VODKA YAUWA WANAUME URUSI

Idadi kubwa ya vifo vya mapema nchini Urusi vinatokana na watu kunywa pombe nyingi , hasa Vodka.

Ripoti hii ni kulingana na utafiti uliofanywa hivi karubini nchini humo.

Utafiti huo kwenye jarida la Lancet unasema kuwa robo ya wanaume nchini Urusi wanakufa kabla ya kufikisha umri wa miaka 55 na wengi wao wanakunywa sana pombe.

Watafiti walichunguza tabia ya ulevi ya wanaume zaidi ya laki moja na hamsini katika miji mitatu ya Urusi kwa miaka kumi.

Pia walitathmini utafiti wa awali kuhusu kiwango cha Pombe walichokuwa wamekunywa wanaume kadhaa kabla ya kufariki.

Utafiti uligundua kuwa idadi ya vifo vilipungua kutokana na matukio ya kisiasa na mabadiliko katika sera kuhusu Pombe.

Mnamo mwaka 1985 chini ya utawala wa aliyekuwa Rais Gorbachev, unywaji pombe uliwekewa vikwazo na hivyo vifo kutokana na ulevi vikapungua.

Kisha baada ya kuporomoka kwa mfumo wa kikomunisti na misukosuko iliyofuata , watu walianza tena kulewa sana huku idadi ya vifo ikiongezeka.

Watafiti wamesema kuwa inatokana na ambavyo warusi hulewa hasa wanaokunywa sana Vodka ambayo inachangia idadi kubwa ya vifo.

Kodi na vikwazo vilivyoanza kutumika mwaka 2006,vimesaidia kupunguza unywaji wa pombe , lakini watafiti wanasema kuwa viwango vya juu vya ulevi ni sehemu ya mtindo wa maisha nchini Urusi na hilo ndilo linahitaji kubadilika.

RAIS KIKWETE ASIKITISHWA NA CHOKOCHOKO ZA GAZETI LA RWANDA, BALOZI WA TZ RWANDA ATOA UFAFANUZI

RAIS Jakaya Kikwete, amesikitishwana chokochoko zinazoendeshwa na gazeti la Serikali ya Rwanda, The News of Rwanda, likimtuhumu kusaidia vikundi vya waasi nchini humo. Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Francis Mwaipaja, ameeleza hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, kufafanua tuhuma zilizoandikwa na gazeti hilo.

"Rais Kikwete amesikitishwa kwa uongo huu na ametoa ushauri kwa wahariri wa gazeti hili, kuacha kutunga madai yasiyo na ukweli, ambayo yanaweza kujenga chuki na kuchanganya watu wa nchi hizi jirani na rafiki.

"Wakati huu ambao Rais Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda, walishakubaliana kuimarisha uhusiano wa kirafiki baina yao na nchi hizi mbili mjini Kampala, Uganda, gazeti hilo linachofanya ni kuweka mazingira magumu ya nia hiyo njema na Rais Kikwete angependa kujua wahariri hao wana lengo gani," alieleza Balozi Mwaipaja.

Balozi alionya kuwa Ubalozi wa Tanzania hautachukulia habari hiyo kirahisi, hasa kwa kuzingatia kuwa gazeti hilo limesambazwa katika vitongoji vyote vya Rwanda.

Tuhuma Kwa mujibu wa taarifa ya Balozi Mwaipaja, gazeti hilo limedai kuwa muasisi wa chama cha Rwanda National Congress (RNC), aliyetajwa kwa jina moja la Dk Rudasingwa, mshauri wa chamahicho, Condo Gervais na makamanda wa ngazi za juu wa kikundi cha waasi nchini humo cha FDLR, Luteni Kanali Wilson Irategeka na Kanali Hamadi, walikuwa Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mbali na kuwa nchini, gazeti hilo lilidai kufanyika mkutano kati ya Rais Kikwete na viongozi hao wa waasi katika makazi rasmi ya Rais.

Gazeti hilo lilidai pia kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Rwanda, Faustin Twagiramungu, alikuwa nchini na alikutana na wawakilishi hao wa RNC na FDLR, Dar es Salaam.

Madai mengine yalihusisha Idara ya Uhamiaji ya Tanzania, kwamba ilitoa hati za kusafiria za Tanzania kwa waasi hao ambazo walizitumia kusafiri katika nchi mbalimbali ikiwamo Msumbiji Desemba 20 mwaka jana. Pia kwamba kuna taasisi imeanzishwa nchini ambayo kazi yake ni kupanga na kusaidia safari za wapiganaji wa FDLR.


Akifafanua hoja moja baada ya nyingine katika taarifa hiyo iliyosambazwa pia kwa vyombo vya habari nchini humo, Balozi Mwaipaja alianza na madai ya mkutano wa Rais Kikwete na waasi hao.

"Hakukuwa na mkutano kama huo katika makazi rasmi ya Rais Kikwete Dar es Salaam wala Dodoma au kokote, tena Rais Kikwete hajawahi kukutana na ofisa yeyote kati ya waliotajwa mahali kokote ndani na nje ya Tanzania.

"Mbaya zaidi, siku ambayo gazeti la News of Rwanda linadai kuwa mkutano huo ulifanyika, Alhamisi Januari 23, Rais Kikwete hakuwa nchini, bali alikuwa Davos, Uswisi akihudhuria Mkutano wa Uchumi wa Dunia (WEF)," alieleza Balozi Mwaipaja.

Balozi alieleza pia kuwa muasisi waRNC na mshauri wake na makamanda wa FDLR, hawakuwa nchini wiki iliyopita na rekodi za Uhamiaji zimethibitisha kuwa hawajawahi kufika nchini katika miaka ya hivi karibuni.

Kuhusu taarifa za Twagiramungu kuwa nchini wiki iliyopita, Balozi Mwaipaja alisema kiongozi huyo hakuwapo wala hakuwa na mkutano wowote na waasi wenzake na zaidi, kumbukumbu za Uhamiaji zinathibitisha kuwa hakuingia wala kutoka nchini.


Balozi Mwaipaja pia alisikitika na madai kuwa Uhamiaji ilitoa hati za kusafiria kwa Wanyarwanda hao na kufafanua kuwa kitu kama hicho hakijafanyika kwa raia wa Rwanda.

"Si kazi ya Tanzania kutoa hati za kusafiria kwa raia wa nchi zingine, "alifafanua.

Kuhusu madai ya kuanzishwa kwa taasisi ya kusaidia waasi, Balozi Mwaipaja alisema gazeti hilo, linapaswa kujua walipo wapiganaji hao na mahali wanakofanyia kazi.

"Taarifa hizi kwa kweli ni uongo wa hatari uliotungwa na wahariri wa gazeti hili na lengo lao baya na la wazi la kumshambulia Rais wa nchi rafiki na kujaribu kuaminisha umma kuwa Tanzania inashirikiana na maadui wanaopingana na Serikali ya Rwanda," alieleza Balozi huyo.


Aliokutana nao siku (Januari 23) ambayo gazeti hilo linadai Rais Kikwete alikutana na waasi Dar es Salaam, alikutana katika Hoteli ya Sheraton jijini Davos na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza, Niuck Clegg na kisha kukutana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jetro ya Japan. Rais pia siku hiyo alikutana nakufanya mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Rajiv Shah.

Baada ya hapo, Rais alishiriki mijadala na mikutano katika Hoteliya Derby jijini hapo, ambayo ilihusu masuala mbalimbali ya uchumi.

Chokochoko hizi zinatokea baada ya majeshi ya ulinzi ya Tanzania kushiriki kupambana na kukisambaratisha kikundi cha waasicha M23 kilichokuwa kikiendesha hujuma zake dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mashariki mwa nchi hiyo. Kikundi hicho kilikuwa kinadaiwa kuhusishwa na Serikali ya Rwanda.

MBUNGE NA MKURUGENZI NUSURA WAZICHAPE

Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema wa Mkoa wa Manyara, Paulina Gekul jana alilazimika kuokolewa na polisi wilayani hapa, kutokana na kushambuliwa na Mkurugenzi wa Halmashari ya Mji wa Babati, Omari Mkombole na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mohamedi Fara, wakigombea kabrasha lenye majina ya wanaopaswa kupewa ardhi.

Katika tukio hilo, Gekul ameeleza kuchaniwa nguo zake, kudhalilishwa na kuporwa fedha zaidi ya Sh5 milioni zilizokuwa kwenye mkoba wake.

Tukio hilo la kushambuliwa kwa mbunge huyo lilitokea juzi saa 12 jioni katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Babati, mara baada ya kikao kilichokuwa kikifanyika chini ya mkurungenzi huyo kumalizika.


Akizungumza mara baada ya kutoka polisi jana kutoa maelezo juu ya vurugu hizo, Gekul alisema kikao hicho kilichosababisha vurugu hizo, kilikuwa kinajadili mustakabali wa ugawaji wa shamba la Sisal Plantation lenye ekari 4200.

Alisema shamba hilo wakulima walilipia mwaka 2000 na Baraza la Madiwani lilikwishatoa uamuzi wa kugawanywa, lakini juzi katika orodha iliyotolewa, alibaini majina mengi yameghushiwa na walengwa wengi hawapo na baada ya viongoziwa halmashauri kubaini amegundua njama hizo, ndipo waliagiza kurejeshwa makabrasha yote.

"Mimi nilikataa kwa sababu orodha hii ina makosa na mimi nawafahamu baadhi ya wakulima wanaopaswa kupewa eneo hili "alisema Gekul.

Alisema Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mohammedi Fara baada ya yeye kukataa kurejesha, aliahirisha kikao na walipotaka kutoka nje ghafla alitokea Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Omari Mkombole ambaye alidai alikwenda Polisi kufuatilia suala la wakulima hao na tayari wanataka kuendesha msako wa waliovamia eneo hilo bila idhini ya halmashauri."

Lakini cha ajabu baada ya kusema hivyo, mkurugenzi huyu akanifuata na kunikaba kwa nguvu, kisha kunichania nguo zangu na kunipokonya karatasi akidhani zina majina ya wakulima hao, Alisema baada ya mlango kufungwaalianza kupokonywa kwa nguvu pochi yake na wakachambua ndani na kuondoka na nyaraka zote, huku ufunguo wa gari ukitupwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri Omari Mkombole, alipopigiwa simu ya mkononi ili kuzungumzia tukio hilo,hakupokea na simu yake iliita bila kupokewa, huku Mwenyekiti wa Halmashauri akikiri kutokea kwa vurugu hizo.

BIEBER AFUNGULIWA MASHTAKA USA

Mwanamziki mashuhuri wa muziki wa 'pop' kutoka Canada Justin Bieber amefunguliwa mashtaka ya kumpiga dereva wa gari la kifahari la kukodisha mwezi Disemba mwaka uliopita.

Bwana Bieber aliye na umri wa miaka 19 alikaribishwa katika katika kituo cha polisi cha Toronto na kikosi kikubwa cha wapiga picha za televisheni pamoja na unyende wa mashabiki wake chipukizi.

Amefunguliwa mashtaka chini ya juma moja baada ya kukamatwa mjini Florida marekani kwa shutuma za kuendesha gari akiwamlevi na mashtaka mengine.

Mwanasheria wa Marekani anayemwakilisha mwimbaji huyo amesema mteja wake hana makosa.

Kwa mujibu wa polisi wa Toronto,yapata saa 02:50 saa za Canada tarehe 30 Disemba, gari la kifahari liliwasili kumchukuwa bwana Bieber na wenzake watanokatika kilabu moja ya starehe ili kuwarejesha katika chumba chao cha hoteli.

Na wakati walipokuwa njiani, dereva huyo pamoja na mmoja wa abiria wake, aliyetajwa kama bwana Bieber, wanasemekana kuanza kufokeana maneno makali.

Abiria huyo "alimgonga dereva wa limousine hiyo kwenye kisogomara kadhaa", polisi wamesema.

Dereva huyo anasemekana kusimamisha gari lake na kisha kutoka nje na kuwaita polisi. Mshukiwa 'alichana mbuga' kabla ya polisi kuwasili.

Bwana Bieber alijisalimisha kwa polisi Jumatano.

Anatarajiwa kufikishwa kizimbani tarehe kumi mwezi Machi.

Howard Weitzman, wakili wa Bwana Bieber mjini California, amesema msanii huyo hana hatia na kwamba anatarajia kesi hiyo itachukuliwa kama kosa dogo tu.

Kuendesha gari akiwa mlevi Kadhalika siku ya Jumatano, ombi la kutaka bwana Bieber atimuliwe nchini marekani lilipata sahihi laki moja.

Ombi hilo liliwasilishwa kwenye mtandao mmoja wa Ikulu ya White House na raia mmoja wa Marekani.

Rais wa Marekani hana madaraka ya kuamuru mtu kuondolewa kwalazima nchini Marekani, na haijabainika iwapo Ikulu ya WhiteHouse itajibu ombi hilo.

Bwana Justin Beiber amejikuta matatani mara kadhaa na maafisawa polisi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Mapema asubuhi Alhamisi iliyopita, bwana Bieber alikamatwa kwenye Ufukwe wa Miami baada ya afisa mmoja wa polisi kumfumania akiendesha kwa kasi gari la kukodi aina ya Lamborghini rangi ya njano kwenye barabara ya umma.

Akimshuku kuwa alikuwa mlevi afisa huyo alimtia mbaroni.

Kadhalika alifunguliwa mashtaka ya kupinga kukamatwa na pia kuendesha gari akiwa na leseni iliyopita muda wa matumizi.

SAMATTA ACHAGULIWA MCHEZAJI BORA TP MAZEMBE

Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na mashabiki wa klabu yake ya TP Mazembe katika ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo iliyopewa jina la"Corbeau d'Or".

Samatta ambaye amepewa jina la utani la"Samagoal"na mashabiki wa TP Mazembe aliwabwaga wachezaji wengine watano waliokuwa wakishindana.

Baada ya zoezi zima la upigaji kura matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:

1. Mbwana Samatta–Kura 248

2. Asante Solomon–Kura 219

3. Robert Kidiaba–Kura 200

4. Nathan Sinkala–Kura 97

5. Rainford Kadaba–Kura 67.

KENYA YATOA TAARIFA YA TISHIO LA NJAA

Serikali ya Kenya imetoa tahadhari kuhusu tisho la nja kwa watu milioni 1.6 kutokana na uhaba wa chakula.

Wizara ya kilimo imesema kuwa chakula kilichohifadhiwa kwa sasa kinaweza kudumu tu hadi mwezi Mei.

Wafanyabiashara wa sekta binafsi wametakiwa kuingilia kati na kununua chakula zaidi kutoka nje ili kuokoa hali.

Hii leo serikali imetoa tahadhari kuhusu uhaba wa chakula lakini wiki jana halmashauri ya serikali ya kukabiliana na ukame ilitoa tahadhari kwa serikali kuhusu tisho la ukame.

Baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na ukame ni maeneo ya Mashariki ambako mvua haijanyesha kwa muda mrefu.

Mkuu wa halmashauri hiyo aliitaka serikali kuchukua hatua mwafaka ili kuzuia ukame na janga la njaa ambalo liliwahi kushuhudiwa nchini humo miaka kadhaa iliyopita.

Katika eneo la Turkana Kaskazini mwa Kenya ambako jamii za kuhamahama huishi, hali inasemekana kuwa mbaya zaidi.

Kuna ripoti za watu kukabiliwa nanjaa pamoja na ukame. Mtoto mmoja aliripotiwa kufariki kutokana na njaa

Inaarifiwa watu kadhaaa wamelazwa hospitalini kutokana na utapia mlo huku familia moja ikilazimika hata kupika nyama ya Mbwa kutokana na ukosefu wa chakula.

JARIBIO LA KUMUUWA WAZIRI LAGUTUKIWA

Kumekuwa na jaribio lililotibuka la kumuua kaimu waziri wa ndani nchini Libya Al-Sidik Abdel-Karim.

Shirika la kitaifa la habari LANA na lile la AFP yamethibitisha tukio. Inaarifiwa kwamba gari alimokuwa Abdel Karim lilipigwa risasi alipokuwa akielekea katika mkutano katika makao makuu ya bunge.

Abdel-Karim anatarajiwa kuhutubia waandishi habari hivi punde.

Abdel Karim aliteuliwa na waziri mkuu nchini Libya kuwa kaimu waziri wa ndani baada ya waziri Mohamed Sheikh kujiuzulu mnamo Agosti mwaka jana.

Seddik Abdelkarim, alikuwa katika gari lake aliposhambuliwa na watu wasiojulikana waliomfyatulia risasi.

Inaarifiwa hakuna aliyeuawa kwenye shambulizi hilo.

Libya imekuwa ikikabiliwa na halingumu ya kisiasa tangu waasi kuipindua serikali na kumuua aliyekuwa Rais Muamer Kadhafi mwaka 2011.

Waziri huyo alikuwa njiani kuelekea bungeni wakati gari lake liliposhambuliwa.

Shambulizi lenyewe limetokea chini ya wiki tatu baada ya mauajiya naibu waziri wa viwanda Hassan al-Droui, aliyeuawa mjini Sirte.

OBAMA ATOA HOTUBA KWA TAIFA

Rais Obama ametumia hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa kuelezea jinsi atakavyotumia madaraka yake kujaribu kuimarisha uchumi wa marekani na pia kukabiliana na bunge la Congress ambalo linashuhudia mgawanyiko.

Bwana Obama ameutaja mwaka 2014 kuwa mwaka wa mafanikio kwa Marekani na kusema kuwa China sio tena mahali bora pa kuekeza bali ni marekani. ''Haya ndiyo matokeo ya juhudi zenu: kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira kwa kiwango kikubwa zaidi katika kipindi cha miaka mitano. Sekta ya nyumba na makaazi iliyofufuka.

Sekta ya utengenezaji bidhaa inayobuni nafasi za ajira kwa mara ya kwanza tangu miaka ya tisini. Mafuta zaidi yanazalishwa hapa nyumbani ikilinganishwa na yale tunayonunua-hili limetokea kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka ishirini.

Nakisi katika bajeti yetu ilipungua kwa zaidi ya nusu. Na kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja, viongozi wa kibiashara kote duniani, wametangaza kuwa China haiongozi tena kama eneo bora la kuekeza duniani bali ni marekani,'' amesema rais Obama.

Kadhalika bwana Obama amesema licha ya kushuhudia miaka minne ya ukuaji wa uchumi na faida kubwa iliyovunwa na makampuni, ukosefu wa usawa umezidi kukitamizizi nchini marekani.

Amesema ametoa mapendekezo ya kuimarisha ukuaji.

Bwana Obama amesema:
''leo, baada ya ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha miaka minne, faida za makampuni ya bei ya hisa zimekuwa juu, na zilizokuwa juu zimezidi kuwa bora. Lakini mishara ya wastani bado iko palepale. Ukosefu wa usawa umezidi kukita mizizi.''

Kuhusu usumbufu wa bunge la Congress, bwana Obama amesisitiza kuwa yuko tayari kuendelea kufanya kazi na wabunge wa Congress kurekebisha baadhi ya mambo, lakini hatasita kutumia fursa nyingi zitakazojitokeza kadri iwezekanavyo kuchukuwa hatua za kurekebisha mambo hata bila marekebisho ya sheria kupitia Congress.

TAARIFA ZA SHAMBULIO HUKO NIGERIA

Taarifa mpya zimeibuka kuhusu shambulizi lililofanywa dhidi ya kanisa moja katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria siku ya Jumapili.

Askofu wa kanisa hilo Yola, Mamza Dami Stephen, ameiambia BBC kuwa wapiganaji walilifunga kanisa hilo, katika kijiji cha Waga Chakawa, baada yamisa na kuwapiga risasi wale wote waliojaribu kutoroka kwa kupita kwenye madirisha. Inaarifiwa takriban watu 30 waliuawa kwa njia hiyo.

Siku hiyo hiyo washambuliaji walivamia kijiji cha Kawuri na kuwaua watu 52. Kundi la Boko Haram limelaumiwa kwa kufanyamashambulizi hayo. Amesema kuwa baadhi yao walikatwa koo zao.

Takriban watu thelathini walifariki kufuatia shambulizi hilo ambalo inasemekana limesababishwa na kundi la wapiganaji wa kiislamu laBoko Haram.

Shambulizi lingine liliwaacha watu hamsini wakiwa wamefariki katika jimbo la Borno.

Wapiganaji wa Boko Haram wanataka kutawala kutumia sheria za kiisilamu katika nchi ambayo imegagawanyika kati ya wasilamu na wakristo.

Kundi hilo limewaua maelfu ya watu katika kipindi cha miaka minne iliyopita, huku kundi hilo likisemekana kuwa tisho kubwa sana kwa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Majimbo ya Borno na Adamawa pamoja na jimbo la Yobe yako chini ya sheria ya hali ya hatari tangu mwezi Mei mwaka jana huku jeshi likijaribu kupambana na wapiganaji hao wa kiisilamu.

WAZIRI MKUU WA UKRAINI AJIUZULU

Rais wa Ukraine, Viktor Yanu-kovich, amekubali ombi la kujiuzulu kwa waziri mkuu wa taifa hilo, Mykola Azrov, pamoja na baraza zima la mawaziri licha ya hatua muhimu kupigwa mnamo Jumanne.

Hata hivyo mawaziri hao waliojiuzulu wanasalia kuwa wasimamizi wa wizara zao hadi pale serikali mpya itakapo buniwa.

Awali bunge la Ukrain lilipiga kura ya kuifutilia mbali sheria kali dhidi ya maandamano ambayo ilizua ghasia tangu iidhinishwe mwezi uliopita.

Kura ya kuifutilia mbali sheria hio ilipigwa na asilimia kubwa ya wabunge wa taifa hilo. Sheria hio ilipiga marufuku waandamanaji kutumia majengo ya umma pamoja na kuvaa vinyago.

Mwandishi wa BBC nchini Ukraine, amesema kuwa upinzani utaiona hatua ya waziri mkuu kujiuzulu pamoja na kufutilia mbali sheria inayozuia maandamano kama ushindi kwao Mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine, ulianza kama maandamano ya amani mwezi Novemba wakati ambapo Rais Yanukovych alipokataa kutimiza ahadi yake ya kushirikiana na Muungano wa Ulaya.

Waandamanaji hata hivyo wameapa kuendelea kuandamana hadi Rais Yanukovych atakapojiuzulu.

IGP AONGEZA NGUVU KUSAKA JAMBAZI LINALOUWA WATU HUKO MARA

Jeshi la polisi nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama linamsaka jambazi aliyehusika na mauaji ya watu nane yaliyotokea katika siku za hivi karibuni katika mkoa wa kipolisi wa Tarime Rorya.

Aidha, mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernesti Mangu, ametuma timu maalum kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi inayohusisha kamisheni ya Oparesheni, Upelelezi na Intelijensia kwenda kuongeza nguvu katika juhudi zinazofanyika na ngazi ya mkoa kuhakikisha kwamba, jambazi huyo anakamatwa upesi ili kuondoa hofu kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Jeshi hilo, Mnamo tarehe 26 Januari, 2014 majira ya saa 12.00 asubuhi huko katika kijiji cha Mogabiri jambazi asiyefahamika kwa jina aliwaua kwa risasi Zakaria Mwita na Erick Maranya baada ya kukutana nao njiani.

Siku hiyo hiyo, saa 4:00 usiku, katika kijiji hicho hicho, jambazi huyo alimuua Robert Kisiri miaka 45 baada ya kuvamia Grocery inayomilikiwa na Chacha Ryoba na kumjeruhi mtu mwingine mmoja.

Tarehe 27 januari, 2014 saa 11:30 alfajiri kijijini hapo, jambazi huyo alifanya mauaji tena kwa kumpiga risasi David Matiko mwenye umri wa miaka 39 na kumpora simu yake aina ya Nokia.

Katika tukio hilo, pia, alimjeruhi Machungu Nyamahemba miaka 19 ambaye bado amelazwa katika hospitali ya Tarime kwa Matibabu.

Siku hiyohiyo ya tarehe 27 Januari, 2014 majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Nkende, jambazi huyo alimuua kwa kumpiga risasi Juma Nyaitara miaka 30.

Baada ya kufanya mauaji hayo, jambazi huyo aliwapora simu zao za mkononi Chacha Magige na Masero Marigiri wote wa kijiji cha Nkende.

Usiku wa kuamkia tarehe 28 Januari, 2014, jambazi huyo aliendelea kuua watu wengine watatu ambao bado majina yao hayajafahamika.

Mtu mmoja alipigwa risasi wakati akiendesha pikipiki katika kijiji cha Nkende nawengine wawili waliuawa baada yakukutwa na jambazi huyo wakiwa wanatengeneza gari lililokuwa limewaharibikia katika kijiji cha Mogabiri na kuondoka bila kuchukua chochote wala kuwapekua.

QUOTE OF THE DAY

"I fear the day that technology will surpass our human interaction. The world will have a generation of idiots." - ALBERT EINSTEIN

MUDA WA KUJAZA FOMU ZA USHIRIKI MAISHA PLUS WAONGEZWA

Habari njema kwa waliokosa nafasi ya kushiriki, Kutoka na na maombi ya wengi tumeongeza muda wa kupokea fomu hadi tarehe 30/01/2014.

1. Kijana wa Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda mwenye umri wa kati ya miaka 21 - 26, jaza moja kwa moja fomu ya kushiriki shindano la Maisha Plus kwa kubofya hapa -->http://maishaplus.tv/MaishaPlusFomu2014.html

2. Kama wewe ni mkulima mwanamke mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea mkazi wa Tanzania ama unamfahamu yeyote, jaza fomu moja kwa moja kwa kubofya hapa -->http://maishaplus.tv/MamaShujaaFomu2014.html

Tunawatakia kila la Kheri.

Kwa hisani ya Bill and Melinda Gates Foundation / Oxfam in Tanzania

MORSI KUSHITAKIWA KWA KUPANGA NJAMA KUTOROSHA WAFUNGWA

Aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa shitaka la kupanga njama ya kuwatorosha wafungwa wakati wamapinduzi ya Hosni Mubarak 2011.

Kosa jengine ni pamoja na kuwaua maafisa wa polisi wakati wa tukio hilo.

Hii ni miongoni tu mwa kesi nne zinazomkabili bwana Morsi.

Zaidi ya walalamishi wengine 130 wakiwemo viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood watawekwa kizimbani na Morsi.

Bwana Morsi hajakuwa huru tangia jeshi limuondoe madarakani mwaka mmoja baadaya kuchaguliwa kama rais.

Wakati huohuo, wizara ya mamboya ndani imesema kuwa afisaa mmoja wa wizara hiyo Generali Mohammed Saeed, alipigwa risasi akielekea kazini.

Mauaji hayo yanatokea wakati mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama katika siku za hivi karibuni na masaa kadhaa baada ya jeshi kumuunga mkono mkuu wake Field Marshal Abdul Fattah al-Sisi kugombea urais.

Hali ya usalama imeimarishwa nje ya ya jengo la wizara hiyo , lakini hakuna hata mfuasi mmojawa Mohammed Morsi amejitokeza.

Vuguvugu la Muslim Brotherhood, limeharamishwa na kutajwa kama kundi la kigaidi na pia wameifanya hatia uungwaji mkono wa kundi hilo.

Makabiliano kati ya wafuasi wa Brotherhood pamoja na vikosi vya usalama, yaliripotiwa kutokeakatika eneo la Ramses mjini Cairo.

Morsi anatuhumiwa kwa kosa la kupanga njama ya kuwatorosha wafungwa kutoka katika gereza laWadi al-Natrun wakati wa ghasia za mwaka 2011.

Mara ya kwanza alipofikishwa mahakamani mwezi Novemba, Morsi alikataa kutambua uhalali wa mahakama wala kuvalia vazi lagerezani.

RWANDA YAKOSOLEWA KWA KUKANDAMIZA UPINZANI

Afisaa mmoja mkuu katika Umoja wa mataifa, amekosoa ambavyo serikali ya Rwanda inawatendea wanasiasa wa upinzani.

Akiongea na BBC, wiki moja baada ya ziara yake nchini humo, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Maina Kiai alisema kuwa karibu kila mwanasiasa, anayejitokeza hadharani kupinga serikali, huishia kwenye matatizo ya kisheria.

Baadhi hukamatwa na kufungwa jela kwa kile kinachosemekana kuwa kueneza uvumi.

Bwana Kiai alisema kwamba alizungumza na mwanamume mmoja akiwa gerezani kuhusu siasa.

Kiai amesema kuwa angali anafanya mazungumzo ya kina naserikali ya Rwanda kuhusu hilo

UPINZANI WAUNGANA A.KUSINI

Chama rasmi cha upinzani nchini Afrika Kusini,(Democratic Alliance) kimemtangaza Dr Mamphela Ramphele ambaye pia alikuwa mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi kuwa mgombea wake wa uchaguzi mkuu mwezi Aprili.

Bi Ramphele, aliyekuwa mwandanani wa mpigania uhuru Steve Biko, aliunda chama chake cha kisiasa cha Agang mwaka jana.

Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance, Helen Zille alisema hakuna mwanasiasa mwingine ana uwezo wa kutawalanchi hiyo kama Bi Ramphele.

Muungano huo uliotarajiwa kuundwa tangu zamani, utashuhudia Dr Ramphele aliyekuwa afisaa mkuu mtendaji katika benki ya dunia na kiongozi wa chama cha Agang South Africa- akiwa kinara wa muungano na mgombea wake mkuu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Aprili.

Tangazo la Muungano huo kati ya vyama hivyo viwili na chama cha Mamphela Ramphele - Agang South Africa - umesifiwa na wafuasi wake kama mwamko mpya wa kisiasa nchini humo.

Baadhi wanasema hii ni dalili ya chama cha DA - kilichoshinda 16% ya kura katika uchaguzi uliopita kuwa katika hali ngumu kisiasa, na pia bado kinaonekana na wengi kama chama cha wazungu.

Dr Ramphele - msomi wa hali ya juu na mkurugenzi wa zamani katika benki ya dunia, licha ya kusifika kwa maoni yake, angali kupata ufuasi mkubwa miongoni mwa wananchi wa taifa hilo.

Chama chake Agang South Africa, kinaangazia zaidi maswala ya elimu, mageuzi ya mfumo wa uchaguzi na ustawi.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Cape Town, Dr Ramphele alisema kuwa kifo cha Mandela mwezi Disemba kilibadili siasa za nchi hiyo na kusema ni wakati sasa wa kuweka hai ahadi za mwaka 1994 - mara ya kwanza ambapo nchi hiyo ilifanya uchaguzi huru.

JENGO LA TIGO LAZUA TAHARUKI

Hofu na taharuki ya kuporomoka kwa jengo la makao makuu ya ofisi za kampuni ya simu za mikononi ya Tigo zilizoko eneo la Makumbusho jijini Dar es salaam zimesababisha kusitishwa kwa huduma katika jengo hilo kwa dharura kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi na wateja wa kampuni hiyo ili kupisha wataalamu wa uhandisi kufanya uchunguzi wa kina kutokana na uwepo wa madai ya tukio la kutikisika kwa jengo hilo la ghorofa tisa.

Tukio hilo limevuta hisia za taharuki kwa wafanyakazi, wateja na baadhi ya wapita njia karibu na jengo hilo.

Wafanyakazi wa kampuni hiyo walitoka nje ya jengo ambapo meneja chapa wa Tigo bwana William Mpinga amesema taharuki hiyo imetokana na uwepo wa nyufa katika sakafu ya ghorofa ya nne ya jengo hilo ambapo mkutano ulikuwa ukifanyika na kusababisha baadhi ya wafanyakazi kukimbia hovyo na kwamba kampuni hiyo imeamua kusitisha huduma katika jengo hilo kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi na wateja wa Tigo.

Tukio hilo limesababisha baadhi ya majengo na ofisi zilizopo karibu na jengo pia kusitisha shughuli zao huku baadhi ya mashuhuda wakielezea kile walichokishuhudia.

Imeshuhudiwa mojawapo ya ufa ulioko kwa nje ya jengo hilo licha ya kuzuiwa na meneja chapa wa Tigo kuingia ndani kwa ajili ya mahojiano na baadhi ya wahandisi waliokuwa ndani ya jengo hilo kuchunguza ukubwa wa tatizo huku jengo hilo likionekana kuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wenye silaha ambapo mkuu wa polisi wa wilaya ya Kinondoni Willbroad Mtafungwa akiwaambia waandishi wahabari kuwa wamepata taarifa ya madai ya kutikisika kwa jengo hilo na kuzua taharuki kwa watu waliokuwemo ndani ya jengo hilo.

PICHA YA SIKU (TUNAOMBA RADHI KWA MUONEKANO)

Picha ni jamaa(Mpasua mbao)aliyejaribu kupambana na Simba baada ya kukutana nae katika hifadhi ya Taifa ya Katavi, Wilayani mlele Mkoa wa Katavi.

Aalikufa Simba na jamaa huyo kujeruhiwa vibaya.

FIELD MARSHALL AL-SISI KUWANIA URAIS MISRI

Viongozi wa kijeshi nchini Misri wamekubaliana Mkuu wa jeshi ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi Abdel Fattah Al Sisi kuwania Urais katika Uchaguzi unaotarajiwa miezi michache ijayo.

Field-Marshal al-Sisi anatarajiwa kujiuzulu kutoka jeshini na kutangaza azma yake ya kuwania urais siku chache zijazo.

Waandishi wa habari wamesema mwanajeshi huyo anapigiwa upatu kushinda kwa urahisi katikauchaguzi unaotarajiwa hapo Apriliambapo hana upinzani mkubwa.

Al Sisi anaaminika kuchangia pakubwa katika kumuondoa madarakani Rais Mohammed Mosri mwaka jana kufuatia maandamano makubwa dhidi yake.

Mikutano ya hadhara ilifanyika wikendi hii huku kukiwa na wito wa kumtaka Bw. Al Sisi kuwania Urais.

Binafsi Al Sisi hajatangaza kugombea lakini kumekua na taarifa kwamba alikua akijitayarisha kujitosa katika kinyang'anyiro cha kuongoza Misri.

Maelfu ya raia walikusanyika katika medani ya Tahiri hapo Jumamosi na kumtaka mkuu wa jeshi kuwania Urais.

Hapo Jumapili Kaimu Rais Adly Mansur alitangaza kwamba uchaguzi wa Rais utafanyika kablaya kuwachagua wabunge.

Wadadisi waliona tangazo hilo kama kumpa nafasi Al Sisi kugombea Urais.

Wafuasi wake wamesema Misri inahitaji kiongozi mkali kama yeye.

Kwa sasa dalili zote ni kwamba Mkuu huyo wa jeshi atashinda kwa urahisi.

Hata hivyo wapinzani wake wanaonya huenda Misri ikarejea katika utawala wa kiimla ambao uliondolewa na maandamano ya raia miaka mitatu iliyopita.

MZEE WA MIAKA 71 AVAMIWA NA KUNYANG'ANYWA BUNDUKI YAKE

WATU wasiofahamika idadi na makazi yao, wamevamia nyumba ya Daudi Karata (71) mkulima na mkazi wa kijiji cha Nguamghanga tarafa ya Mgori wilaya ya Singida mkoa wa Singida, na kunyang'anya bunduki aina ya shot gun na risasi zake nne.

Kabla na kufanya unyang'anyi huo,kundi hilo la watu wasiofahamika,lilimkata kata mapanga mzee Karata sehemu mbalimbali za mwili kwa lengo la kufanikisha azma yao kwa urahisi zaidi.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea januari 21 mwaka huu saa tano asubuhi huko katika kijiji cha Nduamghanga tarafa ya Mgori.

Amesema mzee huyo Karata,alipatiwa matibabu katika kituo kidogo cha kutolea huduma za afya kilichoandaliwa kwa muda kijijini hapo.

"Jeshi la polisi linaendelea na msako mkali ili kuwakamata watu hao na kuwafikisha mahakamani.

Pia linatoa wito kwa raia wema kutoa taarifa pindi wapatapo taarifa zo zote juu ya tukio hilo",amesema kamanda Kamwela.

Habari kutoka kijiji hicho cha Nduamghanga, zinadai kwamba baada ya mzee Karata kunyang'anywa bunduki yake shot gun, saa mbili baadaye, kundi la watu zaidi ya 300 wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa Dodoma, walivamia kijiji hicho huku wakiwa wamebeba mapanga, rungu, pinde na bunduki moja.

Kundi hilo linadaiwa kumuuawa mhudumu wa wanyamapori wa kijiji hicho, Athumani Jumanne Mkatapori kwa kumkata kata kwa mapanga.

Kundi hilo linadaiwa lilikuwa linataka kuwakomboa ng'ombe wao 180 waliokamatwa kwa kuchungia ndani ya hifadhi ya akiba ya msitu wa Mgori.

Hata hivyo,kundi hilo, halikuweza kuwapata ng'ombe wao na badala yake likaishia kunyang'anya ng'ombe 68,mbuzi 101,kondoo sitana punda watatu mali ya Abrahamani Mohammed (60) na kutokomea nao kusikojulikana.

Chanzo: Singida Yetu

ATEKWA, KUTESWA NA KUACHWA PORINI

Katika hali isiyo ya kawaida, kijana mmoja aliyetoweka kwa siku sita nyumbani kwao kwenye mazingiraya kutatanisha amekutwa kwenye Pori la Lumwago kijiji cha Kinyanambo wilayani Mufindi mkoani Iringa akiwa na majeraha makubwa yaliyotokana na mateso aliyoyapata baada ya kutekwa.

Chanzo cha mkasa wa kijana huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mafinga kinadaiwa kuwa ni kupotea kwa Pikipiki katika eneo la Mashine ya Mpunga mjini Mafinga walikokuwa wanapata kinywaji.

Akizungumzia juu ya tukio hilo la kutekwa na kisha kuteswa, ambalo limesababishia majeraha makubwa na kulazwa katika Hospitali hii ya mjini Mafinga, Ezekia Kaganga amesema tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 18 mwezi wa pili.

Hata hivyo Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa Athmani Mungi amesema tayari watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo, ambapo amewataja kuwa ni Alex Ludago na Steven Michael, wote wakazi wa MET Mafinga Iringa.

KIONGOZI WA AL-SHABAAB ASHAMBULIWA

Jeshi la Marekani limefanya shambulizi la makombora dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa mmoja wa viongozi wa kundi la wanamgambo la al-Shabaab nchini Somalia.

Maafisa katika idara ya ulinzi wanasema kuwa wanajaribu kubaini ikiwa shambulizi hilo lilimuua mlengwa ambaye jina lake halijatajwa.

Shambulizi lililenga gari alimokuwa anasafiria mshukiwa huyo Kusini mwa Somalia karibu na mji wa Barawe.

Al-Shabab linasemekana kuwa na uhusiani na kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

Taarifa kutoka katika makao makuu ya ulinzi nchini Marekani zinasema kuwa mlengwa katika shambulizi hilo ni kiongozi wa makundi mawili ya kigaidi.

Mmoja wa viongozi wa al shababaab anaseama kuwa mshukiwa alikuwa Sahal Iskudhuq, kamanda mmoja wa al-Shabaab ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu sana na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeeda.

Hata hivyo hakuna uhakika ikiwa mshukiwa huyo ameuawa.

Marekani iliwahi kufanya shambulizi ambalo lilitibuka dhidi ya mmoja wa viongozi wa kundi hilo katika eneo la Barawe - linalosemekana kuwa ngome kuu ya Al Shabaab mwezi Oktoba.

Al Shabaa waliohusika na mashambulizi ya kigaidi katika jengo la maduka la Westgate, limedhoofishwa na mapambano dhidi yao kutoka kwa wanajeshi wa Muungano wa Afrika Kusini na Kati mwa Somalia.

Marekani nayo imejitolea sana kukabiliana na kundi hilo kwa kutuma kikosi cha ushauri wa kijeshi mjini Mogadishu.

ANC WAKUMBWA NA KASHFA YA KUFUJA PESA ZA MAZISHI YA MANDELA

Upinzani nchini Afrika Kusini unataka uchunguzi kufanywa kuhusiana na madai ya ubadhirifu wa pesa zilizotengwa na chama hicho kwa matumizi wakati wa hafla ya mazishi ya hayati Nelson Mandela.

Matakwa hayo ya upinzani yametolewa baada ya taarifa za jarida moja kusema kuwa, sehemu ya dola elfu miatano zilizotengwa mahsusi kwa shughuli ya kuwasafirisha waombolezaji katika mazishi ya Mandela, zilitumiwa kwa shughuli nyinginezo ikiwemo kushonesha fulana za chama cha ANC.

Chama cha ANC ambacho kimezongwa na kashfa za ufisadi hakijajibu tuhuma hizo.

Duru kutoka mji wa East London zimesema takriban dola laki tano zilitengwa kando kusaidia katika kuwasafirisha waombolezaji wakati wa ibada maalum ya Nelson Mandela.

Hata hivyo fedha hizo zilielekewa kwa kampuni nyingine ambazo hazikua zikitoa huduma za uchukuzi.

Diwani mmoja wa chama cha Democratic Alliance ameambia BBC kwamba zilitolewa risiti bandia.

Manispa hio imesema inasubiri ripoti kamili kuwasilishwa mbele yake mwishoni mwa mwezi huu. Utawala wa Rais Jacob Zuma unakabiliwa na uchaguzi mgumu mwaka huu wakati ukikumbwa nasakata nyingi za ufisadi.

GENERAL AL-SISI APANDISHWA CHEO NA KUWA FIELD MARSHALL

Kaimu Rais wa Misri Adly Mansour ametangaza kwamba mkuu wa jeshi ambae pia ni Waziri wa ulinzi, Generali Abdel Fattah Al-Sisi amepadishwa ngazi na kua Field Marshall{Cheo cha juu zaidi katika Jeshi).

Kuna minong'ono kwamba huenda Generali Al Sisi akawania Urais wa Misri katika miezi michache ijayo.

Anaaminika kuchangia pakubwa katika kumuondoa madarakani Rais aliyeegemea misingi ya kiisilamu Mohammed Morsi mwaka jana kufuatia maandamano makubwa dhidi yake.

Abdel Fattah al-Sisi, anaonekana kupendwa sana kiasi kinachofananishwa tu na alivyopendwa Gamal Abdel Nasser lakini baadhi wanahisi kuwa kutawala kwake kunaweza kurejesha hali ya ukandamizaji ulioshudiwa chini ya utawala wa Hosni Mubarak.

GOOGLE YATAKA UFAFANUZI KUHUSU UDUKUZI

Kampuni kubwa ya Google Imetaka uwazi kutoka kwa Rais Obama kuhusu pendekezo lake la kuzuia baadhi ya udukuzi unaofanywa na idara ya ujasusi nchini humo.

Kufuatia ufichuzi wa aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya ujasusi nchini marekani, Edward Snowden, Rais Obama ameweka viwango vya utumizi wa data ya simu za watu.

Lakini afisa anayesimamia mswala ya sheria katika kampuni ya Google David Drummond ameiambia BBC kwamba Rais Obama anapaswa kutoa maelezo kuhusu viwango vya udukuzi huo katika mtandao.

Bwana Drummond amesema kuwa Marekani haifai kuchukua habari kwa wingi bali inafaa kutoaombi la kupewa habari hizo kupitia agizo la mahakama.

Amesisitiza kuwa kampuni ya Google haina ushirikiano wowotena shirika lolote la ujasusi.

Bwana Drummond aliongeza kwamba serikali zote duniani zinapaswa kubuni sheria za kimataifa kuhusu udukuzi wa taarifa binafasi za watu kwenye internet.

WAZIRI MKUYA AMJIBU PROFESA LIPUMBA

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.

Alisema chama chake, kina wasiwasina elimu ya Waziri Mkuya, kutokanana wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.

Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.

Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.

"Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka," alisema Lipumba.

Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.

"Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka," aliongeza.

Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.


*WAZIRI AJIBU*

Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.

Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.

Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009. "Nimehitimu Shahada ya Uzamili yaUtawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.

"Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam," alisema Mkuya.

LIGI YA MKOA WA KATAVI YAANZA KUTIMUA VUMBI

Mashindano ya Ligi ya Taifa ngazi ya Mkoa katika mkoa wa Katavi yameanza kutimua vumbi katika uwanja wa Azimio uliopo Mjini Mpanda.

Mashinano hayo yanayoshirikisha timu tisa yameanza jana ambapo timu zimepangwa katika makundi mawili.

Kundi A lina timu tano ambazo ni Polisi Katavi, Makanyagio Fc, Kazima Fc, Majalila FC na Veta Mpanda.

Kundi B lina timu za Mpanda United, Mbugani FC, Faya FC na Baruti Kasokola ambapo kundi A litatoa washindi watatu kuingia hatua ya pili na kundi B litatoa timu mbili.

Katika Mchezo wa ufunguzi ulifanyika mchezo baina ya timu za polisi katavi na Makanyagio katika mchezo huo ambao ulihudhuliwa na mamia ya wakazi wa mji wa mpanda timu hizo zilitoka sale kwa kufungana goli moja kwa moja (1-1).

Mshindi wa kwanza wa mashiindano hayo atauwakilisha mkoa wa Katavi katika mashindano ya ligi ya Taifa ya mabingwa wa mikoa.

ASKARI 96 WAMALIZA MAFUNZO

Jumla ya Askari 96 wa Shirikala Hifadhi la Taifa la Wanyama Pori (TANAPA) wamehitimu mafunzo ya miezi mitatu katika chuo kipya cha wanyama pori cha Mlele kilichopo Mkoa wa Katavi na kutoa kiapo cha utii mbele ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.

Askari hao wa TANAPA walimaliza mafunzo hayo hapo juzi kwenye chuo hicho cha wanyama Pori cha Mlele akiwa ni mafunzo ya kwanza hapa nchini kwa TANAPA kutoa mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori kupatiwa mafunzo hayo kabla ya kuanza kazi Katika Risala yao ya wahitimu wa mafunzo hayo ya kulinda maliasili iliyosomwa na Bruno Mbunda walieleza kuwa wamejifundisha mbinu mbalimbali za kulinda rasilimali za Taifa kwa Vitendo na nadharia.

Waliyataja baadhi ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata waharifu kumpekua mharifu na kutotumia nguvu sana katika kukamata mharifu pamoja na pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha.

Walieleza katika kipindi hicho cha mafunzo wahitimi hao walifanikiwa kukamata waharifu hamsini wakati wakifanya doria katika maeneo mbambali ya Mbuga ya Katavi na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa Lwafi.

Wahitimu hao walieleza kuwa mafunzo hayo yaliwashirikisha Askari 99 lakini watatu kati yao wameshindwa kuhitimu zikiwemo sababu mbambali kama utoro na utovu wa nidhamu hari ambayo ilfanya wahitimu waliomaliza kubaki 96 ambapo kati yao mwanamke ni mmoja na wanaume ni 95.

Kwa upande wake mkuu wa mapori ya akiba ya Rukwa Lwafi Joseph Mbung'ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali Alizitaja changamoto hizo kuwani ukosefu wa mawasiliano na ubovu wa miundo mbinu ya barabaa na upungufu wa magari pamoja idadi ndogo yawashiriki wa mafunzo kwa wanawake na ufinyu wa bajeti.

Nae Mkurugenzi wa Hifadhi na Ikolojia Martini Loibook alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata yana umuhimu sana hasa kutokana na changamoto zinazoikabili nchi yetu inayokabiliwa na wimbi la ujangili Pia Mkurugenzi wa utumishi na utawalla wa TANAPA Witnes Shoo aliwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa uaminifu kwa kujituma na wawe na didamu na wasiwe na tabia ya kutowa siri za ofisi.

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliwaasa wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu mkubwa hasa katika shughuli zao katika kupambana kukomesha ujangili Aliwataka kutojihusisha na masuala ya ujangiri na badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao yaujangiri iliyopo ndani ya nchi na nje ya nchi Alisema wapo baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kurubuniwa na mtu yoyote yule au watu.


Chanzo:Katavi Yetu

ARSENAL KUMENYANA NA LIVERPOOL, MAN CITY WAO KUWAKARIBISHA CHELSEA ETIHAD

Droo ya michuano ya kombe la FA imefanywa kwa mechi za mchujo wa raundi ya tano.

Chelsea wamepangiwa kucheza na Manchester City katika mchezo unaotazimiwa na ushindani wa hali ya juu.

Chelsea ambao wamefuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii amesema, "Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora.

"Nao Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwakuiadhibu Watford kwa mabao 4-2.

Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano.

Roberto Martinez ataiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani ya Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni mechi liyokutanisha timu zote za ligi ya England.

Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton. Sheffield Wednesday watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya Championship, Charlton FC.

Mechi zote zitachezwa jumamosi na jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi wa pili.

Mshindi wa mechi kati ya Fulhamama Sheffield United atapambana na mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe hilo ambalo fainal yakeitachezwa kwenye uwanja wa Wembley.


Droo kamili ni kama ifuatavyo;

Manchester City v Chelsea

Sheffield United au Fulham v Nottingham Forest au PrestonNorth End

Arsenal v Liverpool

Brighton & Hove Albion v Hull City

Cardiff City v Wigan Athletic

Sheffield Wednesday v Charlton Athletic

Sunderland v Southampton

Everton v Swansea City


*KATIKA MICHUANO YA TENIS*

Stanislas Wawrinka raia wa Uswis amefanikiwa kutwaa taji la michuano ya wazi ya Australia kwa kumchapa Mhispania Rafael Nadal katika mchezo wa fainali.

Wawrinka alimfunga Nadal aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya mgongo kwa seti tatukwa moja, ikiwa ni kwa matokeo ya 6-3 6-2 3-6 6-3.

Anakuwa raia wa pili wa Uswis kunyakuwa taji la Grand Slam kwa upande wa wanaume kwa mchezo wa tenesi wa mchezaji mmoja mmoja.

Pia ni mtu wa pili kunyakuwa taji kubwa kama hilo akiwa ametoka nje ya vinara wanne wa juu wa dunia wa mchezo wa tenesi, baada ya Juan Martin Del Potro kufanya hivyo kwenye michuano ya US Open mwaka 2009.

Nadal ambaye awali alisema kusumbuliwa na matatizo ya mgongo lakini hakujitoa kwenye michuano hiyo ambayo imefikia tamati huko Melbourne Park."

Sikupenda kusema kwamba sitocheza mchezo wa fainali, ni jambo ambalo nachukia sana hatakama niligundua kuwa nina maumivu ya majeraha" Alisema Nadala mwenye umri wa miaka 27." Huu sio wakati wa kuzungumzia maumivu niliyoyapata, ila ni wakati wa kumpongeza Stan.

Amecheza vizuri sana na ukweli anastahili taji hili.Ni mtu mwema, mtu mzuri na rafiki yangu, nina furaha sana kwake kuwa bingwa" Alisema Nadal.

Naye Wawrinka alimsifu Nadal kwa kuwa bingwa wa kweli na kinara wa kweli wa tenesi duniani kwa wanaume, alikiri hujisikia furaha kupambana na kumshinda bingwa kama Nadal.

Wawrinka hajawahi kushinda hata seti moja katika michezo yote 12 aliyokutana na Nadal huko nyuma, na alicheza fainal yake ya kwanza akiwa kwenye nafasi ya 19 ya ubora wa tenesi duniani.

WAJUMBE WAAFIKIANA KUHUSU HOMS

Mazungumzo ya amani kuihusu Syria yanayoendelea mjini Geneva yanatarajiwa kuingia siku ya nne hivi leo Jumatatu, ili kujaribu kuyajibu maswali makubwa ya kisiasa kama vile sala linalozua utata la kukabidhi madaraka.

Lakini mazungumzo ya leo yataangazia pia maswala ambayo hayajapata suluhu kama vile kuruhusu misafara ya magari yanayobeba misaada ya chakula kuingia maeneo yaliyozingirwa namajeshi ya serikali katika mji wa kale wa Homs. Hapo jana Jumapili ujumbe wa serikali ya Syria katika mazungumzo hayo ulikubali kuwaruhusu watoto pamoja na wanawake kuondoka katika mji huo.

Akitoa hakikisho hilo Naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Syria Faisal Mikdad alisema kuwa serikali ya Syria iko tayari kuwaruhusu watoto pamoja na wanawake kuondoka akisema kuwa Serikali iko tayari kuwapokea na kuwapa misaada ya madawa, makao na mahitaji mengine ya kimsingi ikiwa makundi ya wapiganaji ambayo aliyataja kuwa 'magaidi' yatawaruhusu kuondoka.

Na katika hatua muhimu ya kuleta afueni katika mji huo wajumbe wa upinzani wamesema kuwa wapiganaji waliopo eneo hilo wataweka silaha chini kuruhusu misaada ya kibinadamu iwafikie maelfu ya raia.

Lakini baadhi ya viongozi wa upinzani wameelezea tashwishi kuhusiana na pendekezo hilo la serikali na kutaka hakikisho kwamba hakuna mtu atakaye kamatwa na kuzuiliwa. Mjumbe kutoka barazala kitaifa la upinzani nchini Syria Obeida Nahas amesema hatua hiyo ni muhimu. "Hii ni hatua muhimu ikiwa itaruhusiwa kufanyika.

Utawala haukutilia maanani kuruhusu hili mwanzoni, ulitaka orodha ya raia na watu waliojihami ndani ya mji wa kale wa homs swala ambalo kwa kweli haliwezekani ikiwa tunataka watu hawa waondoke. Lakini natumai watawaruhusu kuondoka. Nina maana ya raia waaruhusiwa kuondoka ikiwa wanataka." anasema Obeida Nahas.

Lakini taarifa kutoka mji wa homs zinasema kuwa raia wanafahamu kinacho endelea katika mazungumzo ya mjini Geneva lakini hawana imani katika serikali.

Mmoja wa madaktari wanaotoa huduma za matibabu kwa raia katika maeneo ya mashinani aliyetambuliwa kwa jina moja tu la Abu, amesema raia hawana imani katika serikali. "Wanafahamu, lakini kuna kitu muhimu-hawataondoka hadi pawe na hakikisho kwamba hawata kamatwa baada ya kutoka maeneo yaliyozingirwa. Tunahitaji hakikisho kutoka kwa utawala au umoja wa mataifa au shirika la msalaba mwekundu kutoa mwanya salama kwao.

Watakapo ondoka maeneo yaliyozingirwa tunapaswa kuhakikisha kuwa hawakamatwi" anasema Abu.

Mpatanishi wa umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi amechangamkia hatua hiyo ya kwanza muhimu iliyopigwa katika mazungumzo hayo akisema kuwa ingawa hapajakuwa na makubaliano kuhusu swala la kuachiliwa huru mahabusu, pande zote zitarejea kwenye meza ya mazungumzo hivi leo Jumatatu.

WALIOPORA KUFIKISHWA MAHAKAMANI MALAWI

Kesi ya maafisa wa zamani wa serikali ya Malawi wanaodaiwa kuhusika katika wizi wa mamilioni ya dola kutoka kwa hazina ya serikali inatarajiwa kuanza Jumatano.

Sakata hiyo ilifichuliwa kufuatia jaribio la mauaji dhidi ya mkurugenzi wa bajeti, Paul Mphwiyo - ambaye ameripotiwa alikuwa tayari kufichua kashfa kubwa zaidi.

Hii imetambuliwa kuwa kashfa kubwa zaidi kuwahi kutoke nchini Malawi.

Kashfa hiyo inayojulikana kama Cashgate imevuruga uhusiano mzuri ulioko kati ya Malawi na wafadhili huku raia wakikasirishwa na wizi huo wa mali ya umma.

Kashfa hiyo inaanzia katika eneo la kompyuta ambapo habari za siri kuhusu uwekaji fedha zimehifadhiwa.

Maafisa kadhaa wa Serikali wamekuwa wakitumia udhaifu fulani katika mpango wa uhifadhi wa kompyuta hizo na kuiba mamilioni ya pesa kutoka hazina ya Serikali.

Inadaiwa kuwa huenda Dola Milioni 250 ziliporwa kwa kuwalipa wafanyabiashara kimagendo kwa huduma ambazo hazikutolewa kwa Serikali.

Habari za uporaji huo wa mali ya umma zilifichuka wakati Mkurugenzi wa Bajeti katika Wizara ya Fedha, Paul Mphwiyo, alipopigwa risasi Septemba mwaka 2013.

Tukio hilo lilitekelezwa siku chache kabla ya mfanyakazi wa Cheo cha chini Serikalini alipopatikana na pesa taslimu ya Dola 300,000 katika buti ya gari lake. Pesa nyingi zaidi zilipatikana na kupokonywa wafanyakazi wa umma manyumbani mwao katika buti zamagari yao.

Wafadhili waku wa taifa hilo walikasirishwa pakubwa.

Wamesitisha utoaji wa Dola milioni 150 wakisubiri kufanya uamuzi baada ya uchunguzi katika kashfa hiyo kufanywa. Zaidi ya asilimia 40 ya bajeti yote ya Malawi hutegemea wafadhili.

Hata hivyo kungali kuna matumaini kwa Serikali ya Rais Banda kwa sababu Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeamua kutoa kwa Serikali jumla ya Dola Milioni 20, ambazo lilikuwa limezuilia.

Matokeo ya uchunguzi wa awali, uliofanywa kuhusiana na kashfa hiyo, kwa ushirika wa wataalamu kutoka Uingereza, umekamilika lakini matokeo yake hayajatangazwa.

Hadi kufikia sasa polisi wameshikilia magari, nyumba na afisi za washukiwa wote wa kashfa hiyo ya Cashgate.

Kesi ya wawili kati ya watu 70 ambao wameshtakiwa kufikia sasa itakapoanza juma hili, wengi wanatarajia kuwa ukweli zaidi utafichuka mahakamani.

WATU 20 WAHOFIWA KUFA KUTOKANA NA MLIPUKO

Watu 20 wanahofiwa kufariki kutokana na mlipuko katika ghalala silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini humo, vimesema kuwa nyumba nyingi ziliharibiwa wakati wa mlipuko huo katika kambi moja ya kijeshi karibu na soko kuu la Mbuji-mayi.

Mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mbuji-Mayi inasemekana ulisababishwa na radiKwa mujibu wa taarifa za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Monusco, zaidi ya watu 50pia walijeruhiwa huku nyumba kadhaa zikiharibiwa.

Lengo la Monusco nchini humo nikupokonya makundi yanayopigana silaha.

DRC inajaribu kutokamana na vita vilivyo sababisha mamilioni ya vifo kati ya mwaka 1998 na 2003.'Nimewaamrisha maafisa wetu walio mjini Mbuji-Mayi kushirikiana na wenyeji ili kusaidiana kukabiliana na hali,'' alisema Martin Koble mkuu wa kikosi hicho cha Monusco.

Mbuji-Mayi ni mji wa tatu kwa ukubwa DRC, na ndio kitovu cha uchimbaji wa madini ya Almasi.

NDGE YA ZAN AIR YAANGUKA HUKO PEMBA

Abiria 17 akiwemo waziri wa katiba na sheria Zanzibar Mhe. Abubakari khamis bakar, na marubani wawili, wamesalimika kifo baada ya ndege ya shirika la ndege la 'Zanz air' kufeli breki, muda mfupi wakati ndege hio ilipo kuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Abeid amani karume, uliopo nje kidogo ya mji wa chakechake mkoa wa kusini Pemba.

Kwa mujibu wa tarifa zilizo tolewa na makamanda wa polisi mkoa kusini Pemba kamishina msaidizi swalehe mohamed swalehe na kamanda wa kikosi cha zima moto na uokozi pemba wamesema ndege hiyo wakati wa kutua ilipata hitilafu ya kufeli breki na kusereka hadi nje ya uwanja umbali wa mita mia mbili kwenye vichaka.

Wamesema abiria wote wametoka salama hakuna alie juruhiwa licha ya ndege hio kuacha uwanja kusereka kwenye nyasi na kungia kwenye mashamba ya muhogo kupita kwenye masiki majiti yalio katwa na kisha kusimama baada ya ringi kujizonga na mizizi ya pori hilo.

Ipo haja kwa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini kutoa taaluma kwa watendaji wa kiwanja cha ndege kisiwani pemba kutoa ushirikiano kwa wandishi wa habari pale inapo tokea dharura kutokana na watendaji wa kiwanja cha ndege kisiwani hapa kushindwa kabisa kutoa ushirikiano kwa wandishi juu ya tukio hili.

MWANAFUNZI AGOMA KWENDA SHULE KUHOFIA KUZOMEWA, BAADA YA TAARIFA YA KULAWITIWA

MWANAFUNZI mmoja (Jina limehifadhiwa umri wake ni 16) wa Darasa la Saba katika Shuleya Msingi Mkombozi iliyopo katika mji mdogo Mbalizi Wilaya ya Mbeya Mkoani hapa ameshindwa kuendelea na masomo tangu shule zifunguliwe akiogopa kuzomewa na wenzie baada ya kuhisiwa kulawitiwa na Mwalimu Mkuu wake.

Hatua ya mwanafunzi huyo kushindwa kufika shuleni kuungana na wenzie kumetokana na madai ya kuzagaa kwa tuhuma za Mkuu wake wa shule kumwingilia kimwili mwanafunzi huyo mwenye jinsia ya kiume wakati wa masomo ya jioni(Twisheni).

Akizungumza na waandishi wa habari Mwanafunzi huyo alisema Mwalimu wake huyo ambaye alimtaja kwa jina la Lusekelo Thom, kuwa anatabia ya kumbakiza yeye peke yake baada ya muda wa masomo ya jioni kuisha na ndipo huenda naye ofisini na kuanza kumvua nguo.

Alisema tatizo hilo limedumu kwa kipindi kirefu tangu Aprili Mwaka jana hadi Disemba 27, mwaka jana baada ya bibi anayemlea kugundua (jina limehifadhiwa kwa ajili ya upelelezi) katika mahojiano kutokana na mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani kila siku tofauti na wengine.

Kwa mujibu wa majirani wa Mwanafunzi huyo walisema kugundulika kwa maovu anayofanyiwa na mwalimu wake kulitokana na upotevu wafedha shilingi 20,000 na ndipo bibi huyo alipomuona mjukuu wake akiwa na mkebe mpya nandipo alipomuuliza kuhusu fedha zake ambapo Mwanafunzi huyo alikataa kabisa.

Walisema baada ya kubanwa zaidi alidai fedha za kununulia mkebe alipewa na Mwalimu wake na amekuwa na kawaida ya kumpa fedha mwanafunzi huyo kila siku ikiwa ni pamoja na kumwambia asilipe ada ya masomo ya jioni kwa madai kuwa atakuwa anamlipia.

Alipobanwa zaidi mwanafunzi huyo alidai kuwa baada ya kupewa fedha na mwalimu huyo huenda naye ofisini na kufunga mlango kisha huvua nguo zake na kumwamuru naye avue na kumlazimisha ashike nyeti za mwalimu wake huku mwalimu naye akimshika shika na huo mchezo ulikuwa ukifanyika kila siku na baada yahapo mwalimu alikuwa akimrudisha mwanafunzi kwa bibi yake majira ya saa mbili usiku.

Mashuhuda wa tukio hilo na baadhi ya walinzi wa shule hiyo walikiri kuwepo kwa tuhuma za udharirishaji wa Mwalimu huyo kwa Mwanafunzi kwa madai kuwa kila siku Mwalimu huyo kujifungia ofisini na mwanafunzi ikiwa ni pamoja na kuongozana naye kila mara.

Aidha baadhi ya ndugu walisema baada ya kubaini hali hiyo walienda kutoa taarifa katika kituo kidogo cha Polisi cha Mbalizi ambapo Jeshi la Polisi lilimkamata Mwalimu huyo Januari 4, Mwaka huu na kufanya naye mahojiano kisha kumpeleka mwanafunzi huyo Hospitalini kwa ajili ya vipimo.

Hata hivyo Mwalimu huyo alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alikataa kuhusika huku majibu ya vipimo vya Hospitali vikionesha kutokuingiliwa kimwili kwa mwanafunzi ingawa Maelezo ya mtoto alidai kuchezewa nyeti zake kila siku na kwamba suala la kuingiliwa kimwili alikuwa akilazimishwa lakini hakuweza kufanikiwa.

Mwalimu huyo aliachiwa na jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha Mbalizi alipokuwa ameshikiliwa kwa ajili ya mahojiano baada ya kuwekewa dhamana na Mratibu wa Elimu kata ya Utengule Usongwe, Fredrick Silumbwe, na kwamba upelelezi bado unaendelea ili kubaini kama kweli mwalimu huyo anafanya vitendo hivyo huku kukiwa na taarifa kuwa Mwalimu huyo baada ya tukio hilo alisafiri na kuelekea KibahaMkoani Pwani ambako yuko hadi sasa.

Kwa upande wake Mratibu Elimu kata alipoulizwa kuhusiana na tuhuma dhidi ya mwalimu wake alisema hata yeye amekuwa anazisikia mitaani na kuhusu kuweka dhamana alikiri kwa madai kuwa alipigiwa na baadhi ya walimu na ndipo alipofanya hivyo kutokana na dhamana ni haki ya kila mtu.

Naye Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Mbeya, Dionice Boay alipoulizwa kuhusiana na tuhuma za Mwalimu wake alikiri kuzipata na kuongeza kuwa kutokana na Mwalimu huyo kufikishwa katika vyombo vya Sheria wao kama Ofisi hawana cha kufanya zaidi ya kusubiri Ripoti ya Polisi ambapo Mwalimu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma.

Alisema kama ofisi hatua ya kwanza ni kumsimamisha kazi na kuteua Mwalimu mwingine kukaimu Ukuu wa Shule ya Msingi Mkombozi wakati ofisi ikisubiri taratibu za Kimahakama kutokana na tatizo hilo kuegemea kwenye makosa ya jinai.

Aliongeza kuwa Ofisi pia inatarajia kufanya ukaguzi katika shule hiyo ili kubaini kama Mwalimu alikuwa na makosa mengine na kujua sababu ya Mwanafunzi kutoenda shule hadi sasa licha ya wenzie kuendelea na masomo.

Hata hivyo Kituo cha Haki za Binadamu kilionesha mshangao kutokana na mtuhumiwa wa tukio hilo kuachiwa kwa dhamana ili hali upelelezi haujakamilika na hakuna hatua zozote ambazo Jeshi la Polisi linaonesha kulifanyia kazi ambapo mtuhumiwa alifikishwa Polisi Januari 4, Mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kituo cha Haki za Binadamu Mkoa wa Mbeya, Said Madudu alisema Jeshi la Polisi limechukulia suala hili kama ni siasa kwa kuchelewa kuchukua hatua kwa wakati huku mtoto akiendelea kukosa haki yake ya msingi ya masomo.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema atalifanyia kazi kutokana na kutokuwa Ofisini kwa wakati huo na kulitolea ufafanuzi unaotakiwa.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa umebaini kuwepo kwa rushwa zinazopelekea upelelezi wa kesi hiyo kuchelewa kutokana na kuwepokwa taarifa za Mtuhumiwa kutoa fedha shilingi Milioni Tatuambazo bado haijulikani mgao wake uliwagusa akina nani.

MAUWAJI YA KINYAMA YAKITHIRI MUSOMA

Vitendo vya Mauaji ya watu katika maeneo mbali mbali vimeanza kujitokeza katika wilayani za Butiama na Musoma Mjini Mkoani Mara, kufuatia watu wawili Kuwawa akiwemo mama mmoja Mkaguru Magee mkazi wa kijiji cha Mkirira na Mzee Aitwaye Shaabani Mkazi Nyakato katika wa manspaa ya mji wa Musoma kuuwawa kikatili na watu wasiojulika.

Wakiongea kwa Nyakati Tofauti Mashuhuda wa matukio hayo wanasema kuwa matukio kama haya yalijitokeza mwaka jana kwa kuuwawa kwa wanawake na wazeezaidi ya 17 katika wilaya hizo kwa kuchinjwa jambo lililowatia hofu na kuiomba Serikali kusaidia kupambana na tatizo hilo kutokana na matukio hayo kuanza tena kujitokeza na kuwafanya washindwe kufanya shughuli zao za kifamilia kwa kuhofia maisha yao.

Ni miongoni mwa akinamama wakazi wa Wilaya za Butiama na Manspaa ya Mji wa Musoma, wakionyesha majonzi yao kufuatiavifo vya mfululizo vya Watu wawili waliouwawa kikatili na watu wasiojulikana na miili yao kutelekzwa katika kijiji cha Mkirilana kiongoji cha msikamano eneo la Nyakato mjini Musoma.


Wakizungumza viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mkirila na mwenyekiti wa kitongoji cha Mshikamano mjini Musoma wameonyesha kukata tamaa kutokana na kukithili kwa matukioya mauaji katika maeneo hayo.

Kwa upande wa viongozi mbali mbali wanasema kuwa matukio yamauaji katika maeneo hayo yanatokana na wakazi wake kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polis ili kuwashughulikia watuhumiwa.

Nae mwenyekiti wa kamati ya Urinzi na usalama wa wilaya ya Butiama mama Anjerina Mabula,anatoa kauli ya Serikali katika kupambana na matukio hayo.

SUDANI KUSINI NA WAASI WAKUBALIANA KUMALIZA VITA

Waakilishi wa serikali ya Sudan Kusini wanasema kuwa serikali imetia saini mkataba wa kusitisha vita na waasi.

Kulingana na mkataba huo uliotiwa saini mjini Addisa Ababa Ethiopia, mapiganao yanapaswa kusitishwa katika muda wa masaa 24.

Aidha mkataba huo unatarajiwa kusitisha vita vya mwezi mmoja vilivyoanza tarehe 15 Disemba mwaka jana kati ya waasi na serikali.

Mazungumzo ya amani yamekuwa yakikumbwa na matatizo kuhusu swala la wafungwa 11 wa kisiasa ambao bwana Riek Machar anayeongoza waasi alitaka waachiliwe kama sharti la kutia saini mkataba wa amani.

Wiki jana wanajeshi wa serikali walifanikiwa kukomboa miji kadhaa iliyokuwa imetekwa na waasi.

Zaidi ya watu 500,000 wamelazimika kutoroka makwao kutokana na vurugu hizo za mwezi mmoja.

CCM YAONYA MAWAZIRI MZIGO NA WAFANYAKAZI

Chama tawala nchini CCM, kimeonya kwamba, hakitasita kuwachukulia hatua kali watendaji wa serikali wakiwemo mawaziri watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kauli ya chama hicho imetolewa siku chache baada ya Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kulifanyia mabadiliko baraza lakela mawaziri huku baadhi ya mawaziri waliolalamikiwa na wananchi pamoja na wabunge kuwa ni mzigo kwa serikali wakiendelea kubakia katika nyadhifa zao.

Mara baada ya Rais Kikwete kutangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, kuliibuka mjadala miongoni mwa wananchi, vyombo vya habari na wachambuzi wa masuala ya siasa kuhoji kulikoni Rais hakuchukua hatua ya kuwatimua mawaziri hao.

Hata hivyo, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, amebainisha kuwa, haikuwa hoja ya chama hicho kuwafukuza mawaziri hao ila ametoa onyo kali kwao ikiwa hawatafanikisha majukumu na amza ya serikali kuwahudumia wananchi.

Mara kadhaa, maagizo ya kuchukuliwa hatua watendaji wa serikali wasiowajibika yamekuwa yakionekana kama kiini macho nawananchi wa kawaida.

Hata hivyo wachambuzi wa siasa walio na shaka na vitisho vya CCM kwa mawaziri mizigo, wanasema kuwa chama cha CCM ikiwa kitachukua hatua dhidi ya maafisa wake wasiotenda kazi vyema kitakuwa kinajiharibia sifa kama chama chenyewe.

Tuhuma dhidi ya baadhi ya mawaziri kupwaya katika utendajiwao zilitolewa na wananchi na kisha Wabunge wakati wa ziara yasiku 26 iliyofanywa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM kitaifa katika mikoa minne iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bwana Abdulrahman Kinana, mwishoni mwa mwaka jana.

Disemba mwaka jana, CCM kupitia kikao chake cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa,ilimtupia mpira Rais Kikwete kuamua hatma ya mawaziri hao, huku kikifafanua kuwa, ilimshauri ama kuwafukuza, kuwahamisha wizara au kuwahimiza wafanya kazi.

Lakini katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Kikwete hivi karibuni mawaziri hao waliendelea na nyadhifa zao

WACHIMBAJI WA MIGODI WAGOMA A.KUSINI

Mgomo mkubwa zaidi wa wafanyakazi wa machimbo ya madini ya Platinum nchini Afrika Kusini, utaanza siku ya Alhamisi, kulalamikia mishahara duni.

Mgomo huo utasitisha uchimbaji wa madini hayo katika migodi ya kampuni tatu mikubwa zaidi duniani kwa uzalishaji wa madini ya Platinum.

Chama cha wafanyakazi wa sekta ya madini nchini humo AMCU kimesema kuwa zaidi ya wafanyakazi elfu sabini wataanza mgomo huo siku ya Alhamisi, hadi matakwa yao yatakapotimizwa.

Huu ni mgomo mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika secta ya uchimbaji wa madini ya Platinum tangu mkasa wa mwaka juzi wa Marikana ambapo wachimba migodi wapatao 34 walipigwa risasi na polisi walipokuwa wakiandamana kuendeleza mgomo wao , uliotajwa na serikali kuwa haramu.


*MGOMO HALALI*

Safari hii gomo huu wa kudai nyongeza ya mishahara unaongozwa na AMCU chama cheye msimamo mkali cha kutetea wafanyaki wa migodini na mafundi katika sekta ya ujenzi.

Wachimba migodi hao ambao hufanya kazi kwenye machimbo ya kina kirefu sana, wanadai mishahara ya takriban dola elfu moja na mia mbili kwa mwezi, ikiwa ni maradufu ya mishahara wanayopokea sasa.

Tofauti na mgomo wa Marikana, mgomo huu wa sasa ni halali kisheria.

Kampuni zote tatu za Anglo American, Impala na Lonmin Platinum zimethibitisha kupokea notisi za mgomo.

Hata hivyo wanadai hawawezi kumudu kulipa nyongeza hiyo inayodaiwa kwa sababu ya gharama za uzalishaji ni kubwa namauzo ni haba.

Afrika Kusini ndio nchi inayozalisha madini ya Platinum kwa wingi zaidi huku asilimia 80% ya madini hayo yakiwa bado hayajachimbwa.

MWANAMKE ABAKWA KUTOKA KWA AMRI YA WAZEE

Polisi nchini India wamewakamata wanaume 13 waliohusishwa na genge la wanaume waliombaka msichana mwenye umri wa miaka 20 katikajimbo la Benghal Magharibi.

Inadaiwa wanaume, hao walimbaka mwanamke huyo kufuatia amri ya wazee wa kijiji ambao wamejipa wenyewe mamlaka ya mahakama ya kitamaduni.

Msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu akiwa hali mahututi.

Inaarifiwa amri ya kumbaka mwanamke huyo ilitolewa na wazee wa kijiji ambao walipinga uhusiano wake na mwanamume kutoka katika jamii tofauti.Hiki ndicho kisa cha hivi karibuni cha genge la wanaume kumkaba mwanamke nchini India.

Tangu kisa cha ubakaji wa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 uliofanywa na genge la wanaume mjini Delhi mwaka 2012 , swala la ubakaji limekuwa likiangaziwa sana nchini India.

Hasira ya mamilioni ya watu iliyotokana na kisa hicho ilipelekea vyombo vya habari nchini India kuanza kuangazia tatizo hilo , swala ambalo wangi walihisi lilikuwa limepuuzwa kwa muda mrefu.

Serikali nayo ilianza kuweka sheria kali kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya wanawake.

Lakini utekelezwaji wa sheria hizo bado ni changamoto katika nchi ambayo ustawi wa kijamii unakuwa kwa kujikokota na ukosefu wa usawa likisalia kuwa tatizo jengine kubwa.

Wengi wameshangazwa kuwa katika kisa hiki, ubakaji umeamrishwa na kikundi cha wazee wa kijiji ambao wamejipa mamlaka kama viongozi wa kijamii.

DOKTA MAGUFULI AWEKA KAMBI DUMILA

Dr. Magufuli aenda kupiga kambi Morogoro ama kusimamia mwenyewe ujenzi wa Daraja la Dumila lililopo mkoani Morogoro ambalo ni kiungo muhimu cha barabara ya Dodoma – Morogoro lililosombwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 22.01.2014 na kusababisha magari kutopita kabisa ama yanayotoka upande wa Dodoma au Morogoro, mbaya zaidi hakuna hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo.

WANARIADHA WATISHIA KUSUSA MASHINDANO, MATA AELEKEA MAN U, HUKU WAKIBANDULIWA NA SUNDERLAND

Wanariadha wa Kenya wameapa kupinga mpango wa serikali wa kuwalazimisha kulipa kodi kutokana na mapato yao.

Siku ya Jumanne, Shirika la utozaji ushuru nchini Kenya KRA ilitangaza kuwa mapato yote watakayoshinda wanariadha, ikiwa ni pamoja na wachezaji wa soka nje na ndani ya nchi ni sharti itozwe ushuru kuanzia mwezi huu.

Lakini wanamichezo hao ambao huchagia kiasi kikubwa cha mapato yao katika uchumi wa taifa, wametishia kususia mashindano yote ya kimataifa ikiwa serikali itaendelea na mpango huo wa kuwatoza ushuru.

Wanariadha hao wamesema fedha wanazopata sio nyingi kwa huwa hawashindi hela kila mwezi na huenda ikawachukua zaidi ya miaka mitano kujiinua tena ikiwa serikali itawatoza ushuru.

Wakiongea mjini Eldoret, Magharibi mwa Kenya wanariadha hao, wakiongozwa na mbunge wa Cherangani ambaye pia ni bingwa wa zamani wa mbioza Boston Marathon Wesley Korir, wanariadha hao wanadai kuwa KRA haina mfumo dhabiti wa kubaini kiasi cha fedha walizoshinda wanariadha, kwa sababu shirika hilo halija orodhesha mbio walizo shiriki na kiasi cha fedha walizoshinda.

Mwaka wa 2012, wanariadha kadhaa akiwemo mshikilizi wa rekodi ya dunia wa mbio za mita mia nane kwa upande wa wanaume David Rudisha, bingwa mara mbili wa dunia wa mbio za Marathon Abel Kirui, walikabithiwa nyaraka na KRA kuwataka kulipa malimbikizi ya kodi inayokisiwa kuwa mamilioni ya madola.


*SUNDERLAND YAIBANDUA MAN U*

Manchester United, kwa mara nyingine tena ilikiona cha mtemakuni pale ilipobanduliwa nje ya kinyanganyiro cha kuwania kombe la Ligi maarufu kama Capital one na timu inayoshikilia nafasi ya pili kutoka mkia kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier, Sunderland.

United ililazimika kuyaaga mashindano hayo baada ya kushindwa kupitia mikwaju ya penalti na Sunderland.

Baada ya muda wa kawaidia United ilikuwa ikiongoza kwa goli moja kwa bila, lakini kuwa walipoteza mechi ya awamu ya kwanza kwa magoli mawili kwa moja, mechi hiyo ilibidi kuongezwa dakika thelathini zaidiza ziada.

Katika muda huo wa ziada Sunderland nusura ifuzu moja kwa moja lakini sherehe hizo zilikatizwa baada ya dakika moja pale United iliposawazisha kupitia kwa nyota wake Chicharito, na hivyo kufanya timu hizo mbili kutoshana nguvu ya jumla ya magoli matatu kwa matatu bada ya dakika mia moja na Ishirini.

Mechi hiyo iliamuliwa kupitia mikwaju ya penalti na kwa mara ya kwanza, makipa wa timu hizo mbili waliokoa mikwaju kadhaa.

Kwa Ujumla mikwaju saba ziliokolewa au kupigwa nje na hivyo Sunderland kujikatia tikiti ya fainali dhidi ya Manchester City kwa magoli mawili kwa Moja.

Fainali ya kombe hilo itachezwa tarehe mbili Machi mwaka huu katika uwanja wa Wembley.


*KATIKA USAJILI*

Ombi la Manchster United la kutaka kumsajili nyota wa Chelsea Juan Matata imekubalika.

Ripoti zinasema United imetumia takriban kitita cha pauni milioni 37 kumsajili mcheza kiungo huyo wa Chelsea.

Mata mwenye umri wa miaka 25,anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baadaye hii leo, kabla ya kukamilisha usajili huo.

Mchezaji huyo kutoka Uhispania anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu hiyo iliyo na makao yake katika uwanja wa Old Trafford.

Mata ambaye aliichezea Chelsea, mechi 32, aliwaaga wachezaji wenzake na wakufunzi wa Chelsea katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham siku ya Jumatano.

REAL MADRID KLABU TAJIRI ZAIDI, MAN U CHALI

Klabu ya Real Madrid imehifadhi taji la kuwa klabu tajiri zaidi duniani kwa msimu wa tisa mfululizo, kuambatana na orodhaya vilabu tajiri iliyochapishwa na kampuni ya uhasibu ya Deloitte.

Klabu nyingine ya Uhispania, Barcelona inashilikia nafasi ya piliikifuatwa na Bayern Munich ya Ujerumani, katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.

Kwa mara ya kwanza klabu ya Manchester United ambayo kwa sasa imekabiliwa na msururu wa matokea mabaya katika ligi kuu ya Premier ya England, imeshushwa miongoni mwa vilabu tatu tajiri zaidi duniani kwamara ya kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na saba iliyopita.

Manchester city imepanda mpaka nafasi ya sita kuzipiku Chelsea(7), na Arsenal(8)

Waandishi wa habari wanasema kuwa ligi ya vilabu vingi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha, nyingi yavilabu hivyo vinaendelea kupata hasara kubwa kutokana na gharama za mishahara na malipo ya usajili wa wachezaji.

NDEGE ISIYO NA RUBANI(DRONE) YATUMIKA KUSIMAMIA MTIHANI

Ndege isiyo na rubani (drone) yatumika kusimamia mitihani.

Shule moja ya nchi Ubelgiji imeamua kutumia ndege isiyo na rubani (drone) kusimamia mitihani baada ya kushindwa mbinu za kawaida kuwazuia wanafunzi kufanya udanganyifu katika mitihani yao.

Ndege hiyo ina kamera ya kuchukua picha za video pamoja na kurekodi harakati yoyote inayotia wasiwasi kutoka kwa mwanafunzi yeyoteyule na kurusha moja kwa moja kwenye TV harakati yoyote ile isiyo ya kawaida.

POLISI WAWAFYATULIA RISASI WANAOTAKA MASHOGA KUNYONGWA

Maafisa wa ulinzi Kaskazini mwa Nigeria wamefyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji, waliokuwa wakishinikiza adhabu ya kifo kwa wanaume saba ambao wametuhumiwa kuwa wanachama wa shirika moja linalohimiza mapenzi ya jinsia moja.

Wanaume hao walikuwa wakishtakiwa chini ya sheria za Kiislamu maarufu kama Sharia, mjini Bauchi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kesi hiyo ilivurugwa na mamia wa vijana waliokuwa wamejawa na hasira ambao walirusha mawe nje ya mahakama hiyo.

Polisi waliwatawanya waandamanaji hao ili kupata nafasi ya kuwarejesha washukiwa hao gerezani.

Nchini Nigeria, vitendo vyote vyote vya mapenzi ya jinsia moja ni haramu chini ya sheria za Kiislamu na hata sheria zingine zakidini na kitamaduni.

Sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja nchini Nigeria, ilifanyiwa marekebisha hivi majuzi ili watakaopatikana na hatia kupewa adhabu kali.

MVUA YAKATISHA MAWASILIANO KATI YA DODOMA NA MOROGORO

Maelfu ya abiria wamekwama katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma, na kulazimika kusitisha safari zao, baada ya mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia siku ya Jumatano, kusababisha mafuriko makubwa yaliyofanya daraja la Magole, linalokatiza mto kikundi katika eneo la Dumila,kwenye barabara hiyo kukatika.

ITV imeshuhudia maji mengi yakiwa yameziba barabara kuu ya Morogoro-Dodoma, huku visiki vya miti vikiwa vimeziba barabara, na eneo la mto Kikundi unaomwaga maji mto wami, ukiwa umefurika na daraja la magole likiwa limebomoka kabisa na kusababisha watu kutoka upande mmoja kushindwa kuvuka kwenda upande mwingine,huku wananchi wa eneo hilo wakidai hii ni mara ya kwanza kwa mafuriko ya aina hiyo kutokea, yaliyosababisha mashamba na makazi ya watu kuharibika na hata daraja kubomoka.

Wananchi hao wameshauri wakala wa barabara nchini tanroads kuzingatia ubora katika ujenzi wa barabara na madaraja, huku meneja wa wakala huo mkoa wa Morogoro, injinia doroth mtenga, akizungumzia athari za uharibifu uliojitokeza, na naibu waziri wa uchukuzi, dk charles tzeba aliyebainisha vituo 11 vya reli navyo kuharibiwa kwa mvua,akiwashauri wananchi kukaa mbali na eneo hilo kutokana na daraja kuzidi kubomoka kadiri muda ulivyokuwa ukiendelea sambamba na magari kutumia njia nyingine mbadala kuendelea na safari.

Baadhi ya wananchi wameiomba serikali kufanya jitihada za haraka, kuwanusuru wananchi waliokuwa mashambani na majumbani,walioweza kujiokoa kwa kupanda juu ya miti, na juu ya paa za nyumba, waliokuwa wamezingirwa na maji,ambapo mtendaji wa kijiji cha magole, amesema mafuriko hayo yameathiri zaidi ya nyumba 300, ofisi za serikali, shule na nyumba za ibada katika kijiji hicho, na mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akibainisha tayari wameomba msaada wa helikopta ya polisi kuwanusuru watu hao.

Kufuatia maafa hayo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu Mh. Wiliam Lukuvi amewataka wasafiri wote waliokwama kurudi walikotoka na kutumia njia mbadala kwani daraja hilo la dumila limeondoka kabisa.

Amesema mafundi wa wakala wa barabara tanroads wapo eneo la tukio kujaribu kurejesha mawasiliano kazi ambayo inaweza kuchukua siku mbili au zaidi.

Ameshauri wanofanya safari kwenda Dodoma kupitia iringa au Arusha na wale waliokwama kurudi walikotoka


Chanzo:ITV

KAYA ZAIDI YA 500 ZAKOSA MAHALI PAKUISHI

Zaidi ya kaya 500 katika kijiji cha Magole wilaya ya kilosa mkoani morogoro hazina mahala pakuishi baada ya nyumba walizokuwa wakiishi kusombwa na mafuriko pamoja na mazao na mifugo yao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.


Wakizungumza na star tv wakazi wa kijiji hicho wamesema mvua hizo zimeleta madhara makubwa kwa upande wao kwani mpaka sasa hawajapata misaada yoyote ya kibinadamu na hawajui wapi pakuelekea.

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini tayari zimeleta madhara kwa wakazi zaidi ya 2500 mkoani morogoro baada ya kusababisha mafuriko yaliyobomoa nyumba na kusomba mazao, chakula pamoja na mifugo Wakizungumza kwa masikitiko kwa kutojua nini hatima yao, wakazi wa kijiji cha Magole wameiomba serikali kupeleka misaada ya kibinadamu ili kunusuru maisha yao.

Mkuu wa mkoa wa morogoro amefika eneo la tukio na kuwaomba wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikijipanga kutoa misaada kwa wahanga wa mafuriko hayo.

Aidha mbali na mafuriko hayo kuleta madhara kwa wakazi hao pia zaidi ya abiria 2000 wamekwama njiani kwa zaidi ya masaa matano kutokana na mafuriko hayo kuvunja daraja la magole barabara ya morogoro dodoma hivyo wasafiri hao kushindwa kuendelea na safari yao.

Mpaka star tv inaondoka eneo la tukio juhudi za uokoaji zilikuwa zikiendelea huku helkopta ya jeshi la polisi ikiwasili kwa ajiri ya kutoa msaada kwa wale walionasa kwenye maeneo hayo.

Chanzo: StarTv

USAJILI WA OKWI YANGA WASITISHWA NA TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wamshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA).

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada yakubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.

Okwi ambaye aliingia mgogoro naklabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi yaEtoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.

Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo.

Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro.

Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.

Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.


*MECHI ZA TANZANIA PRISONS YAZASOGEZWA*


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mechi zaraundi ya 14 na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari 25 na 29 mwaka huu.

Awali Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechihizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.

Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanjahuo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.

ODINGA: JESHI LILITUMIKA KUIBA KURA

Tume ya uchaguzi nchini Kenya imemtaka aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuomba radhi kwa matamshi yake kwamba serikali ya Uhuru Kenyatta ilitumia jeshi kuiba kura wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013.

Tume hiyo imesema kuwa matamshi ya Bwana Raila ni hatari na kwamba yanaweza kuzua vurugu na hivyo kumtaka kuomba radhi mara moja.

Aidha tume hiyo imemtaka Raila kutoa ushahidi wa madai yake la sivyo atake msahama tume hiyo. ''Licha ya kuwa uchaguzi ni siasa, matamshi ya Raila ni siasa mbaya,'' ilisema taarifa ya tume hiyo.

Raila alitoa matamshi yake katika muhadhara wa wafuasi wake katika jimbo la Kisumu Magharibi mwa Kenya ambako anatoka.

Tume ya uchaguzi inahoji kwa nini Raila hakutoa malalamiko hayo kama ushahidi wake wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mwaka jana badala ya kutoa matamshi mwaka mmoja baadaye.

Odinga aliwania uchaguzi kama Rais mwaka 2013 mwezi Machi ingawa alishindwa na punde baadaye aliwasilisha kesi katika mahakama kuu kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Odinga anasisitiza kuwa aliibiwa ushindi wake katika kile ambacho kimewaudhi washirika wa kisiasa wa Rais Kenyatta ambao wamekuwa wakimtaka akubali alishindwa.

TUHUMA ZA MAUAJI YA WAFUNGWA SYRIA

Ripoti iliyotolewa na viongozi watatu wa zamani wa mashitaka ya uhalifu wa kivita inasema kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kuwa Syria imewatesa na kuwaua karibu wafungwa 10,000 tangu kuanza harakati za kumpinga RaisBashar Al-Asaad.

Wachunguzi walipekua maelfu ya picha za wafungwa waliokufa zilizotolewa nchini Syria na mpiga picha mmoja wa jeshi aliyetoroka kazi.

Wanasema miili mingi ilikuwa imekonda na mingine mingi kupigwa na kunyongwa.

Mmoja wa waandaaji wa ripoti hiyo, Professa Geoffrey Nice, aliambia BBC kuwa wingi na uhakika wa ushahidi uliotolewa unaonyesha wazi kuwa Serikali ilihusika katika ukatili huo.


Uchunguzi huo ulifadhiliwa na Serikali ya Qatar inayowaunga mkono waasi wa Syria. BBC imejaribu mara kadhaa kupata majibu ya Serikali ya Syria kuhusu madai hayo lakini Serikali haijatamka lolote.

Madai kuwa wafungwa wamekuwa wakiteswa na kuuawa katika magereza ya Syria yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na wakereketwa wa haki za kibinadamu tangu maasi yaanze nchini humo miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo madai ya sasa yana upya fulani kwa njia ya kipekee.


Habari hizi zina ushahidi kutoka kwa wandani wa Serikali wenyewe; mpiga picha wa kitengo cha jeshi cha polisi aliyetoroka kazi amewasilisha maelfu ya picha ambazo alipiga kabla ya kutoroka.

Na wachunguzi wa kimataifa, waliokuwa viongozi wa mashtaka sasa wanaamini kuwa picha walizoona za miili iliyoharibiwa vibaya, iliyopewa nambari na kupigwa picha mara kadhaa, ni ushahidi wa kuaminika.

Zaidi ya miili 11,000 ilipigwa picha ingawa bado kuna wasiwasi kuwa kuna maelfu ya watu ambao walizuiliwa magerezani lakini sasa hawajulikani waliko.

WAHUDUMU WA AFYA WAUAWA PAKISTANI

Watu waliojihami katika mji wa Karachi nchini Pakistan, wamewaua kwa kuwapiga risasi wahudumu watatu wa afya wakiwemo wanawake wawili waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio.

Hili ni shambulizi la hivi karibuni likiwalenga wahudumu wa afya wanaotoa chanjo ya Polio au ugonjwa wa kupooza.

Walioshuhudia shambulio hilo walisema waliona watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wakiwa wanaendesha Pikipiki wakiwapiga risasi wahudumu wa afya waliokuwa wanatoa Chanjo hiyo kwa watoto wadogo.

Mwanamke mmoja alifariki papo hapo wakati mwingine alifariki akipelekwa hospitalini.

Shambulizi hilo ni pigo kubwa kwa juhudi za Pakistan kupambana na ugonjwa huo unaolemaza.

Kando na Afghanistan na Nigeria, Pakistan ni moja ya nchi ambako ugonjwa wa Polio ni janga kubwa.

Wapiganaji wa Taliban wanapinga chanjo ya ugonjwa wa kupooza nawamekiri kuwaua wafanyakazi waafya wanaotoa chanjo hiyo nchini Pakistan.

MSAFARA WA RAIS KAGAME WAPATA AJALI

Watu wawili wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha mojawapo ya magari ya msafara wa magari ya Rais Paul Kagame nchini Kenya.

Rais Mwenyewe hata hivyo hakujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi katika eneo la Limuru eneo la Kati mwa Kenya.

Dereva wa gari hilo alipoteza mwelekeo katika barabara kuu ya Nairobi-Limuru.

Gari hilo hata hivyo lilipoteza mwelekeo likiwa mbali na msafara wenyewe.

Waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.

Rais Kagame alikuwa anarejea mjini Nairobi kutoka katika kongamano la magavana wa Kenya mjini Naivasha katika bonde la ufa.

Kwa sasa Kagame anakutana na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Rais.

Kagame alialikwa kuhudhuria kongamano la Magavana nchini Kenya kuhusu uongozi mzuri na utawala bora.

Aliwahutubia Magavana hao siku ya Jumatatu na kuwashauri kuwa husisha wananchi katika maamuzi yao ya maendeleo.

Aliwataka kuwahusisha wananchi katika maamuzi ili waweze kujieleza wenyewe kuhusu matatizo na changamoto wanazokabiliwa nazo pamoja na kutafuta suluhisho kwa pamoja.

Mfumo wa serikali za majimbo nchini Kenya ulitokana na katiba mpya ambapo huduma nyingi zilizokuwa zinatolewa na serikali kuu sasa zinapaswa kutolewa na magavana ambao ndio wakuu wa majimbo.

Kumekuwa na maandamanao ya mara kwa mara katika majimbo kutokana na magavana kuanza kuwatoza kodi za ajabu wananchi ili kuweza kupata pesa za maendeleo.

WATU 13 WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI

Watu 13 wamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Isuna mkoani humo.

Habari zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo namba zakeza usajili hazikupatikana mara moja.

Watu 13 waliofariki walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.

Baada ya ajali hiyo, dereva wa lori na msaidizi wake walitokomea kusikojulikana.

CAR YAPATA RAIS MPYA WA MPITO

Wabunge katika Jamhuri ya Afrikaya Kati, wamemchagua Meya wa mji mkuu Bangui, Catherine Samba-Panza, kama Rais wa mpito.

Samba-Panza, ndie mwanamke wa kwanza kuwahi kushikili wadhifa huo.

Wagombea wanane waliwania wadhifa huo ambao ulikuwa unaushikiliwa na Michael Djotodia, aliyeng'atuka mapema mwezi huu kufuatia shinikizo kutoka kwa viongozi wa mataifa jirani.

Panza alimpiku mshindani wake wa karibu Desire Kolingba katika duru ya pili ya kura hiyo.

Wakati huohuo mawaziri wa mambo ya nje wa Muungano wa Ulaya wamekubaliana kukutana Jumatatu kupeleka wanajeshi zaidi nchini CAR.

Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa takriban watu hamsini wameuawa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo mwishoni mwa wiki.

Mapigano yalianza wakati Djotodia alipochukua mamlaka mwaka jana kwa njia ya mapinduzi akiungwa mkono na waasi wa kiisilamu katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya waumini wa kikristo.

Waisilamu wawili waliteketezwa katika mji mkuu Bangui siku ya Jumapili.

Karibu watu milioni moja wameachwa bila makao kutokana na mgogoro huo.

MJI WA BOR WAHARIBIWA VIBAYA

Habari kutoka Sudan Kusini zinasema kuwa mji wa Bor uliokombolewa hivi karibuni na wanajeshi wa Serikari umeharibika kabisa kufuatia mapambano na waasi.

Mwandishi wa BBC aliyetembelea Bor siku moja baada ya mji huo kukombolewa amesema kwa wakati huu hakuna mtu yeyote ndani ya mji huo.

Nyumba zimeteketezwa na Soko Kuu limeharibiwa kabisa.

Maiti zilizoteketea zilionekana kila mahali nje ya hospitali ambayo ilionekana kuporwa.

Wagonjwa walisema kuwa kuna watu waliopigwa risasi ovyo na kuuawa.

Wajumbe kutoka pande zote mbili wanatarajiwa kuanza mashauriano katika mji mkuu wa Ethiopia wakati wowote kuanzia sasa.

Wakati huohuo, wanajeshi wa Sudan Kusini walipambana na waasi Jumatatu huku Umoja wa Mataifa ukisema kuwa wanajeshi walijaribu kuingia kwa nguvu katika kambi yake inayo wahifadhi maelfu ya wakimbizi wa ndani waliotoroka vita.

Maelfu ya raia wasio na hatia wameuawa na karibu nusu milioni kuachwa bila makao huku katika vita hivyo ambavyo vimeingia sasa wiki ya sita.

Mazungumzo ya amni kuhusu mzozo huo nayo yamekwama nchini Ethiopia.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa uhalifu dhidi ya binadamu umefanywa na pande zote kwenye mgogoro huo.

OBAMA ASEMA BORA BANGI KULIKO POMBE

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa kuvuta Marijuanaau Bhangi, sio hatari ikilinganishwa na Pombe.

Lakini Obama amesema kuwa Bhangi bado ni mbaya kwa afya ya binadamu.

Katika mohojiano na jarida la The New Yorker, alisema kuwa ni vibaya kuwa na dhana kwamba kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya ndio jibu kwa maasi mengi yanayotokea katika jamii Bwana Obama alikuwa akigusia hatua ya hivi karibuni ya majimbo ya Colorado na Washington kuhalalisha utumiaji wa Bhangi.

Obama aliwahi kukiri kutumia dawa hiyo ya kulevya alipokuwa kijana.

"kama mnavyojua nyote nilivuta Bhangi nilipokuwa kijana na ninaiona kama tabia mbaya sawa na kuvuta sigara,'' alisema Obama Lakini aliongeza kwamba athari za Bhangi kwa afya ya binadamu sio mbaya ikilinganishwa na Pombe.

Pia alisema kuwa watu masikini wengi wao wamarekani wenye asili ya kiafrika na walatino, waliadhibiwa visivyo kwa kutumia Bhangi wakati watu wenye kipato cha kadri walikwepa adhabu kali."

Ni muhimu kwa jamii kufahamu kuwa sio sawa ikiwa idadi kubwa ya watu wanovunja sheria huwaadhibiwi vilivyo wakati wachache wanapata kuadhibiwa.

''Obama alitaja kuhalalisha Bhangi katika majimbo ya Colorado na Washington kama hali ya kutatanisha.

MABADILIKO YA WIZARA MBALIMBALI YALIYOFANYWA NA MH. RAIS JK

Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-


OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko

Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)-Waziri wa Nchi (Mazingira).

Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)Naibu Waziri

OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA FEDHA

Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) – Waziri wa Fedha

Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb) – Naibu Waziri wa Fedha

Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)- Naibu Waziri wa Fedha

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)-Waziriwa Katiba na Sheria

Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko

WIZARA YA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) – Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi(Mb)- Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)- Waziri wa Mambo ya Ndani

Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko


WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)- Waziri wa Afyana Ustawi wa Jamii

Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)- Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Waziri: Hakuna mabadiliko

Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
Waziri: Hakuna mabadiliko

Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) – Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsiana Watoto


WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) – Waziriwa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Mhe. Kaika Saning'o TELELE (Mb)- Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb) – Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

WIZARA YA MAJI
Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)- Naibu Waziri wa Maji

WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) – Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

WIZARA YA UCHUKUZI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) – Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)-Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)-Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko
Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)Balozi Ombeni Y. Sefue

KATIBU MKUU KIONGOZI

Ikulu

DAR ES SALAAM
19 Januari, 2014

WAASI SYRIA KUSHIRIKI MAZUNGUMZO

Baada ya mjadala mkali, kundi la upinzani nchini Syria limekubali kuhudhuria mazungumzo ya amani mjini Geneva wiki ijayo.

Uamuzi huo ulipokelewa vyema na wafadhili wake wa Magharibi waliosema ni hatua muhimu huku wakionyesha matumaini katika mazungumzo hayo.

Mataifa ya magharibi yenye uwezo mkubwa yamekuwa yakiushinikiza upinzani huo kushiriki katika mazungumzo hayo ambayo pia yatashirikisha serikali ya syria.

Swala la iwapo kuna umuhimu wakuhudhuria mazungumzo hayo yaliugawanya upinzani huo huku wengi wa wanachama wa kundi hilo wakiamua kujiondoa.

Mwandishi wa BBC amesema kuwa kutakuwa na maswala mengi kuhusu vile wawakilishi waupinzani huo walivyo jitayarisha.

Wakati huohuo, waziri wa mamboya nje wa Marekani, John Kerry amepongeza uamuzi wa upinzani wa Syria kwenda kwa mazungumzo nchini Switzerland.

Lengo la mkutano ni kuona ikiwa inawezekana kuunda serikali ya mpito, ili kumaliza mzozo wa Syria.

Mgogoro huo wa miaka mitatu, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 100,000

MWANDISHI WA BBC KOMLA DUMOR AFARIKI DUNIA

Mwandishi wa BBC Komla Dumor amefariki ghafla nyumbani kwake kutokana na mshtuko wa moyo.

Alikuwa na miaka 41 alipopata mauti yake.

Komla Dumor ameelezewa kuwa miongoni mwa waandishi shupavu barani Afrika.

Rais wa Ghana John Dramani Mahama amemtaja marehemu kama zawadi ya Ghana ulimwenguni na kuongezea kuwa Ghana imempoteza mmoja wa wajumbe wake.

Komla hivi karibuni alikuwa anaongoza kipindi cha Runinga kinachozungumzia maswala ya Afrika baada ya kufanya kazi katika radio mmoja nchini Ghana na vilevile radio ya BBC.

Muhariri wa habari za ulimwengu Andrew White head amemtaja kuwa mwadishi shupavu aliyekuwa na uhusiano mzuri na wasikilizaji.

MJI WA BOR WAKOMBOLEWA TENA

Jeshi la Sudan Kusini linasema limeukomboa mji wa Bor kutoka kwa waasi.

Msemaji wa jeshi, Philip Aguer, alieleza kuwa wanajeshi wa serikali wamewashinda waasi kama 15,000 watiifu kwa makamo wa rais wa zamani, Riek Machar.

Bor, mji mkuu wa jimbo la Jonglei, umekombolewa na kurejea mikononi mwa waasi mara kadha katika vita vya mwezimmoja.

Maelfu ya watu wako mbioni wanajiepusha na mapigano.

Mwandishi wa BBC mjini Juba anasema jeshi sasa linaweza kushughulikia mji wa Malakal ulioko kaskazini ambao kwa sehemu bado unadhibitiwa na waasi.

Lakini msemaji wa waasi alieleza kuwa wametoka tu Bor bila ya kupigana kufuatana na mikakati yao.


Brigedia Jenerali Lul Ruai Koang alisema waliondoka Bor kufuatana na amri ya viongozi wao wa siasa, ili kujitayarisha kwamalengo mengine.

Jeneral huyo alieleza kuwa Bor siyo muhimu tena, kwa sababu sasa ni magofu tu.

Pande zote mbili zinazoshiriki kwenye mazungumzo ya amani nchini Ethiopia zinasema zinakaribia kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano

MAREKANI KUPUNGUZA UDUKUZI WA MAWASILIANO

Rais Wa Marekani Barrack Obama amekiagiza kitengo cha ujasusi nchini humo kusitisha ukusanyaji wa habari kutoka kwa simu za mamilioni ya raia nchini humo nahata katika mataifa ya kigeni.

Akizungumza mjini Washington Obama pia amewaahidi viongozi wa nchi washirika wa Marekani kwamba taifa lake halita chunguza mawasiliano yao ya faragha hadi itakapo lazimika kufanya hivyo kutokana na maswala ya ki-usalama.

Tangazo hilo linajiri wakati ambapo kuna hasira ya kimataifa kuhusiana na kiwango cha upelelezi unaofanywa na Marekani kufuatia ufichuzi wa siriza kitengo hicho uliofanywa na aliyekuwa mchambuzi wa maswala kijasusi nchini humo Edward Snowden.

Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema kuwa makundi ya wanaharakati watashangazwa na hatua ya kitengo hicho kuendelea kumilikihabari nyingi za simu walizokusanya na kwamba haijulikana watazifanyia nini habari hizo.

Hadhi ya kitengo cha ujasusi nchini marekani imeshushwa na ufichuzi wa bwana Snowden.

Wakati huo huo hotuba ya rais Obama kuhusu mabadiliko ya mpango wa upelelezi wa marekani yamepongezwa nchini Ujerumani.

Uhusiano kati ya Berlin na Washington uliwekwa katika mizani mwaka uliopita baada ya kubainika kwamba marekani ilidukua simu ya chansela wa Ujerumani Angela Merkel

MAAFISA WA UN NA IMF WAUAWA KABUL

Takriban watu 15 wameuawa mjini Kabul nchini Afghanistan baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kushambulia mkahawa mmoja wa ki-lebanon unaopendwa na raia wa kigeni pamoja na maafisa wa serikali.

Afisaa mmoja mkuu wa shirika la Fedha duniani tawi la Afghanistan Wadel Abdallah pamoja na maafisa wengine wanne wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha yao.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mshambuliaji huyo alijilipua katika mlango wa mkahawa huo katika sehemu ya mji huo ilio na watu wengi.

Watu wawili waliojihami kwa bunduki baadaye waliwafyatulia risasi waathiriwa wa mlipuko huo.

Kundi la wapiganaji wa Taleban limekiri kutekeleza shambulio hilo.

PAPA BENEDICT XVI ALIWATIMUA MAKASISI 400

Takwimu zimejitokeza kuhusu idadi ya makasisi waliotimuliwa kufuatia madai ya kuwalawiti watoto.

Takwimu hizo zinaonyesha kwamba mnamo mwaka 2011 na 2012 aliyekuwa Papa Benedict aliwafuta kazi makasisi karibia 400.

Hii ina maana kwamba idadi ya makasisi waliopigwa marufuku kuhudumu katika miaka iliopita imeongezeka.

Idadi hiyo ilitolewa wakati wa maelezo yaliopewa maafisa wa Vatican wanaotarajiwa kufika mbele ya kamishna wa umoja wa mataifa mjini Geneva mapema juma lijalo.

Hadi kufikia sasa Vatican imeripoti idadi ya visa vya unyanyasaji wa kimapenzi pekee.

Kanisa katoliki limetuhumiwa kwa kuficha vitendo vya unyanyasaji wa kimapenzi vinavyotekelezwa na viongozi wa dini, kwa kuwahamisha makasisi hadi parokia nyengine na kukosa kuwafikisha kwa mamlaka.

PAPA AFUKUZA KAZI MAKADINALI

MAKADINALI wote isipokuwa mmoja waliokuwa wakisimamia benki ya Vatican wamefutwa kazi na Papa Francis. Waliokumbwa na 'fagio hilo la chuma' ni makadinali wanne ambao ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Kadinali Tarcisio Bertone SDB,Kadinali Odilo Scherer kutoka Brazil, Telesphore Toppo kutoka India na Domenico Calcagno kutoka Vatican.Kadinali Jean-Louis Tauran ambayeni Mkuu wa Baraza la Upapa linalohusika na Mijadala ya Kidini, amenusurika kwa mujibu wa gazetila kila wiki la Kikatoliki la The Tablet.

Gazeti hilo lilieleza jana kuwa isipokuwa Calcagno, makadinali hao wote ndio kwanza walikuwa wametimiza miezi 11 tangu wateuliwe katika kipindi cha pili cha miaka mitano, wakiwa wameteuliwa na Papa Benedict XVI muda mfupi kabla ya kujiuzulu.

Benki hiyo ya Vatican ilikumbwa nakashfa ya utakatishaji fedha mwaka2010 baada ya waendesha mashitaka wa Italia kugundua shughuli zenye shaka zihusuzo fedha chafu ndani ya benki.

Mwenyekiti wa Benki hiyo, Ettore Gotti Tedeschi na naibu wake, Paolo Cipriani walichunguzwa baada ya polisi kukamata euro milioni 23 kutoka kwenye akaunti ya benki hiyo.

Ilidaiwa kuwa ingawa benki hiyo ilikuwa inadai kupambana na utakatishaji fedha, ilivunja sheria kwa kujaribu kuhamisha fedha hizobila kutambulisha mtumaji wala mpokeaji, au zilikuwa zinatumika kwa shughuli gani.


Tuhuma hizo zilikanushwa kwa nguvu zote na Vatican. Papa Francisameteua makadinali wengine kuziba nafasi za aliowatimua na kuunda alichokiita Tume ya Makadinali ya Kusimamia Taasisi kwa ajili ya Kazi ya Dini (IOR), ambao ni makadinali Christoph Schönborn (Vienna), Thomas Collins (Toronto); Santos Abril y Castillo´ (St Mary Major) na Kadinali Pietro Parolin (Waziri wa Mambo ya Nje).

Wajumbe wa Tume hiyo watachagua rais katika siku chache zijazo itakapofanya mkutano wake wa kwanza. Kadinali Bertone ndiye alikuwa Rais hadi alipoondolewa.

Kadinali Jorge Mario Bergoglio, ambaye alipewa jina la Papa Francis, ni Papa wa kwanza Muargentina na wa kwanza kutoka nje ya Ulaya kwa zaidi ya miaka 1,000 baada ya kuchaguliwa Machi 13 mwaka jana.

Papa Francis anaweza kuwa haoneshi mapenzi mengi kwa makadinali wake wa benki, lakini anajihusisha zaidi na wanandoa, kwani ametuma mialiko kwao kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Wapendanao pamoja naye.

Kadi iliyoandikwa 'Furaha ya Ndiyo Daima' ilitolewa na Vatican ikiwaalika wanandoa wasio wa jinsia moja kukaa faragha na Papa mwezi ujao.

Kwa hafla hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Upapa la Vatican kwa Familia, washiriki wametakiwa kujiandikisha ifikapo Januari 30 ili kupata nafasi ya kukaa.