WANAJESHI WA SUDAN KUSINI WAUKOMBOA MJI WA BENTIU

Taarifa kutoka Sudan Kusini zasema kuwa wanajeshi wa taifa hilo wamechukua udhibiti wa mji wa Bentiu kutoka kwa waasi watiifu kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar.

Msemaji wa kijeshi huko Juba ameiambia BBC kuwa majeshi ya serikali kwa sasa yamechukua usukani wa mji huo.

Amesema kulikuwa na makabiliano madogo kwani waasi walikuwa wakitumia vifaru katika daraja moja nje kidogo ya mji huo.

Hakuna taarifa iliyotolewa kuhusiana na majeruhi.

Maelfu ya raia wamekimbia mji wa Bentiu ambao ni makao makuu ya jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity kabla ya serikali kuukomboa.

Mpatanishi mkuu katika mkutanowa mazungumzo ya kuleta amani huko Ethiopia anasema kuwa ana imani muafaka wa kukomesha vita utaafikiwa karibuni.

AFUFUKA BAADA YA KUJITOA UHAI

Wananchi wa Kenya wameshangazwa na taarifa ya mwanamume mmoja aliyedhaniwa kuwa mfu kufufuka kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu Nairobi.

Mwanamume huyo Paul Mburu mwenye umri wa miaka 24, alipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai, kutokana na ugomvi wa kinyumbani na babake ingawa alisemekana kufariki Jumatano usiku wakati akipokea matibabu.

Wafanyakazi wa hospitali hiyo walipigwa na butwaa na hata kutoroka walipoona mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki ukisonga na kuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Afisaa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo ya wilaya, Dokta Joseph Mburu, alisema kuwa dawa iliyotumiwa kumtibu Mburuhufanya moyo kupiga polepole hali ambayo huenda ilimfanya muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.

Mwanamume huyo alisikika akimtaka mmoja wa wafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na hapo ndipo mmoja wa wafanyakazi alipotimua mbio kwa hofu.

Nusura Mburu awekwe kwenye jokovu la kuhifadhia maiti.

Jamaa za mwanamume huyo akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha maiti siku ya Alhamisi ili kujiandaa kwa mazishi , lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa hai.

ZITTO NIKO TAYARI

LICHA ya uongozi wa Chadema kutaka wanachama wa chama hicho kuacha kumpa ushirikiano Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, yeye amesema yuko tayari kufanya kazi na kiongozi yeyote wa chama hicho aliye tayari.

"Mimi niko tayari kufanya kazi na kiongozi yeyote wa Chadema ambaye atakuwa tayari kufanya kazinami, kwa sababu naamini suala hapa ni ujenzi wa nchi yetu, ni ujenzi wa Taifa letu na naamini hatakama nina mawazo kidogo, lakini ni kwa ajili ya kuiendeleza nchi yetu," amesema Zitto.

Akihojiwa jana na mtandao wa kijamii wa millardayo.com, Zitto alisema sasa hivi kuna masuala makubwa kuhusu Katiba ya nchi na angependa wananchi wajielekeze huko.

"Sijafurahishwa sana na kinachoendelea hivi sasa, maana yake wananchi wameacha kujadili masuala ya msingi yanayowahusu, nasikitika kuona vyombo vya habari ni habari za Zitto na Chadema, nashukuru jambo hili limekwisha sasa kwa muda huu," alisema akimaanisha mgogoro na chama chake.

Alisisitiza kuwa bado ni mwanachama wa Chadema, licha ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Wilbrod Slaa, kutoa amri ya watu kumnyima ushirikiano "lakini pale nitakapohitajika nitafanya shughuli za Chadema, nitafanya shughuli za nchi yangu.

"Kuhusu ushindi wake wa juzi mahakamani, alisema si ushindi dhidi ya chama, kwa sababu hawezi kushindana na chama chake, kwa kuwa kimemlea na amekitumikia kwa muda wote, zaidi ya nusu ya umri wake."Kwa hiyo salamu ambazo napenda wananchi wazifahamu ni kwamba tunahitaji kuheshimu sana demokrasia na misingi ya haki za binadamu," alisema.

Akizungumzia uamuzi wa Mahakama, uliotolewa na Jaji John Utamwa, alisema utaweka utaratibu kwamba watu ambao ni wanachamawa vyama hawataonewa, hawata dhulumiwa wala kukandamizwa na watakuwa huru kutoa maoni yao wanapohitaji kufanya hivyo.

"Nataka niseme wazi kabisa kwa Watanzania ambao ni wanachama wa vyama vingine, wasio na vyama na kwa wana Chadema, ushindi huu si dhidi ya Chadema, ni wa Watanzania wote wanaopenda siasa safi na taratibu za utawala bora zifuatwe kwenye taasisi zetu."Ni ushindi dhidi ya wanaotaka kukandamiza demokrasia ndani ya vyama, ni ushindi dhidi ya wahafidhina wasiotaka mabadiliko katika vyama," alisema.

Lissu Akizungumza muda mfupi baada ya hukumu hiyo juzi, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema suala ambalo Chadema inalisema kuwa muhimu ni kwa wanachama wake kuhakikisha hawampi nafasi Zitto lakini kama atataka kuandaa mikutano kwa jina lake anaweza kuendelea, kwa kuwa kwa mujibu wa Mahakama bado mwanachama wa Chadema.

Hata hivyo alisisitiza kuwa Zitto ni mbunge wa Mahakama na kwamba 'ubunge wa Mahakama' una mwisho wake, kama mbunge wa Mahakama atapokea posho, atapokea mishahara atakwenda safari za PAC kwa hiyo ana haki zote kama mbunge.

"Kwenye vikao kama ni mwanachama kwenye tawi lake atashiriki, lakini kwenye vikao vingine vya chama ambavyo si mwanachama na si mjumbe hatashiriki," alisema Lissu.

Alisema kambi rasmi ya upinzani ina taratibu zake na moja ya taratibu ni kwamba kama mjumbe wa kambi haendani na matakwa ya kambi, moja ya adhabu ni kuzuiwa kuingia kwenye vikao.

"Zitto anaweza kuzungumzia masuala ya chama mahali popote. Amri ya Mahakama inasema KamatiKuu au chombo kingine cha chama kisizungumzie wala kuamua uanachama wake … haijamziba mdomo kuzungumza masuala ya chama kama ambavyo mimi nawezakuzungumzia mambo ya chama," alisema Mwanasheria huyo.

Pamoja na pingamizi la muda alilopewa Zitto na Mahakama Kuu, kisheria hudumu kwa miezi sita, lakini kuna uwezekano wa mbunge huyo kumaliza ubunge wake kwa kutumia amri hiyo ya Mahakama.

Baadhi ya wanasheria waliozungumza na gazeti hili jana, walisema licha ya sheria ya sasa kusisitiza kuwa pingamizi la muda lidumu kwa miezi sita, lakini iwapo kesi yake ya msingi ambayo imefunguliwa mahakamani itakuwa haijaisha, mbunge huyo anaweza kuomba kuongezwa pingamizi hilo kwa miezi sita mingine.

"Kisheria pingamizi hili linaweza kudumu kwa mwaka mmoja, yaani kwa vipindi viwili tofauti," alisema mwanasheria maarufu Alex Mgongolwa.

Mgongolwa na Mkurugenzi wa Kituocha Haki za Binadamu, Hellen Kijo-Bisimba wote walikubali kuwa mbunge huyo anaweza kumaliza muda wake wa ubunge chini ya amri ya Mahakama iwapo ataendelea kuomba zuio la muda, kutokana na hali itakavyokuwa ndani ya chama chake.

Mgongolwa Mgongolwa akifafanua jambo hilo, alisema mwaka mmoja wa pingamizi hilo ukiisha, ni wazi kuwa kama Chadema itakuwa bado inahitaji kumhoji ni wazi kuwa itamwandikia barua yenye tarehe ya wakati huo."Kisheria hilo ni jambo jipya, hivyo mlalamikaji anaweza kwenda tena mahakamani kuomba zuio lingine lamuda kwa jambo ambalo anaitiwa na chama chake kama jambo jipya,"alisema.


"Kwa macho ya haraka unaweza kudhani pingamizi mwisho wake ni mwaka mmoja, lakini sisi tunaotafsiri sheria, tunaona pingamizi la Mahakama linaweza kudumu hata miaka mitatu … ukitaka kuamini angalia suala la Hamad Rashid Mohamed wa CUF amemaliza miaka miwili sasa chini ya zuio la Mahakama," alisema Mgongolwa. Lakini alisema utoaji amri hiyo ya zuio la muda ni utashi wa Mahakama itakavyoona kwa hali ilivyo wakati huo. Lakini pia amri hiyo inatolewa tu iwapo mlalamikaji ataomba, na Mahakama inaweza kumpa tuzo hiyo au kumnyima.

Bisimba Katika ufafanuzi wake, Bisimba alisema Zitto anaweza kuendelea kupumua kwa nguvu za Mahakama iwapo atakuwa na hoja ambazo zitaishawishi kuendelea kumpa tuzo hiyo ya zuio la muda.

Alisema kesi ya msingi ambayo iko Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kama itakuwa haijaisha kusikilizwa, miezi sita ya awali ikimalizika, Zitto ana haki ya kuomba miezi mingine sita; lakini awe na hoja ya msingi ambayo itaishawishi Mahakama.

"Mahakama inaweza kukataa kama itaona hakuna hoja za msingi na kama mazingira ya kufunguliwa kwakesi hiyo yatakuwa yamebadilika," alisema mwanasheria huyo.

Anguko Bisimba katika mazungumzo yake alisema siasa ni mchezo mchafu na vyama vya upinzani vimekuwa vinavurugika na kusambaratika hasaunapokaribia uchaguzi mkuu.

"Yaliyotokea NCCR-Mageuzi na TLP haikuwa bahati mbaya, vyama hivi vilipata kuwa na nguvu; lakini vilidhoofu na haya yanayoendelea ndani ya Chadema si bahati mbaya,"alisema Bisimba.

Alisema chama cha upinzani ambacho angalau Watanzania waliona kina nguvu ni Chadema, lakini anashangaa chama hicho sasa kinapita kwenye nyayo za vyama vingine ambavyo vilianguka.

Chanzo: Habari leo

MWANAMKE APEWA KICHAPO KWA KUCHELEWA KUPOKEA SIMU YA MUMEWE

MWANAMKE mkazi wa Kata ya Lubaga, Sophia Haji (22) Manispaa ya Shinyanga anadaiwa kupigwa na mumewe na kusababishiwa majeraha makubwa kwa kile kilichodaiwa alichelewa kupokea simu ya mumewe.

Polisi inamsaka mwanamume huyo,Daniel Daud ambaye kutokana na kipigo, mkewe alitokwa na damu nyingi sehemu za siri. Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema wanamtafuta mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Kwa upande wake, mwanamke huyoaliyelazwa Hospitali ya Mkoa Shinyanga, aliwaambia waandishi wahabari kwamba alipigwa kutokana na kuchelewa kupokea simu ya mumewe wakati akivuka ng'ambo ya barabara.

"Nilipofika nyumbani mume wangu alianza kunipiga," alisema.

Alisema alijitetea kwa mumewe, lakini hawakuelewana, na zaidi alimtuhumu kuwa ana uhusiano na mwanamume mwingine. Kwa mujibu wa Sophia, mumewe alimfungia ndani siku mbili huku akiwa na majeraha pamoja na kumnyima chakula.

"Mimi nilichelewa kupokea simu ya mume wangu kwa sababu nilikuwa navuka barabara ili kujiepusha na ajali, nilikuwa na wifi yangu mdogo, lakini nilivyofika nyumbani mume wangu akawa mkali wala hakunielewa na kuanza kunipiga," alisema.


Alisema wifi yake alimtetea, lakini mumewe aliendeleza kipigo. Alisema baada ya kipigo hicho kuzidi, wifi yake alipiga kelele na majirani walifika kuamua ugomvi huo.

Alisema ilipofika usiku, alihisi maumivu makali mwilini akamweleza mumewe ambaye hakumsikiliza, zaidi ya kumfungia ndani siku mbili. Anna Gilbert ambaye ni rafiki wa mwanamke huyo, alisema baada ya kukaa siku mbili bila kumwona, siku ya tatu aliamua kwenda nyumbani kwake na hakumkuta mumewe.

Alisema alisikia sauti ya mtu anayelia ndani na alipochungulia, alimuona yuko mahututi na alichukua jukumu la kumpeleka hospitali. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Dk Fredrick Mlekwa alikiri kumpokea mgojwa huyo.

Alisema alimfanyia matibabu katika vidonda vyake, ambavyo vilikuwa vinatoa usaha na alikuwa na majeraha sehemu za mapajani.

WAASI SUDAN KUSINI WADHIBITI MJI WA BANTIU

Waasi nchini Sudan Kusini wameanza harakati za kuulinda vikali mji wa Bentiu ambao waliutwaa kutoka kwa serikali wakiwa na hofu ya majeshi ya Serikali kuupigania.

Mwandishi wa BBC nchini humo Alastair Leithead anasema kua waasi wameanza kuleta vifaru ndani ya mji huo wenye utajiri wa mafuta huku majeshi ya serikali yakiendelea kuukaribia mji huo.

Maelfu ya watu wametafuta hifadhi katika kambi moja ya Umoja wa Matifa viungani mwa mji wa Bentiu.

Takriban watu 1,000 wameuawa tangu mapigano kuanza tarehe 15 Disemba mwaka jana.

Takriban watu 200,000 wameachwa bila makao kutokana na mapigano Sudan Kusini.

Mgogoro huu ulianza baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu makamu wake wa zamani Riek Machar, kwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi ya utawala wake. Madai aliyoyakanusga vikali.

Bwana Machar anaugwa mkono na waasi wanaoaminika kuwa 10,000, na wapiganaji wengine kutoka kabila lake.

Naye Salva Kiir anatoka katika kabila la Dinka ambalo ndilo kubwa zaidi Sudan Kusini.

Lakini viongozi hao wawili wana watu wanaowaunga mkono kutoka makundi pinzani licha ya mgogoro huo kuwa na hisia za ukabila.

Huku mzozo ukiendelea kutokotaSudan kusini na katika Jamhuri yaAfrika ya kati, mataifa ya Afrika yameanzisha jitihada za kutafuta njia za kusuluhisha mizozo hiyo.

Mkutano unaoendelea nchini Chad ni jitihada ya hivi karibuni katika kujaribu kuutatua mzozo katika Jamhuri ya Afrika ya kati, huku wanadiplomasia wa Kiafrika wanaokutana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa wakijaribu kuutatua ule wa Sudan kusini.

Wapiganaji katika nchi zote wanapuuza jitihada hizo, wapiganaji waliojihami hawaonekani kuwa na hamu ya kutafuta suluhu ya kisiasa na kufikia makubaliano.

Taasisi za kieneo na kimataifa zinahusika kwa kushindwa kuchukua hatua inayohitajika kwakasi. Lakini yanaonekana kukabiliwa na kazi kubwa katika maeneo tofauti Afrika, yalioathirika na mizozo mipya na ya zamani huko Mali, Congo , Somalia, Jamhuri ya Afrika ya katina sasa Sudan kusini..

WANAMGAMBO 38 WA BOKO HARAM WAUAWA

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wapiganaji 38 wa Boko Haram wakati wa mapambano dhidi ya kundio hilo katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi.Msemaji wa jeshi Kanali Muhammad Dule amesema kuwawanajeshi waliokuwa wanashika doria walitibua njama ya mashambulizi waliyokuwa nayo Boko Haram.

Walitaka kuwashambulia raia na wanajeshi katika eneo la Damboa, jimbo la Borno mapema asubhi ya leo .Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, wanajeshi walifanikiwa kuwaua wapiganaji 38 wa Boko Haram huku baadhi wakitoweka na majeraha mabaya.

Moja ya magari yaliyoharibiwa kwenye makabiliano hayo, lilipatikana likiwa na mitungi ya gesi, pamoja na vifaa vingine vya mashambulizi.

Silaha nyinginezo kama bunduki na risasi zilipatikana.

Mwanajeshi mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa kwenye makabiliano hayo.

Boko Haram, ni kundi linalosemekana kuwa la kigaidi kwa mujibu wa serikali za Marekani na Uingereza na limekuwa likipigana na serikali tangu mwaka 2009, likivamia shule ambazo zinafuata mitaala ya mataifa ya magharibi.

Wapiganaji hao pia wamekuwa wakishambulia shule na makanisa.

Serikali ya Nigeria mwaka jana ilitangaza sheria ya hali ya hatari katika jimbo la Borno, na majimbo mengine ya Yobe na Adamawa, katika juhudi za kukomesha ghasia na mauaji ya raia wasio na hatia.

Lakini juhudi za serikali zingali kuzaa matunda kwani kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara dhii ya raia na taasisi za usalama nchini humo.

AL-SHABAB YAHARAMISHA MATUMIZI YA INTERNET

Wanamgambo wa Al Shabaab wenye uhusiano na Al-Qaeda, wamesema kuwa wamepiga marufuku raia wanaoishi katika maeneo wanayodhibiti kutumia internet.

Wapiganaji hao wametoa onyo kwa kampuni zote zinazotoa huduma ya internet siku 15 kufunga biashara zao.

"kampuni yoyote au mtu yeyote atakayepatikana akipuuza onyo hilo atajulikana kama mtu anayewafanyia kazi maaduzi zetu,na ataadhibiwa kulingana na sheria za ziisilamu,'' ilisema taarifa ya kundi hilo ambayo ilitumwa kwenye mitandao yake.

Wanamgambo hao hutumia sheria kali za kiisilamu katika maeneo wanayotawala na kuwakamata watu mara kwa mara kwa tuhuma za kufanya ujasusi.

Internet hutumiwa sana nchini Somalia, taifa ambalo limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidiya miongo miwili, huku kundi hilo likionekana kuwa kikwazo kikubwa kwa amani.

Kundi la Shebab zamani lilikuwa likitawala katika sehemu kubwa za Kusini mwa Somalia na Kati, lakini likaondoa wapiganaji wake baada ya kushindwa na wanajeshiwa Muungano wa Afrika wanaopambana nao.

Majeshi ya Afrika ikiwemo wanajeshi kutoka Uganda, Burundi na Kenya, tangu hapo wamedhibiti sehemu kadhaa kutoka kwa wapiganaji hao.

Lakini mashambulizi ya kuvizia yanayofanywa na kundi hilo dhidiya maslahi ya majeshi ya serikali na yale ya kigeni, yameondoa matumaini ya kunusuru taifa hilo kutokana na vita vya miaka mingi.

SERIKALI YA A.KUSINI YATAKA KUHARAKISHWA KWA UCHUNGUZI WA MAUAJI YA KAREGEYA

Serikali ya Afrika Kusini imeamrisha kuharakishwa kwa uchunguzi kuhusu mauaji nchini humo ya aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Rwanda Patrick Karegeya.

Hadi sasa polisi wangali kumkamata hata mshukiwa mmoja kuhusiana na mauaji hayosiku tisa tangu kuuawa kwake.

Uchunguzi wa mapema unaonyesha kuwa kulikuwa na mvutano kati ya Karegeya na mtualiyemuua kabla ya kifo chake. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa sheria katika tamko la kwanza la serikali ya nchi hiyo tangu kutokea kifo cha Karegeya.Mapema leo Chama cha upinzani cha Rwanda National Congress leo kilitarajiwa kuandaa maandamano ya raia wa Rwanda wanaoishi Afrika Kusini hadi makao ya ubalozi wa taifa hilo mjini Pretoria kulalamikia mauajiya aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi Kanali Patrick Karegeya.

Karegeya alipatakina akiwa amefariki dunia katika hoteli moja mjini Johanesburg mwezi Disemba mwaka uliopita.

Wanaharakati wa upinzani kutoka Rwanda wanaoishi uhamishoni wamedai kuwa serikali ya Rais Paul Kagema huenda ndio iliyohusika na mauaji ya bwana Karegeya.

Ubalozi wa Rwanda nchini Afrika Kusini ulisema kuwa maandamano ya aina yoyote sio tisho kwa serikali ya Rais Kagame.

Karegeya alikuwa mkuu wa zamani wa ujasusi nchini Rwanda,na alipatikana amenyongwa katika hoteli moja mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Mjane wa Karegeya amesema kuwa atazikwa nchini humo.

Taulo iliyokuwa na damu ilipatikana katika chumba ambapo maiti ya Karegeya ilipatikana na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi. Hata hivyo hakuna mshukiwa yeyote aliyekamatwa.

Mauaji ya Karegeya, yamesababisha madai dhidi ya serikali ya Rais Kagame kusema kuwa huenda ilihusika na mauaji hayo.

Karegeya alikuwa mshirika wa karibu sana wa Kagame kabla ya kutofautiana naye.

MALIASILI YAWASIMAMISHA 21

Wizara ya Maliasili na Utalii, imewasimamisha kazi watumishi wake 21 kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaidia ujangili wa nyara za Serikali.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Polisi mkoani Singida, kumkamata ofisa wanyamapori katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili na nyara za Serikali, kinyume cha sheria.

Akitangaza hatua hiyo jana jijini Dares Salaam, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema Serikali inasikitishwa na vitendo viovu vinavyofanywa na watumishi wake na haitavivumilia.

"Tumesikitishwa na kitendo cha ofisa wanyamapori wilayani Singida kukamatwa na bunduki mbili na ndege aina ya Heroe 12 nyumbani kwake, hatua tuliyochukua ni kumsimamisha kazi na kufikishwa mahakamani," alisema na kuongeza:

"Wizara baada ya kufanya uchunguzi, imegundua kuwa kuna watumishi wanaoshirikia na na mtandao wa ujangili, hivyo imewasimamisha kazi watumishi 21 wa Idara ya Wanyamapori na tutachukua hatua zaidi."

Alisema kati ya watumishi hao, 11 wanatoka katika Kikosi cha Kuzuia Ujangili mkoani Arusha, wanne wanatoka Mkoa wa Rukwa katika Pori la Akiba la Lwafu, mmoja Kikosi cha Bunda, watatu Pori la Akiba la Maswa, mmoja Selous, na mwingine mapori ya Lupika, Lumesule na Lusangu.

Akifafanua kuhusu uhaba wa watumishi katika Idara ya Wanyamapori, Nyalandu alisema kwa zaidi ya miaka 10 wizara hiyo haikuwa ikiajiri watumishi hali inayosababisha kukosa watumishi wenye ujuzi.

"Tunajipanga kuajiri watumishi wengine wenye ujuzi na kuangalia maendeleo ya teknolojia hasa kwa kujifunza kwa wenzetu Afrika Kusini," alisema.

Kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili, alisema Serikali imeunda tume ya kimahakama itakayowahoji askari waliohusika na kurudisha taarifa. Hata hivyo alisema wako mbioni kuendelea nayo.

"Rais Jakaya Kikwete ameunda tume ya kimahakama na itatoa taarifa, ila sisi hatutalala, tutahakikisha kuwa tunapambana na ujangili ili kulinda nyara za Taifa," alisema Nyalandu.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wizara yake kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kuwakamata wahalifu."

Jitihada hizi siyo zetu wenyewe, tunashirikiana na vyombo vya ulinzina usalama.

Tunawaomba wananchi washirikiane kulinda na kutoa taariza zitakazowezesha kukamatwa kwa wahalifu.

Tunawaomba watumishi wetu wafanye kazi kwa moyo na uaminifu," alisema Nyalandu.

WAUMINI WASHAMBULIWA MSIKITINI

Watu waliojihami wameshambulia msikiti katika jimbo la Kano Kaskazini mwa Nigeria na kuwaua waumini watatu huku wakiwajeruhi wengine 12.

Polisi wanasema kuwa watu hao waliwafyatulia risasi waumini waliokuwa msikitini katika kijiji anakoishi gavana wa jimbo hilo, Rabiu Musa Kwankwaso.

Babake gavana huyo alikuwa msikitini ingawa alinusurika kifo.

Hakuna mtu aliyewajibikia mashambulizi hayo lakini mmoja wa wasaidizi wa bwana Kwankwaso alisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi hatua ya gavana huyo kuhama chama tawala.

Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram, pia lilifanya mashambulizi kadhaa kama hayao mjini Kano, na katika maeneo mengine mbali mbali Kaskazini mwa Nigeria.

Haijulikani ikiwa Rais Goodluck Jonathan wa chama cha PDP atawania tena urais mwaka ujao.

Kipindi hiki ambapo watu wana hamasa z akisiasa hukumbwa na visa kama hivi vinavyotokana baina ya makundi hasimu ya kisiasa.

Bwana Kwankwaso alikuwa miongoni mwa watu watano mashuhuri waliokihama chama cha PDP na kujiunga na chama cha upinzani cha All Progressives Congress mnamo mwezi Novemba.

Heshimu Suleiman, msaidizi maalum wa gavana huyo alisema kuwa, shambulizi hilo lilinuiwa kumuadhibu bwana Kwankwaso kwa kukihama chama tawala.

Hata hivyo chama cha PDP bado hakijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.

Mnamo mwezi Disemba, rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo alisema itakuwa kwenda kinyume na maadili kwa Rais Jonathan kuwania tena urais mwaka ujao.

Alisema Rais Jonathan ameshindwa kushughulikia matatizo yanayokumba Nigeria ikiwemo Ufisadi na hata kushindwa kukabiliana na kundi la wapiganaji la Boko Haram ambalo limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara.

HELKOPTA YAANGUKA NA KUUWA WANNE

Helikopta ya Jeshi la Marekani imeanguka na kuua watu wanne katika pwani ya Norfolk ambako wanajeshi wa jeshi anga la Marekani walikuwa katika mazoezi.

Taarifa zinaeleza kuwa helikopta hiyo yenye namba HH-60G aina ya Pave Hawk ilikuwa imebeba zana za kivita na ilitaka kutua eneo la mchanga ufukweni mwa bahari kaskazini mwa kambi ya jeshi ya Norfolk.

Suzanne McKnespiey ni mmoja wa wafanyabiashara karibu na eneo la Norfolk anasema walisikia mlio mkali wa ndege hiyo kisha wakaona helikopta ikizunguka ovyo baharini na baadaye kishindo kikubwa.

Vikosi vya uokoaji na wanajeshi bado wapo katika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi huku raia wakiwa wamezuiwa kufika katika eneo hilo kwa usalama wao dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mabaki ya silahazilizokuwa katika helikopta hiyo.

Eneo lenye ukubwa wa mita 400 katika pwani hiyo ya Norfolk limewekewa vizuizi, ambapo afisa wa polisi Sarah Hamlin wa kituo cha polisi cha Norfolk, ametahadhalisha raia kutofika eneo hilo kipindi hiki cha uchunguzi.

MAJESHI YA DRC YAPAMBANA NA WAASI WA MAI MAI MJINI LUBUMBASHI

Takriban watu 26 waliuawa Jumanne katika mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi katika mji wa Lubumbashi nchini DRC.

Wanajeshi walipambana na waasi hao Jumanne asubuhi baada ya makabiliano makali yaliyoendelea usiku kucha.

Mji huo wenye zaidi ya watu milioni moja ulihamwa na wengi waliokuwa wanakimbilia usalama wao.

Mashambulizi yalianzishwa na kundi la waasi wa Mai Mai Kata Katanga, kundi linalotaka Lubumbashi kujitawala.

Waasi hao wanasema kuwa wanapigania uhuru wa mkoa huo ulio na utajiri mkubwa zaidi nchini Congo.

Aidha kundi lenyewe linaongozwana Gedeon Kyungu Mutanga, aliye achiliwa wakati waasi hao walipovamia gereza la Lubumbashi na kuwaachilia huru wafungwa.

Mkoa wa Lubumbashi una kiwango kikubwa zaidi cha madiniya Cobalt duniani na pia huzalisha madini ya Copper kwa wingi.

Mkuu wa polisi wa Lubumbashi aliambia BBC kuwa watu 26 walifariki wakiwemo wanajeshi na waasi.

Wafanyabiashara walifunga biashara zao huku maelfu wakisalia majumbani kwao siku ya Jumanne.

Wanajeshi wa serikali hata hivyo walishika doria baada ya kuwashinda waasi nguvu na kuwasukuma nje zaidi ya mji huo.

Mwezi Machi mwaka jana watu 5 waliuawa wakati washukiwa wa kundi la Mai Mai walipouvamia mji wa Lubumbashi.

MAJAMBAZI WAMUUWA MWENZAO KWA RISASI

Watu wanaoaminika kuwa majambazi waliokuwa na silaha za moto, wamemuua mwenzao kwa kumpiga risasi usoni baada ya majambazi hao kujichanganya wakati wakiwa katika harakati za kutoroka.

Habari zilizopatikana jana zilisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:30 usiku eneo la Captown katika Manispaa ya Moshi baada ya jaribio la majambazi hao kupora katika duka la simu kugonga mwamba.

Habari hizo zilidokeza kuwa muda huo wakati mmiliki wa duka hilo, Ramadhan Sauko akijiandaa kufunga duka lake, waliingia watu wanne waliojifanya wateja na baadaye kumtolea bastola. Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alianzakupiga kelele za kuomba msaada ambapo mmoja wa majirani aliamua kufyatua risasi hewani ambayo iliwafanya majambazi watatu kukimbilia uchochoroni.

"Wakati wananchi wakijikusanya yule jambazi wanne akakurupuka kutoka kule dukani akakimbilia kuleuchochoroni kwa wenzake na ndipomlio wa risasi ulisikika uchochoroni," alidai shuhuda mmoja.


Inadaiwa majambazi wale waliamini aliyekuwa akiwafuata uchochoroni walikokuwa wamekimbilia kujificha alikuwa ni mmoja wa wananchi waliojitokeza kutoa msaada na ndipo walipompiga risasi. Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alipozungumza na wanahabari jana,alisema baada ya kusikika milio ya risasi, alionekana mtu uchochoroni akiwa amejeruhiwa kwa risasi.

Kamanda Boaz alisema baada ya uchunguzi na upekuzi, marehemu alitambuliwa kuwa ni Nicholaus Jacob Mushi (35), akiwa na bastola aina ya Browning yenye namba 043916 ikiwa na risasi nane.

Bastola hiyo imetengenezwa nchini Czech na kusajiliwa nchini kwa namba TZ.TAR 73647.

Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, kumbukumbu za polisi zinaonyeshamarehemu alikuwa mhalifu mzoefu na alishawahi kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuvunja na kuiba.

Kamanda Boaz alisema Polisi linaendelea na uchunguzi ikiwamo kuwatafuta watuhumiwa waliofanikiwa kutoroka kabla ya mauaji ya mshirika wao huyo.

MTOTO MCHANGA AOKOLEWA BAADA YA KUTUPWA CHOONI

Mtoto mchanga mwenye umri wa siku mbili amenusurika kufa baada ya mama yake mzazi, Hadija Pangani (29) Mkazi wa Kijiji cha Mpiruka Wilaya Nachingwea, Lindi kumfunga kwenye kiroba na kumtumbukiza chooni.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpiruka, Simon Rashidi alisema mtoto huyo aligunduliwa na Techla Sameul baada ya kusikia sauti ya kulia alipokuwa anajisaidi kwenye choo hicho.

Simon alisema baada ya kusikia kelele za mtoto huyo, Techla alitoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya kijiji hicho, ambao kwa pamoja na kushirikiana na jamii na kufanikiwa kumwokoa mtoto huyo ambaye alikutwa hai akiwa amezungushiwa gagulo na kufungwa kwenye kiroba.

Rashidi alisema wakazi wa eneo wakishirikiana na uongozi wa kijiji walifanya uchunguzi na kubaini kuwa mtoto huyo alikuwa wa Hadija kwa kuwa alikuwa na ujauzito kwa kipindi hicho.

"Tulimfuata na baada ya kumbana kwa maswali, alikiri kufanya unyama huo kwa madai kuwa ameelemewa na familia, kwani tayari ana watoto watatu kila mmoja na baba yake na hakuna hata mmoja anayetoa masaada.

Kamanda wa Polisi Lindi, George Mwakajinga alithibitisha kutokea katukio na kwamba mtuhumiwa atafikisha mahakamani.

FAMILIA YAZUA VARANGATI KORTINI

Mahakama ya Mwanzo mjini Sumbawanga mkoaniRukwa jana iligeuka uwanja wa mapambano kati ya Polisi wa Kituo Kikuu na familia ya Mzee Anastazio Sikombe (62) baada ya familia hiyo kuanza kuwashambulia polisi waliokuwa wakitaka kuwakamatwa kwa tuhuma za kuingia na kulima katika shamba la mtu mwingine kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Polisi Mkoa wa Rukwa, tukio hilo lilitokea saa nne asubuhi ikiwa ni muda mfupi tangu mzee huyo akiwa na familia yake ya watoto watano wawasili katika viwanja vya mahakama hiyo kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa shauri jingine ndipo polisi mmoja alipotaka kuwakamata kwa madai walilima kwenye shamba la Ernest Mwanisenga (49) kinyume na sheria.

Taarifa zinaeleza kuwa polisi huyo alipojaribu kuwatia nguvuni familia hiyo ikiongozwa na mzee huyo walianza kumshushia kipigo polisi huyo, lakini ghafla polisi wengine wapatao sita walijitokeza na kuanza kumsaidia mwenzao kwa kupambana na familia hiyo, sakata ambalo lilidumu kwa zaidi ya dakika saba hadi kumi na kuwafanya watu kutoka katika vyumba vya mahakama ambako mashauri yalikuwa yakiendelea na kwenda kushangaa tukio hilo.


Baadhi ya watu walioshuhudia tukiohilo walisema kuwa mapambano hayo kati ya familia hiyo na polisi yalikuwa makali kwani wanafamilia hao walikuwa wakijihami kwa kutumia silaha za jadi kama fimbo na marungu, lakini walidhibitiwa napolisi hao kiasi cha mwenzao mmoja kuzimia kwa dakika kadhaa ambapo muda mfupi baadaye gari yao aina ya Defender lilifika na kuwachukua watuhumiwa hao na kuwafikisha kituo cha polisi.

MOYES AANZA KULALAMIKIA WAAMUZI

Meneja wa Manchester United, David Moyes amedai kuwa timu yake inacheza dhidi ya waamuzi pamoja na timu pinzani baada ya kushuhudia vijana wake wakipoteza mchezo dhidi ya Sunderland katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Capital One.

Kocha huyo wa Manchester United alisikitishwa na uamuzi wakuipatia Sunderland penalti na hivyo kuiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

"Tunacheza dhidi yao(waamuzi) na timu pinzani kwa wakati mmoja," ameiambia Sky Sports."Kwa kweli inatisha. Tunaanza kuwacheka kutokana na maamuzi wanayotoa."

Mwaamuzi wa mchezo kati ya Manchester United na Sunderland, Andre Marriner aliwapa penalti wenyeji akishauriwa na mmoja wa wasaidizi wake baada ya Adam Johnson kuanguka katika eneo la hatari alipokabiliana na Tom Cleverley wa Manchester United.

Sunderland iliongoza kipindi cha kwanza cha mchezo kupitia kwa Ryan Giggs, aliyejifunga goli.

Japo kuwa Nemanja Vidic aliisawazishia timu yake mara baada ya kuanza kipindi cha pili, penalti iliyotolewa kwa vijana wa Borini, kunawapa Paka Weusi hao, "Black Cats" kuingia na ushindi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa tarehe 22 Januari katika uwanja wa Old Trafford.


Katika kipindi cha wiki moja, Manchester United imeshuhudia kipigo kingine katika michezo ya kuwania vikombe huko England. Timu hiyo tayari imeng'olewa katika mashindano ya kuwania kombe la FA baada ya kucharazwa mabao 2-1 na Swansea.

Mapema mwezi huu Moyes alisema ilikuwa "kashfa" kwa Manchester United kunyimwa penalti dakika za mwisho katika mechi yao ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England dhidi ya Tottenham.

Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Old Trafford, Manchester United ilitunguliwa mabao 2-0.Hii ni mara ya kwanza kwa Manchester United tangu tarehe 22-26 Aprili 1992 kupoteza michezo mitatu ndani ya wiki moja.

PUNTLAND YAPATA RAIS MPYA

Wabunge katika jimbo la Puntland nchini Somalia wamemchagua waziri mkuu wa zamani wa Somalia Abdiweli Muhammad kama Rais mpya wa jimbo hilo linalojitawala ingawa linasema liko chini ya Somalia.

Abdiweli, alimshinda Rais Abdirahman Muhammad Farole kwa kura 33 kwa 32 katika duru ya tatu na ya mwisho kutokana na wagombea kukosa kupata zaidi yathuluthi moja ya kura zilizohitajika kuibuka mshindi.

Hali ya usalama ilidhibitiwa vikali wakati wa uchaguzi huo ambapo ni wabunge waliomchagua Rais mpya.

Wagombea 11 waligombea katikaduru ya kwanza lakini ni wagombea watatu pekee waliofanikiwa kupata idadi kubwaya kura na kwenda katika awamu ya pili na ya tatu.

Farole alifanikiwa kupata kura 27 kati ya kura 66 katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wenyewe huku Ali akipata kura 13.

Katika awamu ya pili,Farole alipata kura 31, Ali akapata 18 huku mgombea wa tatu Warsame akipata kura 16. Warsame, kutokana na kupata kura chache zaidi katika awamu ya pili hakuweza kufanikiwa kwenda katika raundi ya tatu.

Hii ni mara ya tatu kwa Puntland kufanya uchaguzi kama huu tangu kujitenga na Somalia mwaka 1998.

Bunge la jimbo hilo lina wabunge66 waliochaguliwa na wazee wa kikoo mwaka 2013.

Ali, alikuwa waziri mkuu wa Somalia kati ya Juni mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012.

IDADI YA WAVUTA SIGARA YAONGEZEKA DUNIANI

Idadi ya wavutaji wa sigara duniani imeongezeka kwa karibu bilioni moja kwa mujibu wa takwimu mpya.

Watafiti walioandika katika jarida la Shirika la madaktari la Marekani wanasema hata hivyo kuwa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ongezeko la watu kwa ujumla duniani na kuelezea haja ya juhudi zaidi kufanyika kuwazuia watu kuwa natabia hiyo.

Idadi ya watu wanaovuta sigara kila siku duniani imepanda kwa kiwango cha watu takriban milioni 250 million kati ya mwaka 1980 na 2012, kwa mujibu wa ripoti.

Katika nchi kama vile Urusi, Indonesia na Timor ya Mashariki, zaidi ya nusu ya wanaume wana tabia ya kuvuta sigara kila siku.

Baadhi ya maeneo yenye idadi ndogo ya wavutaji wa sigara ni katika visiwa vya Caribbean vya Antigua na Barbuda ambapo mtu mmoja kati ya 20 huvuta sigara kila siku.

Watafiti wanasema kuongezeka kwa kiwango cha wavutaji wa sigara kinatokana na ongezeko la watu duniani.


Lakini licha ya kuongezeka kwa kiwango cha uvutaji sigara , kiwango cha watu wanaovuta sigara duniani kimepungua. Idadiya Wanaume wanaovuta sigara imepungua kwa asilimia 10 tangumwaka 1980, na wanawake wamepunguza uraibu huo kwa asilimia 4.

Shirika la afya duniani linasema vifo vya mamilioni ya watu vinaweza kuepupika kwa nchi zaidi kuweka hatua kama vile kuongeza kodi ya sigara, kupiga marufuku uvutaji sigara katika maeneo ya umma na kuweka onyo kwenye paketi za sigara.

RODMAN ATETEA ZIARA YAKE KOREA KASKAZINI

Mchezaji mashuhuri za zamani wa mpira wa vikapu nchini Marekani Dennis Rodman ameteta vikali ziara yake ya Korea Kaskazini kabla ya mechi maalum ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un.Katika mahojiano na shirika la habari la CNN, alihojiwa kuhusu ikiwa atazungumzia swala la mfungwa wa Marekani aliye kizuizini nchini humo.

Jibu la Mchezaji huyo wa zamani lilionekana kumlaumu mfungwa huyo Kenneth Bae kwa masaibu yanayomkumba.

Ziara ya Rodman, imekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu, huku Marekani ikisema kuwa Rodman hawakilishi Marekani katika ziara yake.

Wachezaji wa iliyokuwa timu yakeya zamani ya NBA watamenyana na timu ya Korea Kaskazini katika mechi ya maonyesho siku ya Jumatano mjini Pyongyang.

Rodman anasema kuwa mechi hiyo ni ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais Kim Jong-un, ingawa siku rasmi ya kuzaliwa kwake pamoja na umri wake haijatangazwa rasmi.

Aidha ziara ya Rodman inakuja wiki chache baada ya kuuawa kwamjombake Kim , Chang Song-thaek, ambaye wakati mmoja alioenekana kama mtu shupavu.

Kuuawa kwake kulizua wasiwasi kuhusu uthabiti wa nchi hiyo.

Wakati huohuo, uchaguzi wa wabunge nchini humo utafanyika tarehe 9 mwezi Machi.

Wadadisi wanasema uchaguzi huo utatoa ishara ya nani wanasiasa wenye ushawishi mkubwa hasa baada ya Bwana Chang kuuawa.

MORSI KUPANDISHWA TENA KIZIMBANI

Vikosi vya usalama vimeimarisha ulinzi katika mji mkuu wa Misri Cairo , kabla ya kufikishwa mahakamani kwa rais aliyeng'olewa madarakani , Mohammed Morsi.

Yeye na maafisa kadhaa wa serikali yake wanashutumiwa kuchochea ghasia na kuwauwa waandamanaji mwaka 2012 wakati wa utawala wake. Mashitaka hayo ni pamoja na kushirikiana na wanamgambo wa kigeni kuvunja gereza.

Aling'olewa madarakani kwa mapinduzi mwezi julai mwaka jana na kufungwa.

Alipofika mahakamani Mwezi Novemba mwaka jana bwana Morsi alisema kuwa bado yeye ni rais na alifungwa kinyume na matakwa yake.

MWANAMKE MMOJA AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA JNIA

MWANAMKE Mtanzania, Salama Omari Mzale, amekamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini China.

Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.
Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege.

Hadi saa 1 jioni (mida ya Tanzania); mwanamke alikuwa ameshusha kete 63 kwa njia ya haja kubwa

AFISA WANYAMA PORI AKAMATWA NA NYARA SERIKALI NA SILAHA

Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia afisa Wanyamapori katika halmashauri ya Wilaya ya Singida Augustino Lorry kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili na nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi mwandamizi wa Polisi Geofrey Kamwela, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Jumatatu majira ya saa kumi na moja na nusu jioni nyumbani kwake akiwa na bunduki moja ya Rifle na nyingine Shot Gun na ndege 12 aina ya Flamingo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Kamwela amesema siku ya tukio polisi walipata taarifa za siri kutoka kwa raia wema kuwa afisa huyo mwenye dhamana ya kulinda na kutunza maliasili za nchi anamiliki silaha kinyume cha sheria na kufanya biashara ya nyara za Serikali.

Amesema mbali na kumkamata afisa wanyamapori, pia wanamhoji mtu mwingine anayesadikiwa kuwa ni mshirika wake.

Hata hivyo amesema uchunguzi wa kina zaidi unaendelea kufanywa juu ya tukio hilo.

Kamanda Kamwela amesema kuwa watuhumiwa hao wanatarajiwa kupandishwa kizimbani wakati wowote kujibu shitaka la kupatikana na silaha za moto na nyara za Serikali kinyume cha sharia

KIONGOZI WA UPINZANI ZAMBIA AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUMDHIHAKI RAIS

Kiongozi mmoja wa upinzani nchini Zambia, amekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kumchafulia jina Rais wa nchi hiyo Michael Sata baada ya kumfananisha na Viazi Frank Bwalya anadaiwa kumtaja Rais Michael Sata kama "chumbu mushololwa" kupitia kwa Redio sikuya Jumatatu.

Katika lugha ya Bemba, tamko hilo lina maanisha viazi vitamu ambavyo humegeka vinapopindwa , maana yandani ikiwa mtu ambaye hasikilizi ushauri wa wengine.

Bwana Bwalya anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela ikiwaatapatikana na hatia.

Aidha Bwalya ni kasisi wa zamani namfuasi wa zamani wa Rais Sata, ingawa sasa anaongoza chama cha muungano wa vyama vya upinzani (Alliance for a Better Zambia (ABZ).Naibu waziri wa mambo ya ndani, Stephen Kampyongo alisema kwamba, bwana Bwalya alikamatwa kwa kutoa matamshi ya kumharibia sifa Rais Sata.

''Rais Sata ni yule yule aliyekuwa anasikika kwenye vyombo vya habari habari akiwachafulia sifa marais wa zamani, Banda na Mwanawasa na hakuna aliyemkamata,'' alisema katibu mkuu wa chama cha ABZ Eric Chanda.

Viongozi wa upinzani wametaka Bwana Bwalya aachiliwe wakisema kuwa yeye ni mwanasiasa asiyemuogopa mtu.

Waliongeza kuwa matamshi ya Bwalya, "chumbu mushololwa" hayakuwa matusi.

Mnamo mwezi Sepetamba mwaka jana Nevers Mumba mwanasiasa mwingine wa upinzani, alihojiwa na polisi kwa kusema Rais Sata ni muongo.

30 WAUAWA NIGERIA

Watu 30 wameuawa katika kijiji kimoja eneo la kati mwa Nigeria katika jimbo la Plateu ambako kunaishi watu wa dini mbali mbali.

Kijiji hicho kiko katika eneo ambalo limekuwa likikumbwa na mzozo wa muda mrefu wa kikabila.

Duru zinaarifu kuwa watu waliokuwa wamejihami walishambulia kijiji cha Shonong nyakati za asubuhi Jumatatu huku wakiwapiga risasi wenyeji na hata kuteketeza nyumba zao.

Washambuliaji wanaoaaminika kutoka jamii ya Fulani pia waliiba mifugo.

Msemaji wa kijeshi katika eneo hilo alithibitisha mauaji hayo lakini akasema kuwa ni mapema mno kuelezea idadi kamili ya watu waliouawa, ingawa uchunguzi zaidi unaendelea kufanywa.

Maelfu ya watu wameuawa katikakipindi cha miaka mitatu katika mashambulizi ya kulipiza kisasi kati ya makabila hasimu katika mkoa wa kusini wenye wakristo na kaskazini wanakoishi waisilamu.

Vurugu katika eneo la Kati mwa Nigeria huchochewa na mizozo yaardhi kati ya jamii za wahamiaji mfano kutoka jamii ya Fulani na wakulima mfano watu wa jamii ya Berom ambao ni wakristo.

Idadi hiyo ya watu thelathini waliouawa inajumisha watoto na wanawake Maelfu ya watu wameuawa katika mizozo kama hiyo tangu mwaka 2010 lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwaserikali haijachukua hatua za kuridhisha kukomesha mizozo hiyo.

UHAMIAJI WAZUA MJADALA UK

Zaidi ya robo ya raia wa Uingereza wanataka kuona swala la uhamiaji likikomeshwa.

Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na BBC.Takwimu hizi ni za kustaajabisha. Asilimia 77 ya waliohojiwa wanasema wanataka uhamiaji kupunguzwa kiasi, zaidi ya nusu wanasema inafaa kukomeshwa kabisa.

Tangu mwaka 1997 karibu watu milioni 4 waliingia nchini Uingereza na maoni yanazidi kuonesha kuwa swala la uhamiaji ni tata sana Uingereza kuliko mataifa mengine ya muungano wa Bara Ulaya.

Lakini mgawanyiko wa kisiasa ungali ukishuhudiwa katika muungano wa kisiasa kuhusiana na swala hilo.

Katika mahojiano na BBC, Waziri wa chama cha Liberal Democrat anasema kuwa wale Conservatives wametangaza nia ya kupunguza uhamiaji iwe chini ya watu laki moja kwa mwaka haufai na haina maana.

Mhariri wamaswala ya kisiasa wa BBC anasema kuwa swala la uhamiaji limekuwa midomonmi mwa wengi Uingereza hasa uchaguzi mkuu ukitarajiwa mwaka ujao. Wengi wanaonekanakuunga mkono chama cha kisiasa cha UKIP chenye sera yake kuu ya inayopinga uhamiaji.

Chama tawala cha Conservative nacho kimeahidi kupunguza idadiya wahamiaji nchini Uingereza.

MTOTO WA MFALME WA HISPANIA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mwanawe wa mwisho mfalme Juan Carlos wa Uhispania amefikishwa mahakamani kwa madai ya kukwepakulipa ushuru na ulaji rushwa.

Princess Cristina anatazamiwa kufika katika mahakama ya Majorca mwezi Machi baada ya kushukiwa kutenda kosa hilo.

Mumewe Inaki Urdangarin, amekuwa akichunguzwa kwa mwakamzima sasa kwa kushukiwa kwa kosa la ubathirifu wa mamilioni ya Dola za umma zilizotolewa kushughulikia mradi wa kushughulikia jamii.

Amekanusha madai hayo.Mwanahabri wa BBC anasema kesi hiyo imedhalalisha jamii ya kifalme huko Uhispania na kuibua ukosoaji chungu nzima kutoka kwa raia wa taifa hilo.

MWENYEKITI CHADEMA TEMEKE ATEKWA NA KUPEWA KICHAPO

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam.

Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu naalikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyumtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.'Niliomba wasiniue, wamenipiga sana…

Wamenichukua saa tano nyumbani kwanguKwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja..

Tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso,wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote.

NAHODHA WA KILIMANJARO II AHOJIWA

Wakati watu saba wakiwa bado hawajaonekana baada ya boti ya Kilimanjaro II, kupata ajali na abiria kuzama baharini, nahodha wa chombo hicho alitoa taarifa za uongo kuhusu ajali hiyo imefahamika.

Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA), Mhandisi Abdi Omar Maalim, alisema taarifa iliyotolewa na nahodha katika kituocha mawasiliano zilikuwa za uongo na hivyo kusababisha kazi ya uokozikuchelewa.

Alisema baada ya boti hiyo kupigwa wimbi, abiria waliokuwa wamekaa juu waliteleza na kutumbukia baharini lakini nahodha katika ripoti yake alisema hakuna abiria waliotumbukia.

Alisema hata alipotakiwa kupewa msaada na Kituo cha Mawasiliano cha Zanzibar, alisema hahitaji kwa sababu vitu vilivyotumbukia bahari ni vifaa vya uokozi na mizigo.

"Nahodha alitoa taarifa za uongo nakusababisha zoezi la uokoaji kutokufanyika kwa wakati mwafaka, baada ya kutokea ajali hiyo," alisema Mhandisi Maalim.

Alisema ajali hiyo ilitokea saa 3:30 asubuhi lakini kazi ya uokoaji ilianza alasiri baada ya kupokea taarifa kutoka kwa abiria kuwa wenzao wamezama baharini baada ya meli kupigwa na wimbi.


Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Rashid Seif Suleiman amesema nahodha wa chombo hicho alianza kuhojiwa na polisi juzi. Alisema kazi kubwa inayofanyika sasa ni kutafuta watu ambao bado hawajaonekana na baada ya kukamilika ataamua kamakuna haja ya kuunda tume ya kuchunguza ajali hiyo.

Alisema baada ya uhakiki wa majina ya abiria waliosafiri na boti hiyo wamegundua kuwa jumla ya watu 15 walizama baharini baada ya boti kupigwa na wimbi na kusababisha injini kuzimika.

Waziri Seif alisema hadi jana maiti tano zimepatikana na watu watatu wameokolewa.

Msimamizi Mwandamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mnazimmoja, Vuai Jabir Hassan aliwataja marehemu kuwa ni Rashid Said Ali (11) mkazi wa Ilala Dar es Salaam, Akram Khamis Issa (11) wa Mwanakwerekwe, Masoud Hamad (30) wa Wete Pemba, Nushra Khamis (9) na Fatma Asir Khamis (18) wa Magogoni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Aliwataja waliookolewa kuwa ni Ali Maulid Haji (Mwanakwerekwe), Ali Salum Ali (Pemba) na Mahir Ali Issa(Mwanakwerekwe).

Wakati huohuo, huduma za usafiri kati ya Unguja na Pemba zimesitishwa kwa muda kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa katka Bahari ya Hindi. Habari zilisema hatua hiyo ni ya kiusalama.

MKONO ATOA UFAFANUZI DHIDI YA TUHUMA KWA ZITTO

Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ametoa ufafanuzi juu ya uhusiano wake na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

Hatua hiyo ya Mkono imekuja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumukuwa aliwahi kumpa Zitto magari mawili.


Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Mkono alisema kuna magari mawiliyanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.

"Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, FreemanMbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Chadema), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.

"Alisema alitoa gari hilo lililokuwa na Bendera ya Bunge liwachukue Mbowe na Zitto na kuwapeleka Mwanza... "Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia," alisema Mkono.

Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na mpaka sasa bado analipa gharama za kulikodisha..."Hata nyaraka za umiliki wa gari hilininazo mimi mwenyewe kama mmiliki halali.

Ninamiliki magari mengi tu hata wewe mwandishi ukitaka Vogue (aina ya gari) nitakukodisha tu," alisema Mkono.

Alisema wanafahamiana kwa siku nyingi hata kabla ya Zitto kuwa mbunge na kwamba aliwahi kufanya mazoezi kwa vitendo katikaofisi yake (Mkono), alipokuwa mwanafunzi.

Kuhusu tuhuma kwamba anawahonga wapinzani wake wajitoe katika uchaguzi ili apite bila kupingwa alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, 2005 na 2010 alipita bila kupingwa kutokanana uchapakazi wake wa kiwango kikubwa.

Mkono pia alijibu tuhuma zilizotolewa na Zitto jana kwamba Mbowe alipewa mamilioni ya fedhana Mkono kwa nyakati tofauti na kusema hajawahi kutoa fedha zozote kusaidia Chadema.

ZITTO AENDELEA KUWALIPUA VIONGOZI WA CHADEMA

"Lissu anasema nimepewa magari mbili na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono.

Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.

Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m zauchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.

Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni.

Lissu anajuakuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba.

Mzee Mkono ni Mzee wangu naalisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.

Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote.
Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze.

Aeleze aliingia deal ganina Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF.

Awekewazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.
They must know I am not a pushover. Chacha died, I won't.

Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."

SUDAN MBILI KUSHIRIKIANA KATIKA ULINZI WA MAFUTA

Sudan na Sudan Kusini zimejadili swala la kushirikiana katika kushika doria ili kulinda visima vya mafuta Sudan Kusini ambako waasi wanatishia usalama.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini.

Marais wa nchi hizo mbili wameanza mazungumzo ya kupeleka kikosi cha ulinzi ili kulinda visima vya mafuta Kusini ambako waasi wamezusha vurugu kwa karibu wiki nne sasa.

Taarifa hii inakuja baada ya Rais wa Sudan Omar Bashir kwenda mjini Juba kwa mashauriano na Rais Salva Kiir kuhusu mzozo wa kisiasa unaotokota nchini humo.

Mgogoro huo kati ya wafuasi wa Rais Kiir na hasimu wake Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa bwana Kiir ingawa alifutwa kazi pamoja na mawaziri wengine wa serikali.

Takriban watu 1,000 wameuawa kwenye mgogoro huo uliozuka tarehe 15 mwezi Disemba.

HUKUMU YA KIFO SOMALI.

Mwanajeshi mmoja nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi na kikundi cha wanjeshi na polisi mjini Mogadishu , baada yamahakama ya kijeshi kuamuru kuuawa kwake.

Uamuzi wa mahakama ulitokana na madai kuwa mwanajeshi huyo alimuua mwanafunzi mwaka jana.

Umati wa watu wakiwemo watoto walishuhudia kuuawa kwa mwanajeshi huyo, katika kituo cha mafunzo cha wanajeshi mjini Mogadishu kwa mujibu wa picha zilizowekwa kwenye mtandano wa kisomali wa redio Shabelle.


Hukumu ya mauaji nchini Somalia ni kifo.

Wanajeshi wa serikali mara kwa mara hutuhumiwa kwa kufanya vitendo vya uhalifu bila kujali ikiwemo mauaji na ubakaji.

Kituo cha Redio kiliripoti kuwa wanajeshi zaidi watakaopatikana na hatia ya mauaji huenda wakakabiliwa na adhabu sawa na hiyo katika siku zijazo.

Maslah Isse Jimaan alihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mwanafunzi wa shule katika soko rasmi la Bakara, alipokuwa anashika doria mwaka jana.

Aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi pamoja na wanajeshi kumi walioonekana katika picha hiyo kabla ya Jimaan, kufumbwa macho na kufungwa kwenye mlingoti na kisha kupigwa risasi mbele ya umati wa watu.

'Jimaan alikuwa amekiuka kanuni za jeshi, na hii ndio ilikuwa adhabu yake,' alisema mwenyekiti wa mahakama ya kijeshi Libaan Ali Yarow.

Hata hivyo bwana Yarow alisema kuwa hakua na habari kuwa Jimmah aliuawa mbele ya watoto.

WAHAMIAJI WAANDAMANA TEL AVIV

Maelfu ya wahamijai wa kiafrika, waliandamana mjini Tel Aviv Jumapili kupinga wanavyotendewa na serikali ya Israel.

Waandamanaji hao wengi wao wakiwa raia wa Eritrea na Sudan, wameghadhabishwa na sheria ambazo zinaruhusu kuzuiliwa kwawahamiaji haramu kwa mwaka mmoja bila ya kufunguliwa mashitaka.

Aidha wanataka kupewa haki ya kufanya kazi huku wakishinikiza serikali kuharakisha maombi yao ya kupewa uraia.

Msemaji mmoja wa serikali alisema kuwa maandamano yao yalifanywa kwa njia ya amani."sote ni wakimbizi na ndio tunataka uhuru wala hatutaki kufungwa, '' walisema wahamiaji hao.

Mwandishi wa BBC mjini Jerusalem, Richard Galpin, anasema kuwa maandamano yalichochewa na sheria ya kuwazuilia wahamiaji haramu ambayo iliwaondolea matumaini wengi waliotarajia kuwa serikali ingesitisha kabisa msako dhidi ya wahamiaji haramu.

Wahamiaji hao ambao wengi wamekuwa wakiishi Israel kwa miaka mingi na wanaofanya kazi za kipato cha chini, wanasema wote ni wakimbizi ambao wametoroka nchi zao Eritrea na Sudan kutokana na mateso.

Wanasema kuwa hali yao sasa kutoakana na sheria hiyo watalazimika kuishi jela au kurejea nyumbani.

Kutokana na hatari wanazokabiliwa nazo nyumbani kwao, ina maana kuwa hawawezi kurejeshwa makwao kwa nguvu.

Wahamiaji hao wamesema kuwa watafanya maandamano zaidi njeya ofisi za Umoja wa Mataifa na balozi za nchi za kigeni mjini Tel Aviv siku ya Jumatatu.

KITILA NA MWIGAMBA WAFUKUZWA CHADEMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewavua uanachama, aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu Dr.Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba kwa kosa la uhaini ndani ya chama.

Pia uongozi wa Chadema umewapiga marufuku wanachama wake kushiriki katika mikutano ya Zitto Kabwe, kwa madai ya kukiukakatiba ya Chama na kwenda mahakamani kuzuia vikao vya kamati kuu kutojadili ajenda zake.

BOTI YA AZAM KILIMANJARO II YANUSURIKA KUZAMA NUNGWI

Kwa mujibu wa Abiria waliohojiwa wanasema Boti ya Kilimanjaro II ikitokea Pemba kuelekea Unguja imepigwa na dhoruba leo Jan 5 2014 kwenye saa nne asubuhi na kuponea kuzama ilipokua kwenye eneo hatari la Nungwi ambapo ilizama kidogo mbele na kunyanyuka hivyo watu wa mbele wote wakaachwa lakini pamoja na kuwatupa hao watu kwenye maji Nahodha akafanya uamuzi mwingine mgumu.

Aliona akisimama ili kuwaokoa wale watu boti yote ingezama pale hivyo akaamua kuendelea na safari lakini kabla ya kuondoka watukadhaa ndani ya boti wakajitolea kuwatupia life jacket wale waliotupwa kwenye maji ambapo shuhuda anasema kama mtu hajui kuogelea anaweza kupoteza maisha kwa sababu hawakua wamejiandaa kwenye tukio hili la ghafla na sio wote wamepata vifaa hivyo vya kujiokoa.

Shuhuda mmoja anasema 'yani boti ilizama ghafla mbele hivyo watu wakatupwa kwenye maji kwenye hii sehemu ambayo kuna mkondo wa maji, upepo ulikua mkali sana yani unaonawatu wanajaribu kujiokoa mabegi na vitu vingine vinaonekana juu ya maji'Hali ilivyo ndani ya boti ambayo imeendelea na safarini watu kujawa na huzuni na wengine wamebaki wanalia tu.

Boti hiyo ina zaidi ya abiria 600 na chanzo ni upepo mkaliambapo mmoja wa abiria aliehojiwa na Clouds FM amesema toka mwanzo alikua na wasiwasi na safari ya leo manake bahari haijatulia kabisa ambapo kwa sasa abiria wote wamepewa life jacket.

Chanzo: Millard Ayo

PENGO AHOFIA SERIKALI TATU

MUUNDO wa serikali tatu uliomo ndani ya Rasimu ya Katiba iliyokabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwanzoni mwa wiki hii, umezua hofu kwa baadhi ya viongozi wa dini nchini, wakisema huenda ukachangia kuvunjika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka 50 sasa.

Aidha, mawazo ya kutaka serikali tatu yameelezwa yanatokana na watu kutokuwa na upendo wa kutosha na hofu ya Mungu.

Hayo yalisemwa jana na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuula Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati waufunguzi wa ibada ya misa ya shukrani, iliyoandaliwa na Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Alisema wanaolalamika juu ya muungano wa sasa wana yao, kwa kuwa unawazuia kufanya mambo yao wenyewe na kuingia mikataba kwa manufaa yao wenyewe."Kutokana na kuona kuwa wenzao ni kuzuizi, wanalalamika kwa kuwa Muungano unawazuia watu kuingia mikataba kama ya OIC (Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu).

Sidhani kama huu ni umoja," alisema Pengo na kuongeza kuwa, "Hofu yangu kubwa ni kwamba, kuwa na serikali tatu ndio mwisho wa Muungano. Tuombe ili tufikie malengo ya umoja."Alisema inapofikia hatua ya watu kuwaona wenzao kama ni mzigo nakutaka kujitenga haipendezi hata machoni pa Mwenyezi Mungu, badala yake wanapaswa kukaa na kuzungumza ili kujenga umoja thabiti, badala ya kufikiria kujitenga.

Hata hivyo alitoa mwito kwa wanasiasa na wananchi wote kuombea upendano na umoja katika vyama vya siasa ili vifikie maamuzi yaliyosahihi ya haki na yenye kujenga taifa.

Alisema ubinafsi ndio unaochocheamifarakano katika vyama; na watu kujitokeza tu kujitangaza uongozi bila chama husika kukubaliana hali inakuwa mbaya zaidi.

"Kamati za chama zikae kwa haki, ziseme zinamteua nani kwa sifa alizonazo kugombea nafasi fulani la hasha mtu mmoja anajitokeza na kuanza kusema anagombea nafasi fulani bila matakwa ya chama matokeo yake yanakuwa mabaya sana," alisema Pengo.

Katika misa hiyo iliyoongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe, WAWATA walitoa matoleo kwa wagonjwa walioko Taasisi ya Saratani ya Ocean Road yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni nane.

Askofu Mdoe aliwaasa WAWATA kuwa walezi bora wa familia ili watoto wanaotoka katika familia zao wawe na maadili na hofu ya Mungu.
Alisema pia wanatakiwa kuwa kioo cha kutenda mema popote walipo bila kujali ni kazini, nyumbani au barabarani.

"Mama uwe mstari wa mbele kutimiza wajibu wako na kutenda yale ambayo ni haki kwa wote, na haki ya msingi kwa mtoto ni malezimema.

Mkishindwa kuwalea vema watalelewa na ibilisi na atawapa misingi ya kiibilisi, unatakiwa uwe mwakilishi mzuri sana wa Kristo popote ulipo, iwe kazini, mtaani, nyumbani au njiani," alisema Askofu Mdoe.

Alisema katika kumshukuru Mungu kumaliza mwaka na kuwezesha kuanza mwaka mpya wapambane na changamoto walizozipata mwaka uliopita ili kuimarisha imani na umoja wao na pale walipoharibu wamwombe Mungu awaongoze na kuwatia nguvu.

JESHI LA POLISI LAWASHIKIRIA ASKARI MAGEREZA KWA WIZI

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watu watano wakiwemo askari Polisi na mwingine wa Jeshi la Magere za wakihusishwa na tukio la kumteka na kumpora mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia zaidi ya Sh milioni 3.7.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, waliokamatwa ni pamoja na Sajenti Juma Musa (38), askari Magereza Gereza la Ruanda, Mbeya na PC James (32), askari Polisi wa Mbeya.

Wengine ni Mbaruku Hamisi (29), Amri Kihenya (38) na Elinanzi Mshana (29), wote wakazi wa Forest, jijini Mbeya.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Msangi alisema watuhumiwa hao walikutwa na baadhi ya mali walizopora ambazo ni mabegi matatu ya nguo, simu moja ya kiganjani aina ya Samsung na Laptop moja aina ya Samsung.

Alisema vifaa hivyo vilikutwa kwenye gari aina ya Toyota Grand Mark II aina ya GX – 6011835 hukublangeti mbili zikikutwa kwenye buti la gari Toyota Crest GX 100 lenye namba za usajili T 782 BEU.

Alisema tukio hilo la unyang'anyi lilitokea juzi jioni majira ya saa 11:35 katika eneo la Mlima Kawetele Wilaya ya Mbeya Vijijini ambako watu hao walimpora Speedhar Pasupeleti (38) mwenye asili ya Kihindi, mkazi wa Makata wilayani Chunya.

Kamanda Msangi alisema mfanyabiashara huyo akiwa na wenzake wawili kwenye gari aina ya Toyota Pick Up lenye namba za usajili T 756 ABL, alinyang'anywa pesa zaidi ya Sh milioni 3.7 baada ya waporaji kuweka magogo barabarani ili kuzuia magari yasipite.Mbali ya pesa, waliiba pia begi lililokuwa na nguo na vitu mbalimbali baada ya kuwatishia Pasupeleti na wenzake kwa kutumia silaha.

Kutokana na tukio hilo ambalo uchunguzi wake unaendelea, Kamanda Msangi ameitaka jamii kujiepusha na tamaa ya kusaka utajiri wa haraka kwa njia zisizo halali, huku ahimiza watu kufanya kazi halali ili kujiingizia kipato.

Katika tukio jingine, Kamanda Msangi alisema, siku hiyo hiyo mchana, mtoto wa kike mwenye umri wa miezi 10 alikufa katika ajali ya gari iliyotokea mkoani ikihusisha lori la mafuta aina ya Scania na basi dogo aina ya Toyota Hiace.

Watu 13 walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao tisa wakiwa wanawake.

Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Hospitali Teule ya Ifisi, Kata ya Songwe, Tarafa ya Bonde laSongwe wilayani Mbeya Vijijini ambapo gari lenye namba za usajiliT 330 ACK na tela lenye namba T 422 ACK aina ya Scania likiendeshwa na Yusuph Fakhi (45) mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam likitokea Mbeya kuelekea Tunduma liligonga gari lenye namba za Usajili T 897 ALH aina yaToyota Hiace.

Alisema gari lililogongwa lilikuwa ikiendeshwa na Musa Hamisi (25) Mkazi wa Iyunga, mjini Mbeya na kusababisha kifo cha mtoto huyo ambaye bado hajafahamika wala wazazi wake.

Alisema majeruhi wawili wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya na wengine 11 wamelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi akiwemo dereva wa Hiace na hali zao zinaendelea vizuri. Chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa huku dereva wa Scania akiwa anashikiliwa na Polisi.

Chanzo:Habari leo

MAZUNGUMZO YA AMANI SUDAN KUSINI YAKWAMA.

Matumaini ya kupatikana kwa amani Sudan Kusini yameingia mashakani baada ya mazungumzo ya uso kwa uso ya pande zinazopingana yaliyokuwa yakitarajiwa kufanyika nchini Ethiopia kuchelewa.

Waziri wa Mambo ya nje wa Ethiopia Tedros Adhanom amesema mazungumzo hayo yaliyokuwa yafanyike siku ya jumamosi hayatafanyika kama ilivyokuwa imetarajiwa.

Amesema mikutano inaendelea mjini Adis Ababa ili kuandaa agenda za mazungumzo hayo ya uso kwa uso ya pande zinazopingana.

Mwandishi wa BBC aliyepo Juba anasema mapigano makali yanaendelea.

Ambapo pia majeshi yanayomuunga mkono rais Salva Kiir nayo yanajiandaa kwa mashambulizi katika eneo la Bentiu na Bor miji ambayo kwa sasa inashikiliwa na wafuasi wa Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa zamani.

Amesema pande zote zinajaribu kuimarisha udhibiti wa kijeshi kabla ya kuanza kwa mazungumzo.

KAMANDA WA AL-QAEDA AUWAWA LEBANON

Majeshi ya Lebanon yametangaza kuwa kamanda wa cheo cha juu wa kundi la kigaidi la Al Qaeda katika nchi hiyo Majid Al - Majid amekufa akiwa kizuizini.

Kamanda huyo ambaye ni raia wa Saudi Arabia, alikuwa ni kiongozi wa kundi la Abdulha Azzam ambalo lina uhusinao na kundi la kigaidi la Al Qaeda, na ambalo pia limekuwa likikiri kuendesha mashambulizi ya kigaidi na milipuko ya mabomu kulenga maeneo yanayokaliwa na waumini wa madhehebu ya Shia katika siku za hivi karibuni.

Miongoni mwa mashambulizi waliyokiri kuhusika nayo ni shambulizi katika Ubalozi wa Iran nchini Lebanon.

Maafisa wa jeshi wanasema Bwana Al Majid amekufa kutokana na maradhi ya figo na kwamba hali yake ilikuwa imezorota.

Al Majid alikamatwa mwezi uliopita na alikuwa akishikiliwa katika kizuizi cha siri.

VITUO 100 VYA KUPIGIA KURA VYACHOMWA MOTO

Karibu vituo vya kupigia kura 100 Bangladeshi kwenye wilaya zipatazo ishirini nchini humo, vimechomwa moto wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi siku ya Jumapili.

Uchomaji moto huo umefuatia siku mbili za mgomo wa chama cha upinzani cha Bangladesh Nationalist Party ambacho kiligomea kupiga kura kikisema ni kashfa.

Kiongozi wa chama hicho KhaledaZia ameshutumu chama cha Awani League kwa kumweka katika kifungo cha nyumbani jambo linapingwa na maafisa wa serikali.

Chama cha upinzani cha Bangladesh Nationalist Party na wafuasi wake wanataka uchaguzi usimamiwe na serikali isiyoegemea upande wowote.

ARSENAL YAIFUMUA SPURS EMIRATES

*Manchester City wabanwa na Blackburn

*Everton kicheko lakini Aston Villa kilio

Arsenal wamedhihirisha dhamira yao ya kutwaa kombe msimu huu baada ya kuwa adhibu mahasimu wao wa London Kaskazini, Tottenham Hotspur kwa mara nyingine.

Safari hii ilikuwa ni katika hatua ya tatu ya Kombe la FA, ambapo Arsenal walipata ushindi mzuri wa mabao 2-0 dhidi ya timu iliyoonekana kufufuka.

Tangu walipomfukuza kocha wao machachari wa Ureno, Andre Villas-Boas, Spurs walianza kufanya vyema ikiwa ni pamoja na kuwafunga mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England (EPL), Manchester United 2-1 juma lililopita.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na viungo wao Santi Cazorla na Tomas Rosiscky baada ya kocha Arsene Wenger kuwaonya nyota wake kutofanya mchezo kwenye michuano hiyo, vinginevyo hangekubaliana nao.

Hata hivyo, Wenger hakuanza na baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza, ikiwa ni pamoja na kumwanzisha kipa Lukasz Fabianski, nahodha anayeelekea kuondoka klabuni, Thomas Vermaelen, kiungo Serge Gnabry huku watu kama Mesut Ozil, Per Metersacker wakiwa benchi japo wengine waliingia baadaye, huku Theo Walcott akiumia tena.

Wakati hali ikiwa hivyo jijini London, huko Ewood Park Manchester City wanaosifika kwa kasi ya kufunga mabao kwa mafuriko walishikwa shati na vibonde wa Ligi Daraja la Pili (Championship), Blackburn Rovers kwa kuwahenyesha ka sare ya 1-1.

City walisubiri hadi dakika ya 45 kupata bao la kwanza kupitia kwa Alvaro Negredo, lakini dakika tano tu baada ya kipindi cha pili kuanza lilisawazishwa na Scott Dann.

Man City walikuwa nusura waage mashindano hayo kama si jitihada za ziada katika dakika tisa za mwisho kuzuia vibonde hao kuwaaibisha, hasa baada ya mlinzi Dedryck Boyata kupewa kadi nyekundu.

Kocha Manuel Pellegrini hakupenda kuwa na mechi ya marudiano kwa sababu tayari Januari hii ana msongamano wa mechi, ikiwa ni pamoja na mechi ya nusu fainali ya Kombe la Ligi (Capital One Cup) dhidi ya West Ham United waliowang'oa Chelsea kwenye robo fainali.

Blackburn ndio waliokuwa washindi wa pili wa kombe hili msimu uliopita na ni miaka 130 imepita sasa tangu walipotwaa kwa mara ya kwanza Kombe la FA, yaani mwaka 1884. 'Mende' waliendelea 'kuangusha makabati' kwani timu ya League One inayohangaika kujinusuru kushuka daraja ya Sheffield United walipowapiga wale wa EPL, Aston Villa kwa bao la Ryan Flynn na kuwatupa nje ya mashindano haya.

Katika mechi nyingine za awamu hiiya Kombe la FA, Barnsley walifungwa 2-1 walipowa karibisha Coventry, Bolton wakawafunga Blackpool 2-1, Bournemouth na Burton mechi yao ikaahirishwa wakati Brighton wakizidi kuwa aibisha Reading kwa kichapo cha 1-0.

Kwingineko, Doncaster walifungwa 3-2 na Steveage, Everton wa Roberto Martinez wakawacharaza Queen Park Rangers wanaofundishwa na Harry Redknapp (QPR) 4-0, Grimsby wakafungwa 3-2 na Huddersfield huku Ipswich wakiambulia sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Preston.

MWILI WA DR. MGIMWA WAWASILI NCHINI

Mwili wa liyekuwa Waziri wa Fedhana uchumi nchini Tanzania Marehemu Dk. William Mgimwa umewasili leo jijini Dar es salaam majira ya saa saba mchana na ndege ya shirika la ndege la Afrika Kusini na kupelekwa moja kwa moja nyumbani kwake Mikocheni jijini DSM, kisha muda mfupi uliopita, mwili huo umepelekwa katika kuhifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo.

Mara baada ya kuwasili kwa mwili huo ulipokelewa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo mawaziri na manaibu waziri, pamoja na viongozi wa vyama mbali mbali vya siasa hapa nchini.

Watu wengine waliojitokeza kuupokea mwili huo ni pamoja na wananchi wa kawaida na familia ya Marehemu Dk. William Mgimwa.

Marehemu Mgimwa alifariki dunia tarehe Mosi ya mwezi huu huko nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kwa ajili ya kupata matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amin.

MCHINA APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUCHANA NOTI

Raia wa China ambaye ni meneja uzalishaji katika kampuni ya ujenzi Shen Hai,46, amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuchana noti ya shilingi 10,000 ambayo ni mali ya Serikali ya Tanzania.

Akisomewa mashtaka hayo mbeleya Hakimu Mfawidhi wa mkoa Janeth Masesa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Castus Ndamugobas alidai kuwa Mchina huyo alitenda kosa hilo mnamo Desemba 3 mwaka jana katika maeneo ya uwanja wa ndege Wilaya ya Ilemela majira ya saa 10:30 jioni ambapo kwa makusudi aliichana noti hiyo yenye namba AY3748043, ambayo thamani yake ni Sh10,000 mali yaSerikali ya Tanzania.

Mshtakiwa huyo ambaye ni meneja mzalishaji aliyeajiriwa na Serikali ya Tanzania ili kufanya ukarabati katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, alikana mashtaka yote na alirudishwa rumande baada ya kutokidhi masharti ya dhamana na hakimu Masesa aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 8 mwaka huu ambapo itafikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa tena.

Kitendo hicho cha raia huyo wa China kuchana noti kilionyesha dharau kwa nchi ya Tanzania na raia wake.

JWTZ YATOA UFAFANUZI JUU YA OFISA WAKE ANAYEDAIWA KUUWA

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limefafanua kuwa askariwake aliyedaiwa kuua raia alilazimika kufyatua risasi kujihami na watu waliodaiwa kuwa ni vibaka waliomvamia na kumlazimisha kufungua milango ya gari lake.

Ofisa huyo, Meja Abdallah Mzee, alidaiwa kuua watoto wawili kwarisasi siku ya mkesha wa mwaka mpya katika mkasa uliotokea Pugu Kinyamwezi jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya ufafanuzi ya JWTZ iliyotolewa Dar es Salaam jana ilisema kuwa Meja Mzee wakati anarudi nyumbani kwake saa 6.00 usiku akiwa anaendesha gari aina ya RAV4, alivamiwa na vibaka waliomzingira na kumlazimisha kufungua milangoya gari hilo.


Kitendo kilichoelezwa kwenye taarifa hiyo kuwa hakikuwa cha kawaida hali iliyomfanya ofisa huyo kujihami kwa kurusha risasi akihofia kudhuriwa na kuporwa gari.Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Habari Makao Makuu ya JWTZ , Meja Joseph Masanja, ilisema ofisa huyo alikuwa anarejea nyumbani kwake akitokea katika hospitali ya Amana na kwamba alivamiwa na vibaka hao eneo la Pugu Kinyamwezi na kwamba Meja Mzee alikuwa na bastola anayoimiliki kihalali."Alianza kufyatua risasi hewani kwa lengo la kujihami na kuwatawanya watu hao.

Katika tukio hilo ofisa huyo alifanikiwa kujinasua na kuondoka kwenye kusanyiko hilo huku akiamini kuwa watu hao wametawanyika,"ilisema taarifa hiyo ya jeshi kwa umma.

Katika tukio hilo inadaiwa kuwa watu wawili walipoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa.

Awali Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala Marieta Minangi, alisema mwanajeshi huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kuwaua kwa kuwapiga risasi watoto wawili na kujeruhi wengine wawili baada ya kundi la vijana waliokuwa wanasherehekea mwaka mpya kuzingira gari lake.

Minangi aliwataja marehemu hao kuwa ni Ibrahimu Mohamed(16) na Abubakar Hassan (14) wakati majeruhi ni Rupano Wanga (17) na Kassimu Abdul (16)


CHANZO: NIPASHE

WANACHAMA WA CHADEMA WATWANGANA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe (Chadema), kuhusu ombi la kuitaka Mahakama hiyo kuizuia Kamati Kuu ya Chama hicho, kutomjadili katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika leo jijini Dares Salaam.

Jaji John Utumwa alisitisha kutoa hukumu hiyo mpaka siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.

Hata hiyo baada ya Jaji huyo kuahirisha kesi hiyo, nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na vurugu kubwa baada ya kundi linalo unga mkono maamuzi ya Chadema kutwangana na kundi linalo muunga Zitto Kabwe.

Hatua hiyo ilisababisha Askari waJeshi la Polisi kuingilia kati, huku wakiungana na upande wa Chadema na kuwatwanga marundi wafuasi wa Zitto waliokuwa na mambango kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Chadema.

Kesi hiyo ilifunguliwa jana na wakili wa Mbunge huyo Albert Msando huku wakili wa ChademaTundu Lissu akiweka pingamizi, hata hivyo Jaji John Utumwa wa Mahakama hiyo alitupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu,

MFANYA BIASHARA WA KARIAKOO APIGWA RISASI NA KUPORWA FEDHA

Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa12Kasoro jioni) kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.

Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo.

Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG.

Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD nakuelekea katika gari lake dogo ainaya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanyabiashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.

''Niliona watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia mlio wa risasi na kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa kasi kutokea upande wa mtaa wa gerezani na kisha mlio wa pili wa risasi ulikika tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule "muhindi" na baada ya hapo kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana lile begi na kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza kufunga maduka yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisiii"

Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya biashara haokutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eneo hili la Kariakoo.


Chanzo: DSM YETU

MADAGASCAR WAPATA RAIS MPYA

Maafisa nchini Madagascar wanasema kuwa matokeo ya mwanzo mwanzo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Disemba, yanaonyesha mshindi kuwa waziri wa zamani wa fedha Hery Rajaonarimampianina.

Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inasema kuwa bwana Hery Rajaonarimampianina alishinda asilimia hamsini na tatu ya kura zilizopigwa.

Mshindani wake, Jean Louis Robinson anasema kuwa uchaguzi ulikumbwa na wizi wa kura na sasa anasema sharti shughuli ya kuhesabu kura irejelewe.

Uchaguzi huo ulikuwa mpango wakurejesha utulivu kwa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi kufanyika miaka minne iliyopita.

Bwana Rajaonarimampianina alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na kiongozi wa mapinduziya kijeshi, Rais wa zamani Andry Rajoelina.

TIMU YA NETBALL MKOA WA KATAVI UTATA MTUPU

Imetolewa na:
Khalifa Zozi - Mpanda Katavi


Nianze kwa kusema, sina ujuzi sana katika mchezo wa mpira wa pete (netball), lakini kikosi cha netball pamoja na benchi linakuwa na idadi isiyopungua watu 12.

Sijaelewa timu ya mkoa wa katavi mnachezaje mashindano hayog. Pamoja na kufika nusu fainali, kwani nafahamu safari yenu ilihusisha watu sita, wachezaji pamoja na uongozi.

Lakini kwa taarifa za uhakika ni kwamba timu inayocheza kwa jinala mkoa wetu ni timu ya netball BANDARI DAR, na hata katika michezo miwili ya awali hakuna mmoja wenu aliyecheza, nimetafakari kwa kina, nikaona bado watu mnakubali kutumika, na sifahamu nini uwakilishi wenu kama wana katavi.

Mnaishia kufurahia matokeo wanayopata wenzenu, na siku ya mwisho itatajwa timu ya katavi imeingiza wachezaji wengi timu ya Taifa lakini hakutakuwa na mwana'Katavi.

Pia kwamba mbali na huyo kiongoz wao mmoja, Viongoz wote waligoma kwenda sababu kubwa nikuwa tayari kiongoz huyo alipokea pesa kutoka bandari.

Ikumbukwe pia huyu mama ndo aliweka sahihi timu ya small kids kuuzwa.

Fikiri mara mbili timu inaondoka na wachezaji watano ilihali wanatakiwa 7 na reserve 5 haina kocha,.

Walikwenda kuomba michango mkoani mkuu wa mkoa akawatosa kwani watu walimpa taarifa mapema.

Ukitaka uhondo sikiliza Pamoja 98.5 Fm Katavi itakupa ukweli wote jumatatu saa moja na nusu usiku (7.30 Pm)

WANAKWAYA WAJERUHIWA KWA BOMU

WANAKWAYA sita wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Kalory Rwanga, Usa River, mkoani hapa, wamelazwa katika Hospitali ya Misheni na ya Tengeru, Arumeru baada ya kujeruhiwa kwa bomu.

Walikutwa na masahibu hayo juzi muda mfupi baada ya kutoka kanisani kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya saa 6.30 usiku, meta 100 kutoka Kanisa hilo, eneo la Kisangani.

Mganga Msaidizi wa hospitali hiyo, iliyoko chini ya Kanisa Katoliki, Fredrick Mathew, alithibitisha jana kupokewa majeruhi watano, huku wawili wakiwa na hali mbaya na wengine wakiendelea vizuri.

Alitaja majeruhi hao kuwa ni Theresia Lesitare (33), Philipo Ambrose (22), Alphonce Nyigo (19), Mary Merikiory (40) na Anna Mathew (19) wote wakazi wa Lake Tatu, Usa River.

Majeruhi mwingine ambaye hali yake si nzuri, Annet Baltazar (16) amelazwa katika Hospitali ya Tengeru. Alisema majeruhi hao waliumia miguuni kwa kuchanwa na mlipuko huo na baadhi ya vipande vya bomu, vilitolewa kwenye miili yao na baadhi yao kushonwa kwa nyuzi kadhaa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kupata taarifa za tukio hilo na kueleza, kwamba uchunguziwa tukio umeanza mara moja na atatoa taarifa ukikamilika.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Merikiory, alisema baada ya kutoka kanisani akiwa na wanakwaya wenzake, waliondoka kuelekea nyumbani, Lake Tatu.

Alisema wakiwa barabarani, waliona gari aina ya Toyota Land Cruiser likienda kwa kasi na lilipowakaribia, walisikia mlipuko na wakajikuta wamelala kando ya barabara huku baadhi yao wakivujadamu miguuni na tumboni.

Aliongeza kuwa gari hilo, halikusimama na lilipofika mbele waliokuwamo walifyatua mabomu ya kutoa machozi, kutawanya makundi ya watu mbalimbali waliokuwa wakionekana barabarani.

Alisema waliomba msaada kwa Paroko wa Kanisa hilo, Patrick Njau, ambaye alitoa gari na kuwapeleka Hospitali ya Misheni na wengine wakipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Tengeru kwa matibabu zaidi.

Askofu alia Akizungumza huku akitokwa machozi baada ya kutembelea majeruhi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Josephat Lebulu alisema ameshangazwa na tukio hilo. Alisisitiza kuwa Kanisa Katoliki, limechoka kuandamwa na matukio ya aina hiyo.

"Waumini wanakosa gani hadi watupiwe bomu, kwa nini polisi wako kimya hadi leo wasiseme? Kuna siri gani? Kwa nini kila siku ni Wakatoliki tu ndio wanapigwa mabomu, tunataka haki itendeke, watu wametoka kanisani usiku, wamekosa nini? Usalama uko wapi?" Alihoji.

Aliendelea: "Tumekosa nini, kupigwa mabomu kila siku hapa Arusha? Tumeshuhudia Olasiti, tukashuhudia Soweto sasa ni hapa Usa," alisema. "Na kwa hili Kanisa hatutakubali hata kidogo, tunataka wahusika wawajibishwe na walioficha uovu huu wawajibishwe la sivyo viongozi walioficha uovu huu wawajibishwe, Mungu atasimama kwa ajili yetu," alisema.

Mei mwaka jana, bomu lililorushwa liliua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye Kanisa Katoliki la MtakatifuJoseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti, mjini Arusha.

Waumini walikuwa wamejumuika katika misa ya uzinduzi wa Kanisa hilo.

Misa hiyo ilikuwa ikiongozwa na Balozi wa Vatican nchini na Mwakilishi wa Papa Francis, Askofu Francisco Padila kwa kushirikiana na Askofu Lebulu.


Chanzo:Habari leo

WACHINA WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO BANDARINI

TAARIFA KWA UMMA

Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na vyombo vingine vya Dola, tarehe 2 Januari 2014 majira ya saa tatu asubuhi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, imekamata meno 81 ya tembo yenye uzito wa kilo 303 sawa na tembo 41.

Aidha, magamba 120 ya kakakuona na mazao ya bahari nayo yamekamtwa.

Hii ni baada ya Askari wa Bandari kutilia shaka mizigo iliyokuwa kwenye gari ikiingizwa bandarini.

Meno ya tembo yaliyokamatwa bado ni mapya ikiwa na maana tembo hao wameuawa katika kipindi kizichozidi mwezi mmoja uliopita.

Wizara inasikitishwa sana na vitendo hivi viovu vya ujangili ambavyo vimetokea ndani ya muda mfupi. Tayari watuhumiwa wawili wanashikiliwa na Polisi kufuatia tukio hilo.

Majina yao yanahifadhiwa kwa lengo la kutovuruga upelelezi.

Serikali inasisitiza tena kwamba imejizatiti kupambana na vitendo vya ujangili katika mapori yote na maeneo yote ya mipaka ya nchi yetu.

Pia, Serikali inapanua wigo wa upelelezi kuhakikisha wote waliohusika wanapatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Imetolewa na:
Chikambi K. Rumisha

Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii

BENKI KUU KUTOA SARAFU YA SH. 50,000

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.

Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa BenkiKuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu yamatukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa."Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki," alisema Profesa Ndulu.

Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.

"Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake," alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.

Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayatiSheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: 'Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi'.

Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali yaMapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: "Miaka Hamsini ya Mapinduzi", thamani ya sarafuna miaka 1964-2014.


Tanzania daima

KITU KINACHOZANIWA KUWA NI BOMU CHAZUA TAHARUKI JIJINI DAR

Tishio la kuonekana bomu laleta hali ya taharuki eneo la Shekilango DSM.

Taharuki imewakumba baadhi ya wapita njia na wafanyabiashara katika makutano ya barabara ya Morogoro na Shekilango jijini Dar es salaam,na kusababisha baadhi ya shughuli kusimama baada ya wapita njia wawili kuona kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono huku baadhi ya askari polisi wakiwa na kazi ya ziada ya kuwaondoa baadhi ya wananchi waliokuwa wakitaka kushuhudia kitu hicho.

Tukio hilo limevutia hisia za watu wengi katika eneo hilo na kukusanyika kwa wingi wengine katika maghorofa yaliyoko katika eneo hilo kwa lengo la kushuhudia badala ya kusimuliwa jambo lililowafanya polisi kuzungushia kamba maalum kwa ajili ya kuwazuia raia kufika katika eneo hilo ambapo watu wawili mtu na mwanaye ndio walioshuhudia.

Baadhi ya askari ambao wanadhaniwa kuwa wataalam wa mabomu kutoka katika kikosi cha kutuliza ghasia Upanga jijini Dar es Salaam walifika katika eneo la tukio na kuanza harakati za kukichukua kitu hicho kinachodhaniwa kuwa ni bomu kwa tahadhari kubwa na baada ya kufanikiwa kukiondoa wakakiweka katika mfuko maalum na kutoweka katika eneo la tukio
itv kiguu na njia hadi kwa kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa kinondoni kwa ajili ya kupata uthibitisho kuhusu kitu hicho kinachodhaniwa kuwa ni bomu na kujulishwa kuwa taarifa juu tukio hilo inaandaliwa naa baada ya kukamilika kwake kamanda wa polisi wa Kinondoni Camilius Wambura akaitoa taarifa hiyo.

Kamanda Wambura hakusita kutoa tahadhari kwa wananchi pale wanapobaini kitu ambacho si cha kawaida na cha hatari kwa maisha ya binadamu.


Chanzo: ITV

ZITTO ATOA UFAFANUZI JUU YA KUZUIA KAMATI YA CHADEMA MAHAKAMANI

Kutoka Katika Ukurasa wa Facebook wa Zitto Kabwe

Mahakama ni Chombo cha kutoa haki.

Nimeomba mahakama kuzuia kamati kuu ya chama changu kunijadili mpaka rufaa yangu isikilizwe na Baraza Kuu la chama. Sijaomba kuzuia kamati kuu kuendelea na kikao chake. Nimeomba kamati isinijadili maana nina rufaa kwenda Baraza Kuu kwa jambo hilo hilo ambalo kamati kuu inataka kuliamulia.

Wakili wa chama Tundu lissu aliweka mapingamizi akisema mahakama haina mamlaka kujadili masuala ya vyama na wanachama wao. Jaji John Utumwa katupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa naTundu Lissu.
Mahakama ndio Chombo cha kutoa haki. Asante Wakili Albert Msando.

Haki itatendeka tu.

ZITTO AWAPELEKA CHADEMA MAHAKAMANI

Taarifa ambazo zimenifikia hivi punde ni kuwa Zitto Kabwe ameweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kesho.

Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.

Anadai anataka mahakama iagize kamati kuu kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.

Wanasheria wa Chama wakiongozwa na Tundu Lissu wanaenda Mahakamani kusikiliza pingamizi hilo ambalo litakuwa limeenda kwa hati ya dharura.

Chanzo:Jf

MUSHARRAF ALAZWA HOSPITALINI

Mtawala wa zamani wa kijeshi nchini Pakistan, Pervez Musharraf amelazwa hospitali kwa kile kinachoshukiwa kuwa ni matatizo ya moyo, akiwa njiani kuelekea mahakamani ambako anakabiliwa na mashitaka ya uhaini.

Maafisa nchini Pakistan, wameiambia mahakama kuwa Musharraf mwenye umri wa miaka 70, alihamishiwa katika hospitali ya kijeshi ya magonjwa ya moyo huko Rawalpindi.

Hii ni mara ya tatu kwa rais huyo wa zamani wa Pakistan kushindwa kufika mahakamani kufuatia matukio mawili yaliyopita kuhusishwa na wasiwasi kutokana na hali ya usalama.

Mashitaka ya uhaini yanahusishwa na uamuzi wake wamwaka 2007, kusitisha katiba na kutangaza hali ya hatari.

Bwana Musharraf amekana mashitaka hayo na anasema tuhuma zote dhidi yake zinatokana na msukumo wa kisiasa.

MELI YA WANASAYANSI WALIOKWAMA ANTARCTIC WAOKOLEWA

Angalau watafiti 50 waliokuwa wameabiri meli ya Urusi iliyokwama katika bahari ya Antarctic hatimaye wameokolewa.

Meli hiyo kwa jina 'Akademik Shokalskiy' ilikwama kwa siku tisa zilizopita katika bahari hiyo iliyokuwa imejaa theluji.

Ndege aina ya helikopta kutoka katika kampuni moja ya kichina ilifanikiwa kuwaokoa watafiti hao ambao miongoni mwao walikuwa wanahabari na wanasayansi.

Mashine tatu za kusaga theluji zilikosa kuifikia meli hiyo ambayo iliondoka New Zealand mwishoni mwa Novemba watafiti waliokuwa wameiabiri wakiichunguza upya nyayo za karne moja iliyopita za mtafiti Douglas Mawson.

Mawson aliwahi kukwama katika sehemu hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja huku watafiti wake wawili wakiaga dunia wakijaribi kujiokoa.

HALI YA ARIEL SHARON YAZOROTA

Hali ya kiafya ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon - ambaye amekuwa katika hali mahututi, inaendelea kuzorota zaidi.
Inaarifiwa kwamba maisha yake yamo hatarini.

Madaktari wanasema kuwa Sharon mwenye umri wa miaka , 85, anakabiliwa na matatizo ya afya ya viongo vyake vya mwili ikiwemo Figo zake na kwamba vinaanza kuonekana kutofanya kazi vyema.

Hata hivyo madaktari hawakutoa taarifa zaidi kuhusu afya ya Sharon.

Alichukua wadhifa wa waziri mkuu mwaka 2001 na kuugua kiharusi mwaka 2005 na alisifika sana kwa msimamo wake mkali kuhusu hali ya kisiasa kati ya taifahilo na utawala wa Palestina.

Baada ya kupatwa na kiharusi kingine mwaka 2006, Sharon akapotewa na fahamu na amekuwa kwenye mashine ya kusaidia moyo wake kuendelea kupiga tangu hapo.

Sharon alikuwa mmoja wa wanasiasa mashuhuri wenye utata katika siasa za Israe

WATU MILIONI 4.6 WAFANYIWA UDUKUZI MTANDAONI

Akaunti za watumiaji milioni 4.6 wa mtandao wa kijamii wa Snapchat na namba zao simu zimedukuliwa na watu walioziweka data hizo mitandaoni.

Mtandao wa Snapchat DB ndio ulichapisha data hiyo kwa muda kwenye mtandao ingawa ulificha nambari mbili za mwisho za simu zilizochapishwa.

Hata hivyo data hiyo inasemekana imeondolewa kwenye mtandao.

Udukuzi huu umeripotiwa siku moja baada ya kampuni ya usalama ya Gibson nchini Australia kuonya kuwa watumiaji wa programu hiyo walikuwa katika hatari ya taarifa zaokudukuliwa.

Kampuni ya Gibson hata hivyo ilisema kuwa haikuhusika na udukuzi huo ingawa ilijua kuwa wanaotumia programu hiyo walikuwa natika hatari ya kudukuliwa.

Watu waliofanya udukuzi huo , wamesema kwamba walitumia pengo lililokuwepo na ambalo kampuni ya Gibson ilikuwa kutambua kufanya udukuzi wao.

Programu ya Snapchat imekuwa kwa kasi na hutumiwa na watumiaji wake kutumiana picha ingawa wana uhakika kuwa programu hiyo baadaye hufuta picha hizo.

Programu hiyo pia inawaruhusu watumiaji kutumiana picha na kuweza kupata anwani zao kupitia kwa Facebook.

JK AONYA WAHAMIAJI HARAMU

RAIS Jakaya Kikwete ameonya wahamiaji haramu wanaorejea nchini baada ya Operesheni Kimbunga kumalizika na kusema kama wanafanya hivyo, wanajisumbua, hawatadumu nchini.

Kikwete ambaye amesema amepata minong'ono kuwa baadhi ya walioondoka wanarudi kinyemela, amewataka wanaopenda kuishi nchini, wafuatenjia halali.

Suala hilo pamoja na mengine mengi, ikiwemo dawa za kulevya, elimu na Operesheni Tokomeza, aliyasema katika salamu zake za Mwaka Mpya alizozitoa juzi. "Nimepata minong'ono kuwa baadhi ya watu walioondoka wanarudi kinyemela.

Napenda kuwa tahadharisha kuwa wasifanye hivyo. Wanajisumbua bure. Hawatadumu. Ushauri wangukwao ni kuwa kama wanapenda kuishi Tanzania wafuate njia halali za kufanya hivyo," alisema.

Rais Kikwete alisema kukithiri kwa ujambazi katika mikoa ya Kigoma, Kagera na Mwanza ndiko kulimfanya akatoa uamuzi wa kuanzisha Operesheni Kimbunga ambayo imekuwa na mafanikio ya kutia moyo.

Alisema hali ya usalama katika mikoa hiyo inaelekea kuimarika ingawaje ni mapema mno kusema tatizo limedhibitiwa.

Lakini alikemea baadhi ya watu waliokuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria kurudi kinyemela. Kuhusu dawa za kulevya, alisema Serikali yake iko katika hatua nzuri katika matayarisho ya kuanzisha Kikosi Maalum cha Kupambana na Dawa za Kulevya katika mwaka ujao wa fedha.

Alisema katika kupambana na biashara hiyo haramu, wanaitazama upya sheria ya adhabu kwa makosa ya kufanya biashara ya dawa za kulevya ili kuifanya iwe na meno makali zaidi." Vilevile, tutaongeza uwekezaji katika vituo vya tiba na kuwarekebisha watu wanaotumia dawa za kulevya. Mafanikio yanayopatikana Muhimbili na Mwananyamala yanatupa moyo wa kufanya zaidi," alisema Rais Kikwete.

Elimu Alisema mwaka uliomalizika Serikali iliajiri walimu 28,666, lakini hata hivyo bado kuna upungufu wa walimu 57,755 kati yao 20,625 wa shule za msingi na 37,130 wa shule za sekondari.

Alisema mwaka ujao wataajiriwa walimu wapya 36,100 kati yao 18,100 wa shule za msingi na 18,000 wa sekondari ili kupunguza pengo lililopo.

Rais alisema walimu wa masomo ya sanaa wapo wengi na tatizo lake linakaribia kumalizwa. Alisema changamoto kubwa itakuwa kwa walimu wa masomo ya Sayansi.

Operesheni Tokomeza Rais Kikwete ametangaza kuunda Kamisheni ya Uchunguzi itakayo ongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu kwa ajili ya kuchunguza malalamiko juu ya uhalifu na unyama uliofanyika wakati wa Operesheni Tokomeza, Alisema uchunguzi wa kina utafanywa kuhusu kadhia yote hiyo.

"Makosa yaliyofanyika yataainishwa na waliofanya kutambuliwa ili wachukuliwe hatua zipasazo kwa mujibu wa sheria na kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.

"Alisema ni muhimu kufanya hivyo ili haki itendeke ipasavyo. Aliongeza kuwa mtindo wa mzigo wa makosa ya watumishi wa umma kubebwa na viongozi wa kisiasa pekee, tena wasiokuwa na hatia ya moja kwa moja, siyo sahihi.

Rais alisisitiza kuwa ni lazima kila mtu abebe mzigo wake inavyostahili.

"Ni matumaini yangupia kwamba katika siku za usoni kunapotokea matatizo ya namna hii uchunguzi uwe wa kina ili wale hasa waliohusika na kutenda makosa wawajibishwe."

MSIGWA ATAKA KUUNGWA MKONO CHADEMA KUMFUTA ZITTO UWANACHAMA

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ametaka wana Chadema kuunga mkono mpango wa kumfuta uanachama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wao, Kabwe Zitto.

"Kuna mlolongo wa mambo yaliyofanya Chadema ikachukua hatua kali dhidi ya Zitto, mambo hayo yamesemwa sana na viongoziwetu; Januari 3, vikao vya chama vitaanza mchakato wa kuhitimisha suala hilo," alisema.

"Amekwishaandikiwa barua ya kujieleza kwa nini asifukuzwe uanachama, sasa nawaulizeni wana Chadema Iringa afukuzwe au asifukuzwe ili nikifika kwenye kikao nitoe msimamo wa Iringa?" Aliuliza na sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wake wakijibu "afukuzweeee…."Katika mkutano wake Desemba 31,kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa, Mchungaji Msigwa alisema Zitto amekikosea mengi chama hicho, hali iliyowanyima uvumilivu na kuamua kumwondoa katika nafasi zake zote za uongozi.

Alisema pamoja na kwamba alijiunga katika chama hicho akiwa na miaka 16, umaarufu wake kisiasa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na waasisi wa chama hicho, aki wamo Mwenyekiti Freeman Mbowe aliyekuwa akimsaidia kifedha wakati akisoma Chuo Kikuu (cha Dar es Salaam).

Msigwa aliwasifu baadhi ya watendaji wa Serikali, akisema wanastahili pongezi kwa kazi nzuri wanayofanya kuwaletea wananchi maendeleo.

"Lazima tuwe waungwana, inapotokea kuna kazi imefanywa na watendaji, ni lazima tuwapongeze bila kujali wanaitumikia serikali ya chama gani," alisema.

Alitaja watendaji hao kuwa ni Mkuuwa Mkoa, Dk Christine Ishengoma, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk Leticia Warioba na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

Aliwapongeza viongozi hao kwa kukataa stendi mpya ya mabasi ijengwe Igumbilo, pembeni mwa Mto Ruaha Mdogo.

"Najua kuna watu walinunua viwanja kuzunguka stendi hiyo kwa gharama kubwa; na wameniandikia barua wakinitisha, kwamba hawataiunga mkono Chadema endapo nitaunga mkono stendi hiyo isijengwe pembeni mwa Mto huo," alisema.

Alisema watu wanaotaka alifumbiemacho suala la ujenzi wa stendi hiyo karibu na chanzo hicho cha maji ni bora waondoke Chadema kuliko kuwaunga mkono.

"Mbali na shughuli za kilimo, maji ya Mto huo ndio chanzo kikuu cha maji yanayotumika majumbani na wakazi wa Iringa na vitongoji vyake; ikijengwa stendi katika eneohilo kutakuwa na uharibifu wa chanzo hicho unaoweza kuleta madhara kwenye maji ya Mto; sikubali, bora mtoke Chadema na kura zenu msinipe," alisema.

Chanzo: Habari Leo

UN YATAKA MAPIGANO KUSITISHWA SUDAN KUSINI

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini humo.

Hilde Johnson aliyeelezea wasiwasi wa hali mbaya ya kibinadamu nchini humo, amezitaka pande zinazozozana kukubali kufanya mazungumzo yaamani.

Angalau watu 1,000 wamefariki tangu mapigano kuanza mwezi jana kati ya wafuasi wa Rais Salva Kiir na wale wa aliyekuwa naibu wake Riek Machar aliyefutwa kazi pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali ya Rais Kiir.

Pande zote mbili zimewatuma waakilishi kwa mazungumzo nchini Ethiopia lakini hadi kufikia sasa waasi hawajakubaliana kusitisha vita.

Wakati huo huo,Rais Salva Kiir ametangaza hali ya hatari katika sehemu mbili za nchi hiyo zilizokumbwa na vita na ambako waasi wamedhibiti.

Mapigano makali yameripotiwa kuendelea katika mji muhimu wa Bor huku maelfu wakiyahama makwao.

KUMI WAFA SHAMBULIO KENYA

Angalau watu kumi wamejeruhiwa katika shambulizi la guruneti katika eneo moja la watalii mjini Mombasa pwani ya Kenya.

Polisi wanasema kuwa washambulizi walirusha guruneti hilo katika moja ya hoteli za kitalii eneo la Diani usiku wa kuamkia leo.

"tulisikia mlipuko katika baa moja iliyokuwa imefurika watalii na kuwajeruhi watu 10, '' alinukuliwa akisema mkuu wa polisi katika eneo hilo Jack Ekakuro.

Waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini ingawa wengi wao haliyao sio mbaya sana.

RAIA WAZIDI KUKIMBIA MAKAZI YAO HUKO SUDAN KUSINI

Mashirika ya kutoa misaada yamesema kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao kufuatia mapigano nchini Sudan Kusini na wanahitaji misaada ya dharura.

Wengi wamekimbia kambi moja iliyoko ufuko wa mto nile, baada ya kuvuka mto huo kwa mashaua ili kuepuka mapigano yanayoendelea mjini Bor kati ya wafuasi wa rais Salva Kirr na aliyekuwa naibu wake Riek Machar.

Mwandishi wa BBC, mjini humo amesema kuwa wakimbizi hao wamepiga kambi chini ya miti wakiwa na mali yao waliyofanikiwa kubeba.

Afisa mkuu wa Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medicins san Frontiers, MSF limesema hakuna maji masafi ya kunywa.

Amesema watu wanakunywa maji chafu ya mto nile.

Amesema watu wengi wanajisaidia hadharani kutokana na ukosefu wa vyoo na hivyo kuongeza tishio la kuzuka kwa ugonjwa wa kuraha na kutapika.

ALIYEKUWA MKUU WA UJASUSI RWANDA AUAWA AFRIKA KUSINI

Polisi nchini Afrika Kusini wamesema kuwa aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi wa Rwanda, Patrick Karegeya, amepatikana ameaga dunia katika hoteli moja mjini Johannesburg.

Bwana Karegeya amekuwa akiishi uhamishoni nchini Afrika Kusini kwa muda wa miaka sita iliyopita.

Karegeya alipokonywa cheo cha kanali baada ya kutofautiana na mshirika wake wa zamani, rais Paul Kagame wa Rwanda, ambayealimshutumu kwa kuhusika na mashambulio ya kigaidi mjini Kigali.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, na chama chaupinzani cha Rwanda National Congress, RNC, inasema kuwa Karegeya alinyongwa ndani ya chumba chake.

Hata hivyo mamlaka nchini AfrikaKusini haijathibitisha madai hayo.

WAZIRI WA FEDHA DR. MGIMWA AFARIKI DUNIA

Waziri wa Fedha William Mgimwa amefariki dunia leo katika hospitali ya Mediclinic Kloff nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, ambaye amesema Mgimwa amefariki majira ya saa 5:20 saa za Afrika Kusini ambapo ni sawa na saa 6:20 kwa majira ya Tanzania.