeenea nchini na kutakawananchi kuuliza kabla ya kuamua kufanya jambo lolote.

Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso aliliambia gazeti hili jana Dar es Salaam kwamba matapeli hao, wamekuwa wakitangaza vitu ambavyo havipo kiuhalisia na kuwafanya wananchi kuingia katika mkumbo.

Senso alisema hayo kutokana na hadhari ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa wananchi dhidi ya utapeli, unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti.

TCRA imetaka wanajamii kutokutoasimu wala kadi ya simu kwa mtu asiyefahamika, kuitumia.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, mmiliki yoyote wa simu, asitoe maelezo yoyote kuhusu namba ya simu au taarifa za binafsi kwa mtu atakayempigia kutaka taarifa.


Chanzo: Habari leo

WATU SABA WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO MSAKO WA MAJANGILI

Waziri Nyarandu akiangalia meno ya tembo yaliyokamatwa


Kikosi cha Kupambana na Ujangili Kanda ya Kati (KDU) kimefanikiwa kukamata vipande 59 vya meno ya tembo vikiwa na uzitowa zaidi ya kilo 200 vyenye thamani ya Sh176.7 milioni sawa na tembo 29.

Katika msako huo watu saba walikamatwa baada ya kukutwa na meno hayo, akiwamo ofisa mtendaji wa Kijiji cha Kayui wilayani Manyoni, Philomen Kanyonga aliyedaiwa kuongoza ujangili huo.

Akielezea tukio hilo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu juzi, mhifadhi mwandamizi wa Ngorongoro, Robert Mande alisema meno hayo yalikamatwa Machi 28 na 31.

Alisema kikosi kazi hicho kilianza kufuatilia mtandao wa ujangili katika kijiji cha Kiyombo na walifanikiwa kukamata meno hayo 53 ya tembo 26 katika kijiji hicho pamoja na bunduki aina ya SMG yenye namba 40129 ambayo alikamatwa nayo Eliud Selemani.

Alisema katika tukio hilo waliwakamata watuhumiwa watano ambao aliwataja kuwa ni Idd Waziri (29), Leonard Oscar (32), Ramadhani Said (40) na mtendaji huyo ambao wote walikutwa na meno hayo 53 ya tembo.

Mhifadhi huyo alisema katika kijiji cha Chinangali mkoani Dodoma walifanikiwa kukamata watuhumiwa wawili ambao ni David Makasi na Joseph Malima ambao walikutwa nameno sita yenye uzito wa kilo 31.1 yakiwa na thamani ya sh 27.3 milioni baada ya kuuawa kwa tembo watatu.

Baada ya kupokea maelezo hayo, Waziri Nyalandu alisema anataka kuona watuhumiwa hao wanahojiwaili kujua watu wanaowatuma kufanya ujangili huo kwa kuwa sasa anataka kukamata majangili wakubwa ambao wamekuwa na mtandao mkubwa wa kuteketeza tembo nchini.

Alisema katika kuhakikisha wanaboresha ufanisi wa idara ya wanyamapori, wako katika mchakato wa kuifanya idara hiyo kuwa mamlaka inayojitegemea, ili kuweza kupambana na majangili hao.

"Hawa majangili wananiumiza kichwa kila siku; wanaua tembo wetu kwa ubinafisi wao," alisema. Sasa nataka nikamate majangili wakubwa kabisa wanaoendesha mtandao huu wa kumaliza tembo na pia sasa tuko katika hatua ya mwisho kwa ajili ya kuifanya idara ya wanyapori kuwa mamlaka kamili."

MZEE JAJI WARIOBA AISHANGAA SERIKALI

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema waliokuwa wajumbe wa tume hiyo hawajawahi kudai malipo ya pensheni ya Sh200 milioni kama inavyodaiwa.

"Wajumbe wa Tume hawajatoa madai ya kulipwa shilingi milioni mia mbili. Hakuna mjumbe yeyote aliyetoa dai kama hilo na Serikali inajua," alisemaJaji Warioba katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, aliyoitoa kupitia Nyalali, Warioba and Mahalu Law Advocates ali ongeza:

"Nimeona taarifa iliyotolewa na Serikali kuhusu Tume ya Mabadiliko, nimeshangazwa na maudhui na lugha iliyotumika," alisema Warioba akirejea taarifa iliyotolewa na Ikulu juzi ikieleza jinsi tume hiyo ilivyohitimisha kazi zake.

Wiki hii Jaji Warioba alikaririwa akilalamika jinsi yeye na makamishna wake walivyoondolewa ofisini na kunyang'anywa magari kwa haraka bila kusubiri siku waliyopanga kufanya makabidhiano, lakini Ikulu ilimjibu kwamba shughuli za Tume hiyo zilikoma siku ambayo Tume ilivunjwa.

Katika taarifa yake ya jana, Jaji Warioba alisema aliwasilisha Rasimu ya Katiba Machi 18 mwaka huu na Tume ilivunjwa Machi 19 wakati wajumbe wakiwa bado mjini Dodoma.

"Pamoja na lugha ya kejeli inayotumiwa na Serikali kuniita mnafiki, busara ya kawaida ilitakiwa kutumika kufanya maandalizi ya kuwarudisha wajumbe nyumbani na kuandaa makabidhiano," alisema.

Alisisitiza kuwa Serikali ilikuwa na wajibu wa kuwarejesha makwao wajumbe wa tume hiyo, hata kama muda wa kisheria wa kufanya kazi ulikuwa umepita.

"Niliwasilisha Rasimu Machi 18, 2014. Tume imevunjwa Machi 19, 2014 wakati wajumbe wako Dodoma. Pamoja na lugha ya kejeliiliyotumiwa na Serikali na kuniita mnafiki, busara ya kawaida ingeonyesha umuhimu wa Serikali kujipa muda wa kufanya maandaliziya kuwarudisha wajumbe nyumbani," alisema Jaji Warioba nakuongeza:

"Hata kama sheria ilitaja muda wa kuvunja Tume bado ilikuwa ni wajibu Serikali kufanya mipango ya safari ya wajumbe baada ya kumaliza kazi. Sheria haikuizuia Serikali kufanya hilo. Huo ni wajibuwa Serikali na utaratibu wa kawaidaunaotumiwa na Serikali kwa tume zote inazoziunda. Inaonekana Tumeya Mabadiliko ya Katiba iliwekewa utaratibu tofauti. Kulikoni?".

MBUNGE WA NZEGA NA WENZAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI

Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangwalla na wenzake 11wamefikishwa mahakamani wilayani Nzega, mkoani Tabora wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uharibifu wa mali na kufanya mkutano bila kibali.

Mwendesha mashtaka, Merito Ukongoji ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi, alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa la kuharibu mali ya mgodi wa dhahabu wa Resolute yenye thamani ya Sh15.9 milioni.

Pia, alisema watuhumiwa hao ambao walikana mashtaka yote, wanadaiwa kufanya mkutano bila kibali katika mji mdogo wa Nzega Ndogo na shtaka la tatu, ni la kufanya maandamano bila kibali, kitendo kilichodaiwa kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Ukongoji alidai kuwa washtakiwa hao walitenda matukio hayo Machi 23, mwaka huu katika Kijiji cha Nzega Ndogo na walikamatwa pembezoni mwa mgodi wa Resolute wakipanga kufanya uharibifu mkubwa wa mali.

Washtakiwa wengine ni Richard Mayunga, Hamis Charles, Bernard Bitus, Ibrahim Mrima, Fredrick Mbula, Peter Mandege, Razalo Shimba, Maganga Seleli, Elikana Daud na Kankoba Sululi na LuhendeShija.

Mwendeshj mashtaka huyo alidai upeleleza haujakamilika na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Hakimu Mkazi Wilaya, Joseph Ngomello aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 9, mwaka huu itakapotajwa tena.

TFDA YAFUNGA SUPERMARKET 29

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefunga maduka makubwa (supermarkets) 29 kwa makosa ya kufanya biashara bila vibali mpaka pale yatakapotimiza masharti ya sheria.

Pamoja na hatua hiyo, pia TFDA imekamata bidhaa za aina tofauti za maziwa ya watoto ambazo hazikuwa na sifa ya kuuzwa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Hiiti Sillo alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanya operesheni kali ndani ya jiji."

Wakati wa operesheni iliyoanza Machi 10 hadi 21, tulibaini maduka 39 yasiyosajiliwa na mamlaka na tukayaagiza kufunga.

Hata hivyo, kumi kati ya hayo yalitekeleza masharti haraka na kuruhusiwa kuendelea na biashara," alisema Sillo.

Miongoni mwa maduka yaliyofungiwa ni Puma Supermarket, ambayo meneja wake, Jackson Kessi alipoulizwa kuhusu uamuzi huo, alisema anaendelea kutekeleza amri ya TFDA ya kutimiza masharti ya usajili.

"Mpaka sasa tumeshajaza fomu za usajili na ukaguzi na kuzilipia. Na tayari tumeshapata hati ya malipo. Tunachosubiri ni taratibu nyingine zinazofuata za usajili," alisema, Kessy.


Maziwa ya watoto

Katika hatua nyingine, TFDA imekamata makopo 591 ya maziwaya watoto yenye thamani ya Sh17.6 milioni ambayo hayajasajiliwa kwa matumizi hapa nchini.

"Jumla ya maduka 36 yamekutwa yakiuza maziwa ya watoto ambayo hayajasajiliwa na TFDA.

Maziwa hayo ni SMA1, 2 na 3, Promil Gold, S-26 Gold, Nursoy, Progress Gold, Cow and Gate, Isomil 2, Infacare Soya, Nutrikids na Aptimil 1," alibainisha Sillo.

Aliongeza Watanzania wanatakiwa kujua kuwa maziwa yoyote ya watoto yasiyoandikwa kwa lugha za Kiingereza na Kiswahili hayastahili kuwapo nchini kutokana lugha nyingine kutoeleweka na wananchi.

Mamlaka hiyo pia ilikamata makopo 1,526 ya vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks) vyenye thamani ya Sh4.5 milioni nachumvi paketi 6,090 zenye ujazo tofauti za thamani ya Sh5 milioni zisizofaa kwa matumizi.

"Bidhaa zote hizo tulizozikamata tutaziharibu na zile zisizoandikwa kwa lugha za Kiingereza na Kiswahili tutaangalia kama tutazirudisha kwenye nchi zilikotoka," aliongeza Sillo.

Pamoja na kutosajiliwa, mamlaka hiyo ilibaini pia kuwapo kwa bidhaazilizoisha muda katika maduka 23.

Kwa mujibu wa Sheria ya Chakula na Dawa sura namba 219, bidhaa zachakula na dawa zisizosajiliwa haziruhusiwi kuwapo madukani.

Pia sheria hiyo inaitaka TFDA kubaini na kukamata bidhaa zote zilizovunja masharti ya sheria.

NDEGE WA AJABU WATEKETEZWA BUKOBA

Wananchi katika Kisiwa cha Musira mkoani Kagera wameanza kuteketeza ndege waliodaiwa kutoa kinyesi chenye sumu, huku Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ikiendelea kukalia majibu ya utafiti kuhusu ukweli wa madai hayo.

Wizara iliahidi ingetoa majibu ya utafiti huo mapema.

Ilishuhudia idadi kubwa ya viota vilivyokuwa na vifaranga namayai ya ndege hao waliodaiwa kuwa wa ajabu vikiwa vimeharibiwa.

Awali ilielezwa kinyesi chao kilidaiwa kuwa na sumu kali iliyohusishwa na vifo vya mifugo.

Mmoja wa wananchi katika kisiwa hicho Jackson Robert ambaye alikutwa akikata matawi yenye viota ili kuharibu mazalia ya ndege hao alisema wananchi walikubaliana kuwaangamiza ndege hao ili kuepuka madhara yaliyojitokeza.

"Hawa ni viumbe wa ajabu sana, kinyesi chao kina sumu kali kwani kikianguka kwenye bati zinatoboka baada ya muda mfupi, lakini pia wanyama wakila kinyesi hicho hufa," alisema mkazi huyo.

Awali, Mkuu wa Mkoa huo Kanali Mstaafu Fabian Massawe alithibitisha ndege hao kuvamia kisiwa hicho na baadaye Wizara ya Afya kutuma watafiti kuchunguza ukweli wa madai ya ndege hao kutoa kinyesi chenye sumu.

Ilidaiwa ndege hao pamoja na kinyesi chao kutoboa mabati pia kuku 516 na mbuzi 12 walikufa katika mazingira yaliyohusishwa na ukali wa kinyesi chenye sumu kilichosababishwa na ndege hao.

Hata hivyo alipotafutwa Dk. Munda Elias ambaye aliongoza utafiti huo kutoka Wizara ya Afya kutaka kupata majibu ya utafiti huo, mtaalamu huyo alikata simu na kuendelea kufanya hivyo kila alipotafutwa.

Hata baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu kuhusu nia ya kufahamu matokeo ya utafiti huo, hakuna jibulolote lililotolewa pamoja na kuwa ndiye aliyefika katika kisiwa hicho na kuchukua sampuli za ndege hao kwa ajili ya chunguzi zaidi wa kimaabara.

Pia mtafiti huyo wa wanyama na ndege baada ya kufika katika kisiwa hicho wiki chache zilizopita aliwaeleza wananchi kuwa wamefika kuangalia ukubwa wa tatizo na kuwataka watoe ushirikiano ili kupata ufumbuzi wa madai yao.

MKANGANYIKO JUU YA HATI YA MUUNGANO

Utata umezidi kuibuka katika Bunge Maalumu la Katiba kutokana na kutopatikana kwa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ile ya Sheria ya Baraza la Mapinduzi ya kuridhia Mkataba wa Muungano.

Utata huo, umebainika katika Kamati kadhaa siku moja tangu wajumbe wa Bunge hilo waanze kujadili sura ya kwanzana ya sita ya Rasimu ya Katiba, zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wake.

Kamati namba 2 ilimwalika, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Pius Msekwa kutoa ufafanuzi kuhusu hati hizo, lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali.

Msekwa aliitwa kutokana na kwamba ndiye aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati huo.Mwenyekiti wa kamati hiyo, Shamsi Vuai Nahodha, alithibitisha kutokea utata huo na kwamba walilazimika kumuita Msekwa ili kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa.

Nahodha alisema kwa maelezo ya Msekwa, inaonekana hati ya Muungano ipo Umoja wa Mataifa (UN), kwani kabla ya Muungano, Tanganyika ilikuwa na kiti chake UN na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hali kadhalika.

Nahodha alisema baada ya UN kuomba uthibitisho wa Muungano, ndipo walipelekewa hati hiyo na kwamba haijawahi kurejeshwa.

Kauli hiyo ya Nahodha inapingana na kauli ya Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Hamis Hamad ambaye jana alisema hati hiyo ipo Dar es Salaam na ni moja tu, hivyo siyo rahisi kuipeleka bungeni Dodoma.

"Ile hati ya Muungano ipo Dar es Salaam, lakini tunahofia kuileta maana inaweza kupotea kwani ipo moja tu, sasa ambachotutakifanya inaweza kutolewa nakala na kuthibitishwa na mawakili na ikaja nakala hapa Dodoma iwapo wajumbe wanahitaji," alisema Hamad.

Nahodha alipoelezwa juu ya majibu ya Katibu wa Bunge kuwa hati hiyo ipo Dar es Salaam, alishikwa na mshangao na kusema wanamuomba Katibu huyo, aiwasilishe kama ipo.


Sheria za Muungano Katika hatua nyingine, Sheria Namba 22 ya 1964 ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar kuridhia Muungano nayo haijulikani ilipo.

Baadhi ya wajumbe katika Kamati Namba 2 walidokeza kuwa, walipohoji kuhusu sheria hiyo walisomewa kitabu cha aliyewahi kuwa Mwanasheria wa Zanzibar, Abdul Jumbe na kuambiwa kwamba picha za ukumbusho zipo.

Nahodha ambaye aliwahi kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, alikiri kuwa hata yeye hajawahi kuona sheria hiyo.

"Kwa Bunge la Tanganyika ushahidi tumeletewa hapa kuwa waliridhia Aprili 25, 1964 na waliosaini ni Julius Nyerere, Katibu wa Bunge hilo, Pius Msekwa na aliyekuwa Spika Adam Sapi Mkwawa, lakini kwa Zanzibar haupo," alisema na kuongeza:

"Mimi nilikuwa mtendaji mkuu wa SMZ nilipaswa kujua, lakini nisingeweza tu kuanza kutafuta sheria, sheria ambazo zimetungwa Zanzibar ni nyingi, kwani ingeniwia kazi kubwa sana kuipata hati hii kwani msimamizi wake ni Ofisi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Ofisi ya Rais".

Alisema Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman pia alisema hajawahi kuiona sheria hiyo.

Utata wa saini Kuhusu utata wa saini za Nyerere na Msekwa kwenye hati hizo, Nahodha alisema yeye siyo mtaalamu wa maandishi kubaini kuwa hati hizo na saini zake ni halali au la.

Hata hivyo, alisema Msekwa alikiri kwenyekamati hiyo kuwa saini iliyopo kwenye hati ya makubaliano ya Muungano ni yake.

Utata wa saini za Msekwa uliibuliwa na baadhi ya wajumbe ambao walihoji tofauti baina saini iliyopo kwenye sheria hati ya muungano na saini zake katika nyaraka nyingine rasmi.

Wajumbe waliombana Msekwa wakiongozwa na Godbless Lema, pia walitilia shaka matumizi ya kompyuta katika sheria hizo zilizoandikwa mwaka 1964.


"Mwaka 1964 hakukuwa na kompyuta lakini hapa tunaona sheria zimeandikwa kwa kompyuta na hata sehemu ya saini yaMsekwa na Nyerere kuna herufi zimeandikwa kwa kompyuta," alinukuliwa Lema.

Katika maelezo yake Msekwa licha ya kukiri upungufu, aliwakumbusha wajumbe kuwa siku ya kusainiwa hati hizo, picha zilipigwa na zipo hadi sasa.

Jana jioni kamati zilianza kupigia kura suraya kwanza, na Mwenyekiti wa Kamati Namba 5, Hamad Rashid Mohamed alithibitisha kuwa asilimia 90 ya wajumbe wa kamati yake walipiga kura za wazi kupitisha ibara za sura ya kwanza.

Alisema ibara ya 1(1) ilikubaliwa na wajumbe wa kamati hiyo kwa kupata theluthi mbili ya kura kwa upande zote, lakini katika ibara hiyo sehemu ya pili (2), haikuungwa mkono baada ya kukosa theluthi mbili kwa pande zote za Muungano.

Kifungu hicho kinatamka kuwa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ni nchi na shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa nchi mbili zaJamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, ambazo kabla ya hati ya Makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.

Hamad alisema ibara nyingine zilizokosa theluthi mbili kwa Tanzania Bara na Zanzibar ni pamoja na ibara ya 2, 5 na saba. Katika Sura ya kwanza yenye ibara tisa ni tano tu zilizokubaliwa na kamati yake.

Hamad alisema wanatarajia kukutana na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta kuangalia jinsi ya kutengua kanuni ili kuongeza muda wa majadiliano kwenye ibara ya sita ambayo wameanza kuifanyia kazi jana jioni.

Hali katika kamati nyingine tatu, ambazo wenyeviti wake hawajatoa taarifa rasmi bado, mabadiliko ya kifungu hicho yamekosa kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe Zanzibar, huku katika kamati moja kifungu hicho kikikosa kuungwa mkono na theluthi mbili ya pande mbili za Muungano.


Chanzo: Mwananchi

TETEMEKO LAITIKISA CHILE

Tetemeko la pili kubwa la ardhi limetokea Kaskazini mwa Chile saa 24 baada ya tetemeko la kwanza kubwa kutokea Jumatano na kuwaua watu sita huku likiharibu nyumba 2,600 huku likisababisha watu kuhamishwa kutoka maeneo ya Pwani.

Tetemeko hilo lenye vipimo vya 7.8 lilimlazimisha Rais Michelle Bachelet kuondoka pwani ya eneo hilo na kuelekea sehemu salama maeneo ya juu.

Maafisa wa huduma za dharura wameamuru kuondoshwa kwa watu kutoka maeneo yaliyo karibu na pwani ya nchi hiyo.

Hii ni baada ya Rais Bachelet alipokuwa kukagua uharibifu uliosababishwa na tetemeko la kwanza Jumatano.

Mawimbi ya kwanza ya Tsunami yamepiga katika fukwe ya bahari na hapajakuwa na taarifa za uharibifu wa aina yoyote.

Serikali za Chile na Peru zililazimika kutoa tahadhari ya tisho la Tsunami kwa mara nyingine ingawa tahadhari hiyo iliondolewa baada ya mawimbi makali kupiga maeneo ya Pwani.

Tetemeko hilo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ingawa hakuna taarifa zozote za uharibifu zaidi zimeripotiwa.

SERIKALI KUGAWA KONDOM ZENYE MVUTO KWA WANAFUNZI

Serikali ya Afrika Kusini imeanza mpango wa kuwapa vijana wa shule za sekondari kuendelea juu mipira ya Condom zenye rangi tofauti tofauti na ambazo zina harufu nzuri ya kuvutia.

Mpango huu unalenga kuzuia wanafunzi kuchoka kutumia mipira ya kawaida ya condom wanaposhiriki ngono.

Waziri wa afya Aaron Motsoaledi, ameyasema hayo baada ya utafiti uliofanywa nchini humo kuonyesha kuwa matumizi ya mipira ya Condom imepungua nchini Afrika Kusini.

Inaarifiwa kinachosababisha upungufu huo ni kwamba Condom za kawaida zinazotolewa na serikali hazina mvuto wowote kwa vijana.

Afrika Kusini ina watu milioni 6.4 wanaoishi na virusi vya HIV, idadi hiyo ikiwa juu zaidi kuliko nchi yoyote duniani.

Utafiti uliofanywa na kitengo cha serikali cha utafiti wa afya, ulionyesha maambukizi yameongezeka hadi asilimia 12.2.

Takriban watu milioni 2 hupata matibabu ya ARV's au madawa ya kupunguza makali ya HIV.

Hata hivyo baadhi ya mashirika ya misadaa yanaonya kuwa baadhi ya kliniki zinakabiliwa na upungufu wa dawa hizo.

Condom hizo zitatolewa na serikali kwa vijana bila malipo.

MWANAFUNZI AUAWA NA MWALIMU WAKE

Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.

Mtoto huyo inaarifiwa alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini.

Wazazi hao waliandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.

Hata hivyo polisi waliweza kumkamata mwalimu huyo na kumpeleka kituoni huku uchunguzi ukianza kufanywa.

Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi ya Roka Preparatory.

Inaarifiwa alizirai baada ya mwalimu kumchapa kwenye kisogo.

Wazazi hao waliokuwa wanalalamikia kile wanachosema ni wanafunzi kuadhibiwa vikali kwa makosa madogomadogo walitaka mwalimu huyo achukuliwa hatua kali kwa kitendo hicho cha kumchapa mwanafunzi ambacho kimeharamishwa katika shule zote nchini Kenya.

Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine.

Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita. Ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwa jeruhi kukithiri.

MWANAJESHI MAREKANI AUWA WENZAKE

Wanajeshi wanne wamepigwa risasi na kuuawa katika kambi ya jeshi huko Fort Hood jimboni Texas.

Jenerali Mark Milley, amesema mwanajeshi mmoja ndiye aliyewafyetulia wenzake risasi hizo karibu na zahanati ya afya ya kijeshiya Carl R Darnall iliyoko katika kambi hiyo ya Jeshi.

Watu watatu walifariki kabla ya mwanajeshi huyo kujipiga risasi na kujiua.

Wanajeshi wapato wanne wanatibiwa majeraha mabaya ya risasi.

Daktari mkuu wa zahanati hiyo Dakta Glen Couchman anaelezea majeraha wanayotibu.

''Wote walikuwa na majereha mbalimbali ya risasi kwenye vifua shingo na tumbo''.

Waziri wa usalama Chuck Hagel amesema kuwa uchunguzi tayari umeshaanza kubaini chanzo cha kisahicho cha pili kuikumba kambi hii.

Haiwezekani kuwa tukio sawa na lilelililotokea miaka mitano iliyopita litokee tena na tukose kujiuliza kunani.
Tunafahamu kuwa jamaa na familia zilizoko Fort Hood zimejitolea kwa ajili ya usalama wa taifa letu. Tunahuzunishwa sana kuwa tukio hili limerudiwa katika kambi hii

"President Barack Obama''
ninajua kuwa mtangulizi wangu Leon Pannetta aliwahi kusema kuwatukio kama hili mwaka wa 2009 litachungzwa.

Ni wazi lazima kuna kitu kinachoendelea ambacho hakifai.
Lazima tutatue shida hii.

''Rais Obama amehuzunishwa sana na tukio hilo ambalo anasema limetokea katika kambi ambayo inapaswa kuwa salama.

Obama amesema ''amezungumza na maafisa wa FBI na idara ya mahakama kutafuta kwa kina kiini cha makabiliano haya ili kuhakikisha kambi zetu zimekuwa salama.

Hii siyo mara ya kwanza kwa kituo hicho kikubwa cha majeshi ya Marekani Fort Hood kushuhudia ufyetulianaji wa risasi.

Mwaka 2009 wakati dakatari wa magonjwa ya kiakili wa jeshi la Marekani meja Nidal Hasan alipowapiga risasi na kuwaua watu kumi na watatu.

Rais Obama amesema anafuatilia yanayotukia katika kambi hiyo kwa makini.

WAATHIRIWA MABOMU UBALOZI WA MAREKANI DAR KULIPWA

Watanzania walioathirika na mlipuko wa mabomu katika ubalozi wa Marekani yaliyopangwa na Osama bin Laden mjini Dar es Salaam wameshinda kesi yao na sasa watalipwa fidia.

Katika hukumu iliyotolewa na Jaji wa mahakama kuu ya Marekani Thomas Bates mjini Columbas, familia tisa za watu waliokufa na waliojeruhiwa watalipwa jumla ya dola laki nne na ishirini za Marekani.

Hukumu hii inakuja kufuatia kesi iliyofunguliwa mwaka 2000 kwa msaada wa wanasheria wa kimarekani.

Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo huyo alitoa hukumu ya awali tangu mwaka 2011 na kilichokuwa kimebaki ni utoaji wa fidia hiyo.

Mmoja wa waathirika hao Judith Mwila ambaye mume wake alifariki katika mkasa huo, amezungumza namwandishi wa BBC Baruan Muhuza mjini Dar es salaam na kusema kuwa yeye amepata taarifa hiyo kupitia kwenye gazeti tu.

Msimamizi wa waathirika hawa Fuad Latif ambaye ni kiungo kati yao na mawakili wanaoendesha kesi hiyo, ameiambia BBC kuwa Mahakama hiyo inaandaa utaratibu wa kukamata baadhi ya mali za serikali ya Iran na Sudan kwa ajili ya kulipia fidia hiyo.

Nchi hizo zinadaiwa kuhusika na mipango ya kukamilisha milipuko hiyo kwa kumsaidia Osama bin Laden kutekeleza ukatili huo kwa kutumia kundi lake la Al Qaida.

Watu kumi walikufa katika kadhia hiyo ya ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam mwaka 1998.

Kijana Mtanzania Ahmed Ghailani anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Marekani baada ya kukutwa na hatia ya kupanga mashambulizi katika balozi za Marekani mjini Nairobi na Dar es Salaam.

TZ YAENDELEA KUZIMA ANALOGI

Tanzania imeingia awamu ya pili ya mpango wake wa mfumo wa matangazo kuhama kutoka analojia kwenda dijitali, kwa kuzima mitambo ya analojia katika baadhi ya miji ya kati na magharibi mwa nchi hiyo.

Miji iliyoingizwa katika mfumo huo kuanzia jumanne wiki hii ni Singida na Tabora wakati ambapomiji mingine saba ikiwemo Kigoma na Kagera itaingizwa kufikia mwezi Mei mwaka huu.

Mkuu wa mawasiliano wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania - TCRA, Inocent Mungy ameiambia BBC mjini Singida kuwa kufikia Novemba 30 mwaka huu watakuwa wamezima mitambo ya analojia katika miji 11 kwa awamu hii ya pili, huku akidai kuwa kazi ya kukamilisha matangazo ya dijitali kwa nchi nzima itakuwa ndani ya muda uliowekwa.

Wakati Tanzania ikiwa mstari wa mbele katika eneo la Afrika Mashariki , Kenya ipo kwenye mgogoro wa kisheria kukamilisha mpango huo.

Kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa nchi nyingi duniani zinatakiwa kuhamia matangazo yadigitali ifikapo Juni mwaka 2015.

MKE NA MUME WAKAMATWA NA MABOMU

Watu wawili wamekamatwa baada ya kupatikana wakiwa na maguruneti mawili nyumbani mwao wakati polisi wakiendelea na msako mkali mtaani Easteligh nchini Kenya.

Wawili hao, Mume na mkewe walikuwa nyumbani wakati polisi walipopata habari kuwahusu na vifaa walivyomiliki.

Mume mwenye umri wa miaka 60 inaarifiwa aliwauzia vijana vilipuzi ambavyo walitumia kwa mashambulizi mjini Mombasa karibu wiki mbili zilizopita.

Polisi wamekuwa wakifanya msako katika mtaa huo wa Easteligh tangu mashambulizi ya maguruneti kuwaua watu 6 Jumatatu usiku na kuwajeruhi wengine 30.

Mkuu wa polisi alisema kuwa wawili hao walikamatwa pamoja na watu wengine 400 katika eneo hilo huku msako wa polisi ukiendelea.

Polisi wanasema kuwa wanawahoji wawili hao kuona ikiwa wanaweza kupata taarifa zaidi

Takriban watu 657 walikamatwa na polisi Jumatatu usiku mtaani Eastleigh, baada ya shambulizi la kigaidi dhidi ya mkahawa kuwaua watu sita.

AJICHIMBIA KABURI KUKWEPA MATATIZO YA NDOA

Mwanamume mmoja nchini Kenya aliwaacha wakazi wa kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni matatizo ya ndoa.

Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift ValleyMwanamume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.

Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndhio maana akaamua kujitoa uhai.

Mwanamume huyo kwa jina Kipsang , alichimba kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wanalala.

Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumwba na matatizo ya ndoa.

Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.

Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya Ndizi neneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.

MIAKA 30 JELA KWA UBAKAJI

MAHAKAMA Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemtia hatiani mkazi wa Kijiji cha Mpimbwe wilayani Mlele , John Joseph ( 30) na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 65.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Ntengwa baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka, Godfrey Luzabila.Hakimu alisema ushahidi uliotolewa mahakamani na upandewa mashitaka pamoja na mashahidi watatu, ikiwemo taarifa ya uchunguzi wa kitabibu, zimethibitisha mama huyo alikuwa amebakwa na kuharibiwa sehemu za siri.

"Hivyo Mahakama haikuona shaka lolote kukutia wewe mshtakiwa hatiani " alisema hakimu.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 18 mwaka jana saa 12 jioni kijijini Ifukutwa Tarafa ya Kabungu wilayani Mpanda.

Ilidaiwa kuwa mtu huyo, ambaye wakati huo alikuwa kibarua wa kuchimba mitaro ya barabara, alimwona mama huyo akipita barabarani, karibu na alipokuwa akifanya kazi.

Alimvamia kisha akamvuta kichakani na kumbaka. Kwa mujibuwa Hakimu Ntengwa, licha ya mama huyo kumsihi mshitakiwa akatafute mwanamke mwingine warika lake, alikaidi na kuendelea kumshika kwa nguvu kisha kumvua nguo zake za ndani. Mama huyo alipiga yowe kuomba msaada.

Ilielezwa kuwa yowe hizo zilisababisha wapita njia watatu kumsikia.

Waliamua kufutilia kichakani na kukuta akifanya kitendo hicho, wakamkamata.

Chanzo: Habari leo

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LAVURUGIKA

BUNGE la Afrika Mashariki (EALA), limeahirishwa kwa muda usiojulikana baada ya kutawaliwa malumbano jana juu ya suala zima la kumng'oa Spika.

Malumbano ya kisheria ya kutaka kumng'oa Spika, Dk Margareth Zziwa, yalijitokeza jana baada ya kuwapo pande mbili, zilizopingana juu ya suala hilo. Baadhi ya wabunge walidai hoja hiyo, haiwezi kujadiliwa kwa vile ipo mahakamani.

Wengine walisema inaweza kujadiliwa bila tatizo lolote.

Kutokana na malumbano hayo, Zziwa aliahirisha Bunge hilo kwa muda usiojulikana.Hali tete bungeni ilianza kujitokeza mapema jana mchana, kabla ya kuanza kwa kikao hicho. Wakati kawaida kikao huanza saa 8: 00 mchana, jana kilianza saa 9:45 alasiri na kumalizika saa 10:03 jioni. Hali hiyo ilitokana na wabunge wengi kuwa nje ya ukumbi, badala ya kuingia ukumbini.

Waligongewa kengele, lakini hawakuingia. Hata ilipopigwa kengele nyingine, kutaka waingie, meza zao zilikuwa zimewekwa karatasi za shughuli za kazi kwa siku hiyo, huku hoja ya kumng'oa Spika bila kuwemo.

Ilielezwa karatasi hiyo, iliondolewa muda mfupi kabla ya kuanza kwa Bunge ;na waligawiwa karatasi nyingine, zilizoonesha kuwa na hoja ya kumng'oa Spika.

Baada ya sala iliyosomwa na Spika, Katibu wa Bunge hilo, Kenneth Madete, alimtaka mtoa hoja, Peter Mathuki, kusoma hoja yake. Lakini,wakati akifanya hivyo, Mbunge kutoka Uganda, Fred Mbidde, aliomba utaratibu kwa Spika.

Aliporuhusiwa, Mbidde alipinga kuwasilishwa kwa hoja hiyo kwa maelezo kwamba lipo shauri, lililowasilishwa Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ), kutaka ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kumng'oa Spika ulivyo.

Mbidde alisema wakati wakisubiriauamuzi wa Mahakama, si vyema kwa Bunge hilo kujadili tena hoja hiyo. Hoja hiyo ilipingwa na Mwanasheria wa Afrika Mashariki, Wilbard Kahwa, aliyesema pamoja na shauri hilo kuwa mahakamani, haimaanishi wabunge kutojadili.

Malumbano kati yao yaliendelea huku wabunge wa pande mbili, wakipigia makofi hoja wanazounga mkono. Ndipo Spika Zziwa, aliamua kuahirisha Bunge hilo kwa muda usiojulikana.

Nje ya ukumbi wa Bunge, baadhi ya wabunge walisema hawana imani na uongozi wa Zziwa, kutokana na kuwa na upendeleo wakati wa kupanga safari za nje.

Ilidaiwa miongoni mwa wabunge, baadhi wanajirudia katika ziara huku wengine wakipata safari chache. Mkakati wa kumng'oa spikahuyo, ulianza hivi karibuni kwa wabunge wanne kutoka kila nchi mwanachama, kusaini hati ya kusudio hilo na kuwasilisha kwa Katibu wa Bunge, Madete.

Uamuzi wa kumng'oa Spika huyo wa Bunge, lenye wabunge 45, unatokana na madai kwamba ameshindwa kufanya kazi kwa viwango, ikiwemo upendeleo miongoni mwa wabunge.

MHUBIRI WA KIISLAMU BWANA MAKABURI AUAWA

Mhubiri aliyedaiwa kueneza itikadi kali za kiisilamu nchini Kenya Abubakar Shariff anayejulikana kwa jina lengine kama Makaburi, ameuawa.

Duru zinasema kuwa Makaburi aliuawa katika mtaa wa Shanzu mjini Mombasa ambako alikuwa anaishi.

Polisi wamekuwa wakimtuhumu Makaburi kwa kueneza itikadi kaliza kiisilamu miongoni mwa vijanawa kiisilamu mjini Mombasa Pwani ya Kenya na kuchochea vitendo vya kigaidi.

Pia amekuwa akituhumiwa kwa kusajili vijana kuenda kupigania kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia, madai ambayo Makaburi amekuwa akiyakanusha.

Duru zinasema kuwa vijana wameanza kuzua vurugu katika msikiti wa Majengo, Mombasa kufuatia taarifa za mauaji ya mhubiri huyo mwenye utata.

Taarifa za kifo cha Makaburi zilitolewa katika msikiti Musa ambao umekuwa kitovu cha vurugu kati ya maafisa wa usalama na vijana wanaodaiwa kuhubiri na kufuata ikitakadi kali za kiisilamu.

Haijulikani ni nani aliyemuua Makaburi

ATUPWA JELA MIAKA 65 KWA KUMPA MIMBA MWANAE

MKAZI wa Mtaa wa Uhamila katika mji mdogo wa Rujewa, mkoani Mbeya, amehukumiwa miaka 65 jela kutokana na makosa matatu tofauti, yaliyotokana na kumpa ujauzito mwanawe wa kumzaa.

Mahakama ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ilitoa hukumu hiyo jana kwa Benjamin Muyinga (48) baada ya kutiwa hatiani kwa makosa hayo.

Hakimu Mfawidhi Kinabo Minja alimhukumu mshitakiwa kutumikiajela miaka 30 kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake, miaka 30 mingine kwa kubaka mtoto wake na miaka mitano jela kwa kumpa mimba mwanafunzi.

Minja alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hivyo atatumikia adhabu hiyo kwa pamoja kwa maana kwamba atakaa jela miaka 30.

Mashitaka yaliyokuwa yakimkabili mahakamani hapo ni kufanya mapenzi na mtoto wake, kubaka mtoto wake na la tatu ni kumpa mimba mwanafunzi.

Awali ilidaiwa mahakamani na Mwendesha Mashitaka wa jeshi la Polisi, Mazoya Luchagula, mbele ya Hakimu Mfawidhi Kinabo Minja, Oktoba 18 mwaka jana, mwanafunzi (jina linahifadhiwa) aliyekuwa na umri wa miaka 14, alikuwa mjamzito.

Luchagula alidai walimu wa shule hiyo ndiyo walitilia shaka suala la mwanafunzi huyo aliyekuwa darasala tano katika shule ya msingi iliyoko Rujewa kwamba alikuwa na ujauzito.
Alipelekwa hospitali na kwenda kukutwa akiwa na mimba ya miezi minne.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka, baada ya kuhojiwa, mwanafunzi huyo alidai ujauzito ulikuwa wa baba yake mzazi waliyekuwa wakiishi naye wawili nyumbani kutokana na baba yake kutengana na aliyekuwa mkewe ambaye hivi sasa anaishi jijini Mbeya.

Mwanafunzi huyo alibainisha namna alivyokuwa akiishi na baba yake baada ya wazazi wake kutengana na kwamba alimgeuza 'mkewe' kwani alikuwa akilala naye na kufanya naye mapenzi hadi ilipobainika kuwa na ujauzito huo.

Katika kile kilichoelezwa na upandewa mashitaka kwamba kitendo kilichofanywa na mzazi huyo hakikubaliki katika jamii ya Watanzania, Mwendesha Mashitaka aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwake na wazazi wengine wenye tamaa zenye kusababisha ukatili dhidi ya watoto wao.

MUUNDO WA TANZANIA KUJULIKANA IJUMAA

MUUNDO wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza kujadiliwa rasmi kupitia Kamati 12 za Bunge Maalumu la Katiba ambazo zinajadili Sura ya Kwanza na ya Sita za rasimu ya Katiba mpya.

Kutokana na kazi hiyo, jibu la ama Tanzania kuwa na mfumo wa Serikali tatu kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba iliyowasilishwa bungeni hapo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba wiki mbili zilizopita, au aina nyingine ya muundo, litapatikana Ijumaa.Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta aliwaambia wajumbe wa Bunge hilo jana kwamba kazi hiyo ya kuchambua sura hizo inafanyika leo na kesho.

Hata hivyo alisema kazi hiyo ingeweza kuanza kufanyika jana kwa kamati ambazo zilikuwa tayari kufanya hivyo. Alisema siku ya janahaikuhesabika kama siku rasmi ya mjadala kutokana na kuwepo shughuli nyingi za kiutawala.Miongoni mwa shughuli hizo ni pamoja na wajumbe kuelekezwa juu ya mfumo wa mjadala kwenye kamati na pia muundo wa uandishiwa sura hizo kuweka mfumo ambao hautaleta tabu katika uandishi wa Katiba mpya.

Kutokana na hali hiyo, Sitta alisema sura hizo zitajadiliwa kwa siku mbili hadi kesho na Alhamisi itakuwa maalumu kwa Kamati ya Uandishi kufanya kazi yake ya kuandika masuala yaliyojadiliwa na kuafikiwa au kutoafikiwa na wajumbe walio wengi.

Ijumaa, wenyeviti wa kamati hizo watawasilisha taarifa zao bungeni kwa mjadala.

Sitta alisema Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu iliamua kuanza kujadiliwa kwa sura namba moja na sita kutokana na sura hizo kuwa na mambo yanayofanana kuhusu muundo wa Serikali na Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kupatikana kwa muundo kumeelezwa na Mwenyekiti huyo kwamba kutafanya mjadala juu ya masuala mengine kuwa rahisi. "Kama mnavyojua sura namba moja, sura namba sita na sura namba nane zina masuala yanayofanana.

Lakini kwa vile kanuni zinatutaka tujadili sura mbili mbili tutaanza na sura namba moja na sura namba sita ambazo zinafanana maana zinazungumzia muundo wa Jamhuri na Muungano.

"Kamati zitakapojadili kuhusu muundo wa Serikali ya Jamhuri na Muungano masuala kama mahakama, dola na mengineyo yatakuwa rahisi kuyaingiza katika rasimu kwa kuzingatia mfumo utakaokuwa umekubaliwa na wajumbe wengi wa Bunge la Katiba," alisema Sitta.

Marekebisho kanuni yasitishwa Katika hatua nyingine, Bunge Maalumu la Katiba jana limesitisha azma yake ya kuwasilisha marekebisho ya kanuni kama ilivyotangazwa Ijumaa, huku Mwenyekiti Sitta akisema hatua hiyo inatokana na Watanzania kuchoka kusikia wimbo wa kanuni ukiimbwa kila siku bungeni.

"Watanzania wamechoka na mjadala wa kanuni kila siku, hivyo nimesitisha ratiba ya uwasilishaji wa marekebisho ya kanuni na badala yake sasa tutaanza kazi ya kujadili rasimu kwenye Kamati. Kama kuna mgongano wowote wa kikanuni utajitokeza huko mbele tutaangalia namna nzuri ya kuutatua," alisema Sitta.

Waendelea kukosoa 3Wajumbe mbalimbali wa Bunge Maalumu la Katiba, akiwemo NaibuKatibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Nancy Mrikaria wameendelea kukosoa mfumo wa Muungano wa Serikali tatu wakisema unabeba maslahi yawatu wachache.

Akizungumza na gazeti hili jana mjini Dodoma, Mrikaria alisema wajumbe hao wameaminiwa na wananchi na wanapaswa kuangalia maslahi ya taifa na kuweka kando itikadi za kisiasa.

Aliasa wajumbe kuacha kung'ang'ania serikali tatu akisema serikali mbili bado zinafaa. "Tusiangalie serikali itakayobeba maslahi ya watu wachache, cha muhimu ni kuangalia serikali yenye maslahi ya watu wengi," alisema.

Mjumbe mwingine wa Bunge Maalumu, William Ngeleja amesema upo umuhimu wajumbe wa bunge hilo kufanya maamuzi yakuimarisha muungano na kuacha kuwa na maslahi binafsi yenye lengo la kuvunja muungano. Alisema hayo jana mjini hapa huku akisisitiza kuwa muumini wa serikali mbili.

Ngeleja alisema msingi muhimu wa rasimu ni makubaliano hivyo nimuhimu wajumbe wakafanya uamuzi utakaoimarisha muungano licha ya rasimu kutamka serikali tatu.

"Tubishane na tujadiliane kwa hoja, tunaamua hatma ya Watanzania tutimize wajibu wetu kwani wakati wa kujadili rasimu tutaangalia mambo ya kiasiasa na kisheria pia," alisema Ngeleja.

Alisema bado serikali mbili zinafaana jambo la muhimu ni kuangalia changamoto zilizopo na kupatiwa ufumbuzi badala ya kufikiria kuwa na serikali tatu. Alisema kwenye kundi la watu 600 kusitegemewe kuwa na mawazo ya aina moja.

Alisihi Watanzania kuwa na amani na utulivu. Alisisitiza kazi ya kutunga katiba ni ya wananchi wote. Alisema ni halali watu walio nje kuendelea kutoa maoni yao na misimamo tofauti kwani baadaye maoni yanachukuliwa na kuchaguliwa yale yanayofaa na yasiyofaa.


Chanzo: Habari leo

RIPOTI YA CAG YAIBUKUA UTATA KISHERIA

Siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kupokea taarifa kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, utata wa kisheria umegubika suala hilo kutokana na ukweli kuwa ibara ya 143 (4) ya Katiba inataka Rais aiwasilishe bungeni taarifa hiyo ndani ya siku saba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisema jana kuwa suala hilolina madhara katika utendaji wa Serikali."

Kuna madhara makubwa katika mzunguko wa uwajibikaji, kwani ni rahisi Serikali kuichezea taarifa ya CAG kabla haijawa ya umma. CAG anakagua fedha za Serikali kwa niaba ya wananchi kupitia Bunge. Hivyo ni lazima Bunge la Katiba lipishe Bunge la Muungano ili kupokea taarifa ya CAG," alisema Zitto.Aliongeza: "Tangu uhuru, taarifa ya CAG inawasilishwa katika mkutano wa Bunge wa Aprili kila mwaka. Kwa hali ya sasa, Rais atakaa na taarifa hiyo kwa zaidi ya miezi miwili akisubiri Bunge kukutana.

"Hata hivyo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema siku hizo saba ni baada ya Bunge kuanza."

Hakuna utata wowote hapo, ukisoma vizuri kifungu hicho kinasema, Rais atamuagiza waziri anayehusika kupeleka taarifa hiyo bungeni siku saba baada ya Bunge kuanza, siyo siku aliyokabidhiwa. Kitu muhimu hapo ni pale kikao cha Bunge kinapoanza bila kujali kinaanza lini," alisema Balozi Sefue.

"Katika hali ya kawaida, Bunge la Bajeti lilipaswa kuanza Aprili 8. Bunge la Katiba linahitaji pesa kutoka kwenye bajeti. Sioni namna Bunge la Katiba kuendelea kwa sasa. Itabidi liahirishwe mpaka Agosti," alisema.

Suala la kuahirisha vikao vya Bungela Katiba kupisha Bunge la Bajeti lilielezwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyesema atamshauri Rais Kikwete kuangalia uwezekano huo.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila akizungumzia uwezekano huo, alisema Bunge hilo litasubiri ratiba ya shughuli za Bunge la Katiba.

Dk Kashilila alisema Kamati ya Uongozi wa Bunge la Katiba inatarajiwa kutoa ratiba ya shughuli zake kuelekea Bunge la Bajeti.

"Inapofika Juni, Serikali inatakiwa kuidhinishiwa fedha kwa ajili ya matumizi yake, kwa hiyo mpango uliopo ni kuhakikisha kabla ya Juni 30, Bunge la Bajeti liwe limeanza kazi zake," alisema.

SAMATTA AWABEBA MAZEMBE

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata alifunga bao pekee na kuiongoza TP Mazembe ya DR Congo kutinga hatua ya makundi yaLigi ya Mabingwa Afrika, huku mabingwa watetezi Al Ahly wakiagamashindano kwa kuchapwa 3-2 nyumbani na Al Ahly Benghazi ya Libya.

Samata aliingia akitokea benchi na kufunga bao hilo dakika ya 68 na kuipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Sewe Sport ya Ivory Coast na kusonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa 2-2 baada ya awali Mazembe kutunguliwa mabao 2-1 jijini Abidjan.

Samata ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi Abidjan wiki moja iliyopita pamoja na bao pekee la Jumamosi jijini Lumbumbashi. Sasa Mazembe itasubiri kujua wapinzani wake katika droo itakayopangwa Aprili 29 mjini Cairo.

Nao mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri wameaga mashindano hayo baada ya kuchapwa mabao 3-2 nyumbani na Al Ahly Benghazi katika pambano la marudiano lililopigwa mwishoni mwa wiki jijini Alexandria.

Kipigo hicho kinaifanya Al Ahly iondolewe mashindano hayo kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Tunis, Tunisia ambako Benghazi wanatumia kama uwanja wa nyumbani kutokana na machafuko kushinda 1-0.

TANAPA YAKANA KATAVI KUUZWA

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA), limekanusha taarifa zinazodai Hifadhi ya Taifa ya Katavi ipo kwenye mpango wa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini.

Habari hiyo iliandikwa Machi 25 mwaka huu na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki ikiwa na kichwa cha habari kinachosema, "Nyalandu 'auza'Hifadhi".

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TANAPA kupitia Idara yake ya Mawasiliano, ilisema habari hiyo ilidai agizo la hifadhi hiyo kupewa wawekezaji, limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Lazaro Nyalandu Idara hiyo imeongeza kuwa, TANAPA ambayo ndio wasimamizi wa hifadhi hiyo na nyingine 15 nchi nzima, inakanusha habari hiyo na kudai imeandikwa kwa lengo la kupotosha umma.

"Hakuna mpango wala uamuzi wowote uliopo au uliofanywa wa kuingia mkataba wa uendeshaji hifadhi yoyote nchini kati ya TANAPA na mwekezaji yeyote kutoka nchini humo wala African Parks Network waliotajwa katika habari husika.

"Sheria inayosimamia uanzishwaji maeneo ya Hifadhiza Taifa ikiwemo Katavi, imelipa dhamana shirika kusimamia maeneo haya kwa niaba ya Watanzania hivyo ni kinyume cha sheria kukabidhi kwa wawekezaji kwa ajili ya usimamizi kama ilivyobainishwa katika habari hiyo," ilisema taarifa ya idara hiyo.

Iliongeza kuwa, TANAPA bado lina uwezo thabiti wa kusimamia uendeshaji wa hifadhi hiyo ili kuhakikisha rasilimali za wanyama na mimea zinaendelea kutunzwa kwa miaka mingi ijayo kama ambavyo imekuwa ikifanya tangu kuanzishwa kwa hifadhi husika 1974.

Taarifa hiyo ilisema shirika hilo limekuwa na mipango yake ya maendeleo mwaka hadi mwaka ambapo katika mwaka mpya wa fedha ujao, limepanga kuongeza idadi ya watalii katika Hifadhi za Kusini ikiwemo Katavi, Saadani, Mikumi na Ruaha.

Mkakati huo utahusisha kuongeza ubora wa utoaji huduma na malazi ili kukuza utalii wa ndani ambapo TANAPA itafungua ofisi jijini Dar es Salaam, kuimarisha Ofisi za Mwanza na Iringa ili watalii wapate taarifa za hifadhi."

Shirika litaendelea kujitangaza kupitia mitandao ya jamii, majarida, televisheni na kuiboresha tovuti ya shirika kwa kuwarifu wadau masuala mbalimbali yanayojiri kwenye hifadhi zetu.

"Tayari Shirika limeanzisha Kurugenzi mpya ya Utalii na Masoko kwa ajili ya kutekeleza mkakati wa kuzifanya hifadhi za Ukanda wa Kusini kuvutia watalii wengi zaidi," alisema.

Chanzo:Majira

WATU 29 WAJERUHIWA KATIKA AJALI MBILI TOFAUTI

Watu 29 wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali mbili tofauti katika eneo la Mikese na Mkambalani, barabara kuu ya Morogoro-Dar es salaam, moja ikihusisha basi la Nganga likitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya na basi la Sumry likitokea Tunduma ambalo limegongana uso kwa uso na coster likijaribu kulipita gari jingine lililokuwa mbele.

ITV imefika eneo la tukio na kushuhudia ajali hizo, ambapo ajali ya kwanza imetokea majira ya saa 2 usiku katika eneo la Mkambalani, ikihusisha basi la kampuni ya Sumry likitokea tunduma kwenda Dar es salaam ambalo limegongana uso kwa uso na bas dogo la abiria aina ya costa lililokuwa likitokea dar es salaam kuelekea mbeya na kusababisha majeruhi 15, na chanzo cha ajali kikidaiwa ni dereva wa sumry kujaribu kulipita gari lililokuwa mbele, na kukutana uso kwa uso na costa, huku ,ajali ya basi la nganga ikitokea majira ya saa 3 na nusu asubuhi, katika eneo la miembeni mikese, baada ya kupata pancha kwa tairi ya mbele kulia na kusababisha majeruhi 14 na majeruhi hao wamepelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

Aidha mashuhuda wa ajali hiyo waliokutwa eneo la tukio nao wamezungumza kuhusiana na ajali hizo.

Mganga wa zamu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Dk Alex Makala, amesema majeruhi wengine wametibiwa na kuruhusiwa na kwamba wamebaki majeruhi 14 wakiwemo 12 wa Sumry na wawili wa Nganga, na wengi wamepata majeraha madogo madogo na wanaendelea vyema na matibabu, huku kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro faustine shilogile akizungumza kwa njia ya simu, amesema dereva wa basi la sumry mhina mohamed(39) mkazi wa mbeya amejisalimisha polisi majira ya asubuhi baada ya kukimbia kufuatia ajali hiyo, huku dereva wa basi la Nganga Alex Elia(49) mkazi wa Misufini Morogoro akiishikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Chanzo: ITV

SHAMBULIO LA KIGAIDI WATU SITA WAUAWA

Watu sita wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi.

Polisi wamesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha mabomu katika mkahawa mdogo ulio karibu na kituo cha mabasi mtaani humo.

Walioshuhudia shambulizi walisema kuwa walisikia mlipuko wa tatu katika eneo hilo ingawa polisi hawajathibitisha hilo.

Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa wanawake ambao walipata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kwa mujibu wa polisi wale waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mkahawa huo baada ya mlango kufungwa na washambulizi waliorusha mabomu hayo ndani ya mkahawa wenyewe.

Waathiriwa walikuwa wameenda kununua chakula cha jioni.

Idadi kubwa ya wakimbizi wa Somali wanaishi katika mtaa wa Eastleigh.

Inaarifiwa washambuliaji walitumia maguruneti au mabomu ya kutengezwa nyumbani kufanya mashambulizi hayo.