Chadema yaitupia Cuf tuhuma za Ushoga

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa
ripoti iliyotolewa na Umoja wa
Mataifa ‘United Nations
University’(UNU-WIDER) ya mwezi
Aprili 2012 iliyoandaliwa na Aili Mari
Tripp ilionyesha kuwa misaada ya
wahisani kutoka nje katika
mabadiliko ya kisiasa Tanzania
‘Donor Assistance and Political
Reform in Tanzania’, inaonyesha
kuwa Tanzania imepokea misaada
kutoka nje yenye thamani ya dola za
kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka
1990-2010.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa
ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi
inayoongoza kusini mwa jangwa la
Sahara kwa kupokea misaada mingi
kutoka nje ya nchi na hasa kutoka
mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za
Uingereza, Marekani, Ujerumani,
Uholanzi, Norway, Canada, Sweden,
na taasisi kama Benki ya Dunia,
IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo.
Pamoja na misaada yote hiyo, bado
tumeendelea kuwa nchi maskini
sana duniani pamoja na kuwa na
rasilimali lukuki ambazo tumepewa
na Mungu ila tunashindwa kuzitumia
kwa manufaa ya watanzania na
badala yake tumeendelea
kudanganywa na vimisaada vidogo
vidogo na kubadilishana na
rasilimali zetu kama madini,
misitu ,wanyama nk kwa ajili ya
misaada hiyo
.
Mheshimiwa Spika, pamoja na
misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM
bado vyama vya siasa vimekuwa na
mahusiano na baadhi ya vyama
vingine vya siasa katika mataifa ya
magharibi na vimekuwa vikipokea
misaada ya aina mbalimbali kama
fedha , nyenzo na mengineyo kadiri
ya makubaliano na mirengo ya
kiitikadi ya vyama husika.
Pamoja na
ukweli huo bado vipo vyama vya
siasa vinavyopotosha umma
kuhusiana na misaada vinayopokea
kutoka nje ya nchi na vyama hivi
vimekuwa mstari wa mbele kueneza
propaganda za uongo kuwa
vyenyewe havipokei misaada kutoka
nchi za magharibi
.
Mheshimiwa Spika, CCM wao
‘wanajiita’ kuwa wapo mrengo wa
kijamaa/kikomunisti na wamekuwa
wakipokea misaada mingi sana ya
fedha na nyenzo kutoka Umoja wa
Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni
‘Socialist International’ kutoka katika
nchi kama za Ujerumani kupitia
SDP ,Uingereza kupitia chama cha
Labour,China kupitia chama cha
Kikomunist ,Marekani kupitia chama
cha Democrats
.
Pamoja na misaada
ya kifedha na kiufundi ambayo CCM
imekuwa ikipata kutoka nje
wamekuwa hawatangazi hadharani
hata mara moja kuhusiana na kiasi
ambacho wamekuwa wakipokea na
hivyo kila kitu kwao imekuwa ni siri
kuu ya viongozi wao.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa
chama cha CUF, kutokana na itikadi
zake za mrengo wa Kiliberali
ambazo miongoni mwa misingi yake
mikuu ni pamoja na “kupigania haki
za ndoa ya jinsia moja, usagaji na
ushoga”

Hii ni kwa mujibu wa
tangazo lao kwenye mtandao wao
wa umoja wa maliberali
ulimwenguni, likiungwa mkono na
Waziri wa Haki na Usawa wa
Uingereza, Lynn Featherstone kutoka
chama cha Liberal Democrats wakati
chama hicho (www.liberal-
international.org) kilipokuwa
kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa
za jinsia moja kama haki ya mtu
mmoja mmoja, wanashirikiana na
vyama kama vile LPC ya Canada, Det
Radikale Venstre cha Norway, FDP
cha Ujerumani, Israel Liberal Group
cha Israel,PDS cha Senegal na
Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana na umoja huo, CUF
wamekuwa wakipata msaada wa
kifedha na nyenzo nyingine
mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo
vya mrengo wa Kiliberali na msaada
wa mwisho ni hivi majuzi mwezi
Machi 2013 waliposaini makubaliano
na chama cha Kiliberali kutoka
Norway.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa
CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa
Vyama vya Kidemokrasia
Ulimwenguni (International
Democratic Union - IDU). Huu ni
umoja wa vyama ambavyo vipo
kwenye mrengo wa kati na ambavyo
msingi wake mkuu ni pamoja na
kuwa na familia, kama taasisi
muhimu katika jamii, ikimaanisha
kwamba: “tunapinga vitendo vyote
vya ushoga na usagaji”.
Tunatetea
demokrasia, haki za binadamu na
kupambana na ufisadi katika serikali.
Vyama wanachama wa umoja huu
ni pamoja na Conservative Party cha
UK, CPP cha Norway, Republican cha
Marekani na vingine vinavyofuata
mrengo huo
.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya
upinzani Bungeni, inavitaka vyama
vyote ambavyo vimekuwa na
mahusiano na vyama vya nje viweke
wazi mikataba yao na malengo ya
mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na
misaada ambayo vimekuwa
vikipokea kutoka kwenye nchi hizo.

Mkuu wa baraza la Congress Ajiuzulu Libya

Mwenyekiti wa baraza la kitaifa la
Congress nchini Libya amejiuzulu
kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya
inayoharamisha yeyote aliyefanya kazi
katika serikali ya hayati Muamar
Gaddafi kushikilia wadhifa wowote
katika serikali ya sasa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari, Muhammad al-Magarief
alisema kuwa bunge ilipitisha sheria
inayowatenga watu waliofanya kazi
katika serikali ya Gaddafi, na kuwa kila
mtu anapaswa kuitii sheria hiyo.

Aidha sheria hiyo, imekosolewa sana
kwa kuwa na nguvu sana.
Kanali Gaddafi aliondolewa
mamlakani mwezi Agosti mwaka
2011.

"najiuzulu na ninafanya hivyo kwa
roho safi nikiwa najivunia kwa kufanya
hivyo," alisema bwana Magarief,
alipokamilisha hotuba yake ya dakika
40, kwa baraza la Congress.

Hata hivyo haijulikani kwa sasa ikiwa
wanachama wa Congress,
wanahitajika kupiga kura kuhusu ikiwa
watalikubali au kulikataa ombi la
bwana al-Magarief kujiuzulu.

Hata hivyo, kufuatia taarifa yake,
msemaji wa Congress, Omar
Hmeidan, alisema kuwa baraza la
Congress litahitajika kumteua
mwenyekiti mwengine.

Chini ya sheria mpya, mabalozi
waliofanya kazi chini ya utawala wa
Gaddafi hawawezi kuendelea
kushikilia nyadhifa zao.
Kulikuwa na mjadala mkali kuhusu
mabadiliko yanayofanyiwa sheria
hiyo, kuruhusu baadhi ya maafisa
kushikilia nyadhifa hiyo , lakini hilo
bado halijafanyika.

Dr Magarief alihudumu kama balozi
nchini India, kwa miaka miwili, katika
miaka ya themanini kabla ya
kuondoka katika serikali ya Gaddafi.

Aliishi uhamishoni kwa miaka 31 kama
kiongozi wa vuguvugu la ukombozi
wa Libya.

Report toka Hospitali Aliyopelekwa Ngwair

Taarifa hii inayodaiwa kutoka kwa madaktari Millard Ayo kutoka South Afrika kathibitisha kuwa siyo ya kweli.

The Medical report from Helen Joseph
hospital.

Dr Shirley Radcliffe confirming
that albert Mangwair died from “alcohol
toxicity” after drinking too much, Over-exhaustion and drugs overdose.

The
inquest heard that Albert 28, collapsed
in the his friends home had been
more than five-times the legal S.A
drink-drive limit with 416mgof alcohol
per 100 milliliters of blood in his
system.

Radcliffe described the
reasons for ICU admission included
hypoxia and one of his friend found
“two empty vodka bottles[found] on
the Car” and he had been suffering
from the eating disorder Bulimia for
several months before his death and
endless partying session with little or
no resting.

Sample taken from his
stomach showed poly-drug cocktail
and he overdosed Heroin,Cocaine
'crack' and cannabis 0.08gms was also
found in his blood and his death was
caused by massive heart attack and
respiratory failure followed by sudden
Heart stop and end up dead within
seconds!

M23 Haiinyimi Tanzania Usingizi yadai Serikali

Tanzania imesema vitisho
vinavyoendelea kutolewa na waasi wa M23
wanaopigana Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC), haviinyimi
usingizi.

Hata hivyo, imetaka Jumuiya ya Kimataifa
kutopuuza vitisho hivyo.
Kauli ya Tanzania inakuja huku kukiripotiwa
kuwapo kwa mapigano makali baina ya vikosi
vya Serikali waliopambana na waasi hao, ambao
wameanzisha tena harakati ya kuliteka Jimbo la
Goma na maeneo mengine ya jirani.

Mapigano hayo ni ya kwanza tangu M23,
kuondoka mjini humo mwaka jana kufuatia
shinikizo za kidiplomasia.

Umoja wa Mataifa (UN), umesema utaongeza
kasi ya juhudi zake za kutafuta amani kwa
kutuma kikosi cha wanajeshi 3,000 kujaribu
kuzima mapigano hayo, ambayo yalisababisha
watu 19 kuuawa na wengine kujeruhiwa.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe alisema vikosi
vya Tanzania vilivyoko Congo vitaendelea
kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia
weledi na miongozo ya UN.
Kanali Mgawe alisema kauli zozote za vitisho
vinazoendelea kutolewa na waasi hao, haziwezi
kurudisha nyuma juhudi hizo.

Hata hivyo, Kanali Mgawe aliitaka Jumuiya ya
Kimataifa kutopuuzia vitisho hivyo.

“Inawezekana kuna jambo hapa maana kwa nini
Tanzania ipewe vitisho ilhali operesheni hiyo ya
amani inahusisha mataifa mengine?” alihoji
Kanali Mgawe.

Nchi nyingine ambazo zimekubali kutuma wanajeshi wake kupigana na waasi hao ni Malawi na Afrika
Kusini.

Waasi wa M23 wamekuwa wakitoa vitisho kwa wanajeshi wa Tanzania, lakini Serikali imekuwa ikitamba
kuwa hivyo ni vitisho na kazi ya kulinda amani itaendelea kama ilivyopangwa.

Tayari, Katibu Mkuu wa
UN, Ban-Ki Moon ametembelea nchi hiyo.

Al Shabab Washambulia tena Kenya

Takriban watu sita wameuawa katika
shambulizi lililofanywa na wapiganaji
wa kiisilamu mpakani mwa Kenya na
Somalia, kaskazini mwa nchi.

Duru za polisi zinasema kuwa polisi
wawili walifariki kutokana na
shambulizi hilo lililofanywa katika
vituo vya Abdisugow na Damajale.

Msemaji wa kundi la wapiganaji wa
kiisilamu wa al-Shabab, limekiri
kufanya shambulizi hilo na kuwa watu
wanane waliuawa.

Jeshi la Muungano wa Afrika ambalo
limefurusha wapiganaji wa Al
Shabaab kutoka
Mogadishu,limewadhoofisha
wapiganaji hao ingawa hufanya
mashambulizi ya mara kwa mara
mpakani.
Al-Shabab, linatumia sheria za
kiisilamu katika maeneo wanayodhibiti
nchini Somalia.

Wamefurushwa
kutoka maeneo ya mijini ingawa
wanaendesha harakati zao katika
maeneo ya mashinani.

Mkuu wa polisi, Inspekta David
Kimaiyo, aliambia shirika la habari la
AP, kuwa watu sita wangali
hawajulikani waliko, kufuatia
shambulizi la jumamosi usiku.

Sheikh Abdiasis Abu Musab,ambaye
ni msemaji wa shughuli za kijeshi za
al-Shabab, aliambia shirika la habari
la Reuters kuwa siku ya Jumamosi
waliweza kuingia kilomita 35 ndani ya
Kenya na kuvamia kambi za polisi.

Mtandao mmoja wa kundi hilo
ulikuwa na ahabri kuwa watu wawili
walitekwa nyara na kuingizwa Somalia.

Mkuu wa wilaya karibu na kambi ya
Dadaab, Albert Kimathi, alithibitisha
mashambulizi hao mawili dhidi ya
vituo vya polisi.

Wanamgambo hao wamekuwa
wakifanya mashambulizi ya mpakani
nchini Kenya tangu mwaka 2011
ambapo majeshi ya Kenya kwa
ushirikiano na wanajeshi wa AU ,
walipoingia Somalia kupambana na
wanamgambo wa Al Shabaab.

Saigon Waponea ChupuChupu Kwa Warriors

Timu ya Saigon kutoka mkoani kigoma hii leo wameponea chupuchupu kuchezea kichapo kutoka kwa Katavi Warriors ya mkoani Katavi.

Katika uwanja wa Lake Tanganyika Saigon wamefanikiwa kutumia uwanja huo wa nyumba vizuri kwa kuibuka na ushindi wa taabu wa goli tatu kwa mbili.

Kipindi cha kwanza kiliisha kwa kila timu kutoona lango la mwenzie, Walikuwa ni Warriors katika kipindi cha pili walipoanza kupata goli kabla ya Saigon kusawazisha dakika chache baadae.

Aston Villa kama wanavyofahamika katika mitaa ya Majengo, kawajense na viunga vyote vya Mpanda hawakufanya ajizi tena walipopachika goli la pili na kufanya matokeo kusomeka 1-2. Wazee wa mikebuka walirudi kwa spidi na kusawazisha goli hilo na dakika chache kuongeza goli la tatu.

Mchezo wa marudioano utafanyika katika Uwanja wa Azimio katikati ya mji wa Mpanda mkoani Katavi siku ya Jumapili tarehe 2 June. Kabla ya mchezo huo Warriors watapambana na Rhino Rangers kutoka Tabora katika uwanja wa Azimio, mchezo huo ni wakujipima nguvu.

Katavi Warriors wanahitaji ushindi wa goli moja kwa bila ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika michuano hii ya kuelekea ligi daraja la pili. The Warriors wamefika hapo baada ya kuwaondosha Rukwa United na Saigon kuwafungashia virago Mirambo ya Tabora.

Vikongwe Wauwawa Kwa Kuchomwa Moto

MAUAJI ya kikatili yametokea usiku
wa kuamkia leo wilayani Bunda,
mkoani Mara baada ya watu wenye
hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa
kwa kuwachinja kama Kuku kisha
kuwachoma moto vikongwe watatu
kwa kuwatuhumu wanajihusisha na
vitendo vya kishirikina.
Pia watu hao mbali na kuwaua
kikatili vikongwe hao kwa tuhuma
kwamba walimuua kijana mmoja
aitwaye Sale Ligolo, walichoma
moto na kuteketeza nyumba
walizokuwa wakiishi wazee hao
pamoja na kupora kuku waliokuwa
wakiwafuga na kuwatafuna kumaliza
hasira zao.

Kwa mujibu wa wa taarifa ya
mwandishi Masau Bwire aliyepo
Bunda kwa sasa, tukio hilo
limetokea usiku wa kumakia leo
baada ya watu hao wenye hasira
kuwasaka ajuza hao baada ya
kuwepo tuhuma kwamba
walishirikiana kumuua kijana huyo
hivi karibuni.

Kijana huyo alikufa kwa kugongwa
na gari, lakini dereva aliyemgonga
alidai hakuona kama alimgonga
mtu ila mbwa na pia inaelezwa
tangu azikwe kijana huyo alikuwa
akirejea kwa mkewe na kumuita
nyakati za usiku pamoja na
kusumbua familia yao akitaka
apewe chakula na ndipo
wanafamilia hao walipoamua
kwenda kwa mganga kuchunguza
tukio hilo.

Wakiwa kwa mganga,wanafamilia
hao walitajiwa majina ya wanakijiji
watatu wa kijiji hicho ambao hata
hivyo walitoroka kwenda vijiji vya
jirani pamoja na familia zao kabla ya
usiku wa leo kuvamiwa
walipokuwepo na kuangushiwa
adhabu hizo za kinyama.
Wa kwanza kushambuliwa na
kuuwa ni bibi aitwaye Bi Mgala
ambaye alikimbilia kijiji cha jiorani
kwa rafiki yake aitwaye Bi Laya,
ambapo walimkata miguu yote
miwili na kumtenganisha kichwa na
kiwiliwili kabla ya kumchoma moto
ambapo hata hivyo kitu cha ajabu ni
kwamba ziliungua nguo zake tu
huku mwili ukiwa upo vile vile.

Baadaye walimgeukia Bi Laya
aliyekuwa akitaka kuwatoroka na
kumfanyia unyama kama rafikie kwa
kosa la kumhifadhi Bi Mgala kwa
kuamini huenda wanafanya
shughuli za kishirikina pamoja na
baadaye kurudi Kasaula na
kumnasa Bi Chausiku na kumfanyia
kama walivyowafanyia ajuza hao
wengine kisha kuchoma nyumba
tatu.

Bibi wa tatu wanayemtuhumu pia
kwa ushirikina, ametimka kijijini
hapo, lakini nyumba yake
imeteketezwa pamoja na kuku
waliokuwa wakiwafuga kuporwa na
watu hao na kutumia moto
waliouwasha katika nyumba hizo
kuwachoma na kuwala kwa hasira.

Kamanda wa Polisi wa Bunda, Mika
David Nyange amethibitisha juu ya
tukio hilo la kusikitisha na kwamba
wanedelea na upelelezi kwa nia ya
kuwasaka waliohusika na kitendo
hicho cha kujichukulia sheria
mikononi.

Taifa Stars Kuelekea Ethiopia Leo

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka leo (Mei 26
mwaka huu) usiku kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na
kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka saa 5 usiku kwa
ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake
kipa Juma Kaseja.

Timu hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi
ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa
kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya
wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.

Mbali ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho
ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni Mwadini
Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa.

Wengine ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir,
Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba,
Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya,
Athuman Idd na Haruni Chanongo.

Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na
Stars jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara
baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko.

Katika msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim
Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi Mwankemwa
(Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza
vifaa).

The Bavarians Mabingwa Wapya Ulaya

Hatimae timu kutoka Jijini Münch The Bàvarian Bayern Münich wamefanikiwa kuchukua ubigwa wa ligi ya mabigwa ulaya kwa mara ya tano(5)

Bayern imepata ubingwa baada ya kuwapa kichapo ndugu zao Borussia Dortmund kwa goli mbili kwa moja.

Bayern walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa mcroatia Mario Mandzükic katika dakika ya 60 akipokea mpira kutoka kwa Arjen Robben.

Dakika nane baada Dante Borim alimchezea vibaya Marco Reuc na kusababisha penati ambapo Gündogan aliweka wavuni na kufanya matokeo kusomeka 1-1 katika dakika ya 68.

Alikuwa ni Arjen Robben ambaye alipeleka shangwe kwa Munchen katika dakika ya 89 ya mchezo kwa kupachika goli maridadi baada ya juhudi binafsi kutumika.

Bayern wanaungana na Madrid, Ac Milani na Liverpool kuchukua Ubigwa wa ulaya zaidi ya mara tano. Madrid anaongoza kwa kuchukua mara 9 akifuatiwa na Ac Milan ambao wamenyakua mara saba(7) huku Bayern na Liverpool wakiwa wamechukua mara tano kila mmoja.

Barcelona wanafuata kwa kuchukua mara nne(4) Manchester united mara tatu(3) na timu nyingine kutoka uingereza ya N.Forest wakichukua mara mbili(2) na Chelsea mara moja.
Hongera kwa Bayern Münich.

Lipumba Aibua Jambo Zito


MWENYEKITI wa Chama cha
Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim
Lipumba, ameibua suala zito
akikihusisha chama chake na
“kumnusuru” Rais Jakaya Kikwete
katika uchaguzi mkuu uliopita.

Profesa Lipumba alitoboa siri hiyo
katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo,
jijini Dar es Salaam, alikokwenda
kuswali swala ya Ijumaa.
Huku akisisitiza juu ya umuhimu wa
mshikamano wa kiimani, Profesa
Lipumba alianza kwa kuzungumzia
matokeo ya uchaguzi mkuu wa
2010, na ushindani mkali wa kisiasa
uliokuwapo.

Alisema hawaoni matunda ya
jitihada walizofanya kumnusuru Rais
Kikwete asishindwe, kwani hata chini
ya uongozi wake, Waislamu
wameendelea kutothaminiwa.
“Ninyi masheikh mnajua vizuri zaidi
hali ya kisiasa ilivyokuwa, kwamba
ilibidi zifanyike juhudi za makusudi
ili kuokoa jahazi. Lakini pamoja na
kuliokoa jahazi, hali halisi
inaonyesha mpaka sasa hakuna
matunda yoyote yaliyopatikana, na
tupo katika mtihani mgumu zaidi,”
alisema.

Katika hali ambayo inasemekana
ushindi wa Rais Kikwete ulipatikana
kwa mbinu, huku wengine
wakiituhumu Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kuwa ilimnusuru
mgombea wa CCM, kauli hii ya
Profesa Lipumba inadokeza kwamba
anajua mkakati zaidi wa kazi ya
Tume ya Uchaguzi.

Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa
Lipumba anaonekana kuhamasisha
Waislamu kujipanga akisema
“wenzetu wameanza kujipanga”
kuelekea 2015.
“Kwahiyo kama Waislamu tunataka
kupata haki zetu, kama tunataka
kuishi kama raia wa daraja la
kwanza katika nchi yetu, lazima
tujipange kuelekea uchaguzi mkuu
wa 2015; na sisi tuanze kujipanga
kwa sababu wenzetu wameanza
kujipanga, vinginevyo tutaendelea
kubaki maskini na raia wa daraja la
nne katika nchi yetu wenyewe.

“Mwaka 2010 wakati mshindi wa
uchaguzi wa rais alipotangazwa,
mimi nilikwenda kwenye hafla ya
kutangazwa matokeo, na nilikwenda
makusudi tu, siyo kwamba uchaguzi
ulikuwa huru na wa haki, ila
nilikwenda makusudi kwa kujua hali
ya kisiasa ilivyokuwa wakati huo.

“Huku nilikutana na Sheikh Basaleh.
Nilipokutana naye, alinipongeza;
sijui kama yeye anakumbuka,
akaniambia ‘umeweka mbele imani
yako na umekuwa mwelewa wa
mambo.’”
Hata hivyo, licha ya Profesa Lipumba
kuwaambia Waislamu wajipange
kwa ajili ya uchaguzi mkuu,
hakusema wajipange kupitia chama
kipi.

Lakini alisisitiza kwamba uchaguzi
ujao ni zaidi ya siasa au rais yupi
anafaa, bali maslahi, hasa ya
rasilimali nyeti zinazopatikana katika
ukanda wa Pwani ya Mashariki, eneo
ambalo alisema linakaliwa zaidi na
watu wenye imani ya Kiislamu.

Katika moja ya kauli zake, Profesa
Lipumba alisema kwamba kuna
chama kimoja kinataka kuchukua
madaraka ya nchi, lakini kinasaidiwa
na mataifa ya magharibi, yasiyoenzi
wala kuthamini imani ya Kiislamu.
Kwa muda sasa, zimekuwapo tetesi
kwamba CCM imekuwa inafanya
siasa za udini dhidi ya vyama vya
upinzani, hasa inapoona maslahi
yake yapo hatarini.

Mwaka 2010 makada kadhaa wa
CCM walitumia mitandao ya simu
kuchonga (spoofing) ujumbe wa
simu ulioshambulia mgombea
mmoja wa upinzani, ukimhusisha
na imani yake.

Kauli ya Lipumba imethibitisha pia
minong’ono iliyokuwapo muda
mrefu kuwa baadhi ya kura za
Profesa Lipumba zilipotelea kwa Rais
Kikwete.
Katika uchaguzi huo, Lipumba
alitangazwa kushika namba ya tatu,
nyuma ya Rais Kikwete na Dk.
Willibrod Slaa wa CHADEMA.

Alipoulizwa kuhusu ziara yake
msikitini na kauli aliyotoa, Profesa
Lipumba alikiri kwamba alikwenda
kuzungumzia hali ya kisiasa nchini.

Chanzo:Tanzania Daima

Mwalimu Ajifungua Watoto Watano

Mwalimu wa Shule ya Sekondari
Luwawasi iliyopo Manispaa ya Songea, Sophia
Mgaya (28) amejifungua kwa njia ya upasuaji
watoto watano jana asubuhi katika Hospitali ya
Rufaa ya Songea ambapo watatu kati yao ni wa
kiume na wawili wa kike.

Upasuaji huo ambao umefanywa na Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Mgonde
umefanyika kwa mafanikio ambapo ulifanywa
saa 5:15 asubuhi na kumalizika 5:45 asubuhi
baada ya Mwanamke huyo kugundulika akiwa
na tatizo la kutanguliza kitovu wakati ujauzito
wake ukiwa na miezi saba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana
katika wodi ya wajawazito hospitalini hapo,
Ofisa muuguzi msaidizi Vilgilia Mselewa
amesema, walimpokea mama huyo jana saa 6
mchana baada ya kufanyiwa upasuaji na hali
yake pamoja na wanawe inaendelea vizuri.

Amesema, mtoto wa kwanza ni wa kike
amezaliwa akiwa na gramu 730, mtoto wa pili ni
wa kiume  ana uzito wa gramu 810, watatu wa
kiume alikuwa na gramu 670 wanne wa kiume
gramu 820 na watano ni wa kike aliyekuwa na
gramu 430, hali za wototo zinaendelea vizuri na
wapo kwenye chumba cha watoto ambao
hawajatimiza miezi.
Akizungumza hospitalini hapo na Mwananchi,
Mama mzazi wa watoto hao, amesema
amefurahi kupata watoto hao na anamshukuru
Mwenyezi Mungu kwa upendo mkubwa
aliompatia kwani alilia sana alipopoteza
mwanaye wa kwanza wa kike aliyezaliwa
mwaka 2010 na kufariki akiwa na miezi saba.

Aidha amewashukuru madaktari na wauguzi
kwa msaada walimpatia kwani bila wao hali
ingekuwa mbaya na amewataka Watanzania
kuendelea kumwombea yeye na wanaye ili aweze kupata afya njema na kuweza kuwalea watoto wake
kwani ana hamu ya kuwaona wakikua na kuendelea kumfariji katika maisha yake.

Naye baba mzazi wa watoto hao Zacharia James (30) mkazi wa Mkoa wa Njombe amemshukuru Mungu.

Chanzo: Mwananchi.

JWTZ Lakanusha Uvumi kutoka D.R Congo.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa
zilizotapakaa kwenye mitandao
kuwa askari wa jeshi hilo
waliokwenda huko kwa ajili ya
kulinda amani,wameanza
kujihusisha na makahaba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi
ya Habari na Uhusiano, Mtandao wa
www.congodrcnews.com umedai
wanajeshi wa Tanzania wameanza
kujihusisha na ubakaji wanawake
katika Mji wa Sake ulioko Goma.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa askari
mmoja wa JWTZ alihitaji kujamiiana
na mwanamke mmoja(Kahaba) kwa
ujira wa Dola 50. Baada ya kumaliza
shida zake ambazo ilielezwa
alizifanya bila kinga yoyote,askari
huyo alikataa kumlipa ujira
wake,hali iliyoleta tafrani na
mwanamke huyo kupiga kelele.

“JWTZ linapenda kuwaeleza
wananchi kuwa taarifa hizo ni za
uongo mtupu wenye nia ya kulipaka
matope JWTZ na Tanzania kwa
ujumla. “Picha iliyotolewa kwenye
tovuti hiyo ya
www.congodrcnews.com ni ya
wanajeshi wa Tanzania walipokuwa
katika Operesheni ya huko Comoro
mwaka 2008.

Mtu anayeonekana kuwa chini ya
Ulinzi alikuwa ni mshiriki wa Kanali
Mohamed Bacar ambaye
aliondolewa madarakani.
“Vilevile picha hiyo ilitolewa vile vile
katika tovuti za www.apc.net.au/
news/stories ya Machi 26, 2008 na
ww.Seattletimes.com. na pia picha
hiyo ipo pia kwenye tovuti ya Jamii
Forum baada ya kufanya ‘link’
kutoka kwenye Mtando wa
www.google.com.”

Taarifa hiyo ilisema kuwa JWTZ
inapenda kueleza wananchi na
dunia kwa ujumla kwamba
wanaoneza taarifa hizo wana lengo
la kukatisha tamaa juhudi
zinazofanywa na nchi za Maziwa
Makuu na SADC kuleta amani nchini
DRC kwani JWTZ wako DRC kwa
mujibu wa taratibu za kiutendaji za
Umoja wa Mataifa.

Wajerumani Kuwasha Moto Uingereza Leo

Kivumbi kinatarajia kutimka hapo majira saa 3:45 usiku kwa majira ya afrika mashariki katika Uwanja wa taifa wa Uingereza Wembley pale Miamba miwili kutoka Ujerumani itakapo umana katika fainal ya kombe la mabigwa Ulaya (Uefa Champions league).

Nikati ya Borussia Dortmund dhidi ya Bavarians Bayern Munich. Mchezo huo unatarajia kuwa wa kusisimu kwani pande zote mbili ziko katika hali nzuri.

Mario Gotze ataukosa mchezo huo wa fainal kutokana na kuwa majeruhi. Lewandowski na Reuc wataongoza mashambulizi kwa upande wa Bayern Mario Gomez na Muller wakitarajiwa kuongoza mashambulizi hayo.

Borussia na Bayern wameingia fainal kwa kuwaondosha wababe wa Uispania Madrid na Barcelona.

Borussia waliwandosha Madrid, na Bayern nao kwa kutoa kipigo cha paka mwizi kwa Barcelona kwa jumla ya magoli Saba(7) kwa sifuri. Pia Bayern ndiyo bingwa wa ligi ya Ujerumani huku Borussia akiwa wa pili kwa tofauti ya pointi 22.
Bayern wameingia fainal mara mbili mfululizo baada ile ya msimu uliopita 2011-2012 ambapo walifungwa na Chelsea kwa mikwaju ya penati katika dimba lao la Allianz Arena jijini Munich

Vikosi vya msimu mzima unaomalizika wa 2012-2013 ni kama ifuatavyo.

Kikosi cha Msimu cha Bayern Munich

-Manuel Neuer
-Tom Starke
-Maximilian Riedmüller
-Lukas Raeder

Defenders

-Dante Bonfim
-Daniel Van Buyten
-Rafinha
-Jérôme Boateng
-Philipp Lahm
-Diego Contento
-Holger Badstuber

Midfielders

-Franck Ribéry
-Javi Martínez
-Arjen Robben
-Xherdan Shaqiri
-Mitchell Weiser
-Thomas Müller
-David Alaba
-Luiz Gustavo
-Bastian Schweinsteiger
-Emre Can
-Toni Kroos
-Anatoliy Tymoshchuk

Forwards

-Mario Mandžukić
-Claudio Pizarro
-Patrick Weihrauch
-Mario Gomez

Kikosi cha Msimu cha Borussia Dortmund

Goalkeepers

-Zlatan Alomerović
-Mitchell Langerak
-Roman Weidenfeller

Defenders

-Felipe Santana
-Koray Günter
-Marcel Halstenberg
-Marc Hornschuh
-Mats Hummels
-Thomas Meißner
-Patrick Owomoyela
-Łukasz Piszczek
-Marcel Schmelzer
-Neven Subotić

Midfielders

-Mustafa Amini
-Marvin Bakalorz
-Rico Benatelli
-Sven Bender
-Leonardo Bittencourt
-Jakub Błaszczykowski
-Mario Götze
-Kevin Großkreutz
-İlkay Gündoğan
-Jonas Hofmann
-Sebastian Kehl
-Oliver Kirch
-Moritz Leitner
-Nuri Şahin

Forwards

-Bálint Bajner
-Marvin Ducksch
-Robert Lewandowski
-Marco Reus
-Julian Schieber

Kila la heri BVB na BAVARIANS

The Warriors vs Rangers

Timu ya Katavi Warriors inatarajia kupambana na timu iliyofanikiwa kupanda daraja mpaka ligi kuu timu ya Rhino Rangers kutoka mjini tabora, Katika uwanja wa Azimio katikati mwa mji wa mpanda.

Mpambano huo wa kirafiki unatarajiwa kutimua vumbi siku ya jumatano tarehe 29 May 2013.

Timu ya Katavi Warriors a.k.a Aston Villa ikifahamika hivyo katika viunga vya mji wa Mpanda ambayo inashiri ligi ya TFF ngazi ya kanda katika hatua ya mtoano itakuwa na kibarua pevu hapo siku ya Jumapili tarehe 26 May pale mjini Kigoma katika uwanja wa Tanganyika itakapo pambana na Saigon kutoka mkoani humo.

Mpaka kufikia hatua hiyo Saigon iliivurumisha bila huruma timu ya Mirambo kutoka mkoani Tabora kwa jumla ya mabao matano(5) kwa moja(1). Ambapo katika mtanange uliowakutanisha mjini tabora Katika uwanja wa Ali Hassan mwinyi Saigon waliibuka kidedea kwa goli 2-1, na kurudiwa tena katika dimba la Tanganyika mjini kigoma ambapo Saigon waiipa tena kipigo Mirambo cha goli tatu(3) kwa nunge.

Nayo Aston Villa wakiondosha timu ya Rukwa United kutoka mkoan Rukwa kwa jumla ya goli 2-1, Mchezo wa kwanza ulipigwa katika dimba la Azimio mjini Mpanda na matokeo kutoka sifuri kwa sifuri. Aston Villa walitumia vizuri nafasi ya ugenini walipoichapa Rukwa United 2-1 katika uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga na kujiakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Mpambano kati ya Warriors na Rangers Utakuwa niwakujianda kwa raundi ya pili ya mtoano kati ya Katavi Warriors dhidi ya Saigon. Katavi Warriors wameondoka usiku huu kuelekea kigoma kujianda na Mtanange huo.

Kila la Heri Aston Villa

Picha ya Siku | Picture of the Day

Bunge la Tanzania, kwa hali iliyopo mataifa ya nje yanavyochukulia

Tangazo la Ajira Kutoka Utumishi.

Tangazo la Ajira mpya kutoka Utumishi unaweza kuingia, kuangalia na kupakua(download) apa chini

Imetolewa tarehe 22 may 2013

www.ajira.go.tz

AU Yafikisha miaka 50 Tangu kuanzishwa.

Umoja wa Afrika unatimiza miaka 50 tangu kuundwa kwake hapo tarehe 25 Mei 1963 kwa jina la Umoja wa Nchi Huru
za Afrika kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni na kumaliza utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.

Tokea mabadiliko ya kidemokrasia katika Rasi ya Matumaini Mema na kumalizika vita baridi, Umoja huo unatafuta njia
za kuwa na msimamo wake wenyewe. Unalenga kuleta ushirikiano wa kikanda, kuondoa vizuizi vya lugha na biashara
na hatimaye siku moja kuleta muungano wa bara zima la Afrika.

"Mtukufu Mfalme, mwenyekiti, waheshimiwa wenzangu, ndugu na marafiki: Kwa hakika ile hali ya viongozi 32
kukusanyika hapa Addis Ababa ni ushahidi wa wazi wa haja kubwa waliyonayo raia wetu baada ya uhuru. Bara zima
limetupa mamlaka ya kuwa na mkutano huu chini ya msingi wa Umoja wetu." Maneno hayo yalitamkwa tarehe 25 Mei
1963, mjini Addis Ababba, Ethiopia kwenye hotuba ya kusisimua Rais wa Ghana, Kwame Nkrumah, juu ya kibali cha
kuundwa kwa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU). Lengo la pamoja: Umoja wa bara hilo , lenye nguvu kiuchumi na
uhuru wa kisiasa.

Mwanzo wake
Miaka sita kabla ya hapo, muasisi Nkurumah kutoka kile
kilichokuwa kikijulikana kama koloni la Uingereza
"Pwani ya Dhahabu", leo hii Ghana, aliiongoza nchi hiyo
kuwa huru na akawa ndiye baba wa vuguvugu la
uzalendo wa Mwafrika katika kuliongoza jukwaa la
mataifa machanga kupambana dhidi ya ukoloni na
ubaguzi wa rangi.
Muongozo muhimu, ambao ni ule wa kutoingilia
mambo ya ndani ya mataifa mengine huru, ukageuka
hatimae kuwa janga kwa Umoja huo, kwani mtindo wa
mapinduzi ya kijseshi wa miaka ya 1960 na vita vya
wenyewe kwa wenyewe vilipotokea, viongozi wa
mataiafa ya Afrika walibakaia kimya wakiangalia.

Madai kwamba OAU ilishindwa wakati wote ni jambo linalopingwa na balozi wa zamani kutoka Ethiopia, Mengiste
Desta. "Ninayapinga vikali madai kawamba OAU ulikuwa Umoja uliokosa meno ya kuuma. Kinyume ulikua na meno
makali mno -ikiwa mtu atatambua malengo ya kuundwa kwake, yaani kulikomboa bara zima kutokana na ukoloni na
sera ya ubaguzi wa rangi."
Hata hivyo muda si mrefu ulishinddwa kutimiza fikara ya awali, anasema Dr Mehari Maru, mtaalamu wa masuala ya
Umoja wa Afrika kutoka Taasisi ya Masuala ya Usalama (ISS), mjini Addis Ababa. "Kumalizika kwa ukoloni na sera ya
ubaguzi wa rangi, kulifungua njia ya kuwepo mjadala. Nini maswala mapya ya Umoja huo na kutokana na hayo
pakahitajika taasisi mpya kuleta mabadiliko yanayohitajika na hivyo ukaazaliwa Umoja wa Afrika."

Umoja wa Afrika
Baada ya kuupa jina jipya la Umoja wa Afrika (AU) ambao
uliundwa 2002 mjini Durban, Afrika ya Kusini, baada ya
kumalizika vita baridi, madhumuni yake yakawa ni kuleta
muungano wa kiuchumi na demokrasaia.

Kiroja cha mambo katikati ya miaka ya 1990, kiongozi wa
Libya Muammar Gaddafi aliyejitangaza "Mfalme wa
Wafalme" wa Afrika, alilazimisha fikra ya mtazamo wa
Nkrumah wa "Muungano wa Afrika,", ingawa ilikuwa siasa
kwa masilahi ya kisiasa ya Gaddafi kuliko kuwa hatua ya
kifalsafa.

Hata hivyo, mpango wake wa kuwa na jeshi moja, sarafu
moja, biashara na kusafiri bila vizuizi kama ilivyo katika
Umoja wa Ulaya ulisababisha mgawanyiko zaidi kuliko umoja. Kutokana na mvutano huo kukazuka kambi mbili na
Afrika ya Kusini yenye nguvu kisiasa ikasimama kumpinga Gaddafi.

"Bila shaka matokeo kwetu si ya kuridhisha. lakini tunasonga mbele pamoja na nina hakika siku hadi siku tutafikia
karibu lengo la "Muungano wa Afrika." Alisema mjumbe wa Gaddafi kwenye Umoja huo, baada ya kuvunjwa moyo na
kile alichokiona ni udhaifu, aliwaambia wajumbe baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika 2009. Gaddafi
mara kwa mara alikuwa akitowa matamshi makali kwa waliompinga kwa kuzingatia kile alichokiona ni mapenzi ya
Waafrika wengi kwake.

Hatimaye
Ingawa wazo hilo lilizusha mabishano na kutoa sura ya
mgawanyiko miongoni mwa mataifa, Umoja wa Afrika
sasa una waziri wa ndani wa Afrika ya Kusini
Nkosazana Dlamini-Zuma kama Rais wa Halmashauri
Kuu ya Umoja huo, mwana mageuzi aliyetangaza haraka
kwamba anataka kuona unawajibika zaidi.

Halmashauri
hiyo kuu inataka kuendeleza sera ya kuadhibu kwa
kusimamisha uanachama na vikwazo kwa wanaokiuka
katiba na muongozo wake.
Mtihani kwa uwajibikaji na nguvu za kiutendaji za
Umoja wa Afrika, kandoni mwa pigo la ujumbe wake wa
AMISOM nchini Somalia, ni mgogoro katika mataifa ya
Afrika ya Magharibi ya Mali na Jamhuri ya Afrika ya
Kati.

Kwa Maoni ya Mehari Maru kutoka Taasisi ya
Masuala ya Usalama ni kwamba "Leo Afrika ni ya kidemokrasia zaidi kuliko miaka kumi iliyopita ambapo tulikuwa na
serikali chache zilizochaguliwa kidemokrasia. Lakini hili halipaswi kutafsiriwa kwamba ni uongozi wa kidemokrasi.

Demokrasia ni kutambua fikra tafauti, kwani ndiyo msingi wa matatizo ya kisiasa Afrika."

Sherehe za Jumamosi
Katika Sherehe za Jumamosi, miongoni mwa mambo
mengine ni mchuano wa kandanda kati ya wanachama
waasisi Ethiopia na Sudan. Pia Umoja huo unasherehekea
pamoja na Ujerumani, kwa sababu tangu miaka kadhaa,
Ujerumani imekuwa ikiliiunga mkono Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika kwa kusaidia mafunzo.

Afisa anayehusika na masuala ya Afrika katika Wizara ya
mambo ya nchi za nje mjini Berlin, Egon Kochanke,
anazungumzia mustakbali mwema akisema kwamba
malengo waliyokuwa nayo Rais wa Tanzania, Julius
Nyerere, na Kwame Nkrumah wa Ghana miaka 50 iliopita,
yalikuwa ni kuleta maendeleo ya kisiasa na kiuchumi barani
Afrika na kuwa na mtazamo wa pamoja kuweza kuyafikia.

Kidogo mafanikio si kama yalivyotarajiwa, lakini leo hii Umoja wa Afrika una nguvu na msimamo wenye nguvu sana
katika sera ya kigeni na usalama na pia upigaji kura."
Miaka 50 ya Umoja wa nchi huru za Afrika sasa Umoja wa Afrika, bara hilo limezindukana zaidi.

Wakati Rais wa
Ujerumani Joachim Gauck alipozuru Addis Ababa hivi karibuni na kupendekeza kuongezwa mchango wa wanajeshi wa
Ujerumani, hilo halikupata shauku kutoka kwa Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Dlamini-Zuma.

Kauli
mbiu ya " Suluhisho la matatizo ya Afrika ni la Waafrika wenyewe," inapewa kipaumbele miaka 50 mengine ijayo ndiyo
itakayotowa jibu.

Habari kutoka DW

Polisi Mtwara Wapata tuhuma za Ubakaji

Hali ya usalama katika Manispaa
ya Mtwara Mikindani mkoani hapa
imezidi kuwa mbaya baada ya
askari polisi kudaiwa kufanya
unyama kwa k uwabaka
wanawake na kumpiga risasi
mjamzito
Mbali na unyama huo polisi pia
wanadaiwa kuchoma moto
nyumba tatu za wananchi katika
mtaa wa Magomeni na vibanda
vya maduka kadhaa na kupora
vitu vilivyomo ndani.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa
anasema hali ni shwari na kwamba
wananchi watoke nje kuendelea na
shughuli zao kama kawaida.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Rufaa ya Ligula,
Mohamedi Kodi amethibitisha
kupokea mwili wa mjamzito
ukiwa na tundu tumboni,
zinazoaminika kuwa za risasi na
hivyo kufanya idadi ya maiti
zilizopokelewa hospitalini hapo
kufikia mbili na majeruhi 18:

“Ni kweli kwa leo( jana)
tumepokea maiti moja ya
mwanamke ambaye ni mjamzito
wa miezi saba, amepigwa risasi
tumboni. Pia tumepokea
mwanafunzi wa shule ya
sekondari ya Chuno,amevunjwa
miguu yote kwa risasi.”
Habari zinadai kuwa mjamzito
huyo ameuawa akiwa nyumbani
kwake baada ya polisi kuvamia
makazi yake.

Huduma za kijamii zimesimama,
hakuna maduka yaliyo wazi,
hakuna usafiri wa daladala wala
pikipiki, mji upo kimya, sauti za
milio ya mabomu na bunduki
zimetawala, wanajeshi waliovalia
sare wameuzingira mji wakiwa
katika magari na pikipiki.
Wakizungumza na Waandishi wa
Habari kwa nyakati tofauti wakazi
hao wamelalamikia kitendo cha
askari wa jeshi la polisi kuingia
katika makazi yao, kuwapiga,
kuwabaka na kuwapora mali zao:

Popout
“Magomeni A hatuna amani
askari wanaingia majumbani
mwetu wanatupiga na
kutunyang’anya simu, yani
huku Magomeni hatuna amani
kabisa, tumepoteza watoto na
hatujui hata waume zetu wako
wapi” alisema Paulina Idd na
kuongeza:

“Majumba yetu yamechomwa
moto , wanaofanya fujo ni polisi
wenyewe halafu wanakuja
wanatubaka na kuiba mali zetu
halafu tunateseka sisi yaani
tumechoka kabisa na serikali
yenyewe,” alisema Paulina.

Kamanda Sinzumwa alipoulizwa
kuhusiana na tuhuma hizo alisema
hawezi kuzungumzia suala hilo
kwa madai kuwa atapingana na
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk
Emmanuel Mchimbi aliyewasili
Mtwara leo: “Kuhusiana na
suala hilo siwezi kulizungumzia
kwa sasa kwani nitapingana na
Waziri wangu kwani leo ametoa
tamko bungeni na leo
atawasili,” alieleza Sinzumwa
Wananchi wazungumzia bajeti
Wakizungumzia uwasilishwaji wa
hotuba ya Wizara ya Nishati na
Madini wakazi wa hapa
wamesema kuwa hawakubaliani
na ujenzi wa bomba la kusafirisha
gesi kwani mpango huo utawaletea
dhuluma:

“Mpango wa kusafirishwa kwa
gesi asilia hatuna mpango nao
kwa wakazi wote wa Mtwara
kwa kifupi akina mama wa
mtwara hatutaki itoke,” alisema
Fatuma Abdallah.


Chanzo:Mpekuzi

Taifa Stars Wakutana Ikulu na Rais Kikwete

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa
stars) kwa lengo la kuitia moyo katika
mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco
ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta
tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia
kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa
ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele
kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha
katika mchezo wao dhidi ya Gambia
ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa
bao 2-0.

“Maadamu mara ya kwanza mliwashinda
Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi
dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi
sana na mkishindwa tunanyong’onyea
sana,” amesema Rais Kikwete.

Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo
Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa
ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia
timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30
ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu
kwa hatua iliyofikia na kuwataka
wachezaji kujituma ili kuwafurahisha
watanzania ambao hivi sasa wanaipenda
timu yao ya Taifa.

Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Fenera Mukangara amesema
Serikali itaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali wa michezo nchini ili kuondoa
changamoto zinazoikabili timu hiyo.

Kwa upande wake Kocha Poulsen,
amemshukuru Rais Kikwete kwa
kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo
ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili
kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji
wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma
Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na
kuahidi kujituma kwenye mazoezi na
hatimaye kuibuka washindi kwenye mechi
zijazo.

Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya
pili katika kundi C inatarajia kucheza
ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka
huu.

Mapambano ya Mtwara

MTWARA : GESI GESI WAR UPDATE
*. Kuna madai ambayo hayajathibitishwa kwamba wanawake wanabakwa na
maaskari, wanapigwa risasi kutokana na vijana wote kukimbia maporini.
*. Mwanamke anayekadiriwa miaka 25 mjamzito auawa kwa kupigwa risasi
maitiipo Ligula.

*. Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
*. Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za
Askari magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.

*. Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye
amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake.
Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
*. Mabomu yanaendelea kupigwa tofauti kwa sasa hayapigw mfululizo.

*. Mabomu yametulia. Hali ya ukimya imetawala.
*. Mabasi 5 ya Champion yamebeba Wanajeshi yako njiani yanakuja.
*. Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.

*. Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi
kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
*. Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani maaskari
wanaingiamajumbani mwa watu na kumsomba mtuyeyote ambaye ni mwanaume
awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu
unafanywa na maaskari hao hao. Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.

*. RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende
makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
*. Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto

*. Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika
pamoja namilio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu
inaendelea kusikika.

*. Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali
ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.

*. Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.
*. Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni,
Nkanaledi na Mikindani.

*. Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote
Barabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna
njia yakupita.



chanzo:mtwarakumekucha.blogspot.com

Picha Ya Siku | Picture of the Day

Je hii ni kweli Account ya Tanesco?

Shekh Amwagiwa tindikali huko Zanzibar.

Sheha wa Tumondo
Mohamed Omary
Said, amemwagiwa tindikali na mtu
asiyejulikana na hivyo kupata
maumivu makali sehemu yake ya
kifua na jicho kuumia pia.
Sheha huyo alikimbizwa katika
Hospitali ya Mnazi mmoja mjini
Unguja ambapo alipatiwa matibabu
ya dharura.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Mjini Magharibi,Mukhadam
Khamis,amesema chombo
kilichotumika kumwagia tindikali
Sheha huyo kilipatikana eneo la
tukio na kwamba polisi imekichukua
kwa kukichunguza kitaalam ili
kugundua aliyekuwa akikitumia kwa
kuangalia alama za vidole.

Sheha huyo alimwagiwa tindikali
jana usiku wakati alipotoka nje ya
nyumba yake kuchota maji na ndipo
mhalifu huyo alipomwagia tindikali
na kwamba hakuweza kumtambua.

Polisi Wa Bangi Atoroka

JESHI la Polisi mkoani Arusha linamshikilia ofisa wa jeshi hilo, Inspekta Isaac Manoni, kwa
tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa wa usafirishaji wa magunia ya bangi, Koplo Edward.

Koplo Edward ni dereva wa gari la polisi lenye namba za usajili T 2025, aina ya Toyota Land
Cruiser, linalodaiwa kutumika kubeba magunia 18 ya bangi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa katika sakata la
usafishaji wa bangi kwenda Holili, mpakani Kenya, watuhumiwa walikuwa wawili, akiwamo
askari namba G. 2434, PC George, ambao wote wamefukuzwa kazi.

Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa kutoroka kwa askari huyo kunadaiwa kuwa ni mpango
uliotengenezwa na askari wenzake ili kupoteza ushahidi katika kashfa hiyo.

Inaelezwa kuwa askari huyo aliwatoroka askari waliokuwa wakimlinda akiwa nyumbani kwake
baada ya kuwahadaa kuwa anachukua pesa na ndipo alipotokea mlango wa nyuma.

Baadhi ya askari mjini Moshi waliozungumza kwa sharti la kutotaka majina yao yatajwe,
walidai kuwa tukio hilo ni mpango uliosukwa na baadhi ya askari wenzake wa Arusha kwa
lengo la kumwepusha na balaa mmoja wa vigogo wa jeshi hilo anayedaiwa kuwa kwenye
mtandao wa kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.

Askari huyo ndiye anayedaiwa kumpigia simu kigogo mmoja wa polisi mjini Arusha
akimtaarifu kukamatwa kwao na akakaripiwa kwa kukamatwa kizembe huku mpango wa
kuwapa rushwa askari wa doria waliowakamata ukikwama.

“Wakati wakiwa katika nyumba ya mtuhumiwa huyu kulikuwa na askari saba, akiwamo
Inspekta. Isaac ambaye alikuwa kiongozi, hivyo baada ya tukio lazima tumshikilie huyu kwa
uzembe kazini,” alisema kamanda huyo.

Awali watuhumiwa hao walikamatwa Mei 18, mwaka huu, majira ya saa 5 usiku huko Himo na
askari polisi wa Kilimanjaro wakiwa na gari la polisi lenye namba za usajili T 2025, Toyota Land
Cruiser lililokuwa likiendeshwa na Koplo Edward huku likiwa na magunia 18 ya bangi
yakipelekwa Holili, mpakani Kenya.

Hata hivyo jeshi hilo limetoa wito kwa mtu yeyote anayefahamu mahali alikotorokea
mtuhumiwa huyo atoe taarifa polisi na kuwafichua watu wote wenye mtandao wa biashara
haramu ya bangi.

Kamanda Sabas alisema kuwa tayari ameshatoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya
kutoroka kwa askari huyo na hatua zilizochukuliwa kwa askari waliokuwa wakimlinda, hivyo
hawezi kutoa taarifa nyingine kwa njia ya simu.
Katika hatua nyingine, askari PC George, mwenye namba za usajili G. 2434 amefikishwa
mahakamani mkoani Kilimanjaro.

Mbali na askari huyo, pia mfanyabiashara mmoja, Livingstone Urassa, wa Usseri Wilaya ya
Rombo alifikishwa mahakamani pamoja na askari huyo ambapo wote walisomewa shitaka la
kula njama na kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.

Washtakiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Simon Kobelo, ambaye ni Hakimu Mkazi
Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na wakili wa serikali, Abdallah Chavula,
washtakiwa hao wanadaiwa kuwa siku, muda na mahali pasipofahamika walikula njama ya
kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.

Shitaka la pili lilimhusu PC George, ambaye anadaiwa kuwa Mei 18, mwaka huu huko Kilema,
Wilaya ya Moshi, mshtakiwa alisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi magunia 18, ikiwa na
thamani ya sh milioni 81.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 5, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa
hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakamana hiyo kutokuwa na uwezo wa
kusikiliza shauri hilo.


Chanzo:freemedia.com

Vurugu za Mtwara

Mtu moja anamefariki dunia katika vurugu zinazoendelea mjini mtwara.

Na wakati huo huo nyumba nne (4) zaripotiwa kuchomwa na waandamanaji nyumba moja ikiwa ni ya Mbunge na moja ya mwandishi wa habari wa Tbc, pia nyumba nyingine yadaiwa kuwa ni ofisi ya CCM iliyopo karibu na Chuo cha Uhasibu(TIA) Sambamba na uchomaji huo pia kituo cha kuuzia mafuta cha total nacho pia Charipotiwa kuwa kimechomwa moto.

Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto ilikuweza kuwatawanya waandamanaji hao.

Vurugu zimekuja baada ya kusomwa kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini leo mjini dodoma. Ambapo imekuwa kinyume na matarajio mengi ya wanamtwara.

Vurugu hizo zimesababisha kwa kufungwa kwa barabara ya Dar-Mtwara na kuvunjwa kwa daraja linalo unganisha Mtwara na Lindi ambapo magari huishikia katika mkoa wa Lindi.

Raia wa kigeni kadhaa
waliokuwa wakiendelea na
shughuli mbalimbali katika
bandari ya mtwara
wameonekana wakiondoka

Madrid Yatemana na Special one

Rais wa klabu ya Real
Madrid,Florentino Perez amewaambia
waandishi wa habari jumatatu jioni
kuwa Mourinho hatofukuzwa bali
wamekubaliana kumaliza mkataba
wao na kocha huyo raia wa Ureno.

Aidha Madrid, imeongeza kuwa
haijaanza mazungumzo na kocha
yeyote kwaajili ya kuchukua nafasi ya
Mourinho lakini vyanzo mbalimbali
vya habari za michezo zinamtaja
kocha wa PSG ya Ufaransa, Carlo
Ancelloti kuchukua jukumu la
kuifundisha Madrid msimu ujao.

Duru za kimichezo zinasema, Jose
Mourinho huenda akarejea nchini
Uingereza kuifundisha klabu yake ya
zamani ya Chelsea baada ya kuwepo
makubaliano baina yake na uongozi
wa klabu hiyo.

Majambazi Waiba Kanisani.

KATIKA hali isiyokuwa ya
kawaida, usiku wa kuamkia
jana majambazi waliangusha
mfuko wa mamilioni ya fedha
na simu mbili makaburini
wakati wakiwakimbia polisi
baada ya kuvamia, kuvunja na
kuiba fedha hizo katika Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Francisco
wa Sales Parokia ya Mkuza,
Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Kibaha mkoani Pwani.
Katika tukio hilo lililotokea
saa tisa usiku, Polisi walipiga
risasi juu baada ya kupewa
taarifa na majirani, na
kuwafanya majambazi hao
waliokuwa tisa, kutimua mbio
kwa kuruka ukuta upande wa
makaburini na kuangusha
mfuko wenye fedha zaidi ya Sh
milioni tatu, fedha za kigeni na
simu mbili.

Paroko wa kanisa hilo, Padri
Mathew Chavely aliliambia
gazeti hili jana kuwa,
majambazi hao walivunja
mlango wa ofisi baada ya
kuwafunga kamba walinzi na
kuwawekea plasta midomoni
kisha kufanikiwa kuiba fedha
hizo.

“Tulijua wakitoka ofisini,
wanatujia sisi nyumbani, ila
kabla, watu wema walitoa
taarifa polisi na mara polisi
wakaja hapa, walipiga risasi
wale wezi wakakimbia na
fedha zote, asubuhiwakati wa
uchunguzi, kumbe
waliangusha fedha makaburini,
karibu na kanisa,” alisema
Padri Chavely.

Alipoulizwa kwa nini wakae na
fedha nyingi ofisini, Padri
Chavely alisema kanisani hapo
hivi sasa wanaendelea na
ujenzi wa kanisa jipya kubwa,
hivyo Jumapili ya juzi, mbali ya
kukusanya sadaka za kawaida,
kulikuwa na harambee ya
ujenzi wa kanisa hilo.

Padri Chavely aliwashukuru
waumini na majirani kwa sala
na kutoa taarifa polisi na
aliwaombea majambazi hao
wabadilike, wamrudie Mungu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani, Ulrich Matei
alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa,
asubuhi walimshikilia Karani
wa Ofisi, Deus Cosmas kwa
mahojiano, lakini walimuachia
baada ya kupata simu mbili za
majambazi hao
zilizodondoshwa makaburini
pamoja na fedha zote.
“Ni kweli saa tisa usiku leo
(jana) walivamia kanisa hilo,
wezi waliokuwa tisa, wakiwa
na silaha za jadi kama
marungu, mapanga, nyundo na
nyinginezo, tulipopata taarifa
tulifika mara moja na kwa
kuwa hatukujua walioko ndani
wana silaha gani zaidi,
tuliamua kupiga risasi juu,
ndipo walipokimbia kwa
kuruka ukuta nyuma, eneo la
makaburini,” alisema Kamanda
Matei.

Akielezea zaidi tukio hilo,
Kamanda Matei alisema wezi
hao waliwafunga kamba na
plasta walinzi kabla ya
kuvunja ofisi ya kanisa na
kuiba Sh 3,172,450, Dola za
Marekani 13, fedha za Uganda
Sh 18,700, fedha za Kenya Sh
200 na Rupia 328.

Kwa mujibu wa Polisi,
kutokana na ukubwa wa eneo
hilo, majambazi walitumia
ukuta wa nyuma kuruka na
kukimbia na wakati
wakikimbia, katika eneo hilo
lenye makaburi, walikuta
damu kwenye misalaba kadhaa
iliyoharibiwa kwa
kupindishwa na kutokana na
purukushani hiyo, waliangusha
mfuko wenye fedha zote
walizoiba na simu hizo mbili.

Kamanda Matei alisema
usalama umeimarishwa eneo
hilo, na kupitia simu hizo, kwa
kutumia Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (Tehama),
wamebaini mtandao na
mambo mengi ambayo
yatawawezesha kuwakamata
wote wanaohusika na tukio
hilo na matukio mengine
mkoani humo.

Chanzo:Habarileo

Lissu na Kilango Malecela nusura wazichape

Baada ya Bunge kuahirishwa jana,
nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri
baina ya Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge
wa Same Mashariki (CCM), Anne
Kilango Malecela.

Mtafaruku huo uliibuka baada
ya Kilango kusikika
akimtuhumu Lissu kwa
uchochezi, akisema kwamba
amekuwa mbunge pekee
anayeongoza kwa vurugu.

Maneno hayo hayakumfurahisha
Lissu ambaye alishindwa
kuvumilia na kumgeukia Kilango
kwa nguvu huku baadhi ya
wabunge wakishuhudia na
wengine wakimzuia Lissu.

Obama Ajipanga Ziara ya Afrika

Rais wa Marekani Barack Obama
anatarajiwa kuzuru Senegal, Afrika
Kusini na Tanzania mwezi Juni. Hii ni
kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya
White house.

Rais Obama atakutana na watunga
sheria na wafanyabiashara pamoja na
viongozi wa asasi za kijamii.

Ziara ya Obama itaanza tarehe 26 Juni
hadi 3 Julai na itakuwa ziara yake ya
pili Kusini mwa jagwa la Sahara akiwa
rais wa Marekani.
Alizuru Ghana mwaka 2009 .

Rais wa zamani wa Marekani Bill
Clinton na mwenzake George W Bush,
wote walizuru Afrika wakati wa
muhula wao wa pili wa utawala.
Clinton alizuru nchi sita wakati Bush
akizuru nchi tano.

''Rais atatilia mkazo uhusiano kati ya
Marekani na baadhi ya nchi za kiafrika
ambazo zinakuwa ikiwemo maswala
kama ukuwaji wa uchumi, uekezaji na
biashara pamoja na kukuza taasisi za
kidemokrasia na kuendelea kukuza
viongozi wa kizazi kijacho Afrika,''
ilinukuu taarifa kutoka ikulu ya White
House.

Ziara ya Obama pia itatilia mkazo
kukuza uhusiano kati ya Marekani na
watu wa bara la Afrika ili kuendeleza
ushirikiano wa kikanda, amani na
ukuwaji.

Wadadisi wanasema kuwa ziara kama
hizi hufanywa sana na marais wa
Marekani hasa baada ya kuondokewa
na kazi ngumu ya kampeini za
uchaguzi na shinikizo za ndani ya
nchi.

Wakati huohuo, tisho linaloongezeka
kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu
nchini Mali, limefanya kanda hiyo
kumulikwa zaidi na Marekani. Bi
Michel Obama ataambatana na
mumewe katika ziara hiyo.

Polisi Wadakwa na Bangi

Siku chache baada ya Jeshi la Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
kuwakamata askari 16
wakituhumiwa kujihusisha na
biashara ya magendo, askari
wengine wawili wa jeshi hilo
wamekamatwa mkoani Kilimanjaro
wakiwa na shehena kubwa ya bangi
wakiisafrisha kwenda nchini Kenya.

Askari hao walikamatwa Mei 19
mwaka huu saa nne usiku eneo la
Kilemapofu, Wilaya ya Moshi Vijijini
wakiwa na magunia 18 ya bangi
ambayo walikuwa wameyapakia
kwenye gari la Mkuu wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani
Arusha aina ya Toyota Land Cruiser
lenye namba PT 2025.
Akithibitisha kukamatwa kwa askari
hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Robert Boaz alisema
askari hao walikuwa wakipeleka
bangi hiyo Wilaya ya Rombo kwa
mfanyabiashra mmoja ambaye
hakutaka kumtaja jina lake.

Kamanda Boaz aliwataja askari
waliokamatwa na wanashikiliwa
kwenye kituo kikuu cha polisi katika
mji mdogo wa Himo kuwa ni F.1734
Koplo Edward (dereva) wa kikosi
cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani
Arusha na G.2434 Konstebo George
wa kituo cha polisi Ngarenanyuki
Wilaya ya Arumeru.
Alibainisha kuwa kukamatwa kwa
askari hao kunatokana na
operesheni ya kukabiliana na dawa
za kulevya inayofanywa na polisi
katika mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro.

Alisema operesheni hiyo imefanyika
kikamilifu katika Mkoa wa Arusha
uliokuwa ukitumika kupitishia
bidhaa hiyo, na sasa wahusika
wameamua kuutumia Mkoa wa
Kilimanjaro.

“Baada ya kuwahoji askari wale,
walidai kuwa walikodishwa na
mfanyabiashara huyo kuipeleka
bangi hiyo wilayani Rombo tayari
kwa kusafirishwa kwenda nchini
Kenya ambako inaaminika kuna
soko kubwa,” alisema.
Kamanda Boaz alisema hivi sasa
polisi wa Kilimanjaro kwa
kushirikiana na wenzao wa Arusha
wanafanya uchunguzi kubaini
mtandao wa askari hao
unaojihusisha na vitendo haramu.

Aliongeza kuwa hatua inayofuata
kwa askari hao ni kufunguliwa
mashtaka ya kijeshi na iwapo
watakutwa na hatia watafukuzwa
kazi kisha watafikishwa katika
mahakama za kiraia.
Kamanda Boaz alibainisha kuwa
kwa kawaida askari wanapotoka
mkoa mmoja kwenda mwingine
hupatiwa kibali maalumu cha
kusafiria (Movement Order).

Alisema kibali hicho husaini kila
mkoa ambao askari husika hupita,
lakini waliokamatwa na bangi
hawakuwa nacho.
Kamanda Boaz alibanisha kuwa kwa
hali ilivyo askari hao waliondoka na
gari la mkuu wa FFU bila kumpa
taarifa wala kupata kibali chake.

Tanzania Daima limedokezwa kuwa
askari hao wamekuwa wakisafirisha
bangi hiyo mara kwa mara kupitia
mji huo wa Himo bila kukamatwa
kutokana na gari lao kuwa na
namba za kijeshi, hivyo kuwa
vigumu kwa askari wenzao kuwatilia
shaka.

Taarifa zaidi zimedai kuwa
kukamatwa kwa askari hao
kulitokana na gari lao kupata hitilafu
katika eneo hilo la Kilemapofu, na
ndipo askari wa doria walipofika
kwa lengo la kutoa msaada kwa
wenzao, lakini ghafla walisikia
harufu ya bangi.

Mtoa taarifa aliyezungumza kwa
sharti la kutotaka jina lake litajwe,
alisema baada ya askari hao kusikia
harufu ya bangi waliwaarifu viongozi
wao waliowaamrisha walifanyie
upekuzi gari hilo sambamba na
kuwaweka chini ya ulinzi askari wote
waliokuwamo.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa katika
upekuzi huo walibaini uwepo wa
magunia 18 ya bangi yaliyolengwa
kupelekwa nchini Kenya.
Kilibainisha kuwa baada askari hao
kukamatwa, mmoja wao alisikika
akiongea na mtu aliyemuita bosi
kumuarifu kukamatwa kwao.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa bosi
aliyearifiwa tukio hilo alihoji
imekuwaje wakakamatwa kizembe
namna hiyo.

Kilidokeza kuwa bosi huyo alimhoji
aliyempigia simu kuwa wamebaki na
shilingi ngapi ili wawape rushwa
polisi waliowakamata.

“Bosi aliambiwa kuna laki tano, naye
akawaambia wawape fedha hizo
zote, lakini kwa bahati mbaya
hawakufanikiwa,” kilisema chanzo
chetu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha, Liberatus Sabas, hakukiri
wala kukanusha kuwapo kwa taarifa
za kukamatwa kwa askari wake.

Tanzania Daima lilitaka kujua Jeshi
la Polisi mkoani Arusha limechukua
hatua gani dhidi ya askari hao
ambapo kamanda Sabas alisema
hayupo katika nafasi nzuri ya
kulizungumzia jambo hilo kwa kuwa
yupo hospitalini.

Aston Villa Waifurumusha Rukwa United

Hatimae timu kutoka mkoa wa Katavi, Katavi Warriors wameifurumusha timu kutoka mkoa wa Rukwa, Rukwa United kwa ushindi wa Goli mbili kwa moja (Rukwa United 1-2 Katavi Warriors).

Timu hizi ziko katika ligi ya TFF ngazi ya kanda ambapo mechi huchezwa katika mfumo wa nyumbani na ugenini.

Ushindi wa leo umekuja baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa katika uwanja wa Azimio mjini mpanda na matokeo kutoka bila.

Rukwa United wamekubali kichapo hicho katika uwanja wao wa Mandela mjini sumbawanga. Katika Mechi hiyo Katava Warriors walitangulia kufunga katika kipindi cha kwanza kwa goli lilofungwa na Macky kabla ya kusawazisha katika kipindi cha pili na kufanya matokeo kuwa moja moja mpaka dakika za lala salama ambapo katavi warriors hali maarufu kama Aston villa walipoandika goli la pili kupitia mkwaju wa penalti.

Vatican Wa Wasilisha UN taarifa ya Bomu Arusha

Tukio la kutupwa bomu katika
Kanisa Katoliki la Joseph
Mfanyakazi, Arusha limetua katika
Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa (UN) baada ya kuwasilishwa
na Balozi wa Vatican UN, Askofu
Mkuu Frances Chullikatt. Askofu
Chullikatt anakuwa kiongozi wa
kwanza wa Vatican kutoa tamko
kuhusiana na shambulizi hilo
ambalo mmoja wa viongozi wake
alikuwapo.

Bomu hilo lilirushwa katika kanisa
hilo wakati likizinduliwa na Balozi wa
Vatican nchini, Askofu Mkuu
Francisco Padilla Mei 5, mwaka huu
na kusababisha vifo vya watu
watatu na kujeruhi zaidi ya 50.
Wakati wa shambulizi hilo, Askofu
Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo la
Arusha, Josephat Lebulu
walionusurika.

Akihutubia Kikao cha Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa, New
York, Marekani juzi, Askofu
Chullikatt alisema tukio lililotokea
Arusha linadhihirisha kuwa kuna
umuhimu ya kupambana na ugaidi
katika Afrika ili kuimarisha amani na
usalama wa kimataifa.“Unahitajika
mshikamano na ushirikiano wa
pamoja wa mataifa mbalimbali
katika kuchukua hatua za maisha na
kulinda haki za binadamu,” alisema
Askofu Chullikatt, ambaye amekuwa
mwakilishi wa Vatican kwenye
Umoja wa Mataifa tangu mwaka
2010.

Askofu Chullikatt, ambaye ni
mzaliwa wa India, alisema suala la
ugaidi linahitaji kuzuiwa duniani
kote na hasa Afrika kutokana na
matukio hayo kuharibu maisha ya
binadamu na kutokea katika
maeneo wanayofanyia ibada.

Askofu Chullikatt alisema pale ugaidi
unapofanyika kwa kutumia dini,
waumini na viongozi wao ni lazima
wahakikishe wanapambana nao ili
kuutokomeza.

Alisema suala la ugaidi linahitaji
viongozi wa kisiasa, kijamii na kidini
kulilaani kwani ni la kikatili katika
maisha ya binadamu hivyo si vyema
kukaa kimya suala hilo linapotokea.

Askofu Chullikatt alisema ugaidi
unaotokea Afrika unatakiwa
kuangaliwa kimataifa ili kuzipa
uwezo nchi hizo kupambana na
kuzuia matukio hayo.

Shambulio la bomu dhidi ya kanisa
la Arusha lilikuwa tukio la pili la
ugaidi uliolenga kushambulia
wageni nchini.

Mara ya kwanza
ilitokea mwaka 1998, wakati Ubalozi
wa Marekani nchini ulipolipuliwa
kwa bomu na kusababisha vifo vya
watu kumi na moja huku 85
wakijeruhiwa.

Ratiba Ya Kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika Yapangwa

Michuano ya kufuzu kwa fainali ya
kombe la mataifa bingwa barani
Afrika ACN, mwaka wa 2015,
itachezwa kwa muda wa miezi mitatu
pekee mwaka Ujao.
Tangazo hilo limetolewa na shirikisho
la mchezo wa soka barani Afrika CAF.

Uamuzi huo sasa unamaanisha mechi
mia moja na arubaini na nne,
zinazojumuisha timu 48, katika
makundi 12 ya timu nne kila mmoja
itachezwa kati ya Septemba na
Novemba mwaka ujao.
Ratiba hiyo mpya, imepangwa ili
kuwiana na ratiba ya mechi za
kimataifa ya shirikisho la mchezo huo
duniani FIFA.

Vile vile mashindano hayo
hayatakuwa na nafasi mwaka wa
2014, kabla ya fainali za kombe la
dunia itakayoandliwa nchini Brazil.

Hii ni mara ya kwanza kwa fainali hizo,
kuandaliwa nje ya mwaka ambao
fainali za kombe la dunia kufanyika,
tangu ilipoamuliwa kuwa mashindano
hayo yafanyike mwaka mmoja kabla
na baada ya fainali za kombe la dunia.

Na kutokana na matatizo ya usafiri
barani Afrika, ratiba hiyo mpya
huenda ikakumbwa na matatizo hasa
kutoka mashariki hadi magharibi mwa
Afrika.

Matatizo ya fedha

Timu itacheza mechi moja mwishoni
mwa wiki na kupumzika kwa siku mbili
kabla ya kucheza mechi nyingine
kuambatana na ratiba ya FIFA.

Wachezaji wanaoshiriki ligi za kulipwa
ni sharti waruhusiwe na vilabu vyao
kuaklisha mataifa yao katika mechi
hizo.

Mechi hizo zimepangiwa kuchezwa
kati ya tarehe Moja hadi Tisa
Septemba, kisha tarehe Sita hadi
tarehe Kumi na Nne Oktoba na mechi
za mwisho zitachezwa kuanzia tarehe
Kumi hadi Kumi na Nane Novemba.

Rais wa shirikisho la mchezo wa soka
nchini Namibia, John Muinjo,
anaamini ratiba hiyo mpya itawapa
changamoto nyingi.

Amesema kucheza mechi sita za
kimataifa kwa muda wa miezi mitatu
itakuwa ngumu sana na hatari hata
kwa afya ya wachezaji.

Aidha amesema kutokana na matatizo
wa fedha, wasimamizi wa soka katika
nchi kadhaa huenda wakashindwa
kuwasafirisha wachezaji wao kutoka
nchi moja hadi nyingine kwa muda
mfupi.

Baada ya kukamilika kwa hatua ya
makundi, washindi wa kila kundi
watajumuika na timu zingine tatu
zilizoandikisha matokeo mema zaidi
katika makundi yao kufuzu kwa kwa
hatua ya mwisho ya kufuzu ambayo
itaandliwa nchini Morocco kati ya
mwezi Julai na Agosti mwaka wa 2015.

Picture of the day|Picha ya siku

Kila mtu anaamini kilicho kwake

Kim Poulsen Ataja Wakuivaa Morocco

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim
Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu)
ametaja kikosi cha wachezaji 26
watakaoingia kambini kujiwinda kwa
mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia
dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8
mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.

Katika kikosi hicho, Kim ameita
wachezaji wapya sita ingawa baadhi
yao wamewahi kuchezea timu hiyo,
huku akiacha wengine watatu aliokuwa
nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya
Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda
mabao 3-1.

Wapya aliowaita katika kikosi hicho
kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka
huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya
Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally
Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio,
Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya
na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha
ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud
Cholo na Issa Rashid.

Kikosi kamili cha Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager ambacho kabla ya
kwenda Morocco kitapita jijini Addis
Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya
kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya
Sudan ni kama ifuatavyo;
Makipa ni nahodha Juma Kaseja
(Simba), Aishi Manula (Azam), Ally
Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally
(Azam). Mabeki ni Aggrey Morris
(Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin
Yondani (Yanga), Nadir Haroub
(Yanga), Shomari Kapombe (Simba),
Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na
Waziri Salum (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba),
Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo
(Yanga), Haruna Chanongo (Simba),
Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto
(Simba), Mudathiri Yahya (Azam) na
Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam),
Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana
Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho
Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga),
Thomas Ulimwengu (TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).

Kocha Kim amesema kikosi
kitakachoingia kambini kitakuwa na
wachezaji 24 ambapo Samata na
Ulimwengu watajiunga na timu jijini
Marrakech, lakini wachezaji
atakaondoka nao Dar es Salaam
kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo
ataacha kipa mmoja na mchezaji
mmoja wa ndani.

Awali TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars
mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu
dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini
baadaye Algeria ikasema itacheza na
Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo
ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo
ambalo lisingewezekana kwa Stars
kwani ina mechi ya mashindano Juni 8
mwaka huu.

Kwa upande wa Libya mechi hiyo
ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni
2 mwaka huu.

Lakini baadaye Libya
ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli
ambapo TFF ilikataa kutokana na
sababu za kiusalama.

TANZANIA YAJIONDOA MICHUANO YA
COSAFA

Tanzania (Taifa Stars) imejitoa kwenye
michuano ya Baraza la Vyama vya
Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika
(COSAFA) itakayofanyika nchini Zambia
kuanzia Julai 2-26 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah
amesema Stars ambayo iliingizwa katika
michuano hiyo kama timu mwalikwa
imejitoa kutokana na mwingiliano wa
ratiba kati ya michuano hiyo na mechi
za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa
Ndani (CHAN).

Amesema awali Tanzania ilithibitisha
kushiriki michuano kwa matarajio
kwamba Uganda ingekubali ombi la TFF
la kubadilisha ratiba ya mechi za CHAN,
lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu
Uganda (FUFA) likagoma kwa vile
kipindi ambacho kilipendekezwa
lenyewe litakuwa na uchaguzi wa
viongozi wao.

Taifa Stars itacheza na Uganda (The
Cranes) katika mechi za CHAN ambapo
mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es
Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu
wakati ya marudiano itafanyika jijini
Kampala kati ya Julai 26-28 mwaka huu.

Akizungumzia michuano ya COSAFA,
Kocha Kim amesema angependa
kushiriki michuano hiyo kwani
ingekuwa kipimo kizuri kwa kikosi
chake, lakini kwa sasa malengo
makubwa ya Stars kwenye mechi za
mchujo za Kombe la Dunia na
michuano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON) ambayo fainali zake
zitafanyika mwaka 2015.

Sister(Mtawa) Feki Akamatwa Iringa

Mwanamke - anayejiita Sister Phylis
Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini
Kenya akiwa ofisi za kamanda wa
jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada
ya kukamatwa
Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa
Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.

JESHI la polisi mkoa wa Iringa
limemkamata mwanamke Phylis
Wanjiru mwenye umri wa miaka 44
aliyevalia mavazi ya kitawa wa
masister wa kanisa Kathoriki,
ambapo baada ya kupekuliwa
amekutwa na baadhi ya vielelezo
vilivyobaini kuwa ni tapeli.

Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya
Kenya amekamatwa na jeshi la polisi
baada ya masister wenzie kubaini
kama si mmoja wao, kutokana na
kushindwa kufanya baadhi ya
masuala ambayo ni msingi wa
utawa wao.

Akizungumzia mkasa huo, kamanda
wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa
Michael Kamuhanda amesema
mwanamke huyo kabila laKe ni
Muwembu wa nchini Kenya
amekamatwa katika nyumba  za
masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.

Aidha Kamuhanda amesema
mwanamke huyo ambaye awali
aligoma kutoa maelezo ya kina juu
ya ujio wake nchini Tanzania, katika
upekuzi walimkuta na baadhi ya chip
(Line) za makampuni mbalimbali ya
simu ya ndani na nje ya nchi.
Kamuhanda amesema Sister huyo
bandia alikutwa pia akiwa na hati za
kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa
niya Africa Mashariki yenye namba
Ke. 020659 huku hati ya nyingine
ikiwa na jumuiya ya Kenya namba A.
1790366.

Amesema Sister huyo feki katika hati
hizo ilionyesha kuwa alitembelea
nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na
nchini Tanzania ambapo siku za hivi
karibuni alikuwa Mkoani Mara
Tarime.

Sister huyo FEKI amekuwa akitumia
mbinu ya kujiangusha kama mtu
mwenye ugonjwa wa kifafa pindi
anapofanyiwa mahojiano, jambo
linalowawia vigumu jeshi hilo kupata
maelezo ya kina dhidi ya dhamira
yake ya kuingia humu nchini.

Kamuhanda ameitaka jamii kuwa
makini na wageni mbalimbali, huku
akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini
watu kwa muonekano wao,
kutokana na mwanamke huyo
kutumia njia hiyo ambayo
inamfanya kila mtu kumuamini.

Wanafunzi 15 Washikiriwa na Polisi

Wanafunzi 15, wa Shule ya Sekondari ya
Jumuiya ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe
mkoani Mbeya , wanashikiliwa polisi kwa
tuhuma za kuchoma moto bweni la wanafunzi
wa kiume na kusababisha uharibifu wa mali
mbalimbali.

Aizungumzia tukio hilo , Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio
hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku shuleni hapo  na
kwamba wanafunzi hao walifikia hatua hiyo ya
kuchoma moto bweni hilo, wakipinga
kusimamishwa masomo kwa wanafunzi wenzao
watatu kwa utovu wa nidhamu.

Aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo
kwa utovu wa nidhamu kuwa ni Joseph Robert
(18), anayesoma kidato cha nne na Mwita Chacha
(17) na anayesoma kidato cha tatu, wote wakazi
wa Kitunda jijini Dar es Salaam na Mwingine ni
Daniel David (18), anayesoma kidato cha tatu
ambaye ni mkazi wa Ipinda wilayani Kyela.

Alisema kuwa wanafunzi hao watatu
waliwahamasisha wenzao kuwaunga mkono
kupinga adhabu hiyo kwa kufanya vurugu na
kwamba bweni lililochomwa moto walikuwa
wanaishi wanafunzi 50, ambao hawakuwa tayari
kuunga mkono uvunjifu huo wa amani.

Lipumba Muongo "Ikulu"

KAULI ya Mwenyekiti wa
Chama cha Wananchi (CUF),
Profesa Ibrahim Lipumba,
kwamba kuna njama za
kumwongezea Rais Jakaya
Kikwete, muda wa kuongoza
nchi, ni uzushi mtupu na ni
upotoshaji usiokuwa na
msingi.

Taarifa ya Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Ikulu
iliyotumwa kwa vyombo vya
habari juzi, ilifafanua kwamba
Rais Kikwete hafahamu
kuwepo mipango hiyo, na
kumtaka Profesa Lipumba
aisaidie jamii kusema nani
anafanya mpango huo, ili
ukweli ujulikane.

“Aidha, Mheshimiwa Rais
anawasihi wanasiasa na
Watanzania kwa ujumla,
kuacha tabia za uongo na
uzushi na kuwapotezea muda
Watanzania kufikiria mambo
yasiyokuwepo.

“Ukweli ni kwamba, kama
ambavyo amesema mara
nyingi, ni matarajio ya Rais
Kikwete kuwa mchakato wa
Katiba utakamilika mwaka
2014, na kuwezesha Uchaguzi
Mkuu wa 2015 kufanyika chini
ya Katiba Mpya kama
inavyotarajiwa ,” ilieleza
taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Ikulu, Rais
Kikwete anatarajia baada ya
uchaguzi wa 2015, atapata
nafasi ya kustaafu mwisho wa
kipindi chake cha uongozi kwa
taifa letu.

Picture of the Day|Picha ya siku

Kipanya:

Wataka Kuruhusiwa Kujiua

Wanaume wawili wenye ulemavu
mbaya zaidi wanakwenda
mahakamani kukata rufaa katika kesi
inayoonekana kuwa moja ya kesi
inayotaka mageuzi makubwa ikitaka
kubadilisha sheria za serikali kuhusu
haki ya mtu kufa.

Mmoja wa watu hao, Pail Lamb
amekuwa na ulemavu mbaya kwa
miaka mingi pamoja na kupitia
uchungu mwingi, hawezi kujitoa uhai
wake na anataka madaktari
waruhusiwe kumuua bila ya
kukabiliwa na kosa la mauaji baadaye.

Mwanamume mwingine anayejulikana
kama Martin, anataka uamuzi
utakaowaruhusu madaktari
wamsaidie kujiua ingawa waweze
kulindwa kutokana na sheria za
kuweza kuwashtaki kwa kufanya
kitendo cha mauaji.

Wakosoaji wanasema kuwa ikiwa
mahakama itaruhusu wawili hao
wajiue, itakuwa na athari kubwa kwa
watu wazee na wenye ulemavu kutaka
kujinyonga ili kuzuia kuwahangaisha
jamaa zao kuwahudumia.

Akamatwa na Vifaa Vya Kutengenezea Hela Bandia

Jeshi la polisi mkoa wa  Katavi
limemkamata Hilali  Abdalah
(30) mkazi wa mtaa wa majengo
mjini hapa kwa kumkamata
akiwa na vifaa vya kutengenezea
noti  bandia   akiwa katika nyumba
ya kulala wageni
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Katavi Dhahiri Kidavashari alisema
Hilali alikamatwa hapo jana majira
ya  ssa 8 mchana katika nyumba ya
kulala wageni inaitwa
Ambassodor aliyoko  katika mtaa
wa mji wa  zamani  Kata ya
kashaulili  mjini hapa
Alisema mtuhumiwa alikamatwa
kufuatia taarifa za kiitelejensia
kulifikia jeshi la polisi mkoa wa
Katavi kutoka kwa raia wema
kuwa Hilali anajihusisha na
shughuli hiyo ya utengenezaji wa
noti bandia.

Kidavashari alivitaja vifaa
aliwavyo kamatwa navyo
mtuhumiwa kuwa ni  karatasi
ngumu  217 ambazo hutumika
kutengenezea   noto bandia za
shilingi  10,000  bomba mbili  za
sindano zenye dawa maalumu
kwa ajiri ya kubadilishia  rangi ya
karatasi hizo ili zifanane na pesa
hizo.

Alivitaja vifaa vingine kuwa ni
powder chupa moja  kwa ajili ya
ya kumfanya mteja ataakizishika
mapema zisiache alama ya
vidole kwenye pesa beseni  moja
jeusi kwa ajiri ya kusafishia
karatasi hizo mara baada ya
kuzipitishia  kwenye hatua kadha
vifaa ningine alivyo kamatwa
navyo Hilali ni karatasi 21 plain
kwa ajiri ya kufunikia karatasi
ngumu zisipate hewa wakati wa
utengenezwaji wa noti   bandia
soltap 2  kwa ajiri ya kubania
karatasi zisipate hewa mapema
pasi moja ya umeme  kwa ajili ya
kukaushia pesa  hizo  mara baada
ya kuziosha na ugolo vijiko
vitatu   ambao alikuwa akiutumia
kama kilevi wakati akifanya
shughuli hiyo  haramu.

Kamanda waa polisi mkoa wa
Katavi alieleza  awali  mtuhumiwa
alikuwa akijishughulisha na
shughuli za  kuuza mitumba
kaika soko la Buzogwe mjini hapa
na baadae alihamia mkoani
Tanga  na ndiko aliko patia ujuzi
wa kutengeneza noti bandia
Kidashari alieleza  hatimaye baada
ya kupata utaalamu huo alirejea
Mpanda na kuanza  kazi  hiyo
mbaya ya kuvunja sheria za
Nchi.

Alisema katika  maelezo yake ya
awalialikiri kufanya shughuli hiyo
kwa kile alicho kieleza ni
kutokana na yeye  hapo siku za
nyuma aliwahi kutapeliwa pesa
kwa kupewa noto bandia ndio
maana ameamua na yeye kulipa
kisasi kwa watu wengine
Pia mtuhumiwa alitaja sababu
nyingine kuwa ni katika kujitafutia
maisha  kwa njia ya ytafuataji ndio
maana akaamua kujitafutia pesa
kwa njia hii
mtuhumiwa anategemewa
kufikishwa mahakamani  mara
upelelezi wa kesi hii utakapo
kamilika ili aweze kujibu
mashitaka yanayo mkabili.

Chanzo:kataviyetu.blogspot.com

Taarifa toka Ikulu Juu ya Kauli ya Dr. Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mheshimiwa
Wilbroad Slaa, Jumatatu, Mei 13,
2013, amekaririwa na gazeti moja
akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete na timu yake ya kampeni,
“ilikuwa ikisaka kura kwenye
nyumba za ibada na kumwaga
sumu mbaya ya udini ambayo
sasa inaitesa Serikali na taifa”
kwenye Kampeni za Uchaguzi
Mkuu wa 2010.

Aidha, katika habari hiyo
iliyoandikwa chini ya kichwa cha
habari, “Dk. Slaa amlipua JK”
kwenye gazeti linalounga mkono
CHADEMA la Tanzania Daima,
Mheshimiwa Slaa anadai kuwa
migogoro ya sasa ya kidini
“inajengwa au kutengenezwa na
Serikali iliyojikita kusambaza
sumu ya udini katika misikiti
wakati wa kampeni za Urais
mwaka 2010” .

Kwa hakika, hakuna
namna nyingine ama namna bora
zaidi ya kuielezea kauli hii ya
Mheshimiwa Slaa isipokuwa
kwamba kauli hiyo ni riwaya
nyingine isiyokuwa na mshiko. Ni
uongo mtupu. Yake Mheshimiwa
Slaa ni maneno yasiyokuwa na
ukweli wowote. Ni uzushi na
santuri ambayo imezoeleka sasa
kwa wananchi.

Kauli ya Mheshimiwa Slaa
ni mwendelezo wa mtiririko
usiokuwa na mwisho wa ghiriba
ambazo kamwe hazitafanikiwa za
Mheshimiwa Slaa kuwahadaa
wananchi kuhusu ukweli wa
mambo ulivyo katika nchi yetu.

Rais Jakaya Mrisho
Kikwete na timu yake ya kampeni
kamwe hawakufanya kampeni za
Uchaguzi Mkuu wa 2010, ama wa
mwaka mwingine wowote, katika
nyumba yoyote ya ibada iwe
msikitini ama kanisani ama
hekaluni ama nyumba nyingine
yoyote ya ibada mahali popote
katika nchi yetu.
Mheshimiwa Rais Kikwete
hajawahi hata kufikiria
kuchanganya dini na siasa. Hana
sababu ya kufanya hivyo.

Anaelewa fika madhara ya udini
kwa mustakabali wa nchi yetu,
kwa umoja wa taifa letu na kwa
mshikamno wa wananchi wake.

Yoyote anayejaribu kumbebesha
Rais Kikwete msalaba wa udini
ana lake jambo na ni vyema
atuambie fika Rais alitumia
Msikiti upi, ama Kanisa lipi,
mahali gani na kwa nyakati gani
kufanya kampeni.

Vinginevyo, kauli ya
Mheshimiwa Slaa itabakia ni kauli
tu inayostahili kupuuzwa na
wananchi, itabakia ni kauli ya mtu
mzima anayetapatapa na kufanya
jitihada kubwa kujivunjia mwenye
heshima kwa kutunga na
kusambaza uongo.
Tunanapenda kumshauri
Mheshimiwa Slaa kuwa kama hana
jambo la maana la kuwaambia
wananchi ama ameishiwa na hoja
ni vyema anyamaze, awaachie
wananchi waendelee na shughuli
zao za maendeleo, kuliko
kuendeleza riwaya zake
zisizokuwa na mshiko. Yake ni
santuri iliyowachosha wananchi.

Imetolewa na :
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
13 Mei, 2013

Katavi Warriors Yatoshana Nguvu

Timu kutoka mkoa wa Katavi, Katavi Warriors imetoshana nguvu kwa bila kufungana na timu kutoka mkoa wa Rukwa, Rukwa United.

Timu hizi zinashiriki ligi ya TFF ngazi ya Kanda.

Shaffih Kujibu Tuhuma za TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih
Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti
ya www.shaffihdauda.com kutoa
maelezo kuhusiana na barua ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye
mtandao wake huo.

FIFA ambayo ilisimamisha mchakato
wa uchaguzi wa TFF baada ya
baadhi ya wagombea kuulalamikia,
baadaye ilitoa maelekezo kuhusu
mchakato huo kwa barua ambayo
iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar
Lenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na
waandishi wa habari ambao Dauda
alihudhuria alibainisha kuwa barua
hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu,
na kuruhusu waandishi kuisoma
kwa Ofisa Habari wa TFF bila
kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na
waandishi wa habari (Mei 2 mwaka
huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA
ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF
pekee, na viongozi wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.

Hivyo TFF imemtaka Dauda
kutoa maelezo ya mahali alipoipata
barua hiyo ndani ya siku saba.

Chanzo:shaffihdauda.com

Aston Villa Kutupa Karata Yake leo

Timu ya mpira wa miguu Katavi Warriors hali maarufu kama Aston Villa ikifahamika hivyo katika viunga vya mji wa mpanda.

Ambayo imefanikiwa kupanda daraja baada ya kuibuka bingwa wa mkoa wa katavi na kufanikiwa kuingia ligi ya TFF ngazi ya kanda Inatarajia kutupa karata yake leo 12 May dhidi ya timu kutoka mkoan Rukwa, Rukwa United katika Uwanja wa Azimio mjini mpanda muda ni kuanzia saa kumi jioni kwa saa za afrika mashariki.

Katavi inawakilishwa na timu mbili katika mashindano haya, timu hizo ni Katavi Warriors(Aston Villa) na Small kids(kotaz).  Small kinds inashiriki mashindano haya baada ya kushuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza ngazi ya taifa. Kila la heri timu kutoka katavi

"Burundi Mpaka Dar Kwa Bajaj" Dr. Magufuli

WAZIRI wa Ujenzi, Dk John
Magufuli amesema serikali
inaendelea kujenga barabara
kwa kiwango cha lami ifikie
hatua ya watu wasafiri kutoka
Burundi hadi Dar es Salaam
kwa teksi na ikiwezekana kwa
bajaj.

Dk Magufuli alisema hayo jana
bungeni wakati akijibu
maswali bungeni likiwemo la
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Kabwe Zitto aliyesema Kigoma
imefaidika na barabara lakini
hazina maana kama barabara
za kuiunganisha na Tabora
hazitengenezwi.
“Namshukuru Zitto kwa
kupongeza Serikali ya CCM.
Ni
kitendo cha ushujaa kwa
mbunge wa kambi ya upinzani
kupongeza…barabara (za
Tabora) zimeshawekewa jiwe
la msingi, zitaendelea
kujengwa watu watoke
Burundi hadi Dar es Salaam
kwa teksi na ikiwezekana kwa
bajaj,” alisema Magufuli.
Akielezea kusimama kwa
ujenzi wa barabara za Tabora-
Nzega, Tabora-Urambo na
Kaliua, Waziri Magufuli
alisema miezi miwili iliyopita
kulikuwa na mvua nyingi
ambazo ziliathiri matengenezo
yake. Akizungumzia maeneo
ya barabara yaliyoharibika
baada ya ujenzi, Magufuli
alisema wizara inachukua
hatua.

Mojawapo ni mkandarasi
aliyerudishwa katika eneo la
Sekenke kurudia ujenzi kwa
gharama zake na amepewa
mwaka mmoja wa uangalizi
wa barabara hiyo.
Hata hivyo, Waziri Magufuli
alisema serikali iko katika
mchakato wa kupitia sheria
kudhibiti uzidishaji wa mizigo
kutokana na ukweli kwamba
Tanzania ndiyo inaruhusu tani
nyingi kupitishwa barabarani
ikilinganishwa na nchi
nyingine zikiwemo
zilizoendelea.

Kwa mujibu wa Magufuli,
kiwango cha tani
zinazoruhusiwa nchini ni 56
wakati nchi kama vile
Marekani, kiwango chao ni
tani 40, Uingereza ni 44,
Denmark tani 48; Uganda na
Kenya zinaruhusu tani 54.
Awali katika swali la msingi,
Mbunge wa Viti Maalumu,
Martha Mlata (CCM) alihoji
utekelezaji wa ahadi ya
Serikali kwamba katika
awamu ya nne wananchi
wataweza kusafiri kwa teksi
kutoka Mtwara hadi Bukoba.

Akijibu swali hilo, Naibu
Waziri wa Ujenzi, Gerson
Lwenge alisema lengo hilo
limetekelezwa kwa mafanikio
makubwa hadi kufikia asilimia
99 ya barabara yote kutoka
Mtwara hadi Bukoba.

Alisema barabara yote kuanzia
Mtwara-Dar es Salaam-
Dodoma-Singida-Nzega-Tinde-
Usagara-Geita-Bwanga-
Kyamyorwa hadi Bukoba
yenye urefu wa kilometa
zipatazo 1,989 imejengwa kwa
kiwango cha lami isipokuwa
eneo la urefu wa kilometa 26
katika barabara ya Ndundu-
Somanga litakalokamilika
Desemba mwaka huu.